ccm ilikofikia imebakiwa na mbinu moja tu ya kuwabakisha madarakani, ambayo ni kutumia vyombo vya dola, Polisi, usalama wa Taifa na JWTZ. Kama ni kimbunga basi kimbunga pekee kinachoweza kuwakumba na kuwasomba wanamageuzi na wapinzani kwa ujumla ni hivyo vyombo vya dola na si vinginevyo.
Hizi ndoto za
Kibanda kwamba kinana ni kimbunga wacha aendelee kuota mwenyewe sisi huko tulishaondoka siku nyingi. Huwezi kumfananisha hata kidogo Augustine Mrema na Dr. Slaa, hawa ni watu wawili walio mbali sana kiuwezo na kwa muono. Yeye aendelee tu kula matunda ya kumsafisha Lowasa na sasa kumjenga Kinana kwakuwa si haba anajipatia ujira wake na kuweza kusukuma mbele gurudumu la maisha na familia yake, lakini atambue kitu kimoja kwamba ccm ilipofikia hakuna mganga yeyote anayeweza kuinusuru na anguko kuu mwaka 2015, si kinana wala vinana!!