Ukitaka kupima mwisho
wa chama chochote cha
siasa na serikali yake ni
pale kinapoanza kukiuka
misingi muhimu ya haki
za binadamu ,matumizi ya
nguvu kupita
kiasi ,kutumia ubabe ktk
maamuzi yake na
kuwafanya wananchi
wasiokuwa na hatia
kuwa wakosaji.
Mambo hayo ndio
yanayosababisha
waziri mkuu ,m.pinda
kushtakiwa na kituo cha
sheria na haki za
binadamu kwa kuvunja
katiba kutokana na
kauli yake bungeni '
wapigwe '
ktk post yangu ya leo
naona nichambue hali
halisi ya taifa le2u
linalokabiliwa na adui
hatari anayeitwa ' ubabe
' ukizungumza na watu
wa rika zote ,kada
zote ,kila kona ya nchi
wanalalamikia kuwa
ubabe unalipelfkea taifa
mahali pabaya sana ,na
hata watu wenye hekima
wanadai ubabe
ukizoeleka huzaa
usugu .hali hii ikitokea
kwa taifa inaweza kuzaa
maafa ya kitaifa .hivi
sasa taifa letu limeacha
asili ya kutawala na
kuongoza ambayo
iliheshimu matakwa za
wananchi na sasa
limeamua kufuata
utamaduni mpya wa
mizengwe ,ubabe na
uchakachuaji wa kila
fani nina maana ya
kuwa kuna wakubwa
wanaotumia dola dhidi
ya umma uliowachagua
na hili linasononesha
wengi .hebu tuangalie
ubabe wao ni upi na
wapi .
1) ubabe ulisababisha
kashafa ya epa ifunikwe .
2 ) ubabe ulisababisha
richmond iliyovuruga
serikali na bunge ,ubabe
huo ndio uliosababisha
tuwalipe richmond/
dowans.
3) ubabe umesababisha
kuendesha nchi bila
kufuata katiba ambayo
yenyewe tayari ina
viraka .
4 ) ubabe umeasisi udini
ktk taifa kuanzia shule
za msingi hadi vyuo
vikuu udini umeenea na
hivi sasa dini ya m2u ni
sifa ya kuteuliwa au
kutoteuliwa .
5) ubabe umesababisha
vyombo vya dola
vinavyopaswa kuwa
huru viwe mifukoni mwa
watawala.,
takukuru ,dpp .nec ,bunge
na mahakama.
6 ) ubabe ,ufisadi na
rushwa upo ktk ofisi
hata ambazo ni nyeti
kwa mhimili wa taifa .7 )
ubabe umedhilalisha
taifa na kulipotezea
utaifa wake nchi
imekuwa shamba la
wageni.
8 ) ubabe umesababisha
ubinafsishaji usio na
macho wala
masikio ,matokeo yake
ubinafsishaji huo
umeasisi kwa wenyeji
kuwa omba omba.
9 ) ubabe ume2umika
kuzuia chaguzi za
mameya ktk halmashauri
nyingi au hata
kulazimisha chaguzi ktk
manispaa nyingine
ziende kinyume na
utaratibu..10 ) ubabe
umesababisha wabunge
wa upinzani wapigwe
hadharani ,mwanza ,arus
11 ) ubabe umesababisha
wanafunzi wa vyuo
vikuu wapigwe mabomu
kwa kudai haki zao .
Nasema watanzania
wakiota sugu kwa ubabu
huu suluhu itapatikana
kwa gharama
kubwa ,natamka haya
kwa sababu hata hao
polisi wanaotumika
kuwaumiza ndugu zao
kwa mabomu pia wao
wana madai yao siku
polisi wakigoma nani
atatupiga mabomu ?
Watanzania mliyataka wenyewe. Tulieni mliwe vizuri hadi hapo mtakapopata akili 2015. Hiyo serikali mnayoilalamikia si mliiweka madarakani kwa kura zenu wenyewe? Mnapiga kura kama vipofu na kisha mnalalama kama vichaa!
Mud naomba usiichnganye au kuifuta.
Wana jamvi napenda tusaidiane kutafakari. Nisingependa kutaja mtu au jina fulani kwa sababu za uandishi lakini mwenye macho na masikio haambiwi tazama au sikia.
Hiki ni chama, tene cha siasa. kila kukich taarifa zinazagaa kwenye vyombo vya habari kuwa mara huko China, afrika ya kusini, Misri, dubai, hongkong nk wamekamatwa vijana na madawa ya kulevya. Mbaya sana ni vijana ambao tunategemea wangekuwa kioo kwa jamii. Sina shida sana na hilo kwa sababu najua ni njaa tu zinawahangaisha.
Hoja hapa ni nini? Ukifuatilia fununu (taarifa za zisizo rasmi lakini napenda niwahakikishie wasomaji kuwa tupende tusipende hizi ni taarifa rasmi) utasikia ni kiongozi katika chama fulani (utasikia ni mbunge, waziri, mtoto wa mzee (au mwenye kaya) afisa usalama kwa ofisi nyeti nk).
Kama siyo madawa ya kulevya basi utasikia twiga kaondoka kwa ndege mzima mazima au tembo keshatolewa meno au simba nae anaelekea airport kama vile nao siku hizi wanaenda ulaya kusoma masters na degrees.
Hapa kinachonishangaza zaidi, ni pale anapotoka mpayukaji na kusema jamani nimekutana na twiga airport, basi utasikia wahusika watakavyong'aka kuwa "huyu ni mchochezi, muongo, anahatarisha amani na maneno mengine mengi ambayo kwa lugha rahisi najikuta nimelewa bila kunywa.
Stori bado haiishii hapo. utasikia kule baharini kaibuka kinara anasema samaki wetu tuliovua hatuuzi kwa bei hiyoooooo. mwingine kule m....... utasikia haitokiiiiii mpaka tupate ...... Sasa hapo kaa muda tu, utasikia mara kuna mtu kakutwa ameng'olewa meno kwa koleo bila ganzi, wa kule haitokii.... utasikia majamaa imekuja na vifari kama vile wanaenda vitani kuwachakaza wapiga mayowe.
lakini ili nisipoteze ujumbe wangu, haya madawa ya kulevya ambayo kila kijana wa bongo flava na movie anajaribu kupelekwa ulaya ili awe PUNDA (Bongo stars) wa kubeba mzigo? Hii serikali tuliyokuwa tukifundishwa kuwa ina macho, mikono mirefu nayo imebwia UNGa ikalala? Lakini pia mbona tuliotegemea kukimbiilia kwao sasa ndo wa kuishi nao mbali tena zaidi ya tunavyomwogopa SHETANI? Hiki chama ni cha siasa au chama cha Madawa ya kulevya?
Mwenye kujadili na ajadili lakini najua kwa wale Punda na wapanda punda ambao wako humu JF najua watatukana na kukejeli. Kwangu mie msg sent.
,
View attachment 105062huyu Punda ameshafikisha mzigo wake
Sisi kama Vijana tuna jukumu kubwa la kuhakikisha tunalijenga Taifa lililo bora kwa kila mtu kuishi.Sio siri tena Uongozi wa vizazi vilivyotangulia umeshindwa kutujengea Taifa lenye kuleta matumaini.Tunachoshuhudia sasa hivi ni utawala uliokosa dira na mwelekeo;Viongozi waliokosa Uzalendo na rasilimali za Nchi;Ufisadi na Ubadhilifu uliotamalaki katika ngazi zote za Serikali;Ukiukwaji wa Haki za Binadamu;Kunajisiwa kwa demokrasia na mambo mengine mengi tu.
TUFANYE NINI VIJANA?
Katiba mpya ndio fursa yetu pekee katika kuipigania Tanzania mpya tuitakayo.Tusihadaike na propaganda za Vyama vya Siasa wanataka kututumia tu kufanikisha matakwa yao binafsi bali tuipiganie Katiba mpya kwa kuangalia faida zake za muda mrefu kwetu.Napendekeza katika katiba mpya kuwe na mambo yafuatayo:
1) Utawala wa Majimbo
2) Tume huru ya Uchaguzi
3) Mahakama zilizo huru na zenye meno zaidi
4) Usalama ulio huru na unaowajibika kwa Bunge[Kamati ya Usalama ya Bunge]
5) Wateule wa Rais wathibitishwe na Bunge
6) Uhuru wa Vyombo vya Habari