KIBITI: Askari mgambo auawa kwa kupigwa risasi

Askari mgambo wilayani kibiti anayefahamika kama Erick Mwarabu (37) ameuawa usiku wa kuamkia leo mnamo saa 9:00 akiwa nyumbani kwake.
Mwanaume huyo aliuawa baada ya kuonekana akiwa amejificha uvunguni mwa Miranda chake, ndipo watu hao wakamfyatulia misumari takribani mitatu na kutowaka.
KAZI KWAKO IGP SIRO
 
Police wetu bado wanasafari ndefu sana kwa upande Wa intelligence department kwakweli haiwezekani tangu tumeanza kusikia mauwaji ya kibiti na bado yanaendelea na pia hatujuh yatatufikisha wapi wananchi. Then kwa intelligence yenu inaoneka imefika mwisho kwa kuwaambia wananchi mwisho Wa kutembea ni saa 12 jioni.you people you have to do something in kibiti you have to sit down with wananchi.Am sure if our policeman they will be friendly with wananchi of kibiti they will come up with something that can help them in investigation rather than be hard to them.
 
tatizo selikali yetu haitaki kuwa lafiki na wananchi kwaili tutaona mibavu yao itaishia wap
 
Askari mgambo auawa Kibiti

Watu wa karibu katika eneo hilo wamesema marehemu huyo aliyekuwa askari mgambo alipigwa risasi tatu akiwa uvunguni mwa kitanda alikokuwa amejificha.

Soma zaidi: Askari mgambo auawa Kibiti


Mwananchi online
 
Waziri wa Mali asili na utalii Prof. Magembe ndio anaweza kutoa suluhisho. Na wa kilimo nae kwa 20%. Wawezeshe kiuchumi wawafanye wafaidi rasilimali zao they will cool down.
 
So sad. Huko kutakuwa kuna tatizo kubwa ambalo watu hawataki kuliadress, mwisho wa siku wanauwawa wananchi ambao hata kazi wanazofanya haziwanufaishi. Unauwa mgambo, kwa kipi alichonacho?
Dhulma,uonevu,ubabe....chakushangaza bado serikali na vyombo vya usalama vinatoa kauli zile zile za ubabe badala ya kutafuta sababu ya haya mauaji

Unapojarbu kumdhibiti mwanadamu mpaka anakosa raha za maisha matokeo yake ndio hayo
 
Kwa maoni yangu suala la kibiti linaongelewa zaidi midomoni.. Kila linapotokea tukio tunasikia maneno makali, viongozi kutembelea kwenye crime scenes, then wanarudi kwenye maofisi yao na maisha yanaendelea kama kawaida kwao.. Naendelea kushauri kunatakiwa kutafutwa ushahidi wa kisayansi zaidi kuliko huu wa kuwatisha na kuwabughudhi wakazi wa maeneo hayo, ambayo nayo imekuwa ni kero nyingine.. Hawa wauaji wanaacha clues kwenye matukio.. Alama za vidole, risasi zilizotumika, footprints, na mengi mengineyo.. Hapa ndipo Jeshi la polisi lingeomba msaada toka kwa wenye utaalam wa uchunguzi kama huo kama Scotland yard.. Na wala haitakuwa mara ya kwanza kuomba msaada toka Scotland yard au FBI.. Hii issue sasa imeshakuwa kubwa.. Jini limeshatoka nje ya chupa.. Tunahitaji msaada toka kwa wenye utaalam..
Pm majaliwa alisema wanauwezo kwa hiyo hawairaji msaada kutoja nje
Hii ni kipindi akijibu swali juu ya kumtafuta ben saanane
Polen wana kibiti na wafikwa wa majanga.
 
kwa jinsi inavyoelekea, suala si ubora wa IGP. suala linaonekana dhahiri ni uhitaji wa kutendeka haki katika jamii across the board!

kama bunge tu limeshindwa kujipambanua kama chombo cha kutenda haki, seuze huku mtaani?

nchi isharogwa hii!
 
Back
Top Bottom