Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Dah huyu jamaa amechemka sana na amekiuka maadili ya uandishi wa habari kuwa biased kwani Mbowe alipo kuwa anachukua Uenyekiti alikuwa na umri gani?
 
Zito kabwe alisema kuwa hata gombea ubunge kwa sababu hana experience ya uongozi. Iweje leo aweze kuongozi chama wakati alipojithathmini yeye mwenyewe aligundua kuwa hana expirience ya kutosha?
 
Zito kabwe alisema kuwa hata gombea ubunge kwa sababu hana experience ya uongozi. Iweje leo aweze kuongozi chama wakati alipojithathmini yeye mwenyewe aligundua kuwa hana expirience ya kutosha?
Wee wacha hizo,...
 
Naliona anguko la kihistoria la Zitto.

Iam short of words kuona makala kama hii! Duh!

Jamani mimi si mwanachadema....(but witha right candidate I CAN vote Chadema ) lakini naamini kabisa kila mwenye mapenzi mema na chama hiki ingebidi afurahie uamuzi wa Ndugu Zitto kugombea uenyekiti.

Sitaki kuamini kwamba Mbowe ka-endorse hii makala. Kama atakuwa kaikubali basi kweli..Tanzania we are in deep shit than we thought. Siasa ni challenge. Huyu ndugu Kibanda aache wajumbe wataamua. Kwa nini awe na hofu? kwani Zitto aliwekeana mkataba na Mbowe kwamba hatagombea "nafasi yake ya uenyekiti"? Hivi waafrika tuna tatizo gani? harafu jamaa anasema kabisa bila aibu..."Zitto angesubiri aone kama Mbowe atagombea au la..ndo na yeye afanye uamuzi"..Kibanda are you REAL?????????

Kwani kama Mbowe kafanya kazi nzuri wajumbe si wanaona? kwa hiyo watamkataa Zitto. Simple! Ukweli ni kwamba huyu mwandishi ANAOGOPA nguvu ya Zitto na ni dhahiri kwamba Zitto anaweza shinda hiki kiti. Mi nadhani mtu kama Mbowe ingebidi afurahi kumuona kijana aliyemlea..akiitaka ofisi ya juu kabisa ya Chama. N kwa nini Mbowe asipumzike anyway? pass on the torch! Be different..usiogope challenge..CCM has nothing to do with Zitto expressing his democratic right.

Zitto ni msomi, ni mwanasiasa..ni kipi hana ambacho Mbowe au wagombea wenzake wanacho?

Please ndugu Kibanda..this is too low for you! Very low....Kwangu mimi nimeshachoka na akina Mrema, Marando et al.....let Zitto come in...labda atakuja na kitu kipya. Hivi bwana Kibanda kweli unaweza kuona "anguko la mtu simply because kafanya maamuzi ambayo hukubaliani nayo?" kama wewe ni mwanachama..pambana na Zitto kwa hoja siyo makala kama hizi ambazo kwa kweli ni aibu kwa watanzania.

Go Zitto! I wish you well. Usikatishwe tamaa na akina Kibanda`s of this world.

May the best candidate win the race!
 
Zitto anaweza kabisa! ingekuwa umri ni kigezo basi hata Obama asingeruhusiwa kuongoza dola kubwa kama USA. Its about time hizi mentality za kizee ziondoke vichwani mwa watanzania.
 
Kibada anaona mbali, anahisia za chama kuanguka kutokana na uimara wa mbowe kukifadhili na kujitolea kwa chama.

Mbowe akitoka Chadema itaanguka kwa kishindo kikubwa kama hawatapata wabunge wengi mwaka ujao wa uchaguzi. Wote ni Vijana nina imani walikuwa na fursa ya kukaa pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kisiasa. Vinginevyo ukiona dalili kama hizo ujue kuna jambo aidha mamluki wameanza kuingia Chadema. Tusubiri na tuone matokeo yake.

Watu wengi sana na wenye busara wanashauri sana CHADEMA watafute kwanza wabunge wakutosha watakaoweza kuwajengea imani wananchi then dhana nzima ya kugombea urais ndipo ianze. Zitto akigombea urais kwa mwaka ujao akishindwa na CCM ataanguko sana kisiasa.
 
Sina hakika kama Zitto hafaham pesa ya Chadema inatoka wapi na hana mkakati wowote wa kukiimarisha chama. Ina maana ili uwe mwenyekiti lazima uwe na pesa?

Mie nadhani kwa sasa Zitto ana uzoefu wa ndani ya chama na hata katika serikali. Na pia ana elimu ya kutosha. Tumpe nafasi
 
Hapa tutaona yaleyale ya NCCR Mageuzi pale Mbatia aliposhindana na Mabere Marando na kumshinda, wakati huo Mbatia alikuwa Mbunge wa Vunjo na kijana wa miaka 35 wengi walishangilia uongozi wa kizazi kipya lakini ule ulikuwa mwanzo wa mwisho wa NCCR Mageuzi.

Huyu kijana alikaririwa hivi karibuni akidai kustaafu Ubunge kule kwake, je, yalikuwa ni maandalizi ya kugombea uongozi wa Chadema Taifa?
 
Ni vyema kabisa kwa demokrasia ya chama. na ni muhimu wafanye kampeni safi na atakaeshindwa akubali kwa moyo mkunjufu kama ilivyokuwa kwa Ndesamburo na Makani. wote walibaki kama wanachama waaminifu na wanaooelewana hata baada ya uchaguzi.

All the best Chadema
 
Kibanda anajua maana au kirefu cha CHADEMA? Naomba wadau mumsaidie mi simwelewi kabisa acha wachuane kwa sera na si kwa mapenzi ya kibanda.............

Kibanda kajenga kibanda kwa mbowe ndio tatizo....
 
huyu kibanda nae "kashanunuliwa" na mbowe.

kwani hajui maana ya demokrasia? Tena chama kinajiita cha demokrasia!,

Charity begins at home bana! Chadema vipi nyie? Mpeni nafasi Zitto afanye mambo.
 
Watanzania tu wepesi kusahau mambo. Zitto alianza kunesha kubadirika pale alipopingana na chama chake akipigana kwa nguvu zote ili taifa linunue mitambo ya matapeli wa dowans, (RA), Hii mimi ilinistua na kwakujua nguvu ya kipesa waliyonayo mafia wa kitanzania wanongoza nchi hii kwa remote control, nikajua zitto hatunaye tena! Zito ametumwa kufanya anayotaka kufanya, ni Yuda Iskariote wa upinzani
 
NDUGU ZANGU, MIMI KAMA MWANACHADEMA SINA IMANI NA ZITTI AKIPITA KUWA M/KITI ATATUMIWA NA CCM KUKIUA CHAMA CHETU. NAFIKIRIA HIVYO MAANA KWENYE KAMATI YA MADINI AMEHARIBU. Msimamo wa zitto umepungua tangu aingizwe kwenye kamati ya madini.

Hii TZ ni noma sana sidhani kama akili zetu ni njema ingawa tayari tunalipwa mishahara mizuri watu wanatusalilti kwa kupewa pesa. TUCHUKUE TAHADHARI
 
kwani chadema hakuna katiba na sheria mpaka mtu mmoja aweze kuharibu chama?
au wanachadema wote ni vipofu na wasio na uwezo wa kutambua mtu anaaza kuharibu wakamwacha akaendelea kuharibu,mbona mimi huwa nadhani ni chama kilichokomaa kabisa?siamini kama kipo imara hivyo kwa sababu ya kichwa kimoja tu kwamba mnahofia kichwa hicho[mwenyekiti]kikiamua kinaweza kuharibu chama chenu.
acheni majungu na kampeni humu jf kama wewe ni mwanachama kweli wa chadema mnyime kura siku ya uchaguzi na kampeni hizo ukapige kwa wanachama wanaoweza kumpigia au kutompigia kura.
 
huyu kibanda nae "kashanunuliwa" na mbowe.
Kwani hajui maana ya demokrasia?, tena chama kinajiita cha demokrasia!,
charity begins at home bana!, chaadema vipi nyie?, mpeni nafasi zitto afanye mambo.


hamjauelewa mchezo ulioko hapa. Kibanda anatumiwa na wala si mbowe bali na kundi la mafisadi ili kuvuruga uchaguzi wa chadema na kuisambaratisha. Na anatumiwa na walewale!

kuthibitisha maneno yangu kanunuliwa gari la kufanana yeye na Muhingo, Mhariri Mtendaji wa New Habari na yote yametoka kwa mfadhili mmoja na yanafuatana namba. Kibanda ni fisadi kama wengine
 
Mimi namwona Zito Kabwe kama mzalendo halisi anayefikiria na kutenda beyond party politics, yaani anaweka maslahi ya nchi kwanza. Motto ya CHADEMA tangu enzi za Mzee Mtei kama mwenyekiti ilikuwa 'Wananchi nambari wani, CHADEMA nambari two', wakimaanisha kwao waliweka maslahi ya wananchi mbele. Kipindi hicho hii ilikuwa makusudi kupingana na wazo la CCM kujiita 'nambari wani'.

Kwa chama chenye msimamo kama huo, naona Zito is the man for the job. Apewe uenyekiti, kwa maoni yangu anafaa sana.
 
Nyie wana Chadema ndo maana siku zote mimi na FMES na Masanja tunawapasha hapa.

Kwanza mngeshabikia kuwa Zitto kuchukua fomu ni dalili nzuri na inawajenga in Public kuwa kuna demokrasia sio kama CCM yetu yenye zengwe na mwenyekiti ni rais.

Mngemuacha Zitto wajumbe ndio wampe au kumkataa badala ya nyie kuanzisha mpasuko ndani ya chama chenu chenye nguvu kwa sasa!

Haya Prof baregu naye kachukua fomu. Mie nina encourage watu wengi wachukue fomu ili kudumisha na ku demonstrate DEMOKRASIA ya kweli mnayo HUBIRI.

Hizi kampeni za pembeni pembeni zinaonyesha kuwa hamjakomaa na hamna tofauti na CCM
 
hapana ni mapema sana kusema hivyo nadhani killa mwanachama nihi yake ya msingi kugombea cheo chochote katika chama.wanaojitokeza katika kugombea kwanza inabidi wapongezwe,hii siyo tu kuleta ushindani ndani ya chama bali pia kukiimalisha chama.
 
NDUGU ZANGU, MIMI KAMA MWANACHADEMA SINA IMANI NA ZITO AKIPITA KUWA M/KITI ATATUMIWA NA CCM KUKIUA CHAMA CHETU. NAFIKIRIA HIVYO MAANA KWENYE KAMATI YA MADINI AMEHARIBU. Msimamo wa zitto umepungua tangu aingizwe kwenye kamati ya madini.

Hii TZ ni noma sana sidhani kama akili zetu ni njema ingawa tayari tunalipwa mishahara mizuri watu wanatusalilti kwa kupewa pesa. TUCHUKUE TAHADHARI

I did not get you;what points you trying to make?Toka alivyoteuliwa kwenye Tume ya Rais kuona vitu gani virekebishwe kwenye sekta ya madini msimamo wa Zitto Zuber Kabwe umepungua?THIBITISHA MADAI YAKO!

Kumbuka Jaji Salum Masati WAKATI ANAWAACHIA HURU AKINA zOMBE,alihimiza kwa watz kujenga hulka ya kuthibitisha madai yeyote 'without reasonable doubt',anyways nasubiri ni vipi hasa kuwemo kwenye tume ile kumepunguza msimamo wa Zitto kabwe ktk chama cha CHADEMA!

Naheshimu mawazo sana mawazo yako;lkn kwenye mkusanyiko wa great thinkers kama huu lzm kuwepo kupingana pasipo kupigana.
 
Watanzania tu wepesi kusahau mambo. Zitto alianza kunesha kubadirika pale alipopingana na chama chake akipigana kwa nguvu zote ili taifa linunue mitambo ya matapeli wa dowans, (RA), Hii mimi ilinistua na kwakujua nguvu ya kipesa waliyonayo mafia wa kitanzania wanongoza nchi hii kwa remote control, nikajua zitto hatunaye tena! Zito ametumwa kufanya anayotaka kufanya, ni Yuda Iskariote wa upinzani

Unajua watu tu wepesi sana kutoa judgement kuhusu watu....ohh sijui Zito nini, sijui Kibanda kanunuliwa???etc etc. Hapa cha msingi ni uhuru wa watu kutoa hoja zao, iwe ni Kibanda akiona Zito kachemka mwacheni aseme kwa uhuru, ikiwa Zito anataka kugombea tumwache agombee kwa uhuru pia. So kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake au kufanya chochote ili mradi asivunje sheria/katiba etc. Kibanda ameongea vizuri tu bila kuanza kutukana au kuita majina, na hata Zito alipohojiwa nae kazungumza vizuri tu. Sasa iweje hapa watu wa JF tuanze kushutumiana???
Kila kinachofanyika kina sababu zake, +ve or -ve, cha umuhimu hapa ni tuangalie in deep mazao ya hatua zinazochukuliwa, je matunda yatafaa au laa??
Ni jukumu la wanaChadema kuamua sasa kama wanaona kweli Mbowe atatufikisha tunapoenda watampa uenyekiti, wakiona ni Zito basi watampa. Ambao wataona umri wa Zito ni kikwazo hawatampa kura, watakaoona ni damu changa itafaa watampa kura....basi tusubiri tuone nguvu ya demokrasia.
Kibanda hajakosea kumchambua Zito....that's it.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom