Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Ndugu wajumbe, ni siku ya pili tunalala usingizi wa mang'amang'amu, wengine wakichungulia na wengine wakiingia kabisa, na hatujapata taarifa yoyote kutoka kwa Bwana Abou Shaymaa mpishi wetu, pengine kuna jambo limempata au kuna tatizo.

Natoa maagizo miana amor hebu mpigie simu kwa sauti ya asubuhi asubuhi ile tamu lakini usiilegeze sana hebu fanya kama unamjulia hali
Majukum tu kiongozi ila nimeruf
 
Ni hadithi nzuri na yenye hamu ya kuifuatilia hata kama mwisho wake unajulikana ukiunganisha dots ambazo ni
  • Familia ya mzee Mohamed babaake Ussi na mjomba wa Seni kuwa na ukwasi lakini haujulikani chanzo chake
  • Kufariki kwa wafanyabiashara vijana tukiacha wa miaka ya nyuma wale wanafunzi
  • Kuacha kwa maabara kuifanyia vipimo miili ya watu wanaokaushwa damu kwa imani ya wanauliwa na jini na polisi kutojishugurisha na cases za aina hiyo
  • Speed aliyokuwa nayo Ussi baada ya Vuai kupita na mwanamke mwenye niqab
  • Mzigo waliomletea Ussi wale vijana wavuvi
  • Ussi kuchelewa kuleta simu baada ya kuambiwa na babaake ili ampigie insp wa jeshi la polisi kuulizia CCTV Cam
  • Kuparang'anyika kwa vitu nyumbani kwa Vuai ikitafutwa HD na mwisho maelezo ya
  • Dogo aliyekuwa akicheza game nyumbani kwa Vuai na ile vesper iliyoondoka speed na alipoingia ndani akaikuta vesper ya Vuai ikiwa imepark.
Haya tuendelee na uhondo ndugu Abou Shaymaa
Ngoja tuone 😅
 
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA KUMI NA NANE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA: “nani atakuwa ameingia chumbani kwangu, au siyo mwanamke?” ndio swali nililo jiuliza, huku napiga hatua za tahadhari kuingia ndani, ambapo mlangoni nikakutana na viatu vya kike, huku arufu ya udi ikizidi kunukia kwa kunguvu, nikajipapasa kwa lengo la kutoa bastora yangu ndogo aina ya A. G. P -5.2mm, lakini sikuwa nayo, hapo nilitaka niachie tusi zito, lakini nilijizuwia kwa kuchelea kumshtua alie kuwa ndani, lakini kwakuwa nilikuwa na uwezo mkubwa wakupambana kwa mikono yangu nika aamua kuingia ndani, “nikafungua mlango haraka na kuingia ndani, ambako nilijikuta nimetoa macho kwa mshangao kwakile nilicho kuona…..ENDELEA……
Mule chumbani “ni wewe?” niliuliza kwa mshangao huku namtazama Maimuna mwanafunzi wa kidato cha tatu, aliejilaza kitandani, huku amevalia kijigauni chepesi sana kama cha kulalia, kilichoishia usawa wa mapaja na kusabisha niweze kuona mpaka sehemu za ndani ambazo zilikaribiana na ikulu ya bibi, kikweli leo ndio niliweza kuona umbo mwanana la mschana huyu, ambalo siku zote lilikuwa linafichwa na baibui, “ndio mie, nimekuja kukuletea nilivyo kuandalia, jana si ulisema siku nyingine” alisema Maimuna kwa kwa sauti fulani iliyojaa aibu, huku anatabasamu na kukwepesha macho kwa aibu, huku nikipata mafasi ya kutazama vyema nywele zake ndefu zenye afya njema, nadhani ni kwaajili ya kufichwa mara kwa mara kwa hijab.
Hapo kwa haraka nikawaza kuwa nilikuwa naingizwa mtegoni, tena mtego wa fumanizi la aibu, nikifikiria kuwa huyu mschana amekuja bila taarifa yoyote, halafu mwalimu Aisha amenifanyia ziara ya kushtukiza, sasa mwingine nani,
anaekuja baada ya mwalimu Aisha, hapo nikatazama kushoto na kulia kuona kama kulikuwa na mtu mwingine mule ndani, ambae yupo kwenye hilo fumanizi, sikuona mtu yoyote zaidi ya mfuko fulani ulio tuna tuna juu ya meza na baibui lake lililotundikwa kwenye hang ya msumari, ambayo hgongwa ukutani, nikatazama dirishani na kumuona mwalimu Aisha anazidi kuisogelea ile nyumba huku anatoa simu na kubofya namba fulani halafu akaiweka sikioni, na muda huo huo simu yangu ikaanza kuita, nilipoitazama nikaona kuwa ni namba ya mwalimu Aisha, “Mai nini hiki, hebu niambie kama upo na mwalimu Aisha” nilimuuliza Maimuna kwa sauti ya chini, “mwalimu Aish?, kwani anakuja huku?” aliuliza kwa shangao na mshtuko, Maimuna, huku anainuka toka kitandani, “sio anakuja ameshafika yupo nje” nilimueleza Maimuna na hapo nikamuona anatazama dirishani, ambako aliweza kumuona Aisha akiwa amesha karibia nyumba ile ya kijani, huku simu ipo sikioni anasubiri nipokee, “mamaaaaa nimekwisha, lakini Ticha kwanini hukuniambia kama unatembea na mwalimu Aisha” alinishutumu Maimuna kwa sauti iliyojawa na uoga wasi wasi na kukata tamaa, huku anainuka na kunisogelea niliposimama, hapo sikuuliza cha kufanya kwa akili za haraka sana nilizo jaliwa, nilipata wazo la kumficha Maimuna bafuni, kwenye bafu ambalo lipo kwenye korido la kutokea nje, na ningemtoa mara Aisha atakapoondoka, niliamini Aisha asongekaa sana, napengine asingeingia ndani.
Haraka nikanyakuwa lile baibui lake na kumkabidhi mkononi, kisha nikamshika mkono na kutoka nae nje ya chumba kicha nikaokota sendo zake pale mlangoni, halafu nikamsogeza kwenye mlango wa bafu na kumfungulia mlango, “tulia humo humo” nilimueleza Maimuna kwa sauti ya chini, ambae kiukweli sasa niliweza kuona tuchuchutwake jinsi tunavyo karibia kutoboa lile gauni jepesi alilovaa na kwa mara ya kwanza nikajihisi dudu ikisisimka, na wakati huo nikamsikia Aisha akibisha hodi, “Eric hodi” wakati huo tayari simu ilishakata, “kwanini ulikuwa unapiga simu wakati umeshafika mwalimu?” niliuliza huku natembea kuufuata mlango wa kutokea nje, ambao sikuwa nimeufunga, “heeeee! Mwenzangu upo na wifi yangu ama, naona kunukia kama duka la udi” alisema Aisha huku anaingia ndani, “hapana mwalimu Aisha, kuna rafiki yangu alikuwa na mgeni mke wake walikuja kinisalimia” nilimueleza Aisha huku tuna tembea kuelekea chumbani kwangu, “ok! nilidhani umeshapata mtoto wa kipemba” alisema Aisha ambae pia, licha ya kuvaa baibui lake jeusi, alikuwa ananukia Udi kama maimuna ambae sasa alikuwa bafuni, nadhani alikuwa anasikia maongezi yetu, na kwakulijuwa hilo nikaamua nimvimbishe kichwa huko aliko, “niombee mema nitaondoka na mwanamke huku pemba” nilisema huku namalizia kwa kicheko, kabla sijakumbuka jambo na kusimama, “utaingia ndani au?” niliuliza huku na mtazama Aisha, ambae alikuwa nyuma yangu, “ndiyo nitapumzika kidogo, leo mimi ni mgeni wako, huko nyumbani washanitibua” alijibu Aisha na hapo nikaona kuwa nimesha kwama, maana nilitegemea Aisha asingekaa kwa muda mrefu angeondoka na mimi ningemtoa Maimuna kule bafuni ili nimpe anacho taka, nilishazama kwenye mtego wake, “hooooo! Karibu sana” nilisema hivyo kwa sauti ya kuchangamka, japo moyoni nilikuwa nina sikitika kwa kutia kitumbua mchanga.
Nilifungua mlango na tukaingia chumbani, “karibu mwalimu, japo kuna kiti kimoja tu” nilimkaribisha mwalimu Aisha, huku napanga panga vitu vizuri, “wala usijali kwanza sie hatukaagi kwenye viti” alisema mwalimu Aisha huku anaweka mkoba wake wakike juu ya meza, halafu nikamuona anakaa kwenye kiti na kuanza kuvua viatu vyake, hapo nikaona ndio nafasi ya kwenda kumtoa Maimuna ili aondoke zake, ikiwezekana nikamle kimoja cha faster, maana toka niingie Pemba, sikuwa nimeusa mzigo, na baada ya kula kitumbua kwa chai ya wima ndio nimtoe, asije kuonwa na Aisha ambae alisema angekaa sana pale getoni, “sorry nakuja” nilisema huku nafungua mlango na kutoka nje kisha nikaufunga mlango, hapo nikaufuata mlango wa bafuni na kuusukuma, kisha nikazama ndani huku nawaza namna ya kumshawishi mtoto huyu wakipemba, anipe Kitumbua.
Lakini ile natazama mule ndani hapa kuwa na mtu zaidi ya harufu ya Udi, “mh!” nilijikuta na guna kwa mshangao, huku natoka haraka nje na kuelekea mlango wa kutokea nje, nilishawaza kuwa pengine yule hakuwa Maimuna ninae mfahamua, ila ni jini lilikuja kuniteka, maana uondokaji wake sikuwa nimeuelewa elewa, lakini moyo wangu ukatulia baada ya kufika nje na kumuona Maimuna akiwa katika vazi lake la baibui anaelekea kwenye kituo cha gari pale karibu na Green House, na yeye ni kama alikuwa anatarajia kuwa nitatoka nikamuona anageuka kunitazama, kisha akanipungia mkono huku anaachia tabasamu pana na mkono wake ukinionyesha ishara ya kuonyesha upande wa mjini, ili maanisha kuwa tutaonana baadae mjini, ukweli nilifarijika sana na kujipa moyo kuwa licha ya kukwepa kikombe kile lakini pia sijamuudhi mtoto yule wa kipemba, ambae alishaniingiza majaribu.
Niliachana na Maimuna ambae alikuwa anasimamisha chai maharage lililokuwa linatokea Vitongoji, mimi nikaingia ndani na kueleka moja kwa moja chumbani, ambako nilikuta mambo ya kusisimua kidogo, mpaka nikajiuliza “hivi hawa watoto wakike wananichukuliaje mimi?” maana nilimkuta mwalimu Aisha akiwa amevua baibui lake na kile kitambaa cha kichwani yaan hijab na kubakia na gauni fupi jepesi, lililoishia katikati ya mapaja, sijui ni kwa sababu toka nimefika huku Pemba sikuona mtu alievalia suruali ya kubana au gauni fupi, maana nilivutiwa na kiasi kidogo cha mapaja ya mwanamke huyu, ambae alikuwa amejilaza kitandani kifudi fudi anatafuna kipande cha keki, nilidhania amenunua akiwa njiani anakuja, sikujali kuhusu alichokuwa anakula, “naona umesha kuwa mwenyeji” nilimueleza Aisha, huku nakaa kwenye kiti pale karibu na meza, wakati huo kwa macho ya wizi nilitazama makalio madogo ya wastani ya mwalimu mwenzangu, “tena nisubiri nini, na nilivyo na mguu mzuri nimekuta na masurufu yameletwa” alisema Aisha, huku anaonyesha keki na ule mfuko uliokuwepo mezani akimalizia kwa kicheko chepesi, hapo ndipo nilipo ukumbuka ule mfuko aliokuja nao Maimuna, “kweli una bahati maana nimeletewa hata mimi mwenyewe sija ufungua” nilisema huku najichekesha kidogo, maana bado nilikuwa katika mshangao, “ndio ufunue uone, yaani vitu vinaletwa chumbani kwako na unaogopa kuvifunua” alisema Aisha, huku akinitazama usoni na macho yetu yalipo kutana alicheka kicheko chepesi cha aibu ya kike, hata mimi nikajikuta nacheka kivivu, “mh! kwani kila kinacholetwa chumbani lazima kifunuliwe?” niliuliza kwa utani huku naufunua ule mfuko, hapo nikaona vitu ambavyo vingi vyake vilikuwa ni vigeni kwangu, ukiachilia keki niliyokuwa naifahamu, pia kulikuwa na vikoro koro vingi sana, ambavyo baadae nilikuja kuvifahamu kwa majina, kama vile kababu, kaimati visheti na vileja, “utaachaje kufunua ingali kitu kipo chumbani kwako” alisema mwalimu Aisha, huku anageuka na kulala chali.
Ukweli lugha ya mwalimu Aisha, ilikuwa tata kidogo, lakini nikajifanya kama sijaielewa na kupotezea, “dah! leo siendi hata mess kula, nitashindia hivi hivi” nilisema huku nadokoa kileja kimoja na kujaribu ladha yake, kilikuwa kitamu sana, “nikitamu” nilisifia huku naachana na ule mfuko kisha nikafunua computer na kuiwasha, “unaona sasa, ungepataje utamu bila kufunua” alisema mwalim Aisha, na hapo nikashindwa kujizuia nikajikuta naachia kicheko, “lugha yako mwalimu, inakuwa na utata kidogo, hasa kwa kule kwetu” nilimueleza mwalimu Aisha nikitegemea angeacha maongezi ya mtindo ule, “walaaa hakuna utofauti wa lugha hapo, Kiswahili ni kile kile, sasa wewe usicho kielewa nini?” alisema kwa utani akiwa bado amelala chali ananitazama ninacho fanya.
Hapo nikaona dawa yake ni kupotezea yale maongezi ambayo niliona yange sababisha niingie kwenye hatari ya kutupiwa jini, kama alivyosema mwasenga, maana huyu ni mke wa mtu, sikujibu tena zaidi nikaweka movie na kwenda kukaa pale kitandani, tukiwa tume kikata kitanda kwa mapana yake, kisha tukaanza kutazama movie kwa pamoja, na baada ya kama dakika kumi hivi huku nikiwa nawaza nia na dhumuni la ujio wa Aisha pale gareen house, “au amekuja kupima uvumilivu wangu?” nilijiuliza kimoyo moyo.
Lakini nikiwa nawaza hilo tukiwa tuna tazama movie, Aisha akaniuliza, “Eric mbona huniulizi kilicho nisibu mwenzio?” hapo niliona dalili ya kwamba ujio wake unaweza kuwa tofauti na nilivyo waza, “he! Mpaka niulize, hapa nilikuwa nasubiri uanze kunielezea” nilizuga kwa mtindo huo, na hapo Aisha akaanza kunieleza kilicho mfanya Aisha kuja kujipumzisha green house, na hapo Aisha akaanza kunisimulia mkasa wake, ambao nitakueleza kwa kifupi, japo ungeweza kuwa wakusisimua endapo ningekusimulia kwa mapana, ila ni nje ya mkasa huu wa KIFO CHA HAWARA
Nadhani unakumbuka kuwa Aisha aliwahi kunieleza kuwa aliolewa akiwa binti mdogo, aliishi kwa muda mfupi na mume wake huyo ambae alimtaliki baada ya Aisha kuhitaji kujiunga na chuo cha ualimu, na baadae akaja kuanzisha urafiki na mwaume mmoja ambae ni askari wa jeshi la ulinzi, mwenye asili ya mkoa wa morogoro, ambae kwa sasa yupo nje kwenye majuku ya ulinzi wa amani, sasa basi sikuchache zilizopita Aisha alikutana na huyo mume wake, ambae sasa ana mke mwingine na kumueleza kuwa anahitaji warudiane.
Aisha kwa kujuwa ana mwanaume wake, ambae akirudi safari yake wanahitaji kufunga ndoa, akamueleza kuwa haitowezekana, maana tayari ana mume na wanatarajia kufunga ndoa, isitoshe kwa sasa anakaa kwenye nyumba aliyopanga mwanaume huyo mtaa wa makondeko pembeni kidogo ya Macho manne, jibu la Aisha alikukubalika kwa mwanaume wake wa zamani, ambae alimfuata tena na kumueleza kuwa ni lazima warudiane, maana asinge weza kumuacha aolewe na wanaume mwingine tena kutoka bara, “nani anaolewa ni mimi au ndugu yako?” alihoji Aisha, kwa sauti iliyojaa hasira.
Sasa leo mapema alipigiwa simu na baba yake kwamba aende nyumbani kwa wazazi wake hao, na alipofika ndipo alipokutanana wazee wawili mmoja wao akiwa ni mshenga wao wa kipindi hicho, wakiwa na baba yake Aisha na mjomba wake, “Aisha kuwa na kazi haiondoa thamani ya mume kwako” alieleza hayo mmoja wa wazee, kati ya wale wawili na mshenga pamoja na mjomba wake Aisha, akaunga mkono kasoro baba yuake Aisha ambae alikuwa amekaa kimya, “inabidi uolewe na bahati nzuri mume tayari unae” alieleza mjomba wake, na hapo Aisha akajuwa kinacho kusudiwa, “lakini yule nilisha achana nae kwa taraka tatu, kidini hawezi kunioa mpaka niolewe na niachike, isitoshe tayari nina mchumba, nasubiri arudi ili tufunge ndoa” alieleza Aisha, na hapo wote watatu wakatazamana, kama wanaulizana jambo fulani, kisha yule mzee akasema, “swala la kuolewa na kuachika wala usiwe na shaka hilo tuachie sisi” maneno ya mzee huyo yaliashiria kwamba wanataka kutengeneza ndoa bandia, “na vipi kuhusu mchumba wangu baba” aliuliza Aisha huku anamtazama baba yake, “ukweli kwa sasa mimi siwezi nikakulazimisha, maana wewe ndie mwenye kuona kama utaishi na mumeo wa zamani au utamsubiri huyu mchumba wako” alisema baba yake mwalimu Aisha, na hapo mjomba wake akadakia, “kwahiyo unataka kwenda bara Aisha” aliuliza mjomba wake Aisha kwa sauti ya hamaki, kitu ambacho kilimfanya Aisha agundue kuwa kuna jambo mjomba wake alishalipanga, nalo ni kwamba aolewe na mwanaume yule yule wa kwanza, “mjomba kwani bara ndio wapi, mbona wao wanaishi huku kisiwani, isitoshe ni nchi moja” alieleza Aisha, na hapo ikaoneka wazi kuwa Aisha akuwa anahitaji kuishi na mume wake wa zamani, “Aisha, wewe bado ni mtoto wetu, hebu kaa na mwenzio mumalize tofauti zenu” aliongea mjomba wake Aisha, “na hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya mwisho kabla ya kuvunja kikao, na mimi kuamua kukupigia na kuja huku kwako” alisema Aisha, ambae nilimshauri kuusikiliza moyo wake.
Tulishinda pamoja pale Green messi, tukila keki na vireja huku tukitazama movie na kuongea hili na lile, muda wote nilikuwa katika wakati mgumu sana, maana kuna wakati hakuweza kuwa makini na kijinguo chake, ambacho kilipanda kwa juu na kuacha sehemu kubwa ya mapaja ikiwa wazi, sijui nilikuwa na kiu ya kiwango gani, maana kuna wakati dudu ilivimba kiasi cha kitambaa chepesi cha track kushindwa kuzuia muonekano ule, na kuonyesha wazi ramani ya dudu ilivyo jitutumua.
Mida ya saa kumi kasoro ndio mida ambayo mwasenga alinipigia simu kuwa ananifuata kwaajili ya kunipelea mazoezi, japo leo sikuwa naenda kufanya mazoezi zaidi ya kutazama mpira, hivyo tukajiandaa na kusubiri usafiri ambao haukuchelewa sana, ulikuja na sisi tuka panda gari na kuelekea mjini, tukiwa mimi na Aisha ambae aliamua kushinda nje ya nyumbani kwake kutwa nzima na kurudi usiku.******
Naam uwanjani palikuwa pamejaa sana watu, tofauti na siku nyingine zote nilizowahi kuja hapa, ilikuwa tayari mwasenga alisha tushusha toka kwenye gari, karibu na usawa wa geti la Chake chake Hospital tukaingia eneo la uwanja na kutafuta sehemu ambayo tungeweza kutulia na kutazama mpira pasipo kizuwizi chochote, tukaenda kukaa kwenye ukuta wa ofisi za KVZ, ambao umekaa kama ngazi fulani, tulikuta mechi imeshaanza dakika chache zilizopita.
Wakati tuna endelea kutazama mpira, ambapo timu ya Chake, ile ninayofanya nayo mazoezi ikiwa inashambuliwa na kupunguzwa vikapu, mara nikamuona Seni, yule mwanamke mzuri kuliko uzuri wenyewe, ambae alikuwa anaingia pale uwanjani akitokea kule upande wa mjini, yani Marikiti, “Aisha unamuona yule mwanamke?” nilimuuliza Aisha huku namuonyesha kule tuliko ingilia sisi, ambako Seni alikuwa anatokea, “nani Jessenia, namfahamu sana, tulisoma wote Masingini primary, vipi ushampenda, utamuweza lakini mjomba wake tajiri mkubwa” alisema Aisha, akiongeza hata maneno ambayo haya kuwepo, “dah! basi mwenzio siku ya kwanza nilijuaga ni jini” nilimueleza Aisha ambae nilimsimulia mkasa wangu ulivyo kuwa, ila sikumueleza kama mimi ni mpelelezi, Aisha alicheka muda wote wakati namsimulia, hata wakati namaliza kusimulia aliongeza kicheko kwa nguvu, hata baadhi ya watu walimtazama kwa mshangao, na bahati mbaya hata Seni au Jessenia nae aligeuka kututazama, hapo nilitamani kumshtua Aisha aache kucheka, lakini nilishachelewa, maana nilimuona Jessenia akigeuza uso wake kututazama na hapo nilikutana nae macho kwa macho nikamuona anatabasamu, na usiombe kumuona wakati huu, maana lile tabasamu angavu kama jua la asubuhi nyakati za kipupwe (msimu wa baridi) watu wachache walio
mtazama walijikuta wakisahau kuhusu kicheko cha Aisha na kumtazama Seni, ambae sasa alikuwa anatembea kuja pale tulipokuwa tumekaa…… jibu utalipata kwenye sehemu inayofuata,.....



KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA KUMI NA TISA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE: Aisha alicheka muda wote wakati namsimulia, hata wakati namaliza kusimulia aliongeza kicheko kwa nguvu, hata baadhi ya watu walimtazama kwa mshangao, na bahati mbaya hata Seni au Jessenia nae aligeuka kututazama, hapo nilitamani kumshtua Aisha aache kucheka, lakini nilishachelewa, maana nilimuona Jessenia akigeuza uso wake kututazama na hapo nilikutana nae macho kwa macho nikamuona anatabasamu, na usiombe kumuona wakati huu, maana lile tabasamu angavu kama jua la asubuhi nyakati za kipupwe (msimu wa baridi) watu wachache walio
mtazama walijikuta wakisahau kuhusu kicheko cha Aisha na kumtazama Seni, ambae sasa alikuwa anatembea kuja pale tulipokuwa tumekaa.....ENDELEA….
Sijui ni kwanini moyo wangu ulilipuka kwa mshtuko na hofu ya kushindwa kumkabiri mwana dada yule, mwenye urefu unaofaa kuwa miss fulani, nikajifanya napotezea kwa kutazama uwanjani, ambako bado chake chake walikuwa nyuma sana kwa point, bahati nzuri wakati huo huo nikasikia “Pross vipi, mbona umekaa huku, twende ukaokoe jahazi” nilisikia sauti kwa mbali ambayo mwanzo sikujuwa kama ananisemesha mimi, maana jina jilo la bandia sikuwa makini nalo, “sijui anakusemesha wewe” alinishtua Aisha, na hapo nikagutuka na kumtazama msemaji, alikuwa ni mmoja kati ya watu ambao tunafanya nao mazoezi, “njoo basi Pross” alisisitiza yule jamaa na mimi nikaona afadhari, hivyo nikainuka na pale nilipokaa huku moyoni nikifurahi kupishana na Seni, japo sikuwa na kifaa chochote cha michezo zaidi ya viatu nilivyovaa aina raba.
Dah, kwanza kabisa kabla Seni hajatufikia, ilitangulia harufu nzuri ya perfume, ambayo sikuijali sana, nikapiga hatua kuondoka hapo, lakini Seni hakuniacha nipite bure, “Pross ukatuokoe huko naona tuna bugizwa vikapu kama watoto” alisema Seni kwa sauti yake tamu, iliyojaa utani huku anaachia tabasamu pana mfano wa watu tunao fahamiana, sikushangaa kwa yeye kutaja jina la Pross, kwasababu jana alisikia wakiniita hapa hapa mazoezini, siku jibu kitu zaidi ya kucheka kidogo, nikiashiria kuwa ujumbe wake nimesha upata, huku namtazama usoni, hapo nilieweza kuiona sura yake vyema kabisa, hakika huyu mwana dada ukiachilia uchotara aliokuwa nao, pia alikuwa mzuri sana, halafu licha ya ucheshi wake alikuwa ni mwenye aibu ya haraka, maana alitabasamu tena na kukwepesha macho yake kumtazama Aisha, “niambie Aisha asalam aleykum” alisalimia Seni, na mimi sikuwajali tena, nikaondoka zangu kuelekea alipokuwepo yule jamaa alieniita akiwa amekaa pamoja na baadhi ya wachezaji wengine.
“vipi kaka umekuja na vifaa?” aliniuliza mmoja wao, “hapana sikujuwa kama nitacheza” nilijibu hivyo, huku najaribu kutazama kule nilikotoka, yaani kule nilikomuacha Aisha, nako nikamuona Aisha na mwanadada Jessenia, aliekuwa amekaa pale nilipokuwa nimekaa mimi, huku wakiongea kwa furaha na vicheko, ilionyesha wazi kuwa wanafahamiana vyema na kunifanya niamini kama ni kweli walisoma pamoja, “hii ni mechi ya kirafiki sio ligi, unaweza kucheza tu” alisema yule alieniita, na yule Seleman akadakia, “lakini si kuna jezi mbili zilibakia, raba anayo mpeni haraka aingie” sikuwa na pingamizi kuhusu kuingia uwanja, hivyo nikapewa jezi na kuonyeshwa sehemu ambayo naweza kubadilisha nguo.
Naam nilipata nafasi ya kuingia ndani nakuanza kucheza mpira, nikiitendea vyema nafasi yangu, ambapo licha ya kuwa siku zote nacheza kama mshambuliaji Big, lakini kwa leo kutokana na viwango vya wapinzani nilijikuta na nacheza Big na defender, nilianza kurudisha vikapu kwa speed ya ajabu, nakujikuta nikijizolea mashabiki wengi ndani ya siku moja tu, nilipenda sana mechi hii, ambayo licha ya kuwa mechi lakini niliweza kufanya ninachotaka, japo ni mbaya sana kwa afya ya michezo kucheza na watu ambao kiwango chao kipo chini, unaweza ukajikuta na wewe unashusha kiwango kwa kupenda kuanguashia wasio juwa, huku wakati mwingine tabasamu la Seni likinijia kichwani mwangu.
Niliendelea kucheza huku tabasamu la Seni likiendelea kujirudia kichwani mwangu, mara moja moja nilitazama kule walikokaa, na kuwaona wakiendelea kuongea huku wakicheka kwa pamoja kama marafiki ambao mara kadhaa niliweza kusikia sauti zao wakisifia au wakishangilia kile nilichokifanya kwa wakati huo, kiwe kikapu au chenga na manjo njo yoyote ambayo ninge yafanya, japo sio peke yao waliokuwa wanashangilia, nilishangiliwa na ila mtu alie kuja kuishangilia timu ya chake, ata wale wa timu ya mkoani, niliwaona wakipeana ishara, kwa kukubali kile ninacho kifanya pale uwanjani, hasa kipindi timu yetu ilipofikia point zao na kuwapita.
Wakati mpira unaendelea niliweza kutazama nyumbani kwa kina Maimuna, ambapo nilimuona akiwa na mdogo wake Yasin, Maimuna alinipungia mkono kwa nguvu, akionyesha mwenye furaha kubwa, niliishia kutabasamu tu, huku naendelea kucheza, “jamani msimuache kwenye timu yetu ya pemba, safari hii unguja watatutambua” alisema mmoja wa wachezaji wa timu ya mkoani, mara baada ya mpira kumalizika, huku ananipa mkono wa hongera ya ushindi wetu wa point Themanini kwa sitini na nne tulivyo wachapa.
Kama ilivyo ada adhana iliposikika tu, watu walitawanyika kwa dakika sifuri, na pale tuka bakia mimi na Aisha tu, hata Seni alikuwa amaesha ondoka zake, nilibadili nguo na kubeba zile jezi kwa miadi ya kurudisha siku inayofuata mida ya mazoezi, maana ilinilazimu kwenda kuzifua kabla sijazirudisha, tuliondoka taratibu pasipo kumuona Maimuna, nadhani alimuogopa mwalimu Aisha, “basi huwezi amini Aisha, yaani nikipita humu mida ya kurudi, huwa nahisi muda wowote jini linaibuka” nilimueleza Aisha, mara baada ya kuupita msikiti, hapo Aisha akaanza kucheka kwanguvu, “unajuwa nilipomsimulia Seni, amecheka sana, anasema ni kweli alikuona siku moja unamkimbia, sasa akaniuliza kwanini ulimfananisha na jini” alisema Aisha, huku anamalizia kicheko chake, ukweli hapo nilijihisi aibu kubwa sana usoni mwangu, “kha! Kwanini sasa ulimsimulia upuuzi kama huo?” niliuliza kwa mshangao na fadhaha, “alikuwa anauliza maswali mengi kuhusu wewe, sijui amekupenda yule, ndio maana nikamueleza kuwa ulimfananisha na jini” alisema Aisha, wakati huo tunaendelea kutembea na kusikilizia gari kama lingetokea muda wowote, “angekuuliza kwanini ungemjibuje?” nilimuuliza Aisha kwa mshangao, moyoni mwangu niliona kosa nililo lifanya kumsimulia mwanamke huyu juu ya upotofu wangu wa fikta juu ya Jessenia, “aulize?, mwenzio alishauliza zamani hizo, nikamwambia kwa sababu ya uzuri wako, na isitoshe wewe ni mgeni hapa pemba” alisema Aisha, na wakati huo tukaliona gari la jeshi linakuja, “mh! yeye akasemaje?” nilimuuliza Aisha, huku nikilitazama gari ambalo lilikuwa linatupita kwa lengo la kwenda kugeuza ili kuja tupande, “alicheka tu na kuendelea kuulizia habari, mara hoooo! vipi yule ndie shemeji au, anakaa wapi, anafanya kazi wapi?” alisema Aisha, na wakati huo gari lilikuwa linasimama karibu yetu, tukaingia ndani ya gari na Mwasenga akaondoa gari, “nipe matokeo bro” alisema Mwasenga, na mimi nilimpatia matokeo ya mechi, huku Aisha akimimina sifa juu yangu, mpaka tulipomuacha macho Manne, na yeye kuelekea kwenye nyumba anayoishi, na sisi kuelekea Ali Khamis camp, ambako nilioga na kufua jezi, kisha nikaondoka na mwasenga kurudi Wawi, yaani Messi ambako nilienda kupata chakula cha jioni, huku mara kwa mara Tabasamu la Seni na kile kijiaibu chake kikiendelea kunijia kichwani, na kunifanya nianze kumtamani mwanamke huyu ambae sasa nilikuwa na uhakika kuwa sio jini.
Saa mbili na robo, ndio mida ambayo nilikuwa naingia ukumbini, nilimkuta Mwasenga anaongea na bwana Ussi Juma Mohamed aliekaa na mwanamke fulani, ambae sie yule wa jana, kwenye meza yake ile ile ambayo siku zote huwa kwenye kona iliyojificha, na kunuruliwa na mwanga hafifu, nilipita pale na kuwasalimia pia, “hooo! kaka mambo vipi, naona upo kama kawaida yako” alinisalimia kwa uchangamfu bwana Ussi, mara tu baada ya kuniona, “shwali kaka, si unajuwa tena hapa ndio kwa mama, lazima nije kupata chakula cha jioni” nilijibu kwa uchangamfu pia, “nasikia leo umekinukisha vibaya sana pale tenes (pale kwenye uwanja wa mpira wa kikapu)” alisema Ussi ambae, kiukweli sikuwa nimemuona uwanjani, “kidogo tu, tulikuwa tuna wafundisha mpira” nilisema huku nacheka kidogo, kisha mimi na mwasenga tukaenda kukaa kwenye meza moja, ambayo ilikuwa mbali kidogo na ile ya Ussi, ikiwa ni chaguo langu, maana kuna maswali nilihitaji kumuuliza Mwasenga, sikutaka Ussi asikie hata kwa bahati mbaya.
“leo nimemuona yule mwanamke kwa karibu, ni chuma vibaya sana” nilimchokoza Mwasenga, wakati tukiwa tumesha pata bear kadhaa, “nani yule Ticha, halafu umenikumbusha, unajuwa kuwa yule ni demu wa soja mwenzetu?” alisema Mwasenga akimaanisha mwalimu Aisha, “hapana kaka, yule demu sina mpango nae, namzungumzia Seni” nilifafanua kwa Mwasenga, ambae alicheka kidogo, “kaka kabla ya yote hebu nikudokeze kidogo juu ya huyo mwanamke” alisema Mwasenga huku anajiweka sawa, na kuchukuwa chupa yake ya bia nakupiga funda moja, ukweli nilipatwa na msisimko wa kufahamu mengi kuhusu Seni, unajuwa nini, nilihisi kuwa Mwasenga atanieleza mambo mazito kuhusu Jessenia.
Mwasenga akaweka chupa mezani na kujiweka sawa, “unajuwa nini kaka, kwanza mjomba wake anafedha nyingi sana, pia yule demu haingiliki kirahisi, wale makamanda unao kula nao kule ndani wote walisha mtokea yule demu na amewamwaga, sio yeye tu, masoja kibao walishamfukuzia nao pia walimwagwa” alieleza Mwasenga, na hapo nikapata shaka kidogo, kwanini mwanamke mkubwa kama huyu asiwe na mpenzi, kama asingekuwa amesoma na Aisha ninge hisi ni jini, na yale matabasamu yake ambayo yana nichanganya kuwa ni mtego wa kuninasa ili kuniuwa na mimi nishindwe kuendelea na upelelezi, “hivi wazazi wa Seni nao ni matajiri au wa kawaida” nilimuuliza Mwasenga ambae hakupata shida kupatia jibu, “mh! wazazi wake siwajui, namjuwa mjomba wake, huyu binamu yake na shangazi yake basi” hilo ndilo jibu la Mwasenga.
Sikutaka kupoteza muda mrefu pale Messi, nikamuomba mwasenga anipeleke camp, na aliponifikisha nilimpatia elfu kumi ili akaendelee kupata bia, nilifanya hivyo kwasababu yeye alikuwa ananisaidia usafiri, si unajuwa katika mkataba wangu wa kuhifadhiwa na jeshi, haukuushisha usafiri, hivyo yeye alikuwa anajitolea tu kunisaidia, japo pia luten Malambo yaani afisa utawara wa Ali Khamis alitoa maelezo ya kusaidiwa usafiri pale nitakapo hitaji.
Nilijiegesha kitandani huku nikitafakari mambo ya kutwa nzima, kuanzia yule binti Maimuna, kisha ujio wa Aisha na kisa chake, “ina maana Maimuna alikuja kuliwa au!?” niliwaza kuhusu Maimuna, ambae ni mwanafunzi wangu, “na kama ni hivyo inamaana yeye sio bikira, au alikuwa tayari nimtoe bikira, na kama ningemtoa bikira yake unadhani ingekuwaje pale ambapo angejuwa kuwa sikuwa muoaji” niliendelea kuwaza, mpaka niliposhtuliwa na mlio wa simu, nilipoitazama ilikuwa ni namba ngeni, tena ni mtandao ambao makao makuu yake yapo katika visiwa hivi, ndivyo tulivyo watu wengi tulivyo amini.
Nikaipokea ile namba, nilidhania ni simu toka kwa Aisha, pengine ametumia namba ngeni, maana sikukumbuka kama kuna mtu mwingine nimempa namba yangu ya simu, “asalam alaykum Pross” nilisikia sauti ya kike, nyororo tulivu ya chini, ambayo ilitawaliwa na lafudhi ya kipemba, ilinishtua sana, maana haikuwa sauti ya Aisha, na wanawake naokumbuka wanalijuwa jina la Pross ni wawili tu, yani Seni na Maimuna, “waalaykum salam, habari yako?” niliitikia nasalimu pia, “habari yangu mbaya, nilipatwa na msiba, kwanini hukuja dukani siku mbili hizi?” ilisikika ile sauti ambayo ilikuwa inaongea kwa utulivu kama vile hakutaka kumsumbua aliekuwa pembeni yake, au hakutaka mtu mwingine asikie sauti ambayo mpaka hapo nikajikuta natamani kujipiga kibao kwa usahaulifu, na kosa nililolifanya la kutoa namba ya kweli kwa mwanamke ambae nilikuwa nahitaji habari, tena kwa muda mfupi tu, “hooooo! Pole sana Saphia, umefiwa lini, na nani?” nilimuuliza Saphia, yule mwanamke muuza duka la urembo na perfume, “yani siku ile ile tulipoachana pale dukani, mimi naenda msikitini, tunarudi nyumbani hatujakaa sana, tunaletewa taarifa ya msiba yule kaka yangu Masoud,
niliekuambia anakaa macho manne Masikini ajengi” alisema Saphia hapo nilijikuta nashtuka na toa macho ya mshangao, “ina maana yule kaka yako ulie niambia ndie marehemu Masoud Vuai?” niliuliza kwa mshangao na mshtuko mkubwa kiasi cha kumshangaza hata Saphia mwenyewe…… endelea nayo....



KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA ISHILINI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA: “hooooo! Pole sana Saphia, umefiwa lini, na nani?” nilimuuliza Saphia, yule mwanamke muuza duka la urembo na perfume, “yani siku ile ile tulipoachana pale dukani, mimi naenda msikitini, tunarudi nyumbani hatujakaa sana, tunaletewa taarifa ya msiba yule kaka yangu Masoud,
niliekuambia anakaa macho manne Masikini ajengi” alisema Saphia hapo nilijikuta nashtuka na toa macho ya mshangao, “ina maana yule kaka yako ulie niambia ndie marehemu Masoud Vuai?” niliuliza kwa mshangao na mshtuko mkubwa kiasi cha kumshangaza hata Saphia mwenyewe……ENDELEA…….
maana sikutegemea kama Masoud Vuai angekuwa ndie kaka yake Saphia, “ndie haswaaaa, kwani wamfahamu?” aliuliza Saphia kwa sauti ya mshangao na mashaka, “namfahamu, hata siku ile nilikutana nae akiwa anaelekea macho manne” nilimjibu Saphia, ambae nikama alifarijika fulani hivi, “kumbeeee unamfahamu, basi huyo ndie kaka yangu na alikuwa huyo huyo” alisema Saphia, ambae kiukweli licha ya mshangao nilioupata lakini nilimuonea huruma sana Saphia.
Hapo nikataka kujuwa kama na wao wanaamini kuwa ni jini ndilo lililo muuwa Masoud, “samahani Saphia, naweza kukuuliza swali kama hautojali?” nilimuuliza Saphia kwa sauti ya upole na utulivu, “we uliza tu, nikiweza nitakujibu” alijibu Saphia huku anajichekesha kivivu, “hivi mume weza kujuwa sababu ya kifo cha Masoud?” nilimuuliza Saphia kwa sauti fulani ambayo ilikuwa kama ina mtega, “mh! hayo sio ya kuzungumzia usiku, maana hawa wadudu wana masikio marefu, wanasikia kila pahala” alisema Saphia, na hapo nikajuwa alikuwa anamaanisha nini, “ina maana mulienda kutazama kwa talaamu yoyote?” nilimuuliza Saphia nikimaanisha kuwa wameenda kwa mganga yoyote, “mh! nani ajisumbue wakati inafahamika kuwa sio yeye ndie wa kwanza kukutana na jini hilo” alisema Saphia ambae mpaka sasa bado alikuwa anaongea kwa sauti ya chini, “hebu nikuulize kitu, hivi Masoud hakuwa na adui yoyote?” nilimuuliza Saphia, ambae alijibu bila kuchelewa, “wala hakuwa na uadui na mtu” hapo nikavuta pumzi na kuzishusha, ili kumpa nafasi ya kujiandaa kupokea swali, “je unamfahamu mwanamke ambae alikuwa anatembea nae au alikuwa anamtongoza labda kwa nia ya kumuoa au tu alikuwa nae karibu sana” nilimuuliza tena Saphia.
Hapo nikaona kama anavuta kumbukumbu fulani kabla hajajibu, “mh! kwa kweli alikuwa anaongea na wanawake wengi sana, kwa sababu yeye ndie alikuwa anakaa dukani, na pale wateja wengi ni wanawake, lakini kuhusu kuwa na mwanamke, kuna siku alisema kuwa hivi karibuni atatutajia mchumba wake na ataenda kumtolea barua” alisema Saphia, ambae alikiri kuwa hakuwa anamfahamu mwanamke huyo ni nani, “hapo nikaona nimuulize swali moja la mwisho, kabla hajanishtukia, “halafu nimekumbuka, hivi kuna mzee mmoja hivi nilimuona hapo msibani kwenu, ana alama za makovu kichwani unamfahamu?” swali hilo lilimshtua kidogo Saphia, ambae alijibu kwa wasi wasi, “weeee, kwanini unamuulizia usiku huyo mzee Mangeu?” aliuliza Saphia kwa sauti iliyojaa uoga, hapo nikatabasamu kidogo, kwa maana niliamini kuwa naweza kupata dondoo muhimu, “kwanini unasema hivyo kwani unamuogopa?” nilimuuliza kama vile sikujali alicho kisema, “hapana, ila ni mazoea tu” alisema Saphia, ambae alinieleza kwa mapana kuwa, mzee Mangeu au mzee Zidadu Makame, hutumika kwa kazi kunyamazisha watoto wao wanapolia au kukataa chakula, “nitamuita Mangeu akuchukue” ungekuta mzazi anamuambia mtoto kama vile anamtisha, Saphia aliendelea kueleza kuwa mzee Mangeu, ambae anaishi pake yake pale msingini, kila mmoja anamchulia kama mtu wa ajabu na wakugofya , japo nimshiriki mzuri kwenye shuguri za kijamii, ni mtu ambae hajawahi kuonekana kuomba chochote kwa mtu yoyote, japo hakuwa na kazi yoyote zaidi ya kilimo alichokuwa anakifanya kuzunguka nyumba yake, hakuwa na ndugu wala rafiki au mtu wa karibu, “watu wanahisi anafuga majini, maana hawezi kuwa anaishi peke yake kama mwanga” alimaliza Saphia kunielezea, “hivi Saphia unafahamu yale makovu ni ya nini?” nilimuuliza Saphia kabla hatujaagana nae akasema kuwa hakuwahi kusikia habari yoyote kuhusu yale makovu, maana amepata ufahamu wake akimkuta yule mzee yupo vile vile.
Naam nilimaliza kuongea na Saphia kwa ahadi kwamba akifungua duka atanijulisha niende kumsalimia, huku akisisitiza kuwa yeye ndie atanipigia simu, maana bado hakuwa na simu, ukweli nilitulia kitandani nikiwaza ile hadithi ya mzee Zidadu Makame, nilichanganua sana na kuwaza ili na lile, na mwisho nikapitiwa na usingizi.*******
Muda nilipitiwa na usingizi sikuukumbuka, ila nilishtuka baada ya kuona mwanga wa jua uliopenya madirishani na kuangazia ndani, ya chumba changu, ambacho bado kilikuwa kina mabaki ya arufu ya Udi, maana haikuwa kidogo, mchanganyiko wa marashi ya wanawake wawili, yaani Aisha na Maimuna, nilipotazama muda ilikuwa ni saa moja kasoro, nikaamka na kujiandaa kisha nikaenda zangu shuleni, ambako nilikuta ujumbe kuwa nahitajika ofisini kwa head Master, yaani mkuu wa shule, nikafanya hivyo, “hongereni kwa ushindi mkubwa mulio upata, tumeangushwa kidogo na timu ya wavulana” alisema Head master, mara baada ya kusalimiana nae, “usiwe na wasi wasi mwalimu, nadhani kama nitakuwepo kwa muda mrefu hapa, na hakika timu inakuwa vizuri sana mechi ijayo” nilijisifu mbele ya mwalimu mkuu, ambae aliniahidi ushirikiano, halafu tukaagana kisha nikaelekea ofisini na kuungana na wenzangu waliokuwa wamejazana staff office, “asalam alaykum Eric” kila mmoja alinisalimia nilipoingia ofisini, ambako sikumkuta mwalimu Aisha, ambae alikuwa tayari amesha elekea kwenye kipindi, nilikaa ofisini huku nawaza juu ya tabasamu la Seni, ambalo lilinifanya niamini kuwa pengine lilikuwa ni lakunivuta karibu yake, maana lilinivutia na kunichanganya, ukizingatia lilimfanya azidi kuwa mzuri sana, kila nilipo jaribu kuondoa kumbu kumbu hii kichwani, niliweza kwa dakika chache, napengine mawazo yangerudi kwa haraka na kwa nguvu mpya, ila kiukweli Jessenia ni mwanamke mzuri zaidi ya uzuri wenyewe.
Nilikuja kukutana na Aisha mida ya saa nne, alipomaliza vipindi vyake na tuka ungana kwa kifungua kinywa “niambie Eric za toka jana” alisema Aisha, wakati tuna pata supu kwenye mgahawa wa pembeni ya shule, ni ule ambao tunaendaga siku zote, “freshi hofu ilikuwa kwako Aisha” nilimtania Aisha ambae huwa hakosi jibu la pale kwa pale, “mh! unihofie mie mweusi kama baibui, baada ya kumuwazia Jessenia mtoto mweupe wa kiarabu” hapo tukacheka kidogo, Aisha hakujuwa kama jibu lake lilikuwa faida kwangu, “nataka nifike kwa wazazi wake nikatoe mahari” nilimueleza Aisha, kwa sauti iliyojaa utani, lakini moyoni nilihitaji jibu fulani toka kwa Aisha, “mh! utaweza wewe kumchumbia Seni, na mjomba wake alivyo tajiri vile” aliuliza Aisha kwa sauti ile ile iliyojaa mzaha, “ndio maana nime sema nitaenda kwa wazazi wake na sio mjomba wake, au wazazi wake ni matajiri pia?” niliuiza kwa namna ile ile ya utani, “mh! Hata najuwa basi, hata wazazi wake sijawahi kuwa sikia, na kama yupo basi ni mama, ambae atakuwa mswahili, si unajuwa kuwa mtoto ni africast yule” alijibu Aisha likiwa ni jibu la pili kuwa hakuna anae fahamu wazazi wa mwana dada Jessenia, “yani mtu umesomanae toka darasa la kwanza mpaka secondary na usimjue hata mama yake, au hakuwa rafiki yako?” nilimuuliza kwa kumtega Aisha, nae akafunguka, “weeee! Kwani alikuwa na rafiki enzi hizo?, alikuwa mnyonge mpole yaani amekuja kuchangamka ukubwani, tena tuna karibia kumaliza kidato cha nne” alisema Aisha, na hapo nikatulia kidogo nikitafakari kuhusu majibu na maelezo ya Aisha, nikaona kama vile haya jitoshelezi kama nilivyo hitaji, maana nilihitaji kufahamu undani juu ya Jessenia, kama kweli ni binadamu au jini, maana hakutaka kutoka kichwani mwangu, “inashangaza kidogo, maana nikiangalia yeye hafanani na ndugu zake, yaani ni vitu viwili tofauti kabisa, nilipenda kufahamu mama yake anafanana naje” nilimueleza Aisha, ambae alisisitiza kuwa hajawahi kusikia habari za mama yake Jessenia, na wakatia huo huo Aisha akaonekana kukumbuka jambo, “halafu we mwanaume una roho ngumu kweli kweli, yaani ijumaa kuna onyesho la Taarab na unashindwa kunijulisha” alilalamikika Aisha, ukweli nilisha sahau juu ya jambo hilo, na sikutegemea kama Aisha angeongelea, “mh! hivi na wewe unaendaga mess?” milimuuliza Aisha huku nikijifanya nashangaa, japo nilisha ambiwa kuwa panapo onyesho la taarab kila kitu huwekwa pembeni, na wapemba kujimwaga ukumbini kucheza taarab, “nisende kwani sina miguu?” jibu lake lilikuwa fupi sana, ambalo lilifuatiwa na maagizo, “tena ukae ukijuwa tutakuwa sote, mguu kwa mguu, utakapokaa wewe na mimi nipo” mpaka hapo nikajuwa kuwa atakuwa mgeni wangu, nilijikuta na furahia agizo lile na kuona kwamba nitakuwa na mtu wakuzugia zugia.*******
Naam Saa sita mchana, wakati wa mapumziko ya dakika Tano, niliamua kuaga kwa kisingizio cha kuwa kichwa kina niuma, na kwamba naenda nyumbani kupumzika, lengo langu likiwa ni kwenda kupumzika kidogo na kutafakari mwenendo wa upelelezi wangu, toka nilipo anza mpaka nilipo fikia leo hii, maana ilikuwa ni vigumu sana kuunga nisha matukio kwa haraka,
Lakini wakati natoka ofisini nikiwa na mwalimu Aisha, ambae nilikuwa naongea nae hili na lile, huku wanafunzi wakiwa wamzagaa kwenye vibaraza vya majengo ya madarasa, ndipo nikamuona mtu ambae ni kama nilimsahau kidogo, alikuwa ni Maimuna ambae alikuwa amesimama kwenye kibaraza cha darasa la kidato cha tatu pamoja na waschana wenzake, ameshika kitu kama mfuko mdogo uliokunjwa na kujaa mkononi, ni mita kama thelathini toka pale nilipo kuwa, muda wote macho yake yalikuwa kwangu, hata nilipomtazama nilimuona akijitabasamulisha na kuanza kutembea kueleka upande wa vyooni, “Aisha usitembee kwa haraka, kuna kitu nataka nikuulize” nilimueleza mwalimu Aisha, ambae aliganda kama sanamu, “he! Umeanza umbea una nini lakini weye?” aliuliza Aisha, ambae sasa alikuwa anazungusha macho kama kinyonga, ni wazi uzalendo ulimshinda, “kuna mwanafunzi anaelekea upande wa vyoon, mtazame kisha achana nae” nilimueleza mwalimu Aisha, ambae alijifanya kama anajinyosha kisha akamtazama Maimuna ambae alikuwa bado hajafikia jengo la choo cha wanawake, huku ameshika mfuko wake mkononi, “nani Maimuna?” aliuliza Aisha, huku akipotezea kutazama kule chooni, “yes, vipi tabia za huyu mwanafunzi, namuona kama ni mapepe sana” nilimuuliza Aisha, ambae kama kawaida yake huwa hakosi jibu, “mh! ila weye nakutilia mashaka, yaani maswali yako tote yana maana, yaani utasema mpelelezi wa FBI” alisema Aisha, na wote tuka cheka, “kwani vibaya kujuwa tabia za wanafunzi” niliuliza kwa sauti iliyojaa utani, “sawa hebu nikueleze basi, kwa hapa shuleni ni binti mstaarabu kwa kweli huwezi kumuona akiranda na wavulana wala kusimama nao, ila kwa nyumbani kidogo mchangamfu, utamkuta anataniana na wale vijana wa pale tenes, (pale kwenye uwanja wa baskert) hata kule tibilinzi (uwanja unaotumika kwa burudani wakati wa sikukuu, hasa eid) utamuona anavyo jichetua, yani ana mambo ya kijitu kizima huyu mtoto mpaka utashangaa” alisema Aisha, ambae Kiswahili chake sijawaji kukichoka, huku tunatazama upande wa choo cha waschana ambako, tuliweza kumuona mschana yule ambae tayari alikuwa amesha kifikia choo na akuingia ndani baada yake alizunguka nyuma ya choo hicho kilichopakana na msitu, “haya bwana ngoja nikajipumzishe kijitu kizima” nilisema hivyo huku nacheka nakundoka zangu nikimuacha Aisha anarudi ofisini na yeye anacheka kidogo, na kabla sijafika mbali nikasikia kengere inalia ni wazi muda wa mapumziko ulisha malizika.
Dakika kumi zilitosha kabisa mimi kufika Green house, niliifungua mlango wa chumba na kuingia ndani, ambako nilivua viatu nikifuatia nguo zote na kubakia kama nilivyozaliwa kwa lengo la kwenda kuoga, ambako sikutumia muda mrefu sana kuoga, japo wakati naoga nilisikia kitu kama nyayo za mtu zikiingia mule ndani na kutembea kwenye korido, ila haikunishtua maana upande ule ulikuwa na vyumba vitatu, japo utembeaji wa haraka wa mtu huyo ulinivutia sana, nilijifuta maji mwilini na kujifunga taulo kiunoni na kutoka kuelekea chumbani.
Nilitoka bafuni na kuingia chumbani kwangu na kutoa taulo kiunoni mwangu, hapo msomaji kumbuka nilibakia uchi kabisa nikiacha dudu ikiwa inaning’inia, niliamini nipo peke yangu, lakini ile nataka kulitundika sehemu yake nikashangaa kuona sehemu ile kuna baibui na uniform za shule ya fider castor tena ya kike, nikajifunika haraka sehemu zangu nyeti huku natazama upande wa kitandani, nikamuona Maimuna akiwa amekaa kitandani hapo amejikunyata kwenye kona kabisa, amevalia kijigauni chake kama kile cha jana huku macho yake yananikodolea……yap! unadhani Eric atafanyaje hapo na mtoto kautaka? Samahani wote muliokwazika na ukimya wangu na Eid Mubarak kwa wote... ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom