KIBITI: Askari mgambo auawa kwa kupigwa risasi

Kama wamemtafuta mpaka uvunguni lazima wameacha alama, Police watumie DNA test waweze kuwapata
Samahani mkuu hivi kwa tanzania mtu akiacha dna au finger prints tuna database ambayo inafanya reference na kuwatambua au inakuaje naona kama vyanzo (database) vya kupata taarifa hizi havipo
 
DNA ??? Unadhi kirahisi hivyo???? Mambo ya muvi za US unaleta huku kolomije???? Do you have a database anyway!!!!!
Hahaha good point nimemuuliza jamaa kama zile data za vitambulisho vya taifa bado magumash ijekua dna ?
watoto wenyewe wakizaliwa rekodi zao hospitali hazina dna hata utunzaji wake ni wakwenye makaratasi
 
Mkazi wa Kitongoji cha Kazamoyo, wilayani hapa, Erick Mwarabu (37) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku akiwa nyumbani kwake. Watu wa karibu katika eneo hilo wamesema marehemu huyo aliyekuwa askari mgambo alipigwa risasi tatu akiwa uvunguni mwa kitanda alikokuwa amejificha.

Mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Simon amesema watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivunja mlango wa nyumba yake saa 9.00 usiku kisha kuingia ndani na kutekeleza mauaji hayo.

Simon amesema baada ya watu hao na kuingia ndani walipitiliza moja kwa moja hadi kwenye chumba chake ambapo walimkuta mkewe marehemu na kumhoji alipo mumewe. Amesema baada ya kuona mkewe hataji mahali alipo mumewe walianza kumtafuta ndani ya nyumba yake na kufanikiwa kumuona marehemu akiwa amejificha uvunguni mwa kitanda ndipo wakamfyetulia risasi na kuondoka.

Simon amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote. Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Dk Iddy Malinda amesema katika uchunguzi walioufanya walibaini marehemu alikuwa na majeraha matatu ya risasi katika maeneo tofauti ya mwili wake.

“Majeraha mawili yalikuwa kwenye ubavu wa kulia na moja kichwani,” amesema. Dk Malinda amesema mwili huo tayari umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema polisi wanaendelea kufuatilia tukio hilo.

Source: Askari mgambo auawa Kibiti
Iyo hali itaendelea miaka yote kwakuwa serikali inatumia nguvu kutatua tatizo badara ya kutumia akili ili kujua chanzo cha matukio yote
 
Kama walianza kuwauwa viongozi wa ccm wakiisha hawa wa chini watapanda ngazi na kufika pale juu kabisa inabidi serikal ichukue hatua mapema hata vikundi vya kigaidi vinaanza hivi
 
Mkazi wa Kitongoji cha Kazamoyo, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, Tanzania Erick Mwarabu (37) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.

Watu wa karibu katika eneo hilo wamesema marehemu huyo aliyekuwa askari mgambo alipigwa risasi tatu akiwa uvunguni mwa kitanda alikokuwa amejificha
Mkazi wa Rufiji apigwa risasi Tanzania
 
Tusijitoe ufaham katika hili, kwa mfululizo huu wa mauaji ni lazima kuna jambo linaloendelea huko,
1) wanaua bila kuchukua chochote.
2) wanaua watu wenye nyadhifa fulani.
3) hawajulikani na hawakamatwi inamaana wanamafunzo fulani.

Ushauri wangu viongozi wajitafakari kuna mahali kuna matatizo, kama wanaua bila kuchukua chochote wao wanapata maslahi gani.......
 
selikali ituambie ukweli tu ili raia tujitambue kuliko kutuficha maana awajamaa kama c magaid basi uko kibiti watakuwa wanampango wa kujitenga mi cwez kubali kama aya mauaji yanafanywa na mjambaz alafu wasiibe ki2....
 
Haya mambo yanatokea Uingereza na Marekani mataifa makubwa yenye nguvu kijeshi na kiteknolojia itakua kwetu? Msaada upi unahitajika? unataka kusema apeleke jeshi na mizinga akaingamize kibiti nzima? Kupigana na mtu usiyemjua lakini yeye anakujua si jambo jepesi hata kidogo, tusilete siasa kwenye mambo ya kiusalama kama haya mkuu?

Nikusamehe bure tu, sababu hujui unachoongea na kikubwa usiwe unasoma soma mambo kwenye magazeti au stori za vijiweni na wewe ukajiona unajua naomba niishie hapo.
 
amid of these atrocity we believe the perpetrators are going to be revealed.
MHSRIP our Front line Soldier.
 
Magaidi au freedom fighters? "Saint" Mandela aliwahi kutuhumiwa na kushitakiwa ugaidi na Serikali dhalimu ya makaburu. Tanzania inashuhudia low level insurgency Kibiti. Huu ndio ukweli.
Tatizo hawaweki lengo lao wazi,ndo maana wanakosa msaada,kama wanapigania Uhuru wa pili waseme basi.
 
Hivi hao wauaji wako smart mpaka simu hawatumii.thinking aloud pelekeni vijana tcra wafuayilie mawasiliano around kibiti for past three months. M-PESA movements wasafiri , new line registered. Etc
 
Back
Top Bottom