Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Ndugu zangu wapenda maendeleo ya TZ tusiwe wepesi kumlaum huyu jamaa lkn kwa mawazo yake iwe tahadhari ya kiutendaji kwa Dr. Slaa kujiweka sawa, kwani ,dharau mwiba mguu huota tende, kusema ccm ilipofikia haiwezi tena kufufuka, lkn tujuwe kuwa wa TZ wengi hawana elimu ya uraia kama ww na mm tulivyo, chamsingi tuwaelimishe wengine zaidi ili kusije kuwa kama ilivyo mkuta rais wa Zambia wakati ule aliposema hakuna wakunizidi mwisho akang'olewa madarakani kirahisi, Kinana inavyooneka kama amekamia kufufua kile kilichoondoka akili mwa wengi kuwa ccm inaweza fanya miujiza katika system hii walionayo ambayo inaonekana wazi ni mbofumbofu.
Siyo vema kumbeza Kibanda lkn tukubali kuwa Simab timu ninayoipenda toka nikiwa mdogo ilijua haiwezi kufikiwa kwa point na watani wetu, lkn watani wakajipanga leo tumepitwa, ni vema tujiweke tayari kukabiliana na haya anayosema Kibanda ili asije sema nilitabiri yamekuwa.

Hakuna anayepinga kibanda au mtu mwingine yeyote kuwa na maoni ya mawazo yake. Tunachokataa hapa ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi mazima na huyu kibanda kwa malengo yake binafsi.

Nimesema hapo awali kwamba kinachoweza kuwanusuru ccm kubaki madarakani kwa mwaka 2015 ni vyombo vya dola pekee na hakuna kingine. Kinana hana uwezo wowote wa kuihuisha ccm. Umeshafanya tathmini ya ziara alizofanya hivi karibuni mikoa ya Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha na kuona muitikio wa wananchi dhidi ya kinana na ccm kwa ujumla?

Kama kweli kinana mwenyewe anajitambua kwamba yeye ni kimbunga cha kuuzoa upinzani na kuufukia shimoni inakuwaje anakwenda mikoani na kukodi wananchi wa kwenda uwanjani kumsikiliza? kimbunga kikivuma si wananchi/ watu wenyewe wanakisikia na kujikusanya? inakuwaje hiki kimbunga cha kinana kisaidiwe kujaza watu uwanja kwa kuwanunua watu kama alivyofanya hivi karibuni Arusha ambako ni "nyumbani" kwao kwa watu kupewa fedha ili wahudhurie mkutano?

Kama mtu anawakosoa viongozi wetu kwa mambo ya ukweli tutakubaliana nae lakini yeyote atakayethubutu kutengeneza kiwanda cha uongo huyo hatutamuacha apite kimya kimya, lazima tutamjibu kwa tune ile ile aliyotumia kuwahadaa wananchi. Imeshafahamika kwamba kibanda yuko njiani kwenda kwa fisadi Rostam sasa kwanini anahangaika kuwachafua viongozi wetu? kwanini asiondoke kwa amani tu? kwani wangapi waliondoka Tanzania daima lakini bado gazeti linazidi kupata mauzo ya juu? Manyerere Jackton na Deodatus Balile kwa kutaja wachache, waliondoka lakini bado Tanzania Daima haikutetereka.
 
Huyu bado tu hataenda habari corporation?

Kumsifia mtu ndio UKWELI(maadili), kweli hii taaluma inatumika kama mpira wa kiume!

Huwezi amini kama ndio mwenyekiti wa jukwaa la wahariri

Nilipokwambieni TASNIA ya habari imekumbwa na KIDUDU, utapeli na ujinga mkabisha. nakumbuka gazeti hili lilipoanza kumpinnga Mufti juu ya kauli ya Chadema na huyu huyu ndie alietoa makala na tahariri. leo hii ndio hayo hayo. Halbadiri hii imeanza kumkumba
 
Kaka Kibanda kwanza nikupongeze kwa ujasiri wako ambao umekuwa ukiuonesha kwa muda mrefu kwenye fani hii ya Uandishi wa ahabari hapa nchini,ingawa kuna watu ambao hawapendi kukubaliana na wewe katika hoja zako,hili si tatizo kwa sababu huwezi kumlzimisha kila mmoja awe mshabiki wako ama akubaliane na wewe!

Pili kwenye fani ya Uandishi wa habari hauko kwa ajiili ya kumfurahisha kila mtu ama kumuudhi kila mtu,bali uko kwa ajili ya kueleza ukweli kwa jamii na kuufikisha ujumbe kama uivyo bila kuubadilisha ama kuukatakata vipande,na hii ni moja ya mambo ambayo watu hawapendi hasa kusikia,watanzania wamefika mahali pabaya sana na hasa hawa wanaojiita 'wanabadiliko'!

Hawa watu wanashangaza kweli,wnadhani mtusi na kejeli na kushibikia kila hoja inayomsifia mpizani ama kiongozi fulani wa upinzani ndio mabadiliko yenyewe,inasikitisha sana!!!,ni atu ambao hawataki kukuubali ukweli wal kuambiwa ukweli,ikifika hapo ni lazima watakuporomoshea matusi ya nguoni bila kujali wewe ni nani na umetoka wapi?!

Na ndiyo maana mimi nimekuwa nikisema kwamba bado CCM itaendelea kuongoza nchi hii pamoja na matatizo yake chungu mzima,kwa sababu watu hawataki kujifunza na kuujua ukweli wa mambo namna ulivyo na nini kifanyike,watu wamekuwa washabiki wa mambo bila kufanya utafiti na kujua ukweli,nasem hii haisaidii hata kidogo katika kufanya mabdiliko am mpinduzi!!.

Ni lazima watu wajifunze kuukubali ukeli na kua watfiti wa mambo na ha yale ya msingi yanayolihusu Taifa na watu wake,watu wajifunze kuwa wavumilibu wa kusikia na y upande a pili,watu ajifunze kusikia hata yale ambyo hawapendi kuyasikia,yale yanyowachoma moyo,ni vyema ukakubali kunywa Klorokwini pamoja na kamba ni chungu ili uweze kupona mlri,kuliko kunywa Panadol na kuituliza,mwisho wa siku Malria itandelea kukutafuna na mwisho wa iku ni kifo.

Hapa ndipo walipofika watanzania ambo mimi naamini kwamba hawaipendi nchi yao bali wanapenda kushabikia watu fulanifulani,nataka nikiri na kuamini kwamba Mahali ambapo CCM imewafikisha watanzani si pazuri,lakini kam kweli tunahitaji kufanya mabadiliko ya keli na kupata uongozin ulio imara ndani ya CCM ama nje ya CCM ni vyema tukawa wavumilivu na wapembuzi a mambo,tuachane na huu uhuni wa kushabikia mambo ili mrai tu jambo lililosemwa ni la kufagilia Dk.Slaa,Mbowe,Zitto............!!!

Hapa hakika tutakua bado hatuwasaidia watu hawa,hakuna mtu mkamilifu Duniani,wote wameghfilika,kikubwa hpa ni kujaribu kushauriana hata kama mtu amekwenda kinyume aambiwe ajue ili arudi kenye mtari na hatimaye tukamilishe ule mpango etu wa kufanya mabadiliko,vinginevyo tutakuja kuendelea kupiga makelele mara ohhhh tumeibiwa,mara ohhh tumefaniwa kile,kumbe hatukufanya maandalizi.

Ni ukeli kamba mtu aliyewahi kung'ata na nyoka hata akiguswa na jani tu anastuka,CCM kuna kitu imekiona kenye uchaguzi wa mwaka 2010,kwa hiyo kwa vyovyote vile kwa asa inajaribu kufanya kila linalowezekana ili kujisafisha,na kibaya zaidi wapinani wamekuwa wakitumia tu yale madhaifu ya CCM kujieleza ama kujoambanua kwa wananchi,sasa swali la msingi hapa kama CCM ikirekebisha hayo ambayo yanapigiwa kelele na wapizani si ni wazi kwamba itakapofika uchaguzi watu watasema si tayari wamerekebisha hili na hili ambayo bdiyo yalikuwa yakitusumbua,kwa hiyo maan yake ni kwamba wataipatia kura za kuiweka tena madrakani.

Ni vyema tukawa wawazi katika kuwashauri hawa viongozi wetu wa Upinzani kwamba kama kweli wanataka kuchukua nchi na kuingoza ni vyema wakawa na mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ili kuendana na wakati na si kufanya mambo ambayo kesho na keshokutwa yakipatiwa ufumbuzi watu wanakosa hoja!!

Najua kuna watu watakuja na matusi yao hapa lakini mimi sijali kwa ababu huu ndio ukweli wenyewe,Kibanda hongera sana niko p[amoja na wewe,hebu tuendelee kuueleza ukweli na hasa kwa hawa wanaojifanya wapinzani kumbe ni mchwa waliojipenyeza kwa ajili ya kutafuna na kuusambaratisha upinzani,karibuni kwa matusi.Naamini wenye akili timamu watakuja na hoja lakini wale wasiokuwa na akili timamu wataanza kuporomosha matusi kwa Kibanda na kwangu tena kwa maneno mawili,matatu manne au maneno kumi tu!
 
Ndugu Kibanda bila shaka unafahamu vizuri sana ugomvi wa CCM na Watanzania , ni DHULUMA , kwa maana ya rushwa , wizi ,ufisadi ,upendeleo ( ajira nzuri kwa watoto wa vigogo ,rejea ya BOT ) nk , huyu Kinana wako anazo tuhuma ambazo hata wewe unazijua ! Sasa unamsifia kwa lipi ? ikiwa yeye ni mtuhumiwa unadhani ataweza kusafisha uozo ndani ya CCM ? Bila kuondoa DHULUMA ccm haiwezi kupona na Kinana hawezi , wala hakuwahi kuweza , na wala hatakuja weza ! Sifa zinatoka wapi ? Kibanda najua unajiamini sana na ni vizuri , lakini wewe ni binadamu, kuna mengine huyaoni wengine wanayaona , unajua kwa nini Kikwete alimteua Mukama ? Na ni kwa nini kamng'oa ? Hebu umiza kichwa kidogo , ni kweli CDM hawatakiwi kubweteka lakini pia CDM hawana sababu yoyote kumhofia Kinana , hana jipya wala hakuwahi kuwa nalo ! Kama unampenda mtu kwa sababu ya sura yake basi nenda kanywe naye chai - JK NYERERE .

Nimependa simple but not deep analysis ya Kibanada. Lakini nina maswali kadhaa ambayo pengine anatakiwa kuyajibu. Ni imani yangu huwa unapita humu ndani.


1. Udikiteta wa mwalimu kumkataa Kikwete na Kumkubali Mkapa ulikuwa na shida gani kama Huyu Kiwete uliyemkataa wewe 2005 kwa kuona hafai kuwa kiongozi ndo alikataliwa na Mwalimu 1995 kwa sababu zilezile jabo kwa mwalimu umempa cheo cha Udikteta lakini wewe hujajipa cheo?

2. Umelinganisha umaarufu wa mrema na Umaarufu wa vyama vya siasa hasa CHADEMA na baadhi ya vingozi wake tena ukamtaja Dr. Slaa, Je kwa uwelewa wako na uzoefu wako katika tasnia hii ya habari unafikiri umaarufu wa vyama vya siasa hasa CHADEMA leo na viongozi wao hasa Dr. Slaa unatokana na sababu zile zile zilizomfanya Mrema awe maarufu japo kama moto wa mabua?

3. Zijaona ukifanya balanced analysis inayoonyesha strengths za kinana ambazo zina reflect kwenye mapungufu ya uongozi katika vyama vingine vya siasa.


Mwisho: Kibanda badala ya kufanya analysis ya Issues umenalyse Umbea tu.
 
1-Ni malengo gani binafsi unayodhani anayo Kibanda katika andishi lake hili?Eleza/Fafanua Mkuu.

2-Ni tathmini gani uliyofanya na kugunua kwamba mwaka 2015 CCM inaondoka madarakani,au ka maneno haya ya humu JF ambayo yamesimamia ushibiki tena ule wa kijinga kabia ambao hauna hoja?!,

3-Hoja ya Kibanda inahusiana vipi na mazuo ya Gazeti la Tanzania Daima,kwani ni Gazeti la CHADEMA HILI AU?!,

Mwisho Mkuu Mwita Maranya,miongoni mwa watu ambao huwa wanaheshimu hoja zao humu ndani Jamvini ni mimi,lakini leo hii nashangaa umekua na jazba sana na Kibanda,au kwa sababu ameigusa CHADEMA?,mbona siku zote za Nyuma ulikuwa mfuasi mkuu a Kibanda hata kama alikuwa ameandika Utumbo katika kuisifia CHADEMA ama kiongozi yoyote wa CHADEMA,hizi hasira zako za leo zinatoka wapi Mkuu?
 
Nilichoona kwenye mtiririko wa makala hiyo ni mwandishi kujicifia mwanzo mwisho.. kwa cifa alizojimilikisha kwenye makala yake hii hakupaswa kuwako hapo alipo sasa.. Ushauri wangu kwake awe makini.. Binadamu anaposukumwa na njaa kufanya jambo ambalo ni ovu kwa jamii anaweza kueleweka.. Ila pale anaposukumwa na tamaa kupalilia uovu jamii haitamuelewa hata kidogo.. Kibanda hana njaa.. Napenda sana kuamini hasukumwi na tamaa kuandika alichokiandika..

Hivi unadhani asipojisifia mwenyewe nani atakuja kumsifia ama kumsemea kwa yale mazuri ambayo amewahi kufanya kama watu wenyewe ndio ninyi ambao leo hii mnamponda,Acha ajisifu mwenyewe bana kwa sababu akingoja mumsifu hamtafanya hivyo Mkuu.
 
Kwanini asiondoke kwa amani tu? kwani wangapi waliondoka Tanzania daima lakini bado gazeti linazidi kupata mauzo ya juu? Manyerere Jackton na Deodatus Balile kwa kutaja wachache, waliondoka lakini bado Tanzania Daima haikutetereka.
unalitete hilo gazeti kwa interest zipi weka wazi? unahisa au kisa linasifia cha chako au kwasababu ni gazeti la mwenyekiti wa chama therefore ni gazeti la chama?
 
Rafiki yangu Ansbert Ngurumo mzee wa Maswali Magumu naomba na wewe utoe kauli yako juu ya mwenendo wa Bosi wako Absalom Kibanda.

TUMBIRI Ni kwanini unamtaka Ansbert Ngurumo ndiye atoe kauli yake juu ya mwenendo wa Kibanda badala wewe mwenyewe utoe?,kwani wewe huna uwezo wa kujisimamia mpaka usimamiwe?,siki bana ninyi ndio watu mnaotusumbua humu ndani,mnakua fuata upepo hamna uwezo a kujenga hoja ninyi Binafsi mpaka mfukuzie mawazo ya wenzenu,wewe njoo na hoja yako umweleze huyu kibanda na sio kuomba msaada.
 
Kibanda hata kwa kumwangalia anaonekana ni mnafiki. Kuna wakati walipanga maandamano wakapigwa mkwara na Chagonja na wakatepeta kama mlenda.Kiufupi hakuna move hata moja alishawahi kuifanya na ikafanikiwa zaidi ya kupayukapayuka.Sasa hivi kaibuka na mpya eti katiba haitakamilika kabla ya 2015
 
Pro Chadema hawataki kabisa ukweli.Wao wanataka kuiponda tu CCM na wateule wao

Umeona eeee!!! hawa jamaa wakiguswa hapatalalika hasa wakiingia wenyewe kwa hii thread na sikujua Absolom Kibanda kumbe ni Jiwe hasa kwani kajionesha YEYE SIO MPINZANI masika kiangazi yeye twenty two Ukithubutu kuikosoa CHADEMA au kumgusa yeyote miongoni mwa viongozi wake kama nilivyofanya miaka mitatu au minne iliyopita wakati nilipopinga uamuzi wa Zitto Kabwe kugombea uenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa sababu muda wake ulikuwa bado, idadi ya matusi utakayovurumishiwa kama ni mtu ambaye una moyo mwepesi unaweza ukaacha kuandika.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wiki iliyopita wakati nilipowaonya wapinzani kukaa chonjo na Kinana kwani kimbunga ambacho alikuwa akielekeza kukipuliza kuelekea upande wa kambi ya upinzani kinaweza kusababisha upepo unaovuma sasa kubadili njia.
 
kilam2 anao uhuru wa kuwa na maoni nakueleza fikra zake kama huyo mjamaa. 2015 c mbali kiivyo
 
Hivi unadhani asipojisifia menyewe nani atakuja kumsifia ama kumsemea kwa yale mazuri ambayo amewahi kufanya kama atu wenyewe ndio ninyi ambao leo hii mnamponda,Acha ajisifu mwenyewe bana kwa sababu akingoja mumsifu hamtafanya hivyo Mkuu.

Mkuu wapo mbona wanaosifiwa bila ya wao kujikweza..? Katika hali ya kawaida unapojicifia mwenyewe unajaribu kujenga uhalali wa kitu fulani au kuficha udhaifu/upungufu wa kitu fulani..! Itafika wakati kama anastahili cifa atapewa cifa zake.. Wangapi wanaocifiwa sasa kwa haki..?
 
wewe na kibanda akili zenu zinafanana kama si kulingana.

Nimesema hivi na narudia, ccm ilikofikia sasahivi imebakiwa na mbinu moja tu ya kuwabakisha madarakani, ambayo ni kutumia vyombo vya dola, Polisi, usalama wa Taifa na JWTZ. Kama ni kimbunga basi kimbunga pekee kinachoweza kuwakumba na kuwasomba wanamageuzi na wapinzani kwa ujumla ni hivyo vyombo vya dola na si vinginevyo.

Maranya hizi ni propaganda tu,na nahisi ninyi ndio mnaowapotosha hao wanaotaka mapinduzi ya nchi hii,na nashawishika kuamini kwamba wewe utakuwa ni mpinzani namba moja ya wale wanaohitaji mabadiliko kwa sababu unasimamia uongo na upotoshaji.
 
Mwandishi anayeheshimika kama Kibanda anakubali kudhalilisha taaluma yake kwa mambo ya ki..s..en..ge kabisa, shame on him!
 
Mkuu wapo mbona wanaosifiwa bila ya wao kujikweza..? Katika hali ya kawaida unapojicifia mwenyewe unajaribu kujenga uhalali wa kitu fulani au kuficha udhaifu/upungufu wa kitu fulani..! Itafika wakati kama anastahili cifa atapewa cifa zake.. Wangapi wanaocifiwa sasa kwa haki..?

Mkuu hakuna mtu anayeweza kukusifia hata kama ungefanya mzuri kiasi gani,na malipo ya Kibanda ndiyo haya unyoyaona humu ndani hivi sasa,ni huyuhuyu Kibanda niliwahi kuona coment za watu humu JF akimfagilia kweli kisa alikuwa amemsema vizuri Mbowe na Slaa wakati ule wa mvutano wa Uenyekiti ndani ya CHADEMA pale ambapo alimpa bakora za kutosha ZZK za namna ambavyo bado hatoshi kuachiwa chama.

Lakini hebu angalia leo iianavyopondwa na kuchambuliwa kama karanga kwa sababu tu amemsifia Kinana!!! Mkuu hii inanitian mashaka sana ndiyo maana nasema ni bora ajisifu kwa sababu kesho NA KESHO KUTWA ATAKUFA KAMA YULE MSANII 'SHARO' kabla hajayasema haya aliyoyasema bana!
 
Mwandishi anayeheshimika kama Kibanda anakubali kudhalilisha taaluma yake kwa mambo ya ki..s..en..ge kabisa, shame on him!

Wapi alipojidhalilisha,wewe unajua misingi ya Taalum ya Habari au unaongea utadhani um........c......ke..........a?
 
Huyu bado tu hataenda habari corporation?

Kumsifia mtu ndio UKWELI(maadili), kweli hii taaluma inatumika kama mpira wa kiume!

Huwezi amini kama ndio mwenyekiti wa jukwaa la wahariri

Sio kwamba ana kesi huyu Kibanda na anataka kupotezea kwa kusifia MAGAMBA ili afutiwe mashtaka?
 
Umeona eeee!!! hawa jamaa wakiguswa hapatalalika hasa wakiingia wenyewe kwa hii thread na sikujua Absolom Kibanda kumbe ni Jiwe hasa kwani kajionesha YEYE SIO MPINZANI masika kiangazi yeye twenty two Ukithubutu kuikosoa CHADEMA au kumgusa yeyote miongoni mwa viongozi wake kama nilivyofanya miaka mitatu au minne iliyopita wakati nilipopinga uamuzi wa Zitto Kabwe kugombea uenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa sababu muda wake ulikuwa bado, idadi ya matusi utakayovurumishiwa kama ni mtu ambaye una moyo mwepesi unaweza ukaacha kuandika.
Hivi ndivyo ilivyokuwa wiki iliyopita wakati nilipowaonya wapinzani kukaa chonjo na Kinana kwani kimbunga ambacho alikuwa akielekeza kukipuliza kuelekea upande wa kambi ya upinzani kinaweza kusababisha upepo unaovuma sasa kubadili njia.

kama kweli wanahitaji kuiongoza nchi pamoja na sisi watanzania ambao tunaamini ni wajanja ni lazima wakubali kukosolewa vinginevyo hawatapata ridhaa hiyo wanayoitaka!!!!!
 
Back
Top Bottom