Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Propaganda hizo za Chukua Chako Mapema mbona mwenye mke alishindwa mahakaman,,,km kawaida mara Kinana sio raia,,Ulimwengu sio raia,,Mkapa sio raia..Dr.Salim sio raia cha ajabu wote hawa mliwapa uongoz,,,Kwa propaganda mnaweza lkn sio Kumkomboa Mtanzania wa hali ya chini,,,Kiama chenu 2015!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Propaganda hizo za Chukua Chako Mapema mbona mwenye mke alishindwa mahakaman,,,km kawaida mara Kinana sio raia,,Ulimwengu sio raia,,Mkapa sio raia..Dr.Salim sio raia cha ajabu wote hawa mliwapa uongoz,,,Kwa propaganda mnaweza lkn sio Kumkomboa Mtanzania wa hali ya chini,,,Kiama chenu 2015!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
CCM imeharibu sana nchi, mwandishi kama huyu alipaswa kuwa kaona mengi, katest mengi, kasoma mengine mengi, anajua mirengo ya kisiasa duniani na nchini, anafahau mengi kwa ujumla.Ila hana sana tofauti na technicians wa lab, wao watakaaa miaka mingi ili wasaidie wasomi wajao waje na kujifunza haraka kabla ya ku assume responsibilites.

HUyu naye inabidi waje watu wenye upeo na flexibility ay kujifunza mambo kwa uhakika, na haraka kabla y akuchukua majukumu.Huyu jamaa hana principals anazozisimamia zaidi ya kufikiri kuwa kwenda upande fulani kunathibitisha kuwa ni mwandhishi asiye na ushabiki.Wakati anamshabikia Kinana hadi kumwita Kimbunga.NI mwandhis ambaye JK akimpa ukuu wa wilaya leo hawezi jiuliza mara mbili kabla ya kuukata ingawa ni wazi ataukubali na kuanza jichekesha kaumsifia maisha yake yote kama magamba wengine.

Kinana kama kashindwa impress Arusha ataweza mkoa gani tena zaidi ya ktk kundi la wana CCM?Kinana alisaidia na propaganda za enzi ya mwinyi ,kwa mianajili ya dini na ujinga mwingine usiohusika na weledi.Na amekuwa kama akina JK kupata watu wanaoyaona makosa yao kama tactical move na mwishowe hata wahusika kuamini kuwa walifanya kitu kizuri.
 
ADA YA MJA HUNENA.......
UTANGULIZI
Nimeisoma makala nyingine ya Kibanda yenye kichwa kisemacho; “KINANA NI KIMBUNGA” baada ya ile ya kwanza iliyojinadi kwa kichwa kisemacho; “NAMWOGOPA KINANA”. Mwandishi huyu ni hodari sana katika masuala yenye kuhitaji kufanyiwa uchambuzi. Ni msomi mbobezi katika fani yake, mwenye kutenda kazi iboreshwayo na kipaji cha kipekee cha kuzaliwa. Tusisubiri Mtanzania mwenzetu huyu afariki ndipo tummwagie sifa zake anazostahili. Tufanye hivyo sasa ili apate moyo zaidi wa kuendelea kujitolea kutufumbua na kutufundisha sisi tulio-tayari na wenye hamu ya kujiimarisha zaidi kifikra, ki-upeo na kimtazamo. Kwa sehemu kubwa, Kibanda ni darubini muhimu sana kwenye tasnia yake na ndani ya kizazi hiki. Namfananisha na kauli ya Kibiblia isemayo kuhusu SAUTI YA MTU ALIAYE NYIKANI kwa wale wenye msingi wa imani inayokubaliana na falsafa hiyo. Ni rasilimali muhimu kujihusisha nayo kwa majadiliano ya kina katika masuala ya kijamii. Rasilimali bora inapokuwa ng’ambo ya korongo, kuingia gharama ili uitumie kwa manufaa mapana zaidi ni jambo la busara. Kwa mantiki ya kawaida, huwezi kuichukia darubuni kwa kuwa imekusogezea taswira karibu zaidi, nawe ukapata kuona mambo kwa kiwango kilichoboreka ambacho hukipendi. Haya ni matokeo ya kujijenga na kujizoeza kukataa kuona details katika taswira, bali silhouette ili kukwepa kujishughulisha na uhalisia ambao daima ni mchakato unaochosha. Tabia hii ya kukwepa ukweli ni nyenzo ya kufanikisha kuishi kibwetekaji kama mbwekaji abwekaye bandani mwake.

Mtembea kwa miguu mwituni, asikiapo sauti ya kipekee ikitolewa na ndege kichakani au mtini, kwa vyovyote vile fahamu zake zitamwamuru kuchukua hadhari ingawa yeye mwenyewe haielewi lugha ya ndege yule. Ataubadili mwendo wake, kuyafungua masikio zaidi na macho pima, huku moyo ukimdunda kwa kasi iliyoongezeka! Kibanda sio ndege ambaye hata hivyo wenye hekima hawampuuzi, bali ni mtaalamu anayejitolea kuuelimisha umma wa leo ambao miongoni mwao, wengi hutumia masikio kama nyenzo ya kutundika hereni za kujipamba na kwa kusikiliza wanachokiamini. Kibanda endelea......, wa kukusikiliza atakusikiliza na kukuelewa na asiyekuelewa aongeze bidii kubishana nawe ili kuficha umbumbumbu wake. Huyu atafanana na aliyeuficha mwili wake nyuma ya kiganja cha mkono wake kwa kuamini kuwa ni kichaka! Achana na MADIKTETA!

Kibanda umetabiri masikio ya kufa, na hakuna dawa kwani historia imekwisha-waamulia mwelekeo wao. Wamejaliwa kuwa na muda wa kufanya maigizo yao kwa kujitolea na sasa wakipenda, watangulize makoti wakayatundike kwenye geti la Ikulu, baadaye tuyatumie kudeki viwanja vya Ikulu! Wanaukataa ukweli sio kwa kuwa hawaufahamu bali ni kwa kujifurahisha pasipo matumaini ya dhati. Wanaonesha uwepo wao kama samaki wanavyorukaruka majini. Kiashiria cha kuchoka kwao ki-hoja ni kuporomosha matusi na ukishaona hivyo ujue wamelemewa. Huwa nafurahi sana wanapotukana kwani hunidhibitishia kwamba wameishiwa na hoja, wakati waungwana tukipambanisha hoja kwa hoja na umma unaendelea kutupima kwa upeo na sio kwa kiwango kikubwa cha uongo na jazba. Uongo na jazba sio matakwa na sharti la uongozi bora bali ni nyenzo na rufani ya waishiwa (Getting a more mileage before taking a crush landing). A crush is just a crush, no matter sooner or later.

Kama sote tujuavyo, wanasiasa hawa wanaojitambulisha kwa kibandiko cha herufi za rangi nyekundu kuashiria umwagaji damu cha M4C yaani MASTERS FOR CRIMINALITY, huwashawishi wafuasi wao kupita wakiandamana kwa niaba ya magari juu ya lami ya CCM huku wakipoteza muda mwingi ambao ungefaa zaidi kutumika katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao kwa hoja zisizohitimishwa kwa tija bali damu na maumivu ya waghilibiwa wasio hatia. Maandamano yao huishia kwenye viwanja vya Serikali ya CCM, ili kukoleza porojo zao za ghilba wakipaaza sauti zao kwa teknolojia inayoendeshwa kwa nishati iliyopatikana kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo agenda yao inayosisitizwa ni kwamba CCM haijafanya kitu! Hapa ni kwamba wanazungumza kiswahili tu na sio kweli za msingi. They speak good Swahili but not the facts!

Kibanda songa mbele! Umesema; “Kama CHADEMA na mashabiki wanataka kupima kina cha maji kwa sababu tu ya ulevi wa fikra, basi wanao uhuru wa kufanya hivyo. Tusubiri fainali 2015. Huko ndiko tuendako”.

Kinana ni kiongozi mahiri, mtulivu, mbunifu na mwenye kuzungumza kwa hoja na MBOBEZI WA SIASA ZA KUONGOZA. Namwambia Kinana akaze buti aongoze mapambano nasi wanaCCM tupo pamoja naye angani, majini na nchi kavu! WanaCCM tunasema; hatukubali kubeba dhambi ya kuikabidhi nchi yetu kwa madikteta ambao hukerwa hata na tofauti ya kimawazo. Uporaji wa kikaya uliotinga mahakamani ni kiashiria tosha kwamba wakipata fursa hawaachi kitu!

CCM hivi sasa inajipanga kuongoza Awamu ya Tano kifikra na kifalsafa kwa kutumia mikakati na intelijensia ya ndani katika kufanikisha azma hiyo. Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo. Pamoja na mambo mengine, CCM ni KIINI cha kudumu cha IMANI NA MATUMAINI YA WATANZANIA.
 
Duh kinachofuarahisha ni pale CCM wanapofikiri sisi ni mandondocha safari hii amini usiamini Usalama wa Taifa hawatapandikiza mtu tukawaacha salama Ne ne ne
 
ADA YA MJA HUNENA.......
UTANGULIZI
Nimeisoma makala nyingine ya Kibanda yenye kichwa kisemacho; "KINANA NI KIMBUNGA" baada ya ile ya kwanza iliyojinadi kwa kichwa kisemacho; "NAMWOGOPA KINANA".

CCM hivi sasa inajipanga kuongoza Awamu ya Tano kifikra na kifalsafa kwa kutumia mikakati na intelijensia ya ndani katika kufanikisha azma hiyo. Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo. Pamoja na mambo mengine, CCM ni KIINI cha kudumu cha IMANI NA MATUMAINI YA WATANZANIA.

Sasa wewe LUCAS KISIMI mbona katika makala yako na wewe umeishia kutukana tu kama hao unaowatuhumu CDM? Sasa hapo MJINGA ni nani? Yule Kichaa aliyechukua nguo zako au Wewe uliyeamua kumfukuza huyo kichaa ukiwa UCHI wa mnyama?

Think BIG dude!
 
Kibanda anatafuta njia ya kurudi NEW HABARI CORPORATION,I PRESSUME,leo tarehe 5 DESEMBA MAKALA HAJAANDIKA TENA YA KUMWOGOPA KINANA.looh mwanaume wamwogopa mwenzio na wakiri hadharani?yaani KINANA anamtisha KIBANDA kuliko JK EL R AZIZI,wanaume suruali ndo hao!
 
Hovyo sana
Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda baada ya wiki iliyopita kuibuka na Makala isemayo NAMUOGOPA KINANA iliyokuwa ikimwagia kila aina ya Sifa, leo hii ameibuka na makala nyingine ya kumsifu Katibu mkuu huyo wa CCM huku akiponda mashabiki na wanachama wa CHADEMA kwamba ni walevi wa Fikra na anatabiri Kimbunga cha Kinana kwa CHADEMA kitakuwa 2015....Endelea.........


YAKO mambo ya msingi katika maisha ya kitaaluma katika fani zote za kielimu ambayo mtu yeyote anayetambua na kujali vyema wajibu wake anapaswa kuyasimamia na kuyalinda hata kama atafanya hivyo kwa gharama ya kupoteza maisha, kuchukiwa, kudharauliwa au kupuuzwa.

Moja ya mambo ya namna hiyo ni miiko ya kitaaluma ambayo aghalab huongoza na kujenga misingi ya uwepo na kustawi kwa kila fani iwe ni sheria, elimu, uaskari, uhandisi na hata ukachero.

Uandishi wa habari ni moja ya taaluma ambazo zina miiko na maadili yake. Zaidi ya hayo uandishi wa habari na waandishi wa habari wanaishi kwa kufuata na kuzingatia miongozo yao ya kikazi na kitaaluma.

‘Ukweli' ni moja ya misingi mikuu ya uandishi wa habari. Huu unaweza ukawa msingi mama katika taaluma hii adhimu. Ni kwa kuzingatia hilo ndiyo maana uandishi wa habari unatajwa na magwiji wa taaluma hii kuwa ni ‘noble profession'.

Naandika maneno haya huku nikitambua kwa dhati kwamba, mara kadhaa wanahabari wa hapa nchini na kwingineko duniani tumekuwa mstari wa mbele katika kukiuka msingi na muongozo huo muhimu kitaaluma kwa kujua au kutojua, kwa kukusudia ama kwa bahati mbaya.

Pamoja na mapungufu hayo ya kibinadamu katika taaluma hii ambayo siku zote nitabakia kuwa mwanafunzi wake, uandishi wa habari unaendelea na utaendelea kubakia kuwa mhimili wa nne wa dola baada ya serikali, Bunge na Mahakama.

Iwapo hivyo ndivyo, uandishi wa habari ni taaluma ambayo inao wajibu wa kusimama juu ya taaluma zote nyingine ambazo aghalab kwa nafasi zao hakuna hata moja ambayo imepata kuchukua taswira ya mhimili kama ilivyo kwa uandishi wa habari.

Kwa sababu hiyo basi, kama ilivyo kwa mihimili mingine ya dola, taaluma hii inao wajibu wa kukubali changamoto zinazoelekezwa kwake na wakati mwingine kuchukua maamuzi ambayo yanaipa mamlaka na taswira halisi ya kuonekana kuwa ni mhimili unaojitegemea kifikra, kimatendo na hata kimaadili.

Nimelazimika kuyasema yote haya katika utangulizi wa makala yangu ya leo kutokana na kile ambacho kilitokea wiki iliyopita baada ya safu hii kuwa na makala iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: "Namuogopa Abdulrahman Kinana".

Makala ile ilibeba ujumbe rahisi kabisa. Kwanza mbali ya kueleza kwa sehemu tu kuhusu wasifu wa Kinana kwa mtazamo wa mwandishi wa safu hii ambaye ni mimi mwenyewe, ilieleza kwa muhtasari tu sababu ambazo zilimfanya Rais Jakaya Kikwete hatimaye akubali yaishe kwa kumfanya mwanasiasa huyo abebeshwe jukumu la kuwa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kama hiyo haitoshi, makala ile ilieleza kwa maneno yaliyo wazi kabisa kwamba, CCM ilikuwa ikichungulia kaburi na kimsingi mwenendo wa mambo katika kipindi cha miaka michache tu iliyopita hadi sasa ilikuwa ikichukua mwelekeo wa wazi wa kupoteza madaraka ya dola.

Ni kwa bahati mbaya sana kwamba, mashabiki wa vyama vya upinzani ambao siku zote wamekuwa hodari kushangilia hoja zetu za kuikosoa serikali au kuisuta CCM na viongozi wake kwa kuwaangusha Watanzania katika maeneo kadha wa kadha walipatwa na hasira kali waliposoma makala ile na kuona ikiwa na harufu ya kumsifu au kueleza uwezo wa kimikakati, kiutawala, kisiasa na kiintelijensia aliokuwa nao Kinana na pengine safu ya uongozi mpya wa chama hicho tawala iliyoundwa wiki mbili zilizopita.

Kwa sababu tu ya kulemewa kwao na ulevi wa chuki walizoijengea CCM na viongozi wake pasipo hata kuangalia muktadha wa makala ile, wadakuzi hao wa mambo kupitia katika mitandao ya intaneti, majukwaa ya jamii, ujumbe wa maandishi na kwenye simu yangu ya kiganjani na hata kwa njia ya ana kwa ana wakanisuta na kunitukana kila aina ya matusi ili kukidhi matakwa yao.

Lile kosa la wanasiasa na wapambe wao kukosa ustahimilivu ambalo tumekuwa tukiwahusisha nalo watawala, likachukua sura na mwelekeo tofauti.

Siri zikafichuka kwamba ndani ya mioyo ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, wafuasi na mashabiki wao kulikuwa na hulka za hatari za udikteta ambazo ama zinalingana na zile walizonazo baadhi ya wana CCM na viongozi kadha wa kadha wa kiserikali.

Niseme wazi na kwa kujiamini kabisa kwamba, sikutishwa wala kubabaishwa na matukio hayo ambayo kwangu hayakuwa mageni hata kidogo kwani yalifanya kile ambacho nimekuwa nikikabiliana nacho tangu mwaka 1993 wakati nilipoanza kushiriki kikamilifu kuandika makala katika magazeti mbalimbali nchini na wakati mwingine kutoa maoni na mawazo yangu kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa.

Haraka haraka hoja za kishabiki zilizokosa weledi ambazo zilikuwa zikivurumishwa na manazi hao wa kisiasa zilinikumbusha ujasiri niliokuwa nao mwaka 1995 wakati niliposimama imara kupinga mhemko wa kitaifa wa "Homa ya Augustine Mrema" ambayo ililitikisa taifa kwa kiwango cha kumchanganya akili Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Nilikuwa na ujasiri aliokuwa nao Jenerali Ulimwengu wa kumpinga Mrema katika maandishi na hata katika majukwaa ya mijadala.

Bado nakumbuka vyema namna nilivyosafiri kwa daladala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilikokuwa nikisoma hadi Kariakoo zilizokuwa ofisi za NCCR Mageuzi na nikapata fursa ya kuwafikia Mabere Marando na Ndimara Tegambwage nikiwaomba watafakari upya uamuzi wao wa kumpa Mrema dhamana ya kuongoza harakati ghali za mageuzi katika taifa hili.

Makala nilizoandika katika magazeti ya Rai, Mtanzania, Wakati Ni Huu, Nipashe na kwingineko katika kipindi hicho cha 1995 na 1996 ambazo aghalab zilikuwa zikiwaasa Watanzania kupima mambo kwa kina badala ya kutukuza na kuendekeza ushabiki wa kisiasa ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho nilikuwa nikikisimamia na nimeendelea kukisimamia siku zote.

Haikupita hata miaka miwili kabla ukweli wa kile nilichokuwa nikikizungumza na kukitetea kwa njia ya maandishi kuthibitika.

Mrema alifanya kile nilichokiona mapema, akawaangusha aliowaongoza na kuwaporomosha wale waliofikia hatua ya kumuabudu kwa kiwango cha kumuona mkombozi wao wa kisiasa.

Kama ilivyokuwa kwa Mrema mwaka huo huo wa 1995, nilikuwa miongoni mwa wanahabari ambao tulimpinga kwa hoja Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika harakati zake za kulazimisha aliyekuwa mgombea wake, Benjamin Mkapa, ateuliwe na kuwa mgombea wa urais wa CCM.

Katika hili, sikukubaliana na kile ambacho Jenerali Ulimwengu na wenzake walikitetea. Ingawa nilikuwa mpinzani mkubwa wa Mrema, sikufurahishwa hata kidogo na uamuzi wa Baba wa Taifa kupandikiza hulka za kidikteta katika kuchakachua mchakato wa urais kupitia katika tanuri la chama hicho tawala.

Kilichotokea miaka 10 baada ya Mkapa kustaafu urais mwaka 2005 ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho baadhi yetu, japo hatuna majina makubwa tulikiona mapema.Rais huyo pamoja na kuonekana kwamba alikijengea heshima kiti cha urais na kuinunua harufu ya maendeleo ya kiuchumi, alifisha hata ndoto za ‘mentor' wake Mwalimu Nyerere. Hili linahitaji mjadala unaojitegemea.

Sikuishia hapo, mwaka 2005 wakati taifa na fani nzima ya habari ikiimba wimbo wa Kikwete, Kikwete Kikwete katika misingi ya ushabiki unaofanana na ule unaotokea leo, nilikuwa miongoni mwa waandishi wachache ambao tulikataa kuimba wimbo huo huku tukitoa tahadhari za waziwazi kuhusu hatari ambayo ilikuwa ikilinyemelea taifa.

Ingawa wakati huo nilikuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili ambalo mmoja wa wakurugenzi wake alikuwa Rostam Aziz aliyekuwa katikati ya kitovu cha kampeni za Kikwete, nilikataa kuwa bendera fuata upepo na nikaandika mada kadha wa kadha kuhoji kuhusu uwezo wa mwanasiasa huyo kupewa dhamana ya kuongoza nchi.

Ushahidi wa kile nilichoandika kuhusu hilo uko wazi kabisa. Nilitenda na kutoa msimamo tofauti kabisa na ule waliokuwa nao baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wa zama hizo kuhusu nafasi ya Kikwete katika kuliongoza taifa hili.

Hata yeye mwenyewe alipotangaza uamuzi wa kugombea urais kule Chalinze nilikuwa miongoni mwa wahariri na wanahabari ambao tulikwenda na kumuuliza maswali magumu kuhusu kugombea kwake.

Alipoteuliwa na chama chake kuwa mgombea kama ilivyotarajiwa na wengi, nilitafuta fursa na nikafanya naye mahojiano nyumbani kwake Dodoma nikiwa nimeongozana na mwanahabari mwenzangu, Nyaronyo Kicheere, aliyekuwa Mhariri wa Habari wa gazeti dada la The Citizen on Sunday.

Niliendelea na msimamo ule juu ya Kikwete kabla na baada ya kuteuliwa kwake kuwa mgombea urais. Waandishi na wahariri waliokuwa pale ni mashahidi wazuri kwamba, msimamo wangu huo ulipata kusababisha Rostam afikie hatua ya kueleza waziwazi kukerwa nao.

Mara kadhaa aliniita nyumbani kwake akijaribu kunishawishi na kuniaminisha kwamba Kikwete alikuwa ni mwanasiasa hodari na anayeweza kuliongoza taifa hili pengine kuliko mwingine yeyote.

Kilichotokea baada ya hapo kila mtu anakijua, Kikwete alishinda kwa kishindo na baadhi yetu ambao tulionekana kuwa vimbelembele kuhoji uwezo wake tukasutwa kweli kweli kwa kiwango cha baadhi ya wanahabari wenzetu kutuona wendawazimu.

Kwa sababu ya kuendekeza hulka za kishabiki, wanahabari tulishindwa kumuandaa Kikwete kuwa rais bora, tulimnyima fursa ya kujipanga kifikra na kifalsafa na tukaiacha ajenda ya urais iandaliwe kimkakati na kiintelijensia zaidi. Hiki tunachokiona leo ni matokeo ya kuendekeza ushabiki wa namna hiyo.

Ni jambo la bahati mbaya kwamba kile kilichotokea mwaka 1995 na baadaye mwaka 2005 bado kinaonekana kutofundisha Watanzania. Hulka za kinazi na kishabiki katika masuala ya msingi bado zinaendelea kutafuna vichwa vyetu.

Taifa zima linaimba wimbo mmoja tu, Slaa, Slaa, Slaa. Halitaki kusikia lolote. Ukimgusa Dk. Slaa tena kwa hoja za kumtahadharisha, kumuonya au hata kwa minajiri ya kumfanya ajiandae kukabiliana na kimbunga kama hiki cha Kinana, mashabiki wake wanalipuka kwa jazba na kwa hamaki kubwa.

Ukithubutu kuikosoa CHADEMA au kumgusa yeyote miongoni mwa viongozi wake kama nilivyofanya miaka mitatu au minne iliyopita wakati nilipopinga uamuzi wa Zitto Kabwe kugombea uenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa sababu muda wake ulikuwa bado, idadi ya matusi utakayovurumishiwa kama ni mtu ambaye una moyo mwepesi unaweza ukaacha kuandika.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wiki iliyopita wakati nilipowaonya wapinzani kukaa chonjo na Kinana kwani kimbunga ambacho alikuwa akielekeza kukipuliza kuelekea upande wa kambi ya upinzani kinaweza kusababisha upepo unaovuma sasa kubadili njia.

Sitaki kujifanya mimi ni nabii wa siasa za Tanzania. Hata hivyo bado naendelea kuamini na kusisitiza kwamba, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana si mtu mwepesi, si mwanasiasa wa kumbeza wala kumpuuza.

Kama CHADEMA na mashabiki wanataka kupima kina cha maji kwa sababu tu ya ulevi wa fikra, basi wanao uhuru wa kufanya hivyo. Tusubiri fainali 2015. Huko ndiko tuendako.
 
Back
Top Bottom