Kibanda azidi kufunguka, CHADEMA kikaangoni

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,818
Wana-JF!!

Mnamkumbuka mhariri ABSALOM KIBANDA? AMBAE ALITEKWA NA KUTESWA?, amesema yafuatayo kuhusu wahusika ambao walimfanyia vitendo hivyo vya kinyama ambavyo vimempa ulemavu wa kudumu wa jicho lake. Nanukuu;

"Acha niliseme hili jamani pengine moyo wangu utatulia. Mmoja wa watu walio nishambulia ana fanana kwa sura na umbile la Ludovick Rwezaura yule kada wa CHADEMA aliyewekwa ndani na Lwakatare ambae nimemuona kupitia magazeti na mitandao ya kijamii. Nimeshangazwa sana mtu huyu yupo karibu na baadhi ya wahariri wenzangu na hata msaidizi wangu bwana Ansbert Ngurumo, bado napata shaka ni kuwa watu wana fanana au?"

My take;

Ndugu Ludovick ambae kwa sasa bado yupo mahabusu, alikuwa ni mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, chini ya kurugenzi ya ULINZI na USALAMA kabla ya kukutwa na mkasa wake ambao ndio umemuweka rumande mpaka hivi sasa. Kuwepo kwa kijana huyu kwenye hii kurugenzi na maelezo ya bwana Kibanda nadhani wana-JF mnaweza ku-connect dots.

CHADEMA ukweli ni kwamba mwaka 2013 umekuwa mwaka 'tasa' kwenu, kwani mikakati mingi ya kichama imekuwa ikibuma na mbaya zaidi ni pale mpaka siri za ndani ya chama kuzagaa mitaani, haya yote ya kubuma na kuvuja kwa siri ovyo ovyo hivi, kuna sababishwa na 'uchanga' wenu katika kusimamia shughuli za kichama, mna safari ndefu sana.

Source: DIRA YA MTANZANIA.

====================
UPDATE from JamiiForums
====================

Baada ya kuwasiliana na Kibanda, katutumia ujumbe ambao yeye aliuandika. Alichokiandika yeye ni kama kinavyoonekana kwenye mabano chini:

Kibanda said:
Acha niliseme hili jamani pengine moyo wangu utatulia,

Mmoja wa watu walionishambulia anafanana kwa sura na umbile na Ludo ambaye nimemuona kupitia katika picha mtandaoni na katika magazeti.

Bado naendelea kutafakari iwapo ni kufanana (maana watu ni wawili wawili) au wana unasaba na mmoja wa watesi wangu... Jamani hadi sasa hii ni dhana tu maana nimeambiwa kule mahabusu aliko amekataa katakata kuwa alihusika katika tukio langu....==========

1. Nina imani kubwa na jamvi hili ambalo mijadala na wana jamvi wake ni watu walio dhahiri na halisi kwa majina na wasifu wao. Naamini jamvi hili litaleta mabadiliko ya kweli katika taifa hili huko Tuendako. Tusubiri tuone.

2. Bado nina maswali mengi kuhusu kile kilichonifika na kuhusu baadhi ya watu ambao kimsingi ningependa kama taifa tushirikiane kuwachunga na kuwachunguza akiwamo huyo mwana mabadiliko mwenzetu Ludo.

3. Kuchokoza hoja ili hatimaye tupate ufumbuzi na majibu halisi kuhusu kile kilichonitokea hasa baada ya kuwapo kwa jitihada kubwa ndani ya vyombo vya dola na hata miongoni mwa wana habari na wahariri kulipindisha kwa malengo ambayo binafsi siyajui.

Sipendi kuwa mtu wa kwanza kumnyoshea yeyote kidole kuhusu kile kilichonipata. Niseme wazi nilianza kwa kujinyoshea kidole/ vidole mwenyewe kwa tukio lile na kimsingi nimekuwa katika mchakato wa kuangalia nyufa ambazo pengine zilitoa mwanya au kusababisha kijeruhiwa kwangu.

Nataka kutetewa kwa haki na katika misingi halisi na ya kweli. Kwangu Ludo ni kitendawili kigumu sana. Wasifu wake ni tata kweli kweli. Amekuwa mtu wa karibu na watu wengi ambao nimepata kufanya nao kazi kwa karibu na kwa muda mrefu, ingawa hajapata hata mara moja kinifikia au hata kujitambulisha kwangu kwa namna yoyote ile. Bado nautafakari mwenendo huu iwapo ni wa bahati mbaya au uliokuwa umepangwa.

Pamoja na kumpa pole ndugu yangu kifamilia Maggid na mkewe, nilizungumza naye pia namna anavyomfahamu Ludo na kupitia maelezo yake ambayo sina sababu ya kuyatilia shaka nilibaini alikuwa hamjui sawasawa.

Hakujua kwamba ni kada wa Chadema na kwamba alipata kuwa katika Kamati ya Ulinzi na Usalama ya chama hicho. Hakupata kujua kwamba Ludo alikuwa pia uhusiano ambao hadi sasa hauko wazi na baadhi ya wanahabari na wahariri kwa kiwango ambacho nashangaa kinafunikwafunikwa.

Ludo alipohusishwa na Dennis Msacky na kisha Maggid vyombo vya habari vilishabikia sana hoja hiyo lakini alipokuja kuhusishwa na Ansbert, Balile na Chadema hali ikageuka na kuwa mbaya sana.

Angalau moyo wangu ulitulia baada ya kujua kile ambacho Dennis, Balile na Maggid walikuwa wakiwasiliana na Ludovick.

Hadi leo hii bado sijajua kwa ufasaha na kwa undani uhusiano kati ya Ludovick na Ansbert ambaye mbali ya kuwa msaidizi wangu Free Media Ltd, rafiki yangu wa miaka mingi na mwana habari mwenzangu tunayefanya kazi kwa karibu sana hatujapata kukaa na kulizungumza hili kwa kina.

Wana jamvi uhusiano wa Ludo na Nchemba, Lwakatare, Chadema na Wanasiasa wengine ni jambo ambalo pia linaonekana kufunikwa funikwa sana. Iwapo kweli tunadai mabadiliko ya kweli katika taifa hili tutimize wajibu wetu kuyaleta mabadiliko hayo.

Absalom Kibanda
 
Attachments

 • kibanda afunguka.jpg
  kibanda afunguka.jpg
  42.8 KB · Views: 690
 • kibanda afunguka2.jpg
  kibanda afunguka2.jpg
  93.4 KB · Views: 701
Wewe inaonekana taarifa zinakupitia pembeni. Mbona hili jambo lipo wazi kabisa siku nyingi. Tena watu walileta na evidence za Ludovick mwenyewe akijitetea kwamba siku Kibanda amepigwa yeye Ludovick alikuwa ametekwa?

Sasa story ipo hivi:
Baada ya Nchemba kumtuma Ludovick akamrecord Lwakatare, na kupeleka ile video polisi, halafu akaona polisi hawachukui hatua, ndipo alimtuma Ludovick akamshambulie Kibanda ili ionekana mipango ya Lwakatare ndiyo imetimia.

Ndiyo maana mara tu baada ya Kibanda kushambuliwa, video ya Lwakatare iliwekwa kwenye mitandao.

Kwani kisa cha CHADEMA kumtosa Ludovick ni nini? Ni baada ya kugundua kwamba Ludovick ni mmafia. Hilo lipo wazi mkuu, kama hukuwa na taarifa basi uipate saa hivi.

Mwigulu Nchemba ndiye aliyemtuma Ludovick akamdhulu Kibanda ili apate cha kusema kuhusu video ya Lwakatare ambayo waliitengeneza na Ludovick.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu, huyu Hamy D anaishi wapi yuko Dunia hii au yu wapi maskini wa Mungu!

Hii habari iko wazi kabisa na Mwigulu kasema ndio kamtuma Ludovick na pia siku wakati Kibanda anatekwa na Ludovick nae kasema alitekwa na kavuliwa nguo zake zote na pia alisema alipoenda kuripoti Police alisikia Police wakizungumza kwa Radio Call zao kuwa Kibanda katekwa sasa hapa Hamy D unataka ushahidi gani tena mkuu? Siku zote ulikuwa wapi?

Au ulikuwa bado hujapata kibarua hapo Lumumba so ulikuwa hujapata zali la kusoma habari? Lakini hata kwa Tv hujawahi angalia news? Pole sana mkuu sasa habari ni Bomu lililolipuliwa na Police Arusha na kuongezea na silaha za moto risasi kwa kutumia SMG na Bastola sasa hapa nakupa akib ya maneno nani anamiliki SMG Tanzania? Home work nakupa hiyo.
 
Last edited by a moderator:
sio hot cake kwa sasa.

Mkuu, haya matukio bado ni sintofahamu, sasa unaposema sio hot cake sijui wewe unawajua wahusika wa vitendo vya kigaidi na utekaji hapa nchini ama vipi?

Ukiwa kwenye upelelezi, hata habari zikiwa za karne iliyopita kama zina mahusiano na upelelezi, basi zinakuwa ni hot cake.
 
Mia huyu Hamy D anaishi wapi yuko Dunia hii au yu wapi maskini wa Mungu!!Hii habari iko wazi kabisa na Mwigulu kasema ndio kamtuma Ludovick na pia siku wakati Kibanda anatekwa na Ludovick nae kasema alitekwa na kavuliwa nguo zake zote na pia alisema alipoenda kuripoti Police alisikia Police wakizungumza kwa Radio Call zao kuwa Kibanda katekwa sasa hapa Hamy D unataka ushahidi gani tena mkuu?Siku zote ulikuwa wapi?Au ulikuwa bado hujapata kibarua hapo Lumumba so ulikuwa hujapata zali la kusoma habari?Lakini hata kwa Tv hujawahi angalia news?Pole sana mkuu sasa habari ni Bomu lililolipuliwa na Police Arusha na kuongezea na silaha za moto risasi kwa kutumia SMG na Bastola sasa hapa nakupa akib ya maneno nani anamiliki SMG Tanzania??Home work nakupa hiyo.Ndondocha mkubwa wewe!!

Acheni zeni nyinyi, Mwigulu akumtaja jina mtu aliyempa pesa za vifaa kwa ajili ya shughuli ya kumrekodi Lwakatare, kwa taarifa yako, bado yuko humo humo CHADEMA.

Huyu kijana CHADEMA mmeamua kumchinjia baharini lakini sio vyema, hemu angalia alipotoka na CHADEMA;

[h=1] Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)
[/h]
 
KIBANDA AKIWA AFRIKA YA KUSINI ALITANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE - JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI 2015 na thread imo humu JF.

Na mchuano wa mchujo ndani ya chadema atashindana na YUSUFU ASUKILE na OSCAR MWAMBENE!!!... HUYU JAMAA KWAO NI RUNGWE KARIBU NA KIWIRA.
 
KIBANDA AKIWA AFRIKA YA KUSINI ALITANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE - JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI 2015 na thread imo humu JF, .. Na mchuano wa mchujo ndani ya chadema atashindana na YUSUFU ASUKILE na OSCAR MWAMBENE!!!... HUYU JAMAA KWAO NI RUNGWE KARIBU NA KIWIRA.

Washampa kilema cha kudumu, unatarajia bado tu atakuwa na matarajio ya kitu chochote? mimi namshauri ajipumzikie tu na aachane kabisa na CHADEMA kwani ukisoma vizuri maelezo yake mwenyewe anajua fika CHADEMA ni watu wa aina gani.
 • :focus:
 
Acheni zeni nyinyi, Mwigulu akumtaja jina mtu aliyempa pesa za vifaa kwa ajili ya shughuli ya kumrekodi Lwakatare, kwa taarifa yako, bado yuko humo humo CHADEMA.

Huyu kijana CHADEMA mmeamua kumchinjia baharini lakini sio vyema, hemu angalia alipotoka na CHADEMA;

Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Na hela kutoka namba ya Mwigulu Mchemba kumtumia pesa Ludovick zilikuwa za nini?Amemfanyia kazi gani hadi amtumia 50,000 mkuu kweli wewe hufahamu mambo aliyekupa kazi ya kukaa kwa mtandao muulizie uzuri ili usiweweseke hapa ndani sawa mkuu,maake unajiabisha tu.Jaribu kuwaza zaidi kwa kutumia kichwa cha juu epuka kutumia kichwa cha chini katika maisha yako.Hata ukipewa cha kuweka hapa kisome kwanza na kama kuna marekebisho unaweza kurekebisha.Lol kweli Tanzania inazalisha watu wa ajabu ajabu.
 
Mkuu, kwa ukaribu wa Ludovick na Dr Slaa sidhani kama angeweza kumsaliti Dr Slaa kwa kushinikizwa na Mwigulu, hemu angalia Mwampamba anavyotoa ushuhuda wake kuhusu Ludo;
Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)
Ina maana wewe huna taarifa kwamba Ludovick alihamishiwa pesa na Mwigulu kwa njia ya Mpesa kama sehemu ya kumshukuru Ludovick kwa kazi nzuri aliyoifanya? Na hiyo hela Mwigulu kamhamishia Ludovick baada tu ya mkanda kurekodiwa. Kama huamini muulize Mwigulu mwenyewe maana ameyatamka haya yeye mwenyewe Mwigulu tena hadharani wala si kwa kificho.

Sasa ujiulize kama Ludovick ni mtiifu kwa Dr. Slaa, ilikuwaje Mwigulu amtumie hela kwa njia ya MPesa? Mwigulu anafanya biashara gani na Ludovick. Tumia common sense ya kawaida tu, wala huhitaji kwenda kufanya research zenye statistical analysis kubwa.
 
Na hela kutoka namba ya Mwigulu Mchemba kumtumia pesa Ludovick zilikuwa za nini?Amemfanyia kazi gani hadi amtumia 50,000 mkuu kweli wewe hufahamu mambo aliyekupa kazi ya kukaa kwa mtandao muulizie uzuri ili usiweweseke hapa ndani sawa mkuu,maake unajiabisha tu.Jaribu kuwaza zaidi kwa kutumia kichwa cha juu epuka kutumia kichwa cha chini katika maisha yako.Hata ukipewa cha kuweka hapa kisome kwanza na kama kuna marekebisho unaweza kurekebisha.Lol kweli Tanzania inazalisha watu wa ajabu ajabu.

Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.
 
Huyu na Mwigulu wako juu ya sheria. Wanachosema wao ndicho amin na kweli. Wanaamini dola itakuwa upande wao daima.
 
Mkuu, kwa ukaribu wa Ludovick na Dr Slaa sidhani kama angeweza kumsaliti Dr Slaa kwa kushinikizwa na Mwigulu, hemu angalia Mwampamba anavyotoa ushuhuda wake kuhusu Ludo;
[h=1]Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)[/h]

we nawe kumbe uelewa wako ni wa la saba,yaani unaleta tamthiliya za mwampamba hapa ivi unafikiri kweli? Ludo ni swaiba wa mwigulu na connect dot kwa ninni mwampamba anamsapoti ludo kua hawezi kusaliti? Tatzo ccm ni wahuni ila elimu ndogo
 
Acheni zeni nyinyi, Mwigulu akumtaja jina mtu aliyempa pesa za vifaa kwa ajili ya shughuli ya kumrekodi Lwakatare, kwa taarifa yako, bado yuko humo humo CHADEMA.

Huyu kijana CHADEMA mmeamua kumchinjia baharini lakini sio vyema, hemu angalia alipotoka na CHADEMA;

Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)
Sikiliza hii video kuanzia dk ya sita. Utauelewa vizuri uhusiano wa Ludovick na Mwigulu, na CHADEMA wana record zote za hadi mawasiliano ya simu kati ya Ludovick na Mwigulu Nchemba. Hamna pa kukimbili CCM. Mwigulu ni kama Savimbi. Muuaji na mnyonya damu za watanzania.

Last edited by a moderator:
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.
Tatizo lako wewe ni muongo na huna kumbukumbu nzuri. Ina maana umesahau siku Mwigulu aliposema kwamba alimpa hela Ludovick kama rafiki wa kawaida kama anavyowapa akina Nassari? Siku hiyo Mwigulu alisema alishawahi kumpa Nassari shilingi laki tano, na Nassari akampinga vikali na kumtaka athibitishe, lakini Mwigulu aliingia mitini alipotakiwa kuthibitisha. Kama ni uongo Mwigulu Nchemba mwenyewe aje akanushe hapa. Inaonekana wewe umetumwa kuja kuleta propaganda usizosijua.
 
Last edited by a moderator:
Sasa hapo ni KUIUMBUA CCM na Mwigulu, Maana hadi matukio yanatokea alikuwa kwenye Pay Roll ya Mwigulu. Kwa mwenye akili anaelewa sasa ni nani muuaji wa Kibanda.
 
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?

Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.

Sawa sikushangai sana huenda wewe ndio type ya kina Michael Kamuhanda au Nape Nnauye maake mnachimba kweli kweli kama umesoma tamko la Nape wakati analitoa akiwa Dodoma basi huna tofauti sana pia na Lukuvi kama ulisoma habari ya Lukuvi kasema ati Police waliokuwa wakilinda mkutano wa Chadema walikuwa Kaskazini na Bomu lilitokea mashariki sasa kweli huyu nae ni Waziri kweli au kitakataka yaani Police wanalinda mkutano halafu wako upande mmoja sasa hapo wanalinda au walikuwa kama raia wengine?Hapa nimekupeleka kidogo ili kama hujasoma ujaribu kusoma hawa watu niliokutajia na ujilinganishe nao na utaona hamko tofauti sana.Kuhusu la Kibanda badala ya kuminyana/kutoa mapovu peleka ushahidi na usiwe kama ule wa Mwigulu aliosema atautoa Mbinguni na sasa umefulia na atautoa kuzimuni.
 
Back
Top Bottom