Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
thiz z too much ***** weken ushabiki pemben kweli mtu kutumia haki yake kidemokrasia amekuwa mnafiki yan mnataka vijana wasasa waendelee na zle zama za ya dumu mawazo ya mwenyekiti kwa akili hizi sion anguko la zitto bali ni chama chake kama bado cdm wanahitaji kufuata nyendo za ccm za kiongoz kupita bila kupingwa
 
Zitto katubu zambi zako kwa viongozi wako na uache unafiki sasa..
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mkuu Pasco,

Niseme tu kwamba hakuna kijana aliweza kuvutia wengi ktk miaka ya hiv karibuni kama Zitto, binafsi bado sijaona Zitto alikosa nini CHADEMA mpaka aanze kubadilika, kipindi kile mzee wetu Edwin Mtei aliposema kwamba "WE CAN NO CHOOSE A MAN FROM NO WHERE"( if am not mistaken).

alikuwa amemaanisha kwani anajua changamoto za kiuongozi sasa hebu fikiri leo hii Zitto ndio angekuwa mwenyekiti wa CHADEMA na tabia zake hizi sijui chama kingekuwa wapi.

Zitto jua kwamba mpaka muda huu umekwisha poteza imani mbele ya watu wote makini hapa nchini.

Shardcole@Tabora1
 

zitto kuna sehemu atakosea itakula kwake kwenye maisha yake ya kisiasa
 
Macos

Kiongozi makini hawezi kukaa na akina Juliana Shonza na kupanga mikakati wakati ukisoma tu maandishi ya Juliana unajua kuwa ni mtu asiyepevuka kifikra...

Pia msitake kutudanganya kuwa Zitto kalifanyia hili Taifa mambo makubwa, Zitto hajalifanyia hili taifa jambo lolote, bali Zitto AMELIONGELEA hili taifa mambo makubwa. Kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti. Jinsi CDM ilivyokuwa na kuingiza wanasiasa machachari kama akina Lissu na Mnyika ndivyo Zitto alivyozidi kupwaya na ndio maana anajishuku na kutaka kila anachokiamini yeye na mwanachadema mwingine aamini hichohicho.

Kama kuna mtu ana ushahidi na kitu Zitto alichi ITENDEA Tanzania aweke hapa, sio alichoongelea
 
Last edited by a moderator:
Kibanda alisema, namnukuu,

Hivyo ni wazi kwa wale waliokuwa karibu na intelijinsia za CHADEMA (maana si kila mtu ana access nayo), Zitto alikuwa tayari kwenye orbit za CCM na TISS, ila tu kwa kiwango gani nadhani ndilo lilikuwa swali la wakati ule.

Nazidi kupongeza hekima, busara na uvumilivu wa uongozi wa Mbowe na Slaa ktk kushugulikia masuala ya huyu kijana. Mpaka sasa hapa tulipofikia, naamini hata akifukuzwa CHADEMA leo sio CCM na TISS watakaokuwa na political spinning yoyote to their ends
.

 
Ni maneno mazito ambayo hatimaye yameishia leo kwa Zitto kuanzisha uasi dhidi ya chama chake.Zitto ameanzisha kundi la kumpindua Mkiti wake linaloitwa PM7
 
CCM waliwapandikiza mamluki NCCR MAGEUZI enzi zile Mrema moto mkali 1995 .
Ikaibuka migogoro isiyo na kichwa wala miguu. Safari yao ya mwisho ilishia Tanga.
Tafadhalini sana CHADEMA kuweni macho na huyo Kijana ZITTO KABWE yupo hapo kwa Kazi
Maalumu (KUISAMBARATISHA CHADEMA ).
Wanafiki mtawajua kwa matendo yao period.
 
Macos

Naheshimu mawazo na mtazamo wako. Hofu yangu ni kuwa kama umekuja kumtetea sidhani kama umefaulu maana mtu mwenye akili akisoma maneno yako vizuri ataona unamwangamiza Zitto kwa utetezi huu.
Unazidi kuthibitisha tuhuma ambazo hazipo katika tuhuma zinazozunguka sasa. So sad!

Pasco, nadhani bandiko la kibanda lilihitimisha vizuri tu. Wengi tumekuwa tukimsihi kuwa na subira, apunguze jazba na awe more professional. Kwa bahati mbaya hasikii wala haoni.

Kwa tuhuma hizi za uhujumu, anguko lake kisiasa ni dhahiri kama halipo njiani.
Tuhuma zinazomkabili zinamuondolea sehemu kubwa sana ya sifa za uongozi hata kama ni kiongozi kwa mwonekano.

Nafasi aliyo nayo ya kujirudi au kuzuia uharibu ''damage control'' ni yeye kujitoa kimaso maso bila msaada wa vijana ambao kisiasa ni wachanga na kifikra ni weupe sana.

Zitto anapaswa kuachia ngazi katika uongozi kwa sasa ikiwa ni hatua ya kuwajibika na ku-reset the button.

Jitihada zake za kutaka kuona nyumba inaunguka kwa msemo wa 'namwaga mboga mwaga ugali'' zinaweza zizifanikiwe kwasababu washirika wake hawaonekani kuwa watu makini.

Ningemshauri Zitto awaase vijana wake wasimwage mpunga kwenye kuku wengi na kukaa kimya ni busara na msaada kwake

The only window of opportunity ni yeye kuachia ngazi katika uongozi.

Aachie ngazi kwa sababu amedhihirisha betrayal, amepoteza trust na moral authority yake imekuwa severely compromized. Hizi jitihada za kuwatumia immature political gangs kumsafisha zitahitimisha safari yake mapema sana.

Kiwango na umaarufu aliofikia Zitto halafu uangalie timu aliyokuwa anafanya nayo kazi kichini chini ni ushahidi kuwa pamoja na vision na mission anazoonekane kuwa nazo, politically ni immature na ameonyesha poor judgement kama kiongozi. Zitto anahitaji muda akomae kisiasa na hili litabaki kuwa donda ndugu.

Zitto, kama unakipenda chama chako na unapenda ustawi wa taifa hili, ni wakati muafaka kabisa uweke masilahi yako pembeni kwa kuachia uongozi ili uwe mfano wa vijana shupavu wanaokubali kuwajibika.

Kwasasa huna moral ya kumyooshea kidole Mizengo Pinda ajiuzulu kwa kutowawajibisha mawaziri maana wewe hujafanya hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Endelea kuota kijana ukiamka ntakusimulia ndoto zako
Hili sio suala la kuota tena ndio ukweli halisi, Fanya research Mkuu utagundua kuwa sio tu wananchi wa kawaida bali pia hata wanaomsifia ZZK kwa nia tu ya kuvuruga CHADEMA nao pia hawamwamini.
 
Na tatizo kubwa tukitaka tusitake ni umajimbo na na udini

Wewe ndio unafikra za kidini na ujimbo. Yamkini na wewe ni ndugu wa wavaa vipedo maana hawakosi kulalama udini tu kila kukicha.

Kila mtu hapa ananafasi yake juu ya siasa ya CDM, maana huwezi sema ZZK ni zaidi ya Mnyika, au Msigwa Mchg au NAssari, Au Mdee, au Dr. Slaaa au Mbowe nakadhalika, lazima uwe una ubongo wa kupachikwa kama roboti liliosetiwa na CHICHIEM.

Huyo ZZK unaye msifia ni kwa lipi alilofanya? Kila kukicha ni maneno tu ya kujiinua nafsi yake kwenye vyombo vya habari na si kuinua chama. kwani kakufanya nini cha kukumbukwa TANZANIA kama si kuuuza sura kwenye TV?????????????
 

Hii kitu hii Itatafuna yeye Mpaka akizeeka!
 
Du, kuna watu humu tumetoka mbali na ZZK!, nikukukmbuka nilivyomfagilia hapa, na hizi tuhuma zinazoelekezwa kwake saa hizi, naamini ni za uongo, na nitaendelea kusimama nae!.
 
maamuzi aliyoyafanya zitto mwaka 2009 yakuamua kujitoa ndiyo yanayomgharimu leo hii,nadhani huu ni wakati wakuruhusu demokrasia iamue ndani ya vyama vyetu vya siasa.bila shaka zitto hayuko tayari kurudia makosa aliyokwisha yafanya.lets democracy decide.
 
Wanamwamini akina shigela, nape, kafulila, mchange, shonza na masalia wasio na dira. We know the game ahead, ila bora aende mapema atuachie chadema yetu, kwani chadema si mama wala babs kwa nini tamaa zigaribu taasisi yetu

Hahahaaaa awaachie chadema yenu,eeh kumbe chadema ina wenyewe
 
Hahahaaaa awaachie chadema yenu,eeh kumbe chadema ina wenyewe

Ofkoz CHADEMA ina wenyewe na wenyewe ni wananchi wote tunaotaka mabadiliko ya ukweli na si uroho wa madaraka na unafiki wa masalia, pandikizi WAHED wewe yani mngejua mnatuboa sisi ambao hatupo kwenye uongozi wowote lakini tuna mapenzi na CHADEMA.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…