Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU : Naam nikiwa nime bakiza mita kama kumi au ishirini kulifikia lile duka lililokuwa barabarani ghafla nikamuona yule dada akiibuka toka kwenye chochoro moja ya upande wa kushoto ukweli nilitamani kukimbia au kupiga kelele, lakini nikamuona akigeuka na kutazama upande ninao tokea mimi huku sura yake ikiwa katika hali fulani ya tabasamu ………. ENDELEA…….
Kisha akatazama mbele huku anatembea taratibu kuelekea upande wa barabara kuu, hapo mimi nikapunguza mwendo na kuendelea kumtazama yule dada ambae mwendo wake ungesema yupo kwenye jukwaa la walimbwende, huku nikiweza kuona jinsi alivyo jaaliwa katika umbo lake, hasa upande wa mgongoni.
Naam nilimuona yule mschana mzuri sana ambae hata kama ni jini lakini unaweza kujikuta una ingia mkenge, anachepuka nakuingia kwenye lile duka ambalo wakati napita nikatambua kuwa ni duka la vifaa vya watoto kutokana na vitu vilivyo kuwepo pale nje na ndani, ambako pia niweza kumuona yule dada akiongea na muuzaji wa kiume, nilitamani nimueleze yule jamaa kuwa anaongea na jini lakini nikahofia pengine na yeye anaweza kuwa ni jini, maana licha ya kuwa duka kubwa sana kama super market lakini hakukuwa na mteja yoyote zaidi ya wao wawili, na hakuwa na sababu ya kulifungua mida ile, kwa sababu mji mzima haukuwa na watu sasa anamuuzia nani.
Nikaamua nijikaushe na kuendelea na safari yangu, lakini macho yangu yenye kiherehere yakajikuta yametazama tena kule dukani, hapo nilikutana na macho mazuri ya duara ya huyu dada, ambae sikujuwa alikuwa anaongea nini wakati ule maana niliweza kuona tabasamu pana sana usoni kwake, japo alikuwa amegeuka kunitazama, nikatazama mbele haraka na kuongeza mwendo haraka kuingia barabarani, kisha nikaanza kuifuata barabara ya kuelekea macho manne kule ambako nilikotokea wakati nakuja, na bahati ilikuwa upande wangu maana sikutembea sana nilienda kama mita mia mbili hivi nikasikia ngurumo ya gari nyuma yangu, kucheki nyuma lilikuwa ni lile gari la jeshi ambalo lilikuwa limeenda airport, nikashukuru sana kwa kuonekana kwa gari hilo, maana nilikuwa na hofu kubwa ya kutokewa tena na yule jini mrembo, “vipi umeona eeh?, mida hii chake hakuna mtu” aliniuliza dereva wa gari lile la jeshi aina ya land rover defender, huku tunaanza kuondoka kuelekea upande wa kaskazin yaani wete, “mh! natamani nirudi dar es salaam hata leo” hilo lilikuwa ndilo jibu langu, ambalo yule dereva alilichukulia juu juu kwa sababu niliwahi kusikia kuwa kila alie kujapemba kikazi lazima aliwahi kutamka neno hilo “utazowea tu, ukianza kwenda mess pale pana changamka sana, hasa siku za weekend” sikumjibu yule jamaa zaidi nilizatama upande wa kushoto wa barabara ambako kulikuwa na njia panda, barabara kubwa kabisa ya lami ilikuwa inaelekea upande huo wenye majengo pia, ambako licha ya safu ya maduka na ofisi zilizo fungwa pia kulikuwa na jengo kubwa la kanisa, na kingine kwenye barabara hiyo kwa mara nyingine niliweza kumuona kijana mmoja wakiume akija upande wa barabara akiwa juu ya pikipiki fulani ambazo kwa watu wa pemba wanaziita Vesper, alikuwa analitazama kwa umakini sana lile gari letu kwa umakini mkubwa, “ila bro unaonekana kuwa umeichukia sana pemba, maana umekosa amani ghafla” alisema yule dereva wa defender ambae ni askari wa jeshi la ulinzi, na mimi nikiwa naendelea kumtazama yule kijana ambae ni mtu mweusi asie na mchanganyiko wowote, yaani yupo kama sisi wengine, “hapana nadhani ni kwaajili ya ugeni tu kama ulivyosema” nilijibu kwa sauti flani ya kujaribu kujichangamsha, huku natazama mbele tulipokuwa tunaenda tukiwa tumeshapita ile njia panda ambayo baadae niliifahamu kuwa inaelekea Wesha, lakini ukweli nikwamba bado nilikuwa na hofu kubwa sana juu ya yule mwanamke ambae alikuwa ana nifuatilia, ambae mimi niliamini kuwa ni jini, nasema niliamini kwa sababu sikuwa nimethibitisha kama ni jinni au binadamu wa kawaida.***
Nilipitia pale mess kama nilivyoambiwa kuwa ndiyo sehemu ambayo nitapata chakula cha jioni, ukweli mpaka inafika saa mbili na robo za usiku namaliza kula sikuona dalili ya kuchangamka kwa mahali hapa, japo palikuwa na mandhari fulani ya kupendeza na watu wachache waliokuwa wanakunywa bia, huku wengine wakiwa wamekaa na wanawake ambao mavazi yao kiukweli usinge amini kama upo pemba, mavazi ambayo toka nimeingia hapa pemba leo asubuhi siku yaona mahali hapa, na wavaaji wa mavazi hayo walionekana wazi kuwa ni wenyeji wa kisiwa hiki, japo baadhi yao walikuwa sio machotara, japo wapo waliovalia magauni ya kawaida na miushungi vichwani mwao, lakini pia wengine walivaa kama ni gauni basi hawakufunika nywele na zaidi ya hapo basi walivalia tishet na jinsi, nilijiuliza wametokaje kwao na nguo zile sikupata jibu, ila hapo baadae tutajuwa wanatokaje, lakini zaidi ya hapo sikuona kitu ambacho kitanifanya nijisikie vizuri kukaa huku pemba, ukizingatia nilisha ona dalili ya kufuatiliwa na jini.***
Licha ya kwamba story zilikuwa nyingi sana mule ndani, wale maafisa wa jeshi akiwepo na yule afisa utawala, hapo nikajuwa kuwa askari huwa wanafanana akili zao, maana wote walikuwa wakisimulia matuko mbali mbali ya wanawake wao, ambao wengi wao walikuwa wanatokea Tanga, walisimuliana jinsi wanavyo starehe na kupeana vitumbua na waschana hao, lakini mimi siku zifuatilia sana bado nilikuwa nimepoa nawaza kilicho nitokea, bado sikujuwa kama yule ni mtu au jinni, hivyo sikuhitaji kukaa sana pale messi, nilipomaliza kula nikamueleza yule afisa utawala yaani Luteni Simon Malambo, kuwa sitokaa sana pale messi ambapo maafisa wengi yaani wale wenye nyota walikuwa wanalala pale pale, nae akaangiza gari moja linirudishe kambini, yaani kule al khamis camp, yaani vitongoji.
Naam wakati tuna jiandaa kuingia kwenye gari, yaani mimi na yule dereva wa gari la jeshi, ambae ni askari mwenye umri kama wangu, ambae hakuwa na alama yoyote mabegani mwake, ila walimuita private kama cheo chake, mara likaingia Range Rover moja rangi ya silver linang’aa kwa upya wake, ambalo lilikuja na kusimama pembeni yetu, yaani pembeni ya gari letu la jeshi la ulinzi lile land Rover defender, ilichukuwa kama dakika mbili hivi mpaka mlango wa gari kufunguliwa, na ilifunguka yote miwili ya mbele yaani wa dereva na wa abiria, ukweli mimi ni mmoja wawatu ambao walitamani kuwaona watu waliokuwa wanashuka toka kwenye lile gari la kifahari.
Naam hapo nilimuona mwana dada mmoja mzuri sana japo hakuwa chotara, lakini uzuri wake ulionekana wazi kabisa, mschana ambae alikuwa amevalia gauni la kawaida na mtandio kaulaza mabegani, akiachia nywele zake nyeusi na ndefu zionekane kwa uwazi kabisa, na wakati na shangaa yule mwanamke nikakumbuka kuwa hajaja peke yake, nikatazama upande wa mlango wa dereva hapo nikashtuka kidogo, maana nilikutana macho kwa macho na kijana yule ambae nilimuona masaa machache yaliyopita anatokea barabara ya kanisani, yaani ile ya wesha, ni yule alikuwa anaendesha pikipiki aina ya Vesper, na kilicho nishangaza na kunishtua ni kwamba kijana huyu ambae hakuwa na chembe ya uchotara mchana alikuwa na Vesper na sasa ana range rover, tena ya kifahari ambayo ingenunuliwa kwa fedha nyingi sana, hakika niliona ajabu sana, lakini sikupenda kuliweka lile kichwani kwa sababu huwa sipendi kuumiza kichwa kwa mambo ya mtu mwingine, ila kwa muonekano huyu kijana ambae kiumri anaonekana kunizidi kidogo sana, kama sio yeye basi nyumbani kwao wana uwezo mkubwa kifedha, japo uvaaji wake ulikuwa ni wa kawaida tu, hiyo ni kwa jinsi mimi nilivyoona, “asalam alaykum” alisalimia yule jamaa aliekuwa anamtazama yule dereva niliekuwa nae, huku ana geuza uso wake kuni tazama, hapo nikamuona akishtuka kidogo, “waalaykum salaam, niaje Usi” aliitikia yule dereva mwanajeshi, akionyesha kumfahamu yule jamaa ambae na mimi nililifahamu jina lake kuwa ni Usi, “poa dogo naona leo mapema unasepa zako” alisema yule jamaa yaani Ussi kwa lafudhi ya kipemba, “hapana bwana, nampeleka huyu mshkaji halafu na geuka sasa hivi” alisema yule dereva ambae mpaka dakika hiyo sikuwa na mfahamu jina, “ok! kumbe naye ni kamanda” alisema Usi, huku ananitazama akionyesha kuwa ni kama alinikumbuka kama mimi nilivyomkumbuka, “hapana huyu ni mwalimu wa computer pale fidel castor” alisema yule dereva, huku nikisoma jambo jingine kwa huyu jamaa anaeitwa Usi, kiukweli tokea alipoingia hapa alikuwa ananitazama kwa macho fulani hivi, ambayo nilishindwa kuyaelewa ni macho ya nini, kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kukutana nae na nilikuwa na uhakika kuwa hanifahamu, “ok! karibu pemba kaka” alisema yule jamaa, huku anafunga mlango wa gari lake kisha akaingia kwenye gari na kumshika mkono yule mwanamke wake halafu wakaelekea mlangoni tayari kuingia ndani ya ukumbi ule wa messi, huku na sisi tukianza safari ya kueleka kambini kule vitongoji.***
Ukweli nilizidi kuchanganyikiwa kwa jinsi mambo yalivyo kuwa yanaenda, hasa juu ya yule mwanamke ambae ukiachilia uzuri wake ila lile tukio la kunifuatilia halafu akatoweka na kuibukia mbele yangu liliniogopesha sana, ukichukulia ni siku yangu ya kwanza tu ndani ya pemba, usiku kucha niliwaza juu ya jambo hilo, likininyima raha na aman, niliona naelekea kupoteza maisha, hakika nilitamani siku ya pili nidondoke zangu kurudi Dar es salaam, lakini ninge waeleza nini kule makao makuu, ukizingatia waliniamini na kunifanyia maandalizi makubwa na kunipatia fedha nyingi sana kwaaji ya safari hii.
Siku ya pili asubuhi niliamka mapema na kueleka shuleni ambako nilikutana na mwalimu mkuu, ambae alinielekeza kwenye ofisi ya walimu wenzangu, yaani staff ofisi, ambako nilikutana na walimu wengi sana wakike kwa wakiume, ambao kiukweli uvaaji wao ulikuwa tofauti na mimi ambae nilikuwa nimevalia tishert na jinsi na chini nilivalia raba, ndiyo vazi ambalo nalipenda sana, “asalamu alaykum” nilisalimia mara baada ya kuongia ofisini, walimu wenzangu wakaitikia kwa pamoja na hapo mwalimu mmoja wakike akanionyesha sehemu ya kukaa, yaani meza na kiti, na mimi nikaweka vitabu na makablasha juu ya meza ile ambayo ilikuwa karibu na meza ya mwalimu mmoja wa kike, ambae licha ya kuwa na kiuchotara kwa mbali lakini kiukweli alikuwa ni mzuri haswaaaa, na kwa kuzingatia aliyo niambia mwalimu mkuu nikajifanya kumpotezea, “naitwa mwalimu Aisha, karibu sana pemba” aliniambia yule mwalimu wakike kwa sauti yake nyororo yenye lafudhi ya kipemba, huku ananipa mkono, kama salam na mimi nikampa mkono, “asante sana, mimi naitwa mwalim…” kabla sijamalizia akamalizia yeye, “mwalimu Eric, tulipata habari zako toka jana, lakini ukaondoka bila kuja kutusalimia” alisema Aisha, huku mimi nikisilizia joto la kiganja chake cha mkono, ambao haukudumu sana kwenye mkono wangu tukaachana, “ni kweli maana niliwahi kupumzika, si unajuwa usafiri wa huku kwenu, nilikesha kwenye meli usiku kucha” nilisema huku najitahidi kumtazama usoni mschana huyu, ambae kiumri ni kama nilimzidi kwa miaka kati ya miwili au mitatu, “kwanini hukupanda express na ukapanda meli kubwa?” aliuliza Aisha na kuni ng’amua kuwa kuna meli za express, “sikujuwa kama kuna meli za hivyo, zinatumia muda gani kutoka dar es salaam?” niliuliza kwa mshangao ikionyesha wazi kuwa sikuwa najuwa.
Tuliongea mengi na Aisha, ambae hakuwa na kipindi asubuhi ile, alinieleza kuhusu ratiba boti ya express, ambayo ilikuwa inakuja pemba jumanne ijumaa na jumapili, wakti mwingine jumamoss, kwa gharama ya tsh elfu thelathini na tano, na hutumia masaa matano mpaka sita, “dah! kumbe nilibugi, au kwa sababu nilikata tiketi jumatatu” nilisema kwa sauti ya kujilaumu, maana licha ya kukata tiketi jumatatu nilisafiri jumanne siku ambayo kulikuwa na bot ya express.
Tuliendelea kuongea na kuzoeana kwa muda mfupi, hata mida ya chai yaani saa nne, ilinilazimu kuacha kwenda kule kambini baadae yake tulienda pamoja na aisha kwenye mgahawa ambao walimu wenzangu walikuwa wanaenda kununua chai kwa asubuhi na chakula cha mchana, ukweli siku kifurahia kwa siku ile ya kwanza, maana hakukuwa na kitafunwa kingine zaidi ya mikate midogo iliyouzwa shilingi mia mia, ikifahamika kwa jina la boflo, nililazimika kunywa chai ile na mimi ndie nilielipia, huku nikiendelea kuongea na Aisha ambae muda mwingi alikuwa ananitazama kwa macho ya udadisi, “Eric hivi umesha oa weye” aliniuliza Aisha, huku anacheka cheka wakati tunarudi ofisini, “bado sijaoa vipi wewe umesha olewa” nilimwuliza Aisha, ambae pia alitabasamu kabla ya kunijibu, “niliwahi kuolewa, lakini niliachika mume wangu hakutaka nikasome” alisema Aisha, hapo nikatulia kidogo kutafakari aina ya mwanaume wa Aisha, “basi kama hujaoa utapata mke huku pemba kuna waschana wazuri tu” alisema Aisha, ikiwa ni mtu wapili ananieleza jambo hilo, “mh! pemba siwezi kuoa, nitajuwaje kama huyu ni mtu na huyu ni jini?” nilisema kwa namna fulani ya kushtuka kiasi cha kumshangaza hata Aisha, ambae aliangua kicheko kiasi cha wanafunzi wa kidato cha tatu kuchungulia dirishani, “nani kakuambia pemba kuna majini kiasi hicho?” aliuliza Aisha, huku akiendelea kucheka, hapo nikatulia kidogo na kuongeza umakini katika maongezi yale, maana nilisha ona kuwa sitakiwi kukurupuka ila nahitaji kupata habari fulani toka kwa Aisha, hasa zihusuzo majini, “unataka kuniambia kuwa pemba hakuna majini?” nilimuuliza Aisha ambae alikuwa anamalizia kucheka.
Hapo tuka simama kabisa nje ya ofisi yetu, “hizo ni habari tu, mi mwenyewe toka nimezaliwa mpaka sasa nafikia miaka 22 sijamuona jini wala binamu yake jini” alisema Aisha, ambae niliona ni mtu anaejaribu kunitoa wasi wasi, maana jana nilimuona mtu ambae niliamini kuwa ni jini kabisa, “hapana Aisha inamaa hujawahi hata kusikia kuhusu majini?” nilimuuliza tena Aisha, ambae alitazama saa yake ya mkononi kisha akajibu, “kutokana na vitabu vya dini majini yapo na yaliumbwa kabla ya binadamu wa kwanza, majini wapo sehemu zote duniani na wao ni kama sisi, wapo wakorofi na wapo wapole, hawawezi kumfuata mtu bila sababu za msingi, japo kwa elimu nyingine ni kwamba wapo majini wabaya ambao hutumiwa na watu kwenda kutenda uovu” alinieleza Aisha, ambae mara kwa mara alikuwa anatazama Saa yake, “kwahiyo unataka kuniambia kuwa jini kama jini hawezi kukuona njiani na kuanza kukufuata?” nilimuuliza Aisha, nikihitaji uhakika wa kile nilicho kiona jana kule chake chake mjini, “inawezekana Jini akakufuata, ni kutokana na sababu pengine una janaba halafu umepita sehemu ambayo kuna hao majini” alinijbu Aisha, “kwahiyo jini hawezi kukupenda tu na kuamua kukufuata uwe mpenzi wake” nilimuuliza Aisha, ambae alianza kwa kutabasamu, “nasikia kuwa inatokeaga mara chache, jini kutokea kumpenda binadamu, lakini sijawahi kusikia kwa ukaribu swala hilo, nacho fahamu mimi binadamu mwenyewe kumpenda jini pasipo kujuwa na jini kumkubali kwa lengo la kumuadhibu, lakini pia kuna habari za jini la kike ambalo mwenzi mmoja uliopita limetoka kuuwa mtu kule madungu guest house habari za jini hilo nilianza kulisikia toka tunasoma shule ya msingi pale Msingini Primary, lilishawahi kuuwa wavulana wanne, hilo ndilo ambalo naweza kusema kuwa ndilo jini ambalo la kwanza kusikia habari zake, lakini sio kuliona kwa macho” hilo lilikuwa jibu la Aisha ambae aliniaga kuwa anatakiwa kuingia darasani, maana muda wa kipindi chake umesha fika, japo majibu yake ya mwanzo yalianza kunitoa wasi wasi, lakini hili la mwisho lilinirudisha kwenye wasi wasi na uoga mkubwa, usiniulize naogopaje wakati nina bastora, jini huwa hafi kwa risasi.***
Saa nane na nusu ndio muda ambao kengere ya wanafunzi kutoka darasani ilisikika, ndio muda ambao mwalimu Aisha alitoka darasani, niliagana nae na kuahidiana kuwa tutakutana kesho siku ya alhamisi, mwalimu Aisha alipanda kwenye basi la shule ambalo kikawaida hupandwa na walimu na wafanyakazi wa shule tu na sio wanafunzi, ambao niliwaona wakipita mbele ya ile nyumba ninayoishi, yaani nyumba ya kijani na mimi nikiwa nimekaa kwenye ngazi nje ya nyumba ile kabla sijaingia ndani kwa lengo la kutafakari yale niliyoelekezwa na Aisha, ambae aliahidi kuwa weekend atanipeleka mjini kwenye maduka ya watu anao wafahamu ambao wataniuzia vitu kwa bei ya chini kidogo, .
Niliweza kuwaona wanafunzi wakiendelea kupita barabarani, barabara iliyopo mita kama ishirini tu toka kwenye nyumba ile ya kijani, huku wanafunzi wakike wakionekana kunitazama sana kiasi cha kunifanya niingie ndani kukwepa macho ya waschana wale ambao kiukweli macho yao haya kuwa ya kawaida, yalijaa hali fulani ya kuhitaji na mimi niwatazame.**
Jioni ya siku ile nilipelekwa kule mess kupata chakula cha jioni dereva wa siku ile hakuwa yule wa jana, leo alikuwa na cheo cha koplo yaani alikuwa na alama mbili za V, nilifahamu kuhusu vyeo vya kijeshi nilipokuwa na nasoma CUBA, na siku ile niliamua kukaa kidogo ili nitazame jinsi inavyo kuwa eneo lile, ambalo inasemekana kuwa ndiyo sehemu pekee ambayo mtu yoyote hata wale wenye kipato kidogo wanaweza kwenda kustarehe.
Nikiwa nimetulia kwenye meza moja peke yangu na kunywa bia taratibu, huku watu wakiwa wachache, japo walionekana mmoja mmoja wakiingia pale ukumbini, ambapo hata music ulikuwa unasikika kwa sauti ya chini, mpaka baadae kidogo ndipo niliweza kuona mambo mengi sana usiku ule, ni mara tu baada ya sala ya Insha, yaani kuanzia mida ya saa mbili na nusu, ndio muda ambayo watu walianza kumiminika pale Staring mess.
Mpaka saa tatu tayari ukumbi ulikuwa umeshajaa, wanawake na wanaume, askari kwa raia wote walikuwa wanaendelea na burudani zao za kunywa pombe na kucheza music, hata mimi nilishanza kuchangamka na kuondokewa na unyonge ambao toka nije pemba ulikuwa umenishika, ni kama nilisahau kuwa nipo pemba kwa sasa.
Hakika haikuwa pemba ile niliyoiona jana leo asubuhi mpaka mchana, hakika watu walikuwa wamechangamka kweli kweli, hakika ilinifariji, japo sikutaka kulewa sana, kutoka na kwamba kesho yake nilihitajika kwenda pale shuleni, hivyo isingekuwa vyema niende nikiwa na hang over, niliweza kuwaona baadhi ya watu wakipita na kutazama pale nilipokaa, kama vile wanajiuliza huyu ni nani, nikagunduwa kuwa wakazi wengi wa kisiwa hiki wengi wanafahamiana, hivyo hata akiingia mgeni lazima ataonekana wazi kuwa ni mgeni.
Naam katika kung’azang’aza macho nikamuona Ussi, yule jamaa wa jana akiwa ametulia kwenye meza moja ambayo ilikuwa mita chache kutoka kwenye ile meza niliyokuwepo mimi, yaani tulitenga nishwa na meza moja tu! katikati akiwa na mschana mwingine ambae sio yule wa jana, wakiwa wamechafua meza kwa vinywaji huku kasha zima la sigara likiwa limelala mezani, kwa kifupi nikajikuta nayapenda maisha ya jamaa huyu, ambae alionekana kutokea kwenye maisha ya kitajiri sana, “niambie brother naona umekuja kuchek jinsi wapemba wanavyo jiachia” niligutushwa na sauti ya mtu toka toka upande wangu wa kushoto nikageuka na kumtazama……….. ITAENDELEA MUWE NA USIKU MWEMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom