Kibonzo: Mzee Kikwete hapa atakuwa ndio yupi na Rais Samia ndio yupi. Serikali inanichanganya

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,510
Naombeni msaada maana naona kama hapa kuna shida. Jamaa kajichorea watu na kaandika jina la mtu mmoja kuwa ni Kiwete.

Polisi wanasema kakosea huyo siyo Kiwete ni Kikwete. Na huyu anayechezea maji kwenye beseni wanasema ni Rais Samia.

But mchoraji yeye anasemaje? Kwanini wao waone hivyo na hii ni michoro ambayo huwezi thibitisha? Na huo uchambuzi wameutoa wapi? Kwanini wasiseme Baba anaongea na wananchi huku amemwacha mtoto wake wa kike achezee maji badala ya kumpeleka shule.

Kwanini wajenge dhana kuwa maana yake kuwa Rais Samia anaongozwa na Kikwete. Hii wameijenga kwa misingi gani? Au ndivyo wanavyoamini wao kiasi kwamba wanaamini kila mtu anaamini kama wao?

Anaongoza nchi vizuri? Nchi gani? Ya kusadikika? Ya Liberia au Sudan? Ya Mongolibo au ya Chechewani katika Bara la Gubang?

Screenshot_20211011-134929~2.png

Screenshot_20211011-134939~2.png
 
Bila shaka hao ndio wachochezi, Tena wanawataja walengwa Kwa kisingizio mchoraji kamaanisha waliowataja. Hivyo ilifaa hao ndio wawe washitakiwa Kwa uchochezi was kuwataja majina yasiyokuwepo kwenye mchoro wa msanii.
 
Walimzuia korokoroni mchora katuni kwa wiki mbili nzima wakati wanatengeneza tafsiri mpya ya mchoro huu.

Imenikumbusha tangazo lao la vigezo vya ajira walilolitoa hivi karibuni. Lakini akili inakataa kuamini polisi ni vilaza unlimited
 
Walimzuia korokoroni mchora katuni kwa wiki mbili nzima wakati wanatengeneza tafsiri mpya ya mchoro huu.

Imenikumbusha tangazo lao la vigezo vya ajira walilolitoa hivi karibuni. Lakini akili inakataa kuamini polisi ni vilaza unlimited
Ikataze akili yako kuamini hivyo😆.
 
Siku hizi hata humu kwenye mitandao ukiandika mafumbo ,wenye mitandao wanatafsiri wanavyohisi wao kisha wanakushughulikia.

Magu ameharibu sana hii nchi.
 
Huku ni Kupoteza muda na Resources kama Taifa. Ukizingatia kuna changamoto nyingi sana zinazotukabili na huu Uchumi wa Kati
 
Awamu ya nne ya kikwete ilikuwa ya majanga matupu!
Dowans!
Escraw!
Gas ya Mtwara
Bagamoyo Port
nk...................................
 
Back
Top Bottom