Kidono/Kinkuti ni kitu gani?

Kidono/Kinkuti ni kitu gani?

Vita ya majimaji,wale walopakwa dawa wakaambiwa wakipigwa shaba na mjerumani zitageuka maji,wajerumani wakawa wanajipigia shaba.360 scope
Hivi ni kweli ziligeuka maji ? Siyo kwamba ilikuwa ni propaganda ya Mtwa mkwawa kwa majeshi yake ili yaendelee na mapambano wasirudi nyuma hata kama mwenzao "kaonyesha ushujaa" ?
 
Tupe uzoefu wako mkuu maana jina tu linaonyesha naww ni wakwetu.
Tupe elimu boss
Subiri nikipata muda nitaanzisha Uzi wangu mwenyewe,ila sintogusia kiundan zaid isipokuwa nitaweka faida zake na hasara.Elimu hii niliipata toka kwa mkongomani alieitwa Kisimba!Huyu mzee alikuwa hatari sana!Usijali mkuu sisi ndio vijana wa ujiji,kabondo,majengo,rubuga nk ndio pande zetu za kujidai.
 
Subiri nikipata muda nitaanzisha Uzi wangu mwenyewe,ila sintogusia kiundan zaid isipokuwa nitaweka faida zake na hasara.Elimu hii niliipata toka kwa mkongomani alieitwa kisimba!Huyu mzee alikuwa hatari sana!Usijali mkuu sisi ndio vijana wa ujiji,kabondo,majengo,rubuga nk ndio pande zetu za kujidai.
Mkuu huyo mtu kwebye red alikua anaishi kazuramimba?
 
Niliambiwa nisingekuwa na mfupa mmoja ingekuwa rahisi sasa vina uhusiano gani na huu mfupa wakuu


# mshana jr na mondray
Nakuogopa ujue
Kaka mi ninavyo vyote nisaidieni namna ya kuondokana navyo wakuu.

Sio siri hua unafikia wakati mie najiogopa aseee, hua nikifika ugenini najikuta nakua mnyonge, sijichanganyi mahala panapoweza kunipa changamoto, yamenifanywa nikaachishwa mafunzo ya jeshi nateseka sana
 
Binafsi nahisi nilichanjiwa vitu flani kwenye mikono yangu nilipokuwa mdogo enzi naishi na marehemu babu yangu huko mbinga-nyasa(sasa hivi wilaya ya Nyasa).

maana Nina nguvu zisizo za kawaida hususani mikononi.

hata wafanyakazi wenzangu ninapo peana nao mikono,huwa wananiambia mikono yangu inanguvu sana.

lingine ni kwamba nilipofikisha umri wa utuuzima,familia yangu ilinitahalisha sana kutopigana na mtu yoyote.waliniambia sipaswi kumpiga mtu yoyote hata Kofi.

mara ya mwisho kumpiga mtu ilikuwa wakati nikiwa o-level jitegemee sec miaka kadhaa iliyopita.

alikuwa ni konda wa daladala za kutoka ukonga kwenda kkoo.baada ya mabishano ya hapa na pale na purukushani,nilimpiga ngumi moja nzito eneo la mbavuni.

kwa kilichomtokea konda yule,niliapa kutompiga tena mtu maisha yangu yote.taarifa zilipoifikia familia yangu,nililaumiwa sana.nikakumbushwa kuhusu onyo nililopewa la kutompiga mtu au kutopigana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom