KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA KUMI NA TANO
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE : “dah! kwa kweli inatisha” nilisema hivyo, huku nageuza uso wangu kutazama kule walipokuwepo wakina Malambo, lakini kabla sijawaona wao nikamuona yule babu wa jana usiku, mwenye makovu usoni, makovu ambayo yalionyesha wazi kuwa aliwahi kushambuliwa au kukatwa na mapanga, aliekuwa amesimama mita chache sana kushoto kwangu, nivkama alikuwa anatusikiliza tulicho kuwa tunaongea, moyo wangu ulishtuka sana kumuona yule mzee mahali pale, nilitamani kujuwa zaidi kuhusu yule mzee, ambae nilianza kumtilia mashaka kutokana na kujitenga kwake na utazamaji wake……ENDELEA…..
Ni kama yule mzee alishtukia kwamba nimemuona akitusikiliza kwa umakini, maana aliondoka mara moja, “sele unamfahamu yule mzee, unaweza kunieleza kidogo kuhusu yeye” nilimuuliza Sele huku nikimuonyesha alikokuwa anaelekea yule mzee, “unamzungumzia mzee Mangeu, yeye tokea nimepata ufahamu wangu, namuonaga hivyo hivyo, yupo peke yake hana mke hana mtoto wala ndugu ambao wanamtembelea zaidi ya mihogo anayo lima pale nje ya nyumba yake, na ile misheri sheri, hakuna kazi yoyote anayo ifanya, na anaishi na kula kama watu wengine” alisema Sele, na kunishangaza kidogo, na kunifanya niwaze sana juu ya jambo hilo, hata wakati tunarudi mess na wakina Malambo, nilikuwa nawaza na kutafakari kuhusu maelezo ya yule babu, ambae wanamuita Mangeu, nadhani nikutokana na zile alama za usoni mwake, sikuweza kufikiria muonekano wa sehemu anayoishi, pia nilitafakari kuhusu tukio la kuuwawa kwa Masoud kama nilivyosimuliwa na Mahamud, hasa tukio la mbio za pikipiki dakika chache kabla ya mschana kutoka ndani kwa Mahamud, je inawezekana mpanda pikipiki ana husika na tukio lile, kama ni hivyo, kwanini huyo mwanamke asitoe taarifa kituo cha polisi, na pia inawezekana tukio la kule madungu likawa sawa na hili la nyumbani kwa Masoud, hata hivyo niliamini kuwa nitapata majibu nitakapofika Madungu Guest House.
Ukweli sikukaa pale mess, mara baada ya kuwashusha wakina Malambo, Mwasenga akanipeleka kambini, ambako nilibadili nguo na kuvaa nyingene nazo zikiwa za michezo, nikabeba begi langu dogo kama kawaida, pamoja na kiasi flani cha fedha, nikamuomba Mwasenga anipeleke mjini ambako niliongeza mafuta kwenye gari lile la jeshi kwa fedha yangu, ,maan lilinisaidia kufika nilipohitaji, aliponishusha madungu nikamueleza kuwa asogee mpaka karibu na kituo cha polisi, kisha akaegeshe gari na mimi ningempgia simu wakati nitakapo muhitaji, “vipi bro unataka kumleta yule mwalimu au?” aliuliza Mwasenga, wakati anasimamisha gari karibu na Madungu Guest house, “si unajuwa tena kaka, nataka nifanye uzinduzi” nilitania maana sikutaka Mwasenga ajuwe ukweli wa mambo, “ila kaka ilibidi unionyeshe huyo demu, isije kuwa ni jini, maana hii ni pemba pelemba, unakuja na koti unarudi na kilemba” alisema Mwasenga kwa utani, “nitakuonyesha siku moja, nasikia kutakuwa na taarabu nitakuja nae mess” nilimueleza Mwasenga, ambae alijiridhisha na mimi nikashuka kisha yeye akaondoa gari, na mimi nikatazama kushoto na kulia kama ningeona dalili ya jini, lakini hakukuwa na dalili ya jini.
Hapo nikatazama umbari wa kutoka barabarani mpaka kwenye jengo la hii guest house, ukweli palikuwa na mita zisizozidi kumi, nikatazama mazingira ya nje na tabia ya eneo la nyumba ile ya wageni, nikagundua kuwa haikuwa na dalili ya ulevi au huduma nyingine zozote zaidi ya kuwa ni nyumba ya kulala wageni, ukiachilia kuwa ni jengo pekee lisilo na vitoto pembeni, pia lilikuwa kimya kabisa pasipo hata sauti ya music, hapo nikapiga hatua kusogelea mlango wa ile nyumba ya wageni, nikiwa na begi langu mgongoni, na nilipoufikia mlango ambao ulikuwa wazi nikaingia ndani na kupokelewa na jamaa mmoja ambae licha ya kuwa uvaaji wake ni kama wenyeji wa kisiwa hiki sio kanzu, ila shati na suruali bila kuchomekea, “karibu kaka” alikaribisha yule jamaa ambae nilihisi kuwa ndie Hassan, “asante sana asalam alaykum” nilisalimia kwa mujibu wa taratibu za huku” “walaykum salam, karibu ni kuhudumie tafadhari” alisema Hassan, ambae ndie muhudumu wa ile nyumba ya wageni, “nimekuja kuweka oda ya chumba kwa siku ya ijumaa ijayo, kuna wageni wangu wanakuja toka dar es salaam” nilisema hivyo ikiwa ni mbinu ya kuanza maongezi na kijana huyu, “mh! ijumaa” aliguna Hassan huku anachukuwa kijitabu chake, cha wageni na kuanza kupekuwa, alitazama kwa dakika nzima, kisha akatikisa kushoto na kulia, “kuanzia ijumaa na jumamos vyumba vyote vimejaa, wana bendi ya JKU, toka unguja wamechukuwa vyumba, halafu pia kuna wageni wa kisiasa (huku akitaja chama chao cha siasa) nao wame chukuwa vyumba, labda kuanzia juma pili, JKU watakuwa wamesha ondoka, watabakia hao wanasiasa tu” nilitabasamulia moyoni, maana yangeweza kunikuta kama kule dukani kwa Saphia, ambako nililazimika kununua perfume pasipo kupanga kufanya hivyo, “hooo! na yeye ilikuwa anakuja kwenye onyesho hilo hilo la taarabu, na angeondoka juma mosi mchana” nilimueleza bwana Hassan huku natafuta jinsi ya kumchomekea kuhusu kilicho tokea siku za nyuma hapa hotelini, “dah! kwakweli siwezi kukuambia kama pata patikana nafasi, kwamba kuna mtu anaweza kuacha kuja, maana wamesha lipia kabisa” alieleza Hassan, hapo nika jifanya kuaga, “basi poa, wacha nikahangaike nitafute sehemu nyingine ambayo anaweza kufikia..” nilisema huku nageuka na kutaka kuondoka, lakini nikasita ghafla, na kumgeukia Hassan, “samahani bro, hivi wewe ndie Hassan uliekutana na jini hapa hotelini” nilimuuliza huku namtazama kwa namna ya fulani kama ya kuvuta kumbukumbu, hapo nikamuona akiinamisha na kuitikia kwa kichwa hicho hicho, akitikisa juu chini, “ni mimi, kwakweli huwa sitaki hata kukumbuka lile tukio” alisema Hassan kwa sauti iliyopoa, “pole sana bwana Hassan vipi lakini huogopi kuendelea na kazi kutokana na hilo lililokutokea” nilimuuliza kiuchokozi ili kupima anachukuliaje tukio lile la kukutana na jini alietoka kufanya mauwaji, huku narudi tena pale mapokezi, “nilitaka kuachana na kazi hii, lakini ningeenda wapi, elimu sina tabora nimetoka miaka mingi sasa nitakuwa mgeni wa nani” alisema kwa masikitiko bwana Hassan, “pole sana bwana Hassan, hivi unaweza kunisimulia kidogo ilivyo kuwa, napenda kujuwa habari za majini, sikuwahi kusikia hapo mwanzo” nilimueleza Hassan, ambae alianza kwa kusita kidogo, “lakini dogo, unajuwa unapoyazungimzia majini ndio unafanya yakuandame zaidi” alinieleza kwa sauti iliyojaa uoga, “lakini habari hii imezungumzwa na wengi, na sidhani kama jini lime waandama” niliweka sawa wasi wasi wake, na hapo akaanza kunisimulia jinsi ilivyokuwa.
Dakika kumi na tano zilitumika kunisimulia mkasa ule, ambao haukuwa mgeni kwangu, (anza sehemu ya kwanza) “kwa kweli ilitisha sana, hata polisi walipofika walishangaa sana kwa kilichotokea” alimaliza kusimulia bwana Hassan, “samahani bro, unasema ulipofika dirishani ulikuta dirisha likiwa wazi, na jiwe limesogezwa dirishani sio?” nilimuuliza Hassan ambae aliitikia kwa kichwa kukubaliana na mimi, “unakumbuka nini kabla ya wageni wako kuingia, dirisha lilikuwa limefungwa au lilikuwa wazi hivyo hivyo?” niliuliza kama vile tupo kwenye maongezi ya kawaida ya kirafiki, “huwa hatuachagi madirisha wazi, nadhani walifungua kwaajili ya kupunga hewa….” alisema Hassan nakusita kidogo, halafu akajirekebisha mwenyewe, “ila lakini ndani kuna feni, labda jini lilifungua lenyewe wakati linatoka” alisema Hassan ambae ni wazi kwamba alikuwa anaamini kwa asilimia mia moja kwamba Abdulqadir, aliuliwa na jini, “dah! bwana Hassan hiyo iliogopesha sana, vipi utajali kama nitaenda kuona hapo nje jinsi palivyo?” niliuambia Hassan kwa sauti ya kuomba, nae akashtuka kidogo, “kwanini unafanya hayo yote, kwanza umeuliza maswali ambayo hata polisi hawakuwahi kuniuliza, pia unataka kuona sehemu ambayo hata polisi hawakufikiria kuitazama hapo mwanzo” aliuliza Hassan, huku ananitazama kwa mashaka, nikagundua kuwa nilifanya kosa kubwa kwa kuhoji kuliko pitiliza.
Hapo nikaona cha msingi ni kumpoteza na kumuondoa kwa kile anachofikiria kwa sasa, kwanza nilianza kucheka, “hahahaha! Kaka Hassan bwana, mimi ni mwalimu wa computer pale Fidel Castor, lakini napenda tu kuona jinsi majini wanavyo kuwa na uwezo wa ajabu” ndivyo nilivyo mteka akili, “sawa twende ukapaone” alisema Hassan na hapo tuka zinguka upande wa nyuma wa lile jengo nikiwa nyuma ya Hassan, “hivi brother unaweza ukakumbuka huyo mwanamke yupo yupoje?” nilimuuliza Hassan wakati tuna tuembea pembezoni mwa ukuta wa nyumba ile, “hooo kaka ukimuona unaweza kudata, ni mzuri kweli kweli, yaani unaweza kusema sio mpemba, lakini uso wake aliziba” alijibu Hassan kwa sauti ya msisitizo, akimsifia mwanamke huyo jini, “kwanini hukushtuka ulipomuona ameziba uso?” niliuliza swali la kibwege, ambalo jibu lake lipo wazi, “nitamshtukiaje wakati ni kawaida yao wanawake wa huku, huwa wanaziba sura zao pale wanapoingia hapa guest au wanapoenda sehemu yoyote ambayo hawataki wajulikane” jibu la Hassan nilikuwa na lifahamu muda mrefu, hivyo nikaachana na na maswali na hapo nilitembea huku natazama kwa umakini sana, mandhari ya kule nyuma ya jengo, ambako mita ishirini toka ukuta ule wa nyumba ya wageni kulikuwa kuna majengo kadhaa, kama vile mtaa ikiwa nipande mbili yaani upande wa nyuma na upande wa kuelekea chake, japo hapakuwa wazi sana kutokana na msingi flani wa jengo, mita saba au nane, toka kwenye jengo hili la guest house, ambao ulifunikwa na nyasi nyingi sana.
Naam wakati tunaendelea kutembea, pia niliweza kutazama pembezoni mwa ukuta wa guest hii iliyopo mtaa wa madungu, ambao ulikuwa umepambwa na maua mafupi yaliyo tufikia usawa wa kiuno na madirisha mazuri ya vioo ya nayo funguka kwa mtindo wa kuleteza, (slide) tulipolifikia dirisha husika tuka simama na kulitazama, “hili ndilo dirisha la chumba walicho kuwepo” alisema Hassan, na wakati huo niliweza kuona jinsi mazingira yalivyo, ambapo niliweza kuona jiwe kubwa chini yake, likiwa hatua chache toka ukutani, usawa wa dirisha ambapo palionekana kukosa maua, pia dirisha la vioo lilikuwa limefungwa, huku ndani likionekana panzia lililoziba na kufanya ndani kusionekane kabisa, “hili jiwe lilikuwa limesogea hapo karibu na dirisha, na hilo dirisha lilikuwa wazi, hata panzia lilikuwa limefunuliwa kidogo sana” alielekeza Hassan, “hoooo! inaonyesha kuna watu wanapiga chabo sana hapa” nilisema huku nasogea na kukanyaga pale kwenye ile sehemu iliyokosa maua, yaani chini ya dirisha, Hassan hakujibu kitu zaidi ya kujichekesha kama lofa.
Nilitazama kwa sekunde kadhaa lile dirisha, na pasipo Hassan kujuwa nimegundua nini, zaidi nilimuona akinitazama kwa umakini nadhani alitaka kuona nilikuwa nafanya nini, nililaza kiganja cha mkono wangu kwenye kioo na kulisogeza upande wangu wa kushoto, nacho kikateleza kwenye njia yake na kusogea upande wa kushoto, “unataka kusema kuwa mtu aliefungua dirisha alikuwa nje na sio yule jini?” aliuliza Hassan kwa mshangao, “sijui, ila naomba usimueleze mtu yoyote kama nilikuja hapa, na tuliongea kuhusu hilo” nilisema hivyo, huku natoka pale dirishani na kuelekea upande wa pili wa jengo lile, yaani kule kwenye mlango wa kuingilia kwenye jengo hili, huku Hassan akinifuata nyuma, “wala usiwe na shaka, hata hivyo sidhani kama kuna mtu anaweza kuja kuuliza” alisema Hassan, na baada ya hapo nikaagana nae, na mimi nikaondoka zangu kuelekea upande wa kituo cha polisi, ambako Mwasenga alikuwa ananisubiri, lakini kiukweli pale polisi nilihitajika kukutana na insp Haroub, nilitembea huku nawaza njia sahihi ya kumuingia insp Haroub…. ENDELEA
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA KUMI NA SITA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO : “sijui, ila naomba usimueleze mtu yoyote kama nilikuja hapa, na tuliongea kuhusu hilo” nilisema hivyo, huku natoka pale dirishani na kuelekea upande wa pili wa jengo lile, yaani kule kwenye mlango wa kuingilia kwenye jengo hili, huku Hassan akinifuata nyuma, “wala usiwe na shaka, hata hivyo sidhani kama kuna mtu anaweza kuja kuuliza” alisema Hassan, na baada ya hapo nikaagana nae, na mimi nikaondoka zangu kuelekea upande wa kituo cha polisi, ambako Mwasenga alikuwa ananisubiri, lakini kiukweli pale polisi nilihitajika kukutana na insp Haroub, nilitembea huku nawaza njia sahihi ya kumuingia insp Haroub.....ENDELEA…
ambae kiukweli sikujuwa nitamueleza kitu gani mpaka anipe ushirikiano katika swala lile la uchunguzi, mwisho nikakata shauri la kuacha kumuona insp, ili nisije nikajiweka wazi, maana nilikumbuka kuwa unapo mpeleleza mpelelezi lazima uwe makini sana, japo bado nilikuwa na hofu ya jini hasa nilipo mkumbuka yule mwanamke ninae kutana nae mjini mara kwa mara.
Niliungana na Mwasenga ambae alinipeleka mjini, nikamuomba anishushe eneo la sokoni, “kaka leo usichelewe kunifuata” nilimsisitiza Mwasenga kuja kunifuata jioni, wakati tunaagana, “usijali bro, leo mapema sana” alisjibu Mwasenga huku anaondao gari, hapo na mimi nikaondoka taratibu kukatiza mitaa ya mjini, yaani ile barabara ya markiti, ambayo sasa watu wengi walikuwa wanaondoka kurudi makwao, ina maana nilikuwa na pishana nao, na mimi nilikuwa makini sana kuwatazama, nilitaka kuona kama ninaweza kumuona yule mwanamke jini, ambae licha ya ujini wake ila kiukweli alikuwa ni mzuri kweli kweli.
Mpaka na fika usawa wa hospital sikuona dalili yoyote ya jini, nikaingia kwenye gate la hospital, ambao ipo mita kama hamsini toka uwanja wa mpira wa kikapu, ambao niliwahi kufanya mazoezi na leo nilipanga kufanya mazoezi pia, baada ya kutoka hapa hospital niliongoza moja kwa moja mpaka eneo la mapokezi, ambapo kuna mchoro mkubwa wa maelekezo ya sehemu mbali mbali za hosipital ikimrahisishia mgongwa au mtu yoyote kufika sehemu aliyo kusudia kwenda, nilisoma ule mchoro na kupata njia ya kwenda maabara.
Nilitembea kwenye kijinia cha kuelekea kwenye jengo moja kubwa la maabara, huku nikipishana na watu wachache, wakiwepo baadhi ya wagonjwa na wauguzi, mpaka nilipo lifikia jengo hilo na kugonga hodi nikiomba kuingia ndani, mlango ukafunguliwa na mzee mmoja wa makamo, “asalam alaykum” nilimsalimia, “walakym salam, nikusaidie nini tafadhari, maana sidhani kama umeleta sample?” aliongea yule mzee ambae licha ya kuvalia koti la kidoctor pia alikuwa amevalia kofia ya baraghashia, “mzee labda nijitambulishe kwako, mimi naitwa Eric Frank, toka kampuni ya uandishi na sambazaji wa makala mbali mbali ya MSC printers, pia ni mwalimu wa computer hapo Fidel Castor secondary” nilijitambulisha mbele ya yule doctor wa maabara, “ok! karibu unieleze shida yako” alisema yule mzee huku anaongoza kuingia ndani, na mimi nikamfuata.
Mzee yule ambae hakujitambulisha kwangu, aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye ofisi yake, tukipita kwenye ukumbi wa maabara, ambao ulikuwa na vikorokocho vingi sana vya kimaabara, “haya bwana Eric, niambie unashida gani?” aliuliza yule mzee na hapo nikajipanga kuongea kitu ambacho kinge mshawishi huyu mzee ili asisite kujibu au kutoa maelezo ninayo yajitaji, “kwa sasa nipo kwenye uandishi wa makala moja ijusuyo mambo ya vitu vya kufikirika, hasa kuhusu viumbe vinavyoitwa majini” nilimueleza yule mzee ambae alishangaa kidogo, na kunitazama kwa macho ya tahadhari, sasa baada ya kwenda kwa waganga unakuja kwenye maabara ya hospital?” aliniuliza kwa mshangao yule mzee, ambae pia aliongeza kuwa “na mimi binafsi sina elimu yoyote kuhusu majini” alisema yule mzee, ambae baadae nilifahamu jina lake kuwa anaitwa hafidhi, “mzee sidhani kama nahitaji mganga wa kienyeji kupata habari ninayohitaji, naamini nitaipata hapa hapa kwako” nilimueleza mzee hafidhi, huku nacheka kidogo, “ok! bwana Eric lete maneno” alisema mzee hafidhi akimaanisha yupo tayari kunisikiliza, na mimi sikuchelewa nikaanza kueleza nilicho hitaji kukifahamu, “toka nimefika hapa pemba nilisikia kuna habari zinazungumzwa sana kuhusu kifo cha kijana mmoja hivi (yaani Abdulqadir, nilijifanya nime msahau jina), kuwa alifia Madungu Guest house, ni kifo kinachosadikika kuwa aliuliwa na jini, pia leo hii nilienda kwenye mazishi hapo Msingini, na yeye alikuwa nyumbani kwake ameuwawa na jini, imani yangu ni kwamba miili yao ililetwa hapa na nyie ndio mulio ichunguza kwa vipimo, je unaweza kunieleza kwa kifupi majibu ya vifo vya hawa wawili” nilimueleza mzee hafidhi ambae nashukuru jakusita kunieleza, “ukweli hata mimi nilishangazwa na vifo hivyo, ambavyo sio hivi viwili pekee, vilianza kutokea miaka mingi iliyopita, kuna wavulana wadogo wa shule ya sekondari waliletwa hapa wakiwa wamekauka kabisa, utasema wame kufa siku kadhaa zilizopita, tulijaribu kuchunguza vipimo vyetu vilishindwa kubaini tatizo, na hata tulipo peleka vipimo kwenye maabara kuu ya hospital ya muhimbili, ndipo wakasema kuwa kilicho bainika kwenye miili ile ni kwamba marehemu wamekutwa hawana hata chembe ya damu, na chakushangaza ni kwamba hawakuwa na majeraha yoyote ambayo yangewezesha vujisha damu kiasi cha kuwa kausha damu, baada ya hayo matukio mawili, pia vilifuatia vifo kadhaa kama hivyo na majibu yalikuwa ni hayo hayo, hivyo baada ya hapo hatukusumbuka tena kupima pale vifo kama hivyo vinapotokea,” alisema mzee hafidhi, na hapo nilisisimka kidogo, maana sikuwahi kusikia jambo kama hilo hapo mwanzo, “mh! mzee kwanini muliacha kuchunguza, hamuoni pengine munge pata kugundua kitu?” nilimuuliza yule mzee ambae alicheka kidogo, “kuna vitu vipo wazi bwana Eric, hawa vijana wote wamekufa vifo vinavyofanana, katika mazingira yanayofanana, wote walikutwa na umauti wakiwa katika harakati za kufanya ngono, tena na mahawara, na mwanamke ambae wanakuwa nae ni mwanamke anae landana kwa umbo, niwazi ni huyo huyo mmoja” alijibu mzee hafidhi, na hapo nikakumbuka maelezo ya Hassan, kwamba ni mwanamke mzuri sana, nikamkumbuka yule jini ambae nilikutana nae mara mbili, “kwanini huyo mwanamke asikamtwe?” nilimuuliza mzee hafidhi, ungesema yeye ni polisi, “mh! utamkamataje jini, iwapo ile kumtambua tu imeshindikana kama unavyoona, vijana marafiki wanakufa kila uchao?” alijibu mzee hafidhi kwa mtindo wa swali, na hapo ni kama nikajipatia swali mimi mwenyewe, “ina maana huyo jini ni mimi peke yangu ndie ninae mfahamu, au yule mwanamke sio jini kama ninavyo mfikiria?” nilijiuliza kimoyo moyo, kabla sija uliza swali la mwisho, “samahani mzee hivi hakuna kifo chochote kinachofanana na vifo hivyo kilicho wahi kutokea hapo kabla?” nilimuuliza mzee hafidhi, ambae kama kawaida yake hakukosa jibu, “yes kuna vifo kama hivyo pia vilishawahi kutokea, lakini vyote hutokea baharini, kwa watu waliozama kwenye maji na kukutana na jini chunusi” hapo ndipo nilipo choka, maana kwa asilimia kubwa, watu hawa waliamini kuwa muuwaji ni jini, “nashukuru sana mzee wangu, naomba nikuage niwahi mzoezi” nilimueleza mzee hafidhi nikiwa namuaga huku natazama saa ya kwenye simu yangu ya mkononi, ilisha timia saa kumi na robo, “sawa bwana Eric, ukiwa na shida yoyote karibu muda wowote, na mimi pia ninasubiri nakala ya kitabu chako” alisema mzee hafidhi, ambae alinisindikiza mpaka nje ya maabara kisha akarudi ndani, huku mimi nikiondoka zangu kuelekea kwenye lango la kutokea pale hospital, na nilipofika nje nilifuata uelekeo wa kushoto na kuelekea uwanjani.
Hatua kama kumi na tano nilizopiga zilizinifanya nianze kuona watu waliokuwepo uwanjani, mazoezi yalikuwa yameshaanza vijana hawa hawakuwa na muda wa kufanya mazoezi ya viungo wala kutafuta pumzi, wao walikuwa wakifika tu wanapanga timu zao mbili na watu wa akiba kisha wanaanza kucheza mpira, nilipofika nikasalimiana na vijana wengine waliokuwa pembeni, kisha nikatafuta sehemu moja nzuri na kuweka begi langu kisha nikatoa track ya chini na kubakia na bukta nikatoa tishert na kubakia singland, halafu nikaanza kukimbia kuzunguka uwanja kwaajili ya kupasha mwili joto na kutafuta pumzi.
Baada ya kufanya hivyo kwa mizunguko kadhaa, na wakati nakatiza gori la upande wa kusini nikashtuka nikisalimiwa, “asalam aleykum” ilikuwa ni saut ya mvulana mdogo, nikatazama upande uliotokea sauti ulikuwa niule wa jengo la ghorofa linalotumika kama makazi ya wafanyakazi wa serikali, nikamuona yule kijana mdogo Yassin ambae alinipokeaga hapa siku ya kwanza kabisa nilipofika kuanza mazoezi, akiwa amesima kwenye ukuta karibu na lango la kuingilia pale nyumbani kwao, “walaykum salamaa Yasin, mambo vipi?” nilimsalimia huku naendelea kukimbia kuzunguka uwanja, wakati huo nilikuwa na wasikia watu wanazungumzia kwamba kuta kuwa na mechi kesho yake, na timu toka mkoa wa kusini pemba, pia wapo waliozingumzia habari ya onyesho la music wa taarab ijumaa ijayo.
Nilipofika usawa ule wa gori la upande wa kusini, nikatazama pale alipokuwa amesimama Yassin, hapo macho yangu yakakutana na macho ya Maimuna aliekuwa anatoka nje ya lango na kwenda kusimama karibu na mdogo wake, yani Yassin, nikamuona Maimuna ambae alionekana kuwa na tabia mpya jioni ya leo, ukiachia tabasamu pana huku anatazama chini kwa aibu kama mtu mwingine angeona tukio lile angesema kuwa mimi na Maimuna mschana yule wa miaka kumi na nane ni wapenzi wa siri, au tupo kwenye makubaliano ya kuwa wapenzi, nilishangazwa sana na hali ile, lakini nikajitahidi kupotezea kwa kuchukulia kuwa nimuonekano wake tu, ila sio kama ninavyofikiri.
Lakini sikuweza kuishia hapo na kupotezea jambo lile, maana kila nilipotazama upande ule nilikuta Maimuna nae ananitazama na macho yetu yakupo kutana nilimuona akitabasamu na kukwepesha macho pembeni, wakati mwingine akijing’ata kidole kwa aibu na kutoa ishara ambazo kiukweli bado sikutamani kuamini kuwa, zipo kama ninavyo fikiria, kwamba yule mtoto anahitaji dudu, kitu ambacho sijakuambia ni kwamba licha ya kuwa tofauti na wa miaka saba na huyu binti, lakini binti huyu wa kidato cha tatu alionekana kuwa na muonekano mzuri tu, na mwenye kutamanisha kuliwa kitumbua.
Hali hiyo ya kunitazama iliendelea hata wakati nilipopewa nafasi ya kucheza, maana nilipogeuza uso hata kwa bahati mbaya, macho yetu yalikutana na yeye akafanya vile vile, yani akajitabasamulia na kutazama pembeni kwa aibu, ukweli sasa nilisha mzoea na kuanza kujisikia raha kwa kitu kilichokuwa kinaendelea, na kujikuta naanza kutamani kula kitumbua cha Maimuna, nilisha sahau kuwa ni mwanafunzi, si unajuwa mimi sio mwalimu na sikuwa na sifa ya kuwa mwalimu, huku nikijisahaulisha mila na desturi na yale makatazo ya watu mbali mbali kuhusu ngono na waschana wa huku.
Lakini kuna wakati lilitokea jambo fulani, ambalo liliniondoa katika umakini wa kumtazama Maimuna ambae wao walikuwa wanamuita Mai, ni wakati fulani tukiwa tunaendelea kucheza mpira, nisikudanganye, ukweli ni kwamba uchezaji wangu ulikuwa wa hali ya juu sana kuliko wachezaji wote pale uwanjani, kitu kilichopelekea nifunge point nyingi na kuwafanyia ufundi mwingi sana, kiasi cha wao kuogopa kunidefensi
Sasa kuna wakati mpira ulitoka pembeni mwa uwanja, ni usawa ule nilioweka begi langu, upande ambao haukuwa na watu kabisa, na wakati naukimbilia mpira ule kabla sijaufikia bahati nzuri nikaona mpira ule ukizuiliwa kwa mguu wa mtu aliekuwa amesimama karibu na begi langu, nikashtuka kidogo, kilicho nishtua nikwamba mtu huyu alikuwa ni mwanamke, na hapo mwanzo sikuwaza kama kuna mwanamke mwingine pale uwanjani zaidi ya Maimuna.
Nikamtazama vyema mwanamke huyu, ambae aliinama kuokota ule mpira na kunirushia, hakika nilitoa macho, sio tu kwa mshangao, ila ni mshangao wa uoga, maana mwanamke huyu alikuwa ni yule yule ambae amekuwa akininyima amani toka nimeingia hapa Pemba, ni yule mwanamke mwenye asili ya uchotara wa kiarabu na kibantu, uso wa kiarabu umbo la kibantu, mrefu wa kupendeza, alievalia gauni refu rangi ya dhahabu, lenye fito yeupe na blue zilizo haririwa kwa usanifu mkubwa, kichwani mwake alikuwa amejitanda kitambaa cheupe (hijab), na kufunika macho yake kwa miwani nyeusi, tabasamu laini alikukauka mdomoni mwake…..……. Hivi ni kweli Eric au mkono wa jini kama anavyojiita ataweza kuchomoka ndani pemba akiwa salama? tuendelee kufuatilia mkasa huu hapa hapa
JamiiForums