KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TATU: kwamba ile nyumba alivyoinunua kwa vipande vya dhahabu, amuache aishi kijana mwenzie Juma Mohamed, ambae alikuwa na mke na mtoto moja mdogo wa kiume, mwenye miaka mitatu alieitwa Ussi, kijana Juma Mohamed, yeye hapo mwanzo alikuwa ni mfanyakazi kwenye ile nyumba ya mwarabu, aliempatia nyumba Zidadu, kijana ambae naweza kusema ndie pekee aliekuwa anafahamu uwepo wa Aisha pale kwenye kibanda, Zidadu alimuacha aishi pale kutokana na mambo matatu, moja ni kwamba yule kijana alikuwa ni mwenyeji wa Unguja, hivyo lafudhi yake ilikuwa ni ya kizanzibar, na muonekano wake haukuwa na shaka yoyote kama ilivyo kwa Zidadu aliepasuka pasuka usoni…..ENDELEA..
Pili ni kwamba kijana huyu hakuwa na sehemu ya kuishi yeye na familia yake baada ya mwarabu kwenda kwao, hivyo Zidadu akaona itakuwa vyema kama atamuachia aishi pale kwa shariti la kumlea Jessenia mpaka mschana huyu atakapoolewa na kuanza maisha yake ndipo akabidhiwe nyumba yake na kila kitu ambacho kina muhusu, tatu zidadu alifanya hivyo kwa kuhofia usalama wa Josepiner, ambae alimbadilisha jina kabla ya kumkabidhi kwa Juma Mohamed kuwa aitwe Jessenia, maana aliamini kuwa lazima miaka ya hapo baadae familia ya Abdulkarim ingerudi na kutaka kumaliza kile walicho kianzisha, endapo wange gundua kuwa mtoto Josephiner yupo hai, sasa kutokana na uchotara aliokuwa nao na jina la Josephiner vinge leta utata na kumsababishia matatizo mtoto huyu, ambae ukiachilia jumba kubwa alilokuwa nalo pia kulikuwa na hazina kubwa ya mali iliyofukiwa ndani ya kibanda kile cha bwana Zidadu.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha ya kuto kufahamu historia yake mschana Jessenia, ambae alimtambua Juma Mohamed kama mjomba wake, bwana Juma alimlea Josephiner yaani Jessenia wa sasa kwa upendo mkubwa sana, huku akimpatia kila kitu na bwana Zidadu ambae alisimamia malezi ya Jessenia kwa ukaribu mkubwa na kuhakikisha yanaenda kama alivyo taka alijitahidi kuwa karibu na Jessenia ili siku akimueleza ukweli asishangae, alijitahidi kumpatia vijizawadi mbali mbali za vitu wapenda vyo watoto, huku na yeye akipanga kuwa na maisha yake mapya mara baada ya Jessenia kuwa mkubwa na kuwa na maisha yake.
Zidadu alipoteza ndoto za kuwa na maisha mapya miaka saba baadae, ni pale alipoanza kutengwa na jamii kwa kuhisiwa kuwa ni mshirikina, mwanzo hakujuwa sababu, lakini baadae akajuwa sababu ni muonekano wake wa usoni, ilifikia kipindi akawa anatolewa mifano ya kwenye maongezi ya husuyo ushirikina, huku akipachikwa jina la utani kama babu mangeu, hata Jessenia ambae ndie mtu pekee aliemfanya bakie pale kisiwani Pemba ilifikia wakati na yeye akamkimbia na kuwa nae mbali, na pengine kuanza kumchukia kabisa, wakati huo aliendelea kuhakikisha anafanya kila linalowezekana ili Jessenia akulie kwenye maisha ya kifahari na kitajiri, ikiwa ni juhudi za mama yake kuiba mali zile kwa mwarabu Abdi Jamal, hivyo alihakikisha ananunua magari kadhaa ya kifahari na kumkabidhi bwana Juma Mohamed, ambae alionekana kuwa ni miongoni mwa matajiri pale Pemba.
Babu Mangeu anasema kuwa, mambo yalizidi kuwa magumu pale alipoanza kushutumiwa juu ya vifo tata vya watu vinapotokea pale mtaani au mitaa ya karibu, jamii ilizidi kumtenga huku watu wakitumia jina lake la utani la babu mangeu, kama kitisho kwa watoto na watu wazima, hakuna ambae alimsogelea karibu, hakika asingeweza kuoa kwa ile sifa chafu aliyopewa, hakujuwa ni kwanini wananchi wameamua kumpa sifa ile ambayo hakustahili, lakini siri alikuwa nayo yeye na bwana Juma Mohamed.
Mtoto Jessenia aliendelea kukuwa na kusoma kwa juhudi, huku lengo la Mangeu yaani bwana Zidadu likiwa ni kumsomesha mpaka Elimu ya juu ili aweze kujimudu katika maisha yake, hata akiolewa awe tayari mwenye elimu na aweze kusimamia mali zake, japo mschana huyu ambae aliendelea kukuwa na kupendeza alipotimiza miaka kumi na nane, alianza kupata tatizo ambalo kila mmoja alimini kuwa kuna jini lime muingia, na halitaki akutane na mwaume, jini ambalo lilimuuwa kila mwanaume aliemsogelea, na lilisha uwa vijana wengi sana, “hata mimi mwanzo niliamini hivyo, maana nilimuagiza Juma ampeleke Jessenia kwa waganga na mashehe, nao walisema kuwa kuna jini linamzonga, hakika niliona kuwa binti huyu amekosa bahati ya maisha” alisema Mangeu, ambae aliendelea kunisimulia kuwa, kuna wakati alitamani kumuondoa Jessenia kutoka pemba na kumuhamishia bara, ndipo alipoanza kufanya safari za siri kwenda dar es salaam ambako alinunua eneo mbezi msakuzi na kujenga nyumba kubwa sana ya kisasa na yakifahari, ambayo licha ya kuwa na mitambo maalumu ya ulinzi na usalama pia kuna kampuni binafsi inalinda jumba hilo la ghorofa tatu, ambalo lina kila kitu ndani nje, kiasi cha kumfanya mtu yoyote kuweza kukaa ndani yake pasipo kutoka nje kwa mwenzi mzima, huku akiburudika, na zoezi la kumuhamisha Jeseenia alilipanga kuwa siri, hakutaka mtu yoyote ajuwe, maana aliona Jeseenia akiendelea kushi Pemba maisha yake yataishia kuwa ya tabu na misuko suko.
“ujuwe kuna kipindi nilianza kuona kama Juma anamuacha yule kijana wake mlevi amuingize Jessenia kwenye majaribu pasipo kujari kitakacho mtokea kijana wake,(ile siku wameondoka familia yote na kubakia ussi na seni peke yao) na pengine siri ya kwamba Jessenia anaandamwa na jini ingefichuka na watu kuanza kumtenga Jessenie, nilimpa onyo kali sana Juma, nikimtishia kumfukuza pale nyumbani, vinginevyo amuweke mbali kijana wake Ussi na Jessenia, nadhani alifanikiwa maana sijaona tena, na tukio lile mimi ndie niliezuia jambo hilo kwa kumueleza Jessenia kwamba asije akamsababishia kaka yake matatizo, nilifanya hivyo kwa maana mbili, moja kumuepusha Ussi na kifo, na pili ni kwamba, sikutaka itokee hata bahati mbaya Ussi afanikiwe kumuingilia Jessenia na pengine kumuoa, maana angekuwa ndie kijana pekee anaweza kuwa nae baada ya kulishinda jini, sikutaka iwe hivyo kwa sababu Ussi ni mlevi kupindukia na ni mzinzi” alisema Mangeu, ambae alisimulia kitu ninacho kifahamu, yaani alisha nisimulia Jessenia mwenyewe.
Lakini wakati anajiuliza atafanyaje ili amuamishe Jessenia kwenda dar es salaam pasipo hata bwana Juma kufahamu, na yeye akilazimika kumueleza Jessenia kuhusu uhalisia wake, “mara ya kwanza nilikuona wewe na Seni mukiongea huku mukiwa na dalili za wazi za mapenzi, hasa Seni, nikataka kukupa onyo ukanikimbia, nikasema wacha nikufuatilie, nilichukuwa pikipiki yangu na kukufuatilia bahati nikakuona unapanda gari la jeshi, hapo nikajuwa wewe ni mwanajeshi, nikakufuatilia mpaka Wawi, ambapo uliondoka na gari jingine, nikafuatilia mpaka unapoishi na siku ya pili yaani jana nikagundua kuwa wewe ni mwalimu, nikasema lazima nitafute nafasi ya kuongea na wewe haraka, kabla hujauwawa na jini, japo kwa upande fulan nilitilia shaka kuhusu mambo yalivyokuwa yanaenda, maana kipindi kile ambacho alikufa yule kijana Abdulqadir” alinieleza Mangeu tukiwa bado tumesimama nje ya gari, “licha ya kuhisi kuwa unaweza kuingia kwenye hatari pia nilianza kuona dalili ya wewe kuepukana na kifo, baada ya kukuona siku ya pili ukiwa unatoka pale unapoishi na kuelekea shuleni, na jioni nikakuona ukiwa na Jessenia mnafanyiana michezo ya kupuuzi ndani ya gari” alisema mzee Mangeu, na hapo nilishindwa kujizuwia nilicheka kidogo, “ukweli nilipatwa na hofu kubwa sana, nilijuwa huwezi kumaliza hata lisaa kabla hujapoteza uhai, japo nilikuwahi na kukueleza kuwa ukae mbali na Jessenia, nadhani hukunielewa, maana sikuweza kukuambia ni kwanini ukae mbali na Seni, kwa sababu tulipanga iwe siri yetu, yaani mimi Jessenia na bwana Juma” alifafanua Mangeu, na kuendelea kunieleza kuwa, “ila mpaka sasa nadhani tayari kuna jambo limesha fanyika kati yako na Jessenia, nipo hapa kukueleza kuwa shukuru sana kwa kumfungua binti huyu kutoka katika kifungo kikubwa, ila pia ninapenda kujuwa ulitumia dawa gani kufanikisha kuwa nae pasipo wewe kudhurika?” aliniuliza Mangeu, na hapo nika tabasamu kidogo, “kwahiyo unanipeleleza sio?” nilimuuliza Mangeu kwa sauti kavu kidogo, nikijifanya kumpiga biti (kumtishia) “nadhani wewe unajuwa maana ya kupeleleza na mtu anaetaka kujuwa, na usijaribu kunitishia kijana, ujuwe nipo tayari kufanya lolote kwaajili ya amani na usalama wa Seni” alisema Mangeu kwa sauti kavu, akionyesha hakuwa na utani hata kidogo, “sikia mzee, mimi toka napata ufahamu na kujitambua kuwa mimi ni nani, sijawahi kutumia dawa yoyote ya kishirikina, hivyo hakuna chochote nilich tumia” nilimjibu Mangeu, wakati huo nikisikia simu yangu inata toka mfukoni, nikajuwa atakuwa ni Jessenia ndie anaepiga, nikaivungia kwa maana ya kwamba nitampigia baada ya kuachana na Mangeu, “sawa sasa hebu nieleze wewe ni nani hasa na umefwata nini hapa pemba” aliniuliza Mangeu na hapo akanishangaza kidogo kwa swali lile ambalo lilionyesha wazi kuwa anapingana na kazi yangu ya ualimu, “mimi ni mwalimu, au inaihtaji mkalimani kulielezea ilo?” nilimjibu kwa jeuri, ili kumpoteza asiendelee kuuliza swali hilo lenye jibu harisi la ukweli, “sawa kijana, basi kuna mambo mawili naomba niyaweke wazi kwako, kabla sijakuacha ukapumzike, ni kwamba kijana kama ni kweli huku tumia chochote, na wewe mwalimu basi ukae ukitambua vita bado inaendelea, hivyo jihadhari kwa kila unacho kifanya na kwa kila hatua unayokanyaga” alisema Mangeu, na bahati nzuri hilo nilishalitambua, maana kuna watu nimetoka kupeana nao kisago, hapo ngerengere muda mfupi uliopita, “pili kijana wangu, lazima utambue kuwa ukiachana na hilo jini ambalo ni adui yako namba moja, mimi ninaweza kuwa adui yako namba mbili, endapo utafanya jambo lolote la kipuuzi kwa Jessenia, kwahiyo nakuomba uchague moja kati ya mawili, la kwanza ni kumuacha kistaarabu, kama unaona hauna mpango nae wowote, maana hatujui kama una mwanamke mwingine huko kwenu au laa umuoe na kwenda nae bara, ambako naamini mutaishi kwa amani, nipo tayari kugharamia kila kitu na nitawakabidhi kila kinacho muhusu Jessenia, naamini Jessenia mpaka hapo ameweka imani yake na upendo wake wote kwako, kwa kuwa anaamini kile ninacho amini kuwa wewe ndie mwanaume wake wa pekee” alisema yule mzee ambae alimalizia kwa kusema kuwa “nikikuona nae kesho naamini umechagua jambo la mwisho, zaidi ya hapo sitajali wewe ni nani, uwe mjeshi au mwalim, na ume fwata nini Pemba, nitahakikisha nakufukia ndani ya kibanda changu” alisema yule mzee na hapo nilijihisi natetemeka kidogo…..…..ITAENDELEA MUWE NA USIKU MWEMA