KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI: Naam ila nilicho kiona nilitamani nikimbie, “Asalam alaykum” ilikuwa ni sauti ya kike sauti tamu kuliko utamu wa kinubi cha Suleimani, alikuwa ni mwanamke yule yule mzuri kupita maelezo ambayo naweza kukupa juu ya uzuri wake, ni mwanamke ambae kiukweli sio tu hapa pemba hata Tanzania bara na mikoa yote niliyowahi kutembea nchi zote nilizowahi kwenda, labda kwenye tv na majarida ya urembo pekee, lakini huko kwingine sikuwao kuona uzuri wake, ni mwanamke yule yule ambae siku ile nilimuona mitaa hii…….. ENDELEA…..
kilicho nishangaza zaidi ni kwamba mwanamke huyu mrembo ambae leo alikuwa amevalia gauni jeusi baibui lenye kunakshiwa kwa hariri za dhahabu kwenye pindo za mikono na chini, ambae viatu vyake havikuweza kuonekana, aliekuwa mita chache sana anatembea kuja kwenye barabara niliyokuwepo mimi, alinitazama huku anaachia tabasanu pana kama vile ni mwenye kuni fahamu, nilijikuta sauti yangu ikishindwa kutoka wakati najaribu kijibu ile salam, “asala… asalam .. samahani aley..” nilibabaika huku nakijitahidi kuinua miguu yangu ambayo nilianza kuiona inaanza kuwa mizito, yule mwanamke alicheka kidogo na kuendelea na safari yake, maana aliingia barabara ile ambayo nilikuwa natembea mimi na kuelekea kule nilikotoka, hapo nilishukuru na kuongeza mwendo kuelekea upande ule ambao nilikuwa na uhakika kuwa ndiko kwenye ile barabara kubwa ya kueleka Madungu.
Nilitumia muda mfupi sana kuikuta barabara kuu, ambako angalau niliweza kuona watu wawili watatu, niliwaza sana kuhusu kilicho tokea, niliamini kuwa yule jini ameamua kunitokea baada ya mimi kuanza kuchunguza ile kesi, “oya! vipi kaka, naona upo kwenye mizunguko” nilisikia sauti toka upande wa pili wa barabara sikujali kwa sababu niliamini haikunihusu, japo nilitazama kuona kama kuna usafiri upande ambao ungeniondoa sehemu ile kwa haraka, na hapo wazo langu likiwa ni kuelekea kambini, maana sikuwa na amani tena ya kukaa pale mjini, niliamini jini asinge niacha salama kama ningeenda madungu, “kaka hee! Unaonekana upo mbali kimawazo kuna nini?” ilisikika tena ile sauti” na hapo ndipo nilipo tazama vizuri upande wa pili wa barabara karibu na kituo cha mafuta kwenye njia ya kuingilia, nikamuona Ussi akiwa amekaa juu ya pikipiki yake aina ya Vesper, kwaharaka sana nikakumbuka kuwa natakiwa kuficha uhalisia wa hali yangu kwa muda ule, hivyo nikaondoa uso wa uoga na kujifanya mwenye tabasamu, kisha nikakimbia kuvuka barabara kwa haraka kuelekea pale alipokuwepo Ussi, ambae alikuwa amevalia kanzu nyeupe na baraghashia nyeupe pia, maana niliona kuwa yeye ndie pekee ambae angenipeleka Macho manne ambako usafiri ulikuwa mwingi muda wote, hata kama ninge takiwa kulipia fedha ningefanya hivyo, na nisingeweza kumpigia simu mwasenga maana niliamini asingefika kwa wakati, japo hata hivyo nilihisi kuwa Ussi nae anaenda msikitini, hivyo kulikuwa na hatari ya kukosa usafiri toka kwake, “asalam alaykum kaka” nilimsalimia Ussi, yani ni yule jamaa ambae sio tu kwa kuambiwa bali kwa kuona kwa macho yangu kuwa ni kijana mwenye muonekano wa kifedha, ambae anatembelea magari ya kifahari, japo mara nyingi namuona akiwa anatembelea hii pikipiki yake aina ya vesper, mara baada ya mimi kumfikia huku nikijitaidi kuweka hali yangu katika hali ya kawaida nikiondoa uoga niliokuwa nao, “waalaykum salaam teacher, vipi naona upo mtaani kidogo” alisema bwana Ussi, huku akionyesha uso wa tabasamu, “nilitaka ninunue mpira wa baskert, lakini naona maduka yamefungwa, sasa nataka kuelekea macho manne nimekosa usafiri kabisa” nilimueleza Ussi, ambae pikipiki yake ilikuwa imetazama upande wa madungu, akatazama mbele kama vile anatazama usafiri wowote uliokuwa unakuja kisha akatazama nyuma, “dah! sijui tutafanyaje, ukweli ninge kupeleka ila sasa naelekea msikitini na nimeshachelewa” alisema Ussi, akionekana kuwa hakuwa tayari kunipeleka Macho manne, na wakati nafikiria cha kufanya ili nijiondoe hapa chake chake haraka, Ussi akasema “ila muda mfupi baadae watu wakitoka msikitini magari yataanza kupita” alisema Ussi huku anainua uso wake kutazama upande niliotokea mimi, yaani kwenye ile barabara ambako kulisikika ngurumo ya vesper, tuka mwuna jamaa mmoja alievalia kanzu rangi ya dhahabu iliyopauka na balaghashia nyeusi yenye hariri ya dhahabu, akiwa juu ya hiyo Vesper, akiwa amembeba mwanamke wake ambae alikuwa amevalia baibui nyeusi yenye hariri ya dhahabu huku usoni mwake akiwa amevalia niqab.
Kwa upande wangu sikuwajali sana wale mke na mume kama nilivyohisi, ila kwa upande wa Ussi aliwatazama sana mpaka yule dereva ambae alikuwa anaingia barabara kuu ya kuelekea wete alipotazama upande tuliokuwa sisi, Ussi akapunga mkono ikionyesha kuwa anamfahamu yule jamaa, ambae nikweli nilimuona akipunga mkono kwa nguvu ikiwa ni jibu la salamu ile, “wapi hiyo Masoud?” aliuliza Ussi, na hapo ndipo niliposhawishika kumtazama yule jamaa, ambae nilimkumbuka kuwa ni Msoud Vuai, yule ambae alikuwa na Ussi jana pale uwanjani, “naenda home mara moja nitarudi jioni” alisema Vuai, ambae hakusimama ila alizidi kuendesha Vesper yake kuelekea upande wa Macho manne, “poa poa” alisema Ussi huku bado tuna watazama.
Kunajambo lilinishangaza kidogo, ni kuhusu yule mwanamke mwenye niqab ambae nilidhania kuwa ni mke wake, ambae licha ya sisi kusalimia lakini hakujaribu kututazama wala kuhangaika na sisi, nilijaribu kumfananisha na yule mwanamke niliemuona dakika chache zilizopita, yule mwanamke mwenye kunukia kwa marashi ya kuvutia, lakini sikuweza kumfananisha moja kwa moja kwasababu tayari alishaziba uso wake kwa kitambaa chekundu akiachia macho pekee, japo kwa muonekano wa umbo hakika na yeye alikuwa amejaliwa vyema, sikuweza kujaji kuhusu kimo chake kwasababu alikuwa amekaa huku akiachia makalio yake yakichomoza upande wa pili wa Vesper, kiasi nikaanza kujiona mjinga kwa kuona kila mwanamke mzuri.
Wakati namshangaa bwana Vuai na mke wake, nikisahau kuhusu kupata usafiri wa kwenda Macho Manne, mara nikakumbuka kuhusu kumpigia simu Mwasenga aje kunichukuwa, “sasa bro baadae basi, nilimueleza Ussi huku naanza kutembea kuelekea upande wa Macho manne, “Sikia teacher, ngoja niwasiliane na mtu hapa kama akiwa tayari na mzigo wangu basi nikukimbize mara moja kisha nije nionane nae” alisema Ussi, ambae nilipomtazama alikuwa amesha toa simu anabofya bofya, na mimi nikasimama na kumsubiria dakika chache baadae akaanza kuongea na simu, “upo wapi….., ok! haraka basi tukutane njia panda, mimi naelekea Macho Manne….. haraka sana fanya hivyo” alisema Ussi na kukata simu kisha akawasha pikipiki yake, japo wenyewe wanasema Vesper sio pikipiki ila ni chombo, “twenzetu kaka” alisema Ussi na mimi nikapanda, kisha akageuza pikipiki na kufuata uelekeo wa Macho manne, mwendo ulikuwa mdogo mdogo mpaka tulipofika njia panda ya wesha, kule ambako mara nyingi huwa namuona anatokeaga, akasimama na dakika hiyo hiyo ikaja pikipiki ikiwa imepakiza vijana wawili weusi ambao muonekano wao ni kama vile wavuvi au watu waliokuwa wanashuguri fulani ya baharini kwa jinsi walivyo pauka, waliokuwa wamebebana kwenye piki piki kubwa aina ya baja yenye taa mbili kubwa mbele.
Yule aliekuwa nyuma alishuka toka kwenye pikipiki na kumsogelea Ussi kwenye Vesper na kumkabidhi kimfuko fulani chenye kitu kama bomba yaani jembamba mfano wa filimbi ya muanzi, vilivyokuwepo ndani sikuvijuwa, “mzigo huu hapa boss” alisema yule “mmechelewa sana..” alisema Ussi, huku anapokea ule mfuko, sikutaka kujuwa ndani mulikuwa na nini, ila ninacho juwa ni kwamba vijana wengi ambao hutumia mali na fedha za wazazi wao pasipo kuzitafuta wao binafsi huwa na matumizi mabaya, na wengine ujiingiza kwenye madawa ya kulevya, samahani sana boss” alisema yule jaama kwa unyenyekevu, ambae ni kama alikuwa anamgwaya sana kijana huyu tajiri, “poa nyie nendeni baadae nitakuja kuchukuwa samaki” alisema Ussi huku anafungua mkebe wa pikipiki ile nakuhifazi ule mfuko wake kisha akaufunga na kuondoa pikipiki kuelekea Macho Manne, safari hii akiwa kwenye speed kali sana kama kunajambo analiwahi, “wale jamaa ni wavuvi wangu, nina boti mbili za uvuvi” alisema Ussi huku akiendelea kuvuta mafuta kiasi cha kuanza kuniogopesha, nilitaka nimuulize ile speed ya nini lakini ni kama alisoma akili yangu, “ujuwe huku nakukimbiza mara moja ili nirudi kuna mtu inabidi nije nionane nae” alisema Ussi huku safari inaendelea.
Naam bahati nzuri yangu ni kwamba Ussi alinipeleka mpaka Wawi na kuaniacha nje ya lango la kuingilia kwenye ukumbi wa jeshi, bahati nzuri kwangu leo ijumaa chakula cha mchana kinalika huku Mess, ukweli Ussi alionekana kuwa na haraka sana maana hakunipa hata nafasi ya kumshukuru, aliondoka haraka sana kwa speed kurudi upande wa macho manne mjini, nilimsindikiza kwa macho mpaka alipo toweka usoni mwangu, hakika alikuwa katika speed moja kali sana.
Niliingia ndani ya ukumbi wa chakula, niliwakuta wakina Malambo na wenzake wakiwa wanapata chakula cha mchana huku kama kawaida yao wakiendelea kupiga story mbili tatu zinazohusu starehe, na leo walikuwa wanazungumzia kuhusu onyesho la music wa taharab ambalo lingefanyika hapo mess kwa siku za mbele, “hooo! teacher karibu” walinikaribisha wakina Malambo na wenzie kama wanne, hivi, “asante bro, naona nimefika wakati muafaka” nilisema huku na mimi nakaa kwenye moja kati ya viti vilivyokuwa wazi, “ndio mida hii kaka, mwasenga aliniambia ulienda chake” alisema Malambo, wakati huo muhudumu wa pale mess alikuja kuniletea chakula maana hii aina kuuliza utakula nini, kama ni ugali samaki wote ugari samaki kama ni ugali nyama wote ni ugali nyama, wali maharage basi wote mungekula hivyo hivyo, “yah! nilienda kununua mpira kwa ajili ya mazoezi, sema nimechelewa kidogo maana nimekuta maduka yamefungwa, watu wameingia msikitini” nilimueleza Malambo, “ok! huku bwana lazima uende na ratiba yao” alijibu mwingine na wengine wakachangia kidogo ile hoja na baada ya dakika chache wakaendelea na zile story za mwanzo, ni kuhusu hilo tamasha la taarab ambalo lingefanywa na band ya JKU toka unguja, “John unakumbuka mara ya kwanza tulipongia kwenye taarab hapa staring mess, yaani ndio nilianza kupata moyo wa kuishi hapa” alisema mmoja kati ya wale askari ambao kiuhalisia walikuwa ni maafisa wa jeshi wenye kamisheni, “ni kweli Komba, ila kuona mitoto ya kipemba sikuweza kufikilia kama tupo Pemba” aliongea yule alieitwa John kwa sauti fulani ya kusifia na kunifanya na mimi nitamani kuhudhuria tamasha la taarabu, japo moja kabla sijaondoka hapa Pemba, “mimi sikuhangaika na mademu wengine, macho yangu yalikuwa kwa yule demu chotara Senia” alisema Komba, na hapo ni kama wote waliingiwa na utayari fulani, yaani kama aliwavuta fulani hivi, “nakumbuka alikuwa amekaa na shangazi yake meza ya mbele yetu, hakuinuka mpaka mwisho wa tamasha walipoondoka zao” alisema John! Na Malambo akadakia, “ila wakubwa toka nimefika hapa Pemba sijawahi kumuona demu mkali kama yule, yaani ni kisu mpaka nakiogopa” alisema Malambo kwa sauti iliyojaa ukweli wa kile anacho kisema, “unajuwa nini afande yani kuna wakati huwa nawaza mtu anae mvua chupi yule demu, sijui ni waaina gani” alisema mwingine, “ila kiukweli nasikia yule demu hajawahi kuwa na mwanaume” alisema Komba, “ni kweli hata mimi niliwahi kumfukuzia lakini achilia kuto kukubaliwa ile kukutana nae tu ilikuwa inshu” hapo maongezi yakawa juu ya mwanamke huyo anaitwa Senia, ambae alimwagiwa sifa nyingi sana na makamanda hawa wakijeshi kiasi kwamba nilitamani kumuona huyo mschana mzuri kuliko yule jini wakike niliemuona mara mbili, “vipi kaka onyesho linaweza kufanyika hapa?” nilimuuliza Malambo yani afisa utawara, ambae nilikuwa nimekaa nae karibu…..Naam Eric amekutana na mwanamke ambae anahisi kuwa ni jini, unahisi litakuwa jini kweli? na kama ni ndio je limegundua kuwa Eric anaichunguza kesi ya mauwaji anayo yafanya?…… basi endelea kufwatilia mkasa huu hapa hapa JamiiForums
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA: “ni kweli hata mimi niliwahi kumfukuzia lakini achilia kuto kukubaliwa ile kukutana nae tu ilikuwa inshu” hapo maongezi yakawa juu ya mwanamke huyo anaitwa Senia, ambae alimwagiwa sifa nyingi sana na makamanda hawa wakijeshi kiasi kwamba nilitamani kumuona huyo mschana mzuri kuliko yule jini wakike niliemuona mara mbili, “vipi kaka onyesho linaweza kufanyika hapa?” nilimuuliza Malambo yani afisa utawara, ambae nilikuwa nimekaa nae karibu…ENDELEA…..
“yes, JKU wanakuja tena unabahati sana, umekuja tu na wao wanakuja week ijayo” alisema Malambo na kunipa hamu ya kushuhudia music huo, japo kiukweli upenzi wangu juu ya music huo mpaka sasa ni mdogo sana, “tena afande inabidi matangazo yaanze mapema sana nadhani tutakuwa na nyomi la maana hapa” alisema Komba na wenzake wakaunga mkono, “ok! nitamueleza msimamizi wa mess, ili afanye hivyo, apeleke tangazo TV Z, (kwa sasa ZBC) inabidi watangaze kwenye redio na TV”, alisema Malambo huku akiwa na uhakika kuwa kwa kufanya hivyo watapata fedha nyingi sana, “maana watu watajaa sana, halafu bahati nzuri juma tano meli ya vinywaji inatia nanga bandari ya wete” alisema afisa mwingine ambae mpaka muda huu nilikuwa sijamfahamu kwa majina. ******
Yap! Sikukaa sana pale mess kwasababu saa tisa jioni ilitakiwa niende gombani kwaajili ya mazoezi ya mwisho ya kuelekea kwenye mechi ya kesho asubuhi mahali hapo kati yetu, yaani shule ya Fider Castor na ile ya Utahani, hivyo saa tisa kamili nilitoka Green mess kwa lift ya Mwasenga, saa tisa na robo ndio muda ambao nilifika uwanjani na kukuta wanafunzi wakiwa wamesha aanza mazoezi chini ya uangalizi wa mwalimu Aisha, akisaidiwa na walimu waliokuwa wamekuja kutazama mazoezi, “ukimaliza nijulishe nikufuate” alisema Mwasenga wakati anaondoka zake wakati ule nashuka toka kwenye gari la jeshi, niliwaona baadhi ya wanafunzi na walimu waliokuwepo pale uwanjani, wakinitazama kwa macho ya viulizo.
Nakumbuka wakati tukiwa kwenye mazoezi Aisha akaniuliza swali ambalo nahis ni swali lililowasumbua wengi kati yao, kiukweli nilichukuwa sekunde kadhaa kupata jibu la swali hilo, jibu ambalo liliandaliwa toka nikiwa sijajuwa kama kuna safari ya pemba, “hivi Eric, wewe ni mwanajeshi?” ni swali ambalo Aisha aliniuliza bila kujali idadi ya walimu na wanafunzi waliokuwepo karibu yetu, nilicheka kidogo, “mwalimu Aisha kwani kupanda kwenye gari la jeshi ndio mwanajeshi?” nilijibu swali kiujanja ili kupima mauono yao, “lakini Eric achana na kupanda gari la jeshi pia unaishi kwenye nyumba ya jeshi na unakula jeshini” alisema mwalimu mwingine wa kiume, “hivyo ndivyo wizara ilivyoamua kwamba nifikie jeshini kutoka na usalama wangu, si unajuwa kipindi hiki ni cha uchaguzi” nilijibu kama jibu lilivyo pangwa na jopo la wapangaji.
Lakini sasa jibu langu likawa kama limekumbusha jambo, “mh! lakini hatushangai bwana, kipindi hiki cha uchaguzi watu wengi sana huingia kisiwani kwa kwashuguli mbali mbali, sisi tutashangaa tu mara huyu kakamatwa mara huyu amehamishwa na mambo kama hayo” alisema mmoja kati ya wale walimu na wote tukacheka, “jamani naomba ondoeni shaka juu yangu, tena vifaa vya ufundishaji vikiwahi naweza kuondoka kabla ya uchaguzi” nilieleza hivyo huku nacheka kidogo, nashukuru ni kama walinielewa kwa majibu yangu hayo na kubadili maongezi yakabakia kuhusu uchaguzi na nani anafaa kuwaongoza, huku wakikumbushia matukio ya mwaka 2000, ilikuwa hivyo mpaka mida ya saa kumi na mbili pale tulipo tawanyika kwa lengo la kukutana siku inayofuata yaani jumamosi mapema asubuhi pale pale gombani uwanja wa michezo.
Mwasenga alinifuata na gari lake la jeshi, land Rover Defender mali ya jeshi la ulinzi, kisha tukaanza safari ya kuelekea kambini kupitia macho manne na wawi, na wakati tumebakiza kama mita mia moja kuifikia njia panda ya kwenda vitongoji tuliweza kuona magari mawili ya polisi yakitokea upande wa macho manne na kukata kona kwa fujo kufuata barabara kuu, kufuata uelekeo wa Chake, yakiwa kwenye speed kali huku askari wanne kila gari wakionekana wakiwa wameshikilia bunduki zao aina ya SMG, “yaani hakuna kitu nachukia kama uchaguzi, unakuwa na mambo mengi sana hebu ona” alisema Mwasenga, lakini ukweli sikutaka kuamini alichosema, ila nilitamani kufahamu kuhusu lichotokea, lakini sikupata nafasi ya kuuliza wala mtu wakumuuliza, japo ilionyesha kuwa ni wazi kuna tukio limetokea eneo lile la macho manne, maana wakati tunakatiza eneo hilo tuliweza kuona watu wakiwa wamesimama kwa vikundi vikundi kama vile kuna jambo walikuwa wanajadili, “vipi baadae unaingia disco?” aliniuliza Mwasenga ambae alisema kuwa siku ile ya ijumaa pale wawi mesi kuna kuwa na disco, “nitachek kidogo, maana kesho asubuhi kuna mechi pale gombani” nilimjibu Mwasenga huku tukiachana na macho manne, ambapo nikama tiliachana na yale mazingira ya watu kukaa kwa vikundi.
Ukweli japo Mwasenga ambae ni mwenyeji hapa pemba aliepaswa kujuwa tabia na mwenendo wa matukio ya watu wa hapa kisiwani hasa maeneo ya Macho manne wawi chake na vitongoji, kusema kuwa kinachoendelea ni matukio ya kisiasa lakini mimi kwa upande wangu sikutaka kuamini hivyo, ni kutokana na jinsi watu walivyo kuwa makini kujadili walicho kuwa wanakijadili, sikutaka kudadisi sana kwa kuchukulia kuwa haikuwa inanihusu kumbe laiti ningejua.
Saa moja na nusu nilikuwa naingia kwenye ukumbi wa chakula pale Wawi Mess kwa lift ya Mwasenga, ambae tulikubaliana kuwa atanisubiri mpaka baadae nitapo angalia Disco ambalo kama litanifaa nilipanga kubakia mpaka mwisho lakini kama ningeona halinifai ningewahi kwenda kupumzika kwaajili ya kuwahi kesho kwenye mechi ya wanafunzi kule gombani, japo mida hiyo palikuwa kimya kabisa kama siku zote, music ulisikika kwa sauti ya chini ila siku shangaa sana, maana mziki uchanganya mida ya saa mbili baada ya swala ya insha.
Niliingia kwenye ukumbi wa chakula ambako niliwakuta maafisa wajeshi wakiwa wameshaanza kula, jioni hii walikuwa kimya waliongea kwa kupeana nafasi tofauti na nilivyozoea, ukweli nilihisi jambo, nikataazama vizuri na ndipo nilipomuona mzee mmoja wa makamo ambae alikaa kwenye kiti kimoja ambacho toka nimefika sikuwahi kuona kikiwa kimekaliwa, nikatambua kuwa huyu ndie mkubwa wao, na kwa mara ya kwanza nilimuona mkuu wao wa kambi, yaani CO kama unavyoweza kuita kwa kirefu kuwa ni Commanding Office wa kambi la Ally Khamis, ikiwa ni mara yangu ya kwanza kukutana nae, “shikamoo mzee” nilisalimia kwa sauti iliyojaa nidhamu ya hali ya juu, ikiwa ni salamu yangu kwa mkuu huyu wa kambi, lakini nilishangaa kuona mkuu yule wa kambi akinitazama kwa mshangao ungesema nimeingia msikitini na viatu au kanisani huku nimevaa kanzu na balaghashia pasipo kuitikia ile salamu yangu, nikabakia nimesimama nikijiuliza ninastahili kubakia pale au ninatakiwa kutoka mpaka mkuu wao atoke mule ndani.
Lakini wakati najiuliza nikamuona Afisa utawala yaani Luten Malambo, akimtazama CO huku anacheka kidogo, “afande huyu anaitwa Eric Frank, yule mwalimu wa Fidel Castor ambae tuliletewa maelekezo kuwa atafikia hapa kambini” alisema Malambo na hapo yule mzee akanitazama tena na kutabasamu, “Eric unashindwa kusalimia kijeshi?” aliuliza yule mzee ambae niliwahi kudokezwa kuwa anaitwa Inocent Mwanauta, “nitajitahidi mzee nipo na afande Malambo atanielekeza kila kitu” nilisema hivyo huku namtazama Malambo, ambae alinionyesha ishara ya kukaa kwenye kiti cha karibu yake, “ndiyo bwana mwalimu, tena ukipata nafasi uwe unashiriki mazoezi yetu ya michezo, ambayo tunayafanya kila juma nne na ijumaa ili likitokea lolote uweze kujitetea, si unaona mambo yenyewe jinsi yalivyo, watu wanauwana hovyo halafu wanasingizia majini” alisema CO Mwanauta na wote mule ndani wakacheka, na hapo nikaona kuwa nimepata nafasi ya kupata jambo kupitia uzoefu wa huyu mzee, “lakini mzee unadhani ni watu wanajidanganya kuhusu majini?” niliuliza huku nakaa kwenye kiti nilichoonyeshwa na hapo nikaletewa chakula, “lakini hatuwezi kujuwa, ila sidhani kama hizi zinaweza kuwa ni zama za kukimbizana na majini kama enzi za maagano” alisema mzee Mwanauta wenye cheo cha luten Kanali, mwenyeji wa mkoa wa kigoma, hapo wote tukacheka kidogo huku nikipanga swali ambalo litanipa faida katika uchunguzi wangu, hata hivyo nilishangaa sana kwa kaupi ya mzee Mwanauta ambae kiukweli hakuonekana kuamini juu ya uwepo wa majini, wakati mimi mwenyewe nilishuhudia mwanamke wa ajabu masaa kadhaa yaliyopita, lakini kabla sijauliza jambo nikamsikia afisa Komba akiuliza, “ila afande unadhani hili tukio la leo ni jini au kuna mtu amefanya tukio hilo?” kwa swali hilo kengere ya tahadhari ikagonga kichwani mwangu, maana hilo tukio la leo siku lisikia wala kulijuwa ni tukio gani, akadakia afisa mwingine ambae baadae nilimtambua kuwa ni mkuu wa uchunguzi na mahusiano pale kambini kwao, “kwa mujibu wa insp Haroub tukio hilo ni kama lile la Madungu, maana watu waliomuona marehemu mara ya mwisho alionekana akiwa na mwanamke anampeleka nyumbani kwake, na dakika chache baadae wakamuona mwanamke akitoka peke yake na kuondoka zake, akiwa amejiziba na ile minguo yao kama ninja” alisema alijibu yule afisa ambae jina lake ni JC Luge, mwenye cheo cha second lieutinat (luten wa pili) mtu mwenye cheo kama hicho huwa na nyota moja begani mwake, “dah! yule jamaa alikuwa fresh sana, sijui kimemkuta nini” alisema Komba kwa masikitiko, inaonyesha ni mtu wanaemfahamu, “sanaaa jamaa hakuwa na matatizo na mtu” alisema Johh, na hapo zikaendelea hadithi mbili tatu ambazo hazikuwa na faida na mimi katika kazi yangu, nikapata hamu ya kuchunguza zaidi, “sasa kama ni kijana mwenzenu na mulikuwa munafahamiana nae, vyema kama mukienda kuwashika mkono wafiwa angalau kwa dakika chache kisha munarudi” alisema CO, na hapo nikaona ni kama alitoa amri, maana hakuna aliepinga, “nadhani Mwasenga atakuwepo hapa atatupeleka mara moja kisha aturudishe” alisema Malambo ikiwa kama amri ya kuondoka, ukweli niliona kuwa hiyo ni nafasi ya mimi kwenda kupata habari mbili tatu kuhusu marehemu na watu wake wakaribu, inaweza kunisaidia kupata habari muhimu za kiuchunguzi, “vipi naweza kuongozana na nyie” nilimuuliza Malambo, ambae alijibu kuwa ninaweza kwenda nao.
Saa mbili na dakika tano ndio muda ambao tulitoka pale Mess kuelekea upande wa mjini, tulikuwa watu sita, yaani Malambo aliekaa seat ya mbele, dereva wake kijana Mwasenga pia alikuwepo afande komba afande John afande JC, na mimi Mwenyewe, ambao tulikuwa tumekaa nyuma ya gari hilo lenye kuvikwa turubai, ikiwa kama paa lake.
Tulipofika karibu na mjini Chake chake tukaiacha barabara kuu na kuingia barabara ndogo ya vumbi, na hapo kuibukia kwenye mtaa fulani tulivu wenye nyumba kadhaa nzuri za kisasa zilizo jengwa kwa kuachiana nafasi huku baadhi zikiwa na uzio mkubwa sana, zikionyesha ni majumba ya watu wenye fedha ndefu, yaani matajiri, kilicho nivutia ni sehemu moja ambayo tuliweza kupita kijumba kimoja kidogo cha udongo kilichoezekwa kwa bati chakavu kikiwa kimezungukwa na vichaka vya mihogo na miti ya misheri sheri, ambacho kwa usiku huu tuliweza kuona kikiwa kinawaka taa kama sio koroboi ya chemri basi ni kandiri, huku kijumba hicho kikipakana na uzio mkubwa uliopambwa na taa za rangi mbali mbali…..yap! vipi mpelelezi wetu anaweza kuambulia chochote msibani? basi endelea kuwa na mimi katika makasa huu wa
KIFO CHA HAWARA hapa hapa
jamii forums