KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI: nilimuuliza mzee huyu, nikiwa bado nime mminya, “niachie basi tuongee, ujue mwenzio nikivunjika siwezi tena kupona?” alisema Mangeu katika sauti iliyojawa na maumivu, “sawa nakuacha, ila kumbuka ukifanya ujanja wowote utakao ufanya nitakumwaga ubongo” nilimueleza Mangeu kwa sauti ya kitisho, nikiwa bado nime mkamata mzee huyu, ambae sasa niliweza kumtazama vyema na kuweza kuona jeraha jingine kubwa kwenye bega lake la kulia, ni sawa na yale ya usoni, japo hili lilikuwa kubwa sana….. ENDELEA …..
kuliko lenzie, “sawa kijana siwezi kufanya ujanja wowote” alisema Mangeu na hapo nikalegeza mkono taratibu kisha nikamuachia kabisa, “hivi wewe ni mwalimu kweli au mwanajeshi mpelelezi?” aliuliza kwa mshangao babu Mangeu, huku anageuka na kunitazaa usoni, “achana na hizo habari hebu niambie kwanini unanifuatilia?” nilimuuliza Mangeu, nae hakunijibu kwanza baada yake akatazama kushoto na kulia, kisha upande wa barabarani halafu akanitazama mimi, “kuna jambo nataka niongee na wewe, ni muhimu sana kwa wewe kufahamu” alisema Mangeu akionyesha wazi kuwa leo alikuwa kama rafiki, sijui alisha tumia uwezo wake wa kichawi kutambua kuwa mimi ni mpelelezi, maana niliona ni ghafla kwake kuja kwangu kirafiki, “inahusu nini?” nilimuuliza huku nikikaa vizuri kwa kuegemea gari, “kijana kwanza kabisa inakupasa ujuwe kuwa, mpaka sasa wewe ni mwenye bahati sana, maana hakuna mtu aliemsogelea Jessenia na akapona” alisema mzee Mangeu, na hapo nika juwa ni lazima niwe tayari kwa lolote, maana ukiona muuwaji ana tubu mbele yako, ujuwe lazima anataka kuuwa au anahitaji kuacha kile anacho kifanya, “kwanini ipo hivyo mzee na wewe ni nani na kwanini unaishi maisha ya kificho ambayo hakuna mtu anae kufahamu undani wako?” nilimuuliza Mangeu, huku nikiwa nimekazia macho, “ni moja ya mambo ambayo tutaenda kuyaongea, endapo utanihakikishia kuwa utamuoa Jessenia, hasa ukiwa ndie mwanaume wa kwanza kutembea nae” alisema Mangeu, hapo nilitabasamu kidogo, ni kwa mshangao, maana sikujuwa amefahamu vipi au aliambiwa na wakina Ussi, ila hii mbona ni tofauti kidogo, wakati wale vijana wa Ussi wananivamia njiani huyu mzee anakuja kuniambia jambo, “hivi mzee kuna mwanaume ambae anaweza kumuacha mwanamke kama Jesse, wewe nijibu maswali yangu” nilisema hivyo na yeye akatabasamu, “ok! lakini itachukuwa muda mrefu kidogo, na nimefanya hivi kwasababu naamini wewe ni msaada mkubwa kwa mschana yule masikini, ambae hamjui baba yake na wala jajawahi kumuona mama yake kwa macho yenye utambuzi” alisema Mangeu, na hapo akaanza kunieleza kile alicho panga kunieleza.
“Watu wananifahamu kama Zidadu Makame au babu Mangeu” hivyo ndivyo babu Mangeu au Zidadu Makame alivyoanza kunieleza kile alicho panga kunieleza.******
Naam mwaka 1978, ilikuwa ni miaka kumi na nne toka mapinduzi ya Zanzibar yatokee, japo ilikuwa ngumu kuwaondoa moja kwa moja waarabu wale, ukichukulia mapinduzi yali lenga kwa viongozi na masultani, ilikuwa ni juma nne saa saba za usiku, upepo ulikuwa mkali sana, manyunyu ya mvua yalikuwa yana dondoka kwa kwa mbali, giza lilikuwa zito, angani hakukuwa na dalili ya nyota wala mwezi.
Mashariki mwa mji wa Tanga, kilomita thelathini toka pwani, lilionekana Jahazi lililochanua tanga zake, ambazo zilikuwa zina pulizwa na upepo huu mkali na kuliongezea mwendo na kuzidi kuyoyoma kuelekea mashariki kulikokuwa na uelekeo wa kisiwa cha Pemba, kisiwa cha marashi ya karafuu, ndani ya jahazi, hilo kubwa la asili, lililokuwa linakatiza kwenye mawimbi makubwa yanayo toka mkondo wa Nungwi na kuwafanya wasafiri kadhaa waliokaa kwenye shehena ya mizigo ndani ya jahazi hilo, lililotengenezwa kwa mti wa mbuyu, jahazi ambalo lilikuwa na watu kumi na moja tu, vijana watatu wanaume wa kiarabu, na vijana saba wanaume wa kitanzania, sita kati yao, wakiwa ni wafanyakazi wa jahazi lile, huku mmoja pekee akiwa ni abiria wa kawaida akionekana kuwa na miaka zaidi ya ishirini na tano, pamoja na mschana mmoja na wa pekee ndani ya jahazi, mwenye umri mdogo wa kati ya miaka kumi na sita au kumi na saba, ambae pia alikuwa msafiri kama huyu kijana mwenzie.
Jahazi hili la tajiri mkubwa wa kiarab, bwana Abdi khalfani Jamal, ambalo lilikuwa linafanya safari zake mara nyingi kwenye bahari hii ya Hindi, likibeba mizigo mingi mingi, ambayo tajiri huyu alikuwa anaikusanya toka sehemu mbali mbali ya mikoa ya bara, ikiwa ni vyakula kama ilivyokuwa leo pia lilikuwa linakusanya vitu vingine vya thamani kama madini na mali nyingine ambayo ilikuwa inauzika katika nchi za kiarab, ambako alikuwa anazisafirisha na kwenda kuziuza kwa njia ya magendo, maana tayari serikali ya mapinduzi ilikuwa imesha weka utaratibu wa biashara ambao matajiri wa kiarabu waliuona mgumu sana.
Wakati hawa wengine tisa, wakiwa katika hali ya kawaida, kwa wale vijana wa kitanzania wakifanya kazi zao kama vile kuongoza Tanga, kusaidia kuondoa maji yasiyo ya lazima ndani ya jahazi na kuhakikisha mizigo haifunguki, huku wale vijana wawili wa wakiarabu wakiwasimamia wale watanzania kufanya kazi, “pumbavu, fanyakazi huwezi kulipwa bila kazi bwana, kama huwezi shuka rudi Tanga kwa kuogelea” maneno hayo yali ongeza hofu kwa wasafiri wawili ambao walichukuliwa na vijana hawa wa kiarabu toka Tanzania bara kwaajili ya kuwapeleka kisiwani Pemba kwa tajiri Abdi khalfani Jamal, mwenye asili ya Oman, kama wafanyakazi wa nyumbani kwa mwarabu huyo, zama hizo ilikuwa vigumu sana kupata mfanyakazi mwenye asili ya Zanzibar, ambao kufanya kazi kwa waarabu ni sawa na kurudia utumwa, hivyo waarabu ambao licha ya kuwa walisha punguzwa makali ya kuwatumia watu weusi wanavyotaka, lakini bado walikuwa wananyanyasa kwa siri wafanyakazi wao ambao wamewatoa nje ya kisiwa, na kwamba hawakuwa na uwezo wa kurudi makwao, kwasababu usafiri pekee ulikuwa ni majahazi, japo wawili hawa hawakuwa wanafahamiana hapo mwanzo, lakini siku hiyo ndiyo siku ambayo, walikutana ndani ya Jahazi hilo.
Hawa walikuwa ni kijana John Joseph, alielazimika kubadili jina na kuitwa Zidadu Makame, na mschana huyu mdogo, Celine Augustino ambae pia aliitwa Aisha Mohamed, sababu ya kubadili majina yao ni kwamba, maboss wao ambao ni waarabu kama yule ambae wanamfuata kule Pemba, yaani Jamal, hawa kuhitaji kufanya kazi na mtu mwenye majina yasiyo na asili ya kiarabu, hivyo vijana hawa wawili toka sehemu tofauti za mikoa ya Tanzania bara, Joseph akitokea mwanza na Celine akitokea bukoba, walilazimika kubadili majina ili wafanikiwe kwende Zanzibar kufanya kazi na kujipatia chochote ambacho kingesaidia familia zao, japo safari yao ilihesabika kuwa haramu kutokana na serikari ya mapinduzi, kupiga marufuku ya kuleta wafanyakazi wa ndani wenye muonekano wa kitumwa, ambayo ilikuwa inafanywa na hawa waarabu.
Safari ilikuwa ngumu sana kwao, nikutokana na uoga waliokuwa nao wakuto kuwahi kusafiri kwenye maji mengi kama yale, huku mawimbi, upepo na giza nene vikiwakabili, safari ambayo iliwalazimu kutembea kwenye maji masaa zaidi ya ishirini na nne, maana jahazi hili lilikuwa lina tembea kwa kutegemea upepo, hata walipo wasili alfajiri ya siku ya tatu, katika bandari ya pango la mtoro kaskazini kabisa mwa kisiwa hiki cha pemba, sehemu ambayo ilitumika kama sehemu ya kuficha watumwa kipindi wana wasafirisha kuelekea nchi za falme zao, kipindi ambacho biashara hiyo ilikuwa imesha pigwa marufuku na jumuiya za kimataifa. Baada ya hapo ikaja mikokoteni mingi sana inayovutwa kwa ngombe na punda wa bwana Jamal Abdi, na kuanza kusomba mizigo hiyo mingi ambayo ingefaa kubebwa na gari kubwa la tani kumi na nane hadi ishirini, Aisha na zidadu nao wakaanza safari wakiongozana na wale vijana wa kiarabu ambao ndio ndugu wa bwana Jamal.
Siku hiyo ndiyo siku ambayo wawili hawa walifahamia, hata walipo anza kazi katika sehemu mbili tofauti, yaani Zidadu akifanya kazi za nje ya nyumba kama vile kusafisha mazingira kuhudumia mashamba makubwa ya mzee Jamal, na Aisha yani Celine akifanya kazi za ndani, usafi wa nyumba kubwa ya mzee huyu na familia yake kubwa, pamoja kupika na kuosha vyombo, kwa kawaida unaweza kusema ni kazi ndogo sana kwa mwanamke wa kitanzania, ila ukweli naposema kuhusu kupika na kuosha vyombo kwenye familia hii ya bwana Abdi Jamal, ambayo ina watoto kumi na tatu, wake wanne, ndugu na jamaa sita, jumla yao walikuwa ni ishirini na nne, mlo mmoja walikuwa wanakula vyakula vingi sana, kiasi kwamba shughuri ya upikaji ilianzia saa kumi na mbili za asubuhi na kuisha saa kumi na mbili jioni, ambapo sasa alianza kazi ya kuosha vyombo, mpaka saa sita za usiku, na angepata muda mchache sana wa kulala mpaka saa kumi za usiku, ambapo angeanza kufanya usafi wa ndani, katika hayo yote Zidadu hakumuacha Aisha, ambae wakati mwingine alimsaidia kwa baadhi ya kazi kila alipopata nafasi, kitu ambacho kilipelekea wawili hawa kuwa kama ndugu, hakika usingeweza kufahamu kuwa walikutana ndani ya jahazi la bwana Jamal, miaka miwili ilitimia wakiwa nyumbani kwa bwana Jamal wakiendelea kufanya kazi.
Mwaka 1980 mwezi wa sita ndio mwaka ambao, mtoto wa kwanza wa bwana Abd Jamal, yaani Abdulkarim Abdi Jamal, aliingia kisiwani Pemba akiwa na familia yake yenye mke mmoja na watoto watatu wakitokea nyumbani kwao Oman, ambako walikuwa wanaishi kipindi hicho mzee tajiri wa kiarabu bwana Abdi khalfani Jamal, bado alikuwa anaendelea kufanya biashara zake ambazo naweza kusema ni haramu, kwasababu alikuwa anazifanya bila kufuata utaratibu wa serikali, mfano alikuwa anatuma ndugu zake wawili ambao walizunguka mikoa mbali mbali Tanzania bara kusaka madini na vitu vya thamani ikiwepo meno ya tembo pembe za faru na ngozi za chui, kisha kuzileta Pemba kwa kutumia ngalawa yake, baada ya hapo husafirisha kwenda Oman, ambako huuza kwa bei kubwa sana na kujiongezea utajiri mara dufu.
Siku moja usiku wa saa saba, katika mwaka huo 1980, mschana Aisha Mohamed akiwa amesha maliza kazi zake, akaingia kwenye chumba kidogo alichokuwa analala juu ya kipande cha godoro, ambacho alikiweka sawa kwa kukitandika, kisha akajilaza juu yake, lakini ile akaegesha ubavu tu akashangaa kuona mlango unafuguliwa na mtoto mkubwa wa bwana Jamal yaan Abdulkarim, ambae kikawaida alikuwa amemzidi umri mkubwa sana Aisha, maana Abdul Karim alikuwa na miaka thelathini na sita, wakati sasa Aisha alikuwa na miaka kumi na nane.
Ukweli ni kwamba Aisha alishtuka sana ujio wa mtoto huyu wa boss wake usiku kama huu, chumbani kwake, lakini akatulia na kujifanya amelala ili aone alichofuata huyu mtoto wa boss wake, ambae alimuona anatembea kwa tahadhari kubwa, kusogelea pale alipokuwa amelala, na alipomfikia yule jamaa akapandisha kanzu yake na kuishusha kidogo nguo yake ya ndani kisha akashika gauni la Aisha na kulipandisha kwa nguvu na kushusha nguo yake ya ndani, masikini Aisha hakuwa na la kufanya zaidi ya kutulia na kutoa ushirikiano kwa kile ambacho mtoto wa boss wake alichokuwa anakifanya, maana angekataa angejiingiza kwenye matatizo makubwa ya kuzidi kunyanyasika, utulivu na ushirikiano alioutoa katika tendo la ndoa lililofanywa na Abdulkarim, ulizidi kumletea mateso na usumbufu toka kwa kijana huyo, ambae alikuwa hapitishi siku mbili bila kujiiba chumbani kwa Aisha kwaajili ya kula kitumbua, tendo ambalo lilifanyika kwa siri kubwa pasipo mke wa AbdulKarim kujuwa, ambae pia alikuwa ni mwarabu.
Naam miezi minne mbele, mke wa bwana Abdulkarim ndie aliekuwa wa kwanza kujuwa kuwa Aisha alikuwa mjamzito, ni siku ambayo alimfumania ana lamba limao, “wewe hii mimba ni ya nani?” aliuliza mke wa bwana Abdulkarim, ambae kiukweli alishtushwa sana na ujauzito ule, ukweli ilikuwa ni vigumu sana kwa Aisha kusema ukweli, lakini haikuishia hapo swala lile likapelekwa kifamilia, na hapo Aisha aliweza kufumania kikao kikali cha familia, kilichojadili ujauzito wake, “mama nina uhakika ile mimba ni ya mtu wa humu humu ndani, hii ni aibu sana kwa mtwana kuzaa na mmoja wa wanafamilia” alisisitiza mke wa Abdul, huku Aisha alie jibanza nyuma ya dirisha upande wa nje akisikiliza, “inabidi kwanza tumfahamu muhusika wa ujauzito huo, ndipo tuweze kutafuta la kufanya” alisema mama mkwe wake, “mamaaaa unadhani kuna mwingine, mwenzio nina week sasa nimegundua kuwa mume wangu anatembea na huyu mtumwa” alisema mke wa Abdul na hapo mapigo ya moyo ya Aisha yalisisimka kwa kujuwa kuwa siri ipo hadharani, “sasa umepanga kufanya nini?” aliuliza mama yake Abdul, yaani mke wa mzee Jamal, “mama mimi ninachofikiria ni kumuuwa huyu mwanamke, vinginevyo jamii yetu nzima haito tuelewa hasa mimi mke wa Abdul” hayo yalikuwa ni maneno ya mke wa Abdulkarim….. ENDELEA NAYO
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA: “mamaaaa unadhani kuna mwingine, mwenzio nina week sasa nimegundua kuwa mume wangu anatembea na huyu mtumwa” alisema mke wa Abdul na hapo mapigo ya moyo ya Aisha yalisisimka kwa kujuwa kuwa siri ipo hadharani, “sasa umepanga kufanya nini?” aliuliza mama yake Abdul, yaani mke wa mzee Jamal, “mama mimi ninachofikiria ni kumuuwa huyu mwanamke, vinginevyo jamii yetu nzima haito tuelewa hasa mimi mke wa Abdul” hayo yalikuwa ni maneno ya mke wa Abdulkarim …... ENDELEA…..
Maneno ambayo yalimshtua zaidi Aisha yaani Celine, ambae alilisikia tumbo lake lina unguruma sambamba na maumivu ya tumbo hilo hilo, katika utumbo mkubwa wa chakula, maumivu yaliyoenda mpaka karibu na njia ya haja kubwa na hapo Aisha akakimbilia chooni kwenda kutatua tatizo hilo la ghafla.******
Kumbe basi wakati wote Aisha akiwa dirishani anasikiliza yanayoendelea kule ndani, Zidadu yeye alikuwa anamuona kwa mbali kidogo, na hata alipomuona anakimbilia chooni kijana Zidadu Makame au John Joseph aliamua kwenda dirishani kusikiliza kilea ambacho Aisha alikuwa anakisikiliza, maana alihisi kuwa kuna kitu hakipo sawa, yaani kule alikotoka Aisha, sio sababu alikimbilia chooni, ila jinsi uso wake ulivyojawa na wasi wasi.
Hivyo basi kijana mkubwa Zidadu Makame, alitembea kwa tahadhari mpaka pale dirishani, yani pale ambapo Aisha alikuwa ametoka dakika chache zilizopita na kujifanya kukatiza, huku akitupia jicho lake upande wa ndani, akamuona mke wa boss wao akiwa pamoja na mkwe wake, yaani mke wa bwana Abdulkarim, wakionekana kujadili jambo upande wa ndani wa nyumba kubwa, hapo Zidadu akapata hamu ya kusikia kile kilichokuwa kinajadiliwa na wawili hawa.
Ndipo alipo sogea kwenye kiambaza karibu na dirisha na kutega sikio “lakini hilo ni swala zito sana, tutafanyaje ili kulikamilisha? kwanini tusimfukuze hapa nyumbani na kumrudisha bara?” aliuliza mama mkwe, yaani mke wa bwana Abdi Khalfan Jamal, “hapana mama, lazima atarudi kumleta mtoto kwa baba yake, na ukichukulia kwa sasa hawa sio watwana wetu, lazima italeta kashfa na matatizo kwa baba mkwe na familia nzima” alisema mke wa Abdul, kwa msisitizo huku maongezi yao muda wote yakitawaliwa na tahadhari kubwa sana.
Mpaka hapo Zidadu alishaanza kuhisi ni nani anazungumziwa na ni kwanini, japo lilikuwa ni jambo jipya kwake, maana hakujuwa kama Aisha ni mjamzito, “unachosema ni kweli, lakini sasa tunawezaje kumuua huyu mwanamke?” aliuliza mke wa bwana Jamal, “hakuna njia nyingine zaidi ya kumlisha sumu, kisha ataenda kutupwa baharini” alisema mke wa Abdul, ambae alipania kweli kweli kumuondoa Aisha duniani, “hapo sawa na inabidi hiyo kitu ifanyike haraka sana, na hatua za mwanzo tusimshirikishe mtu yoyote mwingine, ila akishakufa tu! ndio tuta watuma vijana wa mpeleke baharini” mke wa mzee Jamal aliunga mkono.
Kusikia hivyo Zidadu akajuwa kuwa, Aisha yupo hatarini na hata yeye mwenyewe anafahamu hatari iliyopo mbele yake, hivyo Aisha anatakiwa kuondoka mara moja katika nyumba hii ya bwana Abdi khalfan Jamal, maana endapo atabakia hapa basi hatomaliza siku kabla hajapoteza maisha, lakini tatizo ni kwamba Aisha hakuwa na sehemu ya kwenda, kwa sababu yeye toka amefika kisiwani Pemba, hakuwahi kutoka hapa nyumabani na kwenda kutembea sehemu yoyote kisiwani hapa, “anahitaji msaada wangu, siwezi kumuacha auliwe na hawa watu wasio na huruma” alijisemea Zidadu huku anatoka pale dirishani na kuelekea upande wa chooni, yani choo cha nje, yaani kule alikoelekea Aisha, ambae mpaka sasa alikuwa bado hajatoka.
Kwahadhari kubwa sana John Joseph, aligonga mlango wa choo, “kuna mtu” alisikika Aisha toka ndani ya choo iliyojaa uoga na wasi wasi, “fanya haraka utoke hapa sio salama kwako” alisema Zidadu kwa sauti ya chini na yakunong’ona, hapo yakasikika maji yakimwagika mfurulizo na kwa haraka, kisha mlango ukafunguliwa akatokea Aisha na hapo hapo, Zidadu akamdaka mkono Aisha na kumvutia nyuma ya banda hilo la choo, “Aisha ni kweli una ujauzito?” aliuliza Zidadu, kwa sauti ya chini yakunong’ona, na Aisha akaitikia kwa kichwa kukubali, “mimba ya nani?” aliuliza Zidadu, kwa sauti ya ile ile ya chini, “Abdul.. mimba ni ya Abdul, lakini…” alisema Aisha ambae alitaka kuuliza Zidadu amejuwaje juu ya hilo la ujauzito, lakini Zidadu akamuwahi, “sikia Aisha, hakuna haja ya kuuliza maswali mengi hapa hapakufai, kinachotakiwa ni wewe kuondoka hapa nyumbani haraka, unaweza kuuwawa muda wowote, kachukuwe unachoona unaweza kubeba kisha tuondoke” alisema Zidadu na huku akimsisitiza kuto kula chochote ndani ya nyumba ile, maana sasa alikuwa hatari ya kulishwa sumu ili afe.
Aisha aliingia ndani ya nyumba kubwa, ambako pia kulikuwa na kile chumba kidogo ambacho Aisha alikuwa analala, Zidadu alibakia pale nje akimsubiri huku anatazama usalama, yani kama kutatokea mtu ambae anaweza kusababisha, kushindikana kwa mpango wake wa kumtorosha Aisha, bahati nzuri kwao ni kwamba mida kama hii watu wengi huwa katika shuguri mbali mbali, hvyo nje palikuwa peupe kabisa, hata pale nyumbani palibakia na watu wachache sana.
Naam Zidadu aliendela kumsubiri Aisha aliechukuwa dakika zaidi ya kumi ndani ya nyumba kubwa, na kilichoanza kumtia wasi wasi Zidadu bwana John, ni pale aliposikia sauti ya mke wa Abdul ikimuita Aisha toka ndani ya nyumba, akajuwa tayari sasa kinachofwatia ni Aisha kwenda kupewa sumu na kuuwawa, ukweli matukio ya wafanyakazi wa jumba la bwana Abdi kutoweka ghafla na kukutwa wamekufa huko baharini, yalikuwa mengi sana, ndicho kitu ambacho kilimfanya Zidadu aamini kuwa Aisha akizubaa pale kwa mzee Abdi Jamal atauwawa kweli kama alivyo wasikia mke wa boss wake na mkwe wake wakipanga kufanya hivyo, tena bila kumshikirikisha mtu yoyote.
Zidadu akiwa anatarajia kumuona Aisha akitoka mafuko mdogo sana, ambao ungekuwa na nguo chache ambazo Aisha alikuwa anazimiliki, aliendelea kutulia pale nje macho mlangoni, huku kichwani mwake akishangaa kitendo cha Aisha kuchelewa kutoka nje, wakati na yeye mwenyewe alikuwa anafahamu vyema hatari ambayo ilikuwa mbele yake, na mbaya zaidi ni kwamba mke wa Abdulkarim alikuwa anaendelea kuita.
Lakini dakika tano baadae, Zidadu alishtuka sana baada ya kumuona Aisha anatoka ndani akiwa anaburuza begi kubwa, ambalo lilonekana kuwa ni zito sana, pamoja na kijishuka kilichofungwa kwa mtindo wa furushi dogo, ndani yake kuwa na nguo chache ambazo alitegemea kumuona nazo, “Aisha ndio unafanya nini sasa” aliuliza Zidadu kwa sauti ya kunong’ona, maana kilicho mshtua Zidadu ni lile begi kubwa lililokuwa linakokotwa na Aisha, “twende Zidadu, wameshaanza kuniita huko ndani” alisema Aisha kwa sauti ya kunong’ona, akionyesha mwenye wasi wasi mwingi sana, “Aisha ni hatari hicho ulichofanya, kwanini sasa umechukuwa hili begi?” aliuliza kwa sauti ambayo ilikuwa na uoga japo hakumzidi Aisha, maana begi lile ni moja kati ya mabegi ambayo boss wao yani bwana Abdi Khalfani Jamal, anatumia kuhifadhia na kusafirishia mali zake zenye thamani kubwa, yaani madini yake yakiwa ni dhahabu na almas kwenda kwao Oman, “tuondoke Kaka Zidadu, hizi zitatusadia baadae” alisema Aisha huku anamuonyesha ishara Zidadu yakuwa amsaidie kubeba lile begi kubwa.
Naam!!! Zidadu hakuzubaa tena, maana tayari ingekuwa tatizo endapo wange kutwa na lile begi kubwa pale nje, hivyo akalinyakuwa nakuanza safari ya kutoka pale kwenye viunga vya jumba la tajiri Jamali, huku wakisikia sauti ya mke wa Abdul ikiita huku anasogea kuja upande wa kule walikokuwa, “Aisha!! we Aisha!! upo wapi wewe!!!” alisema mke wa Abdulkarim kwa sauti iliyojaa hasira, na hata alipotokeza nje ungeweza kuona jinsi alivyojawa na hasira kiasi cha ya rangi yake ya kiarabu kugeuka na kuwa nyekundu, hasa sehemu za pua na mashavu, “Aishaaaa umeamua kujificha sio?” alisema yule mwanamke, kwa sauti iliyojaa hasira huku anatazama kushoto na kulia, kisha akarudi ndani ambako alienda moja kwa moja mpaka kwenye kijichumba kidogo anacho lala Aisha, lakini hakukuwa na mtu, wala dalili ya mtu, maana hakukuwa na nguo wala shuka.
Mke wa Abdul akachomoka mbio kuelekea upande wa sebuleni, “mama! mama! amesha toroka, ina maana atakuwa ameshatusikia tulichokuwa tuna panga” alisema mke wa Abdulkarim, “inabidi tuwatume vijana wakamsake haraka watazame kila sehemu hasa pwani, asije akatoroka kuelekea bara” alisema mama mwenye nyumba, lakini mpango huo ulikuwa mgumu kwao, maana mchana ule wafanyakazi wa kiume wote hawakuwepo nyumbani, ila sasa kilicho wapa moyo ni kwamba ngarawa za kuelekea bara, zilikuwa zinaanza safari mida ya saa kumi na mbili za jioni, hata meli ya MV Mapinduzi nayo ilikuwa inatoka pemba saa mbili usiku, “lakini usimuhusishe Zidadu, yeye ni rafiki yake” alisisitiza mama yake Abdulkarim.
Yap, bwana Zidadu Makame, au John Joseph, alimpeleka Aisha moja kwa moja mpaka kwenye eneo moja kubwa lenye vichaka vingi na nyumba moja moja, jirani kabisa na mji wa chake chake, eneo ambalo ndani yake kulikuwa na shamba kubwa la mihogo na kijumba kimoja kidogo cha nyasi katikati ya shamba hilo lililopakana na jumba moja kubwa la mwarabu mmoja ambae ni mtu wa magendo pia, kama ilivyokuwa kwa bwana Jamal, “hapa ni kwa nani?” aliuliza Aisha, ambae siku zote ni mtu wa kukaa ndani ya jumba la Abdi Jamal, tofauti na mwenzie Zidadu ambae, alikua anaenda kuhudumia mashamba ya tajiri huyo, “hapa nimejimilikisha tu, maana hapakuwa na mtu yoyote anae paangalia, na upande wa kule chini kabisa ndio kuna shamba kubwa la nazi la mzee Jamal, hivyo wewe utakaa hapa mpaka tutakapo pata nafasi ya kuondoka kwenda bara, alisema Zidadu ambae alihakikisha anaweka mazingira mazuri kwaajili ya Aisha, kisha akamuaga na kuelekea nyumbani kwa boss wao, huku akimsisitiza Aisha kuondoa uoga, muda wote akiwa mahali pale, kwamba baadae angeletea baadhi ya vitu ambavyo vingemsaidia katika maisha yake mapya.
Naam mama Abdul na mkwe wake, walikaa huku wametega macho na masikio wakiwasuburi kwa hamu vijana warudi toka kwenye majukumu mbali mbali waliyopangiwa, mpaka saa kumi na moja mida ambayo vijana wafanyakazi walianza kuingia nyumbani wakitokea sehemu mbali mbali, na ndio mida ambayo Zidadu aliingia pale nyumbani kama vile anatoka shambani.
Zidadu akiwa anaelewa kila kitu kinachoendelea, aliwaona wale wa mama wakiwaita vijana watatu wa kiswahili, yani weusi kama yeye mwenyewe, na kuanza kutoa majukumu kwa vijana wale, ENDELEA NAYO…
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA TATU
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI: Naam mama Abdul na mkwe wake, walikaa huku wametega macho na masikio wakiwasuburi kwa hamu vijana warudi toka kwenye majukumu mbali mbali waliyopangiwa, mpaka saa kumi na moja mida ambayo vijana wafanyakazi walianza kuingia nyumbani wakitokea sehemu mbali mbali, na ndio mida ambayo Zidadu aliingia pale nyumbani kama vile anatoka shambani.
Zidadu akiwa anaelewa kila kitu kinachoendelea, aliwaona wale wa mama wakiwaita vijana watatu wa kiswahili, yani weusi kama yeye mwenyewe, na kuanza kutoa majukumu kwa vijana wale, ENDELEA NAYO
Naam tunaomba sapoti yako kwa mtunzi wetu kwa Chochote utakacho kuwa nacho kwaajili ya bando na matengenezo ya vifaa kwa number +255 743 632 247...
japo yeye hakusikia lolote, lakini alijuwa wanaongelea nini, na walipomaliza tu vijana wale waliondoka zao na kutokomea kabisa, yeye hakuhangaika nao, zaidi alitulia na kupiga mahesabu ya namna ya kuiba baadhi ya vyakula vikavu na kumpelekea yani visivyo pikwa, kama vile mchele chumvi sukari unga na maharage, ili akampelekee rafiki yake ambae sasa ni kama ndugu yake, na wakati anawaza hayo mara akaitwa ndani na mke wa mzee Jamal yaani mama mwenye nyumba, “Zidadu mara kwa mara huwa nakuona unamsaidia Aisha kupika, leo utapika baada yake, maana haonekani kabisa” alisema mke wa mzee Abdi Jamal, “naam mama bila shaka” alijibu Zidadu kwa sauti iliyojaa nidhamu ya hali ya juu na kuelekea jikoni kufanya kazi ambazo zilimpasa kufanya Aisha, ikiwa ni pamoja na kupika kuosha vyombo, na wakati mwingine kufanya usafi ndani ya nyumba ile kubwa, kazi hizo hazikumzuia Zidadu kupata muda wa kwenda kwa Aisha na kumpatia mahitaji, na alijitahidi kufanya kazi zake zote kwa wakati, na kwa haraka kisha kwenda kule kwenye kibanda ambako ndio misingini ya leo kumuona Aisha na kumpelekea mahitaji, huku lile begi kubwa likiwa limehifadhiwa chini ya ardhi ndani ya kibanda kile, ambacho kila siku kilikuwa kina zidi kuboreshwa na kuwekwa vizuri, sasa kuta zake zilikuwa zimezibwa kwa tope juu ya fito na nguzo za miti imara.
Siku zilienda vijana wale watatu wakimtafuta Aisha bila mafanikio, lakini walikuwa na hakika kuwa Aisha hajatoka nje ya kisiwa, kwasababu siku ile walikagua kila ngalawa iliyotoka na pia MV Mapunduzi haikuwa na safari ya Pemba, na walifanya ukaguzi siku zote kwenye kila pwani na fukwe ambazo zinatumika kuegesha ngalawa na vyombo vingine vya usafiri wa majini, (kwenye maji), lakini hawakupata chochote, hata mwezi ukapita ukafuata mwezi wa pili, na hatimae miezi tisa ya ujauzito wa Aisha ikatimia, na Aisha akajifungua mtoto wa kike, katika hospital ya chake chake, nae akamuita Josephiner, alikuwa na chembe nyingi sana za baba yake, yaani rangi na sura za kiarabu, lakini kadiri alivyozidi kukuwa mtoto alionekana kuchukuwa umbo la mama yake, maana alikuwa kwa kasi sana.
Lakini siku ngumu ilifika, ni siku ambayo Zidadu yaani kijana John Joseph hawezi kuisahau, ilikuwa ni mwaka mmoja baadae, mtoto Josephine akiwa ana umri wa mwaka mmoja, ni siku ambayo ilikuwa na matukio mawili tofauti lakini yaliyo ingiliana, tukio la kwanza ni serikali kutangaza kwamba inatoa masaa ishirini na nne, waarabu wahamiaji waondoke ndani ya kisiwa cha pemba, ni baada ya kugundulika kwa njama mbovu na biashara haramu walizokuwa wanaziendeleza, pia propaganda za chini kwa chini walizokuwa wanazieneza watu hao ili kuchochea baadhi ya wazawa ili wavunje muungano na wao kupata nafasi ya kurudisha utawala wao wa kinyanyasaji, tukio la pili ni kwamba tayari mke wa Abdukarim, alikuwa amesha letewa taarifa sehemu ambayo Aisha amejificha na binti yake, taarifa ambayo mpaka leo bwana Zidadu hajafahamu ililetwa na nani kwa mama yule, ambae alitaka kuhakikisha haachi mbegu ya mume wake hapa Tanzania, alituma vijana wake kwenda kumuuwa mtoto wa Aisha, huku akiwakabidhi dhahabu nyingi sana kama malipo ya kabla ya kazi ya kumuuwa Aisha, bahati nzuri wakati huo Zidadu alikuwa jirani na kile kijumba anachoishi Aisha, yaani kwenye lile jumba kubwa la kupendeza, akifanya malipo ya vipande kadhaa vya dhahabu, kwa kubadilishana na ile nyumba toka kwa muarabu ambae pia alikuwa anaondolewa nchi kwa amri ya serikali.
Bahati nzuri Zidadu alifanikiwa kupata nyaraka zilizo mmilikisha ile nyumba akiwa na uhakika kuwa yeye na Aisha wataishi kwenye jumba lile kwa raha mustarehe, maana hawatakuwa na mtu wa kumkimbia wala kumuogopa, lakini jaikuwa hivyo maana ile anatoka kwenye lile jumba la ghorofa mbili lililozungukwa na uzio mkubwa wa ukuta, akasikia kilio cha mwanamke toka kule kwenye kibanda cha shambani, ndipo alipotoka mbio kwenda kuangalia kulikoni.
Zidadu anasimulia kwa kifupi kuwa, alicho kikuta kule bandani ni zaidi ya balaa, maana alikuta vijana watatu ambao alikuwa ana wafahamu vyema kabisa, kwa kuwa vijana wale walikuwa ni wafanya kazi wenzake kule kwa mwarabu, wakimshambulia Aisha kwa mapanga na mrungu makubwa ambayo walipaswa kumshambulia mtu ambae aliwadhulumu na kuwa nyanyasa kwa muda mrefu, ukweli Zidadu roho ilimuuma, maana ukiachilia kuona kile alichokipigania kwa muda mrefu leo kinatolewa uhai kikatili, pia Zidadu alishamuona Aisha kama ndugu yake, hivyo akusubiri kitu kile kitokee mbele ya macho yake, hivyo akakimbia mpaka pale nje ya kibanda kile cha udongo ambapo alikuta wale jamaa wanampiga kwa marungu makubwa bi Aisha, ambae alikuwa amemkumbatia binti yake mdogo kwa kumkinga asifikiwe na chochote, huku marungu yale yakituwa sehemu mbali mbali za mwili wake, hasa sehemu za mgongo na kichwani, Aisha alikuwa anavuja damu kwa wingi sana, mwanae Josephiner alikuwa analia sana, Aisha hakutaka kumuachia binti yake, alimzuia asipatwe na kipigo cha aina yoyote, maana kama angefikiwa na rungu hata moja sehemu yoyote ya mwili wake basi mschana huyo mdogo asinge vuta hata pumzi moja baada ya hapo.
Zidadu au John Joseph, hakuuliza akamsukuma mmoja kati ya vijana wale wenye roho ngumu, ambae aliyumba kidogo na kuaguka chini, maana jakutegemea kitendo kile, hapo wale wawili waka shtuka na kumgeukia Zidadu, ambae ile anajiweka sawa akashtuka kuona mmoja kati ya wale wawili akivurumisha lile gongo lake kwa mtindo wa kuuwa nyoka na kulileta usawa wake, lakini yeye akalikwepa na kurukia pembeni, huku lile gongo likipita pembeni, hapo akajuwa kama hato tumia silaha yake pia anaweza kupoteza maisha na kushindwa kumsaidia Aisha na binti yake, ambao ni kama walikuwa wanamsubiri yeye ndipo Aisha akose nguvu, maana sasa Aisha alianguka na kulala chini huku akiwaachia mtoto pembeni.
Kazi ilikuwa ngumu maana wakati Zidadu akijiweka sawa ili kukabiliana na vijana wale watatu, ndipo alipo muona kijana mmoja kati ya wale, akiinua gongo lake na kuliekeza kwa mtoto Josephiner aliekuwa amekaa pembeni ya mama yake analia kwa hofu kubwa, hapo pasipo kujari atajisikiaje Zidadu au bwana John Joseph, alijitosa mzima mzima nakwenda kuzuia lile rungu lisituwe kwa Josephiner, nalo likatuwa mgongoni kwake, hapo akageuka ili kuwakabiri vijana hawa wakatili, lakini ile anageuka akashtuka kuna kisu kikija usawa wa uso wake, ambacho katika harakati za kukikwepa kika mchana kwa nguvu usoni, zidadu anasema alisikia maumivu makali sana, akageuka kuficha uso wake, huku bado ana mkinga mtoto Josephiner asikutane na rungu, ambapo sasa kulisha ongezeka visu, ile anageuka tu, akasikia maumivu makali ya kisu mgongoni kwake, kisu ambacho kilichana kuanzia kwenye bega la kulia, mpaka karibu na kati kati ya ngongo kuja usawa wa uti wa mgongo.
Hapo ndipo Zidadu akaona kuwa, anahitaji kuchukuwa maamuzi magumu, nayo ni kumtupia mtoto ndani ya kibanda huku yeye anavumilia marungu na visu vya mgongo, alimshika Josephiner na kumrushia ndani ya kile kibanda ambacho kilikuwa wazi, kisha akageuka kuwazuia wale vijana watatu wasiweze kuingia ndani ya kibanda kile, lakini ile anageuka akakutana na kisu kingine kilicho mchana tena usoni, hapo ni kama wale jamaa walimpandisha hasira kijana huyu toka tabora, maana Zidadu alijitosa mzima mzima na kumvamia yule mwenye kisu, na kumsukuma kwa nguvu, nae akaanguka chini akijibwaga kwa nguvu kiasi cha kutengana na kisu chake, ambacho Zidadu alikirukia kwa haraka na wakati huo rungu la kichwa lilikuwa lina mfuata, Zidadu hakuwa na muda wa kulikwepa, zaidi alichofanikisha nikukwepesha kichwa chake kilichokuwa kinavuja damu hasa maeneo ya uso, na kukinga upande wa mgongo, lakini lile rungu lilipo tuwa tu na yeye hakusikilizia maumivu akakunjuka na kile kile kisu akikizamisha chini ya mbavu za kushoto za mmoja wao, hakufanya hivyo mara moja, alichomoa na kuzamisha tena kama mara mbili tatu, ni mpaka aliposhtuliwa na rungu la kichwa ambalo lilimtupa pembeni, hata hivyo hakuta kusikilizia maumivu, akainka mara moja na kumvaa mzima mzima yule alie lkuwa anamkabili kwa wakati ule na kumuangusha huku yule mwenzie kuona vile akainua rungu lake na kulivurumisha usawa wa kichwa chake, Zidadu kuona vile akajitupa pembeni na lile rungu lika tuwa kwenye paji la uso la yule aliemuangusha, ambae alizimia pale pale na hapo akainuka kumkabili yule mmoja aliebakia, ambae aliinua tena rungu lake lakini kabla hajalishusha kichwani kwa Zidadu, tayari zidadu alisha mrukia na kumuangusha chini, kisha akainua kisu chake na kutaka kukishusha kifuani kwa huyu jamaa, “Zidadu usiniuwe, mimi ni mtanzania mwenzio, tulitumwa tu….” hakusubiri amalizie akamshindilia kisu cha koo, baada ya kifuani kama alivyo panga mwanzo na kumuona yule jamaa akitapa tapa kwaajili ya kukata roho.
Zidadu hakutaka kusikilizia maumivu aliyo kuwa nayo akamfuata yule aliezimia pasipo kujari kama alikuwa amekufa au amezimia akamshindilia kisu cha shingoni, halafu akamtazama yule kwanza ambae pia alikuwa anamalizia kukata roho, ndipo alipo msogelea Aisha ambae alikuwa na hali mbaya sana, akaona hakuna njia nyingine zaidi ya kumpeleka hospital akapate matibabu.
Zidadu ambae pia hali yake haikuwa nzuri, akamchukuwa Josephiner na kumbeba mgongoni na wakati anamnyanyua Aisha yaan Celine, nae akafumbua mdomo wake, “kaka… wala u..si..ji..sumbue, mi…mi… siponi tena” alisema Aisha kwa tabu, “naomba umlee mwanangu, nae awe mkubwa, akikuwa mueleze kuhusu ndugu zake, wa…wa…bunazi” alisema Aisha dakika za mwisho za uhai wake.
Aisha alipoteza maisha na Zidadu, au kijana John Joseph, akamzika nyuma ya kibanda chake, pasipo kuweka alama sahihi ya kaburi, huku miili ya wale wavamizi akiitupa kwenye pori mita kama mia nne toka pale kwake, akiwa amesha ikagua na kuchukuwa vile vipande vya dhahabu walivyo pewa na mke wa Abdulkarim, ilikuwa ni kazi ngumu sana kutibu majeraha usoni huku anamlea mtoto Josephiner.
Kingine kikubwa kilicho tokea usiku wa kufukuza wahamiaji, ni wananchi wali wavamia wahamiaji hao na kuwaibia mali zao, hivyo serikali ilianzisha msako mkubwa sana juu ya wavamizi hao, kitendo kilicho mfanya Zidadu Makame kuishi kwa kujificha na kuzidi kuwa na wakati mgumu kumlea mtoto Josephiner, kwanza asingeweza kujitokeza hadharani kutokana majeraha ya wazi yaliyokuwepo usoni mwake, pili asingeweza kuishi kwenye jumba kubwa alilonunua kutokana na muonekano wake wa kujeruhiwa lazima angehisiwa kuwa ni mmoja wa wanyang’anyi, ndipo alipoamua kuchukuwa uamuzi ambao aliuona kuwa ni sahihi, kwamba ile nyumba alivyoinunua kwa vipande vya dhahabu, amuache aishi kijana mwenzie Juma Mohamed, ambae alikuwa na mke na mtoto moja mdogo wa kiume, mwenye miaka mitatu alieitwa Ussi, kijana Juma Mohamed, yeye hapo mwanzo alikuwa ni mfanyakazi kwenye ile nyumba ya mwarabu, aliempatia nyumba Zidadu, kijana ambae naweza kusema ndie pekee aliekuwa anafahamu uwepo wa Aisha pale kwenye kibanda, Zidadu alimuacha aishi pale kutokana na mambo matatu, moja ni kwamba yule kijana alikuwa ni mwenyeji wa Unguja, hivyo lafudhi yake ilikuwa ni ya kizanzibar, na muonekano wake haukuwa na shaka yoyote kama ilivyo kwa Zidadu aliepasuka pasuka usoni…..ITAENDELEA