Wanajamvi wote
Tukubaliane kupingana bila kupigana. Tumuache Zitto agombee uenyekiti wa Taifa wa Chadema kwa sababu ni haki yake ya kikatiba na kwa wengine wengi ana uwezo na huu ni wakati wake.
Waswahili husema wakati ukuta na tumuombee ashinde na baada ya hapo kila mmoja atakuwa na la kusema baada ya kumpima. Speculative journalism ni kitu cha kawaida duniani na wala si unprofessional or unethical kama alivyoona mwanazuoni mmoja humu.
Makala yangu (Naliona Anguko la Zitto Kabwe) pamoja na mapungufu mengi ambayo hata mimi ninayaona kutokana na michango ya wanajamvi, haikulenga kumkatisha tamaa Zitto na wale waliomlazimisha kujaza fomu uwanja wa ndege la hasha. Ilikuwa ni ya tahadhari tu.
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba pengine nilishindwa kuufikisha ujumbe niliokusudia. Nimewasiliana na Zitto mwenyewe leo, jana na juzi na tumebadilishana mawazo na kuonyeshana mapungufu ya hapa na pale.
Nimezungumza na Mbowe pia kuhusu maoni ya wanajamvi juu ya kile nilichokiandika na mlichoandika wenzangu. Naamini watatumia fursa hii kuhakikisha wanawanyima mahasimu wao fursa ya kuendelea kuwatuhumu kwa ukabila, ubadhirifu, ubinafsi, utoto na mambo mengi mengine wanayokabiliana nayo. Ni jambo jema kwamba japo kwa maneno wote wanasisitiza kwamba, watahakikisha Chadema inabakia moja hata baada ya Uchaguzi Mkuu.
Zitto amenihakikishia kwamba ameichukua makala ile na nyingine nyingi zilizompinga kama changamoto na kimsingi hawezi kujiangusha yeye mwenyewe, chama chake wala vijana ambao wameonyesha matumaini makubwa kwake. Sina sababu hata moja ya kumtilia shaka kwa msimamo wake huo.
Ni jambo la faraja sana kwamba, hata katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari amekuwa makini kujibu baadhi ya hoja zilizoandika katika makala ile ya anguko kama zile za uchanga wake katika siasa.
Amejenga hoja kuhalalisha uzoefu wake kiuongozi ndani ya chama na ndani ya Bunge. Pamoja na ukweli kwamba, bado naendelea kutofautiana na staili yake ya uchukuaji fomu, ikiwa ni pamoja na kushangazwa na hatua yake ya kukubali kuungwa mkono na baadhi ya watu ambao ama wana visasi, chuki binafsi binafsi dhidi ya Mbowe, Slaa, Komu, Mnyika, John Mrema na watendaji wengine wa makao makuu
Amenukuliwa akisema analo jukumu la kuponya majeraha ya makundi ndani ya Chadema yaliyoibuka kutokana na migogoro iliyowapokonya madaraka watu kama marehemu Chacha Wangwe na kuwakimbiza ndani ya chama hicho watu kama Dk. Walid Kabourou na wengine.
Katika hili naamini atakuwa amejipanga kuhakikisha matokeo ya uchaguzi utakaompa ama yeye au Mbowe ushindi, hayataibua makundi mapya ambayo yatampasa mwenyekiti ajaye kuanza kuyatibu.
Hoja ya Nchimbi ndani ya thread hii kwamba wao CCM hadi sasa wameshindwa kutibu majeraha ya Uchaguzi wa mwaka 2005 ni somo zuri kwa Zitto, Mbowe na viongozi na wanachama wote wa Chadema.
Wito wangu kwa wanajamvi ni kuweka mbele maslahi ya taifa wakati tunapojadili hoja za namna hii, ili kuepuka lugha za kudhalilishana na kupakana matope. Wale wanaoanza kupiga chini ya mikanda na wao wakajibiwa kwa utaratibu wao huo huo wanapaswa kuwa wavumilivu na kukubali kwamba wao ndiyo waanzilishi.
You all deserve my apology. I'm defeated, you have all won. The battle is on but the war have ended.
Goo Zitto...Goo Mbowe...Goo Chadema.. I always wish a strong multi party democracy.