Kidume kapewa kichapo, kisa zawadi za harusi

Kidume kapewa kichapo, kisa zawadi za harusi

Evelyn Salt

Platinum Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
78,654
Reaction score
171,758
Nikasikia makelele pale kwa jirani, kama vile wanapigana nikaona isiwe shida ngoja nijisogeze sio kwasababu za kiumbea lah ni sababu za kimsaada,hata kama ni umbea ni kidogo sana kikubwa msaada nikanyata hadi dirishani nkaona mwanaume kawekwa chini anapigwa,kimoyomoyo nikawaza ya leo kali, angekua anapigwa mwanamke ningejaribu hata kujikoholesha aachiwe sasa kwa kidume si ataona aibu sana mwisho aje anifanye mi mnyonge wake amalizie hasira zake kwangu.

Ikabidi niuchune na kutegesha antena ndani, muda huo kichapo kinaendelea na maneno yanawatoka. Chanzo cha ugomvi sasa: miezi kama kadhaa iliopita walifunga ndoa kila mtu akiishi kwake, kwakua mke ana vitu vya ndani tayari mwanaume akaona sio ishu kununua vingine wakati vipo (hawaishi wote kwa sababu ya kazi), mwanaume akamuomba mkewe kabati alilopewa kwenye kitchen party, mkewe akajibu "kabati lile ni langu na nimeamua kumpa dada yangu kwakua hana kabati".

Mme akasema ni sawa ila mbona haukunishirikisha? Mwanamke akageuka redio mmewe akauliza kwa busara kwahiyo na kile kiwanja na wale mbuzi tuliopewa kwenye harusi ni mali yangu peke angu? Mwanamama kusikia hivo akaamua adandie shingo ya mmewe.Hivi wanandoa mkishaoana vitu vyote si vya kwenu?hata kama unatoa kumpa ndugu si ni vema kushirikishana? Umiliki wa vitu ni kwenu wote hata braa ni yenu.

Nisharudi kwangu mie, karibuni parachichi :smokin:
 
Una uhakika gani kabati alipewa kweli?

uswahilini watu hufanya maonesho tu ya zawadi halafu vitu hurudishwa kwa wenyewe...
vingine hukodiwa madukani

tembea uone

Ni uhakika kabati lake kweli
 
Naombeni kuuliza hela ya mwanamke huwa inafanya kazi/matumizi gani ndani ya ndoa?
 
Hii ni kweli...

Imenifanya nitafakari mara mbili



Una uhakika gani kabati alipewa kweli?

uswahilini watu hufanya maonesho tu ya zawadi halafu vitu hurudishwa kwa wenyewe...
vingine hukodiwa madukani

tembea uone
 
Yani mi nkimuona huwa nahisi aibu nikikumbuka kile kitendo, utadhani nilipigwa mie
akipita pita na singlend yake namuona bure kabisa anaaibisha singlend

Hahahaaa labda alikuona unavyochunguliamo akaamua kumuachia usije kumpeleka dawati la jinsia.
 
Yani mi nkimuona huwa nahisi aibu nikikumbuka kile kitendo, utadhani nilipigwa mie
akipita pita na singlend yake namuona bure kabisa anaaibisha singlend
Teh Teh eti noma sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom