Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
thiz z too much ***** weken ushabiki pemben kweli mtu kutumia haki yake kidemokrasia amekuwa mnafiki yan mnataka vijana wasasa waendelee na zle zama za ya dumu mawazo ya mwenyekiti kwa akili hizi sion anguko la zitto bali ni chama chake kama bado cdm wanahitaji kufuata nyendo za ccm za kiongoz kupita bila kupingwa
 
Zitto katubu zambi zako kwa viongozi wako na uache unafiki sasa..
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mkuu Pasco,

Niseme tu kwamba hakuna kijana aliweza kuvutia wengi ktk miaka ya hiv karibuni kama Zitto, binafsi bado sijaona Zitto alikosa nini CHADEMA mpaka aanze kubadilika, kipindi kile mzee wetu Edwin Mtei aliposema kwamba "WE CAN NO CHOOSE A MAN FROM NO WHERE"( if am not mistaken).

alikuwa amemaanisha kwani anajua changamoto za kiuongozi sasa hebu fikiri leo hii Zitto ndio angekuwa mwenyekiti wa CHADEMA na tabia zake hizi sijui chama kingekuwa wapi.

Zitto jua kwamba mpaka muda huu umekwisha poteza imani mbele ya watu wote makini hapa nchini.

Shardcole@Tabora1
 
Hii ni wakati ule Kibanda alipokuwa hajaingia kwenye ORBIT ya kina Kinana!!

“...CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu mimi… mimi si maarufu kuliko chama. CHADEMA ni taasisi, ni chama ambacho kina misingi ya uanzishwaji wake.

“…(Wanasema) eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi, si kweli. Niligombea ubunge nikitokea shule, sikuwa najulikana. Nilikuta ‘grassroots network’ ya chama, (chama) hakikujengwa na mimi.


Hiiki kijamaa kimekuwa kinafiki hadi kinasahau kimeisha wahi kusema nini hiko nyuma!!
Sikui hizi anasema anadamu ya ke kwenye chama! ana jasho lake, hawezi kuondoka kwenye chama alichoshoriki kukijenga!!!

Wa hovyo sana huyu Zitto!

zitto kuna sehemu atakosea itakula kwake kwenye maisha yake ya kisiasa
 
Macos

Kiongozi makini hawezi kukaa na akina Juliana Shonza na kupanga mikakati wakati ukisoma tu maandishi ya Juliana unajua kuwa ni mtu asiyepevuka kifikra...

Pia msitake kutudanganya kuwa Zitto kalifanyia hili Taifa mambo makubwa, Zitto hajalifanyia hili taifa jambo lolote, bali Zitto AMELIONGELEA hili taifa mambo makubwa. Kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti. Jinsi CDM ilivyokuwa na kuingiza wanasiasa machachari kama akina Lissu na Mnyika ndivyo Zitto alivyozidi kupwaya na ndio maana anajishuku na kutaka kila anachokiamini yeye na mwanachadema mwingine aamini hichohicho.

Kama kuna mtu ana ushahidi na kitu Zitto alichi ITENDEA Tanzania aweke hapa, sio alichoongelea
 
Last edited by a moderator:
Kibanda alisema, namnukuu,

"Watu tunaolifahamu hilo kwa ndani, tunatambua vyema kwamba, kwa CCM na kwa maofisa usalama wa taifa waliolelewa katika mfumo wa siasa za chama kimoja, kuanguka au kuporomoka kwa uimara wa CHADEMA wa leo hii, ni jambo la kuliwekea mikakati na kwa kiwango kikubwa kulishangilia"
Hivyo ni wazi kwa wale waliokuwa karibu na intelijinsia za CHADEMA (maana si kila mtu ana access nayo), Zitto alikuwa tayari kwenye orbit za CCM na TISS, ila tu kwa kiwango gani nadhani ndilo lilikuwa swali la wakati ule.

Nazidi kupongeza hekima, busara na uvumilivu wa uongozi wa Mbowe na Slaa ktk kushugulikia masuala ya huyu kijana. Mpaka sasa hapa tulipofikia, naamini hata akifukuzwa CHADEMA leo sio CCM na TISS watakaokuwa na political spinning yoyote to their ends
.

 
Ni maneno mazito ambayo hatimaye yameishia leo kwa Zitto kuanzisha uasi dhidi ya chama chake.Zitto ameanzisha kundi la kumpindua Mkiti wake linaloitwa PM7
 
CCM waliwapandikiza mamluki NCCR MAGEUZI enzi zile Mrema moto mkali 1995 .
Ikaibuka migogoro isiyo na kichwa wala miguu. Safari yao ya mwisho ilishia Tanga.
Tafadhalini sana CHADEMA kuweni macho na huyo Kijana ZITTO KABWE yupo hapo kwa Kazi
Maalumu (KUISAMBARATISHA CHADEMA ).
Wanafiki mtawajua kwa matendo yao period.
 
Macos

Naheshimu mawazo na mtazamo wako. Hofu yangu ni kuwa kama umekuja kumtetea sidhani kama umefaulu maana mtu mwenye akili akisoma maneno yako vizuri ataona unamwangamiza Zitto kwa utetezi huu.
Unazidi kuthibitisha tuhuma ambazo hazipo katika tuhuma zinazozunguka sasa. So sad!

Pasco, nadhani bandiko la kibanda lilihitimisha vizuri tu. Wengi tumekuwa tukimsihi kuwa na subira, apunguze jazba na awe more professional. Kwa bahati mbaya hasikii wala haoni.

Kwa tuhuma hizi za uhujumu, anguko lake kisiasa ni dhahiri kama halipo njiani.
Tuhuma zinazomkabili zinamuondolea sehemu kubwa sana ya sifa za uongozi hata kama ni kiongozi kwa mwonekano.

Nafasi aliyo nayo ya kujirudi au kuzuia uharibu ''damage control'' ni yeye kujitoa kimaso maso bila msaada wa vijana ambao kisiasa ni wachanga na kifikra ni weupe sana.

Zitto anapaswa kuachia ngazi katika uongozi kwa sasa ikiwa ni hatua ya kuwajibika na ku-reset the button.

Jitihada zake za kutaka kuona nyumba inaunguka kwa msemo wa 'namwaga mboga mwaga ugali'' zinaweza zizifanikiwe kwasababu washirika wake hawaonekani kuwa watu makini.

Ningemshauri Zitto awaase vijana wake wasimwage mpunga kwenye kuku wengi na kukaa kimya ni busara na msaada kwake

The only window of opportunity ni yeye kuachia ngazi katika uongozi.

Aachie ngazi kwa sababu amedhihirisha betrayal, amepoteza trust na moral authority yake imekuwa severely compromized. Hizi jitihada za kuwatumia immature political gangs kumsafisha zitahitimisha safari yake mapema sana.

Kiwango na umaarufu aliofikia Zitto halafu uangalie timu aliyokuwa anafanya nayo kazi kichini chini ni ushahidi kuwa pamoja na vision na mission anazoonekane kuwa nazo, politically ni immature na ameonyesha poor judgement kama kiongozi. Zitto anahitaji muda akomae kisiasa na hili litabaki kuwa donda ndugu.

Zitto, kama unakipenda chama chako na unapenda ustawi wa taifa hili, ni wakati muafaka kabisa uweke masilahi yako pembeni kwa kuachia uongozi ili uwe mfano wa vijana shupavu wanaokubali kuwajibika.

Kwasasa huna moral ya kumyooshea kidole Mizengo Pinda ajiuzulu kwa kutowawajibisha mawaziri maana wewe hujafanya hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Endelea kuota kijana ukiamka ntakusimulia ndoto zako
Hili sio suala la kuota tena ndio ukweli halisi, Fanya research Mkuu utagundua kuwa sio tu wananchi wa kawaida bali pia hata wanaomsifia ZZK kwa nia tu ya kuvuruga CHADEMA nao pia hawamwamini.
 
Na tatizo kubwa tukitaka tusitake ni umajimbo na na udini

Wewe ndio unafikra za kidini na ujimbo. Yamkini na wewe ni ndugu wa wavaa vipedo maana hawakosi kulalama udini tu kila kukicha.

Kila mtu hapa ananafasi yake juu ya siasa ya CDM, maana huwezi sema ZZK ni zaidi ya Mnyika, au Msigwa Mchg au NAssari, Au Mdee, au Dr. Slaaa au Mbowe nakadhalika, lazima uwe una ubongo wa kupachikwa kama roboti liliosetiwa na CHICHIEM.

Huyo ZZK unaye msifia ni kwa lipi alilofanya? Kila kukicha ni maneno tu ya kujiinua nafsi yake kwenye vyombo vya habari na si kuinua chama. kwani kakufanya nini cha kukumbukwa TANZANIA kama si kuuuza sura kwenye TV?????????????
 



“...CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu mimi… mimi si maarufu kuliko chama. CHADEMA ni taasisi, ni chama ambacho kina misingi ya uanzishwaji wake.

“…(Wanasema) eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi, si kweli. Niligombea ubunge nikitokea shule, sikuwa najulikana. Nilikuta ‘grassroots network’ ya chama, (chama) hakikujengwa na mimi.

“CHADEMA ilijengwa na uongozi uliokuwepo, nilikuta uongozi ‘intact’ (imara). Katika kila kijiji kulikuwa na uongozi na hata katika vitongoji vyote. Wakati naingia kugombea ubunge kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wenye kadi wanaofikia 10,800 katika jimbo zima. Hawa sikuwatafuta mimi, niliwakuta na ndio waliofanikisha ushindi wangu.

“...Katika mazingira kama haya utasemaje kuwa mimi ni maarufu kuliko chama wakati chama ndicho kimenipa umaarufu?

“...CHADEMA ni chama ambacho wenyeviti wake wastaafu wanaendelea kuenziwa na kuhudhuria vikao vyote vya chama… ‘institutional memory’ ipo kuliko katika vyama vingine vya upinzani.
“...Alipohama (Dk. Aman Walid) Kabourou, wengi walidhani ndiyo mwisho wa CHADEMA Kigoma, lakini leo hii CHADEMA ni moto Kigoma kuliko ilivyokuwa awali.”


Ni jambo la ajabu kwamba, karibu miaka miwili tangu Zitto mwenyewe akiri kutambua kuwapo kwa njama hizo za kumkosanisha na viongozi wenzake na pengine kukihujumu chama chao, anaonekana akiingia katika mtego ambao miaka kadhaa iliyopita ulipata kukinasa chama kingine cha NCCR Mageuzi kiasi cha kukifanya leo hii kushindwa kufurukuta hata kufananishwa na baadhi ya watu kuwa ni sawa na shirika lisilo la kiserikali (NGo).


Absolom Kibanda-jumatano, 26 agosti 2009

My Take:
Tamko hili lilitolewa siku ya Jumatano, 26 agosti 2009.
Jee Maneno ya Unabii Huu Kutimia Kabla ya 2015?.
Pasco.


Hii kitu hii Itatafuna yeye Mpaka akizeeka!
 
Kibanda, heshima mbele!

Kwanza siamini kuwa Kibanda amenunuliwa na Mbowe bali one thing for sure, Kibanda anajikomba kwa Mbowe, what for ndio sijui ni kutetea kibarua chake, ama kujikomba komba tuu ili mradi kujikomba.

Namuheshimu sana tuu Kibanda kama mwandishi, mhariri na mchambuzi, na Tanzania Daima la Jumatato, ni miongoni mwa magazeti ambayo sio tuu can't afford to miss, bali pia ends up in my achive, hivyo halifungii samaki.ila kwa makala hii, Kibanda amechemsha big time.Hoja ya umri haina mashiko, hapa tunaangalia uwezo wa uongozi kati yao. Kibanda angepaswa kuogopa kama Zitto hana uwezo alionao Mbowe na sio umri.

Kitendo cha Zitto kuwania kugombea uenyekiti wa Chadema, ni kitendo cha kuungwa mkono na waona mbali wengi na kitalaaniwa na myopic wote wenye myopia ambapo Kibanda nae sasa anaingia kwenye kundi hili.Japo mimi sio mwanachama wa chama chochote, ila ni mshabiki wa demokrasia ya kweli, nawaambieni kuingia kwa Zitto kwenye kinyanganyiro hicho ni uthibitisho wa demokrasia ya kweli ndani ya Chadema.

Chadema kama chama cha upinzani kinakubalika sana bara, lakini pia kinashutuma za chini kwa chini za ukabila, Mbowe amepewa chama na Bamkwe, ili kuliondoa hilo, chama kishikwe na mtu baki asiyetokana na Uchagga au uKaskazini ili kuwathibitishia Watanzania kuwa Chadema hakina ukabila.

Kama kilivyo CUF kuandamwa na udini wa kichinichini kuwa ni chama cha Kiislamu, ndivyo Waislamu wenye msimamo mkali wanakiona Chadema kama chama cha Kikristo, tangu kimeanzishwa, wenyeviti wake wote na makatibu wakuu ni Wakristo tuu, kuingia kwa Zitto kutaliondoa hili na kukifanya Chadema chama cha kitaifa zaidi tayari kuchukua nchi, 2015.

Zitto ni reformist na strategist leader, Mbowe ni kiongozi mzuri ila kwa vile politics zake ni spoon fed na bamkwe, hapo alipokifikisha Chadema ndio mwisho wa uwezo wa Freeman kama Lipumba alivyogota na CUF bara. Kuendelea na uenyekiti ni kuididimiza Chadema. Zitto ni damu mpya, damu changa inayoweza kuibua tumaini jipya kwa Chadema, kitendo cha kuamua kugombea uenyekiti, lazima kuna mambo ameyaona ambayo Mbowe hayawezi hivyo anataka kushika usukani aokoe jahazi.

Hongera Zitto for just daring.
Du, kuna watu humu tumetoka mbali na ZZK!, nikukukmbuka nilivyomfagilia hapa, na hizi tuhuma zinazoelekezwa kwake saa hizi, naamini ni za uongo, na nitaendelea kusimama nae!.
 
maamuzi aliyoyafanya zitto mwaka 2009 yakuamua kujitoa ndiyo yanayomgharimu leo hii,nadhani huu ni wakati wakuruhusu demokrasia iamue ndani ya vyama vyetu vya siasa.bila shaka zitto hayuko tayari kurudia makosa aliyokwisha yafanya.lets democracy decide.
 
Wanamwamini akina shigela, nape, kafulila, mchange, shonza na masalia wasio na dira. We know the game ahead, ila bora aende mapema atuachie chadema yetu, kwani chadema si mama wala babs kwa nini tamaa zigaribu taasisi yetu

Hahahaaaa awaachie chadema yenu,eeh kumbe chadema ina wenyewe
 
Hahahaaaa awaachie chadema yenu,eeh kumbe chadema ina wenyewe

Ofkoz CHADEMA ina wenyewe na wenyewe ni wananchi wote tunaotaka mabadiliko ya ukweli na si uroho wa madaraka na unafiki wa masalia, pandikizi WAHED wewe yani mngejua mnatuboa sisi ambao hatupo kwenye uongozi wowote lakini tuna mapenzi na CHADEMA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom