Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA: maana nilimuona ghafla akiacha kumtazama Jessenia na kutoa simu mfukoni na kuipokea, kisha akaongea, “poa” ndio neno pekee alilo ongea kisha akakata simu, halafu nikamuona anaibofya bofya simu yake kwa muda mfupi, kisha akaiweka mfukoni na kutulia pale pale juu ya vesper yake, “Prosper chukuwa sub” alisema Suleiman, ambae alikuwa anatoka ndani ya uwanja, nadhani alikuwa amechoka kidogo, hapo nikaingia ndani ya uwanja, na mimi siku jiuliza mara mbili nikachukuwa nafasi ya Suleimani. ….….. ENDELEA..
Ukweli nilikuwa na tabia moja, ambayo hata mimi sikuwa naipenda sana, maana sio nzuri kwenye swala zima la michezo, mara nyingi kama ninacheza mpira huu wa kikapu au Baskert ball kama unavyoweza kuita kwa lugha ya waingereza, huku mwanamke ambae ni mpenzi wangu au ninae mvizia akiwa nje anatazama, basi ningefanya juhudi ya hali ya juu, ndio kama ilivyokuwa leo, hakika nilicheza mpira huu kwa kasi na uwezo mkubwa zaidi ya ule ambao vijana hawa walikuwa wameuzoea, japo kuna wakati nilihisi miguu yangu inakosa nguvu, nadhani ni kutokana na kazi ambayo nilikuwa nimetoka kuifanya mchana wa leo, hata hivyo haikunizuwia kufanya kila nilichotaka kukifanya, huku mara kwa mara nikitazama nje kumtazama Jessenia, ambae alikuwa anafurahishwa na uchezaji wangu, maana muda wote nilipomtazama alikuwa anatabasamu na wakati mwingine kushangilia, na hata alipogundua kuwa ninamtazama alipunga mkono wa chini chini, kitu ambacho hakukijuwa ni kwamba, Ussi alikuwa anatufuatilia kwa ukaribu sana, na niligundua hilo wakati nilipo kuwa namtazama pia, nilimuona kama sio ananitazama mimi basi anamtazama Jessenia lakini kwa macho yaliyojaa hasira na chuki, na pia niliweza kuona baadhi ya watu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea, maana waliijuwa tabia ya Ussi kwa mvulana au mwanaume yoyote anaejaribu kumkaribia dada yake.
Hilo kwa kweli sikujari, kwasababu niliamini kuwa Ussi asingeweza kufanya lolote mahali pale, sababu kwa sasa Jessenia alisha kuwa mkubwa, na pia hata angejaribu kunivamia asinge weza kunigusa kwa ngumi hata moja, ninge mchapa kama namchapa mtoto mdogo, niliendelea kucheza mpira kama vile hakukuwa na jambo linaloendelea pale uwanjani, jambo ambalo naweza kusema ni vita ya macho, na nusu saa baadae nikamuona Ussi anapokea simu kwa mara nyingine tena, sikusikia alicho ongea lakini alipomaliza aliwasha piki piki yake na kuondoka zake akiwa katika hali yake ile ule ya chuki na hasira.
Zikiwa zime bakia dakika kama kumi na tano hivi, nilitazama kwenye lango la kiuingilia kwenye makazi ya wafanyakazi wa serikali,nikamuona Maimuna yule mwanafunzi wa kike, ambae asubuhi ya leo aliniachia ujumbe kwenye karatasi pamoja namba za simu, ambae nadhani aligundua kuwa nilimtazama, maana licha ya kuwa nilimtazama kwa muda mfupi, lakini aliweza kunikonyeza na hapo nilikwepesha macho yangu kwa haraka sana, sikutaka mtu mwingine ajuwe kama nime konyezwa mimi.
Ukweli mschana huyu sio kwamba sio mzuri, au niliogopa kuanguka nae kwa sababu ni mwanafunzi, lakini kilicho nishinda mimi kwa mschana huyu ni sababu mbili, moja njia ambayo anataka tuitumie kumpatia dudu, ukweli japo sikuwahi kujaribu, lakini pia nisingeweza kujaribu kufanya hivyo, hebu fikiria yeye ni bikira, na nisingeweza kupita kitumbuani, hivyo ningelazimika kuingia upande wa nyuma kwa muda wote ambao tungekuwa chumbani, kama ni msaa manne basi ningepita huko tu, kama ni mchana kutwa basi ningelazima kuingia huko huko, hata wewe ungeweza kweli, hivyo usinione mshamba, pili sikuhitaji kuendelea kuwa karibu na mschana huyu, kwa sababu tayari nilikuwa na Jessenia, ambae kwa heshima aliyonipa sikutaka kumuumiza kwa namna yoyote, isitoshe ingenipunguzia heshima yangu.
Nashukuru Maimuna hakukaa sana pale nje alikuja mdogo wake Yassin na kumueleza jambo kisha wakaingia ndani kwa pamoja, na mimi kuendelea kucheza mpira kwa amani, lakini hazikupita dakika tatu toka Maimuna aingie ndani, akaja jamaa mmoja ambae nilishawahi kumuona mara kadhaa pale uwanjani, ujio wa huyu jamaa uliharibu kabisa usikivu na umakini wa mchezo, maana alikuja na habari ya kuogofya, habari ambayo ilisimamisha mchezo, na watu kumzunguka yeye wakisikiliza habari hiyo toka kwake, “yani leo ni mchana mchana, jamaa amekutwa ameshakauka kabisa, yaani inashangaza sana” alisema yule jamaa, huku mimi nikiwa mmoja wao.
Kwa haraka haraka nilisikiliza na kuelewa kuwa, kuna mtu mmoja amekutwa ameuwawa mita chache toka kwenye ofisi za tanesco, kule Tibirinzi huku kifo chake kikisaidikiwa kuwa kimesababiswha na jini, nikutokana na muonekano wa mwili wa marehemu huyo, ambapo hivi sasa umepelekwa hospital na askari wa jeshi la polisi, “dah! mbona tutaisha wote” alisema mmoja kati ya watu tuliokuwepo pale, “tena jamaa hilo jini lina uwa wanaume tu” alisema mwingine na hapo nikapata nafasi ya kuchomeka swali, “kwani huyo jamaa alikuwa na nani?” niliuliza kama mtego maana jambo hilo nililitarajia, “kuna anae fahamu basi, huyo jamaa ni mnyamwezi, anafanya kazi kwenye majahazi huko baharini” alisema jamaa, na hapo nika tabasamulia ndani kwa ndani, na kukumbuka nilivyomuona Ussi akiongea na simu na kuondoka kwa haraka, “Aroub huko aliko lazima atakuwa amesha nipigia” niliwaza kimoyo moyo huku naondoka zangu na kumfuata Jessenia pale alipokuwa amekaa, “naona ulikuwa unapata umbea hapo, hebu nifahamishe na mimi” alisema Jessenia huku anainuka, tayari kuelekea kwenye gari.
Na mimi nikaongozana nae kuelekea kwenye gari, huku nikimsimulia nilicho simuliwa, sio ninacho kifahamu, “he! basi tuwahi ukaoge kisha tuje macho mane tupate urojo na unirejeshe nyumbani” alisema Jessenia, ambae nilimshangaa kwa kweli, maana mwanzo nilihisi kuwa lazima atakuwa anaona namchelewesha kurudi kwao, kutokana na simu aliyopigiwa na mjomba wake, sasa inakuwaje mschana huyu anataka twende kwanza nikaoge kisha turudi macho mane ambako ni lazima tunge poteza muda kwa kununua na kula chakula, lakini sikutaka kuonyesha dalili za mshangao wangu wala kumkatalia, ila nilitumia busara kumueleza, “nitanenepa mwaka huu, ila Jesse, vipi kuhusu mjomba hato kasirika zaidi?” ilimuuliza Jessenia, ambae hakuonyesha kujari, “achana nae, na ndivyo ninavyo taka haswaa, kwani we hukumuona Ussi alivyojivimbisha, kwahiyo wao walikuwa wanafurahia mimi nilivyo kuwa nina pata tabu?” aliuliza Jessenia, wakati huo tayari tulikuwa ndani gari, na mimi nikawasha gari na kuanza kuliondoa taratibu, huku wale jamaa wakisahau habari za jini na kuanza kulisindikiza gari kwa macho, “na wakati huo huo Simu yake ikaanza kuita, kumbe na yeye aliiacha ndani ya gari kwenye mkoba wake, akaitoa haraka na kuitazama, “mjomba huyoooo!” alisema Jessenia, japo kwa sauti ya uoga, maana alikuwa anatabasamu huku anaipokea, “asalam aleykum” ndio neno pekee nililoweza kulisikia na kuelewa maana yake, zaidi nilisikia tu, “mh….. anhaaa…. mh!mh!” mpaka simu ilipokatwa, kisha, Jessenia akanitazama huku anabasamu, “ataelewa tu! ila sijui kwanini mjomba anakuwa hivi jamani” alisema Jessenia, ambae alinieleza kuwa, mjomba wake alimpigia simu kumkaripia sana kwa kiburi alicho kionyesha Jessenia, na kwamba amewatia aibu kubwa sana, kwa kuonekana anaranda randa na mwanaume mitaani, hivyo ni wazi kuwa Ussi alipiga simu kumueleza baba yake kuwa ametuona hapa uwanja.
Ukweli niliona kuna umuhimu wa kumaliza kazi mapema, kabla mambo hayajawa mazito zaidi, maana niliona sasa wakina Ussi watalazimika kufanya kila wanachokifanya, baada ya kuona wanaanza kugunduliwa na mimi nilitakiwa nifahamu wanafanya hivi kwa lengo gani, kisha nitafute ushaidi ili watiwe nguvuni, kisha niondoke zangu kuelekea dar, japo sikuwa na uhakika wa kuondoka na Jessenia, ambae kila muda nilikuwa nazidi kumpenda, “hivi Jesse, upo tayari kuondoka na mimi kwenda dar es salaam” nilimuuliza Jessenia, huku naendesha gari taratibu kuelekea upande wa markiti, hapo Jessenia alitabasamu kidogo, “Eric, mimi ni mke, nipo tayari kwenda kokote mume anakoenda” alisema Jessenia kwa sauti iliyoonyesha kuwa mwenye furaha, haku hofia kuhusu hasira za Ussi, wala simu ya mjomba wake.
Namimi nikaona nitumie nafasi hii kumuuliza swali la msingi, “hivi itakuwaje kama mjomba wako akisema kuwa usiondoke hapa pemba, uolewe hapa pemba, na yeye anakupatia fedha na biashara zake zote ukae hapa pemba” nilimuuliza Jessenia na hapo alicheka kidogo, “unadhani hiyo itasaidia, siwezi kubakia hapa Pemba, labda na wewe ubakie, hata kama ninge kabidhiwa nyumba zote za chake chake, labda kama tungebakia wote mimi na wewe, vinginevyo uwe umeniacha, hata hivyo nadhani nitakuwa nimekufa kwa kihoro cha kuachwa” alisema Jessenia na hapo wote tukacheka kwa pamoja, huku tuna katiza eneo la msikitini karibu na soko kuu la chake chake, “unakumbuka hapa ulinikimbia” alitania Jessenia, huku tunaendelea na safari, “umezidi kuwa mzuri kama jini” nilimtania Jessenia na tuka cheka tena, niliendesha gari taratibu, huku tuna ongea hili na lile, tukitaniana na kucheka kwa furaha, giza lilikuwa limeshaanza kutanda.
Naam wakati namaliza barabara ya Markiti, na kuingia barabara ya mkoani Wete, nikagundua kuwa kuna pikipiki inatufuata nyuma yetu, ilikuwa ni ile ile vesper, iliyokuwa inatufwatilia toka asubuhi, sikutaka kumjulisha Jessenia kuhusu usindikizaji huo, zaidi niliongeza mwendo kuingia barabara kuu kuelekea macho manne, huku kikipita kimya kifupi, mimi nilikuwa namtafakari huyu jamaa mwenye Vesper, ya kwamba nimfanyaje ili anisaidie katika kazi yangu, sikujuwa Jessenia anawaza nini, lakini yeye ndie alievunja ukimya, “yani leo nitalala usingizi mzito sana, maana umenichosha kweli kweli” alisema Jessenia, huku anacheka kivivu, “kwanini Jesse?” nilimuuliza swali la kijinga, maana alisha fafanua, kuwa nimemchosha, “we unadhani ulicho nifanyia kidogo, yani wewe ni mtundu kweli, nilikuwa nasikia tu wazungu wanalambana huku, leo ndiyo nimeona” alisema Jessenia, huku anaonyesha kwa mkono sehemu zake za siri, wote tukacheka kidogo, kisha kikapita kimya kifupi, mpaka tulipo ifikia kona ya macho manne, “hivi Eric ndivyo unavyo wafanyiaga wanawake wako?” aliuliza Jessenia…….….. ENDELEA.



KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE: “yani leo nitalala usingizi mzito sana, maana umenichosha kweli kweli” alisema Jessenia, huku anacheka kivivu, “kwanini Jesse?” nilimuuliza swali la kijinga, maana alisha fafanua, kuwa nimemchosha, “we unadhani ulicho nifanyia kidogo, yani wewe ni mtundu kweli, nilikuwa nasikia tu wazungu wanalambana huku, leo ndiyo nimeona” alisema Jessenia, huku anaonyesha kwa mkono sehemu zake za siri, wote tukacheka kidogo, kisha kikapita kimya kifupi, mpaka tulipo ifikia kona ya macho manne, “hivi Eric ndivyo unavyo wafanyiaga wanawake wako?” aliuliza Jessenia…….….. ENDELEA..
Huku akicheka cheka kwa aibu, “kuwafanyia nini?” nilimuuliza kwa kumtega japo nilisha juwa ana maanisha nini, wakati huo napunguza mwendo na kukata kona kuingia barabara ya wawi, “kuwalamba huku” alisema Jessenia, huku anaonyesha sehemu zake za siri kwa mkono wake, kama alivyofanya mwanzo, “hapana Jesse, uju wewe ndio mwanamke wa kwanza kukufanyia hivyo” nilimjibu, japo nilikuwa najuwa namdanganya, maana mchezo huo nilijifunzia Urusi nikiwa na masomoni, kwa mschana mmoja wa kirusi, ambae alikuwa mpenzi wangu kwa muda wote wa miezi sita niliyokuwa huko, “kweli! na kwanini ufanye hivyo kwangu tu?” aliuliza Jessenia kwa sauti ya mshangao iliyochanganyika na mstaajabiko wa raha, jibu lilikuwa karibu kabisa, “ujuwe nini Jesse, japo nimetembea na wanawanawake wachache sana katika maisha yangu, lakini kati ya wote, hakuna mwenye uzuri unaokufikia, isitoshe una (nilitaja jina la sehemu zake za siri) nzuri sana” hapo Jessenia akaachia kicheko flani cha raha sana huku anajiegemeza kwenye seat ya gari, na kuziba uso wake kwa viganja vyake vya mkono vilivyo jaa pete za kung’aa, “unasema kweli Eric?” aliuliza kwa sauti iliyoambatana na kicheko chake cha raha, “sasa je, yaani natamani kama vile muda wote ningekuwa na….” nilisema huku nikishindwa kumalizia kuongea nilicho maanisha, japo yeye alinielewa, na kuangua kicheko, “kwani huchoki, mbona mimi nasikia mwanaume akimaliza mara moja lazima apumzike sana” alisema Jessenia, wakati huo tuna katiza Wawi Messi, “inategemea, we unadhani nitachokaje mbele ya (nilitaja kiungo cha kike) nzuri kama yako?” nilisema hivyo huku na tazama kwenye side mirror, nakuweza kuona magari mawili nyuma yangu, huku nyuma kabisa kukiwa na ile Vesper, “Eric bwana, we mkorofi haswaa” alisema Jessenia huku safari ikiendelea.
Naam njia nzima tuliongea hili na lile, tukicheka kwa furaha, pikipiki ile aina ya Vesper haikuacha kutufuata mpaka tulipofika Green House, ile pikipiki ilinyoosha kufuata barabara ya vitongoji, nikaoina imeenda kusimama mita kama mia mbili mbele, niliona hivyo kutokana na mwanga wa taa ya nyuma ya pikipiki ile, nikajuwa lazima kuna jambo wanajaribu kulifanya, hivyo natakiwa kuwa makini zaidi.
Tuliingia ndani ambako tulitoka mida ya saa mbili za usiku tukiwa tumesha fanya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupeana dudu, kitu ambacho Jessenia andie aliekichokoza, baada ya kuomba anisindikize bafuni, ambako aliingia akiwa amevua nguo zote na kushindwa kuvumilia kuiangalia dudu, pasipo kupita kwenye ktumbua chake, na mimi sikumuacha nilimfanyia kila alichopenda kufanyiwa, nae alionekana kufurahi zaidi, nilihofia asije akang’ang’ania kulala hapa Green House, sijui nitamtoaje, lakini baadae nilipuuzia mawazo hayo, kwamba itokee Jessenia kukataa kwenda nyumbani kwao kwaajili ya dudu, maana kesho nayo ni siku.
Baada ya kumaliza kupeana dudu, mwisho tulioga kwa pamoja na kuvaa kisha tukaondoka zetu kurudi macho manne, ile pikipiki ilitufuata kama kawaida yake, ilitufuatilia mpaka tulipofika macho manne, ambapo sikutaka tukae sana pale kutokana na yule jamaa nilimuona akitufuatilia kwa karibu, na yeye akijifanya kununua samaki na mikate, hivyo tulinunua vyakula na kuingia ndani ya gari na kuanza kula, huku tukifanyiana michezo ya utani wa kimapenzi, kama vile kulishana pia kuna wakati tulitekenyana, tuliongea na kucheka kwa furaha, huku tukishushia juice ya bungo.
Wakati huo nilikuwa namuona yule jamaa wa pikipiki, akizunguka zunguka eneo lile, ni wazi kwamba hakuwa na cha kufanya, zaidi ya kutufuatilia sisi tunafanya nini, nilimuona akijaribu kuchungulia ndani ya gari, ambalo vioo vyake vilikuwa tinted, yaani vilikuwa vya giza, hakuweza kuambulia kitu, ila mimi niliekuwa namtazama tu, lakini sikumshtua wala kumueleza Jessenia kuhusu huyu jamaa aliekuwa anazurula nje ya gari, ambapo pia kulikuwa na watu wengine wengi.
Dakika kama kumi na tano baadae, niliweza kumuona huyu jamaa mwenye ndevu nyingi, akisogea pembeni na kuanza kuongea na simu, alikuwa mbali kidogo na pikipiki yake, hivyo nikawasha gari haraka na kuondoka kwa speed huku namuona yule jamaa akikimbilia kwenye vesper yake mpaka naikamata barabara ya kuelekea chake bado jamaa hakuwa ameifikia Vesper yake, na mpaka natokomea kuelekea upande huo wa chake sikuona dalili ya kufuatwa na mtu yoyote, “mbona ghafla Eric, umechoka kukaa na mimi eeh?” aliuliza Jessenia, wakati naingia kwenye ile njia ya kuelekea Msingini, kwa kina Jessenia, “mh! unadhani kuna siku itatokea nikachoka kukaa na wewe Jesse, sema nnimeona nikupeleke nyumbani, ili kesho wasikuzuie kutoka nyumbani, si unajuwa mjomba alikuambia urudi mapema” nilitumia kama kisingizio, Jessenia alitabasamu kidogo, “kwahivyo unahamu ya kukutana na mimi kesho?” aliuliza Jessenia, huku ananitazama kwa macho angavu na mdomo wenye furaha, “sasa je au ulipanga kesho tusikutane?” nilimuuliza Jessenia ambae hakujibu kitu zaidi ya kutabasamu.
Dakika mbili mbele tayari tulisha fika nyumbani kwa kina Jessenia, ambapo palikuwa tulivu kweli kweli, na mimi nilimkiss Jessenia, na tukaagana, tukipanga kuwasiliana baadae na mimi nikaondoka zangu kurudi Wawi Messi, wakati nakatiza kwa mzee Mangeu nilijaribu kutazama kama ningeomuona mzee Zidadu, au bwana John Joseph, jina ambalo wengi hawakuwa wanalifahamu, lakini sikuona dalili ya uwepo wa mzee huyo, nikakanyaga mafuta kuondoka zangu, huku njiani nikijaribu kuangalia kama nitakuta nafwatiliwa na jamaa mwenye Vesper, lakini sikumuona, hata nilipofika macho manne nilijaribu kumtazama yule mandevu aliekuwa anatufuatilia sikumuona, mimi nilienda moja kwa moja Wawi Messi, ambako nilikuta magari machache, ila kulikuwa na utofauti kidogo, maana licha ya lile gari la jeshi, ambalo leo nadhani hakuwa anaendesha mwasenga, pia niliweza kuyaona magari matatu ya kiraia, likiwepo gari aina ya Jeep ambalo niliwahi kumuona nalo Ussi hapa hapa Messi, pia kulikuwa na gari la polisi, lile alilokuwa nalo insp Aroub kule shuleni nyakati za mchana, hivyo lazima insp Aroub atakuwa hapa, na anataka kuonana na mimi, kitu ambacho kisingewezekana maana Ussi nae atakuwepo hapa na kama angeona naongea na insp Aroub na ukichukulia tayari insp alisha muona mzee Juma Mohamed, kuuliza kuhusu wafanyakazi wa Ussi, ambao ni washiriki wa mauwaji, sasa basi kwa namna yoyote lazima insp Aroub atakuwa anafuatiliwa na watu wa Ussi, hapo nikapiga hesabu za haraka, nikapata wazo. “hivyo nikatoka nje ya gari na kulock milango, lakini kabla sijaaanza kutembea kuelekea kwenye jengo la messi ambako nilipanga niingie upande wa ukumbi wa chakula, nikasikia vishindo vikija kwa kasi nyuma yangu, niligeuka kwa haraka sana, huku mkono wangu ukiwa kiunoni, kwenye mkanda wa suruali tayari kuchomoa AGP (automatic gun pisto) yangu………….….. ENDELEA..



KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SITINI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TISA: sasa basi kwa namna yoyote lazima insp Aroub atakuwa anafuatiliwa na watu wa Ussi, hapo nikapiga hesabu za haraka, nikapata wazo. “hivyo nikatoka nje ya gari na kulock milango, lakini kabla sijaaanza kutembea kuelekea kwenye jengo la messi ambako nilipanga niingie upande wa ukumbi wa chakula, nikasikia vishindo vikija kwa kasi nyuma yangu, niligeuka kwa haraka sana, huku mkono wangu ukiwa kiunoni, kwenye mkanda wa suruali tayari kuchomoa AGP (automatic gun pisto) yangu………….….. ENDELEA..
Lakini nilimuona babu Mangeu, aliekuwa karibu kabisa na mimi huku akinionyesha ishara ya kuwa mtulivu, na mimi nilitulia na yeye akanisogelea mpaka pale niliposimama, yani ubavuni mwa gari, “tazama kule” alisema Mangeu, huku anaonyesha barabarani upande wa macho manne, ambako nilimuona bwana Mandevu akiongea na simu.
Sikujuwa kwanini Mandevu alinionyesha huyo jamaa, ambae alinifwatilia toka mchana, je inawezekana Mangeu anamfahamu, na amegundua kuwa ananifwatilia, “vipi amefanyaje?” nilimuuliza Mangeu, ilikufahamu anacho fahamu juu ya mtu yule, “yule jamaa amekuwa akimfuatilia Jessenia toka asubuhi alipokuwa anatoka nyumbani” alisema Mangeu, ambae alisema kuwa baada ya kumwona yule kijana anamfuatilia Jesseni, na yeye akaamua kufuata lakini walimpotea baada ya Jessenia kuingia kwenye gari langu na kuondoka kuelekea upande wa madungu, huku yule jamaa akielekea upande wa sokoni, “niliwaacha nikijuwa kuwa tayari amesha wakosa, lakini haikuwa hivyo” alisema Mangeu, ambae aliendelea kueleza kuwa, “mida ya saa kumi na moja za jioni, nilisikia taarifa flani ya tukio la kushangaza, linalofanana na tukio moja la jana usiku, kuna mtu alikutwa amekufa huko gombani, mtu mwenyewe ni mfanyakazi wa Ussi, ilishangaza sana amekufa kifo ambacho walikuwa wanakufa wale wanaume wanao mfuata Seni” Mangeu alielezea kuwa hata mtu aliekufa jioni hii maeneo ya Tibirinzi pia, alikufa kifo kama hicho, “ila kitu cha kushangaza nae ni mfanyakazi wa Ussi, sasa nilipokuwa na kuja kukueleza hilo nikakukosa, sasa nikiwa na rudi nikasema nipitie hapa Messi kama ninge waona ndio muda ambao niliwaona munapita kuelekea Vitongoji na huyu bwana anawafuata, nae ni mfanyakazi wa Ussi” alieleza mangeu ambae mwishoni akaniachia swali, “unadhani kuna mahusino kati ya hivi vifo na Ussi?” aliuliza Mangeu, ambae muda wote alikuwa anaongea kwa sauti ya chini, ni kweli ilitakiwa kumuweka wazi Mangeu, ili awe makini na Ussi, lakini kwa sasa nililazimika kuangalia kama ninaweza kukutana na mzee Aroub, pasipo Ussi kujuwa, “mzee sikia tuna mengi ya kuongea, lakini sio wakati huu, kuna jambo nahitaji kulishughurikia kwa sasa, cha kufanya niache kwanza nimalize hapa, halafu tutaongea, ila asituone mtu yoyote” nilimueleza Mangeu, kisha tukaagana na yeye akatoka kuelekea upande wa barabarani, na mimi nikaelekea upande wa ukumbi wa chakula, ambako nilimkuta yule askari anae shughurikia maswala ya chakula akiwa anamalizia kufanya usafi, ni wazi walisha maliza kula, “Ticha naona leo umekumbuka kuja kula” alisema yule askari, ambae kwa umri alikuwa amenizidi kidogo, “hapana bro nimeshakula sema nini kuna mtu nataka nimchungulie kule ukumbini, nione kama yupo au laa” nilisema kisha nikamuomba anionyeshe sehemu ambayo ninaweza kukaa na kuchungulia ukumbini, “ipo huku, nifuate” alisema yule askari huku anaelekea upande wa ndani kabisa wa jengo lile, ambako kulikuwa na korido refu, ambalo nilifuata mpaka mwisho, ambako kulikuwa na milango miwili, yani kushoto na kulia, na yeye akafungua mlango wa kushoto, “unaweza kutumia dirisha la chumba hiki” alisema yule askari, huku akinionyesha chumba kile ambacho kilikuwa na giza nene, hakikuwa na kitu chochote, ikionyesha wazi kuwa hakukuwa na mtu anaekitumia, “asante bro” nilimshukuru yule askari, ambae aliondoka zake na kuniacha mimi nikisogea dirishani, ambapo niliweza kuona ukumbi vizuri kabisa na kwa uwazi mkubwa.
Naam siku tumia muda mrefu kumuona insp Aroub, akiwa amekaa meza moja na mwenzie mmoja ambae ni yule dereva aliekuwa amekuja nae kule shuleni, nikatazama vizuri mule ndani nikaweza kuwaona watu wengine ninao wafahamu, akiwepo Malambo, Mwasenga na mke wake, pia nilimuona Ussi akiwa amekaa kwenye ile kona ambayo anapenda kukaa kila siku, leo hakuwa peke yake, ila alikuwa na mwanamke huku meza yao ikiwa imetapakaa vyupa vingi vya pombe, huku mara kwa mara akimtazama insp Aroub, aliekuwa anakunywa soda yeye na dereva wake, hapo nikakumbuka kitu, nikatoa simu mfukoni na kukibofya ili niweze kuitumia, lakini hapo ndipo nilipo gundua kuwa, simu hii sikuwa nimeitumia kwa muda mrefu sana, maana nilikuta missed call nyingi sana toka sehemu mbali mbali, ikiwa ni kwa mkurugenzi Winferad, insp Aroub, na mwalimu Aisha, na sio missed call moja au mbili, ni Aisha pekee ndie alie kuwa ana missed call tatu, wengine wote walikuwa na missed call zaidi nane.
Nikapiga simu kwa insp Aroub, huku namtazama, nikamuona anapokea simu “kijana vipi mbona hupokei simu, nilianza kupata wasi wasi juu yako” alisema insp Aroub, “samahani mzee nilikuwa mazoezini, sasa hivi ndio naikamata simu” nilimueleza insp Aroub, ambae alionekana kufurahi kuona nimempigia, “nimekubari kuwa wewe ni kiboko” alisema insp Aroub Huku anainuka toka pale alipokaa na kumuacha dereva wake peke yake, pale mezani akiendelea kupata soda na yeye akaelekea nje ya ukumbi ule mkubwa, hapo nikamtazama Ussi nikamuona ana mtazama insp Aroub huku anatoa simu yake na kuipiga, “kivipi mzee, mambo yameenda vizuri?” nilimuuliza insp, ambae kwa kupitia dirisha niliweza kumuona akitokomea nje ya ukumbi, “naweza kusema hivyo mwalimu ila ni vyema kama tukionana ili tuweze kuongea” alisema insp Aroub ambae pia alisema kuwa mchana alinitafuta sana, mpaka alipoelekezwa kwa mwalimu Aisha, ambae pia alisaidia kupiga simu na pasipo mafanikio, “na mwisho akasema kuwa nije nikusubiri hapa” nilishtuka kidogo, maana sikutaka Aisha ahusishwe na hili, “Aisha tena, vipi ulimueleza lolote?” nilimuuliza insp ambae alicheka kidogo, “haaaaa kaka, umesahau kuwa mimi ni polisi ninaeifahamu kazi yangu, sijamueleza chochote” alisema insp Aroub, ambae nilianza kupanga nae mchongo na kitu cha kufanya ili tuweze kukutana, nae akakubaliana na mimi.
Baada ya kumaliza maongezi na kutaka simu, nikamuona insp anarudi ndani ya ukumbi na kukaa kwenye meza yake, pale alipomuacha mwenzie, yaani yule dereva wake, na hapo nikatoka mule ndani nikamuaga yule askari msimamizi wa messi, halafu nikatoka nje nikipitia upande nilioingilia na kuingia ukumbini, ambako nilienda moja kwa moja mpaka kwenye meza aliyokuwa amekaa Mwasenga, “hoooo! ticha niaje kaka” alisema Mwasenga kwa sauti iliyochangamka, “kaka leo umekuwa adimu kinoma” nilimueleza Mwasenga, ambae alikuwa amekaa na mke wake, huku nikitazama meza ya Ussi kwa macho ya wizi, nikamuona anatazama upande wetu kwa Macho yaliyojaa hasira, “nilifika mida fulani, nikaona ume jifungia na mtoto ndani” alisema Mwasenga na mke wake akadakia “mtoto wa kipemba amekolea kweli kweli, mpaka anashinda Green House” maneno ya mke wa mwasenga yalitufanya wote tucheke, mpaka hapo nilishamaliza dakika zangu tano za kuwepo humu ndani, maana kuingia kwangu humu, ulikuwa ni sehemu ya mpango wangu na insp Aroub, ambae sikuwa nimemueleza nina mlenga nani, ila nilimuambia kuwa “lazima wauwaji watakuwa wanakufuatilia ili kuwa baini lazima niingie ndani na nikitoka akae dakika moja kisha na yeye atoke, kisha anifuate barabara ya vitongoji ambapo tuta tembea kilomita chache kisha tutasimama kama kuna mtu anatufuatilia basi tutakuwa tumesha muona” hivyo niliamua kuagana na Mwasenga kwamba naenda zangu Ahl Kahamis camp kupumzika, “hoooooo nimekumbuka ticha” alisema Mwasenga kabla sijaondoka, huku akinionyesha ishara ya kuwa nipunguze urefu kidogo, yaani nibonyee kidoo aninong’oneze jambo, kwa kuwa nilikuwa nime simama, ilinilazimu kusogeza sikio langu kwa Mwasenga aliekuwa amekaa kwenye kiti chake, “ujuwe nini Ussi alinipigia simu mchana, ndio maana nilikuja pale Green House, niliokuta umejifungia ndani sikutaka kukusumbua, maana nilijuwa tutakutana hapa kama kawaida” alisema Mwasenga, na pasipo kujari kama alikuwa anaendelea au vipi, nikamkatisha, “alisema kitu kuhusu mimi?” nilimuuliza Mwasenga kwa shauku ya kutaka kujuwa, “alichosema ni kwamba nikuambie kuwa ukae mbali na dada yake, vinginevyo kitakutokea kitu usicho kitarajia, na hata nilipoingia hapa na shemeji yako, amekuja kuniambia hivyo hivyo, tena anaonekana amechukia kinoma” alisema Mwasenga, na hapo mke wake akadakia, “lakini shem we achana nae mjinga yule, anamuoneaje wivu dada yake bwana” ndivyo alivyosema mke wa Mwasenga na wote tukachake kidogo, “ok! aina noma wacha niangalie nitafanyaje?” nilimueleza Mwasenga na mke wake, kisha nikawaaga kwa mara ya pili na kuondoka zangu, lakini wakati natoka nikamuona Ussi anatoa simu yake na kubofya namba, kisha akaweka sikioni, ni kwamba alikuwa anapiga simu kwa mtu flani, sikufuatilia zaidi maana nisingeweza kusikia chochote kutokana na umbali niliokuwepo.
Moja kwa moja nikatoka zangu nje na kueleke kwenye megesho ya magari lakini nilikuwa makini sana, kwa sababu nilisha juwa kuwa yule mandevu ambae mpaka sasa nilikuwa sijamjuwa jina, alikuwepo maeneo yale, japo nilipoingia ndani ya gari na kutazama kwa makini maeneo yale sikumuona, hapo nikahisi mambo mawili kama sio aliondoka zake, basi kuna sehemu amejibanza ili aweze kunifuata ili atimize alicho kikusudia.
Nikawasha gari na kuondoka zangu, huku na piga simu kwa mkurugenzi Winfried, ambae alipokea haraka kabla sijaingia barabara ya Vitongoji, “mpuuzi, hii simu yako ina uzito gani wa kushindwa kuwa nayo mkononi ili inapopigwa uisikie?” ndio neno la kwanza kuliongea mkurugenzi, “tulia kwanza nijieleze mzee, si unajuwa ninapilika nyingi ambazo aziihtaji kelele za simu” niliongea kwa kujiamini, maana nilikuwa na uhakika wa kufanikisha kazi, wakati huo nilikuwa napunguza mwendo kuingia barabara ya vitongoji, nakuelekea upande wa kulia ya upande wa kambini, “mjinga nadhani kuna nini zaidi ya kuwa na mwanamke we mpuuzi, kwani sikupata habari zako, nchi zote ulizokuwepo kipindi cha masomo yako, ulikuwa na wanawake wa kila kabira, bila shaka umesha mpata mtoto wa kipemba Fisher Man” alisema mkurugenzi, akimalizia na jina lanu jingine la utani, likiwa na maana ya mvuvi, niliitwa mvuvi wa wanawake, “hujakosea boss nimemnasa mtoto mkali kinyama nadhani utahusika kuja kupeleka barua” niimueleza mkurugenzi ambae alishindwa kuzuia kicheko, japo hakikuwa kikali sana, “acha upuuzi, sikukupigia simu unipe hiyo taarifa yako ya uzinzi, hebu niambie ulipo pata ile sumu ya hatari uliyoituma” alisema mkurugenzi, kwa sauti ambayo ilikuwa imeshaondoka kwenye utani, “nieleze kwanza ni sumu ya aina gani, na inafanyaje kazi” nilimuuliza mkurugenzi, ili anipe jibu lake….…. ITAENDELEA..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom