Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Mwisho Mkuu Mwita Maranya,miongoni mwa watu ambao huwa wanaheshimu hoja zao humu ndani Jamvini ni mimi,lakini leo hii nashangaa umekua na jazba sana na Kibanda,au kwa sababu ameigusa CHADEMA?,mbona siku zote za Nyuma ulikuwa mfuasi mkuu a Kibanda hata kama alikuwa ameandika Utumbo katika kuisifia CHADEMA ama kiongozi yoyote wa CHADEMA,hizi hasira zako za leo zinatoka wapi Mkuu?

Ndugu yangu WABHEJASANA kwanza nikushukuru kwa heshima unayonipa, tuendelee kuheshimiana Vivyo hivyo.
Mimi siku zote msimamo wangu uko very clear katika mambo yanayohusiana na chama changu na Taifa langu. Kama mtu anaandika ukweli nitamuunga mkono lakini pia mtu akiandika uongo ama upotoshaji ninamuambia ukweli wake papo hapo. Kwahiyo tunaweza kukubaliana katika jambo moja lakini tukashindwana katika jambo jingine, na hiyo ni hali ya kawaida sana katika maisha, jambo la msingi ni kuhakikisha siku zote tunasimamia ukweli tena ukweli mtupu.

Bahati mbaya sana kibanda anajitahidi sana kutaka kuwapotosha watu kwa kumpamba sana kinana as if ni mtu mpya kutoka sayari nyingine wakati ukweli wa mambo ni kwamba kinana ni miongoni mwa watu walioifikisha kubaya nchi hii, kashfa alizonazo hazimpi nafasi kamwe ya kuwa tishio kwa upinzani nchini, na hasa Chadema ambayo kibanda anajaribu kuionyesha kwamba sasa hatuwezi kufukurukuta kwa uteuzi wa kinana kuwa katibu mkuu wa ccm, kitu ambacho si sahihi hata kidogo, isipokuwa anajaribu kuwajengea wananchi uoga usiokuwa na msingi kwa maslahi yake binafsi na ccm ambao tayari kuna taarifa kwamba wameshamalizana nae, na anajiandaa kuhamia habari corporation ili akawafanyie kazi yao vizuri. Sasa njaa yake asiitumie kuwatia uoga usio na msingi wananchi hasa wapenda mageuzi.

Pia naomba kukufahamisha kwamba sijaandika kwa jazba yoyote isipokuwa nimeandika kwa "tune" ile ile aliyotumia kibanda kutujibu katika makala yake hii. Kama comments zangu zimekustua kwa leo naomba uwe na amani bwana shemeji tuko hapa kubadilishana mawazo kwa njia ya kueleweshana na kukosoana. Na jambo kubwa zaidi ni kuona kwamba nchi hii inapata viongozi makini na mahiri wanaoweza kuwatumikia watanzania wote bila ubaguzi ama kinyongo cha aina yoyote, na hakuna namna ccm inaweza kuwa tegemeo la kuyabadili maisha ya watanzania hawa walio mafukara kwa sababu ya sera mbovu za ccm isipokuwa Chadema pekee ndiyo tegemeo la wananchi kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Sio kwamba ana kesi huyu Kibanda na anataka kupotezea kwa kusifia MAGAMBA ili afutiwe mashtaka?

Angalia sasa ulivyo na akili ndogo?!!! hivi wewe na wenzako kweli ndio mnategemea mtushaiwishi kuwapa nchi kweli kwa mawazo finyu ynayopatikana kupitia kwenye .............???!!!!!!!!!!!!
 
Tunamsifia kinana ni "kimbunga" kwasababu ni msafi hivyo anaweza kutupeleka tunakopataka au tunamsifia kwasababu ni mzuri wa propaganda, anaweza kuwapigia mafisadi debe na wakashinda?

Hivi watanzania tunajua tunachokitaka, kwani fisadi kushinda uchaguzi kwa kununua jamii nzima ni sifa?

Njaa itatumaliza tutauza mpaka watoto wetu
 
Maranya hizi ni propaganda tu,na nahisi ninyi ndio mnaowapotosha hao wanaotaka mapinduzi ya nchi hii,na nashawishika kuamini kwamba wewe utakuwa ni mpinzani namba moja ya wale wanaohitaji mabadiliko kwa sababu unasimamia uongo na upotoshaji.

Wewe ndiye unapiga propaganda hapa wabhejasana.
Juzi mwenyekiti wa ccm taifa raisi Jakaya Kikwete amezungumza mbele ya kamera za waandishi wa habari akiwaasa kwamba sasa waache kutegemea polisi kukabiliana na Chadema na hoja zao, kwamba sasa ni wakati muafaka wa wao kujitokeza hadharani kufanya mikutano ya hadhara kujibu hoja za Chadema. Sasa unataka uambiwe ama usikie nini na kutoka kwa nani ili uridhike kwamba usalama wa ccm kubaki madarakani uko mikononi mwa vyombo vya dola?

Hawa ccm tukiachiwa tucheze nao siasa kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi na kama vyombo vya dola vitaamua kufanya kazi zake kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na katiba ya nchi, vikaachana na tabia ya kuilinda ccm, nakuhakikishia kwamba itakufa moja kwa moja. Hilo wanalitambua sana na ndiuo maana wanatumia vyombo vya dola kadri wanavyoweza kuhakikisha kwamba wanaimaliza Chadema kwani bila hivyo hawana uungwaji mkono wowote katika kuiongoza nchi hii.
 
Kibanda inawezekana ulikuwa na mashaka ya dhati kabisa katika mara zote hizo ulizokuwa sahihi
lakini sio siri za mwizi arobaini inawezekana kabisa ikawa safari hii ndio wewe umekosea huwezi kuwa right
siku zote,mi nafikiri safari hii wewe hauko right bali umekosea kwa meno yale ya tembo mnh!!
kinana anaweza akawa mtu mzuri tu lkni tatizo lipo kwenye chama yani watu waliomzunguka hawezi kufurukuta.
 
Huyu bado tu hataenda habari corporation?

Kumsifia mtu ndio UKWELI(maadili), kweli hii taaluma inatumika kama mpira wa kiume!

Huwezi amini kama ndio mwenyekiti wa jukwaa la wahariri
Kama ni ukweli kwamba Kinana ni Kimbunga kwanini asiseme? Sioni ubaya wa kusema hayo!

Ni aibu kubwa kwa waandishi kama hawa katika Tanzania.
Ni kipi ulichoona hakina msingi na kwamba kinaitia aibu taaluma ya uandishi? Tumpinge kwa hoja. kauli ipi umeona haina maana na ni ya aibu?

Kifupi ni kwamba Kibanda anajiandaa kuondoka FREE MEDIA. Ila sasa style anayoondoka nayo ya kutafuta Bifu na mwajiri ndiyo ya kushangaza, a childish and old style.
Sijaelewa bado. Napata taabu sana kuona wengi mnampinga Kibanda pasipo kusema tatizo lake lipo wapi? Anamwongelea Kinana kwamba ni mwanasiasa mwenye nguvu, wewe unasemaje? Ningekuona una hoja kama ungeleta maelezo ya kina kupinga kwamba Kinana hana nguvu, na kueleza ni kwa kiasi gani Slaa au CHADEMA ina nguvu kuliko Kinana.

Walikuwepo wengi wa hivyo wakapita, huyu naye atapita; Na mbwembwe zake zitapita, na uandishi wake Utapita.

Lakini kitu kimoja tu ambacho hakitapita ni UKWELI

Kweli ya Mungu Itabakia na hakuna Changanya changanya
Kweli ni ipi? Tuambie hiyo kweli unayoifahamu kuhusu uwezo wa Kinana, kama hana nguvu kama Kibanda anavyomsifia or not. Na utupe mapendekezo tufanyeje ili kuzikabili nguvu zake.

Wakati mwingine wanachadema tunajisahau sana. Tunafikiri kusifiwa kwa kila kitu hata kile kibovu ndiyo kujijenga. Lakini kwa taarifa yenu kwa kusifiwa ndiyo tunabweteka na kujisahau. Ndiyo maana makelele mengi lakini ushindi kidogo. Ni lazima tukubali changamoto kama hizi. Tunapoambiwa CCM imeteua secretarieti ya kutisha, tuongeze nguvu upande wetu ili kuikabili. Na tumsute Kibanda atuambie ni katika aspects zipi, kinana anatisha na anashauri nini kifanyike kwa wapinzani kukabili hili.

Hizi kauli za reja reja za mara oooh, kwa vile anataka kuondoka oooh uandishi wa aibu hazitatusaidia. Sana sana zinampa faida maana mwaka 2015 tutakapokosa huo ushindi atakuja hapa kutunanga kwa majigambo kwamba yeye alisema. Sasa tusimpe faida, tuchukue hoja zake, tutafute namna nzuri ya kumkabili adui. Unapokwenda vitani, huwa hakuna adui mdogo wala mkubwa. Hakuna askari mtoto wala mtu mzima. Wote ni askari wana slaha, na uuaji wake ni ule ule. CHADEMA tupo vitani na CCM, tusimu-underestmate adui yetu.
 
Ukisoma makala ya mwandishi na maoni ya watu wengi humu janvini utagundua kuwa, mwandishi, CHEDEMA na mashabiki wengi humu jf wana matatizo yaleyale.

Mwandishi yeye anapenda watu wamuone kama perfect in everything. Katika makala yake, sikuona au kusoma sehemu yeyote ambayo ameeleza upungufu au makosa katika maamuzi au maono yake toka mwaka 1995 mpaka anapoandika makala hii zaidi ya kusema yeye siyo nabii wa siasa za Tanzania. Hakuna binadamu perfect in everything hapa duniani. Ningeweza kuona umaana halisia wa kile alichokiandika kama angeonyesha katika makala yake kuwa naye ni binadamu ambaye kuna sehemu maamuzi yake katika miaka 19 ya uandishi wa habari alifanya makosa.

Kile anachokilalamikia kwa CHADEMA na mashabiki kuwa ni walevi wa fikra na yeye ndicho hicho anachokifanya kwa sasa.

CHADEMA na Mashabiki wake wengi lazima nao wajifunze na wakubali kuwa nao sio perfect in everything. Lazima wakubali kukoselewa, na wajifunze kushukuru pale wanapokoselewa kwa sababu siyo rahisi kupata wakosoaji wasiowatakia mema katika utendaji wao. Kutokubali kukoselewa ni dalili ya chama na mashabiki kubweteka na huo mara nyingi huwa ni mtaji wa failure.
 
Kama ni ukweli kwamba Kinana ni Kimbunga kwanini asiseme? Sioni ubaya wa kusema hayo!.
Mkuu unaamini Kinana ni Kimbunga? ndio maandili ya uandishi wa Habari?
 
Mkuu Maranya AHSANTE sana umejaribu kufunguka:

Nakubaliana na wewe kwenye badhi ya maelezo kwenye ufafanuzi wako lakini napingana na maelezo machache tu.

Kwanza ningependa unionyeshe mahali ambapo Kibanda anajaribu kuwapotosha watu kwa kumpamba Kinana,hilo ni moja Lakini Pili Siamini kama Kibanda ameonesha katika Andishi lake kwamba kutokana na Uteuzi wa Kinanan sasa CHADEMA haiwezi kufurukuta tena:Nadhani utakuwa umemuelewa vibaya tena sana Mkuu Kibanda>Alichojaribu kusema Kibnda hapa ni tahadhari kwa CHADEMA kwamba kwa sababu walikuwa wanajaribu kutumia mianya ile iliyokuwepo huko nyuma kuiyumbisha CCM na kuitandika kila kona waliyokuwa wanatka sasa wajaribu kuwa makini kwa sababu Kwa uongozi wa Kinana ni lazima atakuja na njia nyingine tofauti kabisa katika kukiendesha chama,na nadhani katika badhi tu ya mikutano aliyofanya umeona kilichofanyika.

Katika siku za hivi karibuni hakuna kiongozi wa CCM ambaye amediriki kuwaita na kuwasimamisha watendaji wa serikali katika halmashauri za wilaya kujibu matatizo ama malalamiko kwenye mikutano ya hadhara kwa wananchi,ama kutoa maelekezo mbele ya wananchi,achilia mbali yawezekana ni uanii unafanyika lakini machoni kwa wananchi kuna kitu kinakuwa kimeonekana!

Tatu huko nyuma CCM ilikua imejiahahu sana katika kuwasimamia atendaji wa serikali na ndiyo mana umeona vitendo vya ufisadi vimekuwa vikifanyika hadi ngazi ya kijiji huku mtu akiacha bila kufanywa chochote,na ndipo hapo ambapo CHADEMA wamepatia sifa katika kuibua utendaji mbovu wa serikali,kwa hiyo kama endapo kasi hiyo itaendelea na wahusika wakawajibishwa it means kwamba wananchi ataona sasa kumbe serikali ya CCM imeamka na inashughulika na wajanja wachache ambao wanakula fedha zao na mwisho wa siku huu wimbo wa kuiondoa madarakani inaweza kufifia na hivyo kujikuta mwaka 2015b inapata madaraka ka mara nyingine tena.

Kwa hiyo ka uelewa angu nilionao nadhani alichofanya Kibanda kama mfuasi pia wa CHADEMA naamini hivyo kutokana na koment zake na mandishi yake mbalimbali ni kuitahadharisha CHADEMA kamba wakae chini na kuangalia ni namna gani sasa wanajipanga upya katika kukabiliana na siasa hizi za Kinana,hilo linawezekana na tarifa nilizo nazo kam si za uongoz hata cdm wenyewe kasi iliyonayo CCM sasa imewastua na wanaangalia namna ya kujipanga upya ili waingie mitani kivingine kabisa katika kuisambaratisha safi hiyo jambo ambalo kama ni keli nawapa big up!!!!!

Nne siamini kama kweli Kibanda amejaribu kuwatisha ananchi na hasa afuasi wa cdm katika andishi lake na kama kuna mfuasi ambaye ametishika na andiko hilo basi atkua na matatizo ya akili na hakua na mamuzi ya dhati ya kuiunga mkono CDM kwenye harakati za kulikomboa Taifa hili,naanza kupata mashaka na haya mashmbulio anayoperekewa Kibanda wakati ni mtu ambaye juzijuzi tu alikua akifagiliwa kwelikweli na wanCDM?!

Tano na Mwisho kwa sasa mkuu Maranya hebu tujifunze kukosolewa na haa kusikia yale ambayo hatupendi kuyasikia,kwa sababu mwisho wa siku yatakuja kutusaidia,katika harakati hizi za mapambano tusipende kubeza kila kitu ama kushabikia kila kitu tunapaswa kuwa makini na wachambuzi wa mambo ili mwisho wa siku tufikie malengo yaetu,namini hata baadhi ya viongozi wa CDM sio wasafi kama unavyomsemea Kinana kamba ni mchafu,kuna wakina Dk Slaa wamewahi kupata tuhuma nyinginyingi zikiwemo hizo hizo za ufisadi kwenye makanisa huko alikokua,na hata kenye masuala ya ngono!

Kwa hiyo nadhani tujitahidi kuvumiliana lakini kubwa ni kuendeleza mapambano kwa kukubali ushauri pale tunapopewa.
 
Kibanda umetoa tahadhari kwa maono yako na misimamo yako ya nyuma na mambo yalivyo kwenda huko miaka ya nyuma,Fine lakin sasa Watanzania si wale wa 1995 wala wa 2005,ni watanzania wapya waliochoka na mfumo choka na uliopoteza mwelekeo. Isitoshe huyu Kinana Mbona alikuwepo takribani miaka 20 ndani ya kamati kuu ya CCM lakini hakuna jipya? kwanini hakuweza kupenyeza hayo anayoyataka huko na yale unayodhani yatakuwa kimbunga kwa upinzani? Jibu Ni rahisi tu,Kinana kama makamba,kama Mkama atabaki analia tu,maana pia yeye ni gamba linalotakiwa kuvuliwa!

All in all,CDM hatutalala mpaka Kieleweke.
 
Abi Kibanda! Nakushangaa sana. Kwanza wewe ni mwongo msahaulifu na pia jua kuwa atakaye kukosoa hapa ni kijana mdogo.
UMESEMA mwaka 1995 hukuunga mkonn harakati za Mwl . Nyerere (udikteta katka demokrasia) ili Mkapa awe mgombea urais kupitia CCM, na umethibitisha kwa kusema utabiri wako ulitimia kwa Mkapa kuboronga mwishoni. Lakini pia umesema ulipinga 2005 Kikwete kugombea urais na hadi ukakwaruzana na Rostam, hata hivyo Kikwete alishinda na kwamba wote tunashuhudia kuboronga kwake.

Sasa huyu ndo Kikwete aliyepokonywa karata na Mwl. 1995 kwa kumpendekeza Mkapa, sasa 1995 wewe ulikuwa upo kwa mgombea yupi? Au Kikwete wa 2005 uliyempinga alikuwa sio yule aliyefanyiwa udikteta 1995?

Tukiendelea zaidi pia umesema, Mrema 1995 kupitia NCCR hukumkubali. Je mwaka huo basi wewe ulikuwa huna mgombea wa kumpa kura yako?
Au alikuwa wa chama kipi mbali na hivyo viwili.
 
Ukisoma makala ya mwandishi na maoni ya watu wengi humu janvini utagundua kuwa, mwandishi, CHEDEMA na mashabiki wengi humu jf wana matatizo yaleyale.

Mwandishi yeye anapenda watu wamuone kama perfect in everything. Katika makala yake, sikuona au kusoma sehemu yeyote ambayo ameeleza upungufu au makosa katika maamuzi au maono yake toka mwaka 1995 mpaka anapoandika makala hii zaidi ya kusema yeye siyo nabii wa siasa za Tanzania. Hakuna binadamu perfect in everything hapa duniani. Ningeweza kuona umaana halisia wa kile alichokiandika kama angeonyesha katika makala yake kuwa naye ni binadamu ambaye kuna sehemu maamuzi yake katika miaka 19 ya uandishi wa habari alifanya makosa.

Kile anachokilalamikia kwa CHADEMA na mashabiki kuwa ni walevi wa fikra na yeye ndicho hicho anachokifanya kwa sasa.

CHADEMA na Mashabiki wake wengi lazima nao wajifunze na wakubali kuwa nao sio perfect in everything. Lazima wakubali kukoselewa, na wajifunze kushukuru pale wanapokoselewa kwa sababu siyo rahisi kupata wakosoaji wasiowatakia mema katika utendaji wao. Kutokubali kukoselewa ni dalili ya chama na mashabiki kubweteka na huo mara nyingi huwa ni mtaji wa failure.

BIG UP hapo kwenye RED Mkuu pamoja sana,naamini tutafika taratibu ndio mwendo!
 
Abi Kibanda! Nakushangaa sana. Kwanza wewe ni mwongo msahaulifu na pia jua kuwa atakaye kukosoa hapa ni kijana mdogo.
UMESEMA mwaka 1995 hukuunga mkonn harakati za Mwl . Nyerere (udikteta katka demokrasia) ili Mkapa awe mgombea urais kupitia CCM, na umethibitisha kwa kusema utabiri wako ulitimia kwa Mkapa kuboronga mwishoni. Lakini pia umesema ulipinga 2005 Kikwete kugombea urais na hadi ukakwaruzana na Rostam, hata hivyo Kikwete alishinda na kwamba wote tunashuhudia kuboronga kwake.

Sasa huyu ndo Kikwete aliyepokonywa karata na Mwl. 1995 kwa kumpendekeza Mkapa, sasa 1995 wewe ulikuwa upo kwa mgombea yupi? Au Kikwete wa 2005 uliyempinga alikuwa sio yule aliyefanyiwa udikteta 1995?

Tukiendelea zaidi pia umesema, Mrema 1995 kupitia NCCR hukumkubali. Je mwaka huo basi wewe ulikuwa huna mgombea wa kumpa kura yako?
Au alikuwa wa chama kipi mbali na hivyo viwili.

Inaonekana wewe ni mvivu sana wa kusoma,namini hujasoma makala yote ya Kibanda,na kama umeisoma basi uelewa wako ni mdogo sana na napata mashak na elimu uliyo nayo.rudia kuisoma hiyo makala utagundua kwa nini nimesema haya maneno,na naomba ukishagundua urudu humu jamvini useme na utuombe radhi!
 
Mkuu unaamini Kinana ni Kimbunga? ndio maandili ya uandishi wa Habari?
POMPO mimi simjui Kinana, ndiyo maana nataka watu watupe facts za kwanini Kinana si Kimbunga. Huyu mtu amekuwa meneja wa kampeni za CCM tangu mwaka 1995, kwa hiyo anajua propaganda za kisiasa zote, ameshakabiliana na akina Mrema, Lipumba, Mbowe na Slaa. Anawajua inn and out. Ni kwa vipi humuoni kama ni tishio katika anga za kisiasa? Ni nani wa upinzania mwenye uzoefu mkubwa kama wa Kinana? Hapa mimi nafikiri upinzani tujipange tu, na si kubeza uwezo wa Kinana. Namna pekee ya kummaliza Kinana labda ni kuzihuisha hizo propaganda za kwamba ni mwizi. Labda hiyo itasaidia kumpunguzia nguvu, otherwise, ni lazima tukubali ukweli kwamba Kinana ni tishio.
 
Last edited by a moderator:
Wewe ndiye unapiga propaganda hapa wabhejasana.
Juzi mwenyekiti wa ccm taifa raisi Jakaya Kikwete amezungumza mbele ya kamera za waandishi wa habari akiwaasa kwamba sasa waache kutegemea polisi kukabiliana na Chadema na hoja zao, kwamba sasa ni wakati muafaka wa wao kujitokeza hadharani kufanya mikutano ya hadhara kujibu hoja za Chadema. Sasa unataka uambiwe ama usikie nini na kutoka kwa nani ili uridhike kwamba usalama wa ccm kubaki madarakani uko mikononi mwa vyombo vya dola?

Hawa ccm tukiachiwa tucheze nao siasa kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi na kama vyombo vya dola vitaamua kufanya kazi zake kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na katiba ya nchi, vikaachana na tabia ya kuilinda ccm, nakuhakikishia kwamba itakufa moja kwa moja. Hilo wanalitambua sana na ndiuo maana wanatumia vyombo vya dola kadri wanavyoweza kuhakikisha kwamba wanaimaliza Chadema kwani bila hivyo hawana uungwaji mkono wowote katika kuiongoza nchi hii.

Sio rahisi kihivyo mkuu!!!!!!!
 
kwa pro chadema wenye akili hapa kibanda anatoa tahadhali ya chadema kujipanga
 
Kibanda ni mwandishi makini mwenye weledi tatizo kubwa la Pro-Chadema JF hawataki chama chao watu wakijadili wala kiandikwe kwa ubaya.
 
POMPO mimi simjui Kinana, ndiyo maana nataka watu watupe facts za kwanini Kinana si Kimbunga. Huyu mtu amekuwa meneja wa kampeni za CCM tangu mwaka 1995, kwa hiyo anajua propaganda za kisiasa zote, ameshakabiliana na akina Mrema, Lipumba, Mbowe na Slaa. Anawajua inn and out. Ni kwa vipi humuoni kama ni tishio katika anga za kisiasa? Ni nani wa upinzania mwenye uzoefu mkubwa kama wa Kinana? Hapa mimi nafikiri upinzani tujipange tu, na si kubeza uwezo wa Kinana. Namna pekee ya kummaliza Kinana labda ni kuzihuisha hizo propaganda za kwamba ni mwizi. Labda hiyo itasaidia kumpunguzia nguvu, otherwise, ni lazima tukubali ukweli kwamba Kinana ni tishio.
Mkuu 2010 alikuwa kampeni maneja wa JK, mbona alianza kulalamika kuwa familia ya JK inamuingilia majukumu yake?
 
Back
Top Bottom