Kibati hakilipi, mnajidanganya

Kibati hakilipi, mnajidanganya

mbere

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
6,967
Reaction score
6,469
Mnachukua hela zenu mnapeana kwa zamu mi siamini kabisa katika uwekezaji au biashara ya namna hii wa hela wanaofanya watu wengi haswa wanawake (kibati) naona kama kujidanganya vilee.

Kwanini usikae na hiyo hela mwenyewe labda kama ni miezi 3 ukawa umeizalisha zaidi? Ukanunua hiki ukauza hata ukikopesha inalipa kuliko kibati.

Acheni kujidanganya hakuna faida kwenye kibati.
 
Kipi kinaanza, kati ya kuamini jambo kwanza kisha kuona matokeo au kinyume chake?
 
Mnachukua hela zenu mnapeana kwa zamu mi siamini kabisa katika uwekezaji au biashara ya namna hii wa hela wanaofanya watu wengi haswa wanawake (kibati) naona kama kujidanganya vilee.

Kwanini usikae na hiyo hela mwenyewe labda kama ni miezi 3 ukawa umeizalisha zaidi? Ukanunua hiki ukauza hata ukikopesha inalipa kuliko kibati.

Acheni kujidanganya hakuna faida kwenye kibati.
Hiyo tsh.2000 uikusanye mpaka ifike tsh.150000 na shida hii unaweza kweli ,sidhani .
Ila kwa mtindo wa kumchangia mmoja mmoja,inakusanyika vema tu.
Mawazo tu.
 
Mbona mimi naona kina faida kibao tu,chukulia mfano una shida ya haraka ya milion moja inakiwa rahisi sana kukopa vikoba kuliko kwa jirani.
Kikoba na kibati Ni vitu viwili
 
Kibati na kikoba ni tofaut[emoji4] [emoji4]
Kuna tofauti.
Nafikiri kikoba ni kama benki ndogo ndogo kwasababu wana sheria zao kama za benki wanazitumia kwa wakopaji pia nimeona huku kwetu kila mwanachama ana kitabu chake cha hisa....Sidhani kama hizo sheria watu wa kibati wanazo.
 
Kibati ni mtindo ambao unasaidia kufanya savings coz mm ni mmoja wapo wa wanufaika wa hiyo kibati
 
Aisee Elim ya Banking kwa mleta post inakupa shida saaana.
Kwani mtu anapoweka pesa kwenye Fixed Deposit Account inatofauti gani na upatu kwenye ku save
Tofauti ni moja tu kwamba ile Bank huku ni Watu.

Wanaume wa Dar mnashida saana,yaani inafikia wanawake wanaakili kuliko wanaume?au mpaka Upate uandikwe kwa Kiingereza ndio uone faida yake?

Kuna Kinamama wanamajumba kwa Upatu.
Mungu anisamehe,ila kama una Age above 25 yrs na upeo wako ni huo,basi utakuwa unaishi kwa kubahatisha maisha.
 
Kibati ni mtindo ambao unasaidia kufanya savings coz mm ni mmoja wapo wa wanufaika wa hiyo kibati
Ndo sababu watafiti wanasema watanzania tunatumia 1% kuwaza
Kwanini usimnunulie rafiki yako kitu anachohitaji au MTU unayemwamini ukamkopesha kwa mwezi, kila mwezi ukawa na 1?
Ungeweza
1. Kumkopesha hela
2. Nguo
3. T.v
4. Frij
5. Simu
6.shopping ya nguo
7. Saa Kali
8. Pikipiki
9. N.k kadri ya mazingira yako
Kwa faida?
Wee unampa mwenzi hela zako anakaa nazo miezi 3 tuuu unakuja rejeshewa bila faida!???!!!
This 1/2 of your brain work up
 
Aisee Elim ya Banking kwa mleta post inakupa shida saaana.
Kwani mtu anapoweka pesa kwenye Fixed Deposit Account inatofauti gani na upatu kwenye ku save
Tofauti ni moja tu kwamba ile Bank huku ni Watu.

Wanaume wa Dar mnashida saana,yaani inafikia wanawake wanaakili kuliko wanaume?au mpaka Upate uandikwe kwa Kiingereza ndio uone faida yake?

Kuna Kinamama wanamajumba kwa Upatu.
Mungu anisamehe,ila kama una Age above 25 yrs na upeo wako ni huo,basi utakuwa unaishi kwa kubahatisha maisha.
Mkuu Mimi sibaatishi maisha any way hapa siyo pa kushindana tuwaachie akina myweither na diamond
My concept ni
Una 200000
Kwa miezi 3 ni 600000
Kariakoo kuna vitu kibaoo vya 150000 ambavyo unaweza kopesha kwa 250000 kadri ya mahitaji ya wafanyakazi wenzio ndugu jamaa na marafiki hata wa mkoani kwamba mtalipana mwisho wa mwezi
Kwa miezi 3
Utakuwa na zaidi ya ml 1.
Saving saving saving wee endelea kung'ang'ania upata , huo hufanya na watu wasiopenda kujituma
Watu wavivu
Watu waoga
Watu wasiopenda kujaribu.
Watu wanaotumia 1% kuwaza
Kama unamwamini MTU unampa pesa kwanini usimtafute MTU, watu ukawamini ukawapa vitu kwa faida?
Very sorry
 
Unamaanisha "Upatu" mkuu?

Hii kitu nilishampga marufuku Wife kujihusisha nacho.

Mwisho wa siku ni kuzalisha madeni.
NI NJIA MOJAWAPO YA KUHIFADHI HELA ZAKO HASA UKIWA NA MALENGO KUWA NIKIPOKEA HELA HII NITAFANYA JAMBO FULANI NA NDIO LENGO LA MICHEZO HII YA KINAMAMA NA KINA BABA baadhi, WENGINE WANAJENGA KWA STYLE HII MIE MDOGOWANGU WA KIUME ALIKUWA ANACHEZA MCHEZO WA LAKI 3 KWA WIKI NA AMEJENGA NYUMBA KWA MAANA! ZILE HELA ALIKUWA AKIPOKEA NI ZA KWENYE UJENZI TU NA SASA YUPO NDANI YA NYUMBA YAKE...

HAKUNA TATIZO LOLOTE KWENYE MICHEZO HII UNLESS MMOJA WENU ASEPE NA MKWANJA...
 
Kuna mtu namfahamu alianzisha biashara kwa huu mchezo wa 'kupeana'.
Na sasa ni biashara kubwa sana.
 
Aisee Elim ya Banking kwa mleta post inakupa shida saaana.
Kwani mtu anapoweka pesa kwenye Fixed Deposit Account inatofauti gani na upatu kwenye ku save
Tofauti ni moja tu kwamba ile Bank huku ni Watu.

Wanaume wa Dar mnashida saana,yaani inafikia wanawake wanaakili kuliko wanaume?au mpaka Upate uandikwe kwa Kiingereza ndio uone faida yake?

Kuna Kinamama wanamajumba kwa Upatu.
Mungu anisamehe,ila kama una Age above 25 yrs na upeo wako ni huo,basi utakuwa unaishi kwa kubahatisha maisha.
Kweli kabisa mkuu hata maofisini watu huwa wanafanya sana hiyo kitu na wanafaidika. Mimi Binafsi nilifaidika sana kwa sababu ilikuwa kila terehe 15 na 30 anatoka mtu na imenisaidia kufanya mambo mengi tu ya msingi kwao hao wanao yapinga nadhani bado hawajatoka kwenye maisha ya wazazi wao. Hao traffic makao makuu pale Dar ndio zao kucheza huo upatu na mtu akipkea anapata mgao wa maana kabisa.
 
Aisee Elim ya Banking kwa mleta post inakupa shida saaana.
Kwani mtu anapoweka pesa kwenye Fixed Deposit Account inatofauti gani na upatu kwenye ku save
Tofauti ni moja tu kwamba ile Bank huku ni Watu.

Wanaume wa Dar mnashida saana,yaani inafikia wanawake wanaakili kuliko wanaume?au mpaka Upate uandikwe kwa Kiingereza ndio uone faida yake?

Kuna Kinamama wanamajumba kwa Upatu.
Mungu anisamehe,ila kama una Age above 25 yrs na upeo wako ni huo,basi utakuwa unaishi kwa kubahatisha maisha.
Upatu unasaidia sana kama kuna uaminifu kati yenu, mimi kuna dada yangu ameweza kumsomesha mtoto wake sekondary kwa ada ya milioni moja na zaidi kwa mwaka kwa kutumia upatu hadi mume wake amemshangaa.
 
Mkuu Mimi sibaatishi maisha any way hapa siyo pa kushindana tuwaachie akina myweither na diamond
My concept ni
Una 200000
Kwa miezi 3 ni 600000
Kariakoo kuna vitu kibaoo vya 150000 ambavyo unaweza kopesha kwa 250000 kadri ya mahitaji ya wafanyakazi wenzio ndugu jamaa na marafiki hata wa mkoani kwamba mtalipana mwisho wa mwezi
Kwa miezi 3
Utakuwa na zaidi ya ml 1.
Saving saving saving wee endelea kung'ang'ania upata , huo hufanya na watu wasiopenda kujituma
Watu wavivu
Watu waoga
Watu wasiopenda kujaribu.
Watu wanaotumia 1% kuwaza
Kama unamwamini MTU unampa pesa kwanini usimtafute MTU, watu ukawamini ukawapa vitu kwa faida?
Very sorry
Unazungumza kama sio mtanzania wa kawaida vile,inawezekana kuweka 200000/= ila kwa mazingira yetu kurupushi yanayotuzunguka watanzania wa kawaida.Kuweka 200000/=ndani na sawa na kuzuia uharo usitoke.Elewa hivyo,yaweza kawa siungi,ila nina mifano hai ya vijana waaminifu walioamua kufanya huo mchezo wa kibati na mpaka sasa navyokwambia wameweza kufanya mambo yanayoendana na ajira zao.Tatizo la huu mchezo mkipata mtu ambae si muaminifu,na wengi huwafanyi maamuzi ya kukurupuka wakitaka kutenda huo mchezo.Moja mcheze wenye uhakika wa kupata fedha kila muda ukifika,mbili msiwe wengi sana.Mkiwa watano na mnaojielewa,au hata watatu mnaojielewa.Huwa ni akiba nzuri kwa muda muafaka.Ni zaidi ya kukopa benk. fedha kibao halafu unakurupuka na wazo la biashara.Hufaa watu ambao wanataka kutimiza mambo ya kati kwa haraka sana,kama tu mna adabu nao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom