Macos
Naheshimu mawazo na mtazamo wako. Hofu yangu ni kuwa kama umekuja kumtetea sidhani kama umefaulu maana mtu mwenye akili akisoma maneno yako vizuri ataona unamwangamiza Zitto kwa utetezi huu.
Unazidi kuthibitisha tuhuma ambazo hazipo katika tuhuma zinazozunguka sasa. So sad!
Pasco, nadhani bandiko la kibanda lilihitimisha vizuri tu. Wengi tumekuwa tukimsihi kuwa na subira, apunguze jazba na awe more professional. Kwa bahati mbaya hasikii wala haoni.
Kwa tuhuma hizi za uhujumu, anguko lake kisiasa ni dhahiri kama halipo njiani.
Tuhuma zinazomkabili zinamuondolea sehemu kubwa sana ya sifa za uongozi hata kama ni kiongozi kwa mwonekano.
Nafasi aliyo nayo ya kujirudi au kuzuia uharibu ''damage control'' ni yeye kujitoa kimaso maso bila msaada wa vijana ambao kisiasa ni wachanga na kifikra ni weupe sana.
Zitto anapaswa kuachia ngazi katika uongozi kwa sasa ikiwa ni hatua ya kuwajibika na ku-reset the button.
Jitihada zake za kutaka kuona nyumba inaunguka kwa msemo wa 'namwaga mboga mwaga ugali'' zinaweza zizifanikiwe kwasababu washirika wake hawaonekani kuwa watu makini.
Ningemshauri Zitto awaase vijana wake wasimwage mpunga kwenye kuku wengi na kukaa kimya ni busara na msaada kwake
The only window of opportunity ni yeye kuachia ngazi katika uongozi.
Aachie ngazi kwa sababu amedhihirisha betrayal, amepoteza trust na moral authority yake imekuwa severely compromized. Hizi jitihada za kuwatumia immature political gangs kumsafisha zitahitimisha safari yake mapema sana.
Kiwango na umaarufu aliofikia Zitto halafu uangalie timu aliyokuwa anafanya nayo kazi kichini chini ni ushahidi kuwa pamoja na vision na mission anazoonekane kuwa nazo, politically ni immature na ameonyesha poor judgement kama kiongozi. Zitto anahitaji muda akomae kisiasa na hili litabaki kuwa donda ndugu.
Zitto, kama unakipenda chama chako na unapenda ustawi wa taifa hili, ni wakati muafaka kabisa uweke masilahi yako pembeni kwa kuachia uongozi ili uwe mfano wa vijana shupavu wanaokubali kuwajibika.
Kwasasa huna moral ya kumyooshea kidole Mizengo Pinda ajiuzulu kwa kutowawajibisha mawaziri maana wewe hujafanya hivyo.