Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

swala la ccm kurudi tena madarakani ni ndoto mkuu

Sio kweli wazee.
CCM ina mitaji mikuu miwili ya kushindia kura
1. UJINGA
Huu ni mtaji wqo mkubwa sana kisiasa maana kadiri nchi inavyokuwa na wajinga wengi ndivyo nafasi ya kukitoa chama tawala madarakani inakuwa ngumu. Mpaka sasa CCM imefanikiwa kuongeza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika na huu ni mtaji wao mkubwa sana. Wanafunzi wanaotoka sekondari za kati hawajui hata kujieleza sembusa kuinyima kura CCM?
2. VIJIJINI
Mabadiliko yoyote ya kisiasa huletwa na maendeleo. Kura nyingi za CCM zinatoka vijijini. Ni kura hizi ndizo zimemrudisha mugabe madarakani kwa kishindo. CDM hawajafanya juhudi za kutosha kufika vijijini nje ya vijiji vya kaskazini. Katika uandikishaji CCM wanahakikisha watu wa kijijini wanatoka kwa wingi kwenda kupiga kura na mijini mtapewa vichapo na polisi ili msijitokeze.
3. WIZI
Mpaka sasa CDM hawajapata dawa ya kuwadhibiti CCM kwenye wizi wa sanduku la kura zaidi ya kulalama barabarani.
4, USALITI
Chukulia mfano mpaka sasa sijapewa sababu za kutosha kwa nini Mgombea wa Igunga mwalimu Kashindye hakuwakilisha vielelezo muhimu kwenye rufani ya kesi iliyomnyanguanya ubunge Dr. Kafumu. Nilishangaa kuona akipokea kwa mikono miwili kushindwa kwake kwenye mahakama ya rufani. Huu ni usaliti. Tuna wagombea wengi tu ambao wamekuja CDM kwa masilahi yao wenyewe. Hawa wako tayari kuuza nafasi zao kwa CCM kwa gharama yoyote.
Mgombea yeyote wa CCM hata kama amebobea kwenye kuuza unga bado 2015 atashinda kwa kishindo. CDM wataongeza idadi ya viti bungeni.

mkuu suala la CCM kurudi madarakani halipo tena hata wasimamishe malaika, we don't need, They are tired and out of ideas.
50 years after independence, 70% of Tanzanians are dirt poor. Enough is enough
 
mambo uliyoyasema ni challenge lakini wakati umewadia kwa watanzania kupata uhuru wa pili kutoka kwa mabeberu wanaouza nchi huku sisi tukiangalia.

Ujinga ilikuwa factor is no longer the case watu wamesituka mpaka vijijini kama ambavyo chaguzi z hivi karibuni zilivyoonyesha ccm wanaogopa kuitisha uchaguzi hata vijijini.

vijijini.
kama nilivyosema hapo juu ccm wanaogopa kuitisha uchaguzi mpaka vijijini sasa watu wameamka

wizi
kama tutawaruhusu watuibie wataiba lakini tukiwa macho na hasa wakati huu wa science and technology tunaweza kuwa na matokeo ya nchi nzima kabla hata ya tume ya uchaguzi kama ambavyo tumeweza kufanya ktk chaguzi ndogo mbalimbali kwahiyo kwahiyo tukijipanga vizuri tunaweza hata kwa nchi nzima dawa ni kujipanga mapema.

usaliti

Ili ni suala la hulka ya mtu, huwezi kumzuia mtu kama kweli hatazamilia kuufanya na ndio maana cdm wameamua kuachana na mfumo wa wagombea wa papo kwa papo kwa maana hao mara nyingi ndio wamegeuka kuwa wasaliti.

kwahiyo kila jambo lawezekana chini mbingu cha msingi ni dhamira tu kama utawala wa roma ulianguka basi ccm itafuata nyayo za KANU ya kenya.
 
Acheni kujazana ujinga. Ccm kina mizizi imara na mtandao wa uhakika nchi nzima. Hakuna kichama cha upingaji kinachoaminiwa tz kupewa dola. Kidumu sana ccm
 
Mtaji wa ccm ni utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi kwa kiwango cha juu kabisa. Barabara, bora nchini, shule za secondari kila kata, huduma za afya kila kijiji huku vyuo vikuu vikitapakaa kila kona kama njugu
 
mkuu suala la CCM kurudi madarakani halipo tena hata wasimamishe malaika, we don't need, They are tired and out of ideas.
50 years after independence, 70% of Tanzanians are dirt poor. Enough is enough

ccm haiondoki leo wala kesho madarakani. Mtalia na kusaga meno mpaka mkome. Watz wanaipenda sana ccm
 
Sio kweli wazee.
CCM ina mitaji mikuu miwili ya kushindia kura
1. UJINGA
Huu ni mtaji wqo mkubwa sana kisiasa maana kadiri nchi inavyokuwa na wajinga wengi ndivyo nafasi ya kukitoa chama tawala madarakani inakuwa ngumu. Mpaka sasa CCM imefanikiwa kuongeza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika na huu ni mtaji wao mkubwa sana. Wanafunzi wanaotoka sekondari za kati hawajui hata kujieleza sembusa kuinyima kura CCM?
2. VIJIJINI
Mabadiliko yoyote ya kisiasa huletwa na maendeleo. Kura nyingi za CCM zinatoka vijijini. Ni kura hizi ndizo zimemrudisha mugabe madarakani kwa kishindo. CDM hawajafanya juhudi za kutosha kufika vijijini nje ya vijiji vya kaskazini. Katika uandikishaji CCM wanahakikisha watu wa kijijini wanatoka kwa wingi kwenda kupiga kura na mijini mtapewa vichapo na polisi ili msijitokeze.
3. WIZI
Mpaka sasa CDM hawajapata dawa ya kuwadhibiti CCM kwenye wizi wa sanduku la kura zaidi ya kulalama barabarani.
4, USALITI
Chukulia mfano mpaka sasa sijapewa sababu za kutosha kwa nini Mgombea wa Igunga mwalimu Kashindye hakuwakilisha vielelezo muhimu kwenye rufani ya kesi iliyomnyanguanya ubunge Dr. Kafumu. Nilishangaa kuona akipokea kwa mikono miwili kushindwa kwake kwenye mahakama ya rufani. Huu ni usaliti. Tuna wagombea wengi tu ambao wamekuja CDM kwa masilahi yao wenyewe. Hawa wako tayari kuuza nafasi zao kwa CCM kwa gharama yoyote.
Mgombea yeyote wa CCM hata kama amebobea kwenye kuuza unga bado 2015 atashinda kwa kishindo. CDM wataongeza idadi ya viti bungeni.

umeandika ujinga mtupu. Watz hawawezi kuwapa dola watu wanaopanga mipango haramu ya kulisha watu sumu, wanamwagia watu tindikali na wanapora wake za watu. Ccm ni chama pendwa cha watz wote
 
Wamepeleka watu Zimbabwe kujifunza kuiba kura. Tuwe makini kulinda kura, daftari la wapiga kura na tume huru ya uchaguzi. Kwataarifa CCM ilishinda kihalali mara moja tu toka tumeanza mfumo wa vyama vingi na ilikuwa temu ya kwanza ya Kikwete.
 
Hakuna lenye Mwanzo lisikose mwisho.. ccm ndio inaaga madaraka hakuna kitakachoipasisha ccm kwa sasa imechoka ina migogoro taa ndani kwa ndani ina kashfa nyingi haina dira tena haina mwelekeo haina sera haina viongozi shupavu ,waliopo hawana maadili tena wamechanganyikiwa kilichopo saivi ni chukua chako mapema kila penye harufu ya pesa wanavamia kama kundi la mbwamweha likivamiavyo kiswalapala, 90% ya viongozi wa ccm wananuka rushwa wamejaa ufisadi tamaa na visasi, ccm c wamoja tena hata ile salamu ya kidumu chama cha mapinduzi haisikiki tena na hatta ukiisikia haina mvuto wala waitamkao hawana ujasiri
 
Haya mambo ya kuwaita watanzania ni wajinga ni kujifukuzia kura. Ccm itashinda tu nyie mnatoa akilini siye tunacheki upepo huku uraiani. Wasawahili walisema usimwamshe aliyelala...
 
umeandika ujinga mtupu. Watz hawawezi kuwapa dola watu wanaopanga mipango haramu ya kulisha watu sumu, wanamwagia watu tindikali na wanapora wake za watu. Ccm ni chama pendwa cha watz wote

Hata mimi nakubaliana kuwa tatizo sio CCM yetu. CCM yetu iko safi kimuundo na kwa sera pia. Hapa tatizo ni watu kama wewe na wale wote wa aina yako. CCM yetu imetekwa na na watu wa aina yako na wanaitumia kwa maslahi yao hata kama wanaichafua. Binafsi nionavyo kama CCM ingejua mapema na kujitenga na watu wa aina yako basi hadi leo tungeweza kutembea kifua mbele na asijitokeze mtu wa kuizomea.

Wachumia tumbo wachache sana ndio wameifikisha CCM yetu hapa ilipo. Mfano kama wewe mkuu unaweza ukawa ndio chachu ya kufanya CCM yetu ichukiwe na wengi. Huna hoja za msingi mbali na ushabiki usiokuwa na maana. Hizi siasa zenu za CDM na CCM zinalipeleka taifa sipo kabisa. Yaani inasikitisha sana kuona kundi la malimbukeni kama wewe eti wanaipigania CCM kumbe kwa ujinga wao ndio kwanza wanaiangusha aidha kwa makusudi au kwa kutokujua kwa kuwa ni wajinga na wenye upeo mdogo wa kufikiri.

Asilimia kubwa ya maanguko ya CCM katika chaguzi nyingi ni kauli na matendo ya watu wajinga wa aina yako waliojivisha heshima ya kukitetea chama. CCM imejengwa na wana CCM walio wema na wenye busara lakini itavunjwa na wajinga na wachumia tumbo kama wewe. Lakini ipo siku kama ikitokea ikaanguka basi tutaijenga tena kwa kuwa wachumia tumbo na wajinga wote watakuwa wamejitenga kando kwa sababu itakuwa haina tena maslahi kwao. Kidumu chama cha mapinduzi, na pia zidume fikra za mwenyekiti wetu mwanzilishi wa CCM mwalimu JK Nyerere.
 
swala la ccm kurudi tena madarakani ni ndoto mkuu

Hayo aliyosema ni kweli kabisa mkuu. Tuache ushabiki wa majukwaani kama hapa jf na kuelimisha watanzania popote na wakati wowote tunapopata wasaa huo. CCM wanatumia sana mtaji wa ujinga na hofu kwa wananchi wasiojua haki zao. Na pia wanatumia rushwa kwa wagombea wachumia tumbo.

Kama mambo hayo mawili yakichukuliwa kwa umakini mkubwa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa 2015, ccm itakuwa ndio imefika mwisho wa uhai wake.
 
Lakini mkuu hapa mimi sioni kama CCM ndio tatizo. Hapa tatizo haliwezi tatuliwa kwa kubadili chama cha siasa. Kinachotakiwa ni kupata watu sahihi wanaoweza kulinda na kutetea maslahi ya nchi yetu. Dhamira za hawa wanasiasa katika majukwaa ya siasa ni zimefichika sana. CCM sio tatizo bali tatizo lipo katika watu.
 
Nasema ni chama cha kikoloni kwa kuwa:
1.Ukionekana unakosoa au unapinga jambo fulani kwa maslahi ya umma unaonekana mvunja sheria.Hii ndicho chanzo cha kung'olewa meno na kucha bila ganzi,utesaji mfano Kibanda,kubambikiza kesi mathalani viongozi wa CHADEMA,kupigwa risasi mfano tukio la Sheikh Ponda,kuwawa hadharani km mwangosi.
2.Ukionekana unasema ukweli.Hapa ujiandae kufa ghafla kama Amina Chifupa,ujiandae kulishwa sumu kama Dr.Mwakyembe.
3.Ukionekana unadai haki unaonekana mhaini,mchochezi na mvunja amani ya nchi.Chukulia mfano watu wa Mtwara.Watu wamepigwa vya kutosha nk
Sasa kwa nini nisiseme kuwa serikali ya CCM ni ya kikoloni.
Marafiki wa chama cha mapinduzi ni hawa.
1.Waongo na wanafiki.
2.Mafisadi
3.Wala rushwa.
4.Wauza unga.
5.Majangili.
Na maadui wakubwa wa CCM ni
1.Wapenda haki.
2.Wadilifu.
3.Wasio mafisadi.
4.Wasio wala rushwa.
5.Wasio majangili
6.Wasema ukweli.
Watz tubadilike,kama mtakipa chama kingine madaraka halafu kikashindwa kufikia matarajio ya wananchi pigeni chini....hii demokrasia ya kweli.Kwa nini tung'ang'anie chama kimoja tu cha mafisadi ,wala rushwa,majangili.wezi,waongo na wanafiki? Tujaribu chama kingine tuone!!
 
Katika vitu ambavyo ni vigumu kuamini ni pamoja na serikali ya ccm kufumbia macho;mauaji ya raia wasio na hatia kwa mabomu,risasi nk,utesaji wa raia kwa kung'olewa kucha na meno.Najiuliza hii ndio ilani ya ccm?
Haiwezekani,viongozi wa ccm wakisifia serikali ya ccm kuwa ni serikali inayofuata utawala wa sheria.,huku watu wakipigwa risasi,wakiuawa hadharani nk.Hivi hawa ccm wanayaona haya? Je,kwenye vikao vyao wanayazungumzia haya? Na kama wanayazungumzia hatua gani zinachukuliwa? Au ndio kupandishana vyeo kwa kuua? Pia hawa viongozi wana ndugu waliowahi kufanyiwa unyama huu?
Niseme tu kuwa,hakuna serikali iliyo na roho mbaya na ya kiuaji kama ya ccm. Watu wanauawa mnapandishana vyeo,mnachekelea!je hii ndio ilani ya ccm kuua?
Hivi ninyi watu mna roho gani mbaya msioweza kusikia? Hivi wangekuwa ndgu zenu ndio wanauawawa kwa risasi na polisi,je kamuhanda mngepandisha cheo? Halafu mijitu kama Hamy-D,habari ya mujini,Ritz,zermacopolo,Ifweero,Mwigulu na mengine yanakuja kujisifia humu ndani.Hivi nyie watu mna roho gani mbaya isiyokuwa na huruma?
Hakuna kitu kibaya kuongoza nchi kwa urafiki,mkuu marafiki zake wanafanya madudu lakin anashindwa anzie wapi. Au ndio kulipana fadhila?
Hivi hawa akina,Hamy-D nk yalishawahi kuwakuta haya ya mauaji,utesaji nk kwa ndgu au marafiki zenu wa karibu?
Natamani kumuona huyu Hamy-D,Ritz,ze marcopolo nk,serikali inafanya madudu ninyi mnaisifia?Nawaombeni siku moja mzungumze kifupi katika haya
1.EPA
2.Richmond
3.Biashara ya madawa ya kulevya.
4.Mabilioni ya uswisi
5.Umaskini wa watz.
Msikalie kila siku kumfuatilia Dr.Slaa,Mbowe,Lissu,Lema,Mnyika,Zitto na CHADEMA.Teteni hoja tuhuma zinazo wakabili.
 
Mpaka sasa ccm imeshindwa kuongoza nchi. Amani haipo tena watu wanapigwa risasi mchana kweupe,wanateswa kama wanyama,wemeshindwa kutoa ulinzi kwa wananchi.

Wauza madawa ya kulevya wameongezeka mpaka sifa ya nchi yetu kimataifa imeingia dosari.Watanzania hawaaminiki tena nchi za wenzetu kisa tuliowaamini tukawapa ridhaa wameshindwa kuwajibika. Ni wakati sasa umefika CCM lazima ing'oke madarakani. Hapo mwanzo nilikuwa naipenda sana CCM lakini sasa hivi kwa upande wangu haina nafasi tena. Chama gani hakitaki hata kusikiliza maoni mbadala,watu wakisema wanaitwa wachochezi,hata huo uchochezi hawasemi.Wanataka waogopwe na kunyenyekewa kama miungu watu

Chama gani kimeshindwa kuleta mabidilko chanya kwa nchi yetu tunapitwa na hata Rwanda ambaye ilipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka kadhaa?

Nadhani hawatambui kuwa heshima yao inatokana na watu,wasipowachagua mtakuwa mtaani wa kawaida tu.
 
Wananchi wameanza kubadilika, serikali haina maana hii,ccm wasubiri tu 2015 maafa yao,jana nimeangalia itv wamama wanalia tu kwa kunyanyaswa na kufukuzwa kama wakimbiz mahali walipo,ila wananchi wa dar waache wanyanyasike tu kwan wao wanajidai kuipenda ccm..
 
Kwanini mpka 2015??? Ccm isipewe kura chaguzi zozote zile, mkingoja mpaka 2015 tutajidanganya.ikataeni ccm tangu sasa msingoje 2015.
 
WIZI MTUPU!!KWA KIPINDI CHA MWAKA 2009 PEKEE,MANUNUZI YA MAGALI HEWA YA SERIKALI NI JUMLA YA SH. Billion 4,018,535,583/=.KTK MAELEZO WANASEMA KUWA YALIDONDOKA BAHARINI WAKATI WA KUSAFIRISHA,LAKINI-HAKUNA MADAI YOYOTE KWA BIMA AU MSAFIRISHAJI!source!!!CAG.
 
Back
Top Bottom