Kidono/Kinkuti ni kitu gani?

Kidono/Kinkuti ni kitu gani?

Kidono ni Dawa ambayo imetengenezwa kwa mchanganyiko wa vitu mbalimbali (sitavitaja hapa) . Inaweza kukukinga na kitu chenyekuweza kujeruhi eg. Upanga, kisu, rungu, fimbo, chupa n.k.
Kidono kimetofautiana kidogo. Kuna ambacho unachanjwa kwa wembe au Majani makali na Kidono cha kunywa na soda. Ukichanjwa kwa wembe ni wembe pekee utakao weza kukukata lkn ukichanjwa kwa kutumia jani huwezi kujeruhiwa na kitu.
Wanakuchanja ukiwa umekalia baadhi ya vitu vinavyoweza kjeruhi. Pia ukipata kilicho imara hata risasi haiingii mwilini.

KINKUTI.
Hii ni dawa inayoweza kukupatia nguvu za ziada katika kupambana. Ukichanja kinkuti unauwezo wa kuumka mwili wako na ukawa unauwezo wa kupiga hata wanajeshi 100. Hua hakituliziki kirahisi.

MASHARITI YAKE.
Ukiwa na kidono ukijikata au kujipiga na kitu utaumia. Pia ukimruhusu mtu akupige utaumia.
KINKUTI kinafanya kazi mpaka ukiwa na hasira za kuchokozwa ukichokza basi hakifanyi kazi.
Vyote hivyo vinapatikana Kigoma na Congo
Kwa kifupi hii ni sayansi asilia yenye jina almaarufu 'UCHAWI'.
 
Ilitokea mwaka 2003/2004 huko mwambao wa ziwa tanganyika eneo la ikola mpanda mpakani na kongo walikamatwa majambazi wakawa wamevuliwa nguo zote na wajeshi wetu.
Mmoja kati yao risasi ilipigwa ikawa haifanyi kitu katokea kamanda mwingine pale pale alikuwa mngoni akasema nipe mashine nikuoneshe kazi.
Aliinua bunduki juu kama anapiga hewani then akaipitisha chini miguuni mwake kwa style aliyojua yeye alimtwanga yule jambazi kinyuma nyuma bila kumuona na risasi likamlenga akafa pale pale.
Wajeshi wengi wanajua kuwazindua na wakapigwa tu. Dunia duara.
 
Hapo umenena mkuu wangine wanahisi humu tunadanganya tu ila iko hivyo. Trick za kulogoloa hizo dawa watalaam tunazijua so kama mtu anakua anatumia dawa hizo kinyume baaasi tunajua tumfanyaje
 
Nipe maana ya uchawi

Al Azhari ambaye ni mtungaji wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo LisanulArab amesema Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shetani na kwa msaada wake (shetani)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako nikuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli..
Ama Sahaba Ibni Abbas (Radhiya Llaahu ‘anhu) amesema:"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."..
Hayo ni katika kamusi za lugha. Amma katika kamusi ya dini, maana ya neno Uchawi (AsSihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwaFakhruddin Al Razi kuwa; " Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mnahadaa (khidaa)"..
kwa hisani ya google na ndugu zetu wataalamu wa kiiwaislamu.
UCHAWI:1 NINI MAANA YA UCHAWI? | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today[/U]
 
Al Azhari ambaye ni mtungaji wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo LisanulArab amesema Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shetani na kwa msaada wake (shetani)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako nikuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli..
Ama Sahaba Ibni Abbas (Rauídhiya Llaahu ‘anhu) amesema:"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."..
Hayo ni katika kamusi za lugha. Amma katika kamusi ya dini, maana ya neno Uchawi (AsSihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwaFakhruddin Al Razi kuwa; " Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mnahadaa (khidaa)"..
kwa hisani ya google na ndugu zetu wataalamu wa kiiwaislamu.
UCHAWI:1 NINI MAANA YA UCHAWI? | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today[/U]
Ahsante mkuuu.
Nijibu maswali haya.
Unaweza kunithibitishia wapi nimeongelea au kuonyesha uchawi?
Nini tofauti kati ya uchawi na uganga?
Nipe historia ya uchawi ulianzaje.
 
Anayechanjwa anakalia kinu ama kiti cha miguu mitatu. Miguu anaweka kwenye ungo. Ndani ya ungo zinawekwa silaha aina zote. Mdomoni unabunda maji ili msiongeleshane during process then......... Mambo haya basi tu. Dunia hadaa ulimwengu shujaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom