Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA NNE: " kwa maana hatujui kama una mwanamke mwingine huko kwenu au laa umuoe na kwenda nae bara, ambako naamini mutaishi kwa amani, nipo tayari kugharamia kila kitu na nitawakabidhi kila kinacho muhusu Jessenia, naamini Jessenia mpaka hapo ameweka imani yake na upendo wake wote kwako, kwa kuwa anaamini kile ninacho amini kuwa wewe ndie mwanaume wake wa pekee” alisema yule mzee ambae alimalizia kwa kusema kuwa “nikikuona nae kesho naamini umechagua jambo la mwisho, zaidi ya hapo sitajali wewe ni nani, uwe mjeshi au mwalim, na ume fwata nini Pemba, nitahakikisha nakufukia ndani ya kibanda changu” alisema yule mzee na hapo nilijihisi natetemeka kidogo…..…..ENDELEA....
Maana alipokuwa anaongea hakuonyesha dalili ya utani, na alipomaliza akaenda pale upenuni na kuwasha vesper yake, ambayo ilonekana kuwa mpya kabisa na kuondoka zake kuelekea mjini, na ndio wakati ambao nilisikia simu ikikatika mfukoni, ikiwa ni mara ya tano kuita pasipo kuipokea, nilimsindikiza kwa macho mpaka alipotowekea upande mjini.
Naam hapo nilihakikisha milango ya gari kisha nikaingia ndani, huku natafakari simulizi ya Mangeu, nikijiuliza kama ni kweli mzee Mangeu hausiki na vifo vya wanaume wanao msogelea Jessenia au anahusika, na je? kama yeye hausiki ni nani anahusika zaidi ya Ussi, inawezekana Ussi anafahamu kuhusu utajiri wa Jessenia ndio maana anajitahidi kuzuia mwanaume yoyote asimsogelee binamu yake, na kama ni hivyo basi mjomba wake anahusika na hilo, pia niliwaza juu ya maagizo ya Mangeu, yaani Zidadu kuwa nichague moja, kati ya kuachana na Jessenia, au kumuoa, huku akinipa shariti la kutokumtenda mwanamke yule mzuri kuliko uzuri wenyewe, ukweli ni kwamba ukiachana na mali au utajiri aliokuwa nao Jessenia, ambao hata yeye mwenyewe hakuwa anaufahamu, ambao sikuwa na mpango nao, mimi nilishaanza kumpenda mschana huyu ambae alikuwa na kila kitu ambacho mwanamke anapaswa kuwa nacho, hivyo swala la kumuoa Jessenia lingekuwa rahisi sana kwangu, kwa maana Jessenia mwenyewe pia alisha onyesha kuhitaji jambo hilo, lakini swali ni je itakuwaje kama kuna mtu yupo nyuma ya hili, maana dalili nilishaiona kwa kuvamiwa na vijana wa Ussi.
Niliwaza hayo, hata wakati wakuoga, sikukumbuka kutazama missed call mpaka wakati nilipomaliza kuoga na kurudi chumbani nilipojilaza kitandani, hapo nilikutana na missed call kadhaa, tano zikiwa ni kutoka kwa Jessenia, na kumi toka kwa Mwasenga, ilinifanya nitabasamu kidogo, maana moja kwa moja nilihisi tayari kuna jambo Mwasenga alitaka kuniambia, wakati najiandaa kumpigia, mara simu yangu ikaanza kuita, nae alikuwa ni mtoto wa Aisha, yaani Josephiner au Jeseenia, nikajiuliza nipokee au nisipokee, ili ikikatika nimpigie kwanza Mwasenga, lakini kwakuwa Jessenia sio muongeaji sana, nikaamua nipokee kwanza simu yake, “jamani Eric, kwanini hupokei simu yangu, yani umenifanya niwaze vibaya” alisema Jessenia kwa sauti iliyochangamka kidogo, “uliwaza nini Jesse, mbona mimi siwezi kufanya jambo lolote la kijinga ambalo litakuumiza Jesse” niliongea kwa sauti tulivu ya kimahaba ya kiume, nikasikia kicheko laini toka upande wa pili wa simu, “hapo ndipo unaponiwezea Eric, najihisi mwenye bahati kuwa na wewe” alisema Jessenia, kwa sauti tulivu iliyoanza kulegea, “bahati niliyonayo mimi naifahamu mimi mwenyewe, hata wewe hauifahamu” nilimueleza Jessenia kwa sauti ile ile tulivu, “asante mpenzi wangu, mimi nilitaka kufahamu kama bado upo sawa” alisema Jessenia na nilisha fahamu alikuwa anamaanisha nini, nikacheka kicheko cha kivivu, lakini kwa sauti nzito, “ulidhania nimeuliwa na jini?” nilimuuliza Jessenia, huku naendelea kucheka kidogo, na yeye akacheka kidogo, “usichukulie utani Eric, inabidi uwe makini sana, sitaki kukupoteza Eric” alisisitiza Jessenia, pia tukakubaliana kuwa tutawasiliana kesho mapema, na wakati nakata simu, nikasikia ngurumo ya gari linakuja na kusimama nje ya jengo hili la Green House, ambalo naishi ndani yake, kwa ngurumo ile niligundua kuwa lilikuwa ni gari la jeshi lile analoendesha Mwasenga, “mh! anaishugani huyu, au …..?” nilijiuliza huku nikitazama saa kwenye simu yangu, ilikuwa nikama saa nane kasoro, nilihisi kuwa huenda imeshafahamika kama nimewashambulia wale jamaa wawili, na hazikupita hata dakika mbili kabla sijasikia sauti ya mwasenga iliyojawa na hofu, “hoya ticha! ticha hee!” aliita Mwasenga huku anausogelea mlango wa chumba changu, “karibu bro” niliitikia huku nainuka na kuusogelea mlango, na kuufungua, kichwani mwangu nilikuwa najiuliza nikitu gani kimemleta Mwasenga mida hii, “Ticha nilipata wasi wasi sana juu yako, ujuwe kuna tukio limetokea usiku huu, wanasema kuna mtu amekutwa ameuliwa na jini huko barabara ya wete mitaa ya karibu na Gombani” alieleza mwasenga, na kunishangaza kidogo, maana niliiona kuwa ni taarifa mpya ya kushangaza kidogo, ina maana ni kweli kuna jini ambalo linauwa watu na sio mtu kama nilivyoanza kuhisi, “unamaanisha nini kusema umewawa na jini, kwani kuna watu walimuona huyo jini wakati anamuuwa huyo mtu?” nilimuuliza Mwasenga kwa mshangao, “hapana wamekuta mtu ameuwawa, na amekauka kama ilivyokuwa kwa Vuai” alisema Mwasenga ambae alisema kuwa aliingiwa na wasi wasi juu ya usalama wangu, “maana inasemekana ulionekana unaelekea upande wa Macho manne” alisema Mwasenga ambae nilikuwa na msikiliza kwa umakini sana, kama alichokuwa anakisema kama kweli ilikuwa ni wasi wasi na usalama wangi au alikuwa nakingine alichikuwa anakijuwa, “hoo ni kweli, nilipotoka pale Jesse alinipigia simu alikuwa amesahau simu kwenye gari, nilienda msigini kumpeleka tukapiga story mbili tatu kisha nikaondoka zangu kuja huku” nilimueleza Mwesenga, huku nikiendelea kumsoma, “ujuwe nini kaka, ile unaondoka tu, wakaja jamaa fulani wawili, wakawa wanaongea na Ussi, hapo shemeji yako akasema kuwa lazima Ussi anapanga jambo kuhusu wewe, wale jamaa hawakukaa sana wakatoka, hawakurudi tena, zaidi tuliona Ussi anapokea pokea simu na kutoka nje mara kwa mara, halafu alikuwa amelewa sana, na baadae tuka muona akiondoka kwa haraka na hakuonekana tena mpaka tuliposikia kuwa kuna mtu amekutwa ameuliwa na jini huko gombani, nikakumbuka maneno ya shemeji yako kuwa kuna jambo wakina Ussi wanalipanga, hivyo nikasema ngoja nikutafute isijekuwa wanauwa wao halafu wanasingizia jini, sasa kila nikipiga hupokei, hapo nikaona mambo mazito, sasa nilipo warudisha wafanyakazi wa pale messi nikaona nije nikuchek” alisema mwasenga, ambae hakukaa sana akaondoka zake.
Mpaka hapo, Mwasenga ni kama alikuwa ameniletea taarifa muhimu sana, ni wazi kuna kitu kilikuwa kina endelea, kwanini hilo jini limeshindwa kuniua mimi na kwenda kumuuwa mtu mwingine na vipi kuhusu wale vijana wawili wa pale Ngerengere mbona Mwasenga hakuwazungumzia, au waliamka na kuondoka zao, sikutaka kuumiza sana kichwa changu, baada yake nilipanga kesho nikatafute ukweli mjini, kwanza kabisa nikakutane na doctor Afidhi, wa pale hospital ya chake chake ili ajaribu kunitazamia kile kilichopo ndani ya kile kichupa, pili nimtafute insp Aroub, ili nipate chanzo cha kifo cha mtu huyo, bada ya hapo niliamini kuwa muda utakuwa umeenda hivyo natakiwa nikutane na Jessenia, ambae lazima atakuwa amenitafuta vya kutosha.*******
Sijui ni kutokana na kuchelewa kulala, maana nilijiona kama nimelala kwa muda mfupi sana, kabla sijasikia mlango wa chumba changu unagongwa, niliamka kwa kukurupuka huku mkojo ukiwa umenishika vibaya sana, mara nyingi huwa sina tabia ya kuamka usiku kujisaidia, nika ufuata mlango mbio mbio na kuufungua, nikamuona mwalimu Aisha akiwa amesimama mlangoni, “we mwanaume ina maana na leo ulipanga kuchelewa sio?” aliuliza mwalimu Aisha, huku macho yake yenye kimbele mbele yakitazama mbele ya bukta yangu na kuona jinsi dudu ilivyo tutumka, ambae sikumjibu, baada yake nikakimbilia chooni kwenda kupunguza maji, nilipomaliza nikarudi chumbani nikamkuta amekaa kwenye kitanda huku anaangaza angaza macho, “shuguri ya jana ilikuwa nzito kweli kweli” alisema kwa utani Aisha huku anatabasamu.
Ilinishangaza kidogo, maana nilijuwa anazungumzia nini, je amejuwaje, “shuguri gani unaizungumzia?” nilimuuliza kama vile sijui alichomaanisha, huku nachukuwa mswaki na dawa yake, “mh! ila we mwanaume unakizizi kikali kweli kweli, umempataje pataje yule mwanamke?” aliuliza Aisha, ambae ni kama alikuwa na uhakika na anacho kiongea, “usipende kuongea kitu usichokijuwa bwana” nilijifanya kukata kauli, huku naondoka zangu kuelekea bafuni, “nisichokijuwa nini, kwani hakuja hapa na wakati mimi mwenywe ndie niliemuelekeza mpaka mlango wa chumba, na hapa nilipo nasikia harufu ya perfume yake” alisema Aisha huku akicheka kwa kunitania, sikutaka kumjibu, maana alicho niambia hata Jessenia pia aliniambia namna alivyopajuwa ninapokaa.
Bafuni sikukaa sana, nilioga haraka na kupiga mswaki kisha nikatoka na kurudi chumbani, ambako nilimkuta mwalimu Aisha bado ananisubiri, “Eric umesikia tukio la jana usiku?” aliuliza mwalimu Aisha, huku anainuka kwa lengo la kutoka nje ili kunipisha nivae, “tukio gani hilo?” nilimuuliza Aisha japo nilishahisi kuwa ni tukio lile lile la kuuwawa kwa mtu huko gombani, “vaa kwanza bwana, nitakusimulia wakati tunaenda shuleni” alisema Mwalimu Aisha, huku anatoka nje na kufunga mlango, na wakati huo huo nikasikia simu inaita, nilipoitazama alikuwa ni Jessenia, sijui alikuwa anaweka kiasigani cha vocha, maana wakati ule hakukuwa na offer ya dakika, wala bando, ulikuwa unapiga kwa vocha kama ilivyo, “asalam alaykum Jesse” nilisalimia mara tu baada ya kupokea ile simu, “mh! wa walaykum salaam Eric, umeshaamka kujiandaa kwenda kazini?” aliuliza Jessenia kwa sauti yake nzuri, iliyoonyesha wazi kuwa bado alikuwa kitandani, “yaan ndio namaliza kujiandaa hapa ili niende kazini” nilimjibu kwa sauti tulivu kama mwanzo, “sawa, basi ngoja nikuache ujiandae” alisema Jessenia na kukata simu.
Dakika tano baadae, mimi na Aisha tulikuwa njiani tunaelekea shuleni, huku ananisimulia kuhusu tukio lile lile la mtu alie okotwa barabara ya wete karibu na migombani akiwa ameuwawa na kukauka kama ilivyokuwa kwa wakina Vuai, na wengine waliopitia kwenye mikono ya jini, nikasema akisikia Eric hatokaa atoke usiku” alitania Aisha alipokuwa anamalizia kusimulia mkasa huo, “nilikuambia kuwa Pemba kuna majini wewe huku amini” nilimuambia Aisha, na maongezi yetu yakaishia hapo, maana wakati huo tulikuwa tuna jiunga na parade ya shule, yani mstarini.
Wakati parade inaendelea kuna jambo lilitokea, jambo ambalo lilinisimumua, kidogo japo sikutaka kulitilia maanani, maana sisi walimu tulikuwa tumesimama nyuma kabisa ya vikundi vya wanafunzi waliosimama kimadarasa, huku mwalimu wa zamu na mwalimu mkuu walikuwa wamesimama mbele ya parade ile ya shule nzima, mimi na mwalimu Aisha tulikuwa tumesimama nyuma ya kikundi cha kidato cha tatu, sijui nini kilinisukuma kutazama wanafunzi waliojipanga mbele yetu, maana ghafla macho yangu yakakutana na macho ya mwanafunzi wa kike Maimuna, aliekuwa anageuka kutazama nyuma, akatabasamu na kutazama mbele, sikutaka kumtazama tena, lakini sijui macho yana matatizo gani, usichotaka kukitazama yenyewe ndiyo yanacho kitazama, ndivyo ilivyotokea kwangu, maana dakika tano baadae nikajikuta nimesha mtazama tena Maimuna ambae kama kawaida alikuwa ananitazama…. ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom