KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THEMANINI NA TATU
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI: alifoka mjomba wake Jessenia, “nisamehe mjomba, lakini sijatoroka nipo hapa hapa pemba” alisema Jessenia kwa sauti iliyojaa nidhamu, na heshima, “kweli bado hupo pemba, hupo sehemu gani, bado hupo na huyo kijana?” aliuliza mzee Juma, huku sauti yake ikibadirika na kuwa yenye shahuku, “nipo njiani na kuja nyumbani lakini nilitaka nikueleke kuwa na kuja na wageni” alisema Jessenia, kwa sauti ile ile ya upole, na hapo ni kama mzee Juma alishtuka sana kusikia vile…….…. ENDELEA..
“eti! ni wageni gani hao, na wanafwata nini?” aliuliza mzee Juma kwa sauti ya mshtuko na hasira, “ni mchumba wangu anakuja kujitambulisha, atakuwa na mzee Mangeu ndie mshenga wake” hakika sikuwahi kushuhudia mshtuko wa wazi kwenye simu kama huu, leo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza.
Maana mzee Juma alitoa mguno mkubwa wa mshangao, “eti we Seni, mbona unafanya mambo ya ajabu hivyo, unaweza kumshirikisha huyo mzee mchawi, au umesahau kilichokutokea kwa miaka mingi?” aliuliza mzee Juma na hapo nikamuona Mangeu anatikisa kichwa kwa masikitiko, “ndiyo mjomba nafahamu, lakini yeye mwenyewe ndio kamchagua huyo, naomba unikubalie” alibembeleza Jessenia, na hapo zikapita sekunde kadhaa, ni kama mzee Juma alikuwa anawaza jambo, “sawa njooni, mupo wapi kwa sasa” aliuliza mzee Juma, “tuna karibia nyumbani, tunatokea macho manne” alisema Jessenia, “sawa njooni” alisema mzee Juma na kukata simu haraka sana.
Ukataji wa simu na ukubaliji wa mzee Juma, ulinitia mashaka, mjomba wako sasa anapiga simu kwa Ussi, hivyo basi huko ndani kutakuwa na kazi mzito, inabidi muwe makini sana kufata maelekezo yangu kila nitakapo kuwa nawaeleza” niliwaeleza Jessenia na mzee Mangeu, nao wakaitikia kwa vichwa kuonyesha kuwa wamenielewa.*******
Dakika mbili baadae tulikuwa nje ya geti la kina Jessenia, ambapo Jessenia kama mwenyeji wetu ndie alie tukaribisha ndani, ambako tulipokelewa na shangazi yake Jessenia, “karibu jamani” alikaribisha shangazi, kwa sauti ambayo, usingetia shaka yoyote, huku ananitazama usoni kama vile ananikagua, “asante sana” anilisalimia kwa sauti iliyojaa nidhamu na heshima kubwa, “karibu ndani jamani” alisema tena shangazi na safari hii aliitikia mzee Mangeu, “asante jirani, leo nimekuwa mgeni wenu jamani” alisema mzee Mangeu, wakati huo mimi navua raba miguuni mwangu nikibakiza sox, ambazo zilikuwa ni ghala langu la silaha na hifadhi ya tape record, huku mzee mangeu na Jessenia wakivua viatu vyao vya wazi, bila hata kuhangaika.
Baada ya hapo tuka ingia ndani, huku nyuma yetu tukisikia ngurumo ya gari likiingia kwa fujo kwa ujuzi nilionao katika kutambua sauti na ngurmo mbali mbali, ngurumo ya gari hilo haikuwa defender, sio la polisi wala la jeshi, ila lilikuwa ni gari aina ya Parado, hivyo nikajuwa wazi kuwa Ussi alikuwa anaingia pale nyumbani kwao, nilisha yatarajia hayo hivyo siku shtuka zaidi ya kuona mpango wangu unaenda kama nilivyopanga.
Naam Jessenia ambae ndie mwenyewji wetu, alituongoza mpaka sebuleni, huku shangazi yake akibakia pale nje, ni kama alikuwa anamsubiri Ussi, hakika lilikuwa ni jumba kubwa la kifahari, lenye mahadhi ya kiarabu, muonekano wake ulipendeza kwa kweli, “karibu karibu karibu bwana Zidadu, naona sasa umeamua kumtafutia Seni mwanume ambae unaona anafaa kurithi kila kitu sio?” hivyo ndivyo mzee Juma aliekuwa amekaa kwenye zuria la manyoya akiegemea mto wa manyoa pia, ambao ni mmoja kati ya mito kadhaa iliyopo pale sebuleni, hakuna alieshangaa juu ya maneno ya mzee Juma, maana kila mmoja kati yetu alikuwa anafahamu.
Lakini licha ya hivyo, lakini mzee Mangeu akajisaisha, “jirani unaongea nini bwana, vijana wameniomba niwe muwakilishi wao, maana huyu kijana ametokea bara” alisema mzee Mangeu, huku anakaa chini, na wakati huo tukasikia vishindo vingi vya watu vinatokea nyuma yetu, kuja upande wa sebuleni, “Seni hawezi kukubali kukutumia kama mshenga au mzee wa huyu mshenzi, bila wewe kumueleza ujinga wako, najuwa Seni amekuwa akikuogopa toka utoto wake, inakuwaje leo aondoe hofu yake ghafla hivi?” aliuliza mzee Juma kwa sauti ya ukali, wakati huo nageuka kutazama nyuma ili kuona watu waliokuwa wanaingia.
Naam macho yangu yaliona kile nilicho kitarajia, yaani Ussi akiwa ameongozana na watu kama sita hivi, wakiwa na vipande vya miti na mapanga mikononi mwao, “nyie wapuuzi bora mumetupunguzia kazi, mume jileta wenyewe hapa nyumbani, hebu niambieni computer yangu ipo wapi, na kwanini muliichukuwa” alisema Ussi huku ananisukuma kwa nguvu, nikayumba kidogo na kutembea hatua kadhaa mbele kisha nikajiangausha chini makusudi, “jamani kaka Ussi, kwanini unamsukuma shemeji yako?” alisema Jessenia huku ananifuata pale nilipo jiangusha na kuchuchumaa mbele yangu.
“pole Eric, jamani vipi umeumia?” aliuliza Jessenia aliechuchumaa mbele yangu, “hapana sijaumia” nilijibu kwa sauti iliyotoa huruma, “Juma, ndivyo tunavyo wapokea wageni wetu muhimu, si unajuwa jinsi ndoa ya Jessenia ilivyo muhimu?” aliuliza Mangeu kwa sauti iliyojaa mshangao wa ghadhab, wakati huo ndio wakati nilio utumia kupeleka mkono kwenye mguu wangu wa kushoto na kubofya kitufe cha mwisho cha tape record, ambacho ni cha kurecordia, bahati nzuri nacho kikakubali.
“tulia we mpuuzi, leo ndiyo mwisho wa kila kitu, unadhani marehemu mtarajiwa anahitaji kukaribishwa vipi kwenye nyumba ya mtoa roho?” aliuliza Ussi kwa sauti ya kibabe, huku anamsukuma mzee Mangeu, ambae pia anaanguka chini kama kifurushi pale kwenye zuria, Juma mueleze kijana wako ajuwe mimi ni nani, ili aniheshimi kidogo” alisema Mangeu huku anamtazama mzee Juma, ambae kitu cha kushangaza ndio kwanza akamuona anatabasamu kwa dharau, “anajuwa kila kitu, anajuwa kuwa wewe …..” kabla hajamaliza kuongea, mara akatokea mke wa mzee Juma, yaani shangazi yake Jessenia, akiingia ndani mbio mbio, “Aroub yupo nje anahitaji kukuona” alisema mke wa mzee Juma.
Hapo mzee Juma na Ussi wakatazamana kwa macho ya hofu, “nenda kamalizane nae haraka” alisema Ussi huku anamtazama baba yake, “sawa lakini hakikisha hawa wajinga hawapigi kelele wala hawafanyi fujo yoyote” alisema mzee Juma, huku anainuka na kuelekea upande wa nje, huku nyuma Ussi alieshikapanga alinisogelea mimi na wale wengine wakigawana sisi na kutuzingira na silaha zao za jadi mikononi, wakizinyoosha kwetu, huku wakituonyeshea ishara ya kukaa kimya, hapo tukawa kimya kabisaaaa, kiasi cha kusikia hata ngurumo za magari yaliyokuwa yanapita barabarani, ambako ni umbali wa mita kama mia nne toka pale.
“hoooo! bwana Aroub, karibu sana, naona umeishia nje” tuliweza kusikia sauti ya mjomba wake Jessenia, yaani mzee Juma akiongea toka nje kwa sauti iliyo changamka, “yaan nimeishia hapa nje maana shemeji ameniambia kuwa una wageni munakamilisha jambo flani” ilikuwa ni sauti ya insp Aroub, “nikweli bwana, lakini tunaweza kuongea” alisema mzee Juma, kwa sauti ambayo usingeweza kusema kama kuna jambo ameliacha ndani, “nadhani ni vyema kama ukimaliza maongezi na wageni wako, maana nina maongezi yanayohitaji muda na utulivu mkubwa sana, ni kuhusu wizi uliotokea hapa kwako na upotevu wa binti yako” alisema insp Aroub.
Walikubaliana hivyo kisha mzee Juma akarudi ndani, nadhani insp Aroub aliondoka kama tulivyo kubaliana, lakini hakutakiwa kwenda mbali sana, “huyo mjinga amesha ondoka, sasa tuwafanyaje hawa wapuuzi?” aliuliza mzee Juma, huku anaibukia pale sebuleni, “baba mimi nadhani tufanya kama tulivyo panga, tuwauwe kisha tukawatupe baharini” alisema Ussi, huku tape record ikiendelea kuzunguka ndani ya sox ya mguu wangu wa kushoto, “bwana Juma, hii nini, ina maana umepanga kutuuwa?” aliuliza Mangeu kwa sauti iliyojaa wasi wasi, “wewe unaona nini kitatokea juu yako na huyu kifaranga chako, ambacho baada ya kukilea kwa miaka yote hiyo sasa kina jifanya kimekuwa na kujipangia mambo yake” alisema mzee Juma, kwa sauti ya kujiamini sana, “lakini Juma, kwanini ufanye hivi ndugu yangu?” aliuliza mzee Mangeu kwa sauti iliyojaa wasi wasi na kuombleza, “hivi Zidadu, unadhani baada ya yote niliyo yafanya naweza kukubali kupoteza kila kitu, kumuacha Jessenia aende na huyu mpuuzi?” aliuliza kwa sauti yenye kejeli mzee Juma.
Hapo Jessenia akatoa macho ya mshangao, kama vile hakujuwa lolote toka mwanzo, “mjomba una maana gani, una maana hutaki niolewe?” aliuliza Jessenia kwa sauti ya mshangao wakujifanyisha, maana wote walikuwa wanajuwa kinachoendelea, “sasa je mlidhania mimi mjinga” alisema mzee Juma, huku akicheka kwa dharau, kisha akamtazama Ussi, “ngoja kwanza niwaeleze kitu ambacho kitawafurahisha hawa wajinga, ambao walidhania kuwa mimi ndie mjinga” alisema mzee Juma, huku usoni mwake furaha ikiwa imeshamili na kufanya uso wake uchukize usoni pangu,
Na hapo mzee huyu, ambae hakujuwa kama narecord maongezi yake akaanza kuongea.******
Ilikuwa hivi, wakati ule mzee Zidadu, amekuja kwa mwarabu ambae alikuwa anaishi kwenye hii nyumba, ambayo mzee Juma alikuwa mfanyakazi pamoja na mke wake kwa lengo la kununua hii nyumba, lilikuwa pigo kubwa sana kwa mzee Juma, ambae alitegemea kuwa endapo angekosekana mteja basi yeye angejimilikisha nyumba pindi mwarabu yule atakapo ondoka.
Lakini bwana Juma akapata nafasi nyingine ya kucheza karata yake kwa kumchomea mzee Zidadu na bi Aisha, yaani mama yake Jessenia, ambao alimini kuwa endapo watauwawa na wao watapata kujimilikisha nyumba ile.
Ni kweli walifanikiwa kutoa taarifa kwa mke wa Abdulkarim, ambae alituma vijana wake haraka kuja kuwa shambulia na kusababisha kifo cha Aisha Mohamed, yaani mama yake Jessenia, huku mzee Zidadu akifanikiwa kumuokoa Jessenia na yeye mwenyewe akibakia na ngeu za kutosha.
Lakini bado bahati ikabakia kwa mzee Juma, ambae alikabidhiwa nyumba ile kwa shariti la kumlea Jessenia, ambae akiolewa na wao ndio mwisho wa kumiliki mali zake, licha ya hivyo mzee huyo Mangeu aliwahudumia kwa kila kitu, huku akiwafungulia biashara mbali mbali ikiwepo ile ya Ussi ya uvuvi….. ENDELEA
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THEMANINI NA NNE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TATU: Lakini bado bahati ikabakia kwa mzee Juma, ambae alikabidhiwa nyumba ile kwa shariti la kumlea Jessenia, ambae akiolewa na wao ndio mwisho wa kumiliki mali zake, licha ya hivyo mzee huyo Mangeu aliwahudumia kwa kila kitu, huku akiwafungulia biashara mbali mbali ikiwepo ile ya Ussi ya uvuvi…..….. ENDELEA..
Kwa maelezo ya mzee Juma ni kwamba toka Jessenia akiwa na miaka saba, akaanza kumuweka mbali na mzee Mangeu kwa kueneza habari za kuwa mzee Mangeu ni mchawi, sifa hiyo aliieneza sio tu kwa Jessenia peke yake, bali hata kwa watu wengine wa pale msingini, ambao waliamini na kuanza kumtenga mzee huyu, ambae baadae akaanza kuandaa mazingira kwa kijana wake Ussi kuja kumuoa Jessenia, ili mwisho wa siku wamiliki mali zote za Jessenia kama mzee Mangeu alivyopanga kuwa Jessenia akiolewa ata kabidhiwa mali zake.
Pasipo kuangalia tabia chafu za Ussi, yeye na Ussi walihakikisha Jessenia hatengenezi mahusiano yoyote ya kimapenzi, waliuwa watu wengi sana, alisimulia mzee Juma akiwataja kwa majina, “kikwazo kikaja kwa huyu mpuuzi” alisema mzee Juma huku ananionyesha kwa kidole.
Mzee Juma alieleza kuwa, siku ile wakina Ussi walijaribu sana kuniuwa siku ile pale Green Mess, ni ile mida niliwaona wanazunguka zunguka dirishani, hata waliposhindwa vijana wa Ussi, baadae akaja mwenyewe nae akashindwa na ndipo alipoanza mipango ya kuniuwa, “ndio maana tuliwauwa wale wote insp Aroub aliponza kuwatilia mashaka, “sijui ilikuwaje mpaka ukamshinda Mabusi, ila leo ndio mwisho wako” safari hii aliongea Ussi, kwa sauti iliyojaa hasira, “na bahati nzuri mume turahisishia kazi, mumekuja wote watatu” alisema mzee Juma, huku anacheka kicheko cha dharau, kicheko ambacho anacheka mtu alie mnasa panya kwenye mtego.
Unajuwa kilicho fuata hapo na mimi nikaangaua kicheko huku napeleka mkono kwenye mguu wangu wa kushoto na kuzima ile tape recorder, wote wakanitazama kwa mshangao, huku Ussi ananifuata kwa hasira na kushusha teke usawa wa mgongo wangu, lakini nikalikwepa kidogo teke lake pale nilipojaa, “Ussi tulia kidogo maana unacho kitaka hukiwezi hata kwa sekunde” niliongea kwa sauti tulivu huku naendelea kucheka hata wenzake waliokuwa wanataka kunivamia pia wakatulia na kunitazama kwa mshangao, wakijiuliza kwanini najiamini, “unaongea nini we fala, leo utoke humu ndani” alisema Ussi kwa sauti ile ile ya hasira.
Nikacheka kicheko cha kumtia hasira, “hivi Ussi, wewe na baba yako mume shindwa kujiuliza kwanini tumejileta wenyewe hapa nyumbani, au munadhani mzee Mangeu anaweza kukubali, kuwa mshenga wakati yeye ndie ndugu wa Jesse” niliuliza kwa sauti ya tulivu, ungesema tupo kwenye mazungumzo ya kawaida, “kwahiyo unataka kusema nini” aliuliza Ussi kwa jazba, huku baba yake akiwa ametulia anatoa macho kwa mshangao wa tahadhari kumtazama mzee Zidadu, “Ussi unauliza nataka kusema nini ina maana hujapata jibu tu, unadhani Jesse baada ya kukuona ukimkosa kosa na panga na kukumbia siku mbili nzima halafu leo ajileta tu?” nilimuuliza tena Ussi, ambae alimtazama Jessenia kama vile kuna jibu alikuwa anataka kupata.
Lakini alipoona kuwa amekosa jibu, akamtazama baba yake, “baba mimi naona tuwauwe kisha tukawatupe, maana wameshajuwa kila kitu” alisema Ussi, kwasauti iliyoanza kuwa na wasi wasi, “Ussi usifikirie sisi kujuwa fikiria kuhusu video ambayo inaweza kuanza kusambaa mitaani ikikuonyesha unamuuwa Vuai kwa sindano yenye sumu nyumbani kwake” hapo sasa nikawa kama nimemkumbusha kitu Ussi, “baba…. baba … hard disc” alisema Ussi huku anatoka mbio kuelekea ghorofani.
Hapo mzee Mangeu akamtazama mzee Juma, ambae alikuwa amtumbua macho kama vile amesingiziwa wizi ugenini, “bwana Juma ni vyema wewe na familia yako ukajisalimisha polisi hili swala liishe kwa amani” alisema mzee Mangeu kwa sauti ya kusihi, “nyie vijana mnashangaa nini hebu wauweni hawa washenzi” alisema mzee Juma, kwa sauti ya juu na yakupayuka, hapo nikajuwa kuwa sikuwa na muda wa kuomba msaada toka nje kutokana na ukaribu wa watu wale na nikizubaa tu nimempoteza Jessenia na mzee Mangeu, hivyo haraka sana nikapeleka mkono wangu kwenye mguu wa kulia nakuibuka na AGP, ambayo sifa yake moja wapo ni kuto kutoa sauti, ambayo nikamuelekezea mmoja kati ya wale vijana aliekuwa ameinua panga lake kutandika Jesse, nikaminya kifyetulio bila kusita na kuruhusu risasi kutoka.
Kilichotokea kiliwafanya wale wangine wa tano waanze ache walichokuwa wanakifanya toka mbio kukimbilia kolidoni, kuelekea upande wa jikoni ambako sisi tulipitia, maana nilimfumua kichwa yule jamaa na kusababisha ubongo wake kutawanyika kama tikiti lililokanyagwa na fuso, “mamaaaa” Jessenia alipiga kelele, huku mzee Mangeu na mzee Juma wakitoa macho kwa mshangao nikaipiga risasi taa ya sebuleni, halafu nikaminya saa yangu ambayo inatochi maalumu kwaajili ya kusomea ramani, halafu nikaizima na kuiwasha tena, halafu nikaizima, kilikuwa ni kitendo cha haraka wakati huo huo kwa kutumia taa za kwenye ngazi za kuendea ghorofani, nikamuona Ussi anashuka mbio mbio, “baba!! baba!! wameiba ile harad disc” alisema Ussi ambae kiukweli hakujuwa kinachoendelea.
Mara ghafla akasita, ni baada ya kuona giza limetawala pale sebuleni, “Ussi usijaribu kupiga hatua hata moja, ni vyema ukijisalimisha” nilimuambia Ussi, ambae hakujuwa pale sebuleni tupo wangapi na mkononi nina nini, “mpuuzi wewe unadhania ni rahisi hivyo” alisema Ussi kwa sauti iliyojaa hasira kali, huku anavamia giza na panga lake akiwa amelipunga hewani tayari kushambulia yeyote kati yetu, hapo sikuwa na haja ya kuchapa risasi, nilimshindilia ngumi moja nzito usoni nae akajibwaga chini akiangukia kwenye damu za yule niliempasua kichwa.
Hapo Ussi akaamka kwa haraka, huku macho yake yakianza kuzowea giza, kabla haja kaa sawa nikamuongeza teke la usoni tena, ambalo lilimrudisha pale pale, “nyie mbona hamsaidii alipiga kelele Ussi, ambae hakusikia kelele za nje, “simama” ila alikuja kusikia milipuko kadhaa ya risasi, sikutaka kumuuwa Ussi wala mjomba wake, ila nilitaka wafikishwe mbele ya sheria, hivyo nilihakikisha namtandika Ussi kisawa sawa, mpaka akalegea, kuhusu baba yake sikuwa na wasi wasi, maana niliamini kwa umri ule asingeweza kufanya lolote, “mjomba ina maana wewe ndie uliesababisha kifo cha mama yangu” aliuliza Jessenia kwa sauti iliyojaa uchungu, wakati huo tulikuwa tunasikia mke wa mzee Juma, toka nje ya nyumba akiomba asifanywe chochote sababu yeye hausiku, “Seni, huwezi kufanya lolote mama yako alisha kufa zake, jibu hilo alilitoa Ussi ambae alikuwa amechafuka uso kwa damu zilizotoka kwenye mipasuko mbali mbali ya mwili wake iliyosababishwa na ngumi, na mateke.
Kitendo bila kutegemea Jessenia akanipokonya bastora yangu na kumuelekezea Ussi, huku akiminya trigger mara kadhaa, akitandika miguu yote miwili ya Ussi kwenye mapaja, ile nataka kunyang’anya nilichelewa, tayari alisha ielekezea kwa mzee Juma hapo nikafumba macho, nakusikia sauti ya kilio cha mzee huyu, nilipofumbua macho na yeye nikamuona akiwa amechakazwa miguu yake kama ilivyo kwa kijana wake.
Naam dakika chache baadae askari walikuwa wamesha ingia ndani, huku wakitoa taarifa ya kuwa walisha wauwa wale vijana wote watano waliojaribu kutoroka, baada ya hapo insp Aroub nae akaja na kuungana na sisi, akakabidhiwa wakina Ussi baba yake na mama yake, mama Ussi alipelekwa moja kwa moja kituoni, huku mzee Juma na Ussi, wakipelekwa hospital chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.
Wakati huo upande wa pili kule pwani, askari walikamata mashua zote za Ussi na wafanyakazi wake, kisha kuwapeleka kituo cha polisi.******
Naam siku ya pili habari za kukamtwa kwa Ussi na baba yake, zilisambaa vibaya huku sababu zikiwekwa wazi kuwa ni mauwaji yaliyo tikisa kwa muda mrefu, watu wakidhania kuwa ni jinni, ndugu na jamaa za marehemu walilaani sana kitendo kile kilicho fanywa na Ussi na baba yake, wakishirikiana na mama yake, walinisifu sana Eric kwa kusababisha wauwaji kukamatwa, japo hawakujuwa kuwa mimi ni mpelelezi walinitaja kama mwalimu au mchumba wa Jessenia, nilienusurika kuuwawa.
Mwasenga na mke wake walishangaa sana, kugundua kuwa mimi ni mpelelezi, mwalimu aisha hakujuwa kama mimi ni mpelelezi mpaka nilipoondoka, Saphia alifurahi sana aliposikia kuwa mimi ndie niliewaumbua wakina Ussi, nashukuru hakukumbushia kuhusu ndoa niliyo mdang’anya, Maimuna yeye hakuweza kuonana nae.
Mwisho mimi na Jessenia tulielekea dar es salaam ambako nafanyia kazi, japo Jessenia ananyumba yake kule mbezi msakuzi, lakini anaishi kwenye nyumba yangu amefungua maduka manne ya vipodose moja kariakoo msimbazi jingine mbezi jingine mwenge na jingine kibaha maili moja, mzee mangeu alimpatia robo tatu ya mali zote alizochukuwa kwa mwarabu Jamal.
Mzee Mangeu mwenyewe sasa anaishi dar es salaam huku lile jengo kubwa pamoja shamba, amekabidhi serikalini lifanywe shule na makazi ya watoto wasio jiweza, yeye amenunua nyumba kubwa huko kigamboni, ambako amepata mwanamke mmoja mrembo kweli anaishi nae kama mke wake, na sasa ndie mtu pekee ambae tunamchukulia kama baba na ndugu wa Jessenia.
sasa tuna watoto watatu na maisha yanaendelea, ila sikuacha kuwa zawadia wakina mwasenga na mke wake, aisha malambao na wengine walionisidia kwa namna moja au nyingine kule pemba.
Mpaka hapo nimefikia mwisho wa simulizi hii ya KIFO CHA HAWARA asante sana kwa kuwa pamoja na mimi kwa hii miezi mi nne ya simulizi hii munisamehe sana kwa pale nilipowa cheleweshea ni majukumu tu ya kila siku musichoke kufuatilia simulizi nyingine zijazo hapa hapa Jamii Forums Shukran sana kwa support yenu wote na wale walioishia njiani sisi tushamaliza... AHSANTE NA KARIBUNI TENA.