KIBITI: Askari mgambo auawa kwa kupigwa risasi

kulala saa 12
Mwisho kuonekana sa 12

Force imetumika kubwa ila bado hitmen wanafanya yao

Intellijensia ndogo

Au hitmen ni watalaamu sana maana kwa wanavyotekeleza mauaji kimya kimya kama spies wa KGB
Mkuu hawa jamaa ni kama KIDON kile kitengo mahususi cha mauaji chini ya Mossad.
 
Tulishasema eneo hilo linahitaji uchunguzi wenye weledi na si vipigo kwa wasio na hatia.
 
mfano yanayoendele nchi za ulaya na Amerika raia kuuliwa kwa kuchomwa visu,vilipuzi na hata kupitisha gari na kugonga raia wema ni matokeo ya ukandamizaji wa mataifa yao kuwakandamiza mataifa machanga huko mashariki ya kati,wanachofanya ni kutuma message mnachokifanya hata wao wanaumia .the same scenario reflect what happen kibiti and Rufiji.busara ya hali ya juu inahitajika mambo ya mwaga mboga nimwage ugali hayatasaidia wananchi wasio na hatia wanapata tabu.hivo vijiji vitaingia kwenye umasikini nguvu kazi inakimbia yote au mpaka Mwalimu afufuke ndio busara kwa viongozi zitarudi
 
Wazee mlioko JF, naomba tu kuuliza, Je, Kuna ubaya gani, IGP akirudisha majeshi nyuma na kusema, Tupatane!!! Hatutamtafuta muuaji tena, ila tupeni wajumbe, waje kueleza kisa ni nini??
Tuwape Amnesty ya kweli kabisa halafu tukiisha jua chanzo, tuyatengeneze hayo mambo?? Ni wazo tu. Nasema hivi kwa sababu, Rwanda walikubaliana kusahau mauaji ya kutisha tu. South Africa nao walifanya hivyo. Sisi tukifanya hivyo sio woga bali ni kutaka kukomesha vifo vya ndugu zetu.
Naomba nieleweke. Kama Kamanda Sirro katoa donge la 10 mill na bado mauaji yanaendelea, nadhani watu wamelidharau donge hilo. Tujaribu Amnesty. Komesha haya mauaji kwa kuketi tujadiliane.
Naomba niseme; Sina chochote nitapata huko wala sina chochote Kibiti. Ni maumivu ya moyo yalonipata kusikia tena; Ati, kauawa mtu kwa sababu tu alikuwa mgambo. Tupatane kabla hajauliwa mwingine. Wakitudharau, hata Mola yu aona, atawafunua.
 
Haya mauaji ya Kibiti yananikumbusha kuna miaka flani kule Mugumu, Serengeti mkoani Mara watu walijitengenezea Jamhuri yao na kupandisha bendera ya Chui.

Sasa mauaji yanayoendelea Kibiti unaweza ukasema hao wauaji ni kama wamejitengenezea Jamhuri yao yaani ni Untouchable na Jamhuri yetu.

Ubabe haujawahi kuwa suluhu ya matatizo yanayomwandama Binadamu.

Busara itumike ili kuepusha matatizo zaidi kwa ndugu zetu wa Kibiti.
 
Jamani huko kibiti hata wanainchi wameshindwa kujua au kutoa taarifa!! mbona wanaouawa ni ndugu, jamaa na marafiki zao!!

Jeshi la polisi tumieni njia nyingine kama hiyo ya sasa imeshindwa mjue wapi chanzo cha tatizo, sasa majambazi wanaua mtu bila kuchukua chochote huyo ni jambazi kweli! mbona mkewe wamemuacha tena inaonekana hawakuwa na shida na mke kabisa.

Wananchi wa huko msipotoa ushirikiano wa kutosha mbona itakuwa hatari sasa!!!!
 
Back
Top Bottom