Kibongo bongo iPhone ni taashira ya hadhi au?

Kibongo bongo iPhone ni taashira ya hadhi au?

WANATAKA IPHONE HALAFU KUITUMIA HAWAJUI.

IPHONE WATUMIAJI NI WACHACHE KWA NCH ZA KIAFRIKA. MFN TZ, UNAWEZA KWENDA WILAYA NZIMA IPHONE UKAZIKUTA MBILI AU 3

ILA TECNO HADI MTOTO WA SHULE ANAYO

Samsung zimezagaa kama nywele

Sawa lakin iPhone ndio topseller wa dunia nzima hasa mwaka jana
 
Ishu sio kusave, hapa tunaangalia uwezo, unaponunua iPhone kwa pesa ya vizinga au kuhongwa kama ni mwanamke ili uonekane unayo na ukaishiwa mpaka kula unavizia na anayenunua Tecno kwa pesa yake na akabaki anakula ugali unazani nani tajiri hapo? Au nani anaishi kama Ng'ombe na nani ni mchunga Ng'ombe?
kwahiyo wewe kwako kula ndio utajiri?
wewe ndio masikini wa mwisho duniani..
 
wakuu kama kuna mtu yupo kwenye group la whatsapp la iOs naomba atanigusa PM tujumuike pamoja ili kupata maujanja zaidi kuhusu hizi simu zetu pendwa..
 
Natumia iPhone 8 plus(256GB).Nadhani ni suala la hobby tu washkaji zangu huwa wananishangaa why natumia simu ya gharama nawajibu kila mmoja ana interest Zake
Lakini before nilikuwa natumia Tekno boomJ nilikuwa sipo comfortable kabisa ila kwa hiki chuma cha sasa ni shida
 
Mtu kama mimi kwa internet ya hapa bongo hata uniuzie iphone 50000,sinunui ni kujitesa tuu.
 
asilimia kubwa ya watu duniani wanatawaliwa kifikra, wanadhani kuwa na kitu chenye gharama kubwa ndo heshima. Ila mtu anaejitawala kifikra iphone au kitu chochote kile hakiwezi msumbua akili. Maana hakuna kitu chochote chenye gharama kinacho shinda "UHAI" so ukiwa hai hiyo ni hadhi au heshima tosha. huna haja ya kumiliki bugati ili uheshimike, huna haja ya kuwa na iphone ili uheshimike, unahaja ya kuvaa gucci, vasach, luiv nakadharika ili uheshimike au uonekane unahadhi. inabidi uamke we bongolala acha kutawaliwa na material things.
 
Hayo ni maneno tu kiukweli iphone ina sound good ila sio kwamba ina bei kubwa kuna simu inaitwa vertu 2013, 2015 hii inatengenezwa UK gharama yake tu vitz mbili unabakiza na ya mfukoni
 
Hayo ni maneno tu kiukweli iphone ina sound good ila sio kwamba ina bei kubwa kuna simu inaitwa vertu 2013, 2015 hii inatengenezwa UK gharama yake tu vitz mbili unabakiza na ya mfukoni
Vertu umeenda mbali sana.

Kwani kuna iphone ngapi za milioni 1.5,
Ambazo zinakwenda sawa na bei ya androids kibao tu,
 
Vertu umeenda mbali sana.

Kwani kuna iphone ngapi za milioni 1.5,
Ambazo zinakwenda sawa na bei ya androids kibao tu,
Zipo nyingi ila hili wengi wanapenda sifa tu kutumia big brand kama apple na samsung ila kuna simu zina hadhi zaidi ya hiyo sema majina ndio hakuna au saa nyingine upatikanaji na bei zake
 
Mi natumia iPhone si kwasababu ya hadhi ama nini, nimevutiwa sana Na features za hii brand kwakweli ni tofauti kabisa na simu zingine hasa kwenye ishu ya privacy.

iPhone unaweza inadumu, spika, mic, screen zake zina quality nzuri sana bado sijaona simu nyingine
 
Mimi Ninapotaka kununua simu kwanza najiuliza ninunue simu ya Android Device or Iphone ios Device?
kisha hiyo simu iwe na screen size 5.5
Battery life 24hrs
storage and memory ,3 to 4 RAM 64 GB
camera mp 20 MP
 
Alafu simu sio kigezo cha kuoneka upo na high life sema ndio utaratibu uliopo kwa watz

Wabongo utawaweza, mtu ukisema ujitafutie kitu chako cha kudumu kinachokuridhisha, utasikia wanakuita limbukeni, mi siwezi pangiwa lakufanya vile vile kupangiwa aina ya simu ya kutumia.

Mwisho wa siku kila mtu amiliki apendacho atumie apendacho
 
Wabongo utawaweza, mtu ukisema ujitafutie kitu chako cha kudumu kinachokuridhisha, utasikia wanakuita limbukeni, mi siwezi pangiwa lakufanya vile vile kupangiwa aina ya simu ya kutumia.

Mwisho wa siku kila mtu amiliki apendacho atumie apendacho
Kama mie nokia kesha niteka kabisa na ile camera ya carl zesis yaani sio ile yenye window au android kama ina camera ya carl basi mie roho yangu inapoa kabisa
 
Back
Top Bottom