Kibati hakilipi, mnajidanganya

Kibati hakilipi, mnajidanganya

Ukiwa huna nidhamu ya pesa kibati ndio mkombozi lakini kama unaweza kusema nitaweka kila siku shilingi elfu 5 na sita igusa kabisa mpaka baada ya miezi 3 huna sababu ya kucheza kibati, lakini kama ni kweli huwezi kuweka hela yako mwenyewe kwa uaminifu na kutimiza malengo nenda kwenye kibati, ila kiukweli kiabati kina leta faida na majanga, wengi wanatumia hela zilizopitia uchawi ili achukuaye asifanikiwe na ndio maana unakuta mtu anacheza kibati miaka 10 lakini hakuna la maana alilofanya imekuwa kama kawaida tu kucheza basi.
 
Aisee Elim ya Banking kwa mleta post inakupa shida saaana.
Kwani mtu anapoweka pesa kwenye Fixed Deposit Account inatofauti gani na upatu kwenye ku save
Tofauti ni moja tu kwamba ile Bank huku ni Watu.

Wanaume wa Dar mnashida saana,yaani inafikia wanawake wanaakili kuliko wanaume?au mpaka Upate uandikwe kwa Kiingereza ndio uone faida yake?

Kuna Kinamama wanamajumba kwa Upatu.
Mungu anisamehe,ila kama una Age above 25 yrs na upeo wako ni huo,basi utakuwa unaishi kwa kubahatisha maisha.

Wana majumba duh.
 
saving kwa hali ya kawaida kwa wengi ni ngumu, kibati kinalazimisha mtu afanye saving hata kama ni kwa kujinyima ambavyo huenda asingeweza katika hali ya kawaida
 
Kibati ni kizuri tu. Mfano wengi wanaocheza ni wale wenye kipato kidogo na wanaingiza kila siku. Mfano voda voda. Mama ntilie au kina mama wa nyumbani( wanabana ya matumizi). Sasa MTU kuweka 2000 . Kila siku kwa mda wa miezi 3 haiwezekani. Lazima ataitumia. Lalini kwa kutumia kibati anaweza kuhifadhi pesa zake. Hiyo pesa hapo kwa miezi miwili ni laki na ishirini. Hapo akiipata kwa maramoja inamsaidia kufanya shughuli zake. Mfano kuna wanaotumia kulipia kodi.
 
Mnachukua hela zenu mnapeana kwa zamu mi siamini kabisa katika uwekezaji au biashara ya namna hii wa hela wanaofanya watu wengi haswa wanawake (kibati) naona kama kujidanganya vilee.

Kwanini usikae na hiyo hela mwenyewe labda kama ni miezi 3 ukawa umeizalisha zaidi? Ukanunua hiki ukauza hata ukikopesha inalipa kuliko kibati.

Acheni kujidanganya hakuna faida kwenye kibati.
Kwa mtu anayejua kuwekeza na kuzalisha pesa hawezi fanya hii kazi , kwa nini ushindwe kujiamini mwenyewe na kwa nn uzike pesa
 
Ndo hao hao crowdrising sijui saiv naona wana sjui inaitwa ninyanyue sjui
 
Kwa mtu anayejua kuwekeza na kuzalisha pesa hawezi fanya hii kazi , kwa nini ushindwe kujiamini mwenyewe na kwa nn uzike pesa
Ni ajabu sana tena mtu anatete na kusema asiyeelewa na kuukubali mfumo wa kibati ni mwanaume wa dar,
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Mkuu Mimi sibaatishi maisha any way hapa siyo pa kushindana tuwaachie akina myweither na diamond
My concept ni
Una 200000
Kwa miezi 3 ni 600000
Kariakoo kuna vitu kibaoo vya 150000 ambavyo unaweza kopesha kwa 250000 kadri ya mahitaji ya wafanyakazi wenzio ndugu jamaa na marafiki hata wa mkoani kwamba mtalipana mwisho wa mwezi
Kwa miezi 3
Utakuwa na zaidi ya ml 1.
Saving saving saving wee endelea kung'ang'ania upata , huo hufanya na watu wasiopenda kujituma
Watu wavivu
Watu waoga
Watu wasiopenda kujaribu.
Watu wanaotumia 1% kuwaza
Kama unamwamini MTU unampa pesa kwanini usimtafute MTU, watu ukawamini ukawapa vitu kwa faida?
Very sorry
Hapa naona mnalumbana tu kwa hoja ambazo ni tofauti lengo la UPATU ni kuweka na kujilimbikizia pesa wakati wewe hapa unazungumzia biashara. Hayo ni malengo mawili tofauti;

Labda tu nijaribu kukuelimisha kidogo, kuna watu ambao hata 100k kuikusanya pamoja ni ndoto hata umpe mwaka mzima, sasa ili aweze kufanya biashara aliyoilenga au kununua kitu kikubwa alichokusudia ndiyo anaona ni vyema aanze kujilimbizia vijisenti kwa kupitia kwenye upatu. So usione watu wote wanao patua ukajua hawana uwezo wa kufikiria.
 
NI NJIA MOJAWAPO YA KUHIFADHI HELA ZAKO HASA UKIWA NA MALENGO KUWA NIKIPOKEA HELA HII NITAFANYA JAMBO FULANI NA NDIO LENGO LA MICHEZO HII YA KINAMAMA NA KINA BABA baadhi, WENGINE WANAJENGA KWA STYLE HII MIE MDOGOWANGU WA KIUME ALIKUWA ANACHEZA MCHEZO WA LAKI 3 KWA WIKI NA AMEJENGA NYUMBA KWA MAANA! ZILE HELA ALIKUWA AKIPOKEA NI ZA KWENYE UJENZI TU NA SASA YUPO NDANI YA NYUMBA YAKE...

HAKUNA TATIZO LOLOTE KWENYE MICHEZO HII UNLESS MMOJA WENU ASEPE NA MKWANJA...
Ujinga ni pamoja na kuamini unachokijua tu!
Hoja iko hivi:

Mleta mada:
Kibati haina faida.

Wana Kibati:
Kibati inafaida, maana nanihii alijenga nyumba kutokana na kibati

Wana mada:
Hela alizojengea ni za kwake zilizokaa kwa mtu mda mredu bila kuzaa faida,

Wana kibati:
Inawezekana mnapinga kwa sababu mko chini ya umri wa kujua mambo.

Wana mada:
Hakuna umri wa kujua mambo ukampa mtu hela akuhifadhie miezi mitatu bila faida wakati ungezifanyia biashara zingekuwa za kwako na ungekuwa na faida iliyoongezeka.

Hapo mwenye point ni nani?
 
Huu ni mchezo wa mtu wenye tamaa, mwenye matumizi yasiyo na mpangilio, ambae kila anachokiona anakitaka,
Kwa hiyo anaona ili kujisalimisha afanye hivyo badala ya kufungua accout!
 
Ujinga ni pamoja na kuamini unachokijua.
Hoja iko hivi:

Mleta mada:
Kibati haina faida.

Wana Kibati:
Kibati inafaida, maana nanihii alijenga nyumba kutokana na kibati

Wana mada:
Hela alizojengea ni za kwake zilizokaa kwa mtu mda mredu bila kuzaa faida,

Wana kibati:
Inawezekana mnapinga kwa sababu mko chini ya umri wa kujua mambo.

Wana mada:
Hakuna umri wa kujua mambo ukampa mtu hela akuhifadhie miezi mitatu bila faida wakati ungezifanyia biashara zingekuwa za kwako na ungekuwa na faida iliyoongezeka.

Hapo mwenye point ni nani?
Wwee pia ni mjinga kwasababu unaamini hiki ulichoandika unajuaje kama hii pesa mtu anamegua kwenye faida ya kile anachozungusha kwenye biashara yake?!?lengo lake likiwa ni kufanya jambo lake!...pia Si kila mtu anauwezo aa kuzalisha wengine ni wamama tu wa nymbani......
 
Kila mtu anaweza kuzakisha mkuu
Nakuhakikishia kila mtu anaweza na kwa Tanzania kuna fursa nyinngi mno
 
Kila mtu anaweza kuzakisha mkuu
Nakuhakikishia kila mtu anaweza na kwa Tanzania kuna fursa nyinngi mno
INategemea...

Mantik yangu ipo palepale..kuwa kuhifadi hizi hela si upuuxi hata kidogo lets say mtu anaendesha boda anaamua kila siku aweke elfumbili yaani badala ya kulewa viroba yeye anahifadhi kwa lengo lake fulani...
 
Wwee pia ni mjinga kwasababu unaamini hiki ulichoandika unajuaje kama hii pesa mtu anamegua kwenye faida ya kile anachozungusha kwenye biashara yake?!?lengo lake likiwa ni kufanya jambo lake!...pia Si kila mtu anauwezo aa kuzalisha wengine ni wamama tu wa nymbani......
Najua, ili uingie jamii forum hakuna shart la utimamu wa akili kwa hiyo, siwezi kukulaumu maana siyo kosa lako.

Kama ungekuwa na sifa ya kununua na kuuza kwa kutumia mtaji ulioutafuta mwenyewe ki halali, kwa jasho, kuanzia 0 mpaka popote ulipo ungenielewa, kifupi ni kwamba hujui lolote mimi nimepokea jina uliloniita la "mjinga" ila "HUJUI CHOCHOTE"
 
Kumruhusu mwanamke ajiunge kikoba ni sehemu ya kumpa uhuru wa kujiongoza na kujiamini.....acheni ujuaji.
 
Kibati inawasaidia sana kina mama hasa katika kujisogeza katika kununua asset zenye bei kubwa kwao au kusomesha watoto kidogo kidogo kupata hela ya mkupuo ya kulipa ada.
 
Mkuu Mimi sibaatishi maisha any way hapa siyo pa kushindana tuwaachie akina myweither na diamond
My concept ni
Una 200000
Kwa miezi 3 ni 600000
Kariakoo kuna vitu kibaoo vya 150000 ambavyo unaweza kopesha kwa 250000 kadri ya mahitaji ya wafanyakazi wenzio ndugu jamaa na marafiki hata wa mkoani kwamba mtalipana mwisho wa mwezi
Kwa miezi 3
Utakuwa na zaidi ya ml 1.
Saving saving saving wee endelea kung'ang'ania upata , huo hufanya na watu wasiopenda kujituma
Watu wavivu
Watu waoga
Watu wasiopenda kujaribu.
Watu wanaotumia 1% kuwaza
Kama unamwamini MTU unampa pesa kwanini usimtafute MTU, watu ukawamini ukawapa vitu kwa faida?
Very sorry
Mi bado sijaelewa tatizo lako ni lipi!! Hivi kama watu mpo 10, na kila mwezi mtu anatoa laki 2 huoni kama utapata 2m isiyo na riba na utarudisha kidogo kidogo? Mimi hapa nilipo nasubiri 1.5m mwezi huu mwishoni na sasa nshatoa laki 5..ila nikipata hiyo pesa yote naongeza mzigo kwenye biashara...hela ya hicho kibati yote inatoka kwenye biashara!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom