Kidume kapewa kichapo, kisa zawadi za harusi

Kidume kapewa kichapo, kisa zawadi za harusi

Kabisaaa..mpimwe na weight ili muende sawa. Mambo ya kuingia hivi hivi mwisho wake ni kutoka mbio na kikaptula siku kikiwaka.
Teh Teh kwani ni uwanja wa masumbwi?,,,lakini muda mwingine unakuta mwanamke pande la mtu akianzisha mtiti mume salama yake ni kuchelewa kurudi au kukimbia nje....
 
Hivi Mimi Nisivyojua Kupiga mwanamke kila Siku Nitakuwa napigwa tu!!" Atoto Usisome hapa Ukajaribu Kunitia hata Singi Utarudi mbeya ukiwa kibogoyo
 
Khaaaaah!! Mwalimu wewe hiyo ndio ilikuwa lesson plan ati? Wish nami nipate nitakaekuwa namdunda, hadi raha.
 
Ukiwa ndani ya ndoa; kina dada wengi wana hii tabia, si unajua sis huwa tuko poa/netral hasa kwenye shared items/properties..,
Hata wanaume wapo wa hivo unaweza simangwiwa hata maji tu
 
Teh Teh kwani ni uwanja wa masumbwi?,,,lakini muda mwingine unakuta mwanamke pande la mtu akianzisha mtiti mume salama yake ni kuchelewa kurudi au kukimbia nje....

Kukimbia ndio noma zaidi bora tu kubaki ndani
tena akipigwa asitoe sauti anajisemea "yalaaa" ya kichini chini ha ha ha
 
Khaaaaah!! Mwalimu wewe hiyo ndio ilikuwa lesson plan ati? Wish nami nipate nitakaekuwa namdunda, hadi raha.
Jipatie msukuma mmoja, hawana shida hawa hata ukimpiga anakuambia "nitolage doho"
cc Kaveli kwa tafsiri zaidi
 
Last edited by a moderator:
Evelin salt hayo ni mapenzi tu, walikuwa wanacheza kidali po!
 
Jipatie msukuma mmoja, hawana shida hawa hata ukimpiga anakuambia "nitolage doho"
cc Kaveli kwa tafsiri zaidi

Weeee thubutuuu!! Mie nina msukuma na siwezi thubutu hata kumnyanyulia mkono, he is such a gentleman ila when it comes to being a man weee hataki ujinga kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Mmh kwa hiyo ni bora ukung'utwe tu? Inabidi umshtue kidogo ili asijisahau sana, atazoea kukudunda daily teh

hujasikia habari za shoka moja mbuyu chini? unaweza piga ngumi/kelb moja ikawa ndio umemaliza. kuwa mpole inaokoa mengi. halafu jamaa angejibu mapigo ndio angejaza watu ukumbini hiyo nayo ni noma kivyake...
 
Weeee thubutuuu!! Mie nina msukuma na siwezi thubutu hata kumnyanyulia mkono, he is such a gentleman ila when it comes to being a man weee hataki ujinga kabisa.

Huyo msukuma wa kichina bana, wasukuma wapole sana unaweza hata kuwaonea
 
Nikasikia makelele pale kwa jirani, kama vile wanapigana nikaona isiwe shida ngoja nijisogeze sio kwasababu za kiumbea lah ni sababu za kimsaada,hata kama ni umbea ni kidogo sana kikubwa msaada nikanyata hadi dirishani nkaona mwanaume kawekwa chini anapigwa,kimoyomoyo nikawaza ya leo kali, angekua anapigwa mwanamke ningejaribu hata kujikoholesha aachiwe sasa kwa kidume si ataona aibu sana mwisho aje anifanye mi mnyonge wake amalizie hasira zake kwangu.

Ikabidi niuchune na kutegesha antena ndani, muda huo kichapo kinaendelea na maneno yanawatoka. Chanzo cha ugomvi sasa: miezi kama kadhaa iliopita walifunga ndoa kila mtu akiishi kwake, kwakua mke ana vitu vya ndani tayari mwanaume akaona sio ishu kununua vingine wakati vipo (hawaishi wote kwa sababu ya kazi), mwanaume akamuomba mkewe kabati alilopewa kwenye kitchen party, mkewe akajibu "kabati lile ni langu na nimeamua kumpa dada yangu kwakua hana kabati".

Mme akasema ni sawa ila mbona haukunishirikisha? Mwanamke akageuka redio mmewe akauliza kwa busara kwahiyo na kile kiwanja na wale mbuzi tuliopewa kwenye harusi ni mali yangu peke angu? Mwanamama kusikia hivo akaamua adandie shingo ya mmewe.Hivi wanandoa mkishaoana vitu vyote si vya kwenu?hata kama unatoa kumpa ndugu si ni vema kushirikishana? Umiliki wa vitu ni kwenu wote hata braa ni yenu.

Nisharudi kwangu mie, karibuni parachichi :smokin:[dirishani

kumbe we ndo ulikua unachungulia dirishani...nilikuona ila sikutaka kukushtua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom