KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA SITA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: Naam dakika tano baadae yakaingia magari mawili ya deraya, yakiwa yame liweka kati defende la jeshi lenye askari wanne wenye SMG kama wale waliokuwepo pamoja na sisi, “huuuu! Malambo kuna inshu gani huko wete mbona magari yana tisha hivi?” hapo ni kama nilipata nafasi ya kuuliza swali ambalo nilihitaji jibu lake kwa wakati huo Labda nisieleze kwa kirefu, jibu ambalo hata wewe pengine ungependa kusikia, kwa sababu ni nje ya mkasa niliopanga kukusimulia.
Ni kwamba mchana wa siku hiyo huko kaskazini pemba, yaani wete kwenye kitongoji cha Pick kilichomo kilomita chache toka wete mjini, kuna tukio la mauwaji lilitokea………… ENDELEA…..
Ni baada ya wananchi wenye hasira kali na itikadi kali za kisiasa zenye lengo la upinzani kumvamia kijana mmoja askari wa majeshi ya kujenga uchumi ambae ni mgeni, yaani mwenyeji wa kisiwa cha Unguja aliemsindikiza mwenzie kwenda kuwaona wazazi wake huko Pick na kumchinja, ikiwa ni chuki dhidi ya chama Tawala, ukweli ni kwamba ukiachilia sisi ambao tulienda usiku ule pia kuna majeshi wenyeji wa kisiwa kile walienda toka mchana, ikiwa ni jeshi la polisi JKU na KVZ, lakini inasemekana kuwa hawa kufanikiwa kuwa pata wahusika kwa sababu wananchi wote walikuwa wamekimbilia baharini, kwa maana walikuwa wamepanda vyombo vyao vya kienyeji, yaani mitumbwi ambavyo hutumiwa kwa uvuvi na kuelekea ndani ya bahari, huku majumbani wakiwaacha wazee na Watoto.
Tulifika eneo husika saa saba za usiku, nikiwa ndani ya defender njia tulikutana na vikwazo vingi sana, ukiachilia kona za kutisha ambazo ungeziita S mcharazo, pia tulikutana na magogo makubwa ya miti na mawe makubwa yaliyolazwa barabarani kwa lengo la kufunga barabara kuzuia vyombo vya ulinzi na usalama visifike eneo lile kwa uharaka, lakini kwa ustadi kubwa na vifaa vya kisasa wale askari maalumu wa jeshi la ulinzi, waliondoa kila kilichowekwa barabarani na sisi kuendelea na safari huku muda wote nikipapasa na kuhakikisha kama bastora yangu ipo sehemu yake.
Naam kama ilivyo kuwa mchana kwa majeshi mengine yaliyo tangulia, tulifika Pick na kukuta peupe, yaani hakukuwa na vijana wala watu wazima, Zaidi ni wazee vikongwe na Watoto wadogo sana ambao hawajuwi kitu chochote, nikaona wanajeshi wakitumia busara kubwa sana kuongea na wale vikongwe, ambao walisema kuwa vijana wote wamekimbia wakihofia kile walichokifanya, ukweli eneo lile lilikuwa na bendera nyingi za chama Tawala kuliko hata za wapinzani, nikashangaa kusikia eti wafuasi wa chama kikuu cha upinzani wameuwa askari kwa sababu ya chuki za kisiasa, “kwanini wewe hujakimbia, unadhani huwezi kuunganishwa kwenye tukio” kuna wakati nilimuuliza mzee mmoja tuliemkuta nyumbani kwake, ambae hakuonyesha wasi wasi wowote, “kwanini nikimbie wakati aliefanya hayo nina mfahamu, wala sio chuki za siasa, ni vita yake binafsi na familia ya yule kijana” alisema yule mzee kwa sauti yenye lafudhi ya kipemba, hapo nikaona hata kamanda mmoja mwenye cheo cha capten, wa kikundi maalumu tulichokuja nacho akisogea na kuvutiwa na maongezi yangu na yule mzee, “kwanini unamuuza mwana chama mwenzio mzee, au munataka kumtoa sadaka mmoja ili wengine mupone?” nilimuuliza yule mzee ambae uzee wake sio mkubwa sana, “kijana wala sina sababu ya kumtoa sadaka, mimi mwenyewe ni chama Tawala, nadhani hata bendera umeiona hapo nje, huyu bwana Tamimu na kijana wake, wanaugomvi wao na familia ya mzee Omar Haji” alisema yule mzee na kuendelea kueleza kuwa, “familia ya mzee huyu anaemsema na familia ya yule askari ni majirani kabisa, na vijana wao wamekuwa pamoja huku wote wakisoma pamoja, hata wakati walipo fikisha umri wa kujitegemea na yule mwingine kujiunga na jeshi la kujenge uchumi, huyu mwingine alienda kuvua samaki, kwa maana aliamua kuwa mvuvi.
Ugovi ulikuja vipi, kuna wakati ambao bwana Tamimu aliona kuwa kijana wake anahitaji kuoa, hivyo wakaanza pilika za kumfukuzia mschana mmoja binti wa mzee Vuai, mschana mzuri Fatma, ambae alipoelezwa swala lile alishangaa na kushtuka vibaya sana, ndipo alipo mueleza mama yake kuwa hatoweza kuolewa na mtoto wa bwana Tamimu, kwasababu ikiwa ni moja, kwamba kumbe toka siku za nyuma Fatma na kijana wa mzee Omar Haji, yaani yule askari walisha wekeana ahadi ya kufunga ndoa, pale tu kijana huyu atakapo weka mambo yake sawa, na siku za hivi karibuni walikuwa wameshapeana taarifa za kwamba muda wowote wataenda kupeleka barua ya posa, na mbaya Zaidi ni kwamba mtoto wa bwana Tamimu alikuwa anaufahamu urafiki wa Fatma na kijana wa Haji, kitu ambacho Fatma ilimuogopesha na kumuona kijana huyu wa Tamimu ni kama msaliti na mfitinishi mwenye lengo baya juu yake na mpenzi wake.
Kitendo cha kukataliwa posa yao ndicho kilicho mfanya Tamimu na mwanae waanze uchonganishi kati ya wananchi wa wete pale Kijiji cha Pick na kijana wa mzee Haji, wakimshutumu kuwa kijana yule ndie mmoja wa watu wanaopanga mipango ya kuwa nyanyasa kutokana na itikadi yao ya chama pinzani, hata siku waliposikia kijana yule yupo njiani anakuja kuwa tembelea wazazi wake na kumuona mchumba wake na wao wakafanya uchochezi mkubwa sana kwa wananchi wa pale wakisema kuwa kijana yule ametumwa kuja kufanya upelelezi juu ya shughuri zao na mipango yao kuhusu uchaguzi ujao.
Siku ile kijana wa Haji hakuja peke yake, alikuwa ameongozana na askari mwenzie mgeni, yaani mwenyeji wa unguja, waliazima pikipiki moja pendwa sana kule visiwani, yaani Vesper toka kwa askari mwenzao na kuelekea kule Pick, ukweli walienda na kufika salama kabisa pasipo dalili zozote za hujuma dhidi yao, akawaona wazazi wake na baadae mchumba wake akafika pale na kusalimiana nao waliongea mengi sana kabla ya kuaga na kuanza kueleka chake chake, liliko kambi lao.
Naam mara walipo ingia barabara kuu ya lami, ndipo walipoanza kuona dalili za mabadiliko ya tabia ya barabara ambayo walizoea kuwa ni lami isiyo na tatizo, walianza kuona jiwe moja moja na kila waliposogea ndipo waliposhangaa kuona mawe yakizidi kuongezeka barabarani na ile wanashtuka kuwa haikuwa hali ya kawaida tayari wananchi walianza kuibuka toka vichakani na kuanza kuwa sogelea, na wao kujaribu kuongeza mwendo ili kujiokoa na ndipo walipojikuta wana paramia mawe na kuanguka, “kaka acha pikipiki tujaribu kujiokoa, hawa watu nina wajuwa hawata tuacha salama” alisema kijana wa mzee Haji huku anainuka, “kaka siwezi kuacha pikipiki ya watu, nitalipa nini” alisema yule askari mgeni huku anahangaika kuiinua ile vesper kwa anaeifahamu ni pikipiki nzito kweli kweli, huku mwenzie mtoto wa mzee Haji akianza kukimbia kurudi alikotoka akienda kujisalimisha kituo cha polisi akimuacha mwenzie anazungukwa na wananchi wenye hasira kali kama sisimizi kwenye pinje za sukari, “walimnchinja kijana wa watu japo sio mlengwa, na sasa wamekimbilia baharini” alisema yule mzee, “kama ni hivyo basi hiyo ni inshu ya kipolisi, wacha tukawape taarifa ili wafanyie kazi” alisema yule askari wajeshi la ulinzi mwenye cheo cha captain, “mzee hivi hawa wanaoenda huko baharini hawaogopi majini?” nilimuuliza yule mzee ambae alianza kwa kucheka, kabla ya kunipa jibu lililonifanya niache kuendelea kuuliza, “tatizo hadithi na filamu zenu za kisasa zina wafanya muone kuwa jini ni kitu cha mchezo”, Nadhani tuishie hapo kwa mkasa huo wa Pick usiku wa manane, maana ni mrefu sana mbele yake.
Tulifika kambini saa sita za usiku kama Sio saa kumi kasoro, nikaingia ndani ya ile nyumba niliyokuwa naishi yaani Green House, na kujiegesha kitandani huku nawasifu wanajeshi kwa jinsi wanavyoweza kufanya kazi usiku, hasa yule askari Mwasenga, ambae nilimuona amelewa sana lakini aliweza kuendesha gari kwa kasi na kufata zile kona za kustaajabisha za kule pick, huku akiwa amekunywa pombe, sikumbuki ni muda gani nilipitiwa na usingizi ila nakumbuka nilishtuliwa na mlango wa chumba changu uliokuwa unagongwa, nikatega sikio huku nikisikilizia mkojo uliokuwa umenibana kweli kweli, “mh! yupo kweli au alitoka asubuhi?” nilisikia sauti ya kiume ikiuliza niliitambua kuwa ni sauti ya yule koplo wa juzi aliekuja kunionyesha hiki chumba, “kama atakuwepo basi atakuwa anaumwa” hiyo ilikuwa ni sauti ya kike ambayo niliitambua kuwa ni sauti ya mwalimu Aisha iliyojaa lafudhi ya kipemba, ambayo ilikuwa imenyongea kwa kiasi fulani, nikachukuwa simu yangu mezani na kuitazama kwa lengo la kuangalia muda, “mungu wangu saa nne” nilisema kwa sauti ya chini huku najiinua toka kitandani na kama ujuwavyo kitanda cha chuma, kikapiga kelele, “huyooo anaamka, alikuwa amelala sana” alikuwa sauti ya mwalimu Aisha iliyochangamka kwa furaha.
Nikiwa na bukta yangu huku dudu yangu ikiwa imesimama kweli kweli na kuinua bukta niliyoivaa, nadhani ni kwaajili ya mkojo, maana sikuwa na uhaba sana wa vitumbua, nikaufwata mlango na kuufungua, macho yangu yakawatumbulia watu wawili waliosimama mbele ya mlango wa chumba changu, yaani yule koplo alienipokea siku ya kwanza na mwalimu Aisha ambae alikuwa amevalia gauni refu jeusi, maarufu kama baibui huku kicwhani akijitanda kwa hijab ya blue, akiziba kuazia nywele mpaka masikio yake na kubakiza uso pekee, uso ambao ulikuwa katika tabasamu pana lililoashiria furaha ya matumaini, tabasamu ambalo liliyeyuka ghafla na kuwa katika mshangao mara baada ya kutazama kifua changu, na baadae macho yake yenye kiherehere kushuka chini na kutazama usawa wa mbele wa bukta yangu, “unapenda kulala weye mpaka unasahau kazi” alisema Aisha huku anakwepesha macho yake na kutazama pembeni kidogo, “hooo! jana nilipatwa na dharula kidogo nikachelewa kulala…karibu ndani…. karibu pita ndani” nilisema huku natoka nje ya chumba nikipishana na wawili wale waliosimama kwenye korido karibu na mlango wa chumba changu....…ENDELEA…….
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA SABA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: uso ambao ulikuwa katika tabasamu pana lililoashiria furaha ya matumaini, tabasamu ambalo liliyeyuka ghafla na kuwa katika mshangao mara baada ya kutazama kifua changu, na baadae macho yake yenye kiherehere kushuka chini na kutazama usawa wa mbele wa bukta yangu, “unapenda kulala weye mpaka unasahau kazi” alisema Aisha huku anakwepesha macho yake na kutazama pembeni kidogo, “hooo! jana nilipatwa na dharula kidogo nikachelewa kulala…karibu ndani…. karibu pita ndani” nilisema huku natoka nje ya chumba nikipishana na wawili wale waliosimama kwenye korido karibu na mlango wa chumba changu....…ENDELEA…….
Na mimi kuelekea bafuni maana mkojo ulikuwa umenibana kweli kweli, “sasa mwalimu nadhani mwenyeji wako umempata” nilimsikia yule askari Koplo, akisema huku vikifuatia vishindo vya buti zake za jeshi zikitokomea kuelekea nje ikiashiria anaondoka, hakika njaa ilikuwa inanichamanda kweli kweli.
Nilichukuwa dakika nzima kule bafuni nikimwaga kojo, kisha nikatoka na kukuta Aisha hakuwepo mahali pale, nikaingia chumbani sikumuona, nikachungulia dirishani nikamuona amesimama nje ya nyumba ile, nikatabasamu na kuanza kujiandaa kwa kupiga mswaki na kuoga haraka haraka nikitumia dakika kumi na tano mpaka kutoka nje kuunga na Aisha ambae bado alikuwa anisubiri, pole kwa kukukalisha nje” nilimuambia mwalimu Aisha ambae aliishia kucheka baada ya kujibu pole yangu, alionekana mwenye aibu fulani, tulitembea taratibu kuelekea upande wa shuleni, ambako kuna mgahawa ule tulio kula jana asubuhi.
Kimya kilitawala kati yetu, sijui Aisha alikuwa anawaza nini, ila mimi nilikuwa najaribu kumtathmini jinsi alivyo, ni kama nilivyoeleza alikuwa mzuri wa sura na umbo lake potable, japo sio aina ya wanawake ambao nina wapenda sana, kwa juu hakuwa na shida kwangu, ila kuanzia kiunoni huwa napenda wale wenye sehemu kubwa za kukalia, “ushaoga eehn?” aliuliza Aisha, kwa sauti ya uchangamfu, lakini yenye aibu kidogo wakati tukiwa tumesha fika mgahawani, na mimi kuagiza supu ya kuku wa kienyeji yenye pili pili nyingi sana, “yah! vipi nimetumia muda mrefu” hapana ila tumechelewa si unaona hapana mtu yoyote anaekunywa chai saa hizi?” alisema Aisha, ambae kwenye maelezo yake alipoona sijaenda shule bila taarifa yoyote akaona ni bora anifuate kuja kunijulia hali, akaulizia na kuletwa pale kwenye makazi yangu, “lakini umekataa kuingia ndani kwangu” nilimueleza Aisha japo nilijuwa kuwa kutokana na mila za watu wa kisiwa hiki asingeweza kuingia chumbani kwangu, “mh! kwa hali niliyoiona kama mpaka sasa ningekuwa nimetoka basi nisinge kuwa salama, vinginevyo ningekuwa bado na shughulikiwa” alisema Aisha kwa sauti ya utani iliyojaa aibu, tukacheka kwa pamoja, “kumbe ndio maana ulikataa kuingia ndani, nani alikuambia ningefanya hivyo?” nilimuuliza Aisha huku tukiendelea kucheka na kupata supu, “mh! vijana wa bara wala hamna subira, munataka yenu yatimie siku hiyo hiyo, ndio ufanye uoe bwana” alisema Aisha na tukaendelea kula huku tukiongea hili nalile.
Kama ilivyo kuwa jana nilikuwa karibu na Aisha mpaka mida ya jioni huku nikimsimulia mambo ya jana usiku, maana aliomba nifanye hivyo, “unaranda usiku weye huogopi majini” alitania Aisha kwa lafudhi yake ya kipemba, akiona kuwa mimi ni muoga sana wa majini "ningelipata moja ningeenda nalo Dar” na mimi nikatania, “na kwahali niliyo kukuta nayo utalivagaa tu” alitania Aisha, ambae tuliagana saa nane alipopanda gari kuelekea mjini nyumbani kwake.
Ukweli niliona mazoea ya Aisha yanazidi sana kiasi cha kuanza kunipa matamanio ya kucheza na kitumbua chake, lakini nikakemea pepo na kuliomba liwe na subira, “ila akiendelea kujilengesha nitafanya kweli” huo ndio ulikuwa mpango wangu. ***
Naam adhana ya saa tisa alaasiri ilinikutia nikiwa mjini nashuka kwenye daladala chai maharage, eneo la chake Hotel ambapo pana njia panda ya barabara iendayo madungu yaani ile ya kwenda kaskazini Pemba na ile barabara iendayo ndani ya mitaa ya mji huu wa chake chake, yaani madukani na sehemu zote zenye huduma za kijamii kama vile sokoni madukani msikitini na Hospital na kwenye maofisi mbali mbali ya kiserikali na binafsi, ni ile barabara ambayo niliipita siku ile ya kwanza kuingia pemba mpaka nikamuona yule mwanamke ambae niliamini kuwa ni jini, japo leo watu walikuwa ni wengi kiasi, ambao walionekana kama vile wanafunga maduka yao tayari kwenda kuswali, na pengine wasinge rudi tena kwenye biashara zao mpaka siku inayofuata, hapo ndipo nilipopata jibu la kwanini jana sikukuta watu hapa mjini.
Naam nikiwa nimevaa nguo za kimichezo yaani track suit ya chini raba na tishert, huku nikiwa nimebeba kibegi changu kidogo cha mgongoni ambacho nilikuwa nimeweka simu,kisu,camera, bastora na mkebe wa akiba wenye risasi kumi, pia nilikuwa na wallet yangu yenye fedha kidogo na kitambulisho chenye kibari cha matumizi binafs ya silaha niliyonayo na tauro dogo la kujifutia jasho, na lengo langu likiwa ni kuelekea kwenye uwanja wa baskeball kama nilivyoelekezwa na yule askari dereva, yaani Mwasenga, nilianza kutembea taratibu kuelekea ndani ya mitaa, sikuwa na wasi wasi kwa sababu nilikuwa napishana na watu waliokuwa wanatoka eneo la mjini na wengine waliokuwa wanaelekea kweye msikiti mkuu wa hapa chake chake, wengi walikuwa ni wanaume waliovaa mavazi ya kawaida tu ambayo haya kuwa na manjonjo ya kawaida kama vile wapo majumbani mwao au ni maeneo ya karibu na majumbani mwao, na kama ilivyo kawaida chini walivalia sendo au kama vile tunavyoweza kuita makubazi.
Nilifika eneo la hospital kwa kufuata maelekezo ya mwasenga na hapo nikalivuka lango la hospital nikifuata barabara ile ya lami iliyokatiza kati kati ya kuta mbili kubwa, moja ikiwa ni ya jengo la serikali na upande wa kushoto ukiwa ni uzio wa hospital ya chake chake uliounga nishwa na uzio wa majengo ya makazi ya watumishi wa serikali, na nilipomaliza ukuta wa upande wa kulia nikauona uwanja wa baskert ukiwa mbele yangu upande wa kulia pembeni mwa ofisi nyingine ndogo ya serikali na kijengo kidogo cha choo pembeni yake, ikiwa ni upande wa gori la kaskazini huku upande wa kusini yaani kushoto kwangu likiwa ni uzio wa makazi ya wafanyakazi wa serikali na famlia zao, niligundua hilo baada ya kuchungulia ndani ya uzio huo kupitia gate kubwa lililofunguliwa nusu na kuona nguo zilizo anikwa zikiwa ni za jinsia tofauti na rika mbali mbali, huku baadhi ya watu wakitembea tembea mule ndani.
Ukweli uwanja niliupata lakini hakukuwa na watu wala mpira, sikushangaa sana maana ni kweli niliwahi sana, maana nilipotazama muda ilikuwa ni saa kumi kasoro, sikujilaumu kuwahi kwangu, kwa sababu kwa uzoefu wangu mazoezi mengi ya baskert huanza saa kumi na nusu au saa kumi na moja kasoro maana nisingeweza kukaa mpaka mwisho wa mazoezi kwa nilivyodhania ni kwamba lazima yangeisha saa moja kasoro za jioni, hivyo nisingeweza kutembea peke yangu mpaka wawi kwenye ile mess ya kijeshi wala nisingeweza kupata usafiri wa kufika huko, na ukichukulia kuna kamsitu fulani toka chake pale driving school mpaka macho manne kwenye njia panda ya kwenda wawi mpaka vitongoji, hapo nikaweka pembeni lile begi langu dogo kisha nikaanza mazoezi ya kukimbia ndani ya uwanja ule kwa kufuata mistari ya alama za uwanja, nikianza kwenye robo ya key.
Siku maliza hata mzunguko wa kwanza nikashtuliwa na kijana mdogo aliekuwa anatokea kwenye gate la uzio wa nyumba za serikali, “assalam alaykum” alisalimia yule kijana wa kiume ambae umri wake ulikuwa unafikia miaka kumi au kumi na moja, “walaykum salaam” niliitikia huku naendelea kukimbia, “wewe ni mgeni hapa?” aliuilza yule mvulana mdogo ambae alienda na kukaa pembeni ya uwanja” sikuwa na haja ya kukwepa kujibu swali la mvulana huyu au kumdanganya, japo nilishangaa kuhusu swali lile, “yah! ni mgeni hapa, lakini umejuwaje kama mimi ni mgeni au unawafahamu wote wanaofanya mazoezi hapa?” nilimuuliza huku na mimi nikiendelea kukimbia yaani nenda rudi nenda rudi, “ndiyo nawafahamu wote, si nakaa hapo” alisema yule dogo huku akionyesha kwenye nyumba zile nyumba zilizopo ndani ya uzio, “licha ya jibu hilo pia niligundua kuwa vijana wanao cheza baskert ni wachache na wote hucheza uwanja ule ambao ndio ulikuwa pekee unaotumika pale mjini chake chake, “ngoja nikakuangalizie mpira” alisema yule kijana mdogo na kuinuka kuelekea ndani ya uzio ule wa nyumba za serikali, labda nikuambie msomaji kwanini nilibaini mapema kuwa jengo lile ni la watumishi wa serikali, ni kwa sababu nyumba zile zilikuwa ni zaghorofa tatu zilizo kuwa zimekaa kwa mtindo wa kufanana, mimi niliendelea kukimbia kupasha mwili joto na kutafuta pumzi.
Nilikimbia kwa muda wa dakika kumi au Zaidi, kijasho kilinitoka siku hisi kuchoka kwasababu nilikuwa vizuri kwenye mazoezi na nikiwa nimeshazama kwenye mazoezi nilishtuliwa na sauti nyingine, safari hii ikiwa ni ya kike, “asalam alaykum” nikiwa bado katika mwendo nikatazama kule sauti ilikotokea ambako ni upande ule ule wa jengo la watumishi wa serikali, nikamuona mschana nzuri mdogo wa umri kama wa miaka kati ya kumi na saba au kumi nane, akiwa amesimama karibu na gori la upande wa kusini, alievalia gauni refu lenye mauwa mauwa, lilimpendeza kutokana na umbo lake, japo hakuwa na yale ya kukalia makubwa, akiwa ameshika mpira wa baskert, “walaykum salaam” niliitikia huku nikimsogelea mschana yule ambae toka nimefika huku ni mara ya kwanza kumuona mschana alieachia kichwa wazi kwa mtaani Zaidi ya kule mess, “nimekuletea mpira, Yasin anasema unauhitaji” alisema yule mschana mwenye nywele ndefu nyeusi alielaza mtandio wake mabegani, mwenye sauti ya kischana yenye lafudhi ya kipemba, ”hooo asante sana, yeye mwenyewe yupo wapi?” niliuliza huku napokea mpira toka kwa mschana yule huku pua zangu zikikutana na harufu nzuri ya marashi ya udi, ambayo yalinikumbusha hadithi fulani za majini, yaliyonifanya nimtazame usoni mschana huyu mdogo ambae kikawaida nilimzidi miaka kama sita au saba, ambae nilijikuta nikikodoleana nae macho kwa sababu na yeye alikuwa ananitazama kwa macho ya udadisi, alikuwa na macho makubwa na mazuri, “anaswali ndani” nikamuona anakwepesha macho yake wakati anajibu swali langu, hapo nilitegemea kuwa ange geuka na kurudi ndani mwao, lakini jambo la ajabu nikaona nae anaenda kukaa pale alipokuwa amekaa Yassni, ambae baadae niligunduwa kuwa ni mdogo wake, “hooo! kumbe na yeye anajuwa kuswali?” niliuliza huku naweka mpira chini na kuanza tena kukimbia, “he! kwanini, au wamuona mdogo eeh!?” aliuliza yule mschana kwa sauti iliyochangamka huku anaendelea kuni tazama, hapo nikakumbuka kuwa niliuliza swali la kibwege “hapana sio mdogo, ila napenda watu wanao swali” nilizuga huku naendelea kufanya mazoezi, “basi sie sote huwa tuna swali, hata mimi nimeshaswali” alisema yule mschana ambae muda wote alikuwa anaendelea kunitazama, “hivi unaitwa nani vile?” aliuliza yule mwanamke, ambae sikuona umuhimu wa kumueleza ukweli, “naitwa Pross na fanya kazi Zasco (shirika la umeme la Zanzibar) wewe je?” niliuliza baada ya kujitambulisha huku naendelea kukimbia, kwanza nikamuona yule mschana akitabasamu, “naitwa Maimuna” alijitambulisha yule mschana pasipo kusema anachofanya kwa wakati ule japo kwa umri wake alipaswa kuwa mwanafunzi kati ya kidato cha tatu au cha nne.
Niliendelea na mazoezi kwa muda wa nusu saa nyingine huku yule mschana Maimuna akiendelea kunisemesha kwa maswali ya hapa na pale mpaka wachezaji wengine walipofika nikaungana nao na kuanza mazoezi ya pamoja, ni yale madogo madogo kisha tukajigawa na kuanza kucheza mpira huku nikijitambulisha kwa jina lile lile la Pross, ambalo nilikuwa nimejitambulisha kwa yule mschana, ambae hakukaa sana akaondoka zake na kuelekea ndani ya nyumba yao.
Nilishiriki mazoezi pamoja na wale vijana wa chake chake ambao niligundua kuwa hawapendi kujituma katika mazoezi, japo walikuwa na uwezo mzuri katika mchezo ule wa baskert ball lakini hawa kuweza kuugusa wala kuufikia uwezo wangu, japo kuwa nilikuwa nimesimama mazoezi kwa muda mrefu kidogo.
Hakika siku ile niliweza kupata marafiki wengi, kila mmoja alihitaji kunifahamu na kujuwa endapo niliwahi kucheza kwenye timu kubwa za mpira ule wa kikapu, lakini ukweli sikuweza kuwapatia utambulisho wangu wa ukweli, ni moja ya taratibu za kazi yangu ya upelelezi, japo kule shuleni Fidel castor, nilijisajili kwa jina la kweli kabisa yani Eric Frank, kiukweli kitu ambacho nilibarikiwa ni nyota ya kuelewana na watu, nadhani toka umeanza kusoma au kusikiliza mkasa huu umeweza kuona jinsi nilivyoweza kuzoeana na watu kwa haraka…naam mkasa bado upo mwanzoni kabisa, unadhani ule ndio ulikuwa mwisho wa Eric kukutana na yule mwanamke jinni?, basi endelea kufwatilia mkasa huu hapa hapa JamiiForums