Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Chadema ni Chama cha demokrasia.

Kama ni hivyo basi ONYESHENI kuwa kuna hiyo DEMOCRACY!. Wapigeni fullu stopu hawa waandishi uchwara ambao wanawaharibia chama.
 
Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.

nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.

BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI

KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!
 
Watanzania tunajifanya tunataka demokrasia lakini tukiambiwa tuitekeleze kwa vitendo tunarudi kule kule kwenye status quo. Mara huyo mdogo, huyu anatumiwa nk.

Wagombea wengi tena wenye sifa kujitokeza kugombea CHADEMA ni jambo jema kwenye chama lakini pia ni kipimo cha kuwaangalia kama CHADEMA kama chama wamekomaa au la. Chama ambacho hakiwezi kukabiliana na challenges za wanachama wake au viongozi wake kutofautiana hakiwezi kuwa chama cha kidemikrasia.

Ni muhimu CHADEMA kumaliza huu uchaguzi bila kutoana ngeu maana hasira za kushindwa zinaisha haraka lakini majeraha yatokanayo na matusi na ugomvi kwenye uchaguzi hudumu milele.

Binafsi nimeanza kununua popcorns zangu maana huu mpambano inaelekea utakuwa wa patashika nguo chanika.

Nawatakia heri wote wanaogombea.

Mkuu Kitila, chukua form mkuu, hata kama ni unaibu. Tunahitaji watu ambao wanajua nini maana ya mabadiliko kuingia kwenye hivi vyama na kusaidia kuleta mabadiliko ya kweli.
 
Kibanda, heshima mbele!

Kwanza siamini kuwa Kibanda amenunuliwa na Mbowe bali one thing for sure, Kibanda anajikomba kwa Mbowe, what for ndio sijui ni kutetea kibarua chake, ama kujikomba komba tuu ili mradi kujikomba.

Namuheshimu sana tuu Kibanda kama mwandishi, mhariri na mchambuzi, na Tanzania Daima la Jumatato, ni miongoni mwa magazeti ambayo sio tuu can't afford to miss, bali pia ends up in my achive, hivyo halifungii samaki.ila kwa makala hii, Kibanda amechemsha big time.Hoja ya umri haina mashiko, hapa tunaangalia uwezo wa uongozi kati yao. Kibanda angepaswa kuogopa kama Zitto hana uwezo alionao Mbowe na sio umri.

Kitendo cha Zitto kuwania kugombea uenyekiti wa Chadema, ni kitendo cha kuungwa mkono na waona mbali wengi na kitalaaniwa na myopic wote wenye myopia ambapo Kibanda nae sasa anaingia kwenye kundi hili.Japo mimi sio mwanachama wa chama chochote, ila ni mshabiki wa demokrasia ya kweli, nawaambieni kuingia kwa Zitto kwenye kinyanganyiro hicho ni uthibitisho wa demokrasia ya kweli ndani ya Chadema.

Chadema kama chama cha upinzani kinakubalika sana bara, lakini pia kinashutuma za chini kwa chini za ukabila, Mbowe amepewa chama na Bamkwe, ili kuliondoa hilo, chama kishikwe na mtu baki asiyetokana na Uchagga au uKaskazini ili kuwathibitishia Watanzania kuwa Chadema hakina ukabila.

Kama kilivyo CUF kuandamwa na udini wa kichinichini kuwa ni chama cha Kiislamu, ndivyo Waislamu wenye msimamo mkali wanakiona Chadema kama chama cha Kikristo, tangu kimeanzishwa, wenyeviti wake wote na makatibu wakuu ni Wakristo tuu, kuingia kwa Zitto kutaliondoa hili na kukifanya Chadema chama cha kitaifa zaidi tayari kuchukua nchi, 2015.

Zitto ni reformist na strategist leader, Mbowe ni kiongozi mzuri ila kwa vile politics zake ni spoon fed na bamkwe, hapo alipokifikisha Chadema ndio mwisho wa uwezo wa Freeman kama Lipumba alivyogota na CUF bara. Kuendelea na uenyekiti ni kuididimiza Chadema. Zitto ni damu mpya, damu changa inayoweza kuibua tumaini jipya kwa Chadema, kitendo cha kuamua kugombea uenyekiti, lazima kuna mambo ameyaona ambayo Mbowe hayawezi hivyo anataka kushika usukani aokoe jahazi.

Hongera Zitto for just daring.
 
Last edited by a moderator:
Wasi wasi wangu ni pale wakati wa kampeni na uchaguzi maana ikitokea mtu akapiga kampeni za kudhalilisha wakati chama chenyewe ni chakujitolea zaidi mwingine atakuwa na kijeba roho na pia wanachama ndo wengi na you can not afford to get what they believe and act.

Maoni yangu: Mbowe na Zitto wameifanyia mengi CHADEMA. Pigen kampeni za the way forward not nani alichangia kuwepo hapa. Pia makundi yafanyiwe hii induction then after election you will have to come back to UCHADEMASIM.

Thanks
 
Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.

nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.

BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI

KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!

Hayo ndo tunaita mawazo MGANDO. Mimi ni a proud Christian tena mkatoliki mbona ninamuunga mkono Zitto?, soma michango yangu hapo juu.

Ukiwa na dhana kuwa waislamu wanaonewa utaendelea kulalamika MILELE. ACHANA NA MAWAZO DHAIFU ndugu yangu. Kuonewa mtaonewaje wakati marais wawili waliopita ni wakristo na mmoja na aliyekuwapo ni muislamu?

Ni Rais gani aliyechukua taasisi ya serikali/umma akawapa WAISLAMU?

Katoliki wana uwezo gani kuwaonea? kwa kujenga mashule? au Lutheran walivyojenga KCMC na Bugando Hospitals au waanglikan kuwa na Universities?.

One thing for sure mnachokosea na unaendelea kukosea ni kuwa wakati wewe na wenzako mnalalamika WAKATOLIKI, WAANGLIKANA NA WALUTHERI WANAFIKIRIA NAMNA YA KUONGEZA vyuo vikuu, mahospitali na mashule!!!!!.

Thats the difference bro!
 
Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.

nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.

BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI

KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!

usiingize mambo ya dini jadili kilichoandikwa.
 
Naona huu uandishi wa kibanda umekuwa chini sana.
1. Amajaribu kuwajengea watanzania hisia kuwa sasa kuna mgogoro wa uchaguzi ndani ya chadema
2. Ameendelea kuwaonyesha watanzania kuwa Zito bado ni mwanasiasa MCHANGA, achilia mbali yote aliyoyafanya ndani ya kipindi cha miaka 5
3. Anawaeleza Watanzania kuwa demokrasia inayotamkwa ndani ya chadema siyo ya kweli bali ya kupeana
4. Amejaribu kumpaka Mbowe mafuta kwa mgongo wa chupa huku akihusisha umaarufu wa zitto kama vile umejengwa kwa nia ya kuingamiza chadema (yaani zito awepo ndani ya chama na kukiangamiza kama ifanyavyo kansa ya damu)

Uandishi huu wa upande mmoja hivi ni wa kulaaniwa hasa wakati huu ambao tunataka kuona demokrasia ikifanya kazi na sio kusikia kuwa tu kuwa ipo.

Bado naamini kuwa wanachadema wanayo kila sababu ya kuwapima na kuridhika kuwa Mwenyekiti ajaye kasi yake itakuwa kuliko ya jana. Busara na hatimaye sanduku la kura ndio viwe waamuzi na si uandishi wa upande mmoja tena wa kichonganishi na ufitini wa kiasi hiki.

Kila la kheri chadema, kusimama kwenu ndio heri ya Tanzania, na kuanguka kwenu ndio kuanguka kwa Tanzania.
 
hii sio siri tena,kibanda kaahidiwa chochote na mbowe.
naona anaandika akiwa mtu mwenye uchungu sana kana kwamba zito kakufulu.
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima bwana Kibanda ameandika makala kwenye gazeti la Tanzania Daima kumshutumu Zitto Kabwe kugombea uenyekiti Chadema.Kibanda anafanya kazi chini ya gazeti la Mbowe,swali Mwalimu Nyerere alipewa Uenyekiti wa Tanu akiwa chini ya miaka 30,

Chadema ni Chama cha demokrasia kwanini Kibanda aogope Chadema watimize kauli yao ya Demokrasia kwa Vitendo? kama Kigezo ni Umri Marekani wangempa John MC CAIN kwa vile ni mtu mzima ana mvi kichwa chote. Tanzania Daima la leo lina habari mbili zote za Zitto Kabwe.
 
Kibanda huwa nakuheshimu sana na mimi ni msomaji mzuri sana wa Makala zako lakini kwa hili ndugu yangu umechemsha sana, sijui motive ya hii makala yako ila kama lengo lilikuwa ni kumfurahisha Mbowe, ninavyomjua Mbowe utakuwa umemuudhi sana.

1: Kwanza unamfanya Mbowe aonekane kama anamuogopa Zitto, kitu ambacho naamisi si kweli.

2: May be unataka kuwagombanisha Mbowe na Zitto kwa sababu as Mwajiriwa wa Freemedia ukaandika habari za Zitto na Mbowe in such a biased manner hii inaweza kumfanya Zitto afikiri kwamba umeagizwa au umetumwa na Mbowe.

3: Kama namba mbili ni ya kweli basi utakuwa umetumwa na mtu ambaye si Mbowe wala yeyote mwenye kuitakia mema CHADEMA, acha Democracy ichukue mkondo wake coz nahofia kesho Magazeti mengine yanaweza kutoka na habari kwamba Mbowe atumia vyombo vyake kupambana na Zitto huoni kama utakuwa unakiongezea Chama Mzigo mzito wa maswali ya kuyajibu?
 
Wanajamvi gazeti la Tanzania Daima mara nyingi limekuwa likiandika habari kwa kuegemea upande mmoja.Nadhani wakati huu wengi mmepata mstuko kwasababu Zitto kaguswa lakini ukilitazama Tanzania Daima linapoandika habari za viongozi wa vyama vingine vya upinzani au hata CCM unaweza kushangaa kama si kusikitisha.

Mheshimiwa Zitto ana haki ya kugombea uenyekiti CHADEMA,mwandishi wa makala anataka kutuaminisha nafasi ya mwenyekiti CHADEMA ni kwaajili ya Mbowe pekee yake!!!!!.

Mheshimiwa Zitto amesema anataka kupeleka CHADEMA katika level nyingine yaani kushika dola,bila shaka kagundua Bwana Mbowe anakididimiza chama ingawa ukitizama kwa undani Bwana Mbowe kajitahidi sana kuifikisha CHADEMA katika level ya juu sana kuliko wenyeviti waliomtangulia.

Mtazamo wangu au maoni yangu kuhusu Mheshimiwa Zitto ni kama ifuatavyo.
Mheshimiwa Zitto si kiongozi wa kuaminika ushahidi ni suala dowans bado mpaka leo kashindwa kuwaomba radhi watanzania kwa kukubali kuwa kuwadi wa RA & Co.Zitto anaweza kutumiwa na mafisadi kirahisi kuivuruga CHADEMA ili kufanikisha agenda za mafisadi kuendelea kuitafuna nchi yetu.
 
Kibada anaona mbali, anahisia za chama kuanguka kutokana na uimara wa mbowe kukifadhili na kujitolea kwa chama.

Mbowe akitoka Chadema itaanguka kwa kishindo kikubwa kama hawatapata wabunge wengi mwaka ujao wa uchaguzi. Wote ni Vijana nina imani walikuwa na fursa ya kukaa pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kisiasa. Vinginevyo ukiona dalili kama hizo ujue kuna jambo aidha mamluki wameanza kuingia Chadema. Tusubiri na tuone matokeo yake.

Watu wengi sana na wenye busara wanashauri sana CHADEMA watafute kwanza wabunge wakutosha watakaoweza kuwajengea imani wananchi then dhana nzima ya kugombea urais ndipo ianze. Zitto akigombea urais kwa mwaka ujao akishindwa na CCM ataanguko sana kisiasa.

Ninyi wenye mawazo ya ki-CCM ndo matatizo yenu. Kwani akigombea na pengine akashinda nafasi hiyo na labda mbowe akaamua kutosupport chama, mwenyekiti lazima atakuwa anajua ni wapi atafute nguvu ya kukiendesha chama. Nakwa taarifa tu ni kwamba chama hujengwa na wanachama siyo pesa ya serikali.

Ni CCM tu duniani inayotumia pesa ya serikali kuendesha chama, na kibaya zaidi CCM inadiriki kuiba kwa kampuni feki ili ijiendeshe.

Tukirudi kwa zitto, mimi na dhani tuachane na mawazo potofu ya akina vibanda. Zitto wewe chukua form gombea, na hata wanao kutabiria mabaya wakishinda wewe bado kijana utatokea kwenye elimu yako!!!

Zitto wewe siyo sawa na akina makamba ambao ukiwaondoa kwenye siasa, wanakufa baada ya wiki moja. Wewe ni msomi unaweza kujiajiri so pambana tu na vijana tutaku support. Wito wangu kwako zitto ni kwamba, hata kama utashinda uenyekiti, tafadhali ujiepushe na fedha za mafisadi ktk kuendesha chama, la sivyo yanayoikumba CCM yatahamia CHADEMA.
 
Kwanza Wanajamii,let me put clear my Stand ninaunga mkono maamuzi ya KABWE ZITTO.

Mbili;Nimesikitika andiko la Kibanda kuonyesha wazi anafanyakazi ya muajiri wake angeweka wazi msimamo huo mapema ningemuelewa.but akiwa mwanahabari ninae muheshimu nimesikitika sana kuona kuwa Tayari amemuhukumu zitto na kumuona kama ni mkosaji.

Tatu;Ushauri wa Bure kwa zito kabwe,katika kipindi hiki na kwa maamuzi haya utegemee kuchafuliwa,kuhujumiwa kwa kuwa imeonekaam na na nyinyi chadema utamaduni wa viongozi flani kuwa hawaguswi mnao,sasa ni wakati wa kuwa FOCUSED,www na Team inayokuunga mkono msiyumbe,yatasemwa mengi na kipanda ameanzisha,tutegemee wengine kukushukia.

Nakutakia kila la kheri na ninategemea wapigakura wote vijana watakuunga mkono kwani imeanza kuonyeshwa kuwa umri mdogo haufai kuongozwa ni wakati wa vijana wote kushikana mkono ili waweze kuonyesha kuwa dhana ya kipanda na wenzie ni potofu.
 
Kibanda, heshima mbele!


Chadema kama chama cha upinzani kinakubalika sana bara, lakini pia kinashutuma za chini kwa chini za ukabila, Mbowe amepewa chama na Bamkwe, ili kuliondoa hilo, chama kishikwe na mtu baki asiyetokana na Uchagga au uKaskazini ili kuwathibitishia Watanzania kuwa Chadema hakina ukabila.

Hongera Zitto for just daring.

Pasco, heshima mbele.

Una maana wana Chadema waliotoka Kilimanjaro au Kaskazini wasigombee ili kuridhisha Watanzania kuwa Chadema haina ukabila..!!!

Are you Serious.???!!
 
Hii ni Kibanda kushambulia Zitto au Gazeti la Tz Daima ndio wamechapa hii habari? ina maana mhariri akiandika msiyoyapenda yanakuwa yake binafsi sio ya gazeti lenyewe?
 
Nadhani Kibanda ana hofu ambayo inaweza kuwa na mantiki kwake na hata kwa CHADEMA. Ila hofu siku zote huzuia mabadiliko, na mabadiliko ndio njia pekee ya maendeleo.

Kwa mtazamo wangu, sidhani kuwa ni sahihi kwa Kibanda kupiga kampeni kama hizi. Si sahihi kwa kuwa anamnyima nafasi na haki mgombea mmoja na kumtengenezea mazingira ya ushindi mgombea mwingine (waziwazi). Vile vile, si sahihi kwa kuwa haikisaidii chama (CHADEMA) kujionyesha kuwa ni chama tofauti na vyama vingine ambavyo viongozi wa juu hung'ang'ania kubaki madarakani kwa njia zozote na hasa kwa kisingizio cha ufanisi wa uongozi wao, hali bora ya chama kisiasa n.k.

CHADEMA inaweza kupanda chart sana kwa kuruhusu kila mwenye nia ya kugombea nafasi yoyote kufanya hivyo. Wananchi ambao kwa wingi sana wanakiangalia chama hiki kama nuru ing'aayo kwa mbali, watafurahi kuona haki sawa inatolewa kwa wanachama wote kugombea nafasi yoyote ndani ya chama bila kujali umri (endapo umetimia miaka inayokubalika kwa nafasi husika).

Nadhani CHADEMA waachie Demokrasia kuchukua mkondo wake. Waamue kutoa fursa sawa kwa wote ili wanachama wanaohusika wafanye uchaguzi kwa manufaa ya chama chao. Kama wataona Zito anafaa, wamachague, si dhambi. Vinginevyo wamchague kiongozi aliepo madarakani au mwingine yeyote wanaemuamini kuongoza chama hicho kwa ufanisi zaidi. Kila la kheri CHADEMA, uamuzi ni wenu.
 
* Huyu Mwandishi, Kibanda simwamini hata kidogo kwanza anatumiwa na mafisadi nakumbuka sakata la Sitta historia itamuhukumu.

* Mh. Zitto kama kweli anaenda kugombea U/Kiti bila kuwa na shinikizo la Mafisadi CCM tutashukuru saana kwani hapo anaijua Demokrasia.

* Mh. Zitto au Mbowe mmojawapo akishindwa zile kura tunaomba akubali matokeo, kwani hapo ndo ataonyesha DEMOCRASIA ndani ya chama isiwe ndo kuanza yale ya Mabele Marando huko NCCR.

* Nimesikitika Zitto anatangaza heti anaenda kwenye U/kiti kushika dola inamaana asiposhika U/kiti chama hakichukui dola! Naona amekiangusha chama! awemakini kwenye kuongea na vyombo vya habari.

Hapa maji yameshamwagika tuwaachie uwanja.
 
Mie ninachokiona hapa ni ANGUKO la KIBANDA kama mwana habari na sio ZITTO ambaye ni mwanasiasa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom