Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.

nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.

BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI

KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!

Umetumwa na CUF au CCM? Your too obvious....

Kama kilivyo CUF kuandamwa na udini wa kichinichini kuwa ni chama cha Kiislamu, ndivyo Waislamu wenye msimamo mkali wanakiona Chadema kama chama cha Kikristo, tangu kimeanzishwa, wenyeviti wake wote na makatibu wakuu ni Wakristo tuu, kuingia kwa Zitto kutaliondoa hili na kukifanya Chadema chama cha kitaifa zaidi tayari kuchukua nchi, 2015.

Hongera Zitto for just daring.

Sahihisho - Bob Nyange Mohamed Makani ni mwislamu ama uislamu ndio dini anayojitambulisha nayo. Halafu Walid Kabourou alishakuwa katibu mkuu na makamu mwenyekiti. Hili la udini ni propaganda za CCM halina pa kushikia, ushauri wa bure - achana nalo.
 
BY the way:
HOW OLD IS KIBANDA MAN???
Pse it is just a matter of purely curiousity
 
Mawazo haya mgando ni ya Kibanda mwenyewe,si ya CHADEMA, tafadhali tusiyafanye kuwa ndo msimamo wa chama. Katiba inamruhusu Zitto kugombea uenyekiti wa CHADEMA, kama anafaa au hafai wanachama wataamua, wala sio wewe Kibanda, mvivu wa kufikiria.

Kitu kimoja unachotakiwa tilia maanani ni kwamba kama ambavyo gazeti la Uhuru linawakilisha Chama cha Mapinduzi na ndivyo Tanzania Daima linakiwakilisha Chadema. Wanapoongelea gazeti la Tanzania Daima wananchi huwa hawasemi linalotolewa na Freemedia bali wanasema lile gazeti la Chadema. Hapo sasa nadhani unaweza ukakaa na kupembua ufahamu mawazo mgando ya Kibanda yana athari gani ndani na nje ya Chadema.
 
Kabwe Zitto ni msaliti wa Upinzani?
na dk. gideon shoo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilifanya kikao cha Kamati Kuu (CC) mwishoni mwa wiki iliyopita, na ajenda kuu ilikuwa ni kumruhusu au kutomruhusu Zitto Kabwe kushiriki katika Kamati ya Madini iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete.

Uamuzi wa kulifanyia kikao suala hilo la uteuzi wa Zitto kuingia kwenye Kamati ulitokana na hali ya mvutano iliyojitokeza ndani ya chama hicho hususan miongoni mwa viongozi.

Viongozi wa CHADEMA waligawanyika katika suala la Zitto. Mgawanyiko huo ulisababisha kurushiana vijembe na tuhuma zisizokuwa za moja kwa moja, lakini zililenga katika kufanya uteuzi wa Zitto uonekane kuwa na hitilafu ulizua mjadala ambao hatima yake ndiyo kikao hicho cha Kamati Kuu.

Ingawa si rahisi kusema kwamba Zitto aliteuliwa kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini na / au Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, kwa hakika aliyekuwa amelengwa zaidi katika mvutano huo ni Zitto mwenyewe ambaye upande uliopinga kuingizwa kwake katika kamati hiyo ulijitahidi kujenga taswira isiyopendeza ya mwanasiasa huyo.

Zitto, ametuhumiwa kinamna kwamba amerubuniwa, kuhongwa na hata kulainishwa ili ‘awasaliti' wanachama wenzake wa CHADEMA.

Uteuzi wa Zitto ulifanywa na Rais Kikwete na ingawa hakutaja sababu ya kumwingiza katika Kamati hiyo lakini ni wazi kwamba kutokana na mchango wake katika mjadala wa mikataba ya uchimbaji wa madini na hasa suala la Mkataba wa Mradi wa Buzwagi ilikuwa si rahisi kutokumwingiza humo.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA, hata wale ambao walisikika hadharani wakikubaliana na uteuzi wa Zitto, walijitokeza hadharani na kupinga uteuzi huo tena kwa kelele nyingi.

Viongozi hao hata hivyo walikuwa wakimsukuma Zitto ajing'atue kutoka katika Kamati hiyo ili kumpisha mtu ambaye baadhi yao walimwona kwamba ndiye anayefaa zaidi. Hata hivyo, vigezo vilivyotumiwa kuonesha kwamba huyo ‘aliyetakiwa' kuingia katika Kamati hiyo bado ni kitendawili.

Aidha, kumekuwapo malalamiko kwamba eti hadidu za rejea zilizopewa kamati hiyo na Rais Kikwete zilikuwa hazitoshelezi.

Malalamiko mengine ni kwamba baadhi ya walioteuliwa walikuwa ‘si wasafi' kwa vigezo visivyo vya kuthibitika kisheria bali kwa hisia na dhania.

‘Uchafu' wa baadhi ya wateule wa Rais Kikwete kuingia katika Kamati hiyo ni kuhusishwa kwao katika mikataba iliyokwisha kutiwa saini miaka ya nyuma. Mikataba ambayo inadaiwa kwamba ni mibovu na inayoliumiza Taifa letu.

Turudi katika hili la Zitto na nafasi yake katika Kamati ya Madini ya Rais Kikwete. Baada ya mjadala mkali na wakati mwingine uliojaa jazba kilichojitokeza wazi wazi ni kwamba baadhi ya viongozi wa CHADEMA wameonesha wazi kutoridhishwa kwao na uteuzi wa kijana huyo na wamekosa imani naye kama mwakilishi wa umma.

Hata baada ya kuwa kikao cha Kamati Kuu kilimazilika na kuonekana kwamba kuna aina fulani ya muafaka iliyokuwa imefikiwa bado ngurumo za chini ya ardhi ziliashiria kwamba hali si shwari.

Katika jitihada za kutuliza mzuka ambao ulikuwa umewapanda viongozi wa chama hicho kumekuwapo na jitihada za haraka za kumtafuta mchawi.

Pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutangaza kwamba kimekubali na kuridhia Zitto kuingia katika Kamati hiyo ya madini lakini kwa namna tangazo la kuridhia huko lilivyotolewa ni wazi kwamba hilo limefanyika shingo upande.

Mbowe anazungumzia chama hicho kumruhusu Zitto kushiriki katika Kamati hiyo kama vile kijana huyo ameteuliwa kama mwakilishi wa chama hicho kwenye kamati hiyo.

Siamini kwamba uteuzi wa kuingia katika kamati hiyo umefanyika kwa misingi ya vyama kwa sababu kama ndivyo basi tungelikuwa na sura takriban kumi na ushei.

Awali nilisema kwamba sijui vigezo alivyovitumia Rais Kikwete kufanya uteuzi lakini naamini kwamba kwa kumwingiza Zitto moja ya sababu za msingi sana ni mchango wake katika mjadala huu muhimu wa nafasi ya Taifa letu katika sekta ya madini.

Lakini pamoja na Mbowe kuafiki kijana huyo kushiriki katika Kamati hiyo, (na siamini kwamba anao ubavu wa kumzuia) jambo jingine lililojitokeza ni mlolongo wa masharti ambayo mwanasiasa huyo anayatoa kuzuia chama chake kutoikataa moja kwa moja matokeo ya kazi ya Kamati hiyo.

Kitendo cha Mbowe kutaka wananchi waamini kwamba Kamati hiyo haiwezi kutoa ripoti yoyote ile ya maana kama masharti ya chama chake hayatatimizwa ni cha kuupotosha umma.

Masharti ya Mbowe ni pamoja na kuwekwa hadharani kwa ripoti za Tume na Kamati zilizotangulia, suala la uharibifu wa mazingira, haki za binadamu katika maeneo ya machimbo, kutenguliwa kwa wajumbe 'wachafu' n.k.

Orodha hiyo ndefu ya masharti ya kiongozi huyo wa CHADEMA yameelekezwa kwa Rais Kikwete.

Tatizo hapa si masharti kwa Rais Kikwete. Pengine hayo masharti yangeweza kupuuzwa tu. Lakini ukweli ni kwamba Mbowe anahusisha masharti hayo na kazi ya Kamati. Yaani Rais Kikwete asipotimiza masharti yote nane aliyoyatangaza Mbowe kwa waandishi wa habari basi hiyo Kamati haina sababu yoyote ile ya kukutana kwani haiwezi kutoa matunda yoyote yale ya maana.

Mbowe anataka watu waamini kwamba Kamati iliyoundwa na Rais Kikwete ni ya kupoteza wakati tu na kwamba ili isiwe hivyo, masharti aliyoyataja yatimizwe.

Lakini katika kuthibitisha kwamba CHADEMA ilikuwa inajiandaa kuchomeka sana katika spoku gazeti la Tanzania Daima toleo la Jumapili Novemba 25 liliandaa njia kwa ajili ya Mbowe kupita.

Tanzania Daima Jumapili lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na wasomaji wake kujua nini maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu. Gazeti hilo lilitoka na habari kubwa ukurasa wa kwanza; ‘Zitto aruka kihunzi.' Habari hiyo ilikuwa ikielezea kwa kina kwamba kikao kilikuwa kimeridhia Zitto kuendelea na uteuzi katika Kamati ya Madini.

Sanjari na habari hiyo hata hivyo, kulikuwa na habari nyingine iliyokuwa na uzito karibu uliolingana na hiyo hapo juu. Habari hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho ‘CCM, JK waitega CHADEMA kinamna.'

Wakati habari ya kwanza inazungumzia Kamati Kuu ya CHADEMA kuhitimisha ‘mvutano wa viongozi wa chama hicho uliodumu kwa siku kadhaa kuhusu ushiriki wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto, katika kamati ya kupitia upya mikataba ya madini iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, habari hiyo nyingine ilikuwa ikisema: ‘Sasa ni dhahiri kwamba jitihada za vyama vya upinzani kukipoka madaraka Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 au hata 2015 zipo kitanzini.

Ni wazi kwamba habari hiyo ya kuonyesha kwamba kuna njama dhidi ya upinzani na hasa dhidi ya viongozi wanaoinukia wa CHADEMA inalenga katika kuhalalisha mgogoro ulioanzishwa na viongozi wenyewe wa chama hicho.

Katika migogoro ya kisiasa jambo moja huweza kufanyika, nalo ni kuibua mgogoro mpya wa nje kama njia ya kufunika mgogoro wa ndani.

Hatari ya kutumia mbinu hiyo ni kwamba katika kuhalalisha kuwapo mgogoro kutoka nje, unaweza kujikuta ukiibua mgogoro mzito ndani ya chama husika.

Habari hiyo ni dhahiri kwamba inatoa tuhuma nyingi, si kwa chama tawala tu bali kwa viongozi ndani ya CHADEMA.

Lililo baya zaidi ni kwamba habari kuhusu kile kinachoitwa mtego walioingia CHADEMA inazungumzia kwamba Zitto amerubuniwa na Serikali, na hiyo imefanyika kutokana na ushauri wa magwiji wa fitina za kisiasa ndani ya CCM walioshauri "kumsogeza karibu zaidi na Serikali, Zitto, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi kwa kumpangia majukumu mengi mazito ya kitaifa, lakini yenye maslahi bora kwake binafsi."

Maneno yaliyonukuliwa hapo juu ni yaliyochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima.

Tuhuma zinazorushwa kwa Zitto na gazeti hilo ni nzito. Kwamba sasa ‘Zitto ambaye nyota yake inang'aa, ndiye anayelengwa kwa nia ya kumfanya silaha muhimu ya kuisambaratisha CHADEMA…si suala la mjadala wa siri.'

Kwamba kwa Zitto kushirikishwa katika shughuli kama vile Kamati ya Madini ni kumtumia ili kuisambaratisha CHADEMA, pengine hili linahitaji ufafanuzi wa kina kutoka kwa wanaozirusha tuhuma hizo.

Kinachotokea hivi sasa ni kwamba Zitto anatupiwa lawama nzito na viongozi wanaotanguliza maslahi binafsi mbele katika chama chakeKwa nini leo hii kuteuliwa kwa Zitto kuchukuliwe kwamba ni kurubuniwa na kuteuliwa kwa mtu mwingine iwe ni sawa na halali na busara isiyomithilika? Kuna jambo limejificha hapa ambalo halizungumzwi.

Si tu kwamba katika habari hiyo ya gazeti Zitto alifanywa kuonekana kama msambaratishaji wa CHADEMA ambaye anatumiwa na CCM, bali pia ilijengeka taswira nyingine kwamba kijana mwingine wa chama hicho naye amepangwa ‘kushughulikiwa kwa staili ya Zitto'. Kijana huyo ni Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, John Mnyika.

Kwa kujaribu kueneza habari za kuonyesha kwamba CCM inalenga kuwarubuni vijana hao ni kuwajengea woga ili washindwe kujipembua kitaifa, kwani pamoja na kujitokeza na kuonyesha vipaji vyao katika majukwaa ya siasa, ni wazi kwamba kwa kushiriki katika shughuli za kitaifa kama vile tume na kamati teule za Rais vijana kama hao watapaa maradufu katika ulingo wa siasa. Jambo hilo bila shaka linawatisha baadhi ya viongozi katika chama hicho.

Ni wazi kabisa kwamba hicho kinachoitwa njama za CCM ni jitihada za baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA kutaka kuzuia kuibuka kisiasa kwa baadhi ya vijana ambao wana uwezo wa kujieleza, uwezo wa kuchambua mambo kwa uyakinifu na hivyo kuwa na mvuto kwa wanachama wa chama hicho na wananchi wengine sawia.

Ni wazi kwamba kama ndani ya CHADEMA hakutatokea watu walio jasiri na kumulika kwa undani mwenendo mzima wa baadhi ya viongozi, basi hakuna uwezekano wa kukipoka Chama Cha Mapinduzi madaraka, si kwa sababu ya ghiliba na ujanja ujanja wa chama hicho, bali kutokana na kupoteza muda katika masuala yasiyokuwa na maana. Kutangaza kwamba CCM inatumia ghiliba na mbinu kuwarubuni vijana ndani ya CHADEMA ni kuanzisha mgogoro ndani ya chama. Huo ni mgogoro ambao unalenga ama katika kuwaengua vijana hao kutoka katika safu za uongozi wa chama hicho au unaolenga kuhalalisha kushindwa kwa uongozi wa chama kuwa na mikakati endelevu ya kupambana na CCM.

Unawezaje usiwe na mgogoro wa uongozi ndani ya chama kama wale wanaoibuka na kuanza kujipembua kutokana na umahiri wao katika siasa na hususan katika kujieleza kwa umma wanaonekana kwamba ni watu wa kurubuniwa?

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili kuhusu njama za CCM za kuwarubuni vijana wa CHADEMA unahitaji kuanikwa kwa kina zaidi. Kama ni kweli, CCM imemrubuni Zitto na ameingia kwenye mtego wao basi ijulikane hivyo lakini kama si kweli basi aombwe msamaha. Au ni dhambi kuwa kijana mwanachama wa CHADEMA na halafu ukajipembua kama muweza wa masuala ya kisiasa? Kama ni hivyo, basi na ijulikane hadharani.

Kuna dhana inayojengwa na Mbowe na wenzake kwamba kuna wapinzani wa kweli na wapinzani feki. Wapinzani wa kweli ni wale wanaokubaliana na Mbowe na fikra zake na walio feki ni wale ambao wana fikra tofauti. Aidha, hata uzalendo nao unazungumzwa katika kutaka kuonyesha kwamba kuna watu wanaipenda Tanzania zaidi ya wengine.

Source: Rai 29 Nov 2007
 
Achana na udini wewe Nyumbu na wewe umekuwa mvivu kufikiri.
Kama waislamu mbona Kikwete ni muislamu na Mwinyi nae alikuwa muislamu, lakini kaa chini utafakari uongozi wa waislamu na uongozi wa kikristu, mimi siyo mdini ila wewe Nyumbu ukitaka udini hapa patakuwa hapatoshi..

Angalia utendaji wa kazi na siyo dini au kabila sawa.

Mahongo.
 
Kwanza nikiri kukosa maneno ya kusema wazi wazi kwa kuwa sijawasiliana na Zitto. Nitakuwa na nafasi ya kuzungumza kwa uzito unaostahili maana ni mambo mazito sana kwangu binafsi na kwa mustakabali wa Taifa.

Jambo ambalo naona ni vyema kwa sasa nikalitolea ufafanuzi ni kauli za baadhi ya watu kumbeza/kumshambulia Kibanda kwa makala yake ya uchambuzi.

-Kwanza kabisa hayo ni maoni yake na mwingine ana nafasi ya kuandika maoni yake hata kama hana gazeti JF ni bureee, aandike.

-Lakini pili, siamini kabisa na sikubaliani kwamba mawazo ya Kibanda yamesukumwa ama anajipendekeza kwa Mbowe. Nina sababu nyingi lakini moja kubwa ni kwamba Kibanda amekuwa karibu na Zitto kuliko wengi wetu ambao tumekuwa karibu naye. Pia Kibanda amekuwa akiandika mambo mengi ambayo mara kadhaa yamepingana na msimamo wa Mbowe moja kwa moja, tena mengine mambo muhimu yenye athari kwa Mbowe.
-Jambo la tatu ambalo ni vyema tujiridhishe nalo ni staili ambayo Zitto ameitumia. Kuna maswali mengi ambayo pengine yakijibiwa, tunaweza ama kumpinga Kibanda ama kumuunga mkono kwa kuandika maandiko yetu yenye msimamo tofauti na pengine kabla hatujaandika, yeye mwenyewe Kibanda ataandika kujisahihisha na kuomba radhi.

Maswali ambayo yanahitaji majibu ni pamoja na kwanini Zitto amechukua uamuzi huo kwa staili ya aina yake, yaani KIMYA KIMYA bila kujitokeza mwenyewe katika ofisi za chama chake?. Je, ni kweli kwamba Zitto anafanya hivyo kutoa changamoto la kisiasa kwa chama chake kuwa mfano wa kidemokrasia? Je, ni kweli kwamba anafanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na uongozi wa Mbowe? Je, anataka kukivuruga chama ambacho yeye binafsi na watu walio karibu naye wanakiamini kuwa ni chama mbadala? Je, anatumiwa na watu wenye nia mbaya na Chadema? Je, amekasirishwa na jambo/mambo ambayo hana njia ya kuyasahihisha isipokuwa kumkabili Mbowe kwa kuwania uenyekiti? Je, ni kweli kwamba kwa muda wa miezi mitatu sasa hajakutana na Mbowe? Je, amemua kugombea baada ya Mbowe kusema hatogombea? Je, amelazimishwa na viongozi/wanachama wenzake wa Chadema? Je, kuna mkono wa CCM/dola?

Baada ya kujibiwa maswali hayo na zaidi yanaweza kujibiwa na Zitto mwenyewe, ndipo tunaweza kuwa na JUKUMU ZITO la kukabiliana na jambo lililo mbele yetu, lakini kwa sasa naamini ni mapema mno kutoa hukumu, maana inaweza kutokea Chadema ikawa imara kuliko ilivyo leo na jana.

Mwisho napenda kutoa angalizo kwa CCM na Dola kwamba, kukosekana kwa sauti mbadala ya UMMA kunaweza kuwa HATARI KWA USALAMA WA TAIFA kuliko jambo lolote lile na kwamba wananchi wakikata tamaa, nchi HAITATAWALIKA.
 
Last edited:
Kitu kimoja unachotakiwa tilia maanani ni kwamba kama ambavyo gazeti la Uhuru linawakilisha Chama cha Mapinduzi na ndivyo Tanzania Daima linakiwakilisha Chadema. Wanapoongelea gazeti la Tanzania Daima wananchi huwa hawasemi linalotolewa na Freemedia bali wanasema lile gazeti la Chadema. Hapo sasa nadhani unaweza ukakaa na kupembua ufahamu mawazo mgando ya Kibanda yana athari gani ndani na nje ya Chadema.

Sajo,

Tanzania Daima ni mali binafsi ya Freeman Mbowe!
 
Nafirikiri wanachama wa chadema wanatikiwa kuwa makini sana kwenye uchaguzi huu, kwa sababu ni uchaguzi muhimu sana kuelekea 2010 General Election.......!

Viongozi watakaochaguliwa hapo watatupa dira sahihi ya nini tutegemee from Chadema come 2010, ikizingatiwa (na to be honest), Chadema kwa sasa ndio tegemeo pekee ya ukombozi wa kweli kwa wanyonge Tanzania!

Kila la kheri Chadema, na msituangushe huko!
Nawatakieni Kila la Kheri katika uchaguzi huo na pia Tunaomba Mungu kwa ajili ya yote
 
Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.

nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.

BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI

KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!

Kuna wakati inabidi zianzishwe thread za kuwapsha watu!, ikiwezekana hata kutumia lugha za Mgando

wewe! mimi mama yangu mwislamu na na baba yangu mkristo unaniweka wapi?

hakuna nafasi ya dini Tanzania, wakikusikia wenyewe wanashangaa!

Personally ni MLOKOLE NA ZITTO has been my friend since then!

acha ujinga!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
nyie semeni tu ndio aina ya uandishi.

Nilivyoiangalia kwa haraka haraka inaonekana mwandishi anasema Zitto katumwa na ccm ni mbinu ile ile iliyotumika kummaliza maremu Chacha.

Huyu mbowe ni hatari kweli kweli kwa mstakbali wa chama chenu.
 
Ado, Karibu sana... Hata mie nilikuja na vijungu vyangu na vitetesi kibao!!! Badae nikagundua hapa ni great thinkers, kama una uhakika toa ushahidi, la sivyo... Kakojoe ulale

Ha ha haaaaaa! MTM umeniacha HOI mbavu sina, Taabani bin Mahtuti
 
Kwanza nikiri kukosa maneno ya kusema wazi wazi kwa kuwa sijawasiliana na Zitto. Nitakuwa na nafasi ya kuzungumza kwa uzito unaostahili maana ni mambo mazito sana kwangu binafsi na kwa mustakabali wa Taifa.

Jambo ambalo naona ni vyema kwa sasa nikalitolea ufafanuzi ni kauli za baadhi ya watu kumbeza/kumshambulia Kibanda kwa makala yake ya uchambuzi.

-Kwanza kabisa hayo ni maoni yake na mwingine ana nafasi ya kuandika maoni yake hata kama hana gazeti JF ni bureee, aandike.

-Lakini pili, siamini kabisa na sikubaliani kwamba mawazo ya Kibanda yamesukumwa ama anajipendekeza kwa Mbowe. Nina sababu nyingi lakini moja kubwa ni kwamba Kibanda amekuwa karibu na Zitto kuliko wengi wetu ambao tumekuwa karibu naye. Pia Kibanda amekuwa akiandika mambo mengi ambayo mara kadhaa yamepingana na msimamo wa Mbowe moja kwa moja, tena mengine mambo muhimu yenye athari kwa Mbowe.
-Jambo la tatu ambalo ni vyema tujiridhishe nalo ni staili ambayo Zitto ameitumia. Kuna maswali mengi ambayo pengine yakijibiwa, tunaweza ama kumpinga Kibanda ama kumuunga mkono kwa kuandika maandiko yetu yenye msimamo tofauti na pengine kabla hatujaandika, yeye mwenyewe Kibanda ataandika kujisahihisha na kuomba radhi.

Maswali ambayo yanahitaji majibu ni pamoja na kwanini Zitto amechukua uamuzi huo kwa staili ya aina yake, yaani KIMYA KIMYA bila kujitokeza mwenyewe katika ofisi za chama chake?. Je, ni kweli kwamba Zitto anafanya hivyo kutoa changamoto la kisiasa kwa chama chake kuwa mfano wa kidemokrasia? Je, ni kweli kwamba anafanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na uongozi wa Mbowe? Je, anataka kukivuruga chama ambacho yeye binafsi na watu walio karibu naye wanakiamini kuwa ni chama mbadala? Je, anatumiwa na watu wenye nia mbaya na Chadema? Je, amekasirishwa na jambo/mambo ambayo hana njia ya kuyasahihisha isipokuwa kumkabili Mbowe kwa kuwania uenyekiti? Je, ni kweli kwamba kwa muda wa miezi mitatu sasa hajakutana na Mbowe? Je, amemua kugombea baada ya Mbowe kusema hatogombea? Je, amelazimishwa na viongozi/wanachama wenzake wa Chadema? Je, kuna mkono wa CCM/dola?

Baada ya kujibiwa maswali hayo na zaidi yanaweza kujibiwa na Zitto mwenyewe, ndipo tunaweza kuwa na JUKUMU ZITO la kukabiliana na jambo lililo mbele yetu, lakini kwa sasa naamini ni mapema mno kutoa hukumu, maana inaweza kutokea Chadema ikawa imara kuliko ilivyo leo na jana.

Mwisho napenda kutoa angalizo kwa CCM na Dola kwamba, kukosekana kwa sauti mbadala ya UMMA kunaweza kuwa HATARI KWA USALAMA WA TAIFA kuliko jambo lolote lile na kwamba wananchi wakikata tamaa, nchi HAITATAWALIKA.

Kwanza si kweli kuwa Kibanda yuko karibu na Zitto, kama wangekuwa karibu je hawezi kumshauri mpaka aandike gazetini? mkeo unamuonya kwa balozi?

Kibanda ameshindwa kutumia njia mbadala ya amani, maana hii inawagawa Chadema hana busara hizo?

Je kwani mwakani ni lazima Chadema imsimamishe mgombea wa urais?

Kama Zitto akiwa mwenyekiti hatuoni kuwa kuna nafasi kubwa ya kuwa na mapinduzi kama yale ya Mrema 1995???????

wao Zitto na Mbowe wanasemaje???
 
Kuna wakati inabidi zianzishwe thread za kuwapsha watu!, ikiwezekana hata kutumia lugha za Mgando

wewe! mimi mama yangu mwislamu na na baba yangu mkristo unaniweka wapi?

hakuna nafasi ya dini Tanzania, wakikusikia wenyewe wanashangaa!

Personally ni MLOKOLE NA ZITTO has been my friend since then!

acha ujinga!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

huyo jamaa anaweweseka sana
mimi mkatoliki lakini sikiungi mkono chadema harafu kuna watu wanafikiri ukristu ni ukatolic.

Na hata hivyo hizo ndo siasa za mbowe za kukandya kuwasingizia wenzake wametumwa,kawanywesha sumu hiyo watu wengi sana hata hapa jf ukipingana nao basi umetumwa na mafisadi.
 
Kama msoma nyakati na mwanasiasa mkereketwa, jicho langu linaona mbali....

Ni wazi kijana mwenzamgu wa jinsia ya Kiume kwa jina la Zitto Zuberi Kabwe hana lengo la kurudi tena mjengoni.....

He is now an Icon tinapozungumzia siasa za Tanzania,
Ni mpiganaji thoough alitaka kuelekea kuyumba hapo kati,
Ana populality ya hali ya juu hasa miongoni mwa vijana,

Naamini atakapo zunguka 'njhi' hii kutema sumu za kuwania 'hiyo kitu' obvuz chama KIKUBWA kitakuwa kikaangoni na kwenye 'mtihani'

Ni wazi majimbo lukuki yanategemea kutekwa na upinzani, ili kufanikisha hili, hakuna budi kupata mtu mwenye mvuto wa mwatu na easily recognised ktk harakat za Ukombozi.
Wananchi kwa sasa wanapozungumzia Mbowe, picha ni HELCOPTA na KOMBAT.

Hivyo basi, Mh. Mwenyekiti, tungeomba alitambue hilo na AMLINDE kijana.

Tunamuhitaji mkt. Mjengoni, akifuatana na Myika, Mwita Mwikwabi, Rwakatale na wengineo.

Mungu Ibariki Tanzania.

Aguigo.
 
Naomba kuuuliza , kuogombea uraisi uwe juu ya miaka 40 ni katiba ya taifa ama ni katiba ya ccm.?
 
Kumbe Zitto amejibu humu usiku wa manane kuamkia leo. Pengine angekuwa wazi zaidi kujibu maswali yetu!!!!

Democracy at work in CHADEMA............. chama hakitavunjika, kitamaliza uchaguzi kikiwa imara kabisa. tukumbatie demokrasia na tusiihofu.

...................................
 
Nadhani magazeti ya kesho ndiyo yatakuwa na mambo mengi zaidi kwa jinsi ninavyoamini.
 
Naomba kuuuliza , kuogombea uraisi uwe juu ya miaka 40 ni katiba ya taifa ama ni katiba ya ccm.?

katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ngoja nitafute kifungu

39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwamujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini
;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa nachama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbewa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe yaUchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katikaMahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipakodi yoyote ya Serikali.
 
Kibanda huwa nakuheshimu sana na mimi ni msomaji mzuri sana wa Makala zako lakini kwa hili ndugu yangu umechemsha sana, sijui motive ya hii makala yako ila kama lengo lilikuwa ni kumfurahisha Mbowe, ninavyomjua Mbowe utakuwa umemuudhi sana.

1: Kwanza unamfanya Mbowe aonekane kama anamuogopa Zitto, kitu ambacho naamisi si kweli.

2: May be unataka kuwagombanisha Mbowe na Zitto kwa sababu as Mwajiriwa wa Freemedia ukaandika habari za Zitto na Mbowe in such a biased manner hii inaweza kumfanya Zitto afikiri kwamba umeagizwa au umetumwa na Mbowe.

3: Kama namba mbili ni ya kweli basi utakuwa umetumwa na mtu ambaye si Mbowe wala yeyote mwenye kuitakia mema CHADEMA, acha Democracy ichukue mkondo wake coz nahofia kesho Magazeti mengine yanaweza kutoka na habari kwamba Mbowe atumia vyombo vyake kupambana na Zitto huoni kama utakuwa unakiongezea Chama Mzigo mzito wa maswali ya kuyajibu?

Kama nilivyoandika mwanzoni, Kibanda haitakii mema Chadema katika kipindi hiki muhim, nakubaliana na point zako kuwa inawezekana kibanda akafikiri Boss wake Mbowe atafurahia makala hii, ukweli ni kwamba Mbowe hawezi furahia makala hii kwa kuwa inabomoa badala ya kujenga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom