KIBITI: Askari mgambo auawa kwa kupigwa risasi

KIBITI: Askari mgambo auawa kwa kupigwa risasi

Mkazi wa Kitongoji cha Kazamoyo, wilayani hapa, Erick Mwarabu (37) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku akiwa nyumbani kwake. Watu wa karibu katika eneo hilo wamesema marehemu huyo aliyekuwa askari mgambo alipigwa risasi tatu akiwa uvunguni mwa kitanda alikokuwa amejificha.

Mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Simon amesema watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivunja mlango wa nyumba yake saa 9.00 usiku kisha kuingia ndani na kutekeleza mauaji hayo.

Simon amesema baada ya watu hao na kuingia ndani walipitiliza moja kwa moja hadi kwenye chumba chake ambapo walimkuta mkewe marehemu na kumhoji alipo mumewe. Amesema baada ya kuona mkewe hataji mahali alipo mumewe walianza kumtafuta ndani ya nyumba yake na kufanikiwa kumuona marehemu akiwa amejificha uvunguni mwa kitanda ndipo wakamfyetulia risasi na kuondoka.

Simon amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote. Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Dk Iddy Malinda amesema katika uchunguzi walioufanya walibaini marehemu alikuwa na majeraha matatu ya risasi katika maeneo tofauti ya mwili wake.

“Majeraha mawili yalikuwa kwenye ubavu wa kulia na moja kichwani,” amesema. Dk Malinda amesema mwili huo tayari umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema polisi wanaendelea kufuatilia tukio hilo.

Source: Askari mgambo auawa Kibiti

Hata Fundi Mitambo akipanga Microphones kwanza huwa anazijaribu hivyo yawezekana hata hao Wauawaji baada ya Police Tanzania kuwekewa mashine mpya iitwayo IGP sasa na wao wameona si vibaya kuifanyia majaribio ili kuweza kujua uimara wa kutukuka wa IGP machine.
 
Huko kibiti bado ngoma nagwa!kunatakiwa Busara na hekima kutatua matatizo huko syo mabavu....

OvA
Kweli kabisa mkuu.
Huko kunahitaji,busara na hekima tu. Wawayumie viongozi wa dini mbalimbali waone itasaidia vipi.
Lakini serekali yenyewe hii Kama haijali instead wanaadhibu wananchi wasio na Hata Ndio Maana wanakosa ushirikiano.
 
Sasa ujambazi wao ni nini kama hawajaiba kitu zaidi ya kuua mtu na kuondoka, hao ni majambazi au wauaji?
 
Jiulize vitu hiv Kwann Jambazi asichukue kitu chochote kile ata kiberti sote twafaham Jambazi ama Majambazi huvamia kwa lengo moja tu nalo ni kupora mali ya mtu. Pili Kwann hawajamdhuru mke wake moja kwa moja wamemlenga mumewe tena mpaka wanamsaka uvunguni, hawa jamaa inaonesha wanalenga sana shabaa yao.
 
kulala saa 12
Mwisho kuonekana sa 12
Police wametanda kila kona

Force imetumika kubwa ila bado hitmen wanafanya yao na kutoka bila hata ya majirani kujua

Intellijensia ndogo

Au hitmen ni watalaamu sana maana kwa wanavyotekeleza mauaji kimya kimya kama spies wa KGB
ata kama polisi watatanda hawawezi wakalinda kila nyumba..
 
Tuwe wakimya kwani Naamini serikali yetu ni sikivu na hili suala lazima itakuwa inalifanyia kazi kwa ukari sana kwani silakufumbia macho ni swala linahusu usalama wa taifa.
 
So sad. Huko kutakuwa kuna tatizo kubwa ambalo watu hawataki kuliadress, mwisho wa siku wanauwawa wananchi ambao hata kazi wanazofanya haziwanufaishi. Unauwa mgambo, kwa kipi alichonacho?
Labda walimhisi ni spy
 
Hao huwez kuita Majambazi mimi nafkiri kuna mtandao unalipa kisasi kwa mtandao mwingine maana kama hawachukui vitu wanataka nini? Tuachieni nchi yetu nyie Wauaji au mseme mnataka nini tujue moja.
Wanataka roho zetu basi kwahyo tuwape?
 
Katika mauaji ya kuogopesha ni hili la muuaji kutochukua chochote,hapa mauaji yataendelea tu.watu wanataka kulipa kisasi na vitu kama hivyo.tusubiri mengi kama hatua hazitachukuliwa.
 
Back
Top Bottom