Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

Hoja yako imepoteza uhalali. Mbona hii kitu ilisha pitwa na wakati! Kwani kilicho mfanya Ludovick kuachwa solemba na CHADEMA unajifanya hukijui?

Haya, ushatimiza wajibu wako ulio tumwa na MABWANA zako, chapchap Lumumba kasaini vocha.

Nauwakika kwa hii hatolipwa kwani amemuumbua Bosi wake na kukumbushia machungu na aibu ya MACCM.

Inajulikana wazi Membe plus nape, riz1, Nchimbi walimtumia Mwigulu kusuka ili swala na Mwigulu akamtumia Ludo.
 
CCM ni sawa na mfa maji kwa sasa, MWIGULU, LUDOVICK na wenzao ni kama mikono ya ccm inayotumika kushikilia magugu, lakini siku zote njia ya muongo ni fupi kwani sasa hivi wabunge wengi wa chama cha NDIOOOO na kuunga mkono kwa 100% wameanza kushituka na haya yanayofanywa na chama chao yanaipeleka wapi nchi hii.

HIVI KWELI CDM INGEWEZA KUFANYA HAYA YOTE NDANI YA SERIKALI YENYE VYOMBO VYA ULINZI BILA KUBAINIKA AU NI SERIKALI YENYEWE NDIO INAYAFANYA HAYA ili kukipaka matope cdm baada ya kuona ccm imeshindwa kuwaletea maisha bora watz?
 
Hakujiuliza mahusiano ya Ludovic na Mwigulu Nchemba kiasi mpaka Mwigulu kumtumia Ludovic elfu hamsini kupitia M-Pesa?
 
Mkuu wewe kama mgeni JF, unaandika taarifa zinazojulikana halafu unageuza kashfa ya dola kuwa ya Chadema.
Ni polisi wa chadema au ccm waliomtoa nje ya mahabusu na kumhoji na kumrudisha ndani kinyume cha utaratibu?
Ni mbunge wa chadema au ccm aliyemtumia 50,000 kwa njia ya M pesa?
Ni mbunge wa chadema au ccm aliyekuwa anawasiliana na Ludovick mara nyingi kuliko mke wake kabla ya tukio hilo?
Ni polisi wa ccm au chadema waliomkamata Ludovick siku hiyo hiyo Kibanda alipotekwa huku simu yake ikiendelea kuwa hewani kinyume cha sheria?
Ninayo maswali mengi zaidi ya hayo, kwa uzi huu huisaidii ccm, unaizamisha katka matope hayo. Mzee wako hatakanyaga ikulu whether you like or not.
 
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.

Issue si imekwenda mahakamani na wataalamu wa sheria na uchunguzi wameona hii siyo kesi ya msingi ya kigaidi? Mbona unatokwa na povu namnahii kwakutaka kujiridhisha mwenyewe na vitu ambavyo havipo? Mbona hatusikii huyo Ludovick kubakizwa na gesi ya UGAIDI mwenyewe? Mbona analindwalindwa na vyombo vya usalama? Inakuwaje mtu yupo mahabusu lakini anaendesha maisha na madeal yake kama kawaida? MKUBALI TU KUWA HILI ZOEZI MMESHINDWA, NENDENI MKAJIPANGE TENA MJE MUUMBUKE KAMA HILI LA ARUSHA.
 
Mwigulu Nchemba ndiye aliyemtuma Ludovick akamdhulu Kibanda ili apate cha kusema kuhusu video ya Lwakatare ambayo waliitengeneza na Ludovick.

Ulitengeneza wewe?,umeitazama au umesimuliwa!!! mwenyewe kasema Polisi pale ni nyumbani kwake na picha ni yake lkn sauti si yake,miishiyo yenu inakaribia.
 
Acheni zeni nyinyi, Mwigulu akumtaja jina mtu aliyempa pesa za vifaa kwa ajili ya shughuli ya kumrekodi Lwakatare, kwa taarifa yako, bado yuko humo humo CHADEMA.

Huyu kijana CHADEMA mmeamua kumchinjia baharini lakini sio vyema, hemu angalia alipotoka na CHADEMA;


Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Asante sana mhangaikaji! Subiri ufurahie kifo cha CHADEMA ndugu yangu!
Hiyo story ya Mtela Mwampamba haiaminiki tena kwa sababu ni juzi tu ametudanganya kwamba MBOWE alikosa watu kwenye mkutano wa Kampeni Iyela akaishia kuwahutubia wanafunzi wa shule za msingi-matokeo ya udiwani yanaonesha mgombea wa CDM ameshinda kwa kimbunga kutokana na
kura za wananfunzi hao!

Kwa Mwigulu kumtumia fedha mtu anayetuhumiwa kwa UTESAJI NA UTEKAJI, HAKUMUACHI HURU!
Juzi juzi nilikwambia Polisi wetu hawatumii SITUATIONAL GAP FILLERS la sivyo Mwigulu angalikuwa mahabusu
Yuko nje kwa sababu mkuu wa vijana wa kazi ni shem!
 
Hamy-D,

Nimevumilia kwa muda mrefu upuzi na upotoshwaji wako. Uzalendo umenishinda.

I challenge you,
Iwapo Ludovick ni mfanyikazi wa Makao Makuu toa basi ushahidi aliajiriwa lini, nani kamwajiri na kwa barua ya Tarehe ngapi, na Kitambulisho chake ni namba ngapi.

Nadhani upotoshwaji ni lazima ufike mwisho sasa. Kama walivyo volunteers wengi, Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii.

Iwapo utashindwa kutoa ushahidi huo mpaka leo jioni, nitawaomba wanaJF wakohesabu mwongo aliyekubuhi, na JF na Jamii nzima ya Watanzania wakupuuze wewe na posts zako zote.
 
Halafu hapo hapo anatengeneza video ya Lwekatare, Kisha anampa Mwigulu, halafu anapewa Pesa na Mwigulu halafu anaendelea kuwasiliana na Mwigulu kama mtu na mkewe, halafu anahakikishiwa na CCM kuwa atalindwa.

Wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mambo, uko sahihi. Mleta mada ama hajui ama anapindisha ukweli kwa makusudi.
 
Hamy-D,

Nimevumilia kwa muda mrefu upuzi na upotoshwaji wako. Uzalendo umenishinda.

I challenge you,
Iwapo Ludovick ni mfanyikazi wa Makao Makuu toa basi ushahidi aliajiriwa lini, nani kamwajiri na kwa barua ya Tarehe ngapi, na Kitambulisho chake ni namba ngapi.

Nadhani upotoshwaji ni lazima ufike mwisho sasa. Kama walivyo volunteers wengi, Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii.

Iwapo utashindwa kutoa ushahidi huo mpaka leo jioni, nitawaomba wanaJF wakohesabu mwongo aliyekubuhi, na JF na Jamii nzima ya Watanzania wakupuuze wewe na posts zako zote.

Asante Dr kwa kukata mzizi wa fitina.

Kwa kuwa Dr Slaa ndo mwajiri wa wafanyakazi wote wa makao makuu ameshasema hajamwajiri sasa tunasubiri kauli ya mleta uwongo hapa ajitetee. Chadema kama chama kina washabiki wengi na kila mmoja anasaidia chama ktk ngazi mbali mbali kuanzia kijiji/mtaa, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa. Hata katka ofisi za kata wako watu ambao wanajitolea kama sehemu ya mchango wake kwa chama. Sasa kama mtu ana kadi ya chama akaja ofisi ya jimbo akajitolea utamjuaje kama ametumwa na akina Mwigulu Nchemba? Hamy D kajipange tena.
 
Mbona Kibanda hajatuambia mazungumzo kati yake na makamu ya Rais ikulu yalihusu nini na nn walikubaliana.

Pili kama ni ludovick anahusika, je kwan huyo ni cdm, hivi cdm/ccm wa kweli anaweza kufanya jambo la kuumiza chama chake ambacho anajua ndicho kinampa riziki? nasikitika vijana wengi sasa hv mnatumiwa na wazeee kama mavuvuzela, ambalo hata kichaa analishika na kulipuliza bila hata kuwa na uwezo wa kukataa

Vijana badilikeni, tuambieni ukweli huko mnatumiwaje na vyama, kama mnaona wazee wamekuwa tatizo tukubaliane tuunde chama kimoja cha vijana tukiendeshe wenyewe ili tujipime na kuona ni ss wenye matatizo zaidi au ni wazee, period
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Dr. Slaa kwa kumuumbua mlevi huyu wa buku saba.
 
Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii.

Mkuu Dr Slaa, mtu kuwa volunteer, ni sehemu ya jamii anayovolunteer na mara nyingi kwa sisi tuliopita shule mtu hawezi kukubalika/kukubaliwa kirahisi kujitolea kufanya kazi ktk shirika, ofisi au kampuni hadi aaminike.

Mleta mada hana makosa kwani mahusiano ya ludovick na wewe,na lwakatare na maafisa wengine wa chadema yalikuwa makubwa na ameshiriki kazi nyingi za chama ikiwa ni pamoja na hizo anazotuhumiwa nazo.

Usimkatae leo kwa sababu mmeumbuka, mtetee hadi tone la mwisho la damu ndio maana ya ukamanda na upambanaji..vinginevyo huu ni usaliti
 
Hamy-D,
Nimevumilia kwa muda mrefu upuzi na upotoshwaji wako. Uzalendo umenishinda. I challenge you,
Iwapo Ludovick ni mfanyikazi wa Makao Makuu toa basi ushahidi aliajiriwa lini, nani kamwajiri na kwa barua ya Tarehe ngapi, na Kitambulisho chake ni namba ngapi. Nadhani upotoshwaji ni lazima ufike mwisho sasa.Kama walivyo volunteers wengi, Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii. Iwapo utashindwa kutoa ushahidi huo mpaka leo jioni, nitawaomba wanaJF wakohesabu mwongo aliyekubuhi, na JF na Jamii nzima ya Watanzania wakupuuze wewe na posts zako zote. .

Haya HAMY-D umepewa muda na kiongozi uliyemsingizia kuwa kamuajiri huyo muhalifu wenu mliomtuma aende akajitolee kazi CDM kumbe kwenda kutekeleza uhalifu. Tafadhali tunaomba udhibitishe hili la kwamba huyu Ludovick ni muajiriwa wa CDM, lasivyo tutakuchukulia kuwa wewe ni muongo na mpotoshaji katika jamii. Tatizo lenu nyinyi ni vilaza sana, mnafikiri dunia ya leo inaendeshwa bado na propaganda chafu. Nenda huko mahakamani mpeleke ushahidi wenu huu kama ni kweli. Mmetumia vibaya vyombo vya dola mpaka sasa jamii tumekosa imani navyo halafu mnasingizia CDM. Rejea matamko ya Mh. Lukuvi juzi BUNGENI kuhusiana na mlipuko wa Arusha, sasa ushahidi ukija kuwa wazi kama ule wa mwandishi Mwangosi (RIP) bado mtataka kutudanganya. Ipo siku tutawshitaki wote mnaotaka kuliangamiza ili taifa sababu ya uroho wenu isiojali utu wa mtanzania.
 
Kujaribu kumtenga Ludovick wakati huu ni mchezo wa kitoto. Ludovick ni insider na ameshriki operations nyingi tu za CHADEMA. Nadhani mkiendelea kum-frustrate huyu dogo atawaumbua sana. Watch out!
 
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.

weweee, hiyo lumumba itakufanya uonekane chizi, unakomaa nini na uongo sasa! unajua kuanalyse wewe, unajua kudig inside wewe, acha hiyo maneno bwana, watu wajinga wa kuwaokota kwa maneno planned tz siku hizi hawapo, kila mtu ameelimika vya kutosha, hata mkulima asiye na darasa lolote anajua kujumlisha na kutoa na kupata majibu ya kinachoendelea, endeleeni kujidanganya na kujitoa akili
 
Dr.W.Slaa

Wakati mwingine tunajikuta tunalazimika kuyasema hata yale ambayo hatukupanga wala kufikiria kuyasema.,nimekuwa nikipigiwa simu na ndugu zangu na rafiki zangu ambao bado wako chadema wakiniuliza kwanini nimeamua kuyasema ninayoyasema, tena kwa lugha kama hii (inayobainisha), nami nimekuwa nikiwajibu kuwa "hivi haiwi faraja kwenu kuwa yupo mmoja aliyewahi kuwa mfano wenu anayetaka kuwaokoa na hatari yenye kuangamiza..?

Nadhani wengi katika wao wamenielewa lakini nitazidi kuwaeleweshaa wale ambao bado wanaubutu na kutu imejaa katika fikra na mitazamo yao.Nimeeleza juu ya kukanwa na usaliti uliofanywa kwa LuDOVICK na nikaishia hapo, nikidhani kuwa itakuwa imetosha kuwafungua mawazo na kuwasaidia vigezo na vipambanuzi vya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi, maamuzi huru ambayo yatatokana na fikra zinazojitawala za kila mmoja katika upekee wake, si fikra za mkumbo (mob psychology) wala si fikra mgando na zilizosinyaa (dormant and dead reasoning), lakini nitawaongeza na hili la leo kuyaamsha mawazo hayo yaliyoganda na kuwafanya muishi kwa Uhai wa fikra Huru.

Napenda nianze kwa kuwaambia kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kuwakana wapambanaji wao na vijana waliokuwa wanajitolea hali na mali, wanajitolea nafsi na uhai kuipigania Chadema.

Nitawaambieni juu ya wachache waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama ifuatavyo:

-i) DEUS MALLYA:
Kwa mara ya kwanza nakutana na DEUS ilikuwa ni mwaka 2007, nikiwa nimejiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo nilishakuwa mwanachadema kabla ya kuingia Chuo Kikuu, hivyo nilipofika chuo nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa Chadema hasa wale waliokuwa wanatumikia Makao Makuu ndipo nilipokutana na DEUS MALLYA ambae alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa vinabeba ujumbe wa Chadema na falsafa mbalimbali za Ukombozi ambazo chadema ilikuwa ikinajinasbisha nazo.

Nilipokutana na DEUS tulipanga na kupeana ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae aliniunganisha na JOHN MNYIKA ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa Vijana na Afisa wake akiwa Marehemu Regia Mtema, ambapo DEUS alikuwa ni mtu wa karibu na maafisa hao, hasa MNYIKA. Na walikuwa pamoja na kufanya mambo mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;

a) Safari ya DEUS mallya kuelekea LIBYA katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijanakutoka chadema chini ya usimamizi wa Mnyika.
b) Safari ya RUSSIA ambapo DEUS alinieleza kuwa alienda kwa mafunzo maalum. Lakini Mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008, baada ya kutokea kwa kifo cha kutetanisha cha Mheshimiwa CHACHA WANGWE ambapo DEUS alikuwa ni Dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile, JOHN MNYIKA alimkana DEUS mara mbili, mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi juu ya kijana DEUS akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.

Hata baada ya kesi ya DEUS kumalizika na kisha DEUS kuachiwa huru, nilizungumza na DEUS juu ya kukanwa na MNYIKA na DEUS alinijibu kuwa mshikaji alimuomba radhi na kumtaka asahau yaliyopita na DEUS alikiri kumsamehe na imebaki hivyo mpaka hivi sasa (hili anaweza kulithibitisha DEUS MALLYA mwenyewe kwakuwa yu-hai)Lakini haikuishia kwa MNYIKA pekee bali hata BENSON KIGAILA ambae ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo aliwahi kumkana na anaendelea kumkana mpaka leo hii, kiasi kwamba DEUS akienda pale Makao Makuu na akikutana na BENSON huwa anamuambia kuwa asiwe anakuja Makao Makuu maana Chama kitachfuka kwa kuonekana MALLYA pale.Ni mtu ambae hafikiri sawasawa tu ndie atakayeweza kusema USALITI huu hauna asili ya ndani na kuwa ni hulka za viongozi wakuu wa Chadema kuendelea asili yao hiyo.

ANGALIZO:
Nitasema kama nilivyokutangulia kusema hapo awali juu ya hatma ya vijana ndani ya chadema, na leo nitasema hivi;

IKIWA HII MITI MIBICHI INATENDEWA HIVI., JE NINYI MITI MIKAVU MTATENDEWA VIPI..? ambao hata makao makuu ya Chama hamyajui wala hakuna anayewajua zaidi ya kuwatumia kwenye maandamano na mikakati yao
.
 
Last edited by a moderator:
Alikuwa wapi kufunguka kabla au alisubiri kwanza mpango mwingine wa kuua ufanyike halafu mjaribu kuunganisha kama kawaida. Kimsingi mimi binafsi sihitaji mtu afunguke Namhitaji Mungu afunue ukweli
 
Dr.W.Slaa

Soma

Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Kabla ya yote ningependa kuanza na maneno yafuatayo ya Utangulizi wa hiki ninachotaka kukisema hapa kama ifuatavyo:

USALITI;
Usaliti ni neno pana sana...,
Lina madhara mengi sana...,
Hujuma hukwamisha mambo mengi sana...,
Tamaa huzaa usaliti...,
Usaliti huleta maumivu kwa waliokuamini...!

Baada ya Utangulizi huo naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.

Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.

Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukio ya kigaidi.

Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION "BAED") katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa kwanza.

Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na CHADEMA na kuwajengea imani na matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha kuungana pamoja kuijenga CHADEMA. (LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya BAED-history & political science).

Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa CHADEMA kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na kichama. Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya CHADEMA, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na "mwanzilishi pekee" wa Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa CHADEMA mimi nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya hiyo.

Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010 niling'atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang'ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.

Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya CHADEMA kama Volunteer ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii.

Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha, ambapo Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.

Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr. Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-


  1. LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr. SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
  2. Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr. SLAA kuhusu viongozi wengine ndani ya CHADEMA na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa CHADEMA.(Pindi alipokuwa kitengo cha mitandao ya Kijamii)
  3. Credit nyingine aliyoipata kwa Dr. Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr. Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A Sabasaba.
  4. Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa Kagera.


Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo aliongozana na DR. SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.

Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA kwa kupanga na kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka CHADEMA, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa DR. SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa JamiiForums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.

PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU………. INAHUZUNISHA..!

Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.

​
 
Last edited by a moderator:
Kujaribu kumtenga Ludovick wakati huu ni mchezo wa kitoto. Ludovick ni insider na ameshriki operations nyingi tu za CHADEMA. Nadhani mkiendelea kum-frustrate huyu dogo atawaumbua sana. Watch out!

hivi kwa akili za kawaida tu unadhani Cdm hawajui unachokiongelea?..kwanini mwigulu haendi kumpa dhamana?
 
Back
Top Bottom