KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA TISA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE: “bro huku kutumiwa jinsi ni kawaida sana, na ukitka kuona jinsi mambo yanavyo kuharibikia we tembea na mtoto wa mtu yaani mwanfunzi, mdanganye utamuoa halafu umuache au tembea na mke wa mtu halafu jamaa ashtukie, hapo lazima utatumiwa kitu” alifafanua Mwasenga na hapo nikawa kama nimepata uelewa fulani, “vipi kuhsu tukio la pale Madungu, inaweza kuwa mtu katumiwa jini?” nilimwuliza Mwasenga, hapo nilikuwa nahitaji jibu ambalo, moja kwa moja ningelipeleka makao makuu ya MSC yaani Mbogo Spy Com…..ENDELEA……
“ile kwa kweli ni utata, maana jamaa ni mtu mmoja mstaarabu sana, sijui nini kilimkuta mpaka akabeba mke wa mtu na kumpeleka Madungu” alisema Mwasenga ambae hakuwa ametoa jibu sahihi nililokuwa nalitaka, “haaa mwasenga umejuwaje kama ni mke watu bwana” nilimuuliza swali la kichokozi, swali ambalo niliamini lilikuwa la kawaida, kwakifupi sikutaka ajuwe kama nachunguza kuhusu tukio lile, si unajuwa kuwa hapa nilikuwa naongea na mwanajeshi, watu ambao naamini kuwa wana utambuzi wa haraka sana, “bro, kwanza kabisa unaambiwa huyo demu alivaa niqab, ndivyo wanavyofanyaga mademu wengi wanaochepuka, sasa we hujaamini tu kuwa alitupiwa jini?” aliniuliza mwasenga, na hapo nikakubaliana nae kuwa bwana Abdulqadir alikuwa anachepuka na mwanamke wa mtu ambae mume wake alimua kutumia jini kumlinda mke wake, “kwahiyo inawezekana mwenye mke anafahamu kuwa mke wake sio muaminifu ndio akamtegeshea jini?” nilimuuliza Mwasenga, ambae kiukweli hakuweza kujibu swali hilo kiufasaha, “kiukweli hiyo nayo inashangaza kidogo, labda alikuwa anatoka nae kwa muda mrefu mpaka mwenye mke alipogundua na kuamua kuweka mtego wa jini” alijibu mwasenga na jibu lake likaanza kunipa hali fulani ya kuanza kuichunguza lile swala, “nasikia huyu jamaa alikuwa na duka la urembo, hivi duka lake lilikuwa sehemu gani pale mjini?” niliuliza swali ambalo ungesema muulizaji ana ufahamu vyema mji wa chake chake, “duka lake lipo mwanzo tu, ni hapa kwenye safu ya maduka pembezoni mwa barabara ya kuingilia sokoni, duka la nne kulia unaingia kwenye chochoro halafu unahesabu duka la kwanza la pili ndio lake, japo kwasasa limefungwa, ila mtaa una mademu kibao wakali” alisema Mwasenga, akisifia kama kawaida yake pasipo kujuwa kuwa mwenzie tayari nipo kazini.
Naam siku ile sikuchelewa sana kurudi kambini, nilipanga nilale mapema kutokana usiku wa jana kuchelewa kulala, nilipofika nilikaa mezani kujaribu kuweka note baadhi ya mambo ambayo nilifanikiwa kuyapata toka nifike hapa kisiwani, maana sikuwa na utaratibu wa kunote kutokana na kwamba niliamua kuachana na upelelezi huu, lakini kwa maelezo ya Mwasenga yalinifanya nipate hali ya kuamua kuchunguza swala lile, ikiwa ni kwamba kama huyo mwanamke sio jini, ni mke au mtoto wa mtu, basi nifanye juu chini nimfahamu, na kama nikimfahamu na nikimpata huyo mwanamke basi nitamfahamu mume wake ambae nitapata kufahamu ukweli baada ya kumpata huyo mwenye mke au mzazi wa mwanamke huyo, nilitumia kama lisaa lizima nikiunganisha maongezi na dondoo, huku nikikadilia matokeo nitakayo yapata, kwakifupi nilighairi mpango wangu wa kudanganya matokeo ya uchunguzi na kuamua kuingia kazini mazima, hivyo basi nilipanga siku inayofuata nikaanze kutafuta chanzo cha habari cha kuaminika, na sio sehemu nyingine ila ni maeneo yale yale ya dukani kwa marehemu Abdulqadir. siku ya pili niliwahi sana kufika shuleni, niliwahi gwaride la asubuhi la wanafunzi, japo kuna jambo lilinivutia asubuhi ile pale shuleni, ni baadhi ya wanafunzi wakike na wakiume waliokuwa wamevalia sale tofauti na wezao, wao walivaa track suit za michezo za rangi ya njano na blue, japo baadae kidogo niliweza kumuona mwalimu Aisha pia amevalia kama wale wanafunzi, japo kwa upande wa jinsia ya kike, vichwani walivaa vilemba vyeupe, “mwalimu Eric nenda kwa mwalimu mkuu, anakuhitaji haraka” aliniambia mwalimu Aisha, “kuna nini, halafu mbona nyie mumevaa kimichezo na wengine hatujavaa kama nyie au ni ya shule?” nilimuuliza mwalimu aisha kabla sijaenda kumuona Head Master, “we nenda bwana majibu yako utayapata” alisema mwalimu Aisha, na mimi nikakimbilia ofisini kwa mwalimu mkuu, ambae nilimsalimia kama ilivyo taratibu ya salamu za kisiwa hiki, asalamu Alaykum mwalimu” ndivyo nilivyo salimia walaykum salam Eric, karibu sana” alinikaribisha mwalimu mkuu, ambae pia alinieleza kuwa amesikia kuwa nina jihusisha na michezo, hivyo alinitaka kusimamia timu mbili za mpira wa kikapu na mpira wa wavu, yaani Voley ball, “ni jambo la ghafla maana jana jioni kabla sijaondoka hapa ofisini nilipokea simu toka shule ya sekodari ya Utahani, iliyopo huko wete kaskazini mwa pemba kunikumbusha mchezo wa kirafiki ambao tulipanga uchezwe kesho juma moss kwenye viwanja vya gombani, huu ni utaratibu ambao tumejiwekea kwamba kila baada ya miezi miwili huwa tuna kutana na katika michezo ya volley ball na baskert ball wakati mwingine na Net ball, yaani michezo ya ndani, na kila baada ya miezi sita huwa tuna kutana kwa mechi za mpira wa miguu” alinieleza mwalimu, jambo ambalo sikutaka liwe kikwazo cha kuanza kazi yangu ya uchunguzi, “mwalimu wetu wa michezo amesafiri kwenda unguja, hivyo nimekuchagua wewe usimamie timu zote katika siku hizi mbili yaani leo na kesho kwenye mechi, utashirikiana na mwalimu Aisha, ukichukulia bado vifaa vyako vya kufundishia havijafika bado” alisema mwalimu mkuu, Farid Mzee Abdallah, sikuwa na pingamizi, hivyo nikaambiwa niende nikavae nguo za michezo niungane na timu mara moja kwenye mazoezi.
Nusu saa baadae ikiwa ni saa moja na na dakika arobaini na tano, nilikuwa eneo la viwanjani nikitazama timu zote zikiwa kwenye mazoezi, ikiwa ni timu ya Volley ball iliyo kutanisha jinsia zote mbili yaani kike na kiume, huku mpira wa kikapu pekee ukiwa na jinsia moja, yaani wanaume pekee, ukweli licha ya kuvaa track suit lakini hakukuwa na jipya kwa watoto wale wakike, hakuna alienishtua kwasababu ukiachilia nguo hizo kuwa pana, pia hawakuwa na maumbo makubwa ya kuweza kuonekana yaliyo jichora, japo sura za wengi wao zilikuwa za kuvutia sana, “mwalimu Aisha simamia Volley ball, wacha mimi niwaandae wa baskert, nilikubaliana na mwalimu Aisha japo mara chache alikuwa anakuja kuniomba ushauri, na kitu ambacho ningependa ukijuwe msomaji ni kwamba licha ya kucheza sana baskert ball, pia nilikuwa na uwezo wa kucheza soka na volley ball, hivyo nilimshauri vizuri na pia wakati mwingine nilielekeza namna ya kukupokea mpira kuset na kushambulia au kuzuia mashambulizi toka kwa wapinzani wao, mazoezi yaliisha saa nne kasoro huku wachezaji wakionekana kunielewa na kufuata maelekezo yangu.
Saa tano na nusu, ndio muda ambao tulitawanyika pale shuleni ikiwa ni kuwapa nafasi walimu na wanafunzi kwenda kuswali, huku maagizo yakiwa ni kwamba wachezaji wa timu zote tukutane jioni katika viwanja vya gombani kwaajili ya mazoezi, pia baadhi ya walimu wengine walipanga kuja kutazama mazoezi hayo, na muda huu wa saa tano ndio muda ambao na mimi niliamua kwenda mjini kama nilivyo panga, mwanzo ilikuwa ni kwenda kununua mpira, lakini sasa ilikuwa ni zaidi ya kwenda kununua mpira, ni kwenda kutafuta habari za marehemu Abdulqadir, saa sita mchana nilikuwa nashuka toka kwenye chai maharage maeneo ya Cheke chake mjini, njia panda ya sokoni wenyewe wanaita Markiti, watu walikuwa wengi sana mida hii usinge amini kama jioni huwa zinabakia nyumba peke yake kiasi cha kuogopesha.
Nikiwa nimevalia suruali yangu ya jinsi la blue, tishet nyeusi raba nyeusi chini kibegi kidogo cha blue chenye mkanda mmoja, licha ya kubeba wallet yenye fedha elfu hamsini na lessen ya udereva, maana fedha huwa naweka mfukoni, pia nilikuwa na bastora yangu ambayo kama kawaida niliiweka kwenye kijifuko cha mkanda, nikaanza kutemmbea kuelekea upande wa sokoni mpaka nilipokaribia chake hotel, nikaanza kutazama upande wa kulia kwangu ambako niliweza kuona maduka vya vifaa vya kike yaliyo sheheni urembo mbali mbali, manukato na nguo za kike na watoto wadogo wa jinsia zote.
Nilifuata maelekezo ya Mwasenga mpaka nilipohesabu maduka manne, ndipo nilipoiona chochoro niliyo elekezwa, nayo ikiwa na maduka kushoto na kulia, nikaifuata ile chochoro huku nikitembea kwa tahadhari ya kutokukumbana na watu wengi waliokuwepo kwenye ile chochoro, wengi wao wakiwa ni wanawake, duka la pili lilikuwa limefungwa, ni kama nilivyo elekezwa, hapo nikatazama kushoto na kulia kama ningeweza kumuona mtu ambae ninaweza kuongea nae pengine ningeambulia mawili matatu, bahati ikawa kwangu, pale nilimuona mschana mmoja muuza duka, ambae duka lake lilikuwa na mteja mmoja tu tena wakike, duka lake lilikuwa upande wa kulia wa duka la Abdulqadir ambalo lilikuwa limefungwa, japo sikujuwa wala kufahamu wepesi na ucheshi wa wanawake wa kisiwa hiki, lakini nikajipa moyo kuwa kikubwa ni kwamba tunazungumza lugha moja, nikienda kibiashara ninaweza kujenga urafiki wa muda na kuwa chanzo cha kupata kile nachohitaji kukipata au kukijuwa kuhusu mahusiano ya bwana Abdulqadir, nikamtazama mwanamke muuza duka alievalia gauni moja zuri rangi ya dhahabu na kilemba chake, yaani hijab nyekundu, uzuri wa uso wake ulikuwa wakawaida tu kulinganisha na uzuri wa wanawake niliowahi kuwaona kisiwani hapa, hata hivyo nilitembea kwa tahadhari kulisogelea duka lile huku nikapanga namna ya kumuingia.
Naam mpaka nafikia duka lile ambalo lilikuwa mahususi kwaajili ya vipodozi na manukato, mpaka nalifikia duka lile tayari nilipishana na mteja aliekuwa anamhudumia aliekuwa anaondoka zake “asalam aleykum” nilimsalimia muuzaji yule wakike ambae kwa mkadirio wa haraka haraka alikuwa anamiaka kama kumi na nane hivi, ambae sasa alikuwa anaweka fedha sehemu yake, aliposikia salamu yangu aligeuka haraka na kunitazama, “waleykum salam, karibu” aliitikia yule mwanadada, ambae alinitazama kwa jicho kavu la mshangao, hakuonyesha dalili ya urafiki hata kidogo, ukweli muonekano wangu, ulikuwa tofauti na watu wenye asili ya kisiwa hiki ambao uvaaji wao ulikuwa ni wa kanzu au suruali na shati la bila kuchomekea na sendo chini au kanda mbili yaani Makubazi kama wao wanavyoita, sasa mimi nilivaa suruali ya jinsi tishet na raba
Niliuona mshangao wa dada yule, nikajuwa kabisa kuwa hapa mambo yanaweza kuwa magumu endapo nitatumia mbinu ya uteja pekee, hivyo lazima niongeze mbinu, na mimi nikamtazama usoni kwa macho ya mshangao wa kustaajabu, nilitumia sekunde kadhaa kufanya vile, nilimtazama huku taratibu tabasamu likijiunda usoni kwangu mfano wa mtu aliemuona mwanamke mzuri sana wa kuvutia, kiasi kwamba nikamuona na yeye anaanza kunishangaa mimi kwa ushangaaji wangu juu yake, “hallow we kaka…” aliseme yule mschana, huku anajitabasamulisha na mimi nikajifanya kushtuka, halafu nika muongeza na hii, “hongera dada yangu” nilisema kwa sauti tulivu na ya upole, huku nikimtazama kwa macho tulivu na uso wa tabasamu…..... TUNAENDELEA
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA KUMI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA: Niliuona mshangao wa dada yule, nikajuwa kabisa kuwa hapa mambo yanaweza kuwa magumu endapo nitatumia mbinu ya uteja pekee, hivyo lazima niongeze mbinu, na mimi nikamtazama usoni kwa macho ya mshangao wa kustaajabu, nilitumia sekunde kadhaa kufanya vile, nilimtazama huku taratibu tabasamu likijiunda usoni kwangu mfano wa mtu aliemuona mwanamke mzuri sana wa kuvutia, kiasi kwamba nikamuona na yeye anaanza kunishangaa mimi kwa ushangaaji wangu juu yake, “hallow we kaka…” aliseme yule mschana, huku anajitabasamulisha na mimi nikajifanya kushtuka, halafu nika muongeza na hii, “hongera dada yangu” nilisema kwa sauti tulivu na ya upole, huku nikimtazama kwa macho tulivu na uso wa tabasamu…..... TUNAENDELEA....
Kwanza kabisa mtoto wa watu akaachia zinga la tabasamu sambamba na kicheko laini huku anatazama chini kwa aibu, “hongera ya nini” aliniuliza huku akimalizia kicheko chake, “japo sija zunguka sana hapa kisiwani wala Tanzania bara, lakini na amini kuwa sijawahi kuona mschana mzuri kama wewe” nilisema hivyo kwa sauti flani, iliyojaa staha na utulivu, nikamuona anainua macho kwa mshangao na kunitazama, ambapo hakuweza kufanya hivyo kwa muda mrefu, huku macho yake yakionekana kuwa kama macho ya mlevi, akatazama chini kwa aibu, “kaka wewe ni mtundu, embu sema shida yako bwana mwenzio mimi ni mwanafunzi” alisema yule mschana ambae sio kwamba ni mbaya wa sura, hapana, alikuwa na sura ya kwaida ya kupendeza, “ok! samahani kama huku kwenu kumueleza mwanamke sifa yake ni vibaya, ila mimi nahitaji perfume ya #mbogo_land body spray” nilimueleza yule dada nikimtajia perfume moja adimu sana kwa Tanzania bara, wakati huo nilikuwa natazama bidhaa zilizopangwa kwenye flemu za ukutani na kwenye vikabati vya vioo pale mezani, “kwanini unapenda bidhaa za #mbogo_land, ni watu wachache sana hununua bidhaa za huko kwasababu ni ghari sana” alisema yule mschana, huku akijichekesha kidogo, nadhani ni baada ya mimi kuonyesha dalili ya kuzingatia uzuri wake, wakati huo akigeuka na kuchukuwa chupa moja ya perfume, “yah! napenda sana vitu toka nyumbani” niliona kuwa uongo huo utasaidia kwa yeye kupenda kujenga urafiki zaidi, “hooooo, kumbe weye unatokea #Mbogo_land, huko vitu vyao asilimia kubwa ni original, kuanzia mikufu ya dhahabu na vitu vingine” nilimjibu mschana huyu kwa sauti yake yenye lafudhi ya kipemba huku ananikabidhi ile chupa na kujaribu kunitazama usoni, lakini macho yetu yalipokutana nikashindwa na kujikuta akitabasamu na kutazama chini, na mimi nikacheka kidogo huku moyoni mwangu ikiwa ni mshtuko wa mduwazo, maana sikutegemea kama angekuwa nayo ile perfume, “bei gani huku kwenu” niliuliza huku nikifahamu fika kuwa bei yake ni elfu ishirini (kwakipindi hicho unapozungumzia elfu ishirini ujuwe unazungumzia fedha ndefu, maana nakumbka mshahara kima cha chini hakikuzidi elfu hamsini) kwa hiyo kima cha kati mtu angekuwa anapokea elfu themanini au laki moja na kitu, “ni elfu ishirini na mbili tu” alijibu yule dada, huku akinitazama, kwa jicho fulani la tathmini, pasipo kujuwa mimi niliejifanya naitazama ile perfume nilikuwa namtazama kwenye kioo cha meza iliyokuwepo mbele yetu, “mh! dada yangu, nina elfu kumi na tano, vipi huwezi kunipunguzia kidogo?” nilisema, huku nainua uso na kumtazama yule mwanamke kwa sauti tulivu huku tabasamu likiendelea kuangaza mdomoni mwangu, nikiwa na nia ya kujikosesha ile perfume ambayo sikuwa na mahitajio nayo, “mh! kaka atanigombeza” alisema yule mschana huku ananyoosha mkono wake kwangu kuchukuwa ile perfume, “subiri kidogo, si bado tunapatana kwanza” nilimueleza yule mschana ambae, mpaka sasa sikuwa na fahamu jina lake, sauti tulivu nzito ya kubembeleza huku namtazama usoni kwa macho yaliyojaa ukorofi wa kiume, “sawa basi nunua kwa elfu ishirini” alisema yule mschana huku anakwepesha macho yake, “hivi dada unaitwa nani?” nilimuuliza yule mwanadada, “naitwa Saphia” alijibu yule binti kwa sauti ambayo ilijaa raha fulani hivi, “ok! ulisema unasoma wapi?” nilimuuliza tena kwa sauti ile ile tulivu, huku na mtazama usoni kwa macho yale yale tulivu yenye ukorofi wa kushawishi, “nimemaliza kidato cha pili, nasubiri matokeo ya kuendelea kidato cha tatu” ukweli hilo kwangu lilikuwa jipya, ni kwamba kwa Elimu ya visiwa vya Zanzibar, mwanafunzi anapata Elimu ya cheti katika ngazi nne, moja ni darasa la saba, pili kidato cha pili, ambapo mtu uhitimu na kupata cheti, halafu kuna kidato cha nne na cha sita, baada ya hpo mwanafunzi angeendelea na chuo.
Naam naam hapo sasa nikatumia akili ya kuzaliwa, “sikia Saphia, unajuwa mimi siyo mtumiaji wa perfume, hii inaweza kuwa ya kwetu mimi na wewe, siku unafika nyumbani unaikuta na kuitumia” nilisema kwa sauti tulivu, kiasi kwamba ilianza kuwa nzito, unajuwa nini, uigizaji ule ulinifanya nianze kwenda kwenye uhalisia, lakini wakati huo nilikumbuka kuwa katika makosa makubwa huku kisiwani ni kudanganya ndoa kwa mschana.
Nilimuona Saphia akiachia tabasamu moja pana sana, tabasamu ambalo lilijaa kila rangi ya furaha, “lakini mimi sipendi kuwa bi mdogo” alisema saphia kwa sauti ya furaha yenye kila muonekano wa kudeka, ungesema lile swala tulilokuwa tunaliongea ni la kweli, “utakuwaje mke wa pili wakati bado sijaoa, mimi nimepanga kuoa mke mmoja tu” nilimueleza Saphia ambae sasa niliona kuwa anazidi kujaa ninapo pataka, “kweli hen?, basi sawa ila mara hii nikifaulu sitaki kusoma huku, nataka nikasome bongo (akimaanisha dar es salaam) au kwenu #Mbogo_land, si utanichukuwa pamoja na wewe?” aliniuliza Saphia, akionyesha kuwa katika furaha kubwa huku anachukuwa Perfume toka mkononi mwangu na kuanza kuiweka kwenye boxi, nikajuwa kuwa offer yangu ya kumi na tano imekataliwa ila mbinu yangu imekubalika, maana kitu ambacho nilikigundua ni kwamba waschana wengi walipenda kuolewa na watu toka taifa dogo la kifalme la #mbogo_land, kutokana na sifa nzuri za nchi hiyo, wakati huo ilikuwa inaongozwa na king Eugen Mbogo, “usijari Saphia, kama tukifanikiwa basi nitaondoka na wewe ukiwa kama mke wangu” nilimueleza huku na mimi nikiigiza kuwa mwenye furaha, huku nikijiandaa kumtupia swali la kwanza kuhusu bwana Abdulqadir, yeye akaniwahi, “kwani wewe huku pemba unamefuata nini?” aliniuliza Saphia huku akinitazama kwa macho ambayo yalionyesha furaha na upendo ulioanza kumea kwa kasi, “nime kuja Fidel Castor sekondali kufundisha somo la computer, nitakuwepo pale kwa muda wa mwaka mmoja” nilisema hivyo nikiwa na maana ya kwamba, muda huo ni mwingi sana kwa mimi kukaa pemba, lazima nitakuwa nimeshaondoka, hata kama atashtuka nimemdanganya na kuamua kunitumia jinni halitonipata, kwasababu uchawi hauvuki bahari,(watu wa simba wanalijua hili ndio maana waling'ang'ania kwa mkapa) “kumbe wewe ni mwalimu, basi utanisomesha hata ukioa” alisema Saphia kwa sauti fulani ya taratibu, ambayo ilionyesha kiwango cha juu cha furaha na amani ya moyo aliyokuwa nayo mschana huyu, “yah! tena nitahakikisha unasoma mpaka chuo kikuu” nilimjibu kwa sauti ambayo pia niliifanya kuwa yenye furaha kubwa, nashukuru hakuweza kuulizia kuhusu dini, “mbona mimi hujanitajia jina lako” aliniuliza Saphia, wakati huo nikiwa napanga namna ya kuanza kumuuliza kuhusu habari za Abdulqadiri, “naitwa Eric Frank” nilimjibu kifupi, huku nampisha amuhudumie mteja aliyekuwa amefika, mahali pale kwaajili ya kupata huduma, huyu alikuwa ni mteja wa kiume ambae alihudumiwa haraka sana kisha akaondoka zake.
Naam tuliongea mawili matatu na Saphia, huku mschana huyu akizidi kunizoea kwa kasi sana, kisha nikamchomekea lile nililo likusudia, “hivi hili duka si ndio lile ambalo mwenyewe aliuliwa na jini?” nilimuuliza Saphia huku nikionyesha lile duka ambalo lilikua limefungwa, “enheee ndiyo hilo haswaaaa” alijibu Saphia, kwa sauti iliyojaa uhakika, huku wote tukilitazama lile duka lililofungwa, tulitumia kama sekunde tano hivi kisha nikamtazama Saphia ambae pia alikuwa ananitazama, “hivi ni kweli ni majini ndio waliomuua huyu jamaa?” niliuliza kwa sauti fulani kama ya masikitiko hivi, “ndiyo tena alikuwa mmoja tu wa kike” alisema Saphia kwa sauti fulani kama vile ana uhakika wa kile anacho kisema, “weeee, kwahiyo huyo jini alionekana kabisa?” nilimwtuliza Saphia kwa sauti ya mshangao, “ndiyo alionekana, tena wanasema alivaa niqab na gauni refu, liliziba mpaka nyayo zake halafu mrefu hivi” alielezea Saphia, na hapo nikaanza kuvuta picha ya yule mwanamke niliemuona siku ya kwanza kuingia hapa pemba, “dah! sasa kwanini ndugu zake hawafungui duka au alikuwa anauza mwenyewe?” nilianza kuelekeza maswali yangu kule ninako kutaka, “hapana alikuwa anauza mfanyakazi wake, nae hajafungua toka msiba umetokea, nadhani anasubiri maamuzi ya ndugu” alijibu Saphia, na hapo nikaona niulize swali la msingi, “maamuzi ya ndugu au maamuzi ya mke?” nilimuuliza Saphia, ambae ni kama nilisha zoeana na kuonekana ni watu ambao tuna fahamiana kwa siku nyingi, “alikuwa bado kuoa” alisema Saphia, hapo nikaona kuna uwezekano wa hoja ya Mwasenga kuwa ya kweli, kwamba inawezekana Abdulqadiri alikuwa katika harakati za kutafuta mke, ndio maana akaingia kwa mtoto wa watu na kuamua kutaste mitambo kabla hajaweka kitu ndani, “hooooo! Lakini alikuwa na mchumba sio?” nilimuuliza Saphia kwa sauti flani ambayo haikuwa katika userious ilikumpoteza Saphia asigundue kuwa nia yangu ya kifika pale ilikuwa ni kuchunguza juu ya mauwaji ya bwana Abdulqadiri, “mh! sijawahi kusikia kuwa anamchumba, ila siku za karibuni alionekana kuwa busy na simu yake akiongea na mwanamke, nadhani sijui ndio huyo jini au ndie mchumba wake” alisema Saphia, na hapo nikahisi kuwa endapo nikiendelea kuuliza maswali zaidi ya mawili lazima angenishtukia, “lakini munakaa anae mtaa mmoja sio?” nilimuuliza Saphia, nikiwa na lengo la kutaka kupajuwa nyumbani kwa Abdulqadiri ili nikafanye uchunguzi wangu, “hapana yeye anaishi njia ya Airport, na sisi tunakaa msingini, na kaka anakaa macho manne kule maskini hajengi” alijibu Saphia akitaja mtaa ambao kwangu ulikuwa mgeni kidogo, na hapo nikaanza kupata picha kuwa Saphia anauza duka la kaka yake, ambae anaishi kule macho manne, “hooo! sawa kwahiyo umemucha kaka yako na wifi yake peke yao wewe unakaa na mama” nilisema vile kisha tukacheka kidogo, sikutaka kumfahamu kaka yake ni nani, “siwezi kukaa kwake bado hajaoa” alisema Saphia na wakati huo huo ikasikika adhana ya swala ya ijumaa
Kama ilivyo kawaida, hapo ukawa ndio mwisho wa maongezi yetu, maana niliona watu wanaanza kufunga maduka tayari kwenda kuswali “chukuwa mzigo wako lete elfu kumi na tano nitakuongezea mimi iliyobakia” alisema Saphia huku ananikabidhi mfuko mdogo wenye box la ile perfume ya #Mbogo_Land body spray, nilishangaa kwa mshtuko, yaani kautani nilikomfanyia tayari amenipunguzia perfume kwa kiwango kikubwa namna hii, “asante sana Saphia, hakika utaikuta kabla sijaitumia” nilimueleza huku napokea ule mfuko, usoni nimeachia tabasamu, japo moyoni mwangu niliogopa kidogo, nikamtolea note ya elfu kumi moja na elfu tano moja, nikampatia akaziweka huku anacheka cheka, kisha akachukuwa peni na karatasi, “nitajie basi” alisema Saphia huku akiwa tayari kuandika kitu, ambacho sikukijuwa hapo mwanzo, “nikutajie nini Saphia?” nilimuuliza Saphia huku najitabasamulisha, “namba zako za simu” alisema Saphia, na hapo nikamtajia namba za simu nae akaziandika, “lakini kwanini usiandike kwenye simu yako” nilimuuliza wakati anamalizia kuandika, “simu ya dukani wakati mwingine anakaa kaka, akiiona namba yako ataniuliza maana bado hujajitambulisha nyumbani” alijibu Saphia, na hapo nikashukuru kimoyo moyo, “angalau anafanya siri” unajuwa kwanini nilijisemea hivyo kimoyo moyo, ni kwasababu niliamini endapo ingekuwa wazi hii siri basi ingekuwa rahisi kutumiwa jini, huku niki apa sito jaribu kutest mitambo kwa binti huyu wa kipemba, “ok! sawa”.
Naam nilimsaidia kufunga duka kisha tuka toka wote pale dukani kwao kwenye uchochoro, ambako sasa watu walikuwa wamesha ondoka wote, tulitembea mpaka njia kubwa ya Markiti, ambako pia maduka yalishafungwa, niliamini hata maduka ya vifaa vya michezo nayo yatakuwa yamefungwa, nikaona itakuwa vyema endapo nitatumia muda wa kusubiri watu watoke msikitini kuelekea Madungu Guest House kuonana na bwana Hassan ili nipate mawili matatu.
“Kaka yangu atakuwa huku huku msikitini” alisema Saphia, wakati bado hatujaagana na mimi nikamtania kidogo, “anatembea gari au Vesper?” nilimuuliza Saphia, ambae alijibu kwa haraka sana, “weee! ana Vesper nzuri” niligundua kuwa Vesper ni usafiri mzuri sana kuliko gari hapa kisiwani, “sasa Saphia, wacha basi nikuache kaka yako asije kutuona” nilitumia kama gia ya kuagana nae, hapo tukaagana na mimi nikapanga nielekee Madungu Guest house kukutana na Hassan mhudumu wa guest hiyo, mtu ambae inasemekana ndie aliemuona Jini, “sawa basi nikipata simu nitakupigia” alisema Saphia wakati tunaagana, akimaanisha kuwa akiazima simu kwa mtu atanipigia, “poa nasubiri simu yako nikipata mshahara nitakununulia ya kwako” nilijibu hivyo, nikiongeza na ahadi ya uongo “weeeee! Usininunulie mpaka uje ujitambulishe kwetu, wakiniuliza nitawaambia amenunua nani?” alisema Saphia na hapo nikacheka kidogo, huku moyoni nikishangaa kidogo, maana kwa Tanzania bara ingegeuka kuwa deni kubwa la ukoo, “ok! poa basi baadae au kesho” niliaga na yeye akapunga mkono kwa kujiachia, maana wakati huo barabara ile ya Markiti haikuwa na watu wengi, nilitembea taratibu nikifuata njia fulani ambayo kiukweli unapana wa kupita gari moja tu, njia ambayo nilipita siku ya kwanza nilipokuwa na mkimbia yule mwanamke jini.
Naam barabara ile ilikuwa kimya sana kama mji ulivyokuwa kimya, hata ngurumo za gari au pikipiki, zilisikika kwa uchache sana, zaidi ni sauti ya imamu ndiyo iliyosikika kupitia kwenye speeker kubwa za msikiti wa chake chake, pengine ungeweza kuona mtu mmoja ndani ya dakika kadhaa.
Nilitembea kwa haraka kwasababu hofu ya kukutana na jini nilikuwa nayo, na wakati natembea niliweza kumfikiria Saphia, ambae ni kama alianza kuniweka moyoni mwake, nikamuonea huruma sana,kwa sababu ningeumiza moyo wake, hata hivyo nilipanga kuachana nae taratibu bila yeye kujuwa kuwa lengo langu halikuwa kumchumbia kama nilivyosema, nilifikiria madhara yatakayonipata endapo nitabainika kuwa nimefanya ulaghai, nikajifananisha kuwa kitanitokea kilichomtokea Abdulqadir, hapo mwili usinilisisimka,
Naam nikiwa nimepiga hatua kama hamsini ambazo ni sawa na kutembea mita hamsini au sitini, nikaanza kusikia harufu nzuri ya marashi (perfume) fulani ya kuvutia, mimi sio mpenzi sana wa marashi hata haya ya leo nilinunua tu bila kutegemea, na kila nilipopiga hatua kusogea mbele ndivyo pua zangu zilipozidi kunusa harufu hiyo ya perfume, ambayo ilikuwa inazidi kuwa kali puani mwangu, nikaanza kuingiwa na wasi wasi, hivyo nikaamua kuongeza mwendo kusonga mbele zaidi huku mwili ukinisisimka mpaka nywele.
Sasa basi wakati nikiwa navuka chochoro moja ambayo sikuwa nimeizingatia sana, ghafla nikasikia vishindo vya ko! Ko! Ko! Mfano wa mtu mwenye kuvaa viatu virefu au kwatu za ng’ombe anae tembea kwenye lami au sementi, nika geuka haraka kutazama kule kwenye uchochoro, ili kuona zile kokoko! Zinatokwa wapi na kwanini.
Naam ila nilicho kiona nilitamani nikimbie, “Asalam alaykum” ilikuwa ni sauti ya kike sauti tamu kuliko utamu wa kinubi cha Suleimani, alikuwa ni mwanamke yule yule mzuri kupita maelezo ambayo naweza kukupa juu ya uzuri wake, ni mwanamke ambae kiukweli sio tu hapa pemba hata Tanzania bara na mikoa yote niliyowahi kutembea nchi zote nilizowahi kwenda, labda kwenye tv na majarida ya urembo pekee, lakini huko kwingine sikuwao kuona uzuri wake, ni mwanamke yule yule ambae siku ile nilimuona mitaa hii……..NAAM Eric amekutana na mwanamke ambae siku zote hakutamani tena kukutana nae nini kitatokea? tukutane sehemu inayofuata..