Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Hakuna anayepinga
kibanda au mtu mwingine yeyote kuwa na maoni ya mawazo yake.
Tunachokataa hapa ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi mazima na huyu
kibanda kwa malengo yake binafsi.

Nimesema hapo awali kwamba kinachoweza kuwanusuru ccm kubaki madarakani
kwa mwaka 2015 ni vyombo vya dola pekee na hakuna kingine. Kinana hana
uwezo wowote wa kuihuisha ccm. Umeshafanya tathmini ya ziara alizofanya
hivi karibuni mikoa ya Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha na kuona muitikio
wa wananchi dhidi ya kinana na ccm kwa ujumla?

Kama kweli kinana mwenyewe anajitambua kwamba yeye ni kimbunga cha
kuuzoa upinzani na kuufukia shimoni inakuwaje anakwenda mikoani na
kukodi wananchi wa kwenda uwanjani kumsikiliza? kimbunga kikivuma si
wananchi/ watu wenyewe wanakisikia na kujikusanya? inakuwaje hiki
kimbunga cha kinana kisaidiwe kujaza watu uwanja kwa kuwanunua watu kama
alivyofanya hivi karibuni Arusha ambako ni "nyumbani" kwao kwa watu
kupewa fedha ili wahudhurie mkutano?

Kama mtu anawakosoa viongozi wetu kwa mambo ya ukweli tutakubaliana nae
lakini yeyote atakayethubutu kutengeneza kiwanda cha uongo huyo
hatutamuacha apite kimya kimya, lazima tutamjibu kwa tune ile ile
aliyotumia kuwahadaa wananchi. Imeshafahamika kwamba kibanda yuko njiani
kwenda kwa fisadi Rostam sasa kwanini anahangaika kuwachafua viongozi
wetu? kwanini asiondoke kwa amani tu? kwani wangapi waliondoka Tanzania
daima lakini bado gazeti linazidi kupata mauzo ya juu? Manyerere Jackton
na Deodatus Balile kwa kutaja wachache, waliondoka lakini bado Tanzania
Daima haikutetereka.

issue siyo kujaza watu mikutanöni bali mikakati ya ushindi ambayo hamna
CDM, wanazi wa CDM ukiwaeleza hili wao wanachofikiri ni wizi wa kura tu.
Chukulia mfano kwenye kata 22 ambazo CDM walishindwa na CCM, je mikutano ya CDM haikujaa
watu? Ni wangapi kati ya wahudhuriaji waliopiga kura?
 
Nimemsoma Kibanda between the line anatatizo moja tu;muumini wa historia kale bila kuzingatia mabadiliko yaliyopo katika jamii anayoishi ndiyo maana pamoja na hoja zilizoibuka kwenye makala yake ya awali bado leo tena amerudia mrundiko wa wa historia kale za Mkapa, Mrema, Kikwete bila kueleza what exactly Kinana can do to overturn the current political storm.

Ndiyo maana headline ya Makala yake ni tofauti na content. Utaanzaje na headline ya HUYU NDIYE KINANA NINAYEMFAHAMU halafu ndani (I mean kwenye content) umejaza Riwaya za nyuma za akina Mrema, Mkapa, Nyerere na Kikwete? Tulitegema angekuja na facts za ni kwa vipi Kinana atasababisha kifo cha Upinzani nchini lakini wapi.Blaa blaa zilezile tu.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo hiyo Tume ya Uchaguzi ya Rais ndio iliyowatangaza washindi John Mnyika, Joseph Mbilinyi, Halima Mdee, Godbless Lema, Freeman Mbowe na wengine.

bila wananchi kukesha hayo maeneo usalama wa taifa na polisi walishaamua kuyachakachua,.
 
Sidhani kama ni sawa sana mtu kama wewe kuandika vitu kama hivi?!,labda nikwambie ukitaka kujua urijali wangu we nambie nikukute chumba namba ngapi ili ujue niko sawa au siko sawa,mimi nilikuwa naamini humu ndani tunakwenda kwa hoja lakini kumbe naona huna hoja umeanza matusi,wewe sema uko chumba namba ngapi mimi nije



Huko koooote ulikopita ulikuwa unazunguka mbuyu tu hapo kwenye nyekundu ndiyo ilikuwa target yako kwakuwa hiyo ndiyo kazi mliyokabidhiwa juzi wakati wa mkutano wenu mkuu wa dodoma.

Tuhuma za Dr. Slaa kanisani zimekuwa zikitungwa na ninyi ccm lakini kanisa Katoliki limekanusha hizo taarifa kwamba sio za kweli.
Kuzungumzia mahusiano ya kimapenzi ya mwanaume mwenzako ni dalili mbaya kwako wewe binafsi, kwani inamfanya mtu aanze kutathmini uwezo wako (urijali wako) katika mahusiano ya kimapenzi.

Sidhani kama ni sawa sana mtu kama wewe kuandika vitu kama hivi?!,labda nikwambie ukitaka kujua urijali wangu we nambie nikukute chumba namba ngapi ili ujue niko sawa au siko sawa,mimi nilikuwa naamini humu ndani tunakwenda kwa hoja lakini kumbe naona huna hoja umeanza matusi,wewe sema uko chumba namba ngapi mimi nije ili uone na katika hili sipepesi macho,nawaomba mods msiiondoe wala msiniban kwa sababu yake mmeiacha imekuja,so nipeni haki yangu na mimi!![/QUOTE]

WABHEJASANA,
Pole sana kauli za matusi ndio msingi wa hoja kwa hawa Pro-Chadema JF.
 
Last edited by a moderator:
Ni mali ya kiongozi wa CHADEMA; 'unajifanya' hujui au mkwara tu?! Haya Lete lingine!

CEO wa chadema na gazeti la tanzania daima ni freeman mbowe,kibanda amejaribu kutahadhalisha hatari ya chadema mbele na kwa maoni yake hamkubali dr slaa kama presidential material,lakini pia ana kerwa na pro chadema ambao hawataki kusikia hata ushauri mbaya wa sura ya chadema
 
Huyu bado tu hataenda habari corporation?

Kumsifia mtu ndio UKWELI(maadili), kweli hii taaluma inatumika kama mpira wa kiume!

Huwezi amini kama ndio mwenyekiti wa jukwaa la wahariri

Tumeambiwa anaanza kazi kwa Bashe (Habari Corporation) very soon, kuna thread inaongelea suala hilo humu humu JF
 
We mhariri ningekuona wa maana kama ungekuwa unaongelea ni jinsi gani taifa letu linaweza kujikwamua na mikataba mibovu, kupunguza rushwa kwenye mahakama na polisi barabarani ili watu wa kawaida wapate ahueni. We hizi porojo za kusifia viongozi ili uteuliwe kuwa mkuu wa wilaya, hazitasaidia nchi wala watanzania wa enzi hizi sio wakusikia kusifia watu badala ya kuandika makara zitakazo saidia wananchi wapate ahueni ya maisha. UNALETA SIASA KWENYE TASNIA YA HABARI? KWELI UKIPOKEA BAHASHA UNAKUWA KAMA KICHAA!
 
Mi mwenzenu huwa naogopa sana nikiona mtoto wa kiume ameshupalia kumsifia mwanamme mwenzie, bora hizo sifa ziwe za kweli, au asifie once. Lakini akirudia rudia na wengine hawaoni hivyo huwa naogopa kweli. Thank god ak sio mwanangu
 
issue siyo kujaza watu mikutanöni bali mikakati ya ushindi ambayo hamna
CDM, wanazi wa CDM ukiwaeleza hili wao wanachofikiri ni wizi wa kura tu.
Chukulia mfano kwenye kata 22 ambazo CDM walishindwa na CCM, je mikutano ya CDM haikujaa
watu? Ni wangapi kati ya wahudhuriaji waliopiga kura?
kuisifia ccm kushinda chaguzi ndogo ni ufinyu wa mawazo, kwa nini serikali ya ccm inakataa kuboresha daftari la wapiga kura kila panapotokea uchaguzi wa marudio?
wasifu ccm wakishinda uchaguzi km watakubali kuboresha daftari la wapiga kura kwanza kila unapotokea uchaguzi mdogo!
 
Nimemsoma Kibanda between the line anatatizo moja tu;muumini wa historia kale bila kuzingatia mabadiliko yaliyopo katika jamii anayoishi ndiyo maana pamoja na hoja zilizoibuka kwenye makala yake ya awali bado leo tena amerudia mrundiko wa wa historia kale za Mkapa, Mrema, Kikwete bila kueleza what exactly Kinana can do to overturn the current political storm.

Ndiyo maana headline ya Makala yake ni tofauti na content. Utaanzaje na headline ya HUYU NDIYE KINANA NINAYEMFAHAMU halafu ndani (I mean kwenye content) umejaza Riwaya za nyuma za akina Mrema, Mkapa, Nyerere na Kikwete? Tulitegema angekuja na facts za ni kwa vipi Kinana atasababisha kifo cha Upinzani nchini lakini wapi.Blaa blaa zilezile tu.

WOWOWO,
Historia katika siasa zetu ni jambo la muhimu sana. Naona unajidanganya na upepo wa mwaka 2010 uliowapitia Chadema wakapata viti vya ubunge 23 vinawapa upofu mnajisahau mnadhani Chadema mnakubalika kila kona ya nchi yeyote atakayewakosoa lazima hatakuwa mpinzani wa Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Hatimaye mbivu na mbichi zinaanza kujitenga. Taraatiiiibu ukweli unaanza kujibainisha. Kibanda ameanza kuionesha sura halisi ya cdm na kuwaonya watanzania kuiogopa kama ukoma. Hapo dikteta anayemsemea Kibanda ni Slaa. J.K kanyaga twende acha wafu wa chadema wazikane wenyewe.
 
WABHEJASANA,
Pole sana kauli za matusi ndio msingi wa hoja kwa hawa Pro-Chadema JF.

Ni aibu, tena aibu kubwa kwa mwanaume kuthubutu kuzungumzia mahusiano ya kingono ya mwanaume mwenzako. Hilo sio tusi bali ni ukweli halisi na mnapaswa kuutambua. Ni bahati mbaya sana kwamba baadhi yenu hamna hoja ya kuandika ama kujadili juu ya Dr. Slaa zaidi ya mambo ya mahusiano yake ya kingono ambayo hayatusaidii chochote kama Taifa.
 
bila wananchi kukesha hayo maeneo usalama wa taifa na polisi walishaamua kuyachakachua,.

Mkuu hoja yako mbona dhaifu sana...kama Dr Slaa alishinda urais mbona watu hawakuingia barabarani na kukesha.
 
Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda baada ya wiki iliyopita kuibuka na Makala isemayo NAMUOGOPA KINANA iliyokuwa ikimwagia kila aina ya Sifa, leo hii ameibuka na makala nyingine ya kumsifu Katibu mkuu huyo wa CCM huku akiponda mashabiki na wanachama wa CHADEMA kwamba ni walevi wa Fikra na anatabiri Kimbunga cha Kinana kwa CHADEMA kitakuwa 2015....Endelea.........


YAKO mambo ya msingi katika maisha ya kitaaluma katika fani zote za kielimu ambayo mtu yeyote anayetambua na kujali vyema wajibu wake anapaswa kuyasimamia na kuyalinda hata kama atafanya hivyo kwa gharama ya kupoteza maisha, kuchukiwa, kudharauliwa au kupuuzwa.

Moja ya mambo ya namna hiyo ni miiko ya kitaaluma ambayo aghalab huongoza na kujenga misingi ya uwepo na kustawi kwa kila fani iwe ni sheria, elimu, uaskari, uhandisi na hata ukachero.

Uandishi wa habari ni moja ya taaluma ambazo zina miiko na maadili yake. Zaidi ya hayo uandishi wa habari na waandishi wa habari wanaishi kwa kufuata na kuzingatia miongozo yao ya kikazi na kitaaluma.

‘Ukweli’ ni moja ya misingi mikuu ya uandishi wa habari. Huu unaweza ukawa msingi mama katika taaluma hii adhimu. Ni kwa kuzingatia hilo ndiyo maana uandishi wa habari unatajwa na magwiji wa taaluma hii kuwa ni ‘noble profession’.

Naandika maneno haya huku nikitambua kwa dhati kwamba, mara kadhaa wanahabari wa hapa nchini na kwingineko duniani tumekuwa mstari wa mbele katika kukiuka msingi na muongozo huo muhimu kitaaluma kwa kujua au kutojua, kwa kukusudia ama kwa bahati mbaya.

Pamoja na mapungufu hayo ya kibinadamu katika taaluma hii ambayo siku zote nitabakia kuwa mwanafunzi wake, uandishi wa habari unaendelea na utaendelea kubakia kuwa mhimili wa nne wa dola baada ya serikali, Bunge na Mahakama.

Iwapo hivyo ndivyo, uandishi wa habari ni taaluma ambayo inao wajibu wa kusimama juu ya taaluma zote nyingine ambazo aghalab kwa nafasi zao hakuna hata moja ambayo imepata kuchukua taswira ya mhimili kama ilivyo kwa uandishi wa habari.

Kwa sababu hiyo basi, kama ilivyo kwa mihimili mingine ya dola, taaluma hii inao wajibu wa kukubali changamoto zinazoelekezwa kwake na wakati mwingine kuchukua maamuzi ambayo yanaipa mamlaka na taswira halisi ya kuonekana kuwa ni mhimili unaojitegemea kifikra, kimatendo na hata kimaadili.

Nimelazimika kuyasema yote haya katika utangulizi wa makala yangu ya leo kutokana na kile ambacho kilitokea wiki iliyopita baada ya safu hii kuwa na makala iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: “Namuogopa Abdulrahman Kinana”.

Makala ile ilibeba ujumbe rahisi kabisa. Kwanza mbali ya kueleza kwa sehemu tu kuhusu wasifu wa Kinana kwa mtazamo wa mwandishi wa safu hii ambaye ni mimi mwenyewe, ilieleza kwa muhtasari tu sababu ambazo zilimfanya Rais Jakaya Kikwete hatimaye akubali yaishe kwa kumfanya mwanasiasa huyo abebeshwe jukumu la kuwa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kama hiyo haitoshi, makala ile ilieleza kwa maneno yaliyo wazi kabisa kwamba, CCM ilikuwa ikichungulia kaburi na kimsingi mwenendo wa mambo katika kipindi cha miaka michache tu iliyopita hadi sasa ilikuwa ikichukua mwelekeo wa wazi wa kupoteza madaraka ya dola.

Ni kwa bahati mbaya sana kwamba, mashabiki wa vyama vya upinzani ambao siku zote wamekuwa hodari kushangilia hoja zetu za kuikosoa serikali au kuisuta CCM na viongozi wake kwa kuwaangusha Watanzania katika maeneo kadha wa kadha walipatwa na hasira kali waliposoma makala ile na kuona ikiwa na harufu ya kumsifu au kueleza uwezo wa kimikakati, kiutawala, kisiasa na kiintelijensia aliokuwa nao Kinana na pengine safu ya uongozi mpya wa chama hicho tawala iliyoundwa wiki mbili zilizopita.

Kwa sababu tu ya kulemewa kwao na ulevi wa chuki walizoijengea CCM na viongozi wake pasipo hata kuangalia muktadha wa makala ile, wadakuzi hao wa mambo kupitia katika mitandao ya intaneti, majukwaa ya jamii, ujumbe wa maandishi na kwenye simu yangu ya kiganjani na hata kwa njia ya ana kwa ana wakanisuta na kunitukana kila aina ya matusi ili kukidhi matakwa yao.

Lile kosa la wanasiasa na wapambe wao kukosa ustahimilivu ambalo tumekuwa tukiwahusisha nalo watawala, likachukua sura na mwelekeo tofauti.

Siri zikafichuka kwamba ndani ya mioyo ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, wafuasi na mashabiki wao kulikuwa na hulka za hatari za udikteta ambazo ama zinalingana na zile walizonazo baadhi ya wana CCM na viongozi kadha wa kadha wa kiserikali.

Niseme wazi na kwa kujiamini kabisa kwamba, sikutishwa wala kubabaishwa na matukio hayo ambayo kwangu hayakuwa mageni hata kidogo kwani yalifanya kile ambacho nimekuwa nikikabiliana nacho tangu mwaka 1993 wakati nilipoanza kushiriki kikamilifu kuandika makala katika magazeti mbalimbali nchini na wakati mwingine kutoa maoni na mawazo yangu kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa.

Haraka haraka hoja za kishabiki zilizokosa weledi ambazo zilikuwa zikivurumishwa na manazi hao wa kisiasa zilinikumbusha ujasiri niliokuwa nao mwaka 1995 wakati niliposimama imara kupinga mhemko wa kitaifa wa “Homa ya Augustine Mrema” ambayo ililitikisa taifa kwa kiwango cha kumchanganya akili Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Nilikuwa na ujasiri aliokuwa nao Jenerali Ulimwengu wa kumpinga Mrema katika maandishi na hata katika majukwaa ya mijadala.

Bado nakumbuka vyema namna nilivyosafiri kwa daladala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilikokuwa nikisoma hadi Kariakoo zilizokuwa ofisi za NCCR Mageuzi na nikapata fursa ya kuwafikia Mabere Marando na Ndimara Tegambwage nikiwaomba watafakari upya uamuzi wao wa kumpa Mrema dhamana ya kuongoza harakati ghali za mageuzi katika taifa hili.

Makala nilizoandika katika magazeti ya Rai, Mtanzania, Wakati Ni Huu, Nipashe na kwingineko katika kipindi hicho cha 1995 na 1996 ambazo aghalab zilikuwa zikiwaasa Watanzania kupima mambo kwa kina badala ya kutukuza na kuendekeza ushabiki wa kisiasa ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho nilikuwa nikikisimamia na nimeendelea kukisimamia siku zote.

Haikupita hata miaka miwili kabla ukweli wa kile nilichokuwa nikikizungumza na kukitetea kwa njia ya maandishi kuthibitika.

Mrema alifanya kile nilichokiona mapema, akawaangusha aliowaongoza na kuwaporomosha wale waliofikia hatua ya kumuabudu kwa kiwango cha kumuona mkombozi wao wa kisiasa.

Kama ilivyokuwa kwa Mrema mwaka huo huo wa 1995, nilikuwa miongoni mwa wanahabari ambao tulimpinga kwa hoja Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika harakati zake za kulazimisha aliyekuwa mgombea wake, Benjamin Mkapa, ateuliwe na kuwa mgombea wa urais wa CCM.

Katika hili, sikukubaliana na kile ambacho Jenerali Ulimwengu na wenzake walikitetea. Ingawa nilikuwa mpinzani mkubwa wa Mrema, sikufurahishwa hata kidogo na uamuzi wa Baba wa Taifa kupandikiza hulka za kidikteta katika kuchakachua mchakato wa urais kupitia katika tanuri la chama hicho tawala.

Kilichotokea miaka 10 baada ya Mkapa kustaafu urais mwaka 2005 ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho baadhi yetu, japo hatuna majina makubwa tulikiona mapema.Rais huyo pamoja na kuonekana kwamba alikijengea heshima kiti cha urais na kuinunua harufu ya maendeleo ya kiuchumi, alifisha hata ndoto za ‘mentor’ wake Mwalimu Nyerere. Hili linahitaji mjadala unaojitegemea.

Sikuishia hapo, mwaka 2005 wakati taifa na fani nzima ya habari ikiimba wimbo wa Kikwete, Kikwete Kikwete katika misingi ya ushabiki unaofanana na ule unaotokea leo, nilikuwa miongoni mwa waandishi wachache ambao tulikataa kuimba wimbo huo huku tukitoa tahadhari za waziwazi kuhusu hatari ambayo ilikuwa ikilinyemelea taifa.

Ingawa wakati huo nilikuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili ambalo mmoja wa wakurugenzi wake alikuwa Rostam Aziz aliyekuwa katikati ya kitovu cha kampeni za Kikwete, nilikataa kuwa bendera fuata upepo na nikaandika mada kadha wa kadha kuhoji kuhusu uwezo wa mwanasiasa huyo kupewa dhamana ya kuongoza nchi.

Ushahidi wa kile nilichoandika kuhusu hilo uko wazi kabisa. Nilitenda na kutoa msimamo tofauti kabisa na ule waliokuwa nao baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wa zama hizo kuhusu nafasi ya Kikwete katika kuliongoza taifa hili.

Hata yeye mwenyewe alipotangaza uamuzi wa kugombea urais kule Chalinze nilikuwa miongoni mwa wahariri na wanahabari ambao tulikwenda na kumuuliza maswali magumu kuhusu kugombea kwake.

Alipoteuliwa na chama chake kuwa mgombea kama ilivyotarajiwa na wengi, nilitafuta fursa na nikafanya naye mahojiano nyumbani kwake Dodoma nikiwa nimeongozana na mwanahabari mwenzangu, Nyaronyo Kicheere, aliyekuwa Mhariri wa Habari wa gazeti dada la The Citizen on Sunday.

Niliendelea na msimamo ule juu ya Kikwete kabla na baada ya kuteuliwa kwake kuwa mgombea urais. Waandishi na wahariri waliokuwa pale ni mashahidi wazuri kwamba, msimamo wangu huo ulipata kusababisha Rostam afikie hatua ya kueleza waziwazi kukerwa nao.

Mara kadhaa aliniita nyumbani kwake akijaribu kunishawishi na kuniaminisha kwamba Kikwete alikuwa ni mwanasiasa hodari na anayeweza kuliongoza taifa hili pengine kuliko mwingine yeyote.

Kilichotokea baada ya hapo kila mtu anakijua, Kikwete alishinda kwa kishindo na baadhi yetu ambao tulionekana kuwa vimbelembele kuhoji uwezo wake tukasutwa kweli kweli kwa kiwango cha baadhi ya wanahabari wenzetu kutuona wendawazimu.

Kwa sababu ya kuendekeza hulka za kishabiki, wanahabari tulishindwa kumuandaa Kikwete kuwa rais bora, tulimnyima fursa ya kujipanga kifikra na kifalsafa na tukaiacha ajenda ya urais iandaliwe kimkakati na kiintelijensia zaidi. Hiki tunachokiona leo ni matokeo ya kuendekeza ushabiki wa namna hiyo.

Ni jambo la bahati mbaya kwamba kile kilichotokea mwaka 1995 na baadaye mwaka 2005 bado kinaonekana kutofundisha Watanzania. Hulka za kinazi na kishabiki katika masuala ya msingi bado zinaendelea kutafuna vichwa vyetu.

Taifa zima linaimba wimbo mmoja tu, Slaa, Slaa, Slaa. Halitaki kusikia lolote. Ukimgusa Dk. Slaa tena kwa hoja za kumtahadharisha, kumuonya au hata kwa minajiri ya kumfanya ajiandae kukabiliana na kimbunga kama hiki cha Kinana, mashabiki wake wanalipuka kwa jazba na kwa hamaki kubwa.

Ukithubutu kuikosoa CHADEMA au kumgusa yeyote miongoni mwa viongozi wake kama nilivyofanya miaka mitatu au minne iliyopita wakati nilipopinga uamuzi wa Zitto Kabwe kugombea uenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa sababu muda wake ulikuwa bado, idadi ya matusi utakayovurumishiwa kama ni mtu ambaye una moyo mwepesi unaweza ukaacha kuandika.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wiki iliyopita wakati nilipowaonya wapinzani kukaa chonjo na Kinana kwani kimbunga ambacho alikuwa akielekeza kukipuliza kuelekea upande wa kambi ya upinzani kinaweza kusababisha upepo unaovuma sasa kubadili njia.

Sitaki kujifanya mimi ni nabii wa siasa za Tanzania. Hata hivyo bado naendelea kuamini na kusisitiza kwamba, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana si mtu mwepesi, si mwanasiasa wa kumbeza wala kumpuuza.

Kama CHADEMA na mashabiki wanataka kupima kina cha maji kwa sababu tu ya ulevi wa fikra, basi wanao uhuru wa kufanya hivyo. Tusubiri fainali 2015. Huko ndiko tuendako.
Mimi ndiyo maana niliachaga hata kusoma makala zako,nilijua umenunuliwa na lowasa na leo kina Rostam wameshakupata kwa bei yako cheap...kajenge kibanda na hiyo hela yako ya kuhongwa na Lowasa.
 
Ni aibu, tena aibu kubwa kwa mwanaume kuthubutu kuzungumzia mahusiano ya kingono ya mwanaume mwenzako. Hilo sio tusi bali ni ukweli halisi na mnapaswa kuutambua. Ni bahati mbaya sana kwamba baadhi yenu hamna hoja ya kuandika ama kujadili juu ya Dr. Slaa zaidi ya mambo ya mahusiano yake ya kingono ambayo hayatusaidii chochote kama Taifa.

Yaani kiongozi wa kitaifa ambaye watanzania wanamtegemea kuwa rais katelekeza familia mke wake pamoja na watoto na kesi ipo mahakamani unataka kutufunga mdomo tusijadili uadilifu wa kiongozi wa taifa kisa wewe umesema ni aibu.

Watu hawajamsingizia Dr Slaa yote kayafanya nyie Pro-Chadema JF ndio mnatakiwa mkae na Dr Slaa na mwambieni ni kitendo cha aibu alichokifanya kiongozi ni kioo cha jamii.

Hakuna aibu kumjadili kiongozi ambaye hana maadili.
 
POMPO mimi simjui Kinana, ndiyo maana nataka watu watupe facts za kwanini Kinana si Kimbunga. Huyu mtu amekuwa meneja wa kampeni za CCM tangu mwaka 1995, kwa hiyo anajua propaganda za kisiasa zote, ameshakabiliana na akina Mrema, Lipumba, Mbowe na Slaa. Anawajua inn and out. Ni kwa vipi humuoni kama ni tishio katika anga za kisiasa? Ni nani wa upinzania mwenye uzoefu mkubwa kama wa Kinana? Hapa mimi nafikiri upinzani tujipange tu, na si kubeza uwezo wa Kinana. Namna pekee ya kummaliza Kinana labda ni kuzihuisha hizo propaganda za kwamba ni mwizi. Labda hiyo itasaidia kumpunguzia nguvu, otherwise, ni lazima tukubali ukweli kwamba Kinana ni tishio.

Lakini kumbuka kinana huyo huyo ndiye alishusha ushindi wa Kikwete kutoka 80% (mwaka 2005) hadi 61% (mwaka 2010). Na kinana huyo ndiyo alisababisha majimbo zaidi ya 15 ya CCM kupokwa na CHADEMA mwaka 2010. Sasa sijui mnaangalia tu past history yake tu au inakuwaje..
 
tarehe moja disemba anaanza kazi pale kijiweni new habari huyo ni mtu wa lowasa na anapelekwa pale kwa mkakati maalumu,
 
TUMBIRI Ni kwanini unamtaka Ansbert Ngurumo ndiye atoe kauli yake juu ya mwenendo wa Kibanda badala wewe mwenyewe utoe? Kwani wewe huna uwezo wa kujisimamia mpaka usimamiwe.

Mkuu WABHEJASANA,
Hivi mtu ukitaka mtu fulani atoe kauli yake juu ya jambo fulani maana yake hawezi kujisimamia? Na tunavyotaka kauli ya Rais Kikwete juu ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa maana yake watu wote tumeshindwa kujisimamia? Jipange vizuri Boss wangu.
 
Alafu heading ya hii thread haijakaa vizuri. Mkuu Kimbunga eti wewe ndiye Kinana? Naona heading ya thread inasomeka "Kinana ni Kimbunga"!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom