KIBITI: Askari mgambo auawa kwa kupigwa risasi

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
9,036
2,000
Mkazi wa Kitongoji cha Kazamoyo, wilayani hapa, Erick Mwarabu (37) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku akiwa nyumbani kwake. Watu wa karibu katika eneo hilo wamesema marehemu huyo aliyekuwa askari mgambo alipigwa risasi tatu akiwa uvunguni mwa kitanda alikokuwa amejificha.

Mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Simon amesema watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivunja mlango wa nyumba yake saa 9.00 usiku kisha kuingia ndani na kutekeleza mauaji hayo.

Simon amesema baada ya watu hao na kuingia ndani walipitiliza moja kwa moja hadi kwenye chumba chake ambapo walimkuta mkewe marehemu na kumhoji alipo mumewe. Amesema baada ya kuona mkewe hataji mahali alipo mumewe walianza kumtafuta ndani ya nyumba yake na kufanikiwa kumuona marehemu akiwa amejificha uvunguni mwa kitanda ndipo wakamfyetulia risasi na kuondoka.

Simon amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote. Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Dk Iddy Malinda amesema katika uchunguzi walioufanya walibaini marehemu alikuwa na majeraha matatu ya risasi katika maeneo tofauti ya mwili wake.

“Majeraha mawili yalikuwa kwenye ubavu wa kulia na moja kichwani,” amesema. Dk Malinda amesema mwili huo tayari umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema polisi wanaendelea kufuatilia tukio hilo.

Source: Askari mgambo auawa Kibiti
 

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,523
2,000
Mwigulu Nchemba your ignorance itawamaliza ndugu zetu.

Hapa tulipofikia jeshi letu la polisi linahitaji msaada, please be brave and do what needs to be done.

Mpaka lini? au mpaka mji ubaki na magofu ndiyo mjue muuaji, you are so comfortable on this matter.

If you can't make change be the change and step out now!!.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom