Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

That doesnt matter. Kwani Ludovick si ni muasi na msaliti kama ulivyo wewe? Mnajifanya kukipenda chama, tunawapa dhamana na vyeo vikubwa tukiamini ni wenzetu kumbe mnatumiwa. Ludovick kuaminiwa kwa kiwango kile haishangazi ni kama Juliana alivyoaminiwa na kupewa umakamu mwenyekiti wa BAVICHA na huku ni nyoka.

hiyo dhana ya uasi imepandikizwa na akina slaa ili kukwepa kukiumbua chama chao na kuficha maovu wanayofanya
Hujajibu hoja mkuu! Angalia post yangu na jibu lako.
 
Tukutane mahakamani maana kuna watu wanazani huu ni mchezo wa kuigiza.
Poor you Mwampamba! Mahakamani kwa kesi ipi? Si uende ukatoe ushahidi kwenye kesi ya Ludovick kwamba ndiye aliyemuumiza Kibanda? Sasa unataka nini tena hapa? Unayemtishia kwenda naye mahakamani ni nani hapa, ili kiwe nini?
 
Wewe inaonekana taarifa zinakupitia pembeni. Mbona hili jambo lipo wazi kabisa siku nyingi. Tena watu walileta na evidence za Ludovick mwenyewe akijitetea kwamba siku Kibanda amepigwa yeye Ludovick alikuwa ametekwa?

Sasa story ipo hivi:
Baada ya Nchemba kumtuma Ludovick akamrecord Lwakatare, na kupeleka ile video polisi, halafu akaona polisi hawachukui hatua, ndipo alimtuma Ludovick akamshambulie Kibanda ili ionekana mipango ya Lwakatare ndiyo imetimia.

Ndiyo maana mara tu baada ya Kibanda kushambuliwa, video ya Lwakatare iliwekwa kwenye mitandao.

Kwani kisa cha CHADEMA kumtosa Ludovick ni nini? Ni baada ya kugundua kwamba Ludovick ni mmafia. Hilo lipo wazi mkuu, kama hukuwa na taarifa basi uipate saa hivi.

Mwigulu Nchemba ndiye aliyemtuma Ludovick akamdhulu Kibanda ili apate cha kusema kuhusu video ya Lwakatare ambayo waliitengeneza na Ludovick.

Yaani sijui kwanini kuna watu wanaushabiki wa kijinga sana hasa hasa kikiwa kitu ni cha kisiasa,watu wote wanajua wazi kuwa lodovick alifanya umafya kwa faida ya chama chake na hilo lipo wazi,lkn kwa upuuzi tu mtu hata km ana kinyesi usoni akuambiwa ataanza kukipamba kinyesi kile na kionekane ni poda,suala la wahariri kudhuriwa inajulikana wazi kuwa ni mpango wa wazi wa chadema kwa faida wanazozijua wao,lkn cha ajabu lazima tu wamuingize mtu mwengine ili ile taswira ya umafia iondoke ktk sura za watu,suala la kuwadhuru wahariri ni mpango wa wazi wa chadema na sio kuanza kuwaingiza akina nchemba,ubaya wa hawa watu wananchi washaujua na upo wazi
 
Last edited by a moderator:
Hapo picha ipo wazi. Ludovick aliweza kujipenyeza ndani ya CHADEMA kwaajili ya kuitumikia CCM na.serikali yake.

Kwa hiyo Ludovick na Mwigulu walitengeneza video halafu wakaenda kutaka kumwua Kibanda ili ionekane Lwakatare ndiye aliyefanya uovu huo.

Hapa inayoumbuka ni CCM na usalama wa TAIFA maana Ludovick nii mtu wao. Kila wanalofanya CCM na usalama wa TAIFA, siri nje.

Swali ni je, CCM na TISS watakubali.kumwadhibu mtu wao waliyemtuma kuihujumu CHADEMA?

Hujajibu hoja mkuu! Angalia post yangu na jibu lako.
 
Hamy-D,

Nimevumilia kwa muda mrefu upuzi na upotoshwaji wako. Uzalendo umenishinda.

I challenge you,
Iwapo Ludovick ni mfanyikazi wa Makao Makuu toa basi ushahidi aliajiriwa lini, nani kamwajiri na kwa barua ya Tarehe ngapi, na Kitambulisho chake ni namba ngapi.

Nadhani upotoshwaji ni lazima ufike mwisho sasa. Kama walivyo volunteers wengi, Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii.

Iwapo utashindwa kutoa ushahidi huo mpaka leo jioni, nitawaomba wanaJF wakohesabu mwongo aliyekubuhi, na JF na Jamii nzima ya Watanzania wakupuuze wewe na posts zako zote.

Dr.W.Slaa,

Kwanza nikusahihishe kuwa mimi sio mzushi wala mpotoshaji, sijawahi kuwa na sitokuwa na hizi tabia kwa kuwa nina hofu na Mungu.

Pili, nimesema kuwa Ludovick alikuwa mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, wewe umeleta kitu kipya hapa cha kunitaka nianze kuchambua aina ya wafanyakazi, sasa sidhani kama uchambuzi huo utakuwa na faida yoyote kwenye hoja ya msingi.

Kubwa hapa ni kwamba alikuwa ana fanyakazi CHADEMA makao makuu tena kwenye kurugenzi nyeti ya chama, masuala hayo unayoyaleta ni katika kukimbia mjadala tu.

Sasa kama CHADEMA mmekuwa hamjitambui kiasi cha kupitiliza cha kufanya muwaweke ma-volunteers kwenye idara nyeti hilo ni tatizo lenu, na halifuti taswira ya kuhusika kwa CHADEMA katika tukio la kumteka na kumtesa Kibanda.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, ni kweli bwana Kibanda kuwa ange subiri, ila roho ina muuma sana, na sabcu ya kusema haya ni katika kutafuta pumziko la nafsi yake, kwani amekiri mwenyewe katika maelezo yake hapo.

haswaa mkuu. kibanda alisema kuwa atakuwa tofauti na dr stephen ulimboka. kweli amedhihirisha kuwa yupo tofauti
 
hakuna janga kubwa ndani ya taifa hii kama vijana wa bavicha. fuatilia tu utagundua kuwa hawa vijana wanatumika vibaya na vizee vya chadema.

Mbona hilo lipo wazi,na linajulikana sana,yaani hiki chama cha wakaskazini natamani ht kifutiliwe mbali ili alau nchi itulie wamekuwa na fujo tuu na hii nchi hawataishika labda tz yote wabadili makabila wawe wachaga,japo kuwa namimi ni mchaga lkn sikipendi hiki chama.
 
Dr.W.Slaa,

Kwanza nikusahihishe kuwa mimi sio mzushi wala mpotoshaji, sijawahi kuwa na sitokuwa na hizi tabia kwa kuwa nina hofu na Mungu.

Pili, nimesema kuwa Ludovick alikuwa mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, wewe umeleta kitu kipya hapa cha kunitaka nianze kuchambua aina ya wafanyakazi, sasa sidhani kama uchambuzi huo utakuwa na faida yoyote kwenye hoja ya msingi.

Kubwa hapa ni kwamba alikuwa ana fanyakazi CHADEMA makao makuu tena kwenye kurugenzi nyeti ya chama, masuala hayo unayoyaleta ni katika kukimbia mjadala tu.

Sasa kama CHADEMA mmekuwa hamjitambui kiasi cha kupitiliza cha kufanya muwaweke ma-volunteers kwenye idara nyeti hilo ni tatizo lenu, na halifuti taswira ya kuhusika kwa CHADEMA katika tukio la kumteka na kumtesa Kibanda.

kwa vile tukio la kibanda linashabihiana na tukio la ulimboka, na kwa vile kibanda anasema kuwa amemtambua ludovick kuwa ni miongoni mwa waliomtesa, tukubaliane kuwa chadema ndo wamehusika na matukio yote mawili
 
Sasa ukweli unaanza kupatikana ila angalieni baada msiyakane maneno yenu huyu mtajwa hapo ilisj=hasemekana yupo karibu sana sana na viongozi flani flani wa chama tawala na alikuwa akitoroshwa rumande usiku kwenda kufundishwa namna ya kujieleza sasa kazi kwenu.....Kibanda bomoka kaka hapa atapatikana mhusika mkuu wa hizi mission
 
Mkuu, ni kweli bwana Kibanda kuwa ange subiri, ila roho ina muuma sana, na sabcu ya kusema haya ni katika kutafuta pumziko la nafsi yake, kwani amekiri mwenyewe katika maelezo yake hapo.
Mkuu hamy kibanda hana alichokosea ni haki yake kusema ukweli hali iliyomkuta inauma na inakela sana na tunaomba afike tena polisi na awaeleze polisi hawa waliomtesa.
 
Yaani sijui kwanini kuna watu wanaushabiki wa kijinga sana hasa hasa kikiwa kitu ni cha kisiasa,watu wote wanajua wazi kuwa lodovick alifanya umafya kwa faida ya chama chake na hilo lipo wazi,lkn kwa upuuzi tu mtu hata km ana kinyesi usoni akuambiwa ataanza kukipamba kinyesi kile na kionekane ni poda,suala la wahariri kudhuriwa inajulikana wazi kuwa ni mpango wa wazi wa chadema kwa faida wanazozijua wao,lkn cha ajabu lazima tu wamuingize mtu mwengine ili ile taswira ya umafia iondoke ktk sura za watu,suala la kuwadhuru wahariri ni mpango wa wazi wa chadema na sio kuanza kuwaingiza akina nchemba,ubaya wa hawa watu wananchi washaujua na upo wazi
Kama una muda wa kutosha sikiliza hii video. Hizi mbinu mlizitumia kuiua NCCR mageuzi na CUF, na sasa mnatumia mbinu hizo hizo kuimaliza CHADEMA. Kwa ajili tu ya kutafuta kuendelea kubaki madarakani, mmekuwa tayari kuwaua watanzania wasio na hatia. Yale makontena ya mapanga ambayo Mahita alisema CUF wameingiza yaliishia wapi? Mkasema CUF wameingiza silaha kwa ajili ya kuanzisha vita nchini, hizo silaha ziko wapi hivi sasa? Na kwanini mmeungana nao hivi sasa, baada ya CUF kufa? Hizi mbinu zenu za kitoto hazitafanikiwa kwa CHADEMA.

Last edited by a moderator:
Kwani mtu akifanya kazi kwenye chama cha upinzani hawezi kuwa agent wa TISS??

Hebu kamuulize Mrema, Bagenda na wenzao...!!

Nakuunga mkono 100%, kwani watz inabidi tuelewe haya mambo yanavyo kwenda. Bila kuwaza vyakutosha tutajikuta tunagombana wenyewe kwa wenyewe.
 
Kama una muda wa kutosha sikiliza hii video. Hizi mbinu mlizitumia kuiua NCCR mageuzi na CUF, na sasa mnatumia mbinu hizo hizo kuimaliza CHADEMA. Kwa ajili tu ya kutafuta kuendelea kubaki madarakani, mmekuwa tayari kuwaua watanzania wasio na hatia. Yale makontena ya mapanga ambayo Mahita alisema CUF wameingiza yaliishia wapi? Mkasema CUF wameingiza silaha kwa ajili ya kuanzisha vita nchini, hizo silaha ziko wapi hivi sasa? Na kwanini mmeungana nao hivi sasa, baada ya CUF kufa? Hizi mbinu zenu za kitoto hazitafanikiwa kwa CHADEMA.
Mkuu haya mbona ni maneno tu ambayo hata kwenye khanga yapo kwani nccr na cuf walizoua kutokana na tamaa zao za madaraka na fedha hakuna chama kinaua chama mwenzake huko ni kudanganya watu na kutaka kujaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.
 
Dr.W.Slaa,

Kwanza nikusahihishe kuwa mimi sio mzushi wala mpotoshaji, sijawahi kuwa na sitokuwa na hizi tabia kwa kuwa nina hofu na Mungu.

Pili, nimesema kuwa Ludovick alikuwa mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, wewe umeleta kitu kipya hapa cha kunitaka nianze kuchambua aina ya wafanyakazi, sasa sidhani kama uchambuzi huo utakuwa na faida yoyote kwenye hoja ya msingi.

Kubwa hapa ni kwamba alikuwa ana fanyakazi CHADEMA makao makuu tena kwenye kurugenzi nyeti ya chama, masuala hayo unayoyaleta ni katika kukimbia mjadala tu.

Sasa kama CHADEMA mmekuwa hamjitambui kiasi cha kupitiliza cha kufanya muwaweke ma-volunteers kwenye idara nyeti hilo ni tatizo lenu, na halifuti taswira ya kuhusika kwa CHADEMA katika tukio la kumteka na kumtesa Kibanda.
Nimeshamjibu mwenzako Nambalapala, kwamba kuwa mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, hukutoi ushahidi kwamba alitumwa na CHADEMA kufanya aliyoyafanya. Kama tukiongelea kuhusu watu wa karibu wa CHADEMA basi wewe, Mtela Mwampamba, na Juliana Shonza, pia mlikuwa ni watu wa karibu wa CHADEMA. Tena wengine kati yenu tukawaamini na kuwapata nafasi ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA, na wengine mkapewa madaraka makubwa katika BAVICHA ilihali mnawatumikia akina Mwigulu. Kwahiyo hata Ludovick alikuwa ni mtu wa aina kama yenu. Anajifanya mtiifu kwa CHADEMA huku anawatumikia akina Mwigulu.

Kikubwa ni kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba Ludovick alitumwa na Mwigulu kumshambulia Kibanda ili wapate sababu ya kutoa video ambayo Mwigulu amekiri kumpa Ludovick kamera ya kurekodia.
 
Last edited by a moderator:
Someni kwa uchambuzi kwa kutumia akili huru

2013/4/17 Ansbert Ngurumo <ansbertn@yahoo.com>
Mazungumzo yangu na Kibanda

Baada ya stori ya gazeti la MTANZANIA leo, iliyotuhumu wahariri wanne na mwanasiasa mmoja kuhusu ushiriki kwenye mtandao hatari, nimefanya utafiti kujua kilichotokea, maana nimehusishwa na uchafu na ujinga usiofanana na haiba na hulka yangu.

Nimezungumza na watu wengi kujua mwelekeo wa habari hii na hatua za kuchukua. Hatumaye, nimezungumza na Kibanda kwa simu mnamo saa 10 jioni.

Bahati nzuri, naye alikuwa ameshazungumza na watu kadhaa, wakiwamo wahariri na viongozi wenzake wa New Habari. Kimsingi, amekerwa na kinachotokea kwenye vyombo vya habari kuhusu sakata la kutesana kwake.

Kwa kifupi, anasema stori anayoiona yeye ni jinsi ambavyo Ludovick ameweza kujipenyeza na kuwazoea wahariri na wanablogu kwa sababu anazojua yeye.

Anasema stori si kuwahusisha wahariri na ujambazi. Anasema hii ni njama ya kufunika mambo na kuwalinda wahalifu wa kweli. Akasema anadhani wametumia njama ya kugombanisha wahariri, ili kugawa vyombo vya habari katika makundi, waweze kutimiza malengo yao.

Anasema Charles Mulinda amekuwa na hisia kwa muda mrefu kwamba Ansbert Ngurumo anamchukia. Mulinda, hata alipokwenda Afrika Kusini, alimwambia Kibanda kuwa Ansbert amekuwa anampigia Bashe simu, akimtaka amfukuze kazi. Anadai pia kwamba Ansbert ndiye alimshauri Msama amfukuze kazi katika gazeti la Dira. Anadai pia kwamba mwaka 2009 Ansbert aliporejea kutoka masomoni, alikuwa anadhamiria kumfukuza kazi, kwa madai kwamba yeye (Mulinda) ni mla rushwa.

Mulinda anadai pia kwamba timu ya wahariri inayochunguza tukio la Kibanda ilipomhoji, miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni kwamba inasemekana amekuwa akipokea rushwa kwa jina la Kibanda. Mulinda anadai kwamba mtu aliyewapa swali hilo ni Ansbert.

Inasemekana pia kwamba Ratifa alimwambia Kibanda kuwa Ansbert amemwambia Bashe kuwa yeye (Ratifa) ni shushushu.

Hivyo, watu hawa wawili walipopata taarifa za mawasiliano ya Ludovick na Ngurumo, wakaamua kumshughulikia. Kwa maneno ya Kibanda, Mulinda na Ratifa "wametumia moyo" badala ya kichwa.

Lakini anasisitiza kwamba hata kama hayo yangekuwa kweli, haikuwa sahihi kuandika stori mbaya hivi dhidi ya wahariri. Anasema kwamba wao wamefanya hivyo kama kulipa kisasi, hasa kwa kuwa Tanzania Daima lilichapisha tamko la Marando likitaja majina na simu za watu, akiwamo Denis.

KIBANDA amesikitika kwamba newsroom ya MTANZANIA imemwacha Mulinda kufanya atakavyo. "How can you have an editor who is an unguided missile?" alisema. Anasikitika kwamba yeye ambaye angeweza kudhibiti tabia hii ndiye ameumizwa, kwa hivyo hawezi kuchukua hatua.

Amesema ana uhakika Ofisi itachukua hatua mwafaka.

Tayari amezungumza na Bashe na kutaka Mulinda ahojiwe, ataje chanzo chake cha habari hiyo, ili hatua hiyo isaidie katika hatua zinazofuata, hasa kujua wanaofanya jitihada za kutumia media kuficha wahalifu.

Amesema pia ni vema wahariri wakutane haraka iwezekanavyo na kuweka msimamo kabla ya mabaya zaidi kuwakuta.

Tayari Jukwaa la Wahariri limeitisha Kikao cha dharura kesho, Dar es Salaam.

UFAFANUZI WA BAADHI YA KAULI

Nimemjibu Kibanda ifuatavyo:

1. Sijawahi kumfukuza kazi Mulinda. Nilimlea kazini akiwa correspondent (2006), baadaye Kibanda alipokuja akamwajiri na kumpa uhariri Tanzania Daima. Niliporejea kutoka masomoni, alijiondoa mwenyewe kwa woga, akidai kwamba nilikuwa nataka kumfukuza kazi kwa rushwa.

2. Sikuwahi kumwambia Msama amfukuze kazi. Msama mwenyewe ndiye alikuja Ofisini kwangu kuomba radhi kwa niaba ya Mulinda, kuhusu stori iliyokuwa imeandikwa kwenye gazeti la Dira kuhusu Free Media kuchelewesha mishahara, ikidai Mbowe ndiye amechota pesa na kuelekea Club Bilicanas. Msama alisema anashangaa stori hiyo kwani hata yeye alikuwa hajalipa mishahara, na Mulinda hajapokea wa kwake. Akasema Mulinda amekuwa anamgombanisha na watu anaofahamiana nao. Akaazimia kwenda kumfukuza kazi.

3. Ni kweli nilimweleza Bashe kwamba Mulinda ni mlarushwa, na haandiki stori kubwa bila kupewa pesa. Nilitilia shaka mwenendo wa stori zake kupotosha suala la Kibanda. Nikamshauri Bashe stori zao wasiwe wanamwachia Mulinda na Ratifa peke yao, bali wazijadili kwenye vikao, wakubaliane. Nilisema mkimwachia aamue peke yake atawaumiza nyie na watu wengine. Ndilo limetokea!

4. Kuhusu Ratifa, sikusema ni shushushu, bali ni msiri mno. Nikasema nimeshuhudia mara kadhaa akigombezwa na Kibanda kwa kumficha mhariri chanzo cha stori. Nikamshauri kwamba katika suala tete kama hili, ni vema waandishi wote wawe wanataja vyanzo vya habari kwa wahariri na wenzao katika Chumba cha Habari, ili kudhibiti dhuluma.

5. Nilisema chanzo cha habari yao hakikuwa na nia njema, na wao walitumia mawasiliano ya Ludovick kama kificho cha majangili ili kuwanusuru wanaotuhumiwa kushirikiana na Ludovick kwa mabaya.

Wasiwasi wa wengi, akiwamo Kibanda, ni kwamba chanzo cha habari cha Mulinda kinaweza kuwa kinatumiwa na UWT au Polisi kuua stori HALISI. Ndiyo maana Kibanda amependekeza kwamba Mulinda ataje chanzo chake cha Habari.

Ansbert Ngurumo
Dar es Salaam
Tanzania
 
Hivi nyie watetezi wa mwigulu mbona hamtaki kujibu ela zilitumwa kwa ludovick kutoka kwa mwigulu za nini? Na kwa nn alipiga simu nyingi kuliko mkewe kabla ya tukio?
Somerhing is to be revealed here.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ili ujue kwamba Ludovick si wa Chadema angalia jinsi walivyomuacha katika dhamana kama ni wao wangemdhamini. Just connect things to get a clear picture on this issue.
 
Ili ujue kwamba Ludovick si wa Chadema angalia jinsi walivyomuacha katika dhamana kama ni wao wangemdhamini. Just connect things to get a clear picture on this issue.
mwampamba alishawaeleza kitambo kuwa ni mwendelezo wa usaliti. nini sasa hujui?
 
Back
Top Bottom