KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SITINI NA TANO
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NNE: Namkumbuka mida ya saa nne kasoro nilipigiwa simu na insp Aroub, ambae nililazimika kutoka nje ili nikaipokee, “asalam aleykum mzee” nilimsalimia mzee Aroub, maana hii ndiyo salam pendwa na ya kipekee kwa huku kisiwani, “walaykum salaam bwana Eric, upo wapi saa hizi, tunaweza kuonana?” aliuliza insp Aroub akionyesha kuwa alikuwa na jambo muhimu sana la kuniambia, “nipo shuleni mzee, vipi kuna jambo lolote?” nilimuuliza insp Aroub, ambae nilijuwa tu lazima ataniambia kila hatua anayoipitia….…. ENDELEA..
Maana alikuwa anafanya kazi yake kwa kupitia maelezo yangu, “yah! kuna jambo ambalo nimegundua juu ya hii kesi ya mauwaji, nilienda asubuhi kukutana na wale wafanyakazi wa Ussi, nikauliza juu ya wenzao ambao hawakuwepo, na kwanini walinidanganya juu ya mwenzao mabusi kuongozana na yule marehemu kwanza” alisimulia Aroub na wakati huo kengere ya mapumziko ilisikika na wanafunzi wakaanza kutoka madarasani, na insp Arouba akaendelea kunisimulia, huku mimi nikitembea kuelekea nyuma ya jengo la ofisi ya walimu, sikutaka mwalimu Aisha anione na kuniharibia maongezi yangu, “wale vijana wakasema kuwa wao hawakujuwa lolote juu ya wawili hao, nikawauliza kama kuna mwingine zaidi ya Mabusi, ambae jana hakuwepo wakati naongea nao, wakanikatalia kuwa hakuna mtu mwingine ambae hakuwepo wakati nawahoji” alisema insp Aroub, ambae nilimuuliza sababu ya kuhitaji tukutane, “inshu ni kwamba kuna mida hii nipo njiani kwenye msafara natoka airport, tumekuja kuwapokea wakuu wajeshi la polisi toka Unguja, ambao wamekuja kama utangulizi wa ziara ya raisi ambae anakuja kesho kutwa, alisema Aroub ambae alinifanya niithibitishe kile nilicho kiona asubuhi kambini, askari walikuwa busy wana fanya parade na usafi pale kambini, “halafu kimetokea nini?” nilimuuliza Aroub, huku nikiwa na shauku ya kujuwa kilichomfanya anipigie simu, “sasa wakati tupo pale Air Port nimemuona Ussi anawapokea wageni sita, ambao sijawahi kuwaona hapa Pemba, kilicho nishtua ni kwamba, mara baada ya kuniona alishtuka sana, na kuongeza haraka ya kuondoka pale uwanja wa ndege huku akijificha ficha” alisema insp Aroub, na wakati namsikiliza insp mara nikaguswa mgongoni, “kwahiyo una utilia mashaka huo ugeni?” nilimuuliza insp huku nageuka kumtazama alienigusa mgongoni, moyo wangu ulishtuka kwa kile nilicho kiona, hapo haraka sana nikatazama kama kuna watu walikuwa wanatutazama, “yah! natilia mashaka makubwa sana, maana ule mshtuko wa Ussi ulikuwa ni mkubwa, lazima kuna kitu kinaendelea” alisema insp Aroub, sikushtuka kuhusu ugeni huo, maana haikuwa habari mpya kwangu, kilichoongezeka na kunishangaza ni kwamba wageni walikuwa wanatokea Unguja, nilitafakari hayo huku nikiwa na mtazama mwanafunzi wa kike aliekuwa amesimama karibu yangu ananitazama kwa uso wa tabasamu, sambamba na macho ya kulegea na kujawa na aibu fulani ya kike, ambayo mtu yoyote angeona tu lazima ange bashiri jambo la uvunjaji wa sheria unaotaka kutokea baina yangu na mschana huyu mwenye kumiliki bikira yake, “kwahiyo una mpango gani mzee?” nilimuuliza insp Aroub, ambae kwasasa nilijuwa yupo busy na ugeni, huku nikimtazama mschana huyu na kumpa ishara ya kuondoka asije akatukuta mtu mwingine na kuleta picha mbaya, lakini basi ilikuwa ni kazi bure maana alikataa kwa kutikisa bega, huyu alikuwa ni Maimuna, “ndio maana nimekupigia simu ili tujadili kwa pamoja” alisema insp Aroub, na hapo nikatabasamia tumboni, kwamba mtego wangu bado unafanya kazi, kwamba insp Aroub hawezi kufanya jambo mpaka aniulize mimi, “unaweza kupata nafasi ya kutoka ofisini mida hii?” nilimuuliza insp Aroub, ambae alisema ndiyo anaweza kutoka, “ok! tafuta sababu ya kuingia pale kwa bwana Juma, nadhani utapata picha kamili ya ugeni huo na wasi wasi wa huyo jamaa” nilimueleza insp nae akakubaliana na mimi, Naam wakati nakata simu, ili nimkabiri Maimuna, mara nikasikia sauti ya mwanamke ikiniulizia upande wa pili wa ukuta wa ofisi, karibu kabisa na kona ya kujia pale tuliposimama, “hivi mume muona yule mwalimu mgeni hapa” ilikuwa ni sauti ya mwalimu Aisha, hapo nikamtazama Maimuna kwa jicho la kuomba afanye ninacho mueleza.
Lakini ndio kwanza nikamuona Maimuna anakataa kwa kutikisa kichwa na bega, hapo nikamuonyesha tena ishara ya kuondoka kwamba taongea baadae, lakini haikusaidia kitu ndio kwanza akanyoosha mkono kuelekeza kule green house, kiwa ni ishara ya kwamba anataka kuelekea kule ghetoni, hapo nilichezesha akiri kwa haraka sana ilikupata jibu kabla Aisha hajatokezea upande ule, maana wakati huo nilisikia mwanafunzi mmoja akijibu, “nilimuona anaelekea upande wa hukoo” hapo nikajuwa sekunde chache zijazo Aisha anaibukia upande niliopo.
Niwazi Maimuna alikuwa anataka twende tukafanye kile alichokusudia kufanya na mimi, na sehemu yenyewe ni kule kule green house, sehemu ambayo ipo ndani ya kambi la jeshi, sehemu ambayo leo ilikuwa na pilika nyingi za usafi, ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya rais wa Zanzibar, hivyo hakuwa na ujanja wa kuingia pale green House mida hii, “poa fanya haraka nakuja” nilimueleza huku naanza kutembea kuelekea kule ambako Aisha anakotokea na hapo nikalishuhudia tabasamu pana usoni kwa Maimuna au kama wenzake wanavyomuita Mai, ambae pia alianza kutembea kuelekea upande wa nyuma wa ofisi na kufanya kama tunapishana.
Naam ile natokea upande wa mbele tu, nusu nigongane na Aisha, “we mwanaume vipi leo huna mpango wa kula au leo hunitoi out?” aliuliza Aisha kwa sauti yake yenye lafudhi ya kipemba iliyojaa utani, “kwaajili yako hata kiatu nitauza nikutoe out” na mimi nilimtania huku namzuia asitazame kule nilikotoka, bahati nzuri na yeye hakuonyesha kujari sana, maana alisimama mbele yangu, “mh! una maneno weye, ndio maana Seni amekuganda kweli kweli” alisema Aisha kisha tukacheka kwa pamoja, huku tunaelekea upande wa mgahawani, ambako tulienda kupata supu nzuri ya kuku wa kienyeji.
Nusu saa baadae tayari tulikuwa tumesha rudi eneo la shule, tukiwa tushamaliza kupata supu, wakati wote nilikuwa nawaza juu ya Maimuna, ambae alikuwa ameelekea kule Green House, sijui kwanini yalinijia mawazo ya ghafla, kuwa anaweza kuwa amepata upenyo na kuingia ndani, maana mida hii ya saa nne, huwa ni mida ya kupata chai, hivyo angeweza kupata nafasi hiyo kiurahisi, nikajilaumu kwa kumkubalia mschana yule kuelekea Green House, lakini ningefanya nini kumzuia, hasa kwa wakati ule ambaon Aisha alikuwa anakuja kunikuta katika hali tata.
Lakini mawazo yale butu yakaisha baada ya kengere kusikika na wanafunzi kuanza kuingia darasani, ndipo nilipomuona Maimuna akikimbilia darasani kama wenzake, nikatabasamu kwa ushindi huku naongozana na mwalimu Aisha kuingia ofisini.********
Yap! siku ile nilishinda ofisini, huku nikiwa jirani sana na Aisha, ambae hakuwa na kipindi chochote mida ile ya kuanzia saa nne, nakumbuka mida ya saa sita hivi, nilipigiwa simu na bwana JJ, yaani mzee John Joseph, ambae kisiwani hapa amekuwa akitambuliwa kama mzee Mangeu, nilitoka kwenda kupokelea nje maana nilijuwa fika kuwa lazima kuna lolote naenda kupewa, “niambie mzee wangu” nilisema mara tu baada ya kupokea simu, “nikweli kuna wageni wameingia ndani, lakini ni wakaida tu, ukiachilia kutokuwa na pilika zozote, pia nime mpigia bwana Juma amesema ni wageni wa kawaida tu” alisema Mangeu, “hapo ndipo unapoharibu mzee, kwanini umeuliza bwana” nilimlalamikia Mangeu kwa kitendo cha kukurupuka, “lakini wewe si ulisema kuwa tuchunguze kila hatua na pia nisinge uliza lazima angeshangaa, maana huwa nauliza kila kinachoendelea pale” alisema Mangeu, “kwahiyo umeridhika na jibu hilo?” nilimuuliza Mangeu, “kwani unadhani kuna jambo wamenificha?” aliuliza Mangeu, na hapo nikaona kuwa si vyema kama nitamueleza juu ya wasi wasi wa insp Aroub, ila ni muhimu na yeye afanye uchunguzi ili kupata majibu mawili yanayoendana, “mimi nakushauri fuatilia kimya kimya, halafu ukipata jibu niambie” nilimueleza Mangeu kabla hatujakata simu.
Nilirudi ofisini na kuendelea kupiga story na mwalimu Aisha, mpaka muda wa nusu saa tu nikaisikia simu yangu inaita, nilipotazama nikaona kuwa alikuwa ni insp Aroub, “subiri kidogo nikaongee na baba” nilimuambia mwalimu Aisha, huku nainuka nakutoka nje nikaenda kwenye kona ile ile ya asubuhi yaani kwenye kiambaza cha ofisi, kisha nikaipokea, “ndiyo mzee vipi kuna jipya?” nilimuuliza insp Aroub kwa sauti ya chini, “nilitaka nikuambie kuwa, nilienda mpaka nyumbani kwa mzee Juma Mohamed, lakini sikuwaona wageni sebuleni, zaidi nilipata kuona maandalizi makubwa ya chakula, unaweza kusema kuna harusi inaandaliwa, lakini hakuna watu” alisema insp Aroub, ambae alionekana kuwa sehemu yenye watu wengi.
Ukweli hapo nilijiuliza maswali mawili yaliyo fuatana, kwahiyo wageni wameshaondoka?, na kwama wamesha ondoka kwanini Jessenia hajanipigia simu kunijulisha chochote?, sijui kwanini nilijihisi vibaya, maana niliamini kwa ukoleaji wa Jessenia lazima ange nipigia simu mapema sana mara baada ya wageni kuondoka, sasa ukimya wake nilihisi kuwa amenidharau au hakuwa ananipenda kama ninavyofikiria, “ulimuona Jesse na maanisha yule mwanamke anaeishi pale kwa mzee Juma?” nilimuuliza mzee Aroub, huku nikijitaidi kuzuia sauti yangu, isiwe yenye kupanic.
Kwanza nikamsikia mzee Aroub akiachia kicheko flani cha chini chini, kama vile ananicheka, “sishangai kuona kuwa unamfahamu huyo mschana mrembo kuliko warembo wote hapa kisiwani, yeye sijamuona wala sikuona dalili ya uwepo wake ila nilikuta shangazi yake na waschana wengine watatu wanasaidiana kuandaa vyakula” alijibu insp Aroub, na hapo nikashtuka kidogo, na mapigo ya moyo wangu kuanza kwenda kasi kwa wivu, “kwa hiyo wageni wamesha ondoka?” niliuliza tena huku nikijitaidi kuificha sauti yangu isibainishe hali niliyokuwa nayo moyoni, “hicho ndicho kilichonifanya nikupigie simu, bwana mwandishi” alisema insp Aroub, na hapo nikatega sikio kwa umakini ili nikupata hiyo habari, “nilimuuliza mzee Juma kama kulikuwa na sherehe yoyote pale nyumbani kwake, kutokana na vyakula vile, nae akanijibu kuwa hapakuwa na sherehe yoyote, ila alikuwa na ugeni hivyo vyakula vile vilikuwa ni kwaajili yao, nikamuuliza wako wapi wageni wale, akasema kuwa wageni wapo ghorofani wamepumzika maana wametoka unguja, ukweli mzee Juma hakuonyesha wasi wasi, na mimi nilijitadi kuongea nae kwa utaratibu pasipo kuonyesha dalili ya kumtilia shaka” alieleza insp Aroub, na hapo akaniachia swali jingine la kwamba, inakuwaje Jessenia hayupo nyumbani kwao, wakati wageni bado wapo nyumbani kwao na kwanini anipigii simu, hapo nikaona wazo zuri ni kumpigia simu Jessenia pengine kuna lolote naweza kusikia, niliamua hayo nikichanganya hisia za mapenzi ambazo kiukweli zilisha nitawala kwa kiasi kikubwa kichwani mwangu, “kwa sasa mzee upo wapi?” nilimuuliza mzee Aroub, “nipo chake hotel, ambapo wageni wetu wamefikia, na nikitoka hapa nitakuwa kwenye msafara wa kwenda mkoani kuwapokea wageni wanaotoka unguja na kuwapeleka madungu Hotel, ambapo watafikia” alisema insp Aroub, ukweli sikuwa na lolote la kumtuma insp mpaka nijuwe kinachoendelea, “sawa mzee nadhani ukimaliza kazi zako halafu mimi nifikirie la kufanya” nilimueleza insp, kisha maongezi yetu yakaishia hapo, na mimi sikutumia hata sekunde kuwaza, ile kukata simu tu nikampigia Jessenia, simu iliita weeee mpaka ikakatika bila kupokelewa, nikapiga tena na na tena, haikupokelewa, niliingiwa na wasi wasi uliochanganyika na wivu, hapo ndipo nilipogundua kuwa ninampenda kiukweli Jessenia.
Sikuwa na la kufanya, nilirudi ofisini huku nawaza nifanye nini, japo nilijitahidi kuficha unyonge niliokuwa nao lakini Aisha aligundua, “Eric vipi, mbona kama haupo sawa” aliuliza Aisha, “haaa mzee anasumbua” nilidanganya, huku najitahidi kujiweka sawa toka kwenye uzuni, “hoo! ni mambo ya kifamilia hayo, nilidhania kuwa umevurugana na Seni” alisema kwa utani Aisha, na hapo nikama alitonesha kidonda moyoni mwangu lakini nilijikaza kiume nisionyeshe wazi wazi.*****
Saa nane na nusu ndio muda ambao kengere ya mwisho wa vipindi iliposikika, na mimi nikaondoka zangu kuelekea Green house, nikiwaacha wakina mwalimu Aisha wakipanda gari la shule tayari kuelekea mjini, na wakati nakaribia Green house nikasikia simu yangu inaanza kuita toka mfukoni, hapo mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, kwa kihoro, “huyoooo anapiga simu” nilijisema huku natoa simu mfukoni, lakini nilipoitazama na kuliona jina la mpigaji nikajikuta nasonya na kuachia tusi kali sana la nguoni, alikuwa ni mzee Mangeu, hata hivyo sikuwa na budi kuipokea, pengine ingenipa ufanananuzi wa kinachoendelea nyumbani kwa akina Jessenia, nikaipokea na kuiweka sikioni, “hallow mzee nipe habari” niliongea kwa sauti tulivu nikijitahidi kuzuia hali niliyokuwa nayo, huku nageuka kutazama nilikotoka usawa wa duka lile ninalo nunuaga maji na soda.
Naam hapo ghafla moyo wangu ulishtuka vibaya sana kwa kile nilicho kiona.. ….…. ENDELEA NAYO
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SITINI NA SITA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TANO: “huyoooo anapiga simu” nilijisema huku natoa simu mfukoni, lakini nilipoitazama na kuliona jina la mpigaji nikajikuta nasonya na kuachia tusi kali sana la nguoni, alikuwa ni mzee Mangeu, hata hivyo sikuwa na budi kuipokea, pengine ingenipa ufanananuzi wa kinachoendelea nyumbani kwa akina Jessenia, nikaipokea na kuiweka sikioni, “hallow mzee nipe habari” niliongea kwa sauti tulivu nikijitahidi kuzuia hali niliyokuwa nayo, huku nageuka kutazama nilikotoka usawa wa duka lile ninalo nunuaga maji na soda.
Naam hapo ghafla moyo wangu ulishtuka vibaya sana kwa kile nilicho kiona.….…. ENDELEA..
Ilikuwa ni pikipiki aina ya Vesper, ambayo niliitambua kuwa ni ya yule bwana mandevu, ambae toka jana ananifUatilia, ikiwa imegeshwa pembeni ya duka lile, “kijana kwa kweli mpaka sasa hakuna ninacho kiona, maana mpaka sasa sijamuona mzee Juma akitoka wala Ussi au Jessenia, nadhani wageni waliokuja ni wa muhimu sana kwa Juma” alisema mzee Mangeu, ambae hakuonyesha kutilia mashaka yoyote juu ya wageni wale wa mzee Juma Mohamed, “kwahiyo ndio umeishia hapo mzee?” nilimuuliza mzee Mangeu, huku natazama vizuri pale dukani, ambapo pembeni ya duka kulikuwa na watu wanacheza bao la kete chini ya mti mkubwa wa muembe nikawatazama vizuri watu wale na kugundua kuwa mmoja wao ni mandevu.
Sikutaka kuhangaika nae, niliendelea kutembea huku namsikiliza mzee Mangeu, ambae naweza kumtaja kuwa ndie ndugu pekee wa Jessenia ninae mfahamu kwa sasa, “najuwa we kijana nilianza kukuamini, lakini saa naona mpango wako unakuwa fake, kwanini wang’ang’ania vitu visivyo na maana au una wivu leo hujamuona Seni” alisema mzee Mangeu kwa jazba, hapo nikashusha pumzi ndefu kujaribu kushuha hasira zangu, maana niliona kuwa mzee huyu ananizingua, “ok! tutaonana baadae, ila kaa kwa tahadhari hapo nyumbani kwako” nilimueleza na kukata simu, wakati huo nilikuwa naingia kwenye nyumba ya kijani, ambako niliweza kuwaona askari wakiendelea na usafi wa mazingira, kama vile kupunguza nyasi kupanga mawe vizuri pembezoni mwa barabara yakiwa yamenyooka vyema, huku wakiyapaka chokaa, (rangi nyeupe) kuokota kila taka taka ambayo inaonekana mahali pale.
Ukweli binadamu tumeumbwa na aibu, maana nilishindwa kupitiliza ndani nikalazimika kujiunga nao kuendelea na kazi ya kufanya usafi, mwanzo nilikuwa na kijiunyonge fulani, maana nilikuwa nawaza nini kinachoendelea kule kwa akina Jessenia, lakini kadiri muda ulivyozidi kusonga ndipo na mimi nilipoanza kusahau na kuchangamka kutokana na story zilizokuwa zinaendelea wakati wa kazi toka kwa wanajeshi wale, story zilikuwa ni mchanganyiko ungesikia wakizungumzia matukio ya wakati wa mafunzo, kwenye vyuo mbali mbali vya kijeshi, mara wangehamia kwenye simulizi za majukumu ya kivita au ulinzi wa amani, pia usinge kosa, maongezi ya matukio ya kimapenzi, ukweli nilipenda sana maongezi yao, ambayo yalinifanya nifanye kazi kwa masaa mawili pasipo kuchoka, hata mkuu wa kambi ambae hapo mwanzo hakuwepo, nilisikia askari wakisema kuwa, alienda kuwapokea wageni toka unguja na dar es salaam, ambao ni makamanda wakuu wa jeshi waliokuja kwaajili ya ziara ya raisi wa Zanzibar, alipokuja na kuniona alisifu sana kitendo kile cha mimi kushiriki kazi za usafi wa kambi, wenyewe wanaita fatik, “ticha habari ya kazi bwana” alisalimia mkuu wa kambi, ambae alikuwa ameongozana na baadhi ya wanadhimu wake, yani afisa utawala, sajenti mkuu wa kambi, wenyewe wanaita, Regment Surgent Major, yani RSM, walikuwepo na baadhi ya maofisa wengine kama vile wakina Luge, Komba na wengineo, “safi tu mzee, tupo tunawajibika” nilijibu kwa sauti ya uchangamfu, maana nilisha acha kuwaza juu ya nyumbani kwa kina Jessenia, “karibu mess jioni, kutakuwa na wageni wengi sana” alisema mkuu wa kambi, huku anaondoka na jopo lake, akiwa amesha toa maagizo kuwa askari waende kupumzika na kujiandaa kwaajili ya kesho kuja kazini.
Lakini wakati naelekea kwenye jengo la Green House, nikasikia, “shemeji! shemeji! samahani shemeji” ilikuwa sauti ya kike toka nyuma yangu, nikageuka na kumtazama muitaji, “hooo! shemeji niambie” alikuwa ni mke wa Mwasenga, ambae alikuwa amevaa sale za kazi zile za kijani, wenyewe wanaita OG, ikiwa ni kifupi cha Over Green, yaani shati la kijani mpauko sana, na skirt ya kijani iliyo pitiliza, juu kofia ya kijani iliyofanana na rangi ya skirt yake, sokx na viatu vyote vikiwa ni vyeusi, siyo buti ni right shoes, “mambo shem, yani afadhari nimekukuta, maana nilikuwa nawaza nitaendaje nyumbani, halafu mbaya zaidi natakiwa kurudi mess jioni” alisema mke wa Mwasenga akiwa amesha nifikia.
Mkewe wa mwasenga aliniambia kuwa lengo la kunifwata ni kwamba alikuwa anahitaji gari, maana gari lake lilikuwa limeishiwa mafuta, hivyo alitumia gari la jeshi kuja kazini, sasa alichokwama ni kwamba alitakiwa kuwahi nyumbani akajiandae ili akasimamie wahudumu wa kiraia pale mess waliochaguliwa kuwa hudumia makamanda wageni, waliokuja toka sehemu mbali mbali kwaajili ya ziara ya Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, hivyo tukakubaliana kuwa nijiandae haraka akaniache uwanjani, kisha Mwasenga ambae leo alikuwa ni mmoja wa madereva wanao waendesha wakuu mbali mbali waliokuja toka dar es salaam na unguja, angekuja kunichukuwa na kunipeleka pale wawi mess, ambapo ningelikuta lile Toyota spacio, na kuelekea Ali Khamis Camp.******
Saa kumi na moja kasoro ndio muda ambao nilifika uwanjani na kukuta mazoezi yameshaanza, sikuwa nimepokea simu ya aina yoyote toka kwa Jessenia insp Aroub au babu Mangeu, nilikuwa katika hali ya sinto fahamu, sikuweza kuchukuwa maamuzi ya kwenda mtaani kwao kujaribu kuchunguza, maana nilisha juwa kuwa tayari Ussi na vijana wake walikuwa wanafahamu wkuwa ninatembea na Jessenia, na ukichukulia kuwa Ussi alikuwa na wivu mkubwa sana na dada yake, wivu ambao mpaka sasa sikuwa najuwa sababu za msingi za wivu huo kwa dada yake, kiukweli ingekuwa ni hatari kwangu.
Nilijiunga kwenye mazoezi na kucheza mpira kama ilivyo kawaida yangu, huku shemeji yangu akiondoka kurudi tulikotoka kwa lengo la kwenda nyumbani kwao Macho manne, akabadili nguo na kuelekea Wawi,wakati nimezama kwenye mchezo ni kama niliondokewa na unyonge, kwa kujisahaulisha ukimya wa Jessenia, maana hao wengine sikuwafikiria sana, maana nilishaona kuwa hawakuwa na mawazo kama ya kwangu, yani kuwatilia mashaka wageni wa mzee Juma, waliopokelewa na Ussi asubuhi ya leo, nilicheza mpira kwa uchangamfu nikifanya vyema kama kawaida yangu.
Lakini wakati tunaendelea kucheza, mchezo ukiwa umekolea kweli kweli, nikamuona Maimuna akiwa amesimama karibu na lango la kuingilia kwenye uwanja wa makazi yale ya watumishi wa serikali, akiwa pamja na mdogo wake yaani Yassin wakitazama mpira wa kikapu, na hata macho yetu yalipokutana, nilimuona akitabasamu na kutazama chini kama vile anaona aibu flani hivi yenye kusisimua, sikujali sana, maana akirini mwangu sikuwa namfikiria Maimuna katika swala la kupeana dudu, hasa kutokana na aina ya mapenzi aliyokuwa anataka tushiriki, lakini haikusaidia kitu, maana kila nilipotazama upande wake kwa bahati mbaya, nikamuona ananionyeshea mkono wake alioufumbata kiganja, akimaanisha kuwa kunakitu kwaajili yangu kwenye mkono wake, haikunishtua maana nilijuwa nitapata njia ya kumkwepa tu.
Wakati tuna endelea kucheza mpira sasa tukiwa tunakaribia kumaliza mazoezi, mara nikaona watu wanatazama upande wa barabara inayotokea hospital yaani ile njia tunayojia, sio wale tu waliosimama nje ya uwanja, hata wale waliokuwa wanacheza nao walitazama upande ule, ni wazi kuna kitu walikuwa wanatazama na kama ujuavyo binadamu huwezi kuepeuka kutazama, hivyo na mimi nikashawishika kutazama upande huo.
Naam hapo sasa kwa macho yangu mawili, niliweza kumuona Jessenia akiwa anakuja kwa mwendo wa taratibu kama vile anavihurumia viatu vyake vizuri alivyo vivaa, kwamba asivikanyage kwa nguvu, huku wakiwa katika muonekano wa kupendeza sana, ukiachilia uzuri wake wa sura na rangi ya ngozi yake, ambayo iling’aa kama mwarabu pia alipendeza kwa nguo alizovaa, ungesema alikuwa na mwaliko harusini, hakika ungemuona jioni yaleo, ungesema ni binti mfalme wa #mbogo_Land, ambae alitembea taratibu huku macho yake yana tazama kushoto na kulia, kama vile anaangalia kitu fulani eneo lile la uwanja, na alipokikosa akama tazama ndani ya uwanja tulipokuwa tuna cheza, hapo macho yetu yaka kutana, nikamuona anaachia tabasamu moja pana sana lililosheheni furaha, kiasi cha kuwashangaza wale wote waliokuwa wanamtazama na wasijuwe anamtabasamulia nani.
Jeseenia alisalimiana na watu wawili watatu waliokuwa karibu na kule alikokuwa anapita akienda moja kwa moja na kukaa kwenye kiambaza cha ofisi za KVZ, kisha kwa mara nyingine akaelekeza macho yake kwangu, na macho yatu yalipokutana tena safari hii akapunga mkono huku anaachia tabasamu pana sana, kiasi cha kunishangaza hata mimi mwenyewe, maana sikufikiria kama binti wa kipemba anaweza kufanya hayo hadharani kwa mwanaume ambae, hajaenda hata kujitambulisha nyumbani kwao, hapo watu wote wakageuza nyuso zao kuni tazama ninae pungiwa mkono, ambae pia nilishindwa kujizuia na kujikuta nikiwa nimeinua mkono kumpungia yeye, kisha nikaendelea na mazoezi.
Nakumbuka baada ya adhana kusikika, na kukatisha mazoezi nikatazama pale aliposimama Maimuna na mdogo wake, wote hawakuwepo, sikuwajali sana nikageukia pale nilipoacha vifaa vyangu, yaani begi langu,hapo ndipo niliposhtuka, maana niliweza kumuona Yassin akiwa amesimama huku amrshikilia begi langu, ambalo vifaa vilivyomo ndani huwa ni hatari sana kwa mtoto kama huyu kuvishika.
Nikaongeza mwendo kumfuata, huku najiuliza kwanini yule dogo amefanya hivi, yaani kushikia begi, swali ambalo nilipata jibu lake muda mfupi baadae, “niambie dogo, mambo vipi?” nilimsalimia dogo huku napokea begi toka mkono mwake, “safi, umecheza vizuri sana leo” alisema yule dogo huku ananiachia begi, ambalo alikuwa ameambatanisha na kipande cha karatasi, ambacho nilipogundua kuwa amenipatia nikakishika vizuri na kufungua begi langu nikakiweka ndani yake, wakati huo tayari dogo alisha ondoka zake, na mimi nikamfuata Jessenia, huku nimemkazia macho usoni kwake, nikijaribu kumsoma hisia zake na hali aliyokuwa nayo, nikiambulia tabasamu na macho yaliyojaa aibu, nikaendelea kumfuata huku nikiwa na hamu ya kujuwa kilichojili nyumbani kwao, hasa juu ya wagen
wao toka unguja na wakati huo huo najiuliza kilichokuwepo ndani ya kipande cha karatasi aliyonipatia Yassini, yani mdogo wake Maimuna, “pole sana naona umenipigia sana….….…. ENDELEA..
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SITINI NA SABA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA SITA:na mimi nikamfuata Jessenia, huku nimemkazia macho usoni kwake, nikijaribu kumsoma hisia zake na hali aliyokuwa nayo, nikiambulia tabasamu na macho yaliyojaa aibu, nikaendelea kumfuata huku nikiwa na hamu ya kujuwa kilichojili nyumbani kwao, hasa juu ya wagen
wao toka unguja na wakati huo huo najiuliza kilichokuwepo ndani ya kipande cha karatasi aliyonipatia Yassini, yani mdogo wake Maimuna, “pole sana naona umenipigia sana….…. ENDELEA..
lakini na mimi nilipiga sana ukawa hupokei simu, hivyo nikajionea nije kukutazama hapa” alisema Jessenia huku tabasamu likiwa halikauki usoni mwake, “nadhani nilikuwa nimeshaanza mazoezi” nilimjibu hivyo huku na fungua zip ya begi langu na kutoa simu yangu na kuibofya, nikaona missed call kadhaa toka kwa Jessenia nyingine toka kwa mzee Mangeu, ambazo sikuzijari sana, maana nilijuwa hatokuwa na jipya, “mbona gari sijaliona au amesha lichukuwa mwenyewe” aliuliza Jessenia huku anajiinua toka pale alipokaa na kushika mkanda wa begi langu kwa nia ya kulipokea, “yah! amelichukuwa, ila baadae atakuja kunichukuwa” nilisema hivyo huku na mzuwia asilichukue begi, “nataka ni badili nguo” nilimueleza huku naweka begi kwenye kimbaza cha KVZ nakulifungua, halafu nikatoa tishert na truck kwaajili ya kuvaa, “pole sikupokea simu zako, nilikuwa na maongezi na wakina shangazi” alisema Jessenia, kwa sauti ya chini na yenye kubembeleza huku ananitazama mimi niliekuwa navua tishrt niliyotoka nayo uwanjani, hapo kuna kitu kikagonga akilini mwangu, ni kuhusu wageni waliofika nyumbani kwao, nikaona ndio wakati wakuanza kupata habari, “vipi walikuwa wanakusimanga au” niliuliza huku naweka lile tishert kwenye ule msingi wa kiambaza cha KVZ, “bora ingekuwa kunisimanga peke yake, kuna makubwa yame tokea huko” alisema Jessenia, huku anachukuwa lile tisherit nakulishika mkononi pasipo kuwa tazama watu waliokuwa wanaondoka zao, ambao walikuwa wakitutizama kwa macho ya wizi wizi, niliwaona lakini sikutaka kuwaonyesha kama nawaona, “he! kumbe lakini si uliniambia kuna wageni pia” niliuliza nikijifanya sijui lolote, “haswaaa ndio walioleta mtafaruku, yaani huko nyumbani hakuna anae msemesha mwenzie” alisema Jessenia, na hapo nikaanza kupata jibu la kile nilicho kihisi.
Nilimaliza kuvaa truck ya chini juu ya bukta niliyofanya nayo mazoezi, huku Jessenia akinisaidia kuweka tisht kwenye begi, halafu tukaondoka zetu taratibu kuelekea upande wa markiti na yeye akianza kunisimulia kilichotokea nyumbani kwao.*******
Ilikuwa hivi, leo Jessenia aliamka mapema kidogo, japo hakutoka kitandani alibakia hapo anawaza hili na lile, hasa mambo ambayo tuliyafanya jana wakati tuna peana dudu, mawazo ambayo yalimfanya atamani kuja Green Mess nimpe dudu, lakini ndiyo hivyo tena alishaambiwa kuwa kuna wageni wanakuja pale nyumbani kwao, na hata baada ya kuongea na mimi na akatoka nje ambako alishangaa kukuta wanawake kadhaa, ambao walikuwa wakijishughurisha kuandaa mapishi, ambayo yalionekana kuwa ni ya chakula kizuri na maalumu, “ilinishangaza kwa sababu sikuelewa umuhimu wa wageni hao, maana maadalizi yalikuwa makubwa sana” alisema Jessenia huku tukiwa tuna endelea kutembea kukatiza eneo la sokoni, na kuikamata barabara kuu itokayo mkoani kwenda wete, tukapanga tutembee taratibu mpaka kwenye ile njia panda ya juu, kisha tuingea misingini kupitia upande ule.
Lakini kilicho mshtua zaidi, ni kitendo cha shangazi yake kumueleza kuwa anatakiwa kuoga na kujiandaa kwaajili ya ujio wa ugeni huo, Jessenia hakuwa mbishi akaenda kuoga na kujifungia chumbani akijiandaa kwa ajili ya ugeni, hukuelewa kuwa lengo la shangazi yake ni kuwa kutokana na kuwa yeye ni mwanafamilia lazima wageni wamkute katika muonekano mzuri, japo yeye ni mzuri tu.
Jessenia akiwa hajuwi lolote akaingia ndani na kujiandaa kueleka bafuni, ambapo mpaka saa nne alikuwa amesha maliza kuoga na kuvaa, huku muda wote akiombea wageni waondoke haraka ili aje akutane na mimi, akatoka akiwa amesha jipodoa kweli kweli, wakati huo tayari wageni walikuwa wamesha ingia pale nyumbani, “we! Hutakiwi kutoka nje hebu rudi ndani, subiri nitakacho kuambia” Jessenia aliambiwa na shangazi yake mara tu alipoonekana akitoka nje ya chumba chake, “hapo nikaanza kuingiwa na mashaka juu ya ugeni ule na ukichukulia kuwa nilikuwa na ugomvi na mjomba kwaajili yako” alisema Jessenia, ambae aliendelea kueleza kuwa safari hii hakuingia chumbani peke yake, aliingia pamoja na mama mmoja mtu mzima, na dakika chache baadae akaingia shangazi yake na kuzidi kumtia mashaka, hasa alipoona analetewa chai na huduma nyigine kule kule chumbani, “shangazi, kwani kuna nini kinaendelea?” aliuliza Jessenia, ambae mpaka muda huo hakuwa amewaona wale wageni ambao aliambiwa wamesha ingia wala kujuwa walikuwa wamekaa wapi, maana kuna sebule ya chini na juu, pia kulikuwa na sebule ya michezo ya watoto, ambayo haikuwa inatumika sana, maana hawa kuwa na watoto, “wasi wasi wa nini Seni, tulia vitu vizuri havitaki haraka” alijibu yule mama mwingine, na hapo Jessenia akatulia kidogo kujitafakari na majibu ya tafakari yake yalikuwa ni kwamba, lazima kuna jambo ambalo linataka kutokea, na mpaka sasa limefanywa kuwa siri, na jambo hilo linamuhusu yeye Jessenia moja kwa moja.
Hakika alianza kujiwa na mawazo mengi sana, ukizingatia jinsi mambo yalivyokuwa yanaenda, yana fanana na siku ambayo alikuja kuchumbiwa na yule kijana anae fanya kazi #mbogo_land, kijana ambae kwa sasa ni marehemu, “au Eric ameamua kunifanyia surplise” aliwaza Jesenia, ambae aliona ni vyema kama atapiga simu kuniuliza juu ya swala hilo, lakini ile anachukuwa simu tu! shangazi yake akamdaka, “hebu achana nayo kwanza, huwezi kusubiri kwanza mambo muhimu yapite” ndivyo shangazi yake alivyosema, huku anamnyang’anya simu na kuiweka juu ya kabati, “shangazi kwani kuna nini ambacho huwezi kuniambia” aliuliza Jessenia, lakini hakuna aliemjibu.
Naam hapo Jessenia akatulia kusubiri kitachotokea huku mawazo yakimtawala na kujaribu kubashiri jambo linalotaka kutokea, na lile alilo lihisi kwa kiasi kikubwa ni kuchumbiwa, “kwanini sasa ameamua kufanya siri, si angenijulisha tu ili nijuwe nisiwe na kihoro” aliwaza Jessenia na wakati huo huo akaanza kusikia simu yake inaita toka juu ya kabati, hakujuwa ni nani anapiga, lakini bahati mbaya hakuruhusiwa kwenda kuichukuwa simu yake, ambayo iliita kwa muda mrefu na kukatika, ikaita tena na tena, lakini hakuruhusiwa kuipokea wala kuisogelea, ilimchukiza sana Jessenia, ambae alijitahidi kujizuia asionyeshe jinsi alivyo kasirika.
Hivyo basi Jessenia akiwa hana hili wala lile, akaendelea kusubiri mule chumbani, mpaka alipoamriwa atoke chumbani na kwenda kuandaa chakula cha wageni, ambao sasa aligundua kuwa walikuwa sita ndani ya ile sebule ambayo ilijengwa kwa lengo la kuchezea watoto, ambamo mulikuwa mume andaliwa vizuri sana kwa kutandikwa majamvi na mito (mapillow) wageni walikuwa wamevalia kanzu zao nzuri tena mpya kabisaaa, na baraghashia zao pia mpya kabisa, kati ya wale wageni sita lakini kitu cha ajabu, hakuweza kuniona mimi wala mtu anae mfahamu, labda kama wakina Mwasenga au mashekhe au majirani, maana hata kule jikoni wale wanawake hawakuwa wa pale jirani.
Hapo akiwa na wasi wasi na mashaka mengi, Jessenia akaendelea kuwahudumia wale akishirikiana na waschana wengine wawili, huku kila anapopita mbele ya wale wageni waliokuwa wamekaa na mjomba wake na binamu Ussi, huku kilichomtia mashaka zaidi ni kwamba, kitendo cha uwepo wa wale wageni pekee pasipo wazee wengine anao wafahamu, “sijui kuna kitu gani kinaendelea?” alijiuliza Jessenia baada ya kuona kuwa tukio lile halikufanana na tukio halisi la kuchumbiwa, lakini bahati nzuri jibu akalipata baada ya lisaa limoja, yaani mida ya saa nane, baada ya wao na wageni kumaliza kupata mlo wa mchana, ndipo wa mama kadhaa walipoingia chumbani huku wakionekana wenye nyuso za furaha, lakini hakukuwa na vigeregere kama ilivyo kawaida, “hongera mwanangu, umepata mchumba, kijana tajiri kijana mzuri, anaishi unguja sasa unachotakiwa ni kwenda sebuleni akakuone” alisema shangazi yake Jessenia, huku yeye na wenzake wakiwa na nyuso za furaha, lakini tofauti na mchumbiwa mwenyewe alie kuwa ametoa macho kwa mshangao, na kabla haja uliza chochote, akashikwa mkono na kuanza kupelekwa sebuleni kimya kimya, pasipo vigeregere wala shangwe, ni kama hawakutaka mtu mwingine yoyote wa nje ya nyumba ile asikie, “shangazi naomba tuongee kwanza” alisema Jessenia, akimueleza shangazi yake ambae hakutaka kumuelewa, “tutaongea baada ya kumaliza swala hili, wewe si unahitaji kuolewa, sasa mchumba amesha patikana” hilo ndilo lilikuwa jibu la shangazi.
Hapo Jessenia hakuwa na lakufanya zaidi ya kuelekea sebuleni, ambako mjomba alimtambulisha kwa wageni, “jamani huyu ndie binti ambae mumehitaji aolewe na kijana wenu, bahati nzuri kwenu na yeye alikuwa anahitaji kupata mwenza kwa muda mrefu sasa” alisema Mzee Juma, akiwa mwenye uso wa wenye tabasamu pana, kisha akatazama Jessenia, ambae alikuwa ameinamisha kichwa chake chini,
Jessenia akaona tayari mambo yanaanza kuchanganyika, “Seni, hawa wageni wamekuja kwaajili yako, huyu kijana Mussa Nyange Makame, toka Unguja” alisema Mzee Juma Mohamed, huku akitarajia kumuona Jessenia, anainua uso wake kumtazama kijana huyo alie mtambulisha, lakini haikuwa hivyo, Jessenia alibaki ameinamisha uso wake, “kama ulivyo utaratibu, sisi ndio wenye kukubali uchumba, hivyo tumeridhia Jessenia kuolewa na Mussa, kwa hivyo kinachofuata ni kesho kuandaa ndoa mara moja ili muondoke na mke wenu” alisema mjomba wake Jessenia, na hapo yakapigwa makofi machache bila vigeregere, ni kama waliambizana swala lile liwe la kimya kimya, hawa kuacha kupeana mikono ya pongezi.
Hapo kiukweli Jessenia alihisi tumbo lina unguruma kwa mshtuko, “samahani mjomba” alisema Jessenia kwa sauti ya upole na tulivu, huku uso wake ameuinamisha, watu wote wakatulia na kumtazama Jessenia, “hapana Jessenia, huwezi kuongea katika kikao hiki, hapa ni maauzi ya baba na wazee tu” alisema shangazi yake Jessenia, huku anamshika mkono na kutaka kumuinua pale alipokaa, lakini Jessenia akajipapatua toka kwa shangazi yake, “hapana ni lazima niongee hili hata yeye Mussa ajuwe” alisema Jessenia, na hapo mjomba akaingilia kati, “haya tutaongea, ila sasa tumesha kamilisha swala hili, wewe nenda chumbani kwako mimi nakuja huko huko, alisema mjomba na hapo Jessenia akainuka na kuongozana na shangazi yake kuelekea chumbani kwake, wakifuatiwa na wamama wengine wawili, hivi “Seni, mbona unataka kutia aibu kiasi hiki, kosa letu kukutunza toka utotoni, tume kulea kama binti yetu, tumekupa kila kitu leo unataka kututia aibu namna hii kwanini lakini?” alianza kuongea shangazi kwa sauti ya chini, lakini yenye kujaa lawama na ulalamishi, “lakini shangazi, si nilisha kuambia kuwa nina mchumba” alisema Jessenia kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kujawa na machungu ya kile kinachoendelea, “lakini yule sio wa huku, isitoshe sio dini yetu” alisema shangazi yake Jessenia kwa sauti ya sisitizo, “hiyo sio sababu shangazi” alisema Jessenia, lakini haikusaidia kitu, ulizuka mjadala mkubwa na mrefu, ukitumia masaa mawili yani mpaka saa kumi na moja kasoro, mjomba alipoingilia kati na kumaliza kikao kile ambacho sio rasmi, “kwanza hapa munapoteza muda wenu bure tu, kila kitu kimesha malizika, kesho unaolewa na utaondoka jioni na mume wako” alisema mjomba na kutaka kuondoka, lakini Jessenia akamuwahi, “mjomba sijajuwa tatizo nini, kama ni kuolewa na Mussa mimi sipo tayari, ila kama ni kuolewa ili nitoke hapa nyumbani basi mchumba ninae, na ninaweza kuondoka hata sasa hivi, ilimradi nyie mumeridhia” alisema Jessenia kwa sauti tulivu, maana muda wote alikuwa anajitahidi kujizuwia asiongee kwa hasira, “Seni, kama mimi nilie kulea toka utotoni utaolewa na mussa” alisema mzee Juma huku ametoa macho kwa jazba, “hapana mjomba, kwa heshama yangu sito
olewa na mwanaue mwingine zaidi ya huyu nilie nae sasa, zaidi ya hapo nitakosa uaminifu kwa mwanaume yoyote” alisema Jessenia akionyesha kuto kukubaliana na mjomba wake, ambae sasa alighairi kutoka nje na mjadala ukaanza upya, “kwahiyo umekuwa na kiburi kwaajili ya wanaume huyo sio, hivi angekuwepo mama yako ungefanya unayo yafanya?” aliuliza shangazi yake, “mama asinge zuwia kuolewa na mwanaue ambae amemaliza tatizo langu, hata nyie nashangaa ni kwanini munashindwa kuliona hilo, nilitegemea baada ya kulijuwa hilo mnge jaribu kukutana na huyo kijana, kweli mjomba unaweza kuniozesha bila hata kuniuliza mahari yangu ni kiasi gani, au kwa kuwa mimi sio binti yako?” hapo ndipo Jessenia alipoona mjomba wake na shangazi yake wakitazama kwa macho ya kujilaumu, kwamba kuna jambo walilikosea….….…. ITAENDELEA MUWE NA USIKU MWEMA