Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mpaka Kieleweke, Aug 19, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Leo Katibu Mkuu wa CHADEMA ametoa tamko rasmi la Mkutano Mkuu wa Ndani ya Chama nalo ni kama ifuatavyo;


  TAARIFA KWA UMMA WA WATANZANIA.

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawatangazia wanachama wote wa CHADEMA na umma wa Watanzania wapenda Maendeleo kuwa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa ndani ya Chama utafanyika tarehe 03-04/09/2009 Jijini Dar Es Salaam .

  Mkutano huu utatanguliwa na Mikutano mbalimbali kama ilivyoorodheshwa kwenye ratiba yetu ikiwa pia ni kwa mara ya kwanza uzinduzi rasmi wa Mabaraza ya Chama utaweza kufanyika pamoja na Uchaguzi wa Viongozi wa Mabaraza husika.

  Hivyo wanachama wote kutoka Mikoani, Wilayani, Katani na Vijiji mbalimbali wenye nia, uwezo,uadilifu na sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya Taifa mnataarifiwa kwenda kuchuka fomu za kugombea na Fomu hizo zirejeshwe Makao Makuu zikiwa zimejazwa kwa ukamilifu na kwa kuzingatia muda uliowekwa na Kamati Kuu ya Chama .

  Fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali zimeshatumwa tangu August 10 2009 kwenye kila ofisi za Chama Mikoani ,hivyo tangazo hili ni kwa ajili ya kuwakumbusha wanachama wetu kuhusu ratiba ya mchakato mzima wa uchaguzi ndani ya Chama. Kwa wale ambao hawajachukua fomu,bado wanayo nafasi kwani tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu ni August 24, 2009 saa kumi kamili mchana.

  Fomu zilizotumwa ni kwa ajili ya kugombea nafasi zifuatazo;

  (a) Mwenyekiti Taifa
  (b) Makamu Mwenyekiti Bara
  (c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
  (d) Wajumbe wa kuchaguliwa kuingia kwenye Kamati Kuu na Baraza Kuu kwa mujibu wa Katiba ya Chama .
  (e) Wenyeviti wa Mabaraza ya
  (i) Wazee
  (ii) Wanawake (BAWACHA).
  (iii) Vijana (BAVICHA).
  (f) Makamu wenyeviti wa mabaraza ya
  (i) Wazee
  (ii) Wanawake (BAWACHA)
  (iii) Vijana (BAVICHA).

  Ratiba kamili ya Mikutano hiyo ni kama ifuatavyo;

  (i) Kamati Kuu tarehe 30/08/2009.
  (ii) Mkutano Mkuu wa Baraza la Wazee 31/08/2009.
  (iii) Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana (BAVICHA) 31/08/2009.
  (iv) Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) 01/09/2009.
  (v) Mkutano wa Baraza Kuu 02/09/2009.
  (vi) Mkutano Mkuu wa Chama (Siku mbili ) 03-04/09/2009.
  (vii) Mkutano wa Baraza Kuu 05/09/2009.
  (viii) Mkutano wa Kamati Kuu 06/09/2009.

  Hivyo basi tunapenda kuwafahamisha Wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa hii ndio ratiba yetu rasmi ya kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa Chama na pia ni hatua muhimu sana katika Mapambano yetu dhidi ya Mafisadi na Ufisadi na kuhamasisha uwajibikaji na kutetea rasilimali za Taifa.

  Ni muhimu ikazingatiwa kuwa ndani ya CHADEMA kila Mwanachama anayo haki ya kugombea nafasi yeyote ile kwa mujibu wa Katiba ya Chama,hivyo basi kila Mwanachama atumie haki yake ya kidemokrasia kuchukua fomu .

  Ahsante sana kwa ushirikiano wenu.

  ………………
  Dr. Willibrod P. Slaa (Mb)
  Katibu Mkuu.
  19/08/2009.
   
  Last edited by a moderator: Aug 25, 2009
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kila jambo jema .Wekeni mambo kwa uwazi na mimi nitafika kusikiliza kinacho endelea .
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwenye Mkutano wake na waandishi pia alijadili kwa kina mambo mbalimbali kama ;
  1.Kuendelea kumjadili Mkapa.
  2.Waraka wa Wakatoliki
  3.Kesi ya Zombe
  4.NEC walivyovunja Katiba kwa kukiuka ibara ya 100 ya Katiba kwa kumpa Spika maelekezo ya Kijinga.


  Pia kwenye Mkutano huo aliambatana na wakurugenzi wa Chama , na LISSU Alitoa ufafanuzi juu ya hoja hizo hapo juu kisheria.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nafirikiri wanachama wa chadema wanatikiwa kuwa makini sana kwenye uchaguzi huu, kwa sababu ni uchaguzi muhimu sana kuelekea 2010 General Election.......!

  Viongozi watakaochaguliwa hapo watatupa dira sahihi ya nini tutegemee from Chadema come 2010, ikizingatiwa (na to be honest), Chadema kwa sasa ndio tegemeo pekee ya ukombozi wa kweli kwa wanyonge Tanzania!

  Kila la kheri Chadema, na msituangushe huko!
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kila la kheri CHADEMA lakini ktk mchujo mjihadhari na mamluki watao ghushi kadi zenu za chama na mkawachagua kuwa viongozi alafu hapo baadaye wataanza kuwasumbua hasa uchaguzi wa mwakani ukifika.
   
 6. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,577
  Likes Received: 925
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa kwa kweli wako poa sana,ni chama ambacho kwa kweli hata wengine ambao tunaona siasa ni CHAFU tunaweza tukajiunga nao.
  Kuweni makini Chadema,jiepusheni na mamluki.
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wish you all the best!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Nabashiri Mwenyekiti ni Dr. Slaa.
  M/M bara Mbowe
  Katibu Mkuu Zito
  M/K Bazala la Wazee -Kimesera
  M/K Baraza la Vijana-Mnyika
  Baraza la Wanawake-Owenya
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huu ni uchaguzi muhimu kwa Chadema kwa namna ya pekee:

  a. NI wakati wa kuwaonesha Watanzania kuwa wamejiandaa kuongoza taifa; yaani timu itakayoingia madarakani ndiyo ambayo itakiongoza chama hiki kuelekea uchaguzi mkuu na hivyo ni lazima iwe timu ambayo inaweza kuunda serikali.

  b. Ni wakati muafaka wa kumaliza kabisa migongano ma malumbano yoyote ndani ya Chama hicho kama wanataka wawe na nafasi yoyote ya kuliongoza taifa. Endapo mkutano huu utaingia madudu kama ule wa CUF au kwa namna yoyote kutokea migongano ya binafsi (siyo ya kiitikadi au kikampeni) basi utakuwa ni mwisho wa chadema kama tunavyoijua.

  c. Uongozi huo mpya ndio bila ya shaka utaandaa agenda ya uchaguzi mkuu kwa Chadema; hivyo ni lazima uwe ni uongozi ambao unaweza kukubaliana na kutokubaliana kwa hoja na pale wanapokubaliana basi wawe ni viongozi ambao hawatodhoofishana. Hiyo ajenda ndiyo itaamua chama kitakuwa na nafasi gani 2010.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  naamini Lwakatare ataingia mahali fulani hapa
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,091
  Trophy Points: 280
  wapo wengi tu, akina Kitila Mkumbo, Mrema, Mdee, Lwakatare, Edson Mbogoro, Mwita Mwikabwe nk. Tuwape nafasi sawa wote. Chadema inawatu wengi makini. Ninawatakia uchaguzi mwema, uliojaa democrasia ya kiwango stahili.
   
 12. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nadhani ni uchaguzi takribani wa nne sasa ndani ya CHADEMA. Hatua kwa hatu chadema mmekua na mmeweza kukabiliana na mawimbi mbalimbali hadi kufikia nafasi hii ya kuonekana kuwa chama mbadala kwa ccm. Hii sasa imefanya chadema kuwa kichefuchefu kikubwa kwa ccm na washirka wake. Nguvu kubwa sana itatumika hasa katika chaguzi zijazo na baada ya chaguzi kukidhoofisha chama pamoja na msingi kiliojiwekea.

  Ni wakati wa kuwa makini kuliko kipindi kingine mlichowahi kupitia katika chaguzi kwani chadema ndio target namba moja sasa katika siasa Tanzania. Viongozi mtakaowachagua ndio watakaotoa dira ya chadema na nafasi ya chadema katika uongozi wa taifa letu hasa kuelekea uchaguzi mkuu.

  Nawatakia uchaguzi mwema, ulio makini sana lakini pia uli wa kidemokrasia na usigubikwa na vitendo vya rushwa, majungu na uchafu mwingine.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hakuna fomu katika mtandao wenu Chadema?
  Hii itawafanya wengine wasisumbuke sana hasa wale walio na uwezo wa kuifikia internet
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Form mamluki wa CCM watajazana .

  KIla jambo jema Chadema .Nina imani kubwa kila atakeya omba kugombea na hasa nafasi ya Juu ya Chama hiki .Nasema mfaniwe tuendeleze mapambano .
   
 15. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #15
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Chadema ni vyema mkajipanga vyema katika uchaguzi huu. Kama mjuavyo, CCM kwa sasa ipo hoi. Watanzania 'wanaojua' nini kinaendelea wanawategemea sana ninyi. Ukweli ni kwamba kwa sasa ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa watu wenye fikra pevu. Angalizo, ningeomba CHADEMA, mfanye kila liwezalo kutafuta vijana ambao mnawafahamu, muwavuta ili wapate nafasi nzuri katika chama na muweze kujijenga zaidi kuelekea 2010. Ukweli ni kwamba kuna vijana wengi wanaweza kuwasaidia na wanawakubali sana lakini kwa sasa wa[o nje ya ulingo wa siasa au wapo neutral au ni wanaCCM wafu(wana kadi za CCM lakini hawaikubali CCM).Nipo tayari kuwasaidieni kuwatafutia vijana wa namna hiyo wekeni e-mail yenu na simu tuonane kwa ushauri zaidi. Mnyika fuatilia hilo wewe ni kijana na nina amini unawajua vijana wengi wenye uwezo ila kutokana na mbio za maisha bado hawapo CHADEMA.
   
 16. A

  ALI KIBERENGO Member

  #16
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHADEMA Msitufanyie Kiini Macho hivi Kwanini Mnavuruga DEMOKRASIA ya Chama kiasi hiki kwa Ubinafsi wenu tu uliokuzongeni? na baya zaidi Msajili wa Vyama JOHN TENDWA amekaa kimyaaaa akiangalia CHADEMA inavyoivunja katiba yake ya CHAMA.

  Tuna Mtaka Msajili wa Vyama azuie mara Moja Mkutano Mkuu wa CHADEMA hadi pale CHADEMA itakapo fanya CHAGUZI zake Kikatiba Kuanzia MATAWI, KATA, WILAYA, MKOWA na Mwishowe ndio TAIFA.
  Hivi uhalali wa Viongozi haowanaotaka Kuchaguliwa utakuwa upo wapi? ikiwa wale wanaokuja kuchakuwa hawakuchaguliwaa kihalali? kwa mijibu wa Katiba ya CHADEMA.

  Uongozi huu wa sasa ulopo wa CHADEMA ni BOMU au ni MAMLUKI Kwani kwa Taarifa RASMI Chadema haijafanya CGhaguzi zake za ngazi ya chini kikatiba ndani ya hii TANZANIA yetu BARA na VISIWANI na hili ni KOSA ambalo litatumika KIsheria Kuwapinga WAGOMBEA WOTE WA CHADEMA 2010 WATAKAO AMUWA KUGOMBEA KUANZIA UDIWANI, UBUNGE, URAIS KWA SABABAU HAWAKUCHAGULIWA KISHERIA KWA KUWA VIKAO VILIVYOWACHAGUWA HAVIKUWA HALALI KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHADEMA, TENA MUTALIA NA NANI? NA HILI LIPO NA LITAFANYIKA.

  WACHENI KUENDESHA CHAMA KAMA KAMPUNI TANZU YA MBOWE NA SLAAA, KAJIFUNZENI KWA WENZENU VIPI CHAMA KINAVYOUNDWA, MKIONA VINAELEA VIMEUNDWAA.
   
 17. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa akichaguliwa Mwenyekiti nadhani hapatatosha kwani JK atakuwa na upinzani mkali kwelikweli na hii itasaidia kuleta wabunge wengi ndani ya CHADEMA. Ila Dr. Slaa bado tunamuhitaji Bungeni zaidi ya kitu chochote.
   
 18. Mzeeba

  Mzeeba Senior Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi huu ukitumika vizuri utatoa nafasi kubwa kwa CHADEMA kujitangaza zaidi kwa vile vyombo karibia vyote vya habari vitafuatilia kwa ukaribu. Ikiwezekana hotuba na uchaguzi wa viongozi wa kitaifa uonyeshwe moja kwa moja kupitia TBC na stesheni nyinginezo. Hii itaonyesha demokrasia inavyofanya kazi ndani ya chama. Mungu awaangazie wote watakaochukua fomu na kupiga kura wafanye hivyo kwa maslahi ya taifa letu Tanzania.
   
 19. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni point. Tunaomba wana CHADEMA waliomo humu JF watufafanulie kuhusu hili kwani saa ya mwisho Presha inaweza kupanda/kushuka tafadhali.
   
 20. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chadema hiki ndio kipindi cha kunyoa au kusuka, mamluki watakuja wengi muwe makini nao. kuna wengi wasiowatakia mema na wanaweza pandikizwa. Chagueni kwa kuzingatia vigezo hasa ili kweli muzidi kujiimarisha kama chama mubadala. Ni kama munaenda kwenye shopping kwa ajili ya uchaguzi wa 2010!!!!!

  All the best, na nawatakia Uchaguzi mwema na wenye mafanikio.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...