KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA SABA: Hapo Jessenia akapakuwa chakula, akala kabisa na kisha akajiunga na kaka yake binamu kwa kuanza kunywa wine yake, sambamba na binamu yake ambae kila dakika alikuwa anazidi kulewa, wakati huo Jessenia hakujuwa kuwa nia ya Ussi ni kula kitumbua chake, yeye alijiachia zake wakinywa pombe pamoja, huku wakiongea na kutaniana kama ilivyo mazoea ya tabia mpya waliyo kuwa wameianzisha, na leo walikuwa wawili tu ndani jumba lile kubwa la kifahari…… ENDELEA……..
Masaa manne baadae ndipo Jessenia alipogundua nini kilikusudiwa na Ussi, ni baada ya kujisogeza karibu yake na kuanza kumshika shika sehemu nyeti, lakini Jessenia ambae alitamani kuwa itokee hata kwa bahati mbaya, apewe dudu na binamu yake, akakumbuka maneno ya babu Mangeu kwamba, “ole wako utembee na Ussi, kitakutokea kitu ambacho utakijutia Maisha yako yote” hapo ndipo akili ilimkaa sawa Jessenia, ambae alijiuliza swali gumu, “sasa huyu alijuwaje kama leo Ussi anataka kunifanya hivi?” akajipa jibu hapo hapo, “mchawi yule mshenzi” aliwaza huku anainuka na chupa yake mkononi, akaeleka chumbani akimuacha Ussi anadhania kuwa Jessenia anaenda halafu anarudi, lakini haikuwa hivyo Jessenia alipoingia chumbani kwake akajifungia mlango kwa ndani na kuendelea kunywa pombe yake taratibu huku anawaza juu ya babu Mangeu, alitamani hata akamchome moto kwenye kile kibanda chake afie ndani moja kwa moja, pengine itakuwa mwisho wa kuandamwa na majini na yeye kupata mwanaume atakae muhitaji.
Baada ya kupita nusu saa, Jessenia akiwa anaendelea kunywa wine yake, ndipo akasikia mlango unagongwa kwafujo, “kwanini umejifungia wewe, hebu fungua bwana nije tumalize mchezo” alipiga kelele Ussi, huku anagonga mlango kwa fujo, “hivi babu Mangeu alijuwaje kama nia ya Ussi ni kufanya mapenzi na mimi” aliwaza Jessenia huku akizidi kuamini kuwa Babu Mangeu ndie anaempa shida katika Maisha yake, japo hakujuwa sababu ni nini.
Siku ya pili Jessenia alitoka pale nyumbani mapema akielekea mjini, akimuacha Ussi bado amelala, kule mjini Jessenia akiwa hana kitu cha kufanya aliamua kuingia kwenye mtaa wa maduka ya urembo ili akanunue baadhi ya vitu, maana vitu hivyo ndiyo moja ya burudani yake.
Sasa basi Jessenia akiwa kwenye duka mmoja wapo ndipo alipokutana na Kijana chotara wa kiarabu, ambae licha ya kumfahamu kwa muda mrefu lakini hakuwa na mazoea nae, kwa sababu sio makaaji wa pale dukani, ila cha kushangaza siku ile kijana yule aliejitambulisha kwa jina la Abdulqadir, alijichangamsha sana mbele ya Jessenia, huku akimlipia kila alichohitaji, ukweli baada ya pale walipeana namba za simu na kuanza kutongozana, huku kijana yule akihitaji kumuoa kabisa, lakini ukweli safari hii Jessenia alikuwa mgumu kidogo kukubali, maana alihofia kutokea yaliyo tokea.
Siku ile jioni mzee Juma Mohamed na mke wake walirudi toka wete wakitanguliwa na dada wa kazi alierudi mchana, hawakuuliza chochote kilicho tokea ila siku tatu mbele shangazi alimchukuwa Jessenia na kumpeleka Ngezi kwa mganga, ambako mganga alisema kuwa Jessenia asingeweza kuolewa na mwanaume yoyote, maana kila mwanaume ambae angemgusa angekufa kifo kibaya sana kutokana na jini ambalo lilikuwa linamuandama mschana huyu, ispokuwa mwanaume mmoja tu, ambae ni binamu yake, yaani Ussi, ambae kutokana na kuwa na undugu wa mbali jini lile lisingi weza kumdhuru, hapo ndipo Jessenia alipogundua kwanini babu Mangeu alimkataza kutembea na Ussi.
Naam zilipita siku mbili Jessenia akitarajia lolote kutoka kwa Ussi, ambae kiukweli licha ya kuwa tayari kufanya nae mapenzi na ikiwezekana awe mume wake, lakini hakupendezwa na tabia zake za kushinda bar akibadili wanawake kila kukicha, siku hiyo jioni akiwa anakaribia nyumbani kwao anatoka mjini kutazama mazoezi ya mpira wa kikapu, akashangaa kumuona mjomba wake akiwa amesimama na babu Mangeu, hakushangaa kuwaona wakiwa wamesimama, ila usimamaji wao ndio uliomshtua, ni kwamba babu Mangeu alikuwa anaongea muda wote akionekana kufoka na kuongea kwa ukali, huku mjomba wake akiwa ameinamisha kichwa chini, kiunyonge kweli kweli, mikono ameiweka nyuma, alionyesha uoga na nidhamu ya hali ya juu, ilimshangaza sana Jessenia, ambae alitamani kusikia japo neno moja tu kati ya mengi aliyokuwa anayaongea Mangeu, lakini walipomuona tu, waliagana na kila mmoja akaondoka zake, ukweli Jessenia aliingiwa na hofu kubwa sana, akiona kuwa hata mjomba wake alikuwa anamuogopa huyu Mangeu.
Siku zilienda, Jessenia hakuona dalili ya Ussi kuomba kitumbua kwake, wala kuonyesha dalili ya ile michezo yake ya ajabu, huku shangazi na mjomba wake wakijitahidi kuwaweka mbali, kwa upande fulani Jessenia alishukuru, maana Ussi hakuwa kijana mzuri kutokana na tabia zake za ulevi na uzinzi, ambazo wazee wa pale mtaani hawakuwa wanazifahamu, ila pia Jessenia alitamani kuona kama kweli kuna mtu anaweza kufanya nae mapenzi bila kudhurika, na mtu mwenyewe ni binamu yake Ussi.
Ilipita miaka miwili Abdulqadir alikuwa anamtongoza kwa siri, Jessenia alitongozwa na watu wengi sana, ambao aliwakataa, sio kwa kuhofia usalama wao pia wengi wao hakuwa tayari kuingia nao katika mapenzi, huku yeye akitamani kupewa dudu, ndipo alipo katashauri la kumkubalia Abdulqadir, lakini kabla ya kumkubalia kwanza aliamua kutafuta mganga wa kuondoa majini, safari hii alifanya kwa siri.
Alifanikiwa kwenda kwa waganga watano, hakuna hata mmoja alieliona jini ndani yake, wote walimuambia kuwa hakuna tatizo lolote na alikuwa huru kuolewa na mtu yoyote, majibu hayo yalimfanya Jessenia aamini kuwa baada ya kuhangaika kwa muda mrefu sasa majini yameondoka, ndipo alipoamua kumkubalia Abdulqadir na kwenda kutesti nae mitambo pale madungu Guest house.
Siku ile ilikuwa hivi, baada ya Abdulqadir kumtuma mhudumu wa pale guest House kwenda kununua chakula, na wao kuingia ndani ya Guest na yeye Jessenia akimini kuwa siku ya yeye kunyanduliwa imeshafikia, alipoingia chumbani na Jessenia alingia bafuni kwa lengo la kwenda kuvua nguo na kuvaa kanga kwaajili ya kujiachia mule ndani, lakini ile anatoka bafuni, akashangaa kumuta Abdulqadir akiwa amelala chini, amekuwa mweusi kama mkaa, japo kuwa kijana yule alikuwa ni chotara wa kiarabu kama yeye, hapo Jessenia ambae licha ya kushtuka sana, lakini hakushangaa kilichotokea, akaamua kuvaa haraka akajifunika niqab yake na kutoka haraka kabla yule mhudumu hajarudi kule waliko mtuma.
Na japo alikutana nae njiani lakini hakumtambua, na yeye kuondoka zake, japo habari zilipoanza kusambaa zilimtaja kuwa Abdulqadiri aliuliwa na jini la kike ambalo katika maelezo ya watu na polisi, ambae alikuwa anasimamia upelelezi yani insp Aroub, yalishabihisha mwili wake kama ulivyo kasoro sura ambayo hakuna alieiona, safari hii Jessenia hakusimulia nyumbani kwao, japo walisha fahamu kwa sababu ilisha zoeleka kuwa kifo kama kile siku zote husababishwa na jini la Jessenia, ambae mwenyewe alimua kwenda tena kwa shekhe ambae anatibu kwa kitabu, kuangalia tatizo ni nini kama waganga watano walisema hakuwa na jini lolote.
Naam baada ya kusomwa sana wa kitab na kuwasha udi na ubani, majibu yalipatika kuwa ni kwamba, “tatizo lipo binti yangu, kuna mtu anakufanyia kijicho usiolewe, lakini sioni kinacho fanyika, tena yupo karibu kabisa na hapo unapoishi, sio ndugu yako wala si mtu wa karibu na familia, alisema yule mganga, ambae alisema dawa ni kwamba, afanye siri kubwa wakati anaingia kwenye mahusiano, maana mtu huyo hatakiwi kujuwa wala kuyaona mahusiano yako, vinginevyo njia salama ni wewe kuhama pemba hii na kuhamia mbali ambako utaweza kutengana nae, huko unaweza kuolewa na ukapata familia nzuri kabisa, kuhusu Maisha yako sina shaka, unaonekana ni mwenye bahati, nyota yako ina nguvu” niwazi sifa na tabia zilizotajwa zilikuwa ni za babu Mangeu, sasa kilichobakia ni kufanya kila anachokifanya ili kumkwepa mzee huyu asigundue kila anacho kifanya, cha kwanza kukifikiria ni kupata mwanaume ambae sio mkazi wa hapa Pemba, ikiwezekana aondoke nae kuelekea huko bara, ambako kiukweli hakuwahi kufika hata siku moja, akimini kuwa ndio sehemu salama kwake, ambako Mangeu hatoweza kufika, lakini licha kuwaza hivyo sio kwamba angemkubalia mwanaume yoyote, ila angechagua mwanaume anaempenda toka moyoni mwake.
Siku ya pili toka siku ile Jessenia atoke kwa shekhe, kama kawaida yake alitoka nyumbani kwao mida ya saa kumi na nusu kuelekea tenes kwenye mazoezi ya mpira wa kikapu, ambako alikutana na kijana Vuai, ambae ni mmoja wa marafiki wa kaka yake Ussi, ambae alimsogelea na kumueleza ya moyoni, lakini njia ambayo Vuai ambae pia hakuwa ameoa alitumia, ni njia ya kulazimisha penzi, kwa sababu ni kwamba siku za nyuma alishawahi kumtongoza na akamkatalia, “yaani nimekueleza haja yangu muda mrefu ukamuona Kadir ndie mwanaume unadhani hakuniambia kama ulimkubali” kauli ile ilimshtua sana Jessenia ambae kiukweli alijuwa kuwa Vuai anaelewa kila kitu kilichotokea Madungu Guest House, na kwamba yeye anahusika, “unaongea nini Vuai, mbona sikuelewi” alisema Jessenia, akijitahidi kukwepa shutuma, naelewa kila kitu, na safari hii ukinikatalia namueleza kila mtu” alisema Vuai na hapo Jessenia akaanza kutetemeka.
Hebu nikuweke sawa hapo, unajuwa Jessenia alidhania kuwa Vuai anazungumzia kifo cha Abdulqadir, lakini haikuwa hivyo, japo Jessenia alikuja kufahamu hilo baadae sana na alikuwa ameshachelewa, Vuai alicho maanisha ni kwamba atawaeleza watu kuhusu yeye kumkubalia qadir, akiamini kuwa itampunguzia thamani yake, kwa kuonekana kicheche, basi “sawa nitakupa jibu lako” alisema Jessenia, ambae kimoyo moyo, alikuwa anashangaa kwamba Vuai licha yakujuwa kilichotoke kuwa ni kitu cha hatari, lakini kwanini na yeye anataka, “hapo ndipo tunapokosana mimi na wewe, utanijibu lini wakati unaweza kujibu sasa hivi?” aliuliza Vuai, kwa sauti ya chini lakini ya kulazimisha, mpaka hapo licha ya kwamba Jessenia alikuwa na hamu ya kunyanduliwa, lakini alishamchukia huyu Rafiki wa binamu yake Ussi wa utotoni, ambae sasa alikuwa anajihusisha na biashra ya urembo na manukato, “sawa nimekubali, lakini je utanioa?” aliuliza Jessenia, kwa sauti ya chini yenye kujawa na aibu, ambae ni kama alikuwa anakiona kifo cha mtu mwingine kikija siku za usoni, “tutaongea siku ukija nyumbani kwangu” alisema Vuai, kwa sauti ile ile ya chini yenye kulazimisha,“nyumbani kwako masikini hajengi itawezekana vipi, au unataka ukanifanye?” aliuliza Jessenia kwa sauti ile ile iliyojaa aibu safari ikiwa na kijimshangao fulani, “kwani vibaya au haupo tayari nitangaze kila kitu?” aliuliza Vuai, ambae toka amekutana na Jessenia, alikuwa amekunja sura, “lakini si unajuwa mwenzio bado sijawahi kufanya hivyo..” alisema Jessenia, ambae kiukweli hakuwa tayari kutoa kitumbua chake kwa Vuai, sio kwamba alikuwa ni kijana wa hovyo, ila ni ile kuonekana anamlazimisha ndio hakupenda kabisa jambo hilo, “kwani wewe hujui bwana, usijifanye mtoto kwani wengine wanafanyaje na bado wanaolewa na bikira zao, kama hutaki we niambie tu!” alisema vuai, kauli ile ilimsisimua Jessenia, na kuhisi kama kuna kitu kina mchoma kwenye makalio yake na kumuumiza, akajikuta anabana makalio, maana alielewa fika kuwa Vuai anamaanisha atamwungilia kinyume na maumbile, “jamani kaka Vuai, mwenzio sijawahi kufanya huo mchezo, kwanza ni laana kwa muumba wetu” alisema Jessenia kwa sauti ya kulalamika, “kwani shida ipo wapi, we usihofu, kwani wengine walianzaje” alisema Vuai ambae alionyesha wazi kuwa alipania kuingiza dudu kwenye makalio haya makubwa ya Jessenia….. ENDELEA NAYO….
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA NANE: akajikuta anabana makalio, maana alielewa fika kuwa Vuai anamaanisha atamwungilia kinyume na maumbile, “jamani kaka Vuai, mwenzio sijawahi kufanya huo mchezo, kwanza ni laana kwa muumba wetu” alisema Jessenia kwa sauti ya kulalamika, “kwani shida ipo wapi, we usihofu, kwani wengine walianzaje” alisema Vuai ambae alionyesha wazi kuwa alipania kuingiza dudu kwenye makalio haya makubwa ya Jessenia…. ENDELEA NAYO...
Kitu ambacho Jessenia hakuhitaji kimtokee, sasa alitamani lile jini lifanye kazi yake, “kwahiyo jiandae ijumaa mchana nitakuja kukufuata mjini” alisisitiza Vuai, na wakati huo huo Ussi akaingia pale uwanjani, alikuwa na pikipiki yake aina ya Vesper na kujiunga nao, huku wao wakijishtukia kwa maongezi ambayo walikuwa wametoka kuyafanya.
Jessenia hakutumia muda mrefu mahali pale, aliondoka zake huku akiona umuhimu wa kuondoka kabisa pemba na kwenda kuishi mbali, na sababu ya yeye kuondoka Pemba ni kupata mwanaume toka nje ya kisiwa hiki, akiwa anatembea mschana huyu alikuwa anaomba kimoyo moyo akutane na mwanaume wa aina hiyo, ambae yeye Jessenia ataanza kumpenda.
Jessenia ambae hakuwa tayari kuingiliwa kinyume na maumbile tena na mwaume ambae ametokea kumchukia, akiwa anakaribia mitaa ya markiti akamuona kijana mmoja mrefu kiasi mwenye mwili wa mazoezi aliekuwa mbele yake akija kwa mwendo wa taratibu, akionekana mgeni kabisa mazingira haya, kutokana na kutazama tazama kushoto na kulia na pia uvaaji wake ulikuwa tofauti kabisa, na alikuwa mgeni machoni pake, Jessenia akajikuta anaachia tabasamu pana, maana alikuwa na uhakika kutokana na uzuri wake inaweza kuwa rahisi kwake kutengeneza urafiki na kijana huyu mgeni, ambae yeye alihisi kuwa anaweza kuwa ni askari wa jeshi la ulinzi, ambalo ndio lina idadi kubwa ya watu toka bara waliopo hapa kisiwani.
Lakini kabla hawajakutana, Jessenia alishangaa kuona kijana yule akisimama ghafla na kumtazama kwa mshangao, kama vile ameona mtu asie wa kawaida machoni pake, hivyo na yeye akaongeza mwendo ili kuwahi kukutana na yule kijana amuulize anashida gani, lakini ile anaongeza mwendo, akashangaa kumuona kijana yule akigeuka alikotoka na kuanza kutembea kwa haraka kama vile kuna mtu anamkimbia, na yeye akaongeza mwendo kumuwahi, lakini kijana yule hakufika mbali akaacha barabara ya kutokea chake hotel na kuingia kwenye njia moja ya kwenda kutokea usawa wa kituo cha mafuta, na yeye alipofika kwenye ile njia na kutazama upande ule, akamuona kijana yule akiwa amesha fika mbali kidogo, lakini aligeuka na kumtazama macho yao yalipokutana akajaribu kutabasamu, pengine kijana yule angeamua kusimama na kumsubiri, lakini haikuwa hivyo, ndio kwanza kijana yule akageuka na kuzidi kutembea mbele.
akiwa hajui cha kumueleza kijana yule endapo angekutana nae, alifuata njia moja ya mkato ambayo lazima ingekutana na ile anayopita yule kijana, na ikawa hivyo yeye aliwahi kutokea kwenye barabara kuu kabla yule kijana hajatokea, lakini haikusaidia kitu, kwasababu kijana yule alipita mahali pale bila kusema au kufanya chochote, ila yeye pia akaona itakuwa vyema kama atamtazama yule kijana kuona anakoelekea, ambako alihisi kuwa itakuwani maeneo ya karibu,kwa sababu kwa muda ule asinge weza kupata usafari wa kwenda mbali.
Lakini haikuwa hivyo, maana muda huo huo, likatokea gari la jeshi na kumchukua kijana huyo kisha gari likaondoka huku yule kijana akimtazama kwa macho ya mshangao, huku dakika tano baadae Jessenia akimuona Ussi anatokea upande lilikoelekea gari akiwa na pikipiki yake, hapo yeye akaondoka zake kuelekea msingini, kichwa kikimzunguka kwa mawazo ya ijumaa siku ambayo angeingiliwa na Vuai.
Siku ya ijumaa ilifika kwa haraka sana, siku ambayo hakupenda ifike, lakini hakuwa na ujanja, hivyo akajiandaa na kuelekea sehemu ya makutano, wakati huo Ussi alikuwa ameshatoka nyumbani kwamba anaelekea msikitini, ndio siku ambayo alikutana tena na yule kijana mgeni, wakati anaelekea sehemu ya ahadi kukutana na Vuai, lakini hakupata nafasi ya kuongea nae, maana yule kijana alishtuka sana, hata baadae alipomuona akiwa na Ussi pale kwenye kituo cha mafuta, alimuona bado mwenye wasi wasi, kitu ambacho kilimfanya Jessenia aanze kuhisi pengine kijana yule anafahamu kilichotokea kwa Abdulqadir, maana kijana yule alionyesha kumuogopa sana.
Walifika nyumbani kwa Vuai, yaani masikini hajengi, ambako walimkuta kijana mmoja anacheza game kwenye computer, nae alikuwa ni Mahamud ambae aliombwa apishe kidogo, ili mambo mengine yaendelee, ndipo kijana yule yaani Mahamud alipotoka nje ya nyumba ile na wao kuelekea chumbani, ambako Vuai alivua suruali yake na kubakia na bukta na Tishert, wakati huo Jessenia amekaa kitandani ameshaondoa niqab yake usoni, huku anatetemeka kwa hofu ya kuingiliwa kinyume na maumbile yanavyo takiwa, kwa mara ya kwanza Jessenia aliomba jini la babu Mangeu lifanye kazi yake, “mbona huvui sasa, ujuwe hatuna muda wakupoteza, usihofu nitaingiza taratibu” alisema Vuai, ambae alikuwa na hamu ya kufanya kile alichokikusudia kumfanyia Jessenia, huku anamsogelea na kuikamata hijab yake na kutaka kuitoa.
Lakini ukweli ni kwamba, Vuai hakufanikiwa, maana muda huo huo ikasikika hodi mlangoni toka sebuleni, hivyo Vuai akaacha kumvua nguo Jessenia na kutoka mule chumbani akaelekea sebuleni, ambako kulisikia mlango ukifunguiwa na kufatiwa na mshtuko sambamba na mtu kuanganguka, ndipo Jessenia alipovaa vizuri pamoja na kujifunika niqab yake kisha akatoka na kwenda kutazama kilichotokea huko sebuleni, ambako alimkuta Vuai akiwa amelala chini, Uso wake ukianza kubadilika rangi na kuwa mweusi, na yeye kuona hivyo akatoka haraka na kuanza kuondoka zake, huku akikutana na kundi la watu waliokuwa wanashangaa kitu fulani ambacho yeye binafsi hakukijuwa.
Siku mbili mbele akakutana na yule kijana muoga pale uwanja wa Tenes, akiwa anacheza mpira wa kikapu, uchezaje wake ulimvutia na ndio siku aliposikia kuwa kijana yule siyo mwanajeshi ila ni mwalimu ambae alikuja kwa muda pale Pemba na baadae ataondoka kurudi dar es salaam, Jessenia alitamani kufahamiana nae, lakini hakujuwa aanze vipi, lakini siku chache baadae akapata nafasi hiyo, ni siku ya mechi ya mpira wa kikapu ambapo Jessenia alimkuta kijana yule akiwa na Aisha, mwanzo aliingiwa na huzuni wa kukata tamaa akidhania kuwa kijana yule ni mpenzi wa Aisha ambae alisoma nae hapo zamani, lakini alipiga moyo konde na kwenda kuwasalimia, japo alipishana nae maana kijana huyu aliitwa kwaajili ya kuingia mchezoni, lakini aliweza kuongea na Aisha akimuuliza juu ya mahusiano yao, na pia kazi ya kijana yule, ambapo aisha alimueleza kuwa ni mwalimu mwenzie ambae alikuja pale kwa muda, na kwamba hakuwa na mahusiano nae, pia Aisha alimsimulia kisa cha kijana yule aliemfahamu kwa jina la Eric, japo yeye alimfahamu kwa jina Prosper, kuwa alipomuona kwa mara ya kwanza alidhania ni jini kutokana na uzuri wake.
Swala lile lilimfurahisha sana Jessenia, ni pale alipoambiwa kuwa alidhaniwa jini kutokana na uzuri wake, Jessenia hakuishia hapo, aliuliza kuhusu Maisha binafsi ya kijana huyu na sehemu anayoishi, ndipo walipo panga wao kwa pamoja kukutana kwenye taarab, ambayo hata Eric pia alisema angeenda, siku ambayo Jessenia alijikuta akifurahi sana kuliko siku zote, siku ambayo alikunywa wine na kijana huyu mwenye kuonyesha kumjali na kumpa sifa yake, japo baadae binamu yake alionyesha kuchukizwa na kitendo kile, hata kumsema sana siku ya pili, siku ambayo Jessenia alienda kwa shekhe wake na kumuuliza cha kufanya juu ya kijana yule mgeni, “unaweza kufanya nae urafiki, lazima uwe wa siri sana adui yako asijuwe, japo ninaona giza mbele yenu, maana kuna misuko suko mutaipitia, ila unapaswa kumueleza ukweli mapema” alisema Shekhe.
Wakati wa kurudi nyumbani, Jessenia alikutana na Eric, kijana ambae kiukweli alishaanza kumpenda toka moyoni, japo hakutaka kijana huyu aingie matatizoni, ila hakuwa na jinsi zaidi ya kujaribu bahati yake, “Eric wewe ndie mwanaume wangu wa pekee ambae jini limeshindwa kukufikia, hakika sitaki nikupoteze, nataka unichukue jumla uniondoe huku pemba” alisema Jessenia, ambae alitumia masaa mawili kunisimulia hadithi yake hiyo yakutisha na kuhuzunisha, huku akimaliza kwa kilio chapesi, “uliwahi kumueleza mjomba wako juu ya mtu ambae una muhisi anafanya hayo, yani mzee Mangeu?” nilimuuliza Jessenia ambae alikataa kwa kichwa, “sikutaka hata yeye mwenyewe ajuwe kwamba nimesha mgundua, si unajuwa wachawi huwa wanatuma majini kusikiliza kila kinachosemwa juu yao” alisema Jessenia, kwa sauti yake ambayo iliambatana na kilio cha kwikwi, nilitulia kidogo na kutazama muda kwenye saa ya simu yangu, nikaona kuwa muda ulikuwa ni saa sita kasoro, “pole sana Jesse, naamini karibu tunapata ufumbuzi na shida zitaisha” nilsema kwa sauti ya upole, “Eric unakumbuka ulisema huto niacha?” aliuliza Jessenia, huku anaishika mikono yangu miwili na kunitazama usoni kwa macho yenye kubembeleza na kutia huruma, kitu ambacho kilizidi kumfanya azidi kuonekana mzuri, nikamvutia kifuani kwangu na kumkumbatia, na yeye akanikumbatia kwa mikono yake, “Jesse mpenzi wangu, siku chache mbele utafahamu kuwa nimekuja pemba kwaajiili yako, sito kuacha peke yako mpenzi wangu” nilimueleza Jessenia, ambae baada ya kusikia hivyo, nikamsikia akicheka kwa raha, huku akivuta mafua ya liyosababishwa na kilio cha kwikwi, “Eric nitakupenda Maisha yangu yote” alisema Jessenia huku akishindwa kuzuia furaha yake iliyo ambatana na kicheko na kilio cha chini chini, “ok! sasa naona muda umeenda sana, we nenda nyumbani ukapumzike, kesho tutajuwa tuanzie wapi” nilimueleza Jessenia, ambae sikumueleza jinsi ninavyo sakamwa na babu Mangeu, na yale maneno aliyoniambia siku ile, kwamba nikae mbali na Jessenia kama ninataka kurudi nyumbani salama, pia sikumueleza ukweli juu ya watu walioonekana kule Green messi wakiranda randa nje ya nyumba wakati sisi tuna nyanduana, japo leo katika maelezo ya Jessenia, niliweza kubaini kuwa Ussi alikuwa na wivu mkubwa sana kwa huyu binamu yake, “Eric usije kubadili maamuzi yako, nakuomba mpenzi wangu, ningeweza ningeongozana na wewe tukalale pamoja nyumbani kwako” alisema Jessenia kabla hajaingia ndani mwao, na mimi kuelekea kule kwenye kituo cha mafuta ambako niliacha gari, huku njiani nikiwaza juu ya simulizi ya Jessenia, huku nawaza nitaanzia wapi kukabiliana nalo, sio tu kuwa ni jukumu ambalo limenileta, ila pia nikumsaidia mpenzi wangu, ambae kiukweli nilitokea kumpenda sana Jessenia kuliko wanawake wote ambao niliwahi kupita nao, na kilicho nichanganya ni kwamba, ni kitu gani huwa kinafanyika ili kuwa uwa watu wanao ingia katika mahusiano na Jessenia, je Ussi na vijana wake walikuja kufanya nini pale Green Mess.
Nilimkuta yule jamaa wa pale sheri, ambae nilimpatia shilingi elfu mbili kwa kunilindia gari, nae akapokea na mimi nikaingia kwenye gari na kuondoka zangu, huku njiani nikiendelea kuwaza namna ya kukabiliana na swala hili, njiani sikukutana na Mangeu, hata nilipo pita Wawi mess nilikuta music bado unaendelea huku baadhi ya watu wakianza kundoka, na pele nje ya ukumbi niliiona ile pikipiki ya wale jamaa wawili ambao nawafahamu kuwa ni vijana wavuvi wa Ussi, ambao mchana niliwaona wakivizia pale Green house, sikuhangaika nao nikakanyaga mafuta kuelekea vitongoji liliko kambi la Alli Khamis.
Lakini basi baada ya kupita wawi mess na kutembea kama mita mia mbili hivi, nikaona kitu kama mwanga wa piki piki nyuma yangu, mwanzo sikushtuka lakini baada ya kutembea tena mita kama mia hivi, nikashtuka kuona ile pikipiki ikiwa imenikaribia hapo nikachungulia kwenye sinde mirror, nikaoina piki piki ikija kwa kasi nyuma yangu, ni pikipi kubwa ambayo ni ile ile inayo tumiwa na vijana wa Ussi, hapo nikakanyaga mafuta kuongeza mwendo, huku nikithibitisha wivu wa Ussi, maana nilijuwa fika ujio wa vijana wale wa Ussi ulikuwa ni wakuja kunishambulia, sio kwamba nilikuwa na waogopa, ila nilikuwa nina wasogeza kwenye eneo ambalo tunaweza kujuwana tabia.
Juhudi zangu za kuwakimbia vijana wale zilikwama maeneo ya kona ya kambi ya mwanzo ya Jeshi la kikosi cha ngerengere, ambacho mita kama mia mbili mbele yake kuna pori fulani dogo, ambalo nilikusdia kulitumia kuwadhibiti wale jamaa pasipo ushaidi wowote, ambapo ile napunguza mwendo kuingia kwenye ile kona, na wao wakapita na mia, na mimi nilipoimaliza ile kona nikakanyaga mafuta kwa nguvu kuwafuata, lengo langu lilikuwa ni kuwanyima nafasi ya kufanya lolote katika kunitegea umbushi, japo haikusaidia maana walipotea kabisa mbele yangu, mpango wangu ulienda kama nilivyo ufikiria, kwa sababu na wao walikuwa wanafikiria ninacho kifikiria mimi.
Maana ile natokea kwenye ile kona nikakutana na mwanga mkali wa pikipiki ambayo ilikuwa imesimamishwa kati kati ya barabara kwa kuikatiza, huku taa imeelekezewa ninakotokea, nilichofanya ni kupunguza mwendo kwa haraka, na kusimama mita kama thelathini toka iliposimama pikipiki, na mimi sikuzima taa, maana iliniwezesha kuwaona wale jamaa wakiwa wamesimama pembeni ya barabara, huku mmoja wao yule ambae alikuja dirishani kule Green messi, akiwa ameshika kile kijimfuko cha prastic, yani Rambo, nikawatazama vizuri na kuwapimia kwa macho kuona kama wana uwezo wa kumudu japo kwa dakika moja kupokea ngumi zangu, kabla sijawakalisha, nikawaona kuwa ni watu walioshupaa kweli kweli, nadhani ni kwaajili ya kazi ngumu za kila siku wanazo zifanya, na sasa niliwaona wanakuja kwa mwendo wa haraka kunifuata mimi …….. ENDELEA NAYO
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA TISA: huku taa imeelekezewa ninakotokea, nilichofanya ni kupunguza mwendo kwa haraka, na kusimama mita kama thelathini toka iliposimama pikipiki, na mimi sikuzima taa, maana iliniwezesha kuwaona wale jamaa wakiwa wamesimama pembeni ya barabara, huku mmoja wao yule ambae alikuja dirishani kule Green messi, akiwa ameshika kile kijimfuko cha prastic, yani Rambo, nikawatazama vizuri na kuwapimia kwa macho kuona kama wana uwezo wa kumudu japo kwa dakika moja kupokea ngumi zangu, kabla sijawakalisha, nikawaona kuwa ni watu walioshupaa kweli kweli, nadhani ni kwaajili ya kazi ngumu za kila siku wanazo zifanya, na sasa niliwaona wanakuja kwa mwendo wa haraka kunifuata mimi …….. ENDELEA…..
Huku yule mmoja akiingiza mkono kwenye ule mfuko na kutoa kijichupa fulani chenye rangi kama ya zambarau, akatia kitu ambacho sikukiona vizuri kwa udogo wake, na kukifungua kile kichupa kisha akatumbukiza kile alichokishika, ambacho bado sikukitambua, na baada ya hapo nikamuona akitoa kitu kama kijibomba fulani kidogo, mfano wa filimbi ya mchawi wa bahari, (chanzo ni hadithi za kale), na kukiweka kile kidude ndani yake, ambacho sasa niliweza kukiona vyema kuwa ni kitu mfano wa sindano au mwiba mdogo sana.
Hapo nikajuwa lazima kuna kitu ambacho kinataka kufuatia juu yangu, na sio kitu kizuri, hivyo nikafungua mlango kwa haraka na kushuka huku ndani ya gari nikiiacha simu yangu inaanza kuita, mpigaji akiwa ni Jessenia “jamani kwani nime wakosea nini” niliwauliza kwa sauti ya uoga, huku nikiwasogelea kwa tahadhari kubwa, “wewe si unajifanya kidume, ngoja uipate dawa yako” alisema mmoja yule muendesha pikipiki kwa sauti yake yenye lafudhi ya kisukuma, kisha akamtazama mwenzie, “na wewe fanya haraka tuondoke” alisema kwa sauti kavu kisha akatazama kushoto na kulia, huku mwenzie akiinua ile filimbi na kuilekezea kwangu huku ana iweka mdomoni mwake, sikuwapa nafasi, fumba na kufumbua niliruka chini na kubiringita kama tairi lililochomoka kwenye gari lililokuwa linashuka kitonga au msela nyoka na kwenda kuinukia mbele ya yule mwenye kijifilimbi, ambae nilimpiga ngumi ya koo na kufanya baada ya kupuliza hewa kama alivyo kusudia sasa akavuta ndani na kumeza kile kimwiba kilichokuwa ndani ya filimbi, nikamuona anatoa macho ya mshtuko na kuachia kila alichokishika na kuwahi kujidaka shingo, kama vile anajaribu kuzuia, lakini mwishoe akatulia hivyo hivyo, hapo siku taka kuangalia kilicho kuwa ninamtokea yule jamaa, ni karusha ngumi mkato (cross, ambayo hutumika sana kwenye boxing) kwenda kwa yule wa pembeni, ambae kutokana na kuwa katika mshangao wa kutotegemea alichokiona, alikubari kuipokea ngumi ile kwa shavu lake la kushoto, na kuyumba kidogo kwenda kulia huku akitoa mguno wa maumivu, hapo hapo kabla hajakaa sawa nikampeleka ngumi tano mfululizo, zilizotuwa sawa kabisa eneo la uso wake, nikimmalizia teke mzunguko lilotua usoni kwake upande wa sikio la kushoto na kumrusha juu kisha likamtupa chini kama mzigo, mwalimu wangu, Tak Fujj wa Okinawa kule Japan, alinisisitiza sana kutumia mapigo machache yenye nguvu, ili kumshinda adui, kabla sijaishiwa nguvu.
Haraka sana nikamgeukia yule wa kwanza, huwezi amini, nilimkuta amesimama vile vile huku macho yame mtoka kama vile amekabwa na kitu kingumu kooni, halafu kilichonitisha ni muonekano wake, uso wake ulianza kuwa mweusi sana, hapo hapo akajibwaga chini puh! kama furushi, lakini mikono yake bado ilikuwa shingoni, japo ulikuwa ni usiku na pale ni kichakani, lakini sikutaka mtu yoyote anikute, hivyo nilichukuwa kile kichupa na kumtazama yule ambae nilimpiga wash kiki, nikamuona amelala pale chini anageuza geuza macho kama vile anataka kukata roho, nikaachana nae kuingia ndani ya gari, ambalo bado lilikuwa linauguruma, na kuondoka zangu nikipenya pembeni kabisa ya pikipiki ile ambayo ilikuwa imesimamishwa barabarani na kutokomea zangu kueleka Ali Khamis Camp, huku simu ya Jessenia ikiendelea kuita, sasa sikuona sababu ya kuacha kuipokea, “hallow mke wangu hujalala bado?” niliita kwa pose flani lililosababisha sauti kusikika kwa uzito wake, huku nakanyaga mafuta kutokomea upande wa vitongoji, “Eric, ukiendelea na masihara ya hivi utanisababishia pressure muda si mrefu, hivi kwanini huelewi we mwanaume, mwenzio wewe ndie pekee nilie nae” alisema Jessenia kwa sauti ambayo ilionekana wazi kuwa bado ilikuwa katika wasi wasi kwa kiasi fulani, “ondoa shaka Jesse, ndio nakaribia kufika sasa” nilimueleza Jessenia, na hapo nikamsikia akivuta zile pumzi za kujipooza, “sawa fika halafu unipigie, sawa Eric” alisema Jessenia kwa sauti ya kubembeleza na kusisitiza, “sawa mpenzi wangu nikiingia kitandani nitakupigia” ndivyo nilivyo mjibu, kisha nikakata simu,
Naam niliendesha gari huku nikijiuliza maswali kadhaa kichwani mwangu, moja kati ya swali lililoniumiza kichwa ni kwanini vijana wa Ussi, wanivamie, ina maana mzee Mangeu anawatumia vijana wa Ussi kuwadhuru wanaume wanao taka kuingia kwenye mahusiano na Jessenia, au Ussi anashirikiana na babu Mangeu kufanya hivyo, na ni kwanini wafanye hivyo, kuna sababu yoyote ya wao kufanya hivyo, na vipi kuhusu kile kichupa kinahusiana na vifo vya watu wanao msogelea Jessenia kimapenzi na kwamba sio jini, “hapa inabidi nifanye mpango mzee Mangeu akamatwe akahojiwe” niliwaza hivyo, nikiwa nimeungana na Jessenia kumshuku Mangeu juu ya mauwaji yanayoendelea, ukichukulia mtindo wake maisha ikiwa na tabia yake ya kutoweka kwa muda mrefu na kuibuka ghafla.
Naam mawazo hayo yalibadilika, nilipokuwa nakaribia kuingia Green House, niliacha kuwaza na kurudisha akili yangu kwenye kile nilichotoka kukifanya mchana, ukweli sikutaka Jessenia aingie kwenye hatia, kwasababu nilisha mpenda kweli kweli, na nilijikuta namwonea huruma kutokana na historia yake, kingine kilicho nivuta na kunilegeza kwa Jessenia, ni kile kitendo cha yeye kunipa nafasi ya kuwa wanza kupita kwenye njia yake, ya kitumbua, “dah! ila ameumbika” nilijisemea kimoyo moyo, huku na simamisha gari na kulizima, kisha nika chukuwa kile kichupa cha wale vijana wa Ussi, kisha nikashuka na kufunga gari na wakati huo ndio nilioshtuka kuwa kulikuwa na pikipiki aina Vesper ikiwa imeegeshwa ubavuni mwa nyumba ile ambayo nilikuwa nakaa peke yangu, ilikuwa ni Vesper mpya kwa kiasi flani, kama sio imenunuliwa karibuni, basi mmiliki alikuwa ni mtunzaji mzuri, ni Vesper ambayo masaa kadhaa yaliyopita niliikuta karibu na njia ya kuingilia Wawi mess, na wakati huo huo nikasikia nyayo nyepesi nyuma yangu, nikajuwa tayari mapambano yameanza upya.
Sikutaka kushangaa juu ya hilo, maana nilisha juwa kuwa, kazi hii hutakiwi kuzubaa, yani ukizubaa umekufa, niligeuka huku nikiwa nimevuta ngumi moja nzito ubapa wa kiganja cha mkono wangu wa kulia uliokunjwa, wajapan wanaita jumbiundo, fumba na kufumbua nilimuona mzee Mangeu akiwa amejikunyata kwa uoga, huku mikono ameikusanyia usoni mwake, nadhani hakutaka kuongeza ngeu nyingine usoni mwake, hakuonyesha kama ana uelekeo wa kupambana na mimi, nikabadili gear angani kwa kumshika mangeu na kumsogeza kwenye ubavu wa gari, kisha nikaukamata mmkono wake na kumzungusha kwa nyuma, huku mkono mwingine nikimkandamiza mgongoni, “dogo!..... dogo!.... hebu niache, waulize pemba yote hii, wenzako wananijuwa Mangeu ni nani” aling’aka Mangeu kwa sauti iliyoonyesha wazi maumivu aliyokuwa nayo kwa wakati ule, “wanaokuogopa hawakujui najuwa haupo kama ulivyosema, kwanini unanifuatilia? vinginevyo nitakupasua pasua” nilimuambia Mangeu kwa sauti ambayo haikuwa na chembe ya uoga, japo moyoni nilikuwa naogopa mzee huyu asije akayaachia majini yake, yani kaushe, “usiniuwe kijana, sina ubaya na wewe, hii ni kwa faida yako” alilalamika babu Mangeu, akionyesha anaumia kwa jinsi nilivyo mminya mzee huyu, unashida gani na mimi, je ni kwaajili ya lile onyo lako la kukaa mbali na Jesse?” nilimuuliza mzee huyu, nikiwa bado nime mminya, “niachie basi tuongee, ujuwe mwenzio nikivunjika siwezi tena kupona?” alisema Mangeu katika sauti iliyojawa na maumivu, “sawa nakuacha, ila kumbuka ukifanya ujanja wowote utakao ufanya nitakumwaga ubongo” nilimueleza Mangeu kwa sauti ya kitisho, nikiwa bado nime mkamata mzee huyu, ambae sasa niliweza kumtazama vyema na kuweza kuona jeraha jingine kubwa kwenye bega lake la kulia, ni sawa na yale ya usoni, japo hili lilikuwa kubwa sana….. ITAENDELEA….. Usimsahau Mtunzi Kwa Chochote Kitu Kwaajili Ya Kumpa Sapoti Tuma Kwa Namba Yake +255 743 632 247