Kibongo bongo iPhone ni taashira ya hadhi au?

Kwahyo mlitaka hata meseji tuandikie ziko kwenye mikoba au mfukoni tuwe tunaficha Sema hiv iPhone ikitolewa nje ikashikwa mkonon kuandika meseji au kuongea hata uwe chato halafu niko dar unaiona tuuuu tunda linapendeza sana

Mkuu ninatania kunogesha genge, my priorities kwenye simu ni Fast Internet, display size and resolution and battery durability.

Otherwise sina wasiwasi nikiona mtu ameshika iPhone kwa sababu najua ni priorities, na sinunui simu kwa fasheni, na anayenunua kwa fasheni hanishangazi pia.
 
Hahahahahah, Acha tujiliwaze, kwani nisiponunua IPhone ndo ntakuwa Tajiri au Matatizo yataisha!

Mie Maskini Mwenye IPhone na Maskini mwenzangu Mwenye Techno Mbona Hana nafuu Kwa hiyo aliyosave!
Ishu sio kusave, hapa tunaangalia uwezo, unaponunua iPhone kwa pesa ya vizinga au kuhongwa kama ni mwanamke ili uonekane unayo na ukaishiwa mpaka kula unavizia na anayenunua Tecno kwa pesa yake na akabaki anakula ugali unazani nani tajiri hapo? Au nani anaishi kama Ng'ombe na nani ni mchunga Ng'ombe?
 
Acha Watu wajiliwaze Mkuu!

Matatizo ukiyavalia Mkwiji utaumiza Kiuno!

Hata Maskini nae Ana haki ya kufurahi hata Kama gharama ya furaha ni ghali kiasi gani!
 
Halafu hiyo laki 7 uliyosave unaenda kuhonga Mwanamke au kulewea kwa wiki Moja !
Nakuambia haya yote cause mimi ni mmoja kati ya watu waliotumia iPhone karibu generation zote kasoro hii iliyotoka juzi, baada ya kuibiwa hii ya mwisho niliyokuwa nayo nikaona haina maana tena ya kumiliki simu ya 1m wakati kuna investment nyingi naweza kuifanyia hiyo hela, technology is too expensive hasa ukitaka kwenda na wakati! Lakini mwisho naheshimu kila mtu na mawazo/kitu anachokipenda katika maisha.Mimi nishatoka huko kabisaa, inatosha.
 
Mkuu ninatania kunogesha genge, my priorities kwenye simu ni Fast Internet, display size and resolution and battery durability.

Otherwise sina wasiwasi nikiona mtu ameshika iPhone kwa sababu najua ni priorities, na sinunui simu kwa fasheni, na anayenunua kwa fasheni hanishangazi pia.

Yani hzo x-tics ulizotaja ndo kama mimi baaasi
 
Nianze na fasili kwanza maana wengi wenu nyie 'millennials' hamjui lugha. Iwe Kiswahili au Kiingereza, hamko vizuri kivile. Ni wababaishaji tu:D.

Taashira maana yake ni ishara/ au dalili. Naamini mnajua maana ya ishara na dalili.

Sasa kuna jambo nimeliona ambalo ningependa kusikia maoni ya wengine kulihusu.

Hivi hapa bongo iPhone ni ishara ya hadhi [ya juu]? Nauliza hivyo kwa sababu nimeshapigwa sana mizinga ya 'Ngabu naomba niletee iPhone basi...hata kama ni iPhone 5 au iPhone SE'.

Kwa nini iPhone kwa sana na si Samsung, LG, Motorola, au zinginezo?

View attachment 632283

Mkuu uliposema “Hivi hapa bongo Iphone ni ishara ya hadhi ya juu?” Una maanisha nini na neno ‘hapa’ ili hali unadai hauko hapa nchini? Au una maana (hapa=Jamiiforums) naweza sema hapana kwani wanaokuomba uwaletee si wanajamiiforums
 
Ni wapi nimedai sipo hapa nchini?
 
Back
Top Bottom