Binafsi nahisi nilichanjiwa vitu flani kwenye mikono yangu nilipokuwa mdogo enzi naishi na marehemu babu yangu huko mbinga-nyasa(sasa hivi wilaya ya Nyasa).
maana Nina nguvu zisizo za kawaida hususani mikononi.
hata wafanyakazi wenzangu ninapo peana nao mikono,huwa wananiambia mikono yangu inanguvu sana.
lingine ni kwamba nilipofikisha umri wa utuuzima,familia yangu ilinitahalisha sana kutopigana na mtu yoyote.waliniambia sipaswi kumpiga mtu yoyote hata Kofi.
mara ya mwisho kumpiga mtu ilikuwa wakati nikiwa o-level jitegemee sec miaka kadhaa iliyopita.
alikuwa ni konda wa daladala za kutoka ukonga kwenda kkoo.baada ya mabishano ya hapa na pale na purukushani,nilimpiga ngumi moja nzito eneo la mbavuni.
kwa kilichomtokea konda yule,niliapa kutompiga tena mtu maisha yangu yote.taarifa zilipoifikia familia yangu,nililaumiwa sana.nikakumbushwa kuhusu onyo nililopewa la kutompiga mtu au kutopigana.