KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA SITINI NA MBILI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MOJA: ukimpata muulize kwa kina, zaidi ya hapo unaweza kupata jambo la kukusaidia” nilishauri insp Aroub, na hapo nikawa kama nimejichongea, maana wakati naweka gari pembeni ili ni mshushe aingie kwenye gari lake, akaniuliza, “kijana nikuulize kitu, hivi wewe ni mwandishi, au mpelelezi toka Tanzania Secret Agent?” aliuliza insp Aroub, akiwa makini na uulizaji wake, ambao haukuwa na na dalili ya utani hata kidogo….…. ENDELEA..
lakini mimi nilicheka kidogo, “kwa hiyo mzee ninafaa kuwa mpelelezi?” nilimuuliza kwa sauti iliyojaa utani, na yeye akacheka kidogo, “nikweli waandishi ni wajuzi wa kufwatilia habari na kufichua yaliyo jificha, lakini kiukweli kwa upande wako umekuwa tofauti kidogo, maana ndani ya masaa machache nimeweza kugundua mambo mengi sana, ambayo nilishindwa kuyagundua kwa miaka mingi sana” alisema insp Aroub, wakati huo gari la polisi lilikuwa lina simama nyuma ya gari langu, “sidhani kama una sababu ya kuwaza hivyo, cha msingi fanya nilicho kuambia ili kupata majibu” nilimuambia mzee Aroub, ambae alicheka kidogo, “haya bwana Eric, nadhani kuna majibu zaidi nayahitaji, moja kuhusu muuwaji, na sababu ya kufanya mauwaji, pili nitahitaji kujuwa wewe ni nani na una kazi gani haswaa ukiachilia ualimu na hiyo ya uandishi” alisema kwa utani insp Aroub, huku anashuka toka kwenye gari langu, huku anacheka kidogo, “ndio maana mara nyingi huwa tunaogopa kulisaidia jeshi la polisi” nilimtania insp Aroub, na hapo tukacheka kwa pamoja, huku akiwa amesimama nje ya gari, na mlango bado upo wazi, “basi bwana Eric, nikuache uka pumzike, kesho asubuhi nitaenda kwanza kule pwani, kisha saa mbili asubuhi nitaungana na msafara wa RPC, kuelekea uwanja wa ndege, kuna wageni tunaenda kuwapokea” alisema Aroub, kisha akafunga mlango wa gari, na mimi nikaondoa gari langu kwa speed huku natazama kwenye side mirror, na kumuona insp Aroub anaingia kwenye gari la polisi, ambalo liliondoka na kuelekea mjini, yani tulikotoka na mimi nikakanyaga mafuta kuelekea vitongoji, lakini mpaka nafika sikuweza kumuona madevu, yaani muendesha vesper.
Naam nilipofika Green House na kuona Vesper ubavuni mwa nyumba ndipo nilipokumbuka juu ya kuwa nilikuwa na ahadi na babu Mangeu, kwamba tukutane nje ya pale Wawi Messi, na alipotazama vizuri pale kwenye Vesper, nikamuona japo palikuwa na giza nikaweza kumuona mzee Zidadu akiwa nyuma ya Vesper ananionyeshea ishara ya kuingia ndani bila kumtazama, wala kumuongelesha, hapo sikuhitaji masomo ya ziada kuelewa alicho nieleza babu huyu, moja kwa moja nikaingia ndani ya nyumba na kutokea mlango wa nyuma, kisha nikazungukia kule alikokuwepo mzee Zidadu, ambae nilimkuta ametulia anatazama upande wa barabarani, “we mzee unamtazama nani huko barabarani?” nilimuuliza babu Mangeu kwa sauti ya kunong’ona, nae akashatuka na kunionyeshea ishara ya kukaa kimya, kisha akanionyesha kule anakotazama yeye, yaani barabarani upande wa kuelekea vitongoji,
Naam baada ya kuangalia vizuri na macho kuzowea giza, nikaweza kuona kitu kama kimvuli cha mtu, aliekaa kwenye pikipiki, alikuwa umbali wa mita kama mia mbili hivi, toka pale tulipo kuwepo mimi na mzee Mangeu, “nani yule?” nilimuuliza babu Mangeu kwa sauti ya kunong’ona, japo nilikuwa nimesha gundua kuwa yule alikuwa ni yule mandevu, “ni mpuuzi mmoja anaitwa Othman, ni mfanyakazi wa Ussi, mtoto wa Juma” alijibu Mangeu, huku akitazama kwa umakini sana, “unadhani anafuata nini huku” nilimuuliza Mangeu, ili nione kama kuna jambo amesha ligundua katika sakata zima la mauwaji yanayoendelea na familia ya bwana Juma Mohamed yaani mjomba wa bandia wa Jessenia, “weee ni hatari kubwa sana, hawa vijana nadhani kuna jambo wanalifanya, na ndio maana nimekuja kukueleza ili uwe makini” alisema mzee Mangeu, na kuanza kunieleza wasi wasi wake juu ya kile alicho kigundua.
Mzee Mangeu, aliniambia kuwa jana usiku wakati ananitafuta pale Wawi Messi, aliwaona vijana wawili wa Ussi, wakiingia na pikipiki, hivyo yeye akaona isiwe kesi akanyoosha huku Green House, lakini asubuhi akasikia taarifa ya kuwa mmoja kati ya vijana wale amekutwa ameuwawa huko gombani, na mida ya jioni akasikia kuwa mwingine tena ameuwawa, “we huoni kama kuna kitu kinaendelea hapo, na wote wameuliwa na jini” alisema mzee Mangeu, kwa sauti ya kunong’ona, ambayo ilionyesha mashaka makubwa, unadhani ni kweli mauwaji yana sababishwa na jini?” nilimuuliza Mangeu, ambae alitulia kidogo kama vile anatafuta jibu, na baada ya sekunde kadhaa akanijibu, “mh! kijana hilo swali ndilo ninalo jiuliza kwa miaka mingi sana” alisema Mangeu, akionyesha kutofahamu jibu sahihi, “unadhani ametumwa na Ussi kunifuatilia?” nilimuuliza Mangeu, katika hali ya kuchunguza hisia zake juu ya kinachoendelea.
Wakati huo huo tukasikia pikipiki ikiwashwa, na tukatazama kule alikokuwepo Mandevu, tuka ona taa ya pikipiki ikiwa imewashwa, na kisha kuondoka kuelekea mjini, “huyoooo anaondoka zake mshenzi huyu, lazima Ussi amemtuma, yani ameng’ang’ania kuweka wivu kwa huyu Seni” alisema Mangeu kwa sauti iliyojaa chuki, wakati ile pikipiki ikipita usawa wa macho yetu, na kutokomea upande wa mjini, “unadhani kwanini Ussi ana kuwa na wivu sana kwa Jesse?” nilimuuliza’ mzee Zidadu, huku naanza kutembea kutoka kwenye maficho ya giza, huku mzee Mangeu akinifuata, “unajuwa ni kawaida kwa vijana wa pemba kuona wivu kwa dada zao hasa wanaotembea na vijana toka nje ya Pemba, ni angalau akiwa ametoka unguja, lakini wivu wa kijana huyu unashangaza sana, inafikia hatua nahisi bado huyu mshenzi anamtamani kutembea na Seni” alisema mzee Mangeu, akionyesha wazi kuwa hatamani kitu kama hicho kitokee, “kwani anafahamu kuwa Jesse sio dada yake?” nilimuuliza mzee Mangeu, wakati huo tulikuwa tumesimama sehemu ya mbele ya nyumba, ambayo ilikuwa inafikiwa na mwanga wa taa.
Naam kwa swali hilo, niliweza kumuona mzee Mangeu akinitazama kwa macho ya ung’amuzi, “kwanini umeniuliza swali kama hilo, au wewe ni mpelelezi?” aliuliza mzee Mangeu, kwa sauti ya mshangao huku ananitazama kwa macho ya ung’amuzi. “kwanini niwe mpelelezi, au kuna jambo unalijuwa halafu unanificha?” nilimuuliza kwa namna flani ya kumtega, ili mzee huyu alie onekana kuwa amegundua jambo aweze kufunguka anacho kujuwa, “hapana kijana, ila swali lako lime nifanya nihisi kitu, inawezekana kabisa huu ni mpango wa Juma familia yake, kwamba Seni asiolewe na mtu yoyote, au aolewe na Ussi ili mali za Seni, wabakie nazo wao, ndio maana wakati ule alitaka wawili hawa wafanye upuuzi” alisema Mangeu, ambae ungemuona wakati huu, ungefahamu kuwa alikuwa amepata jambo jipya kabisa katika maisha yake, “kwani mzee hukuwahi kufikiria hivyo toka mwanzo?” nilimuuliza mzee Zidadu, kwa sauti ya udadisi, “yaani sikuwahi kufikiria kabisa, ujuwe leo nimewaona wana hangaika sana juu ya hawa watu walio uwawa, na pia nadhani polisi wameshaanza kuwasonga songa, leo nimuona Aroub amekuja pale nyumbani” alisema mzee Mangeu, huku bado akiwa katika hali ya mshangao, “ok! sasa unafikiria nini?” nilimuuliza Mangeu, ili kusoma alichokifikiria baada ya kugundua jambo hilo, “hapo kwa kweli ni kufanya mpango ukajitambulishe haraka kama unataka kumuoa Seni, naamini hato kataa kuolewa na wewe, na baada ya hapo muondoke kuelekea dar” alisema Mangeu, nilipata jibu la kuwa bado mzee Mangeu hajajuwa kinachoendelea kwa upande wa mauwaji, lakini sikutaka kumfanya aelewe, “lakini mimi siwezi kuondoka haraka hapa Pemba, kwasababu bado sija maliza……”….…. ITAENDELEA..
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SITINI NA TATU
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MBILI:“ok! sasa unafikiria nini?” nilimuuliza Mangeu, ili kusoma alichokifikiria baada ya kugundua jambo hilo, “hapo kwa kweli ni kufanya mpango ukajitambulishe haraka kama unataka kumuoa Seni, naamini hato kataa kuolewa na wewe, na baada ya hapo muondoke kuelekea dar” alisema Mangeu, nilipata jibu la kuwa bado mzee Mangeu hajajuwa kinachoendelea kwa upande wa mauwaji, lakini sikutaka kumfanya aelewe, “lakini mimi siwezi kuondoka haraka hapa Pemba, kwasababu bado sija maliza..... ENDELEA..
Kabla sijamaliza kusema, mzee Mangeu akadakia, “kijana kumbuka kila kitu cha Seni nitakiacha mikononi mwako, hivyo Hutokuwa na Haja ya kufanya kazi ya ualimu, tena unaweza kwenda kufungua shule yako na kuajili walimu” alisema mzee Mangeu kwa msisitizo, “Huwezi kunielewa mzee, naomba nipe muda, ujuwe bado hatuja fahamu kuhusu vifo vya wanaume ambao wamekuwa wakimfuata Jesse” nilimueleza Mangeu ambae alionyesha kunielewa kidogo, “sawa ni muhimu kufahamu kwanini jambo hilo limekuwa likitokea, lakini hatuwezi kusubiri zaidi, unadhani itakuwaje kama jini litakuuwa?” aliuliza mzee Mangeu, na mimi nikamrudishia swali, “itakuwaje kama jini linatumwa kuzuia mtu asimuoe Jesse” hapo mzee Mangeu akatulia kidogo, akitafakari jambo kwa sekunde kadhaa, kabla hajavunja ukimya, “hivi inawezekana jini linatumwa na Juma na kijana wake Ussi?” aliuliza Mangeu, huku ananitazima, na mimi nikamtupia swali, “unaonaje ukihisi kuwa muuwaji sio jini ni mtu wa kawaida ambae anazuia mtu asimuoe Jesse, na pengine akaamua kukuuwa wewe au Jessen mwenyewe” nilimuuliza mzee Mangeu, ambae alionyesha kushtuka kidogo, “hilo ndilo ninalolitafuta kila siku, na ninatumia gharama kubwa ili niling’amue hilo” alisema Mangeu na hapo nikahisi jambo kuhusu huyu mzee, “unatumiaje gharama kutafuta jibu hilo? au umekodi wapelelezi wa kujitegemea?” nilimuuliza Mangeu, kwa maana ya kuhitaji kuthibiisha hisia zangu.
Hapo nikamuona Mangeu akinitazama kwa macho ya tahadhari, kama vile alishuku jambo juu yangu, “unadhani unapaswa kulijuwa hilo mapema kiasi hiki, manaa hata wao wenyewe niliowapa kazi hawanifahamu?” aliniuliza mzee Mangeu, mpaka hapo nikagundua kuwa huyu ndie alietoa kazi ofisini kwetu, tufanye uchunguzi wa mauwaji haya, yaani mmilikiwa wa Gmail, ya
j_jos@gmail.com kwa maana ya John Joseph, “hoooo! kumbe, sasa unaonaje tukikutana na huyo mpelelezi, tujuwe amefikia wapi, na sisi tumpe mawazo yetu” nilimshauri mzee Mangeu ili kumpima kama anaweza kusema ukweli au laa.
Kwanza John Joseph alicheka kidogo, kicheko cha kujidharau, “kosa nililo fanya ni moja kati ya mkataba ambao nimeingia nao, ni kwamba hakuna kufahamiana majina wala kukutana, hata malipo nimefanya benk, na niliwasiliana nao kwa simu na email” nilitabasamulia ndani kwa ndani, “ok! mimi nimepata wazo, unaonaje kama na sisi tukianza upelele wetu?” nilimueleza babu Zidadu, ambae aliachia basamu pana, lililoashiria kukubaliana na wazo langu, “eti eeh, sasa tutafanyaje?” aliuliza Mangeu, na hapo sikutaka kuwa na haraka kwa kumuambia cha kufanya, maana hata mimi sikuwa na juwa la kumtuma mzee huyu, “usijari juu ya hilo, cha kufanya wewe katulie ufikilie nini kifanyike, wakati huo unafuatilia mwendeno wa mzee Juma, na mimi nitakuwa nawaza jambo la kufanya, ila kabla hujaondoka tupeane namba za simu” nilishauri kwa mzee Mangeu, ambae aliunga mkono, huku akisistiza jambo, “lakini kuwa makini Seni asijuwe lolote” alisema hivyo Mangeu kabla hajawasha pikipiki yake na kuondoka zake, huku tukiwa tumesha peana namba za simu, na tukikubaliana kukutana siku inayofuata na kuwasiliana pale tunapata habari yoyote mpya ya kutilia shaka.
Naam na mimi niliingia ndani huku natoa simu yangu na kumpigia Jessenia ili kumjulisha kuwa nimeshafika nyumbani, lakini hakupokea, nikajaribu mara ya pili, lakini ilikuwa hivyo hivyo, kwa maana Jessenia hakupokea, hapo nikaachana nae na kuingia bafuni kuoga, nilipotoka nikakuta simu inaita, na wakati huo huo niliweza kuona alama ya missed call, na mpigaji alikuwa ni Jessenia, siku subiri mpaka nivae nikaipokea mara moja, “kwanini hupokei simu zangu” niliuliza kwa mtindo flani wakujifanya nina wivu, japo nilijuwa fika kuwa alikuwa nyumbani kwao na asingeweza kutoka kwa usiku ule, “jamani Eric, acha wivu, yaani ungejuwa mwenzio niliwekwa kikao wala usingesema” alisema Jessenia na hilo halikunishtua hata kidogo, maana nilijuwa lazima iwe hivyo, kutokana na kiburi alicho kionyesha Jessenia, kwa kutokukubari maagizo ya mjomba wake ya kurudi nyumbani, na ukizingatia kuwa niwazi walikuwa wanafahamu kuwa alikuwa na mimi, na walizijuwa sehemu zote tulizokuwepo au kutembelea, ukiachilia taarifa walizopewa na Mandevu ambae sasa niliweza kulifahamu jina lake kuwa ni Othman, pia Ussi alituona kwa macho yake pale uwanjani, “dah! sasa mjomba amesemaje?” nilimuuliza Jessenia, nikijifanya kama nimeshtuka na sikutarajia kutokea kwa jambio kama hilo, “yani mjomba na shangazi wamenisema sana, toka muda ule umeniacha hapa nyumbani ndio wana maliza sasa hivi” alisema Jessenia katika hali ya uchangamfu, niwazi hakushtuliwa na gombezo la walezi wake, ambao mpaka sasa yeye alikuwa anaamini kuwa ndio ndugu zake halisi, “hee! kwahiyo walikuwa wanasemaje?” nilimuuliza nikiweka kilombwezo cha kushangaa, “wamenisema sana, eti nimeanza tabia mbaya, na nimekuwa na kiburi, nimeonekana naranda randa na mwanaume, nina waaibisha” alisema Jessenia, ambae aliendelea kunisimulia jinsi alivyoongea na walezi wake, kwamba yeye aliwaeleza kuwa, mimi nina nia ya kumuoa, hivyo yeye Jessenia aliwaomba wavumilie kidogo ili nije kujitambulisha kwao na kuanza utaratibu wa kuoa, lakini Jessenia anasema kuwa mjomba na shangazi yake walikataa katakata, kwamba hawanitaki kabisa nifike pale kwao, kwaajili ya kuoa, hapo maongezi yakawa marefu sana, Jessenia aking’ang’ania kuolewa na mimi, na walezi wake, wakisisitiza kuto kunikubaria mimi, huku wakitoa sababu ya kwamba mimi ni mtu kutoka bara, hapo bado walikuwa hawajagusia swala la dini.
Jessenia alinieleza kuwa walezi wake yani shangazi na mjomba wake, walimsema weeee, na mwisho wakamueleza kuwa kesho kuna wageni wanakuja na hato takiwa kutoka pale nyumbani hata kidogo, “inabidi ufanye mbio mbio uje kunitolea barua Eric, na uwajulishe wazazi wako huko bara” alisema Jessenia, kwa sauti ya msisitizo alipokuwa amemaliza kunieleza jinsi walivyoongea na walezi wake, “usijari Jesse, kila kitu kitakuwa sawa, si unajuwa kuwa leo ni siku yetu ya pili toka tuwe wapenzi” nilimueleza Jessenia lakini sio kwa lengo la kumkatalia kwenda kujitambulisha kwao, “una maana gani Eric, ni vyema ukaja nyumbani kujitambulisha ili mjomba ajuwe kwamba nia yako ni kunioa nasiyo kunichezea” alisema Jessenia kwa sauti ambayo ilianza kunyongea, “sikia Jesse, sina maana ya kukataa kufanya hivyo nilimaanisha wacha kwanza hasira zao zipungue kisha tufanye utaratibu na tutaongea vizuri kesho jioni tukikutana” nilimueleza Jessenia kwa sauti tulivu yenye kumpa matumaini, “kwanini iwe jioni, kwani mchana utakosa muda?” aliuliza Jessenia, kwa sauti ya kulalamika na kujidekeza, “Jesse, kwani umesahau kuwa umeambiwa kuwa kesho kuna wageni wanakuja nyumbani kwenu na unatakiwa kuwepo nyumbani?” nilimuuliza Jessenia, kwa namna ya kumkumbusha, “mimi siwasubiri hao wageni wao, kwani kuna umuhimu wowote wa mimi kuwepo” alisema Jessenia kwa sauti ambayo haikuwa na dalili yoyote ya utani, “hapana Jesse, ukionyesha kiburi watazidi kunichukia, cha msingi wewe bakia kwanza mpaka wageni watoke” nilimshauri Jessenia, ambae sasa alinielewa nia yangu, “hapo sawa, kuwa kile alichokielewa haikuwa nia yangu halisi, nia yangu ilikuwa ni mpaka nitakapo kamilisha kazi yangu, niangalie kama bado nitakuwa katika mapenzi na Jessenia, na kama yatakuwa katika kiwango hiki, basi nifanye taratibu za kumbeba jumla jumla, tena kwa kumtumia huyo huyo Mangeu, “usijari Jesse, kila kitu kitaenda sawa” nilimjibu, kabla ya kukata simu tukikubaliana tuwasiliane kesho asubuhi. ….…. ITAEENDELEA