Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 2,117
- 5,240
- Thread starter
- #1,481
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SITINI NA TISA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NANE: vyema kama tutaondoka kimya kimya tukiwapiga chenga ya mwili, lakini swali likaja tutawatoroka vipi, lakini wakati nafikiria hilo nikakumbuka kuwa mzee Mangeu anaishi ndani ya shamba hili, hapo nikamshika mkono Jesssenia, “twende kwa mangeu” nilimueleza Jessenia kwa sauti ya kunong’ona, ambae mwanzo aliinuka na kutaka kunifuata lakini aliposikia nilichosema akasimama kwa kukataa kuelekea nilikomueleza, “hapana kwahuyo mzee hunipeleki, huyo ndiyo chanzo cha hayo yote” alisema Jessenia kwa sauti ya kunong’ona…….….…. ENDELEA..
nikamuonyeshea ishara ya kukaa kimya, maana tayari watu saba walikuwa wamesha karibia pale tulipokuwepo, maana walikuwa wanakuja usawa wetu, nikampa ishara ya kubonyea kisha tukaanza kutembea taratibu kuelekea upande wa kibanda cha babu mangeu, na baada ya kutembea kama mita kumi hivi, tukachuchumaa chini, maana tayari walishakaribia usawa ule, na kama tungeendelea kutembea wangetuona au kusikia vishindo, japo vilikuwa hafifu.
Naam nikweli mawazo yetu yalikuwa sahihi, maana wakati tukiwa chini tuliweza kuwaona watu wakikatiza usawa ule kuelekea mbele zaidi, japo kulikuwa na kijigiza kidogo, lakini tuliweza kuona vizuri tu maana mita kumi sio mbali sana, huku mimi nikijitahidi kuwatazama watu wale ambao sasa walikuwa wameondoa vitambaa usoni mwao, “tuongeze mwendo kabla hawaja fika mbali” alisema mmoja wao huku wanaendelea kutembea kwa haraka kukatiza eneo lile katika mtindo wa mstari mmoja, nikamuona Jessenia akinitazama kwa mshangao, huku anaonyesha kidole kule walikokuwa wale jamaa, kuna kitu alitaka kuongea nikamziba mdomo haraka sana, “tena huku wamejileta machinjio, yaani hakikisheni wote tunawamalizia huku huku” safari hii ilikuwa ni sauti ya Ussi, na hapo Jessenia akageuza uso wake kwa haraka kutazama upande ule, lakini ndio kwanza walikuwa wanamalizikia, “Eric njoo huku” tulishtuliwa na sauti ya Mangeu toka nyuma yetu, na hapo Jessenia akageuka kutazama ilikotokea sauti ile na kumuona Mangeu ambae alikuwa karibu yetu kabisa, akamtazama kwa macho ya mshangao, huku na mimi nikimtazama Jessenia kuona atavyo pokea jambo lile.
Kama mtu ambae alikuwa ameshikwa na mshangao mkubwa kupita kiasi, akanitazama mimi kama vile ananiuliza ina maana unafahamiana na huyu mzee, hapo na mimi nikampa ishara ya kutulia na hakuwa mbishi, nikamshika mkono kisha tukainuka na hapo pasipo kuongea lolote tukaanza kutembea kuelekea upande wa juu, tukitoka nje ya shamba la Mangeu na kuingia kwenye vichaka hafifu pembezoni mwa kuta ndefu za uzio za majumba yale ya kifahari, ikiwa ni upande wa nyuma, “ni hatari sana kwenu endapo mutaendelea kubakia hapa” alisema mzee Mangeu kwa sauti tulivu, huku akiongoza njia mimi nikiwa sambamba na Jessenia ambae bado alikuwa katika mshangao mkubwa sana, asielewa kinachoendelea kati yangu na Mangeu, “gari lako lipo wapi, au kuna ulazima wa kuwatafutia gari jingine?” aliuliza Mangeu, na hapo ndipo nilipokumbuka kutoa simu yangu na kumpigia Mwasenga, ambae hakuchelewa kupokea, na bahati nzuri kwetu, Mwasenga alikuwa pale Mess na kamanda aliekuwa ana muendesha alikuwa na wenzie wanaendelea kunywa bia, na alikuwa ni mmoja kati ya wageni waliofikia pale pale Messi.
Nikiwa naongea kwa sauti ya chini, nikimuomba aje anichukue kwenye eneo lile la karibu na njia ya kuingilia huku Msingini, “yani muda wote nilikuwa natazama simu kuona kama umepiga, inaoekana ulikuwa juu ya kifua eeh” alisema Mwasenga ambae kiukweli alikuwa na dalili zote za kwamba alikuwa amelewa, “tutaongea kaka, naomba ufanye haraka si unajuwa usiku huu” nilimueleza Mwasenga nikimsisitiza na kukata simu, wakati huo tulikuwa tunaendeelea kutembea huku Jessenia ni kama alikuwa hajaelewa elewa hivi, maana alikuwa anatushangaa na kumtazama mzee Mangeu kwa uoga, sijui alikuwa anawaza nini huyu mwanamke, ila kwa haraka haraka unaweza hata wewe msomaji kuhisi alicho kuwa anawaza Jessenia, kwamba wakati amegundua kuwa Ussi ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanatufukuza huku akiwa amemuona mtu anae mfahamu kati ya wale saba, pia anakuja kugundua kuwa mimi na Mangeu ni watu tunao fahamiana, na chakushangaza zaidi ni kwamba Mangeu anatoa msaada wa kututorosha pale Msingini.
Dakika kumi baadae tulikuwa tumeshaibukia barabarani, Jessenia akilalamika nyayo zina muuma, “umeona nilichokuwa namaanisha mzee” nilimuuliza mzee Mangeu, huku tukiwa tume simama pembeni sana ya barabara tukitumia maficho ya kichaka flani, “Eric sidhani kama huu ni wakati wa kuongelea hilo, japo nadhani Mashaka yangu yalikuwa sawa ” alisema babu Mangeu, na hapo Jessenia ambae alikuwa bado amenishika mkono akikaa ubavu wangu wa kushoto akijitenga kabisa na Mangeu akakosa uvumulivu, “munaweza kuniambia nini kinaendelea, maana nimemuona Ussi na wakina Mussa wakitufukuza na panga, sasa namuona Mangeu na wewe munafahamiana kuna kitu gani kinaendelea Eric” aliuliza Jessenia huku ananitikisa mkono, akitaka nimueleze kinachoendelea, nilimtazama Mangeu ambae alikuwa anamtazama Jessenia, huku anatabasamu, sasa kama ukibahatika kuliona tabasamu la Mangeu ndio ungetafuta pakutokea, maana sijui nifananishe na nini, ujuwe yale mapanga usoni kwa mzee huyu yalikuwa yame muharibu sana,
Jessenia alimtazama mzee Mangeu kwa Macho ya tahadhari, akimuona anavyo tabasamu, kisha akamsikia akiongea kwa sauti ya upole, “Jessenia hapa tulipo hatuwezi kuongea chochote ukanielewa, maana tuna muda mfupi sana” alisema Mangeu na kisha akanitazama mimi, “Eric naamini Jessenia yupo salama pamoja na wewe, hivyo hakikisha unamaliza hili salama na mimi siwezi tena kuwa hapa karibu, nitaenda kujificha sehemu mpaka kila kitu kiwe sawa” alisema Mangeu kisha akatoa kijimfuko mkononi mwake na kunikabidhi ni kitu mfano wa chupa bapa, nilisha juwa kuna umuhimu wa kumficha Jessenia na anatakiwa kufichwa mpaka usiku wa leo, nitakueleza baadae ilikuwaje cha msingi nenda na Jessenia mpaka Mantariff Lodge, mtakuta nimesha weka oder ya chumba, najuwa huwezi kukosa gari, ukikwama jambo lolote nijulishe, hizo kwenye mfuko ni fedha zitawasaidia, lakini usiku huu musilale maeneo ya hapa karibu, sasa hivi ni saa mbili kasoro munaweza kufika lodge mapema sana” alisema Mzee Mangeu na kumuacha mdomo wazi Jessenia, kwamba mzee Mangeu ndie wakuweka oder Mantariff, inawezekana vipi, wakati huo huo tukaona mwanga wa gari unatokea upande wa macho mane, sambamba na ngurumo ya gari, ambalo niligundua kuwa ni defender la jeshi.
Unapo taja Mantariff Loder, unazungumzia hotel moja kubwa ya kifahari yenye hadhi kubwa ya kimataifa iliyoko pemba kaskazini kwenye ras ya panga la mtoro, hivyo watalii na watu wenye fedha nyingi pekee ndio huenda mahali hapo kuenjoy na kula maisha, mimi nilisha wahi kufika, lakini ilikuwa ni kuangalia mazingira na kuendelea na safari zangu, “sawa mzee lakini kuwa makini ukae ukijuwa na wewe hawato kuacha salama endapo watakupata” nilimueleza mzee Mangaeu huku natokeza barabarani kusimamisha gari, ambalo lilikuwa limesha karibia, “nalijuwa hilo, na nimesha andaa mipango yote, usisahau kunipigia, hakikisha Jessenia anakuwa salama” alisema Mangeu, huku anaanza kutembea kuifuata njia ya kuelekea msingini ile ambayo hata magari yanapita, huku akimuacha Jessenia anashangaa jinsi babu Mangeu anavyoonyesha kumjali.
Gari lilisimama na sisi tukaingia ndani ya gari, na safari ikaanza kwa mwasenga kugeuza gari kuelekea macho manne, “hooo shemeji naona kama kawaida mnaeda Mess kula bata au?” aliuliza Mwasenga ambae alionekana amesha lewa tayari, “hapana tunahitaji kupumzika kaka, ila nahitaji gari lako” nilimjibu Mwasenga huku Jessenia akiachia tabasamu la kuzuga, maana bado alikuwa na maswali kichwani ambayo hayakuwa yamepata majibu, “gari mbona lipo tu, halafu nimelipiga kiwese cha kutosha jioni hii, si unajuwa kukiwa kuna wageni kama hivi mafuta yana kuwa mengi sana” alisema Mwasenga ambae alikuwa amevalia sale za kazi, zile zenye mabaka baka, yaani combat, huku anamalizia kuliweka gari sawa na kulielekeza upande wa Macho manne na kukanyaga mafuta kuelekea upande huo, itakuwa vuzuri sana, maana nataka niende sehemu moja hivi na shemeji yako nikale kuku kidogo” nilimueleza Mwasenga, wakati huo tumesha tembea kama mita mia moja hivi.
Naam na hapo ndipo kwa msaada wa gari tuliweza kuwaona vijana Saba wanatokea kichani, na kuibukia barabarani, mimi na Jessenia ambao tulikaa seat ya mbele tukatazamana, maana tuliwatambua kuwa ni wakina Ussi, “ndiyo maana sijamuona mess leo kumbe anamishe mishe zake” alisema Mwasenga huku anapunguza mwendo akitaka kusimamisha gari amsalimie Ussi, “twende twende usisimame” nilimnong’oneza Mwasenga nae akakanyaga mafuta huku anapiga honi za kuwasalimia wakina mwasenga, “nilitaka nisahau wivu wa Ussi kwa dada yake” alisema Mwasenga akimalizia kwa kicheko, na sisi tukacheka huku tukigeuza vichwa vyetu kutazama tulikotoka tuka waona wakina Ussi wakiwa wamesimama wanalitazama gari, mpaka tulipo tokomea.
Dakika baadae tayari tulikuwa tumeshafika wawi mess, ambapo tulichukuwa gari jingine, yaani lile Toyota spacio na kuondoka zetu kueleka Ali Khamis Camp, ambako nilipanga nika lchukuwe lap top yangu ambayo ina mambo mengi ya kazini, pamoja na nguo chache kisha tuje macho mane tuchukue nguo za kubadili za Jessenia, kisha tuanza safari ya kaskazini, ambako tungetumia kama lisaa lizima maana kipindi kile barabara zilikuwa hazina lami, lami ilikuwa inaishia wete mjini.
Naam ile tunaikamata barabara ya vitongoji Jessenia akanipachika swali, “Eric sasa unaweza kuniambia kinachoendelea?” aliuliza Jessenia aliekuwa amekaa kwenye seat ya pembeni yangu, “nitakueleza kila kitu Jesse, sikuweza kukueleza mwanzo, maana usinge amini” nilimueleza Jessenia kwa sauti tulivu, ili kumtuliza na yeye mwenyewe, wakati huo huo nikaona mwanga wa taa ya pikipiki ukija kwa kasi nyuma yetu, mwanzo sikuitilia mashaka ile pikipiki, lakini baada ya kufika njia panda ya wawi ambapo tuliifuata ile bara bara ya vitongoji na ile piki piki kutufuata ndipo nilipoitilia mashaka, hapo nikapunguza mwendo ili niitazame kama ni pikipiki ya Mandevu au la.
Ukweli Mandevu hakuwa na umakini wakufuatilia mtu, maana alikuja karibu yetu na kupunguza mwendo akiwa mita kama ishirini nyuma yetu, hapo nikaweza kumuona vyema kabisa kuwa ni yeye Mandevu, “simuachi huyu mjinga” nilisema hivyo huku naongeza mwendo, nikamuona Jessenia nae anatazama nyuma kutazama nani anae tufuata, kwa kuwa nilikuwa nimesha sogea mbali kidogo hakuweza kumuona kutokana na mwanga wa taa wa ile Vesper.…. ENDELEA..
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SABINI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NANE: Ukweli Mandevu hakuwa na umakini wakufuatilia mtu, maana alikuja karibu yetu na kupunguza mwendo akiwa mita kama ishirini nyuma yetu, hapo nikaweza kumuona vyema kabisa kuwa ni yeye Mandevu, “simuachi huyu mjinga” nilisema hivyo huku naongeza mwendo, nikamuona Jessenia nae anatazama nyuma kutazama nani anae tufuata, kwa kuwa nilikuwa nimesha sogea mbali kidogo hakuweza kumuona kutokana na mwanga wa taa wa ile Vesper.…. ENDELEA
“Ni nani huyo” aliuliza Jessenia, huku ananitazama kwa macho yaliyojaa wasi wasi, yule jamaa mwenye mandevu ulie sema ni mfanyakazi kwenye majahazi ya Ussi” nilimuambia Jessenia huku nazidi kuongea mwendo, “kha sasa kwanini anatufuata” aliuliza Jessenia, huku anageuza shingo yake kutazama tulikotoka, yaani nyuma na kwa kupitia kioo cha nyuma aliweza kuona mwanga wa pikipiki kwa mbali ukionyesha kwamba mwendesha pikipiki alikuwa anajitahidi kutufuata kwa kasi, hapo sikumjibu Jessenia, nikazidi kukanyaga mafuta huku kichwani nikiwa nimesha panga kitu cha kumfanyia, “sasa nime shajuwa kwanini mjomba alikuwa anajuwa kila tunachofanya, kumbe anawatuma watu wananifuatilia” aisema Jessenia kwa sauti ya ung’amuzi iliyosheheni hasira za hali ya juu, bado sikusema lolote, maana nilijuwa ingezuwa maswali mengi na kuchochea kumueleza kile ambacho nilitakiwa kumueleza baadae, maana kwa sasa nilikuwa na kazi ya kufanya na huyu bwana Mandevu, “umejuwaje kama ni yeye na anatufata sisi?” aliuliza Jessenia, ambae wasi wasi wake ulizidi mara dufu, “toka jana asubuhi, na pia kuna wengine walikuwa wanatufuatilia toka siku ya kwanza ulipokuja huku kwangu” nilimjibu, huku napunguza mwendo kuingia kona ya ngerengere, ambayo ni kona kali sana, nilipoimaliza nikakanyaga mafuta kwa nguvu na kulifanya gari likimbie kwa speed mia ishirini kwa saa, huku nikichungulia kwenye side mirror sikuona dalili ya mwanga wa taa za pikipiki, niwazi kuwa tulikuwa tumemuacha mbali, niliendesha gari kwa speed kali sana mpaka tulipofika eneo linaloanza kijipori kidogo nilizima taa za gari na kupunguza mwendo kisha nikaingiza gari pembeni ya barabara nikigeuza nilikotoka, lakini nikiwa nje ya barabara, “Eric, unataka kufanya nini, akituona ataenda kumuambia Ussi” alisema Jessenia huku akionyesha wasi wasi mwingi, “kwani unaogopa akimuambia?” niliuliza kwa kumtega ili kujuwa anaelewa nini juu ya kilicho tutokea mida ile, wakati huo gari lina unguruma lakini nilikuwa nimezima taa zote na gia nimeweka P, sikuweka hand brake, maana sikutaka aone taa yoyote, “kwani we hujamuona Ussi alivyotaka kunipiga na panga, yupo na wale wageni wao” alisema Jessenia na hapo nikajuwa kuwa tayari amesha anza kuona hatari iliyopo mbele yake, na kwamba sitokuwa na kazi ngumu kujieleza mbele yake, “hivi wale wengine ndio wageni toka Unguja?” nilimuuliza Jessenia, “ndiyo ni hao hao, nimewaona kwa macho yangu, na Ussi ndie alitaka kunikata na panga, nimegundua pale tulipo wamulika na taa za gari” alisema Jessenia, akimaanisha kuwa alimtambua mtu alietaka kumkata na panga kuwa ni Ussi, baada ya kumuona akiwa hajajiziba uso, wakati ule tukiwa kwenye gari la Mwasenga, “unadhani kwanini Ussi alitaka kukukata na panga?” nilimuuliza swali la pili la kumtega Jessenia, ambae bado alikuwa na wasi wasi na hofu kuu moyoni mwake, “yeye na mjomba watakuwa wamechukia nilivyo kataa kuolewa na Mussa, halafu pia wamechukia waliponiona nipo na wewe, ndio maana hata walituita wezi” alisema Jessenia, na wakati huo huo tukaona mwanga wa taa ya piki piki, yani jicho moja ukija kwa kasi sana upande wetu, “huyooooo anakuja, Eric wapigie simu wanajeshi waje wamkamate, wanaweza kutuuwa hawa” alisema Jessenia huku anachukuwa begi langu toka seat ya nyuma kwa lengo la kupekuwa ili atoe simu, “Jesse unaweza kutulia kwajili yangu, amini siwezi kuruhusu mtu akuguse” nilimueleza Jessenia nae akaacha begi na kutulia, akiitazama Piki piki.
Naam nilihesabu mwendo wa pikipiki, ambayo ilikuwa inakuja kwa kasi sana, na ilipokaribia kwetu kwa umbali wa mita mia moja nikaingiza gia ya kuendeshea yani D, halafu nikahesabu, moja mbili tatu, huku Vesper ikiwa inakuja kwa kasi na kubakiaza kama mita ishirini, nikawasha taa zote yaan full, ambao ulimpiga usoni Mandevu na kumchanga kidogo, halafu kama haitoshi nikakanyaga mafuta kwa nguvu kama naingia barabarani, halafu nikasimama, hapo nikamuona Mandevu akishika brake za ghafla, ambazo zilimyumbisha na kumfanya akose uelekeo na kujibwaga kwenye lami, kisha kuseleleka akisota juu ya lami hiyo sambamba na piki piki yake, kwa msoto wamita kama ishirini hivi, wakati huo tayari nilikuwa nimesha shuka, toka ndani ya gari, nikiwa nimezima taa za gari, na kukimbilia upande ilipoelekea pikipiki ambako kulikuwa na giza maana hata taa ya pikipiki ilikuwa imesha zima, nadhani kwaajili ya ule mdondoko.
Nilipokaribia niliweza kumuona Madevu akijichomoa toka kwenye pikipiki iliyomkandamiza mguu mmoja wa kulia na kufanikiwa kusimama huku akiwa anachechemea na aliponiona namfuata akasimama na kunitazama kwa hasira, “unaweza kuniambia ni kwanini munafanya mauwaji kwa wanaume wanaotaka kumuoa Jesse?” nilimuuliza yule jamaa, yani Madevu kwa sauti tulivu, huku nazidi kumsogelea Mandevu ambae alionekana kuwa katika maumivu makali sana ya mguu, ambao niliona ukiwa unavuja damu kwa mchupuko mkubwa ulioupata, Mandevu hakujibu lolote zaidi alijipapasa kwenye paja la mguu wa kushoto, ambao haukuwa umeumia kama ule wa kulia, kisha akaingiza mkono kwenye upido wa nusu suruali yake maeneo ya kiunoni na kuibuka na kisu kirefu kinachong’aa kwa makali yake.
Ushikaji wa kisu wa Mandevu, haukuwa wakipiganaji, ushikaji ambao nilisha juwa atakitumia vipi kunishambulia, alishika kama vile anataka kukata mua, “ni vyema kama unge achana na hicho kisu halafu unijibu maswali yangu” nilimueleza Mandevu kwa sauti tulivu kama mwanzo, sauti hii ni silaha kubwa sana, hasa unapo pambana na mtu hatari, maana huonyesha wazi kuwa unajiamini, lakini haikusaidia kitu, niliweza kumuona Mandevu akivuta kisu chake kwa nguvu na kukileta kwangu kwaspeed kali sana, hapo niliudaka mkono wake kwaharaka na mkono wangu wa kushoto, huku naachia ngumi moja nzito kwa kumkono wangu wa kulia , ambayo ilitua usoni kwake usawa wa kati ya pua na mdomo, ambayo ilimlegeza na kumfanya ayumbe kidogo, lakini bado aling’ang’ania kisu chake ambacho kilishikwa na mkono wake wa kulia niliokuwa nimeushika kwa nguvu, hapo nikamvuta kwangu na kumzungusha kwa nguvu mfano wa mtu anaecheza music wa charanga na mpenzi wake, nae akaja usawa wa kifua changu akiwa ametazama kule nakotazama mimi, huku kisu alicho kishika mwenyee kikipita shingoni mwake na kuanza kurusha damu kwa nguvu, ilikuwa rahisi kumuuwa mandevu, lakini yenye kuhitaji moyo mgumu kama vile kumuibia kipofu, yaani ni rahisi sana, ila ukiwa na moyo wa huruma huwezi kufanya hivyo.
Nilipomuachia Mandevu nikamuona akipepesuka kama mlevi, kisha akajibwaga chini karibu na piki piki yake, hapo nikarudi kwenye gari haraka, na kuondoa gari kuelekea Vitongoji, sikuwasha taa mpaka tulipompita Mandevu na Piki piki yake sikutaka Jessenia ajuwe kilichotokea, “mbona amelala pale, kwani ameumia sana alivyoanguka?” aliulizaJessenia wakati tuna pita alipolala Mandevu, “achana nae ameshindwa hata kunieleza chochote” nilimjibu Jessenia, huku nakanyaga mafuta na kuwasha taa za gari, maana tayari tulikuwa tumeshapita eneo lile, lenye picha ya kutisha ya Mandevu aliechinjwa kama mbuzi, picha ambayo kama Jessenia angeiona sidhani kama tungeweza kuelewana kwa muda huu, “lakini Eric unakumbuka babu Mangeu alisema tukalale Mantariff, yaani huku kwako lazima watatufuata tu” alisema Jessenia kwa sauti ya uoga, “huku kuna vitu naenda kuchukuwa, kisha twende zetu Mantariff” nilimueleza Jessenia.
Ilikuwa hivyo, green house nilitumia muda mchache sana nikichukuwa lap top na vifaa vyote vya kazi, ikiwa kisu nguo chache, viatu na fedha za kutosha, japo nyingine alisha nipatia babu Mangeu, nilitandika kitanda vizuri na kuzima taa za ndani, nikafunga mlango kisha tukaondoka zetu nikiwa nimevaa tisht nyingine maana lile la mwanzo lilikuwa limechafuka damu za Mandevu, lakini sikuliacha nililihifadhi ndani ya begi kwenye mfuko wa pembeni.
Tulitoka kwa mwendo wa speed lengo langu likiwa ni kuwahi kupita pale Ngerengere, kabla watu hawajaona mwili wa Mandevu na kuita Polisi, lakini haikusaidia lolote, maana tulipokaribia eneo lile nikaona kuna mwanga wa taa za gari, na mbaya zaidi tulikuwa kama mita mia moja tu kufikia pale kwenye tukio, hivyo nikapunguza mwendo na kutembea mwendo wa kawaida kusogelea eneo la tukio, “watu wameenda kumsaidia” alisema Jessenia, kwa sauti ambayo bado ilikuwa na hofu, ni baada ya kuanza kuona watu wakiwa wamezunguka eneo lile ambalo lilikuwa linamulikwa na taa za gari, lakini mimi tayari nilisha gundua kuwa wale mbele yetu ni polisi, “Jesse nenda seat ya nyuma” nilimueleza Jessenia kwa sauti ya chini, huku nazidi kupunguza mwendo, japo tulikuwa tunazidi kusogelea eneo lile, ambapo nilimuona polisi mmoja mwenye cheo cha constable, akisogea barabarani na kutupungia mkono kutusimamisha, hapo nikapunguza mwanga wa taa za gari huku nasimama, wakati huo Jessenia akiwatayari amesha hamia seat ya nyuma.
Yule askari alisogelea kwenye mlango wa dereva, ambako nilikuwa nimekaa, nikashusha kioo , “habari kaka naona mupo kazini” nilimsemesha yule polisi kabla hajaniambia chochote, ndiyo kamanda si unajuwa kazi zetu ni sawa tu na nyie” alijibu yule polisi, akidhania kuwa na mimi ni askari wa jeshi la ulinzi, “unadhani mimi nikamanda basi, mimi ni mwalimu, sema ninakaa kambini” nilijibu huku tazama pale chini, ambapo tayari walisha uondoa mwili wa Mandevu na pikipiki yake na kabla yule polisi hajajibu kitu, akaongezeka askari mwingine , hapo moyo wangu ukalipuka kwa mshtuko, “Ticha Eric, afadhari nimekuona” ilikuwa ni sauti ya insp Aroub, ambae alikuwa amekuja moja kwa moja kwenye mlango wa gari, sasa walikuwa wawili, “salama tu mzee, naona leo upo busy sana” nilimjibu Aroub ambae kiukweli sikutamani mzee huyu agundue kama Jessenia yupo ndani ya gari, au kufungua mdomo wake kuongea lolote juu ya uchunguzi wetu na sikutaka Jessenia apate wazo la kumshitakia Ussi kwa insp Aroub, “busy kweli kweli, lakini ilikuwa muhimu tuonane, alienipa moyo ni Malambo, ambae alisema kuwa lazima ungekuja pale Mess kwa chakula cha jioni” hapo nilishaona dalili za maongezi ya muda mrefu, ambayo yange haribu mambo….…. ENDELEA..