Je na wale walokamatwa niwatu gani basi wawaachie kama walengwa bado wanaendelea kusumbia!yani hao jamaa bana, hata kukamatwa hawakamatwi sjui hata kama polisi wetu wanajua walipo
Kuna mtu niliona mahali akisema wauaji huacha ujumbe wa kuchoshwa na ukandamizaji. Uonevu nk.Wazee mlioko JF, naomba tu kuuliza, Je, Kuna ubaya gani, IGP akirudisha majeshi nyuma na kusema, Tupatane!!! Hatutamtafuta muuaji tena, ila tupeni wajumbe, waje kueleza kisa ni nini??
Tuwape Amnesty ya kweli kabisa halafu tukiisha jua chanzo, tuyatengeneze hayo mambo?? Ni wazo tu. Nasema hivi kwa sababu, Rwanda walikubaliana kusahau mauaji ya kutisha tu. South Africa nao walifanya hivyo. Sisi tukifanya hivyo sio woga bali ni kutaka kukomesha vifo vya ndugu zetu.
Naomba nieleweke. Kama Kamanda Sirro katoa donge la 10 mill na bado mauaji yanaendelea, nadhani watu wamelidharau donge hilo. Tujaribu Amnesty. Komesha haya mauaji kwa kuketi tujadiliane.
Naomba niseme; Sina chochote nitapata huko wala sina chochote Kibiti. Ni maumivu ya moyo yalonipata kusikia tena; Ati, kauawa mtu kwa sababu tu alikuwa mgambo. Tupatane kabla hajauliwa mwingine. Wakitudharau, hata Mola yu aona, atawafunua.
Huyo mtu abavujisha siri vijiji vyote ??Kuna mtu anavujisha siri kwa hao wauaji na ndio maana wao wanafata kuua kwa malengo hawaendi hovyo na huwa hawamkosi mtu
Ataenda mwenyewe kuwatafuta ? Au atatumia watu walewale ,Hata Fundi Mitambo akipanga Microphones kwanza huwa anazijaribu hivyo yawezekana hata hao Wauawaji baada ya Police Tanzania kuwekewa mashine mpya iitwayo IGP sasa na wao wameona si vibaya kuifanyia majaribio ili kuweza kujua uimara wa kutukuka wa IGP machine.
Kazamoyo Ipo ikwiririIGP Siro , mtihani wa kwanza huo .
Tunasubiri majibu yake, maana wameanza kufata watu na kuwaua hadi uvungni mwa kitanda.
maana wasipodhibitiwa watakuja kuwafata wenye mchanga wa makanikia hadi huko shimoni.
R.I.P mgambo wa kibiti.
Tanzania hatuna database ya DNA na hatuna Criminal Investigation Laboratory hivyo kuwajua kwa vipjmo hivyo ni ngumu sanaKama wamemtafuta mpaka uvunguni lazima wameacha alama, Police watumie DNA test waweze kuwapata
Yawezekana ni mauaji ya visasi, wanadai watu wa huko walikuwa wanategemea sana mazao ya misitu kama mkaa na mengineyo kuendesha maisha yao, na kumekuwa na uonevu mkubwa sana kwao toka kwa viongozi wa vijiji, maafisa misitu na mgambo labda pia na askari. Nimesikia tu na sijathibitishaSo sad. Huko kutakuwa kuna tatizo kubwa ambalo watu hawataki kuliadress, mwisho wa siku wanauwawa wananchi ambao hata kazi wanazofanya haziwanufaishi. Unauwa mgambo, kwa kipi alichonacho?
Kuna mtu niliona mahali akisema wauaji huacha ujumbe wa kuchoshwa na ukandamizaji. Uonevu nk.
Kwa hali hiyo ni ngumu kujua uonevu kwa upande upi maana nchi yetu ni kubwa na yanayotokea ni mengi sana pande mbalimbali.
Jaribu tuu kufikiri yaliotokea bungeni juzi, wengine hawakuridhika na wengine wanachekelea,
Sasa ukiangalia waandishi wanaopita huko kibiti wanakuja kuandika inaonekana jamaa hawana pa kusemea na pengine hawaoni kama kuna jinsi yoyote ya kusikilizwa hivyo ni namna ya kufikisha ujumbe kwa wahusika.
Mawazo yangu, katika pitapita zangu humu.