FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,778
- 46,868
Upatu ni sawa na benki uchwara
Mnachukua hela zenu mnapeana kwa zamu mi siamini kabisa katika uwekezaji au biashara ya namna hii wa hela wanaofanya watu wengi haswa wanawake (kibati) naona kama kujidanganya vilee.
Kwanini usikae na hiyo hela mwenyewe labda kama ni miezi 3 ukawa umeizalisha zaidi? Ukanunua hiki ukauza hata ukikopesha inalipa kuliko kibati.
Acheni kujidanganya hakuna faida kwenye kibati.
Hii kitu haina faida. Hela kuzimudu kwanza lazima uwe na nidhamu ya hela. Lazima ujue kuweka hela. Lazima ujue kutumia hela vizuri.Hiyo tsh.2000 uikusanye mpaka ifike tsh.150000 na shida hii unaweza kweli ,sidhani .
Ila kwa mtindo wa kumchangia mmoja mmoja,inakusanyika vema tu.
Mawazo tu.
Ujinga ni pamoja na kuamini unachokijua tu!
Hoja iko hivi:
Mleta mada:
Kibati haina faida.
Wana Kibati:
Kibati inafaida, maana nanihii alijenga nyumba kutokana na kibati
Wana mada:
Hela alizojengea ni za kwake zilizokaa kwa mtu mda mredu bila kuzaa faida,
Wana kibati:
Inawezekana mnapinga kwa sababu mko chini ya umri wa kujua mambo.
Wana mada:
Hakuna umri wa kujua mambo ukampa mtu hela akuhifadhie miezi mitatu bila faida wakati ungezifanyia biashara zingekuwa za kwako na ungekuwa na faida iliyoongezeka.
Hapo mwenye point ni nani?
Hii kitu haina faida. Hela kuzimudu kwanza lazima uwe na nidhamu ya hela. Lazima ujue kuweka hela. Lazima ujue kutumia hela vizuri.
20 to 80 rule. Asilimia 20 ya matumizi yetu huchukua asilimia 80 ya ujira ama vipato vyetu.
Ukishajua ni wapi unatumia pesa nyingi ktk mahitaji yako, kinachofuata ni kuona ni kwa namna gani unaweza weka control ya matumizi yako ktk hiyo nyanja kuhakikisha unapunguza matumizi ili ukuze ziada utakayo wekeza ktk Biashara ambayo itarudisha Faida.
Hili ndio somo gumu tunalolikimbia kila siku kwa kuendekeza vikoba, saccos, na hata Mabank.
Na wajanja wachache kama Mabenki yanatumia ujinga wetu kutupiga hela.
Hivi hujiulizi kwanini ni lazima ukatwe pesa kuchangia mfuko wa hifadhi ya Jamii? Unaambiwa ni Akiba ya Uzeeni? Hivi unaamini ni kwasababu unapenda sana na Serikali ndio maana ni lazima uchangie?
Akiba ni ya Muhimu sana. Maana ndio pesa ya kuwekeza.
[HASHTAG]#Stuka[/HASHTAG]
〣( ºΔº )〣Good explanation..ingawa hata ww hujui jibu ni nini sababu hujawahi fanya ivyo..try upate jibu lililokua verified na research yako ww mwenyewe..watu wanazalisha biashara mpya kila siku sbb ya hii michezo..